Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Wakulima na wafugaji wa kata ya Nkiniziwa , Nzega wanufaika na huduma za mawasiliano za Airtel

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula katikati akikata utepe wakati wa kuzindua manara wa mawasiliano wa mwakashahala ulipo kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa Wilayani Nzega ambapo pamoja na mnaro huu Airtel imewasha minara mingine mitatu ya mawasiliano katika kata za Kahamanhalanga , Songambele na Itumba na kuwawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kupata huduma za mawasiliano mkoani Tabora. wakishuhudia wapili kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel Tabora, Fidelis Lugangila akiwa pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji cha Ngukumo.


wakulima na wafugaji wa kijiji cha Ngukumo  kata ya Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameipongeza Airtel kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya uhakika na kuwawezesha kuangalia bei za bidhaa na kutafuta masoko kupitia simu zao za mkononi


 Hayo yalisemwa na wakazi wa kijiji cha Ngukumo wakati wa uzinduzi huduma za mawasiliano utakaowawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kutoka katika vijiji 6  kupata huduma za mawasiliano baada ya Airtel kuwasha minara ya mawasiliano  katika maeneo ya Mwakashahalala Kahamanhalanga, Songambele  Itumba mkoani hapo


 ‘’Tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana ikiwemo mawasiiano hafifu ambapo ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za mawasiliano, Tunaishukur kampuni ya Airtel kwa kuona ni vyema kutufikishia huduma za mawasiliano hapa na kutuunganisha na ndugu jamaa  na wafanyabiashara   katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi alisema mkazi wa kata ya Nkiniziwa, John


 Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupula  alitambua na kupongeza juhudi zinazo fanya na Airtel katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wote kufatia mchango wake muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kusema ni muhimu kuwa na mawasilino bora kwani kichocheo kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania na kurahisisha shughuli zao za kijamaa na kiuchumi.


 “naamini mawasialiano haya yataweesha biashara katika wilaya hii kukua, na wakulima watanufaika na huduma mbalimbali za simu zitakazowawezesha kutafuta masoko ya bidhaa zao, kuangalia bei ya mazao, lakini pia watatumia huduma ya Airtel Money kwaajili ya kufanya malipo na manunuzi kwa njia ya simu. Nawaasa wakazi wa wilaya ya Nzega kutumia mawasiliano haya vyema na kuboresha maisha yao” aliongeza Ngupula


  Kwa upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa Tabora, Phidelis Lugangila  alisema “Airtel imejipanga kutoa huduma bora na za uhakika na kuwaomba wakazi wa kijiji cha Ngukumo na vijiji vya jirani kutumia huduma na bidhaa za Airtel kupata kipato  kupitia huduma zetu kama vile Airtel Money kwa kuwa mawakala na kupata kamisheni kila mwezi na vilevile kutengeneza ajira kwa vijana wengi.


Wakazi wa mwashala wanajishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi,pamba ,Karanga na Mpunga pamoja na ufugaji

AHMAD AHMAD AMBWAGA ISSA HAYOTOU UCHAGUZI WA CAF

$
0
0
Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) umemalizika kwa mgombea Ahmad Ahmad kutoka nchini Madagascar kupata kura 34 dhidi ya 20 za aliyekuwa rais wa zamani Issa Hayatou uliofanyika leo nchini Ethiopia. 

Uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa pande zote uliweza kuhitimishwa na wanachama washiriki kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kupiga kura za kumchagua ni nanai atakayeongoza shirikisho hilo kwa kipindi kijacho. 

Pamoja na uchaguzi huo, CAF wameweza kuipitisha Zanzibar kuwa mwanachama rasmi ambapo kwa sasa atakuwa mshiriki rasmi wa michuano ya kimataifa iliyo chini ya CAF pamoja na kuwa na timu ya Taifa inayojitegemea. 

Nchi takribani zote ziliweza kukubali kupatiwa kwa uanachama huo na nchi 51 kukubali na 3 kukataa ambazo ni Benini, Sychells na Madagascar.
Rais Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) Ahmad Ahmad kutoka nchini Madagascar

MARAIS WASTAAFU WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU SIR GEORGE KAHAMA

$
0
0
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Sir George Kaham, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamini Mkapa akiwafariji watoto wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Sir George Kaham, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
 Mjane wa Marehemu Sir Georeg Kahma, Mama Janeth Kahama akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa mumewe, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam leo.
 Waziri wa Habari Sanaa  Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

MICHUZI TV: HATMA YA KESI YA UCHAGUZI WA TANGANYIKA LAW SOCIETY

WAZIRI UMMY MWALIMU ATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA IRINGA

$
0
0
Hayo ameyasema wakati wa ziara ya kikazi mkoani Iringa leo tarehe ambapo ametembelea Kituo cha Damu Salama cha Mkoa pamoja na Hospitali ya wilaya ya Mafinga

“Pia naagiza Uongozi wa Hospitali zote za Mikoa na Wilaya kuanzisha Wodi za Watoto Wachanga na Watoto Njiti mara moja” alisema Mh. Ummy.

Mbali na hayo Waziri Ummy ameagiza kujengwa kwa Kitengo cha Wagonjwa wa Dharura (Emergency Unit) kwa hospitali hizo mara moja ili kuboresha huduma ya afya kwa wakazi wa Iringa.

Akitoa taarifa ya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa mbele ya Waziri wa Afya, mhe. Amina Masenza, mkuu wa Mkoa wa Iringa alieleza hatua mbalimbali wanazochukua katika kuboresha utoaji wa huduma ikiwemo kuboresha miundombinu ya vituo vya Afya, upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba, utoaji wa elimu ya uzazi wa mpango pamoja na lishe kwa wananchi bila kusahau kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF).

Hata hivyo, zipo changamoto kadhaa zinazowakabili mkoa kufikia lengo la lao kutoa huduma bora za Afya. Mathalani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Iringa haina wodi/kitengo cha dharura, upungufu wa watumishi, Ufinyu wa eneo la Hospitali, ukosefu wa Gari la Kubebea Wagonjwa na ukosefu wa baadhi ya vitendanishi.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu ameagiza kuanzishwa duka la Dawa ndani ya miezi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI MBABANE SWAZILAND LEO KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane – Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.

Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.

Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.

Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.

Imetolewa na 
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbabane – SWAZILAND.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikagua gwaride la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia vikundi vya Burudani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march,16, 2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasili Heshima kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Swaziland alipowasili kwenye Uwanja wa kimataifa wa Mfalme Mswati wa III mjini Mbabane Swaziland leo march 16,2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) ambapo Makamu wa Rais amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA WA DAWA NA VIFAA TIBA KUTOKA SERIKALI YA WATU WA CHINA

$
0
0
Mkurugenzi Bohari Kuu ya Dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad amesema upatikanaji wa huduma ya dawa muhimu katika wodi za wazazi umefikia asilimia 96 na wazazi wamekuwa wakipata huduma bila usumbufu.

Amesema Bohari Kuu ya dawa hivi sasa imeimarika na wamekuwa wakisambaza dawa hizo katika Hospitali na vituo vya Afya kwa wakati kwa mujibu ya mahitaji yao.

Mkurugenzi Zahrani ameeleza hayo Ofisini kwake Maruhubi baada ya Wizara ya Afya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba venye thamini ya zaidi ya shilingi milioni 420 kutoka Serikali ya Watu wa China.

Amesema kuimarika kwa huduma ya dawa na vifaa tiba, ni juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wafadhili wengine wa maendeleo katika kuwapunguzia wananchi umasikini.

“Bohari Kuu hivi sasa imejaa dawa na tumeboresha sana huduma katika wodi za wazazi hasa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja,” alisisitiza Ndugu Zahrani.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya dawa alisema wamekuwa wakifuatilia kwa karibu mazingira ya kuzihifadhi dawa hizo katika vituo vya Afya na kuhakikisha zinawafikia walengwa.

Alisema msaada uliotolewa na Serikali ya China, ikiwa ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi miezi mitatu, sehemu kubwa ni kwa ajili ya wagonjwa wa maradhi ya kuambukiza, sindikizo la damu na sukari ambapo hulazimika kuzitumia kwa muda mrefu na bei zake ni ghali.

Akimkabidhi Waziri wa Afya msaada huo, Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema nchi yake itaendeleza mashirikiano ya kihistoria yaliyoanzishwa na waasisi wa nchi mbili hizi Abeid Amani Karume na Maotse Tung kwa faida ya wananchi wake.

Ameahidi kuendelea kutoa mashirikiano zaidi katika uchumi wa Zanzibar kwa kuimarisha miundo mbinu na kusaidia vifaa tiba na dawa za aina mbali mbali.

Nae Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo aliishukuru China kwa misaada inayotoa kwa Zanzibar na hasa sekta ya afya ambayo imesaidia kuboresha upatikanaji wa huduma katika Hospitali na vituo vya afya.

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

GAPCO yatoa baiskeli kwa wanafunzi wenye ulemavu

$
0
0
GAPCO Tanzania ikishirikiana na Network 21 ya Afrika Kusini imetoa baiskeli kwa wanafunzi wenye ulemavu wa Shule ya Matumaini ya Jeshi la wokovu ikiwa ni sehemu ya mchango wa kampuni hiyo kwa jamii.

Akikabidhi msaada huo, Afisa Rasilimali Watu wa GAPCO, Chrispin Kayombo alisema waliguswa na mahitaji ya shule hiyo kwani wao pia ni sehemu ya jamii na wana jukumu la kusaidia hasa wale wenye mahitaji maalumu.

“Tumeshirikiana na Network 21 kuwasaidia hawa wanafunzi kufikia malengo yao kwani baiskeli hizi zitawasaidia kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo za kielimu. Ulemavu sio kushindwa na ndio maana tuko hapa leo kutoa msaada na kuwahimiza wasome kwa bidii,” alisema.

Alisema baiskeli nyingine zilikabidhiwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pugu wenye ulemavu. Mkurugenzi wa shule hiyo, Luteni Thomas Sinana aliishukuru GAPCO na Network 21 kwa msaada huo na kuomba makampuni mengine pia yajitokeze.

“Tumefarajika mno kupokea msaada huu inatia moyo sana kuona jinsi mnavyowakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii hususani wenye ulemavu. Kama mlivyoona, wanafunzi hawa wana mahitaji mengi kama chakula, madaftari, vitabu, kalamu, sare za shule na ndio maana natoa wito kwa makampuni mengine pia wajitokeze kutusaidia, alisema.

Alisema watu wenye ulemavu wakiwezeshwa wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika jamii kwani wana uwezo pia. Kaka mkuu wa shule hiyo, Ernest Timothy, aliishukuru GAPCO kwa msaada huo na kusema baiskeli hizo zitawasaidia mno katika masomo yao.

“Tumefarajika na kuguswa mno kuwaona hapa leo na kitendo cha kutukumbuka na kutuletea msaada huu kina maana kubwa sana kwetu ndio maana mnaona sote tuko hapa kusema asante,” alisema na kuomba makampuni megine yaige mfano huo wa GAPCO.
Afisa Rasilimali Watu wa GAPCO Tanzania, Chrispin Kayombo akitoa msaada wa baiskeli kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Matumaini ya Jeshi la Wokovu, Masoud Omary Babu ili kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu. Katikati ni Mkurugenzi wa shule hiyo, Luteni Thomas Sinana huku wanafunzi wakishuhudia.

TANGA UWASA INAHITAJI BILIONI 15 KUTEKELEZA MPANGO WA KUSAFISHA MAJITAKA

$
0
0
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka katika Jiji la Tanga (Tanga-Uwasa), linahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kwa ajili ya kutekeleza mpango wa kusafisha majitaka yaweze kutumika kwa shughulinyingine za kibinadamu ikiwemo kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumza katika semina kwa wanahabari Jijini hapa Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Injinia Joshua Mgeyekwa, alisema kutokana na kuzaliza kiasi cha mita za ujazo zipatazo 2,700, wameonelea wayasafishe kwa kujenga mfumo utakaosaidia maji hayo kutumika tena.Mgeyekwa alisema tayari wametenga eneo la Utofu kama sehemu itayokusanya maji taka ambayo kwa sasa kiasi cha asilimia 10 cha wateja wao maji wanayoyazalisha kupelekwa baharini hivyo mfumo huo utasaidia suala zima la uchafuzi wa mazingira.

“Tupo na mpango wa kuyatumia maji taka kwa shughuli nyingine kama kilimo cha mbogamboga, unaimani kwa kufanya hivyo tutaongeza kipato cha mtu mmoja moja…Lakini ili mpango huu uweze kutimia tunahitaji kiasi cha shilingi bilioni 15 hadi 20 kutekelezwa,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa mfumo wa kutumia majitaka kwa shughuli nyingine za kibinadamu umekuwa ukitumika katika nchi zilizoendelea kama China, Israel na kwingineko ambako teklonojia hiyo imeanza.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorra Killo akizungumza jambo wakati wa kikao hicho leo 
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu maadhimisho ya wiki ya Maji.

ALIKIBA, DIAMOND KUSHIRIKI PAMOJA NYIMBO YA KUHAMASISHA SERENGETI BOYS

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.



KUELEKEA fainali ya kombe la Mataifa Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 nchini Gabon, kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys inayoongozwa na Mwenyekiti Charles Hilal imeandaa wimbo wa pamoja utakaoimbwa na wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Naseebb Abdul ‘Diamond’ na Ali  Saleh ‘King Kiba' pamoja na wasanii wengine.



Wimbo huo wa pamoja ni maalum kwa ajili ya kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys itakayofanyika mwezi wa tano nchini Gabon ambapo zitapatikana nchi nne zitakazokwenda kombe dunia la vijana nchini India.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Charles Hilal amesema kuwa kwa pamoja wimbo utakaowahusisha wasanii wengine mbalimbali utakuwa na lengo kuu la kuhamasisha wananchi, wadau na wapenda michezo kuichangia timu hiyo ya vijana kwa lengo la kuisaidia malengo waliyokuwa wameyafikia ya kuipeleka timu hiyo kwenye fainali za kombe la Dunia nchini India.

Hilal amesema kuwa hatua hii ya kusaidia Serengeti Boys kutawajenga vijana hawa kufanya vizuri katika michuano ya mataifa Afrika kwa vijana ikiw ani pamoja na kupata kambi nje ya nchi na kuchgeza mechi kadhaa za kirafiki kutoka nchini jirani lakini hata hivyo bado wanafikria kutafuta mechi ya kirafiki itakayochezwa hapa hapa Jijini Dar es salaam ikiwa ni kwa ajili ya kuwaaga kuelekea nchini Gabon.

Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.

“Tayari wasanii Ali kiba na Diamond wameshakubali kurekodi nyimo hiyona wameahidi kufanya haraka kuingiza sauti kwenye ala ambazo tumeshawatumia na baadae wasanii wengine kama Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee nao wataweka sauti zao,"amesema Kitenge.

Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.

Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu, yumo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas, Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.

Pia, Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.



Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya Serengeti Boys kueleka kwnye kombe la Mataifa Afrika chini ya miaka 17 yatakayofanyika nchini Gabon. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas na Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano 

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa kwa Serengeti Boys , Charles Hilal akiwa pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge wakiwasikilizisha waandishi ala za wimbo unaotarajiwa kutumika kwa ajili ya kuhamasisha kuichangia Serengeti Boys.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMEBELEA ENEO LA UJENZI WA IKULU MPYA KIJIJINI CHAMWINO, DODOMA

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) wakati walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza wakati  Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea na wafanyakazi wa TBA  wakati wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitoa maelekezo  wakati alipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakikagua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa wakichanganya mchanga na saruji na kusaidia kufyatua matofali walipotembelea na  kukagua eneo linapojengwa Ikulu mpya kijijini Chamwino nje kidogo ya mji wa Dodoma leo Machi 16, 2017.

TANGAZO LA KUPOTEA KWA KIJANA ERICK RAPHAEL MSYALIHA ,ANATAFUTWA NA NDUGU ZAKE

$
0
0





Pichani ni Kijana anayefahamika kwa  jina la ERICK RAPHAEL MSYALIHA anayeishi Sinza-Mugabe ametoweka Ghafla Tarehe 13.03.2017 majira ya usiku alipochukuliwa na watu wasio famika akiwa mitaa ya  nyumbani kwake. Mpaka sasa hajarejea nyumbani, hivyo anatafutwa na ndugu zake, Tunaomba  yeyote atakayemuona au kupata Taarifa zake atujulishe kwa namba +255718105959 au atoe Taarifa katika Kituo cha Polisi kilicho jirani nae,Tunatanguliza Shukurani zetu

KIPINDI CHA BBC DIRA YA DUNIA

Msifungishe ndoa bila ya kuona vyeti vya kuzaliwa vya wahusika

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Katiba Na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe ameagiza kuwa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017  ndoa zote zifungwe baada ya wanaotaka kufunga kuwasilisha kwa vyeti vya kuzaliwa kwanza. 

Hivyo, amewataka wananchi wote wanaotarajia kufunga ndoa waanze kutafuta vyeti vya kuzaliwa mapema kwa sababu hawataweza kufunga ndoa kuanzia tarehe 1 Mei, 2017. 

Agizo hilo amelitoa kwa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) leo tarehe 16/3/2017 akiwa ziarani mkoani Morogoro kukagua utendaji wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria.

TANGAZO YA KIFO CHA MR. RAPHAEL FREDERICK MALIKA

$
0
0
Family ya Frederick Malika ya Kijitonyama Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao mpendwa Mr. Raphael Frederick Malika kilichotokea Jumanne Tarehe 14 March 2017 hospitali ya Muhimbili.  Habari ziwafike ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. 

RATIBA YA MAZISHI:
Jumamosi, 18 March 2017
•            Saa 7 Mchana – Misa Takatifu - St Albans Church, Dar es salaam City Center
•            Saa 8 Mchana - Heshima za mwisho kwa Marehemu -  St Albans Church, Dar es salaam City Center
•            Saa 9 mpaka Saa 10 Mchana - Safari ya kuelekea Makaburi ya Kinondoni - Shughuli za Mazishi kwenye Makaburi ya Kinondoni (Ndani) 

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, 
jina la Bwana lihimidiwe.
 AMEN!

www.wasafi.com mkombozi wa wanamuziki tanzania amewasili

$
0
0
Hii ndio namna ya kununua Nyimbo ya msanii umpendae kwenye @wasafidotcom com kwa Wateja wa @VodacomTanzania ...Hii ni kwa walioko Tanzania tu... walioko nchi zaa jirani ntawapostia soon maelezo yenu! kwa maelezo zaidi follow @Wasafidotcom

HBD THE LEGEND DJ JD!

RAIS WA TFF AREJEA, AZUNGUMZIA UCHAGUZI WA CAF

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
JOPO la viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limeingia mchana huu kutoka Addis Ababa, Ethiopia kulipokuwa na uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira barani Afrika (CAF) uliofanyika jana.
Katika uchaguzi huo mgombea Ahmad Ahmad kutoka nchini Madagascar alimuangusha aliyekuwa rais wa Shirikisho hilko Issa Hayotou kwa kipindi cha miaka 29 kwa kura 34 kwa 20.
Rais wa TFF, amesema kuwa uchaguzi ulikuwa ni wa haki na umeonyesha mabadiliko makubwa sana katika maendeleo ya soka barani Afrika na amewaahidi wwatashirikiana nae bega kwa bega.
Kabla ya kwenda Addis Ababa, Malinzi hakuweka wazi kuwa kura yake atampa nani kwani aliamini wote ni wazuri na wanafanya kazi zao kwa uweledi mkubwa.
Waziri wa michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (pili kulia) akiwa na viongozi wa Zanzibar Football Association (ZFA) mara baada ya Zanzibar kutangazwa kuwa mwanachama wa 55 wa CAF jijini Addis Ababa, Ethiopia 
Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wakiongozwa na Rais Jamali Malinzi (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Nchini kutokea Addis Ababa, Ethiopia kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwsili uwanja wa ndege kutoka Addis Ababa Ethiopia kulipokuwa na uchaguzi Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
  Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha soka cha Mpira (FAT) na mjumbe wa heshima wa  Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) Said El maamury  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwsili uwanja wa ndege kutoka Addis Ababa Ethiopia kulipokuwa na uchaguzi Shirikisho hilo.




MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YAFUNGWA RASMI MKOA WA MBEYA

$
0
0
Mhandisi Cosmas Kinasa akizungumza machache wakati akifunga rasmi semina ya ujasiriamali ya "Manjano Dream-Makers" kwa wanawake wa mkoa wa Mbeya akimwakilisha meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya. Mafunzo ya ujasiriamali hayo yametokewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya wiki mbili ya ujasiriamali, vipodozi na urembo kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya  wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana naMhandisi Cosmas Kisana Akizungumza Machache Wakati akifunga Rasmi Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Mbeya Kwa Niaba ya Meneja wa Sido Mkoa wa Mbeya.Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 30 kutoka Mkoa wa Mbeya  Yamemalizika. Wanawake 30 wa Mkoa wa Mbeya  ni Miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara Kutoka SIDO Mkoa wa Mbeya  wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo kama hayo yatafanyika pia kwenye mikoa ya Mtwara,Tabora na Kigoma mwaka huu wa 2017.
Washiriki walionufaika kwenye mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mhandisi Cosmas Kinasa. 
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru Mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

MSEMAJI WA JESHI LA POLISI NCHINI UGANDA AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

$
0
0
Msemaji na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kaweesi pamoja na walinzi wake wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya leo na watu wasiojulikana mita chache kutokea nyumbani kwake, Kulambiro jijini Kampala. Kikosi cha Usalama cha nchi hiyo kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Pichani ni Gari alitokuwa akiitumia  Msemaji na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Andrew Felix Kawees.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images