Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

Filam ya Kiumeni kuanza kuonyeshwa kesho katika ukumbi wa sinema wa Mlimani City

0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Filamu ya Kitanzania ya Kiumeni chini ya Muigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Ernest Napoleon itaonyeshwa kwa mara ya kwanza Jumatano hii katika ukumbi wa sinema wa Mlimani City Century Cinemax Jijini Dar es salaam.

Filamu hiyo ambayo imeandaliwa kwa kipindi cha miezi mitatu na kugharimu zaidi ya sh. milioni 50 imewakutanisha waigizaji kama Muhogo Mchungu, Irene Paul, Idris Sultan, Ernest Napoleon pamoja na waigizaji wengi wachanga ambao walionyesha uwezo mkubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Century Cinemax, Mlimani City Jijini Dar es salaam muda mchache baada ya waandishi kuonyeshwa filamu hiyo, Ernest Napoleon alisema filamu hiyo ni filamu ambayo itawafanya watanzania na wapenzi wa filamu nchini kupenda filamu zao kutokana ubora wa filamu hiyo.

“Kesho ni siku ambayo filamu yetu ya Kiumeni ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu itaonyeshwa kwa mara ya kwanza hapa Century Cinemax, Mlimani City. Kuanzia saa 12 jioni watu wataanza kupata picha za red carpet na saa mbili usiku filamu itaanza kuonyeshwa. Kwahiyo ni filamu ambayo tumeigizia uswazi kabisa, stori ni nzuri hata baadhi ya vijana ambao wameonekana tumewatoa huko huko mtaani na wengine hawakuwai hata kuigiza lakini wameonyesha uwezo mkubwa,” alisema Napoleon.

Aliongeza,”Filamu ni nzuri na ina ubora ndio maana hata hapa Century Cinemax tunaendelea kupewa nafasi, mara ya kwanza wakati tunazindua filamu ya Going Bongo tulipewa siku tatu za kuionyesha lakini baada ya kuona watu wanapenda wakatuongezea wiki na baadaye wiki mbili kwa maana ikaonyeshwa kwa wiki mbili. Filamu ya Kiumeni ilivyowafuata tu wakaniambia itaonyeshwa kwa wiki mbili. Kwa hiyo hiyo ni dalili nzuri kwa filamu zetu kwa sababu tulianza hawatuamini mpaka sasa wanatuamini,”

Pia alisema baada ya uzinduzi wa Tanzania ataenda kufanya uzinduzi nchini Kenya na baada ya hapo itaachiwa kwenye mfumo wa DVD ili iweze kupatikana nchini kote.

MJENGONI BENDI KUFANYA UZINDUZI RASMI MARCH 3 KATIKA UKUMBI WA TRIPLE A SPORT BAR

0
0
Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mjengoni classic band inatarajia kufanya utambulisho wao rasmi kwa mara ya kwanza mapema march 3 katika ukumbi wa Triple A spot bar uliopo ndani ya jiji la Arusha

Akiongea na waandishi wa habari Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital) alisema kuwa pamoja kuwa bendi hiyo imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi katika siku hiyo ya alyamisi.

Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na wanamuziki wa bandi ya mjengoni

Kwa upande wake mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdeme alisema kuwa bendi yake imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.

Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya jirani kuhuthuria onyesho hilo kwani bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.

Alisema kuwa bendi hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa mbili usiku adi majogoo ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha

wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu

Rais wa bendi ya mjengono Robert Mukongya (Digital) akiwa anaimba ndani ya jukwaa .Habari picha na Woinde Shizza,Arusha  

MAKAMU WA RAIS APOKEA TAARIFA YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA UAMUZI WA KUHAMIA DODOMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma uhakikishe unaondoa vitendo vya ukiritimba kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambavyo vinaweza kusababisha ucheleweshaji au kukwamisha ujenzi wa miji mipya mikubwa mitano ya kisasa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 14-Mar-2017 wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kupokea taarifa ya Kikosi Kazi kilichoundwa na serikali kwa ajili ya kuratibu shughuli mbalimbali za Serikali kuhamia Dodoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma kujiimarisha na kujipanga ipasavyo katika kupokea wawekezaji wenye nia njema ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali mkoani humo hasa wakati huu ambao serikali inahamia Dodoma.

Ameonya kuwa wawekezaji matapeli kamwe wasipewe nafasi ya kuwekeza Dodoma na ametaka uongozi wa mkoa wa Dodoma kuwa makini makundi hayo ili wasije kuvuruga mipango ya serikali ya kujenga Makao makuu ya kisasa katika Manispaa ya Dodoma.

Makamu wa Rais pia ameuagiza uongozi wa mkoa wa Dodoma kulinda na kuendeleza maeneo yote yenye uoto wa asili ili yasije yakaharibiwa kutokana na uwekezaji utakaofanyika mkoani humo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi na Wadau wa mkoa wa Dodoma kwenye mkutano wa kazi ambapo Taarifa ya Awali ya mkoa wa Dodoma na utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma iliwasilishwa katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
ZXCCC


MAKAMU WA PILI WA RAIS BALOZI SEIF ALI IDDI ATAHADHARISHA WANANCHI UPATIKANAJI WA MAFUTA ISIWE SABABU YA KUBWETEKA

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha Wananchi kwamba itakapofikia hatua ya kupatikana kwa rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Visiwani Zanzibar isijekuwa chanzo cha sababu ya Wananchi kubweteka na mradi huo kwa kuacha shughuli zao za Kiuchumi ambazo huwapatia riziki zao za kila siku.

Alisema Rasilmali hiyo endapo itapatikana kufuatia utafiti unaoanza kufanywa hivi sasa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto nyingi zinazoikabili Serikali Kuu pamoja na Wananchi kwa ujumla.Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa Ndege itakayofanya Utafiti na hatimae uchimbaji wa Rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume nje kidogo ya Kusini ya Mji wa Zanzibar.

Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika yaliyoanza kuzalisha miradi hiyo kwa matumaini makubwa ya kuimarisha Uchumi wao lakini hivi sasa zimekuwa na changamoto zaidi za Kiuchumi hali ambayo Zanzibar na Wananchi wake wanapaswa kuwa makini na
kujifunza matukio hayo.

Hata hivyo Balozi Seif alisema safari ya Zanzibar kuelekea kwenye uchumi Mkuu imeanza mara baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitisha Mswaada wa kuanzisha sheria inayoiruhusu Zanzibar kutafuta na kuchimba mafuta yake yenyewe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braza la Mainduzi kusaini Sheria hiyo.

Alisema busara za Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete za kusimamia utaratibu wa kupelekwa mswada Bungeni zimepelekea suala la mafuta na Gesi Asilia hivi sasa kutoka katika mambo ya Muungano.

Msimamizi wa Kampuni itakayofanya Utafiti waUtafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Bell Geospace  Inteprises Limited Bwana Stephane Kunar kushoto akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi Kulia nanma ndege Maalum itakavyofanya utafiti huo katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar. Kati kati ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira  mhg. Salama Aboud Talib, wa nyuma yake ni Katibu Mkuu wake Nd. Ali Khalil Mirza na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mhmoud.

  Balozi Seif akiangalia baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyochunguza maeneo yenye daliliza uwepo wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.
 Balozi Seif  akijaribu kugusa vifaa vitakavyotumika katika kazi kufanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia sehemu zenye dalili ya uwepo wa Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
 Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

PROF. MUHONGO AZINDUA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA PWANI.

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa Tatu kushoto), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kulia), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kulia), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga (wa kwanza kushoto) wakifunua Jiwe la Msingi kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.


Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga.


Watendaji kutoka kampuni ya Steg International Services wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani. Kampuni hiyo itatekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo wa Awamu ya Tatu.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye fulana ya Bluu) na Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakifukia nguzo ya umeme kwa udongo ikiwa ni ishara ya kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani.

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Salum Inegeja (wa kwanza kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Mashariki, Julius Sarota (wa pili kushoto) wakifuatilia shughuli ya uzinduzi wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini, Awamu ya Tatu katika mkoa wa Pwani.

Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo,  amezindua mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.

Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.

Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni  kampuni ya Steg International Services.

Kupata taarifa zaidi BOFYA HAPA

MWENYEKITI WA CCM DKT MAGUFULI AFUNGA SEMINA YA WATENDAJI, WENYEVITI NA MAKATIBU WA WILAYA NA MIKOA MJINI DODOMA LEO

0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa wakati wa kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli  wakati akifunga kufunga semina ya watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa  katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.

  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na watendaji, Wenyeviti na Makatibu wa CCM wa Wilaya na Mikoa baada ya kufunga semina yao katika ukumbi w White House mjini Dodoma leo Machi 14, 2017.

PICHA NA IKULU

NAPE KUWACHONGEA VIONGOZI WANAOKALIA TAARIFA

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema  kuna athari kubwa za kutotoa taarifa muhimu na za wazi zinazohitajika na wananchi hivyo kuwanyima haki ya kujua utendaji wa Serikali.

Waziri Nape alisema kwa sasa utoaji wa habari na taarifa za Serikali kwa umma si utashi tena wa Afisa Habari au kiongozi wa Ofisi ya Umma bali ni matakwa ya kisheria ambayo yamewekewa kanuni na misingi katika Sheria za Huduma ya Habari na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa  za 2016.

“Kwa sasa kutoa habari zilizo wazi tena kwa wakati, sio utashi wa mtu tena bali  ni matakwa ya Sheria  hivyo ni wajibu wa kiongozi kutoa taarifa kwa umma” alisisitiza Waziri Nape.

Aidha alisema kuna baadhi ya Maafisa Mawasiliano ambao mpaka mwaka unakwisha hawajawahi kuandika taarifa yoyote kwa umma wala kutoa ufafanuzi kuhusu utendaji wa Serikali hivyo kuijengea Serikali taswira mbaya kwa Wananchi.

“Katika awamu hii hakuna “Mungu Mtu” katika utoaji wa taarifa hivyo ni wajibu wa viongozi kutoa taarifa au ufafanuzi pale inapohitajika na sio kukwepa waandishi wa habari, na kutofuatilia kero za Wananchi ” alisema Waziri Nape.

Waziri Nape aliwataka Maafisa Mawasiliano na Viongozi katika Taasisi za umma nchini kutekeleza Sheria ipasavyo kwa kutoa habari na taarifa kwa umma bila urasimu.

“Ndugu zangu msikalie taarifa maana kama hutoi ushirikiano kwa wana habari na wote wanaohitaji taarifa watatunga zakwao ,hapo sasa mnaanza kukimbizana kukanusha” ,Alisisitiza Waziri Nape.

MICHUZI TV: USHAHIDI KESI YA WEMA SEPETU NA WENZAKE BADO HAUJAKALIMIKA, KUSIKILIZWA TENA APRILI 11

0
0
Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akiwasili  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo alipofika kusikiliza kesi inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya. 


Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Upande wa Mashtaka katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili msanii marufu wa filamu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili umeileza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umefikia hatua za mwisho.

 Mwendesha Mashtaka, Constantine Kakula amedai hivyo leo mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati keai hiyo ilikuwa inatajwa.
"Mheshimiwa hakimu, kesi leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika ila uko katika hatua za mwisho", amesema Kakula".

Katika kesi hiyo, watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matatu yanayohusiana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

 Hati ya mashtaka inadai kuwa Aprili 4, Mwaka huu, katika eneo la Kunduchi Ununio washtakiwa walikitutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08.

Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo alipofika kusikiliza kesi inayomkabili ya kukutwa na dawa za kulevya.
Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu akitoka mahakamani, baada ya kesi yake ya matumizi ya dawa za kulevya kuahirishwa hadi Aprili 11, mwaka huu. Mwenge suti nyeusi kulia ni mbunge wa Arusha, (Chadema), Godbles Lema akimsindikiza. Nyuma ni wapambe wao.

Engine, gear box na spares za Discovery, Defender na Range Rover zinapatikana bei nafuu

0
0
Tunauza Engine za Discovery, Defender Range Rover, Gear Box, na Spare nyingine kwa bei nafuu. Bei ya Engine ni 4.7 Milion Gear Box 2.5 Milion. tunaleta kutoka U.K zipo Dar es Salaam kwa maelezo zaid wasiliana nasi Tell: +255 652 444 311+255 717 669 548 on Whats app +447723550406

TTB STRATEGIZES TO FULLY PENETRATE INTO EUROPEAN AND AMERCAN TOURIST MARKETS.

0
0
Tanzania Tourist Board (TTB) has signed special contracts with three consultant agencies from Europe and America to develop special marketing strategy for Germany, U.S.A and United Kingdom as part of initiatives to intensively penetrate into world tourist markets as well stipulated in its five years International Marketing Strategy.

The signing ceremony took place in Tanzania pavilion at the International tourism fair (ITB) whereby the Managing Director of TTB Ms DevotaMdachi and the chief Executive Officers of the Africa Oracle Company from UK, 7o7 Marketing GmbH from Germany and Tourism Intelligence International from U.S.A signed for their organizations respectively.

According to Tanzania Tourist Board’s Marketing Manager Mr. GeofreyMeena the procedures for Public Procurement were properly adhered to for awarding tender for the consultants and that the awardees are supposed to finish the strategies and submit to TTB by June this year ready for implementation.

He said that though the five years International Marketing Strategy has specified about twelve tourists’ source markets in the World but TTB has selected UK, USA and Germany to start with because they are among the leading four tourist markets for Tanzania which are USA, UK, Italy and Germany.

“We have selected these three to start with but later on we will bring on board other countries. It is great hope that once strategies for these three countries are ready they will be very useful for our mission to intensively tap those markets” noted Mr Meena.

The move to officially engage these consultants has come just one day after Tanzania tourist Board signed Memorandum of Understanding (MoU) with Mauritius Tourism Promotion Board to forge partnership in which the two organizations will jointly promote their countries as twin destinations.
The Managing Director of Tanzania Tourist Board (TTB) Ms DevotaMdachi (left) and the Managing Director of Tourism Intelligence International of USA signing a contract for USA tourist Market. Witnessing from behind is the TTB chairman Judge (rtd) Thomas Mihayo.
Ms DevotaMdachi, the TTB’s Managing Director (right) and the Director of 7o7 Marketing GmbH Limited Mr. RecknagelMarkus(left) exchanging the signed documents of contracts for the German Market.
Dr.Auliana Poon, the Managing Director of the USA based company namely Tourism Intelligence International (right) and her counterpart of Tanzania Tourist Board Ms DevotaMdachi (left) exchanging the signed contracts.
Director of the 7o7 German Company Marketing GmbH Ltd Mr.Recknagel Markus and the Managing Director of TTB Ms DevotaMdachi show up copies of TTB’s magazine in Dutch language meant for German market and other Dutch speaking countries.

Kivuko cha MV Sabasaba chaendelea kupiga mzigo

0
0
Kivuko cha MV Sabasaba kinachotoa huduma ya kuvusha magari na abiria kati ya Kigongo na Busisi katika Ziwa Victoria kikiwa kinaelea katika ziwa hilo mjini Mwanza.
Baadhi ya magari ya watu binafsi na mabasi ya abiria yakisubiri kuingia katika kivuko cha MV SENGEREMA kinachotoa huduma zake kati ya Kigongo na Busisi katika ziwa Victoria jijini Mwanza tayari kwa kuvuka kuelekea Kigongo kutokea Busisi.PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO TEMESA

BREAKING NYUZZZZZ.....: TRA YAPIGA KUFULI OFISI ZA TFF MCHANA HUU

0
0
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifungia ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) leo na kuamrisha kuacha kila kitu ndani, hali hiyo imefikiwa kufuatia deni kubwa la kodi wanalodaiwa TFF. Kampuni ya Yono Auction Mart kwa idhini waliyopewa na TRA walihusika katika kuzifunga ofisi hizo na kuwataka kutotoka na kitu chochote ndani.

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA KAHAMA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha maombolezo ya Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya kwanza, Sir George Kahama ,nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimfariji mjane wa Marehemu Sir George Kahama Bibi.Janet Bina nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAZISHI YA SIR GEORGE KAHAMA KUFANYIKA KESHO, SPIKA MSTAAFU ANNE MAKINDA ATOA POLE KWA WAFIWA

0
0

Na Dotto Mwaibale


MAZISHI ya aliyekuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe Sir George Kahama yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mwili wa marehemu utawasili nyumbani kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business leo hii saa 11 jioni na kukesha hadi asubuhi.

Kesho mwili wa marehemu utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa mbili kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters) Oysterbay Dar es salaam saa tano na nusu 5.30 asubuhi kwa ibada.

Ibada ya mazishi itafanyika katika makaburi ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu 9.30 alasiri.
Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sofia Simba akimpa pole mjane wa marehemu, Janeth Kahama.
Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.
Pole zikiendelea kutolewa kwa mjane wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa msibani.

WAAJIRI NA WATUMISHI WA UMMA NCHINI: OPRAS IPO KWA SHERIA HIVYO NI WAJIBU KUITEKELEZA IPASAVYO.

0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (wa kwanza kulia) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC One kuhusu Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS). Wengine katika picha ni Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila Shoo (katikati) na Mwongozaji wa kipindi hicho, Bw. Rashid Salim.
Mtangazaji wa Kipindi cha “JAMBO” kinachotangazwa na TBC One, Bw. Rashid Salim (kushoto) katika mahojiano na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba, pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila Shoo. Kipindi cha Jambo maudhui yake yalikua kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba (kulia) akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila Shoo. Wengine ni waongozaji wa kipindi hicho, Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.
Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais – Utumishi, Bi. Veila Shoo (kushoto) akizungumza mapema leo katika kipindi cha JAMBO kinachotangazwa na TBC Taifa kuhusu umuhimu wa Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Waajiri na Watumishi wa Umma nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba. Wengine ni waongozaji wa kipindi hicho kushoto ni Bi. Anna Mwasyoke na Bw. Paul Alphonce.

NI WAJIBU WA MAOFISA MAWASILIANO KUHUISHA TOVUTIZAO-DKT JABIRI

0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao (kulia)  akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma,kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas. 

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Hassan Abbas (kushoto) akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo BI. Nuru Milao.

 Mtendaji Mkuu Wakala wa Serikali Mtandao Dkt. Jabiri Bakari akitoa mada juu ya hali halisi ya uhuishaji wa Taarifa za Serikali kwenye Tovuti Kuu ya Serikali na Taasisi za Serikali katika Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano  Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma. 
 Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Idara ya Habari (Maelezo) Bi. Zamaradi Kawawa akichangia mada katika kikao  Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea katika ukumbi wa Hazina mkoani Dodoma.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kutumia tovuti za ofisi na tovuti kuu ya Serikali kwa kuweka taarifa mbalimbali zinazohusu huduma na bidhaa zinazotolewa na taasisi hizo ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu huduma hizo kirahisi.

Rai hiyo imetolewa leo Mkoani Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Dkt. Jabir Bakari alipokuwa akitoa semina juu ya matumizi na umuhimu wa tovuti za Serikali katika kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachoendelea Mkoani humo.

Dkt. Bakari amesema dhana ya Serikali Mtandao ni  kuhuisha matumizi ya TEHAMA kwenye utoaji wa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi hivyo ni muhimu kwa kila taasisi kuwa na tovuti zenye taarifa za uhakika na zinazoendana na wakati ili  kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo.

“Wakala kwa kushirikiana na TAMISEMI pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tumetengeneza mfumo unaotumia muda mfupi kwa taasisi za Serikali kutengeneza tovuti zao ili ifikapo Juni mwaka huu taasisi zote ziwe na tovuti zao zitakazowarahisisha wananchi kufahamu huduma kirahisi,”alisema Dkt.Bakari.


NAIBU MEYA TEMEKE AAGIZA SOKO LA STERIO APEWE MZABUNI

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Feysal Salum, ameagiza kuanzia sasa Soko la Matunda la Temeke Sterio kupewa mzabuni wa ukusanyaji mapato ili kuongeza ufanisi katika mapato ya Halmashauri.

Salum ametoa agizo hilo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujifunza kazi kwa maofisa masoko wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke na Madiwani, ambao walikwenda kujifunza namna jinsi gani halmashauri ya Ilala imeweza kufanikiwa kupata mapato kupitia masoko kupewa wazabuni kukusanya masoko.

“lazima niwaambie ukweli kuwa soko hili tunalipeleka kwa wazabuni,ili tuweze kupata mapato, haiwezekani kukusanya mapato milioni 50 kwa mwezi na gharama za uzalishaji kuwa juu ya hiyo fedha, hivyo hapa hakuna namna lazima tuligawe hili soko ili tuweze kupata faida” amesema Salum.

Amesema kuwa kwa ziadi ya miaka mitano soko hilo lilikuwa likiendeshwa kwa hasara kwa fedha kutoka Halmashauri, hivyo kuanzia sasa imefikia tamati .

Kwa upande wake Naibu Meya Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wanasiasa kuacha kukumbatia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwaletea jeuri maofisa masoko na wakusanya ushuru kwa sababu wanafahamiana na viongozi.

Ametaja kuwa kama viongozi wa juu watakuwa mstari wa mbele kusimamia makusanyo bila ya kumwangalia mtu wataweza kufanikiwa katika mfumo huo wa ukusanyaji kupitia mzabuni ambao una manufaa makubwa sana kwa Halmashauri.
Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Faysal Salum akitoa maagizo ya soko la Sterio kupewa mzabuni mara baada ya kumalizika kwa kikao cha mafunzo kutoka kwa watendaji wa Manispaa ya Ilala
Baadhi ya Madiwani na Watendaji kutoka Temeke wakisikiliza kwa makini maelekezo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke.
Naibu Meya Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza katika kikao hicho cha madiwani na maofisa masoko kutoka Temeke na Ilala.

RAIA SITA WA PAKISTANI NA MMOJA WA SRI-LANKA WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU WAKITUHUMIWA NA MASHITAKA SABA

0
0
Karama Kenyunko wa blogu ya jamii.

Raia sita wa Pakistani na mmoja wa Sri-Lanka wanaoishi  jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakamani wakikabiliwa na mashitaka saba likiwemo la kula njama, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisabishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya Sh. Milioni 459.

Washtakiwa hao wamesomewa mashitaka yao leo  mbele ya Hakimu Mkazi Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.  Jamhuri imewakilishwa na Mawakili wa Serikali Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Mwanasheria Mkuu wa TCRA, Johannes Karungula.

Wakili Katuga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni, Dilshad Ahmed,Rohail Yaqoob, Khalid Mahmood, Ashfaq Ahmad, Muhammad Aneess, Ramesh Kandasamy na Imtiaz Ahamad Ammar.

Katika shtaka la kwanza imedaiwa, kabla ya Novemba mwaka Jana, jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la matumizi ya Huduma za network kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili, washtakiwa hao wamedaiwa, kati ya Novemba mwaka Jana na Februari mwaka huu, bila halali na kwa makusudi washtakiwa wakiwa na nia ya kukwepa malipo halali walitoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila leseni ya TCRA.  

QUALITY GROUP WADHAMIRIA KUKUZA KIPATO CHA WANANCHI NCHINI

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


KAMPUNI ya Quality Group imedhamiria kuendelea kujikita zaidi katika sekta mbalimbali zikiwemo za madini, kilimo cha sukari na kuanzisha kwa kiwanda na  usambazaji wa  matrekta nchini.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni hayo Nicholaus Raphl   Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa kampuni ya Quality toka ianzishwe nchini imeweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya laki sita (667,300) na imejikita zaidi katika kuwaajiri wazawa.

Quality Group katika kukuza sekta ya viwanda nchini imeingia mkataba na kampuni ya Solanika International Tractors Limited na mradi huo utaanzia mkoa wa Morogoro ambapo takribani matreka 1000 yataanzia kule na watanzania takribani 1200 watapata ajira na mradi huu utakamilika 2018.

Uanzishwaji wa mradi huo utawasaidia watanzania kupata matreka yatakayokuwa na ubora mzuri na yatakuwa ya bei nafuu na kila mkulima anaweza kuwa nalo kwani yatatengenezwa hapa hapa nchini kwa kushirikiana na kampuni ya Solanika.

Pia, Raphl amesema Quality wamedhamiria kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kujenga vituo 4,000 vya afya sehemu mbalimbali nchini na itamuwezesha kila mwananchi kupata tiba sahihi na itakayokidhi umuhimu wa mgonjwa na tayari kampuni kutoka nchini Urusi wameshaingia nao makubaliano ya kusambaza dawa kwenye vituo hivyo.

Mbali na hayo, Quality wameweza kujikita katika kukuza elimu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya ujasiriamali wa uvuvi kwa wananchi wanaoishi kando ya Ziwa Victoria na kuwapatia vifaa vinavyostahili kwa kutumika kwenye uvuvi.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Quality Group Nicholaus Ralph akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya kimaendeleo itakayofanywa na kampuni hiyo.
Baadhi ya Wanabari wakifuatilia mkutano huo. 

WANAFUNZI WA S/SEK KATA YA PANGANI WATEMBEA KM 34 AMA KUTUMIA PIKIPIKI SH.10,000

0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

WANAFUNZI wa shule ya sekondari ya kata ya Pangani,Kibaha Mji,wanakabiliwa na adha ya kutembea umbali wa km.34 kila siku,hali inayosababisha baadhi yao kuwa watoro, kukatisha masomo na kupata mimba.

Aidha shule za msingi zilizopo katika kata hiyo,zina uhaba wa walimu ambapo shule yenye wanafunzi 950 ina walimu kumi pekee hivyo kusababisha muda mwingi wanafunzi kucheza.

Hayo aliyasema diwani wa kata ya Pangani,Agustino Mdachi,wakati alipokuwa akizungumzia changamoto za kielimu ,kwenye ziara ya mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha,Silvestry Koka,aliyoifanya katika kata hiyo.

Alisema,wanafunzi wanaosoma kwenye ya shule ya kata wanapata usumbufu na wapo katika wakati mgumu.
Diwani wa kata ya Pangani,Agustino Mdachi akizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye ziara ya mbunge wa jimbo la Kibaha Mji,Silvestry Koka aliyoifanya katika kata hiyo.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Pangani,wakisikiliza jambo katika ziara ya mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha, Silvestry Koka kwenye kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka,akizungumza jambo katika ziara yake kata ya Pangani .(picha na Mwamvua Mwinyi).


Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images