Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1613 | 1614 | (Page 1615) | 1616 | 1617 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo amesema kuwa fedha zinazotolewa na Benki ya Dunia kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa miji zinatakiwa kusimamiwa kwa umakini.

  Jaffo ameyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja katika eneo la Tuangoma jijini Dar es Salaam, amesema kuwa Temeke inakwenda kwa kasi katika utekelezaji wa mradi uboreshaji wa miji.

  Amesema kuwa baada ya miaka mitano jiji la Dar es Salaam itakuwa imebadilika kutokana na mradi wa uboreshaji miji na kuondokana na mafuriko ya mara kwa mara inayotokana na tatizo la miundombinu.

  Jaffo amesema wakandarasi wanaosimamia miradi lazima wafanye kazi kwa kufatilia ili miradi hii iweze kudumu kwa muda mrefu na sio kuwa miradi ambayo baada ya mwaka mmoja kukamilika na kuanza nyufa.

  Aliongeza kuwa watu ambao wanatakiwa kufidiwa atafatilia kwa mthamini mkuu wa serikali waweze kufidiwa ili mradi uende kwa kasi na Temeke iwe ya kwanza kuwa mji wa kisasa.

  Aidha amesema kwa kutokana na mradi huo uko chini ya ofisi yake atafatilia kwa ukaribu katika kuhakikisha jiji la Dar es Salaam linakuwa na ubora na maji mengine duniani.
  .Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akizungumza na watendaji wa Manispaa ya Temeke pamoja na wakandarasi wa mradi wa uboreshaji miji DMDP la Tuangoma leo alipofanya ziara katika maradi huo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  .Mkuu wa Wilaya ya Temeke , Felix Lyaniva akimpa maelezo Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo juu ya mradi wa Mji wa Temeke katika eneo la Tuangoma.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa manispaa ya Temeke na wakandarasi wa mradi DMDP.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais –Tamisemi Suleiman Jaffo akiwa katika picha pamoja na wakandarasi wa mradi wa DMDP leo.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Muonekano wa mradi katika mji waTuangoma leo 


  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akiongoza Kikao kazi cha Shirika la Uzalishaji mali la Magereza ambapo katika Kikao hicho cha siku mbili Wakuu wa miradi watapata fursa ya kuelezea maendeleo ya miradi mbalimbali ya shirika hilo. Kikao hicho kimeanza leo Machi 15, 2017 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga – Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wakuu wa miradi mbalimbali ya Shirika la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa katika Kikao kazi cha Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(hayupo pichani).
  Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akimkaribisha Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi katika ufunguzi wa Kikao kazi hicho.
  Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. David Mwangosi ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Shirika la Magereza (wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Miradi ya Shirika la Magereza(wa pili toka kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Edith Mallya (Picha zote na Jeshi la Magereza).


  0 0

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakemea vikali tukio la kubakwa kwa binti wa miaka saba (jina limehifadhiwa) mkazi wa kata ay Kitanzini, mwanafuzi wa darasa la awali shule ya SUN Academy iliyoko kata ya Kwakilosa, manispaa ya Iringa.

  Wizara imesikitishwa na taarifa za awali kuwa mtoto alibakwa katika mazingira ya shule mahali ambapo tunategemea pawe salama kwa mtoto kuishi. 

  Wakati wote Serikali imekuwa ikisisitiza walezi wa watoto kuhakikisha wanalinda watoto dhidi ya vitendo vyote vya ubakaji kwani vitendo hivi vimekuwa vikitaarifiwa kuwahusisha watu wa karibu wanaomzunguka mtoto katika familia, shuleni na jamii.

  Wizara inapongeza vyombo vya habari vyote vinavyoibua matukio ya ukatili, kwa kufanya hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambao utekelezaji wake unahusisha wadau wote nchini.

  Wizara inamini kuwa Polisi kwa kutumia weledi na umahiri wao watashirikiana na wananchi, walezi, walimu na marafiki wa mtoto, kuhakikisha kuwa watuhumiwa wanafichuliwa na kuchukuliwa hatua stahiki.

  Wizara inawakumbusha wazazi na walezi kuwa vitendo vya ukatili ukiwemo ubakaji dhidi ya watoto wa kike havikubaliki katika nchi yetu kwani vitendo hivyo vinatia doa kubwa taifa letu. Natoa rai kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika kuwafichua waliohusika na ubakaji wa mtoto aliyeripotiwa kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika, ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua stahiki.


  Erasto T. Ching’oro
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino Serikalini
  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

  0 0

  Mashindano ya kutafuta bingwa wa Taifa wa mchezo wa kuogelea yamepangwa kufanyika Aprili 7 na 8 kwenye bwawa la kuogelea la shule ya Heaven of Peace Academy (Hopac) iliyopo Kunduchi Mtongani.
  Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya timu 19 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na visiwani.

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alizitaja timu ambazo zinatarajia kushiriki kuwa ni Dar es Salaam Swimming Club, Taliss swimming club, Bluefins, JKT, Morogoro International School, Champions Rise, Braeburn International School na shule ya sekondari ya Makongo.

  Timu nyingine ni ISM Leopards, Arusha Swim Club, Mwanza Swim Club, Kennedy School Arusha, Stingrays Swim Club, Tanzania Marines, Hopac Swim Club, Genesis Swim Club, KMKM, Wahoo –IZS na Zanzibar Dolphins.
  Waogeleaji hao watashinda katika stali nne ambazo ni freestyle, backstroke, Individual Medley na breaststroke. Pia kutakuwa na mashindano ya ‘relay’ ambayo yatashirikisha waogeleaji wa kike na wa kiume.

  “Tunatarajia kuwa na mashindano myenye ushindani mkubwa kutokana na maandalizi ya kila timu, mchezo unakuwa na timu zinazidi kuongezeka, kwa kifupi kuna mwamko mkubwa sana katika mchezo, tunawaomba wadhamini wajitokeze kutusaidia,” alisema Namkoveka.

  Alisema kuwa kwa sasa wapo katika maandalizi ya kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha kimataifa na kwa kutumia sheria za shirikisho la mchezo huo duniani, Fina.

  “Mashindano yatakuwa ya umri, kutakuwa na umri kati ya miaka 9 -10, 11-12, 13-14, 15-16 ba zaidi ya 17, hakuna muogeleaji atakayeruhusiwa kushiriki katika shindano zaidi ya moja, viongozi wote wa timu watanakiwa kufika kwenye mkutano utakaofanyika Hopac kabla ya mashindano kuanza, mkutano huo utaendeshwa na kamati ya ufundi,” alisema.
  Wogeleaji wakishindana katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.
  Peter Itatiro ‘akikata’ maji katika mashindano yaliyopita ya kuogelea.

  0 0

  TFF YAGONGA MWAMBA TRA, OFISI ZAENDELEA KUFUNGWA


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeendelea kuwa katika sintofahamu baada ya ofisi zake kufungwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) baada ya kuwa na malimbikizo ya mda mrefu.

  Maofisa hao kutoka kampuni ya YONO Auction Mart walipewa mamlaka na TRA ya kufungia ofisi hizo za TFF huku wakiwambia hawaruhusiwi kuendelea na kazi mpaka pale watakapomalizana na TRA.

  Kwa mujibu wa deni hilo, TFF wanadaiwa deni la nyuma ambalo lilikuwa chini ya uongozi wa Leodigar Tenga ikiwemo kodi ya aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Marcio Maximo na kodi ya mechi ya Taifa Stars na Brazil.

  Katika sakata hilo ambapo timu ya Serengeti Boys ipo kambini ndani ya Shirikisho hilo, wameendelea kusalia lakini wamepewa masharti ya kutokutumia uwanja huo kwa mazoezi mpaka pale watakapomalizana na TRA.

  Baadhi ya viongozi wa TFF walijaribu kwenda ofisi za TRA mkoa wa Ilala kujua ni jinsi gani wanalimaliza sakata hilo liligonga mwamba na kushindwa namna ya kujikwamua kwenye adha hiyo.
   Maofisa wa Yono Auction wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TFF wakiwapa maelezo ya kutokuendelea kuwepo ndani ya viunga vya ofisi hizo
   Ofisi za TFF zikiwa zimefungwa.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali,wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa jiji la Dar,viongozi wa Dini mbalimbali,Wasaniii na vijana kutoka vituo mbalimbali vya matibabu ya dawa za kulevya walijitokeza kumsikiliza RC Paul Makonda ambaye leo alikuwa anatimiza mwaka wake mmoja wa Uongozi tangu aapishwe na Rais wa awamu ya tano,Dkt John Pombe Magufuli.
  Baadhi ya waathirika wa Madawa ya Kulevya wapato zaidi ya 1500 kutoka vituo mbalimbali vinavyotoa matibabu ya Dawa za kulevya,wakiwa ndani ya bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokuwa akizungumza nao mambo mbalimbali,ya kimaendeleo pamoja na kupewa elimu mbalimbali ihusuyo dawa za kulevya.RC Makonda leo anatimiza mwaka mmoja tangu aapishwe kuwa mkuu wa mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,
  Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini,walialikwa kwenye hafla hiyo fupi ya kutimiza mwaka mmoja kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar,Paul Makonda
  Pichani ni baadhi ya wasanii walioshiriki na kutoa neno katika hafla hiyo,wasanii hao ni TID,Diamond Paltnumz,Harmonize,Banana Zorro,Mrisho Mpoto na wengineo ambao walijitokeza kumuunga mkono RC Makonda katika suala zima la kupambana na Dawa 
  za kulevya.
  Vijana waliothiriwa na Madawa ya kulevya ambao kwa sasa wameahidi kuacha kutumia wakiwa wameandika bango lao la kumshukuru RC Makonda kwa kazi yake nzuri aifanyayo ya kupambana na Dawa za Kulevya.
  Vijana mbalimbali walikokuwa wakitumia dawa za kulevya wakimshukuru RC Makonda kwa juhudi zake kubwa za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokea ndani ya jiji la Dar kwa namna moja ama nyingine
   

  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye (pichani) amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano ya Rais, Ikulu, 
   na Idara ya Habari MAELEZO kwa ubunifu na weledi wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa kutumia teknolojia mbalimbali za habari na mawasiliano.
  Waziri Nape alisema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili Maafisa Mawasiliano wa Serikali wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali ,amewataka kuwa wabunifu kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano hasa mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nafuu na rahisi.  
  “Nawapongeza sana wakurugenzi vijana Dkt. Hassan Abbasi wa MAELEZO na Greyson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu  wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa”alisema Waziri Nape.
  Waziri Nape aliongeza kuwa pamoja na ubunifu wao katika mitandao ya kijamii, utayarishaji wa makala za Serikali na kujibu hoja kwa haraka kupitia taarifa kwa umma,  wameweza pia kubuni vipindi vya TUNATEKELEZA na SAFARI YA DODOMA ikiwa ni mkakati wa kusukuma mbele ajenda za Serikali.
  Aidha, Waziri Nape amewataka Maafisa Mawasiliano kutumia fursa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari binafsi  kupitia vipindi vya bure kwenye Televisheni, redio na magazeti  kuhakikisha mambo mazuri yanayotekelezwa na Serikali yanatangazwa na kuweza kusikika kwa Wananchi.
  “Nimezungumzia hoja na haja ya mabadiliko kiutendaji, lakini nikiwa kiongozi ambaye pia katika maisha yangu nimefanya kazi ya kuongoza kitengo cha habari na uenezi nafahamu changamoto zinazoikabili kada hii,lakini unaweza ukageuza changamoto kuwa fursa,kwahiyo tujiongeze ndugu zangu ” alisema Waziri Nape. 
   Waziri Nape alitoa wito kwa Makatibu Wakuu, Wakurugenzi,Wakuu wa Taasisi pamoja na watendaji wakuu katika ofisi za umma kuhakikisha wanatenga fedha katika bajeti kwaajili ya kununua vifaa vya kutendea kazi ili kuviwezesha vitengo vya Mawasiliano Serikalini kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na ufanisi katika kuisemea Serikali.
  6

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Machi 15, 2017  0 0

   Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed na Nafue Nyange wameamua kufungua shule ya urembo watakayokuwa wakitoa elimu kwa njia ya mtandao. Akizungumza jijini Dar es Salaam Nargis alisema kuwa wameamua kuandaa mafunzo hayo maalum katika fani ya urembo ili kuweza kuwawezesha wanawake na vijana waweze kujikwamua kiuchumi. 

  Nargis aliongeza kuwa mafunzo hayo maalum yamewalenga watu wote na wanaweza kuyapata kidigitali, ikiwemo kwa njia ya simu au mtandao kwa gharama ya shilingi elfu kumi (10,000) tu za Kitanzania kwa mwezi. "Mafunzo hayo hayachagui jinsia; nia yetu kubwa sisi ni kuwawezesha wenzetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujiinua kiuchumi kama wajasiliamali na kujijenga kimaisha sambamba na mpango wa serikali yetu kujenga ajira na kujikwamua kutoka kwenye umaskini," alisema Nargis.

   Kwa upande wake Nafue Nyange aliongeza kuwa mafunzo hayo yanapatikana kwa bei nafuu kabisa kupitia tovuti ya www.glammadamlive.com
  Pia anawaomba watanzania wasajili wataweza kufanya malipo kupitia Vodacom M-pesa na Tigo Pesa. Kwa wale walio nje ya nchi wanaweza kutumia kadi tofauti kama VISA, MasterCard, American Express.
  Miss Tanzania 2014, Nargis Mohamed (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo nia yao ya kuanzisha darasa la urembo la kidigitali. Pembeni ni Mjasiliamali Nafue Nyange. 
  Mjasiliamali Nafue Nyange akisisitiza jambo. 


  0 0


  0 0  0 0

  Daktariwa Kinywa na Meno Hospitali ya Sinza Dar es Salaam, Idd Khery akimfanyia matibabu ya Kinywa na Meno mwanafunzi wa Darasa la 3 Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija, Rajabu Yahaya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga leo kuelekea Wiki ya Kinywa na Meno ambapo watoto 53 jana na leo wamepatiwa huduma hiyo bila malipo, (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
  Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya (wa pili kulia) akifunga Wiki ya Kinywa na Meno Mkoani humo katika Shule ya Msingi ya Wanafunzi Jumuishi ya Buhangija Mkoani Shinyanga leo, kuanzia kushoto ni Dkt. Anold Gemoniani kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kishapu, Mwalimu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Profesa Bakari Lembariti ,Daktari Bingwa wa Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa na Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro
  Rais wa Chama Cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dkt. Lorna Carneiro (wa pili kushoto) akimtambulisha Dkt, Arnold Mtenga wakwanza kushoto kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwanamsiu Dossi (kulia) mara alipoongozana na ujumbe wake kwa lengo la kumuaga baada ya kumaliza matibabu katika Kituo cha watoto Buhangija, wa tatu kushoto ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu mara baada ya kuwasili ofisini kwake.

  Na: Sylvester Raphael
  Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na  utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii.

  Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa nchini Tanzania (IOM, UNICEF na UNDP) aliwasili Mkoani Kagera Machi 13, 2017 na ujumbe wake ili kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo na Kijamii inayofadhiliwa na Umoja huo katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.

  Miradi aliyoitembelea Bw. Rodriguez ni pamoja na mradi wa ujenzi wa vyoo, madarasa,  mabweni na jengo la utawala katika shule ya Msingi Mgeza Mseto Manispaa ya Bukoba ambapo mara baada ya kukamilika mradi utagharimu Dola za Kimarekani (318,000 USD) ambapo ujenzi wa vyoo umekamilika, madarasa mabweni na jengo la Utawala ujenzi upo katika hatua ya msingi.
  Bw. Rodriguez akiongea na wanafunzi, walimu na wananchi waliofika kumpokea katika shule hiyo alisema kuwa amefurahishwa kufika katika shule hiyo na kujionea hali halisi ya watoto wenye ulemavu wa albinizimu na walemavu wengine aidha, alisema kuwa Umoja wa Mataifa uliamua kutoa fedha hizo ili kurejesha miundombinu ya shule hiyo baada ya kuharibiwa na Tetemeko la Ardhi lilitokea Septemba 10, 2016.

  “Nilipokuwa Dar es Salaam niliambiwa na Waziri Profesa Joyce Ndalichako kuwa nikifika Kagera nitembelee Shule ya Msingi Mugeza Mseto pia nilipofika Kagera Mkuu wa Mkoa ameniambia nitembelee shule hii sasa nimejionea na kujua ni kwanini walinisistiza, shule inahitaji msaada mkubwa. Aidha, Umoja wa Mataifa unapenda kusaidia lakini Tanzania shule  za namna hii zipo nyingi na ndiyo maana tunasaidia kidogo kidogo ili kuongeza mahitaji muhimu.” Alisistiza Bw. Rodriguez.


  0 0

  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  leo imevitembelea vituo vya utangazaji vya CLOUDS MEDIA GROUP, ikiwa katika ziara ya kawaida ya kuvitembelea vituo vya utangazaji nchini katika kutoa elimu ya uboreshaji wa maudhui ya utangazaji nchini. 
  Pichani kushoto ni Ruge Matahaba, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Maudhui ambao ni Mwenyekiti Valerie Msoka,  Joseph Mapunda, Abdul Ngalawa. Derek Murusuri   Zainabu Mwatawala.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa (RC) wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana amezikumbusha taasisi za elimu ya juu nchini kuhakikisha zinaongeza uwezo wa madawati ya mikopo yaliyopo katika taasisi zao ili yaweze kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kutatua changamoto za utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

  Mkuu wa Mkoa huyo ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 17, 2017) wakati akifungua mkutano wa kazi wa siku mbili kati ya watendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na maafisa mikopo zaidi ya 100 kutoka taasisi za elimu ya juu nchini wanaokutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Baadhi washiriki wa mkutano wa kazi kati ya HESLB na maafisa wasimamizi wa madawati ya mikopo ya elimu ya juu kutoka taasisi za elimu ya juu wakiwa katika picha ya pamoja mjini Dodoma leo (Alhamisi, Machi 16, 2017).

  “Majukumu ya Bodi ni mazito na hivyo Bodi inahitaji ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wadau mbalimbali mkiwemo nyie maafisa mikopo mliopo vyuoni na mnaokutana na wanafunzi kila siku,” amesema Rugimbana katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi (Elimu) wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Gosbert Damazo.

  Akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema Bodi yake inatambua mchango mkubwa unaotolewa na maafisa mikopo hao katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu waliopo katika taasisi mbalimbali.

  “Maafisa hawa ndio wanaotuunganisha na wanafunzi katika utendaji kazi wetu wa kila siku, hivyo ni watu muhimu sana kwetu na tunathamini sana mchango wao na wa taasisi zao kwa ujumla,” amesema Bw. Badru.
  Afisa Tawala Msaidizi (Elimu) wa Mkoa wa Dodoma Bw. Gosbert Damazo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kazi wa siku ya mbili kati ya HESLB na maafisa wasimamizi wa madawati ya mikopo ya elimu ya juu kutoka taasisi za elimu ya juu mjini Dodoma leo.

  Kwa mujibu wa Bw. Badru, Bodi yake itatumia mkutano huo wa siku mbili kuwakumbusha maafisa hao wajibu wao katika kutunza kumbukumbu muhimu za wanufaika wa mikopo na majukumu yao muhimu ili kuongeza ufanisi na hivyo kupunguza malalamiko ya wadau wakiwemo wanafunzi wanaoufaika wa mikopo ya elimu ya juu.

  Aidha, Mkurugenzi Mtendaji huyo alikumbusha kuwa mwaka 2011, Serikali ilivielekeza vyuo vyote vya elimu ya juu nchini kuanzisha madawati ya mikopo ya elimu ya juu ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali.

  “Tangu wakati huo (2011), kumekuwa na mafanikio makubwa katika utendaji wetu kutokana na kuongezeka kwa ufanisi. Hivi sasa, malalamiko kutoka kwa wanafunzi yamepungua sana kwa kuwa wana sehemu ya kuwasilisha hoja zao palepale chuoni …wito wangu kwao ni kuwa wayatumie madawati haya vizuri,” amesema Bw. Badru.
  Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru akiongea katika mkutano kazi wa siku ya mbili kati ya HESLB na maafisa wasimamizi wa madawati ya mikopo ya elimu ya juu kutoka taasisi za elimu ya juu mjini Dodoma leo.

  Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Taaluma) Prof. Lawrence Msoffe, ambaye alihudhuria hafla ya ufunguzi, amesema mkutano huo ni muhimu kwa kuwa utaisaidia Bodi kupata mrejesho kutoka kwa maafisa hao ambao ndio wanaosimamia masuala ya utoaji mikopo katika vyuo kila siku.

  HESLB ilianzishwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili, pamoja na mambo mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watanzania wasio na uwezo na pia kukusanya mikopo iliyoiva iliyotolewa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.

  0 0

  Serikali imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi. 

  Aidha viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana. Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda mkoani Simiyu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa huo pamoja na tovuti ya Mkoa. 

  Prof. Mkenda amewasihi viongozi wote wa serikali ngazi za mikoa na wilaya nchini kujivunia uwepo wa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa ambao ni wazawa kwani wao ni chachu ya kuongeza kwa ajira za vijana. 

  Amesema kuwa si vyema wafanyabishara kutukanwa, kutolewa lugha zisizokuwa sahihi na kuonekana kama wana uadui na serikali, na badala yake watukuzwe ili kuweza kulipa kodi pamoja na kufuata sheria na taratibu za nchi. 

  “hawa wafanyabishara hasa wazawa na wajasiriamali tuwaone kama wenzetu, ndugu zetu na watu muhimu, kwani wameajiri vijana wetu, wanalipa kodi ili nchi ipate maendeleo, lakini wanatekeleza kauli mbiu ya Rais, Tanzania kuwa nchi ya viwanda, tuwathamni” alisema Prof.Mkenda. Katibu Mkuu huyo amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga maeneo kwa ajili ya wawekezaji wakubwa na wadogo kwa ajili ya kujenga viwanda. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (anayetazama kamera) akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu nje ya ukumbi wa Kanisa Katoliki Bariadi wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili kwenye sherehe za uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji na tovuti ya mkoa wa Simiyu.(Picha zote na Thebeauty).
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani humo ulioratibiwa na ESRF chini ya ufadhili wa UNDP. Mgeni rasmi Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye sherehe ya uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji mkoani Simiyu ulioenda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya mkoa wa Simiyu.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mholanzi Hans Van De Pluijm yuko mbioni kujiunga na timu ya Singinda United ambayo imepanda ligi kuu msimu ujao ikiwa ni katika kukiboresha kikosi hicho.

  Timu hiyo kwa sasa ipo chini ya mwenyekiti wa kamati ya Usajili Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba ambaye amedhamiria kufanya usajili utakaokuwa na tija.

  Mwenyekiti huyo ambaye ni  mshabiki wa Yanga na alionesha dhahiri kutaka kuendelea kuwapo kwa Mholanzi huyo katika kikosi cha Yanga lakini ilishindikana na tayari ameshavunjiwa mkataba na wanajangwani.

  Uwamuzi wa Pluijm kwenda Singida ni moja ya mikakati ya Mwenyekiti huyo wa kamati ya usajili ambaye ameweka nia ya kufanya usajili wa nguvu utakaowashangaza watu wote na sio kuletewa wachezaji watakaokuwa hawana msaada na timu.

  Pluijm alikaririwa akisema kuwa atasaini katika klabu moja wapo ya ligi kuu nchini hivi karibuni lakini sio Simba kwahiyo hatma yake itajulikana hivi punde tu wapi atakapoelekea mholanzi huyo na tayari ameshaonekana katika picha ya pamoja na kiungo wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe aliyesajiliwa hivi karibuni.
  Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo wa kimataifa Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn FC kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni usajili wa awali.

  Kutinyu anayecheza ligi ya Zimbabwe atajiunga na Singida United wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi June mwaka huu.

  0 0

  Kituo namba moja kwa vijana East Africa Television (EATV) Limited kikishirikiana na Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA foundation) kinapenda kutoa shukrani za dhati, kwa umma wa watanzania  kwa  kufanikisha kuchangia kwenye kampeni ya Namthamini.

  Namthamini  ni kampeni iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa wanafunzi  wa Sekondari, kutokana na takwimu kuonesha karibia asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

  Kwa wastani wanafunzi wa kike wengi hupoteza siku tano hadi saba kila mwezi kutokana na ukosefu wa pedi za kujisitiri, na kwa mwaka inakadiriwa kukosa masomo kwa takribani siku 60 hadi 70.

  EATV na East Africa Radio katika kufikisha mchango wake kwa jamii, na kwa kuangalia Siku ya Wanawake Duniani, Machi mosi tuliamua kuanzisha kampeni hii kwa kuishirikisha jamii ili kumuwezesha mwanafunzi wa kike asikose masomo yake na kumfanya kutofikia lengo lake kimasomo kwa kukosa pedi pale awapo kwenye hedhi.

  EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673 kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.

  Katika kampeni hii ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonyesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.
  Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akizungumza mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusua mafanikio yaliyopatikana kupitia kampeni ya 'NAMTHAMINI',Basilisa amebainisha kuwa kupitia EATV na East Africa Radio pamoja na Taasisi ya Haki za Wanawake (Hawa Foundation) imefanikiwa kukusanya michango ya fedha taslim na pakiti za pedi zitakazowawezesha takribani wanafunzi wa kike wapatao 673 kutokukosa masomo yao kwa muda wa mwaka mzima.Pichani kulia ni Mratibu wa Vipindi Eastafrika Radio,Irene Tillya na kushoto ni Mratibu wa Vipindi EATV,Sophie Proches.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo kuhusiana na mafanikio makubwa waliyoyapata kupitia kampeni hiyo ya 'NAMTHAMINI',Kiria emesema kuwa Katika kampeni hiyo ambayo wananchi walijitokeza kuichangia katika kuonesha kumjali mtoto wa kike aliyepo shuleni zilichangwa jumla ya shilingi 20,176,110, ambazo fedha taslim shilingi 11,774,610 na pedi za thamani ya shilingi 8,401,500.
   Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko akifafanua zaidi mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),kuhusiana na mafanikio ya kampeni hiyo 'Namthamini',iliyolenga katika kuchangia pedi (Taulo za Kike) kwa wanafunzi wa Sekondari,ambapo takwimu zinaeleza kuwa karibia asilimia 45 ya wanafunzi wa kike hukosa masomo wakiwa katika hedhi kutokana na kukosa pedi za kujistiri.
   Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika mapema leo jijini Dar.


  0 0

  KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya mwenyekiti wake Alex Msama, limeanza kutaja waimbaji wa nyimbo za injili watakaoshambulia ‘tamasha la mwaka huu.

  Mwimbaji wa kwanza kutajwa na Kamati hiyo katika mkutano wake na waandishi habari jijinin Dar es Salaam leo , ni Jesca Honole maarufu kama ‘Jesca BM.’

  Msama amesema leo kwamba, mwimbaji huyo amepata bahati ya kipekee ya kuwa wa kwanza na kwamba wengine watawekwa hadharani baada ya kupitishwa rasmi na Kamati.“Tunamshukuru Mungu kwa sababu maandalizi ya Tamasha letu la Pasaka ambalo safari hii linakuja kitofauti zaidi, waimbaji wameanza kupitishwa, ikiwa ni hatua nzuri ya tukio hili la kimataifa,” alisema Msama na kuongeza.

  ‘Mwimbaji aliyebahatika kuwa wa kwanza kuthibitishwa ni Jesca Honoli maarufu kama ‘Jesca BM’, mmoja wa waimbaji mahiri kwa sasa.Alisema nguvu ya kuanza kutangaza waimbaji watakaohudumu katika Tamasha hilo litakaloanzia Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 16, ni baada ya kupata kibali rasmi cha tukio hilo.

  Kuhusu kibali, Msama ametoa shukrani kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kutoa baraka kwa tukio hilo la kimataifa ambalo litatikisa katika mikoa ipatayo mitano ya Tanzania bara.Alisema, baada ya Tamasha hilo kuzindiliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, litahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma kabla ya kutua katika mikoa mingine mitatu.

  Alisema mbali ya Tamasha hilo kubeba malengo yake ya msingi yakiwamo ya kueneza neno la Mungu na kutumia sehemu ya mapato kufariji makundi maalumu, safari hii litatumika kama jukwaa la kumuombea nch Rais John Pombe Magufuli na nchi kwa ujumla.

  Manufaa mengine ya Tamasha hilo linalofanyika tangu mwaka 2000, ni kuweza kukuza muziki wa injili kiasi cha kuwa ajira kwa vijana wenye vipaji.
  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo jambo kwa kina mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar leo kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 16 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili.
  Muimbaji wa nyimbo za Injili Jesca Honole maarufu kama ‘Jesca BM.’ambaye amechomoza katika tamasha la Pasaka,akionesha uwezo wake wa kuimba na kupiga kinanda kwenye moha ya maonesho yake

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiongea na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mashirika ya DAWASA na DAWASCO pamoja na Waandishishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yanayoanza leo tarehe 16 hadi kilele chake 22 Machi, 2017 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) Bw. Kiula Kingu akijibu baadhi ya maswali toka kwa Waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yanayoanza leo tarehe 16 hadi kilele chake 22 Machi, 2017 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Meneja Mahusiano ya Jamii Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bi. Neli Msuya akifafanua baadhi ya hoja na kujibu maswali toka kwa Waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yanayoanza leo tarehe 16 hadi kilele chake 22 Machi, 2017 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari pamoja na Watendaji toka Mashirika ya DAWASA na DAWASCO wakifuatilia taarifa mbalimbali toka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda pamoja na Watendaji wa DAWASA na DAWASACO kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani yanayoanza leo tarehe 16 hadi kilele chake tarehe 22 Machi, 2017 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)

older | 1 | .... | 1613 | 1614 | (Page 1615) | 1616 | 1617 | .... | 3272 | newer