Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1599 | 1600 | (Page 1601) | 1602 | 1603 | .... | 3286 | newer

  0 0

  The Rabbit Bliss ni Kampuni inayojihusisha na ufugaji wa Sungura na kutoa Mafunzo ya namna ya kufuga Sungura hapa nchini, wanapatikana Majohe mbele ya Gongo la Mboto, Jijini Dar es salaam. 

  kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa namba hizi +255 713 448 899

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiwa na Mhe, Airlangga Hartarto miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia pamoja na Viongozi wa wengine wa Nchi hiyo pia akiwepo na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed (kulia)alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Nchi Indonesia,Rais Shein anamuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini Indonesia, [Picha na Ikulu.] 05/3/2017.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari juu ya Matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba). Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi

  Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alipozungumza nao na kutoa matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kusitisha uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba).
  ……………………………………………………………………………
  Kama mnavyofahamu unywaji wa pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, ajali na vifo zivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizi, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. 

  Madhara haya ndiyo yaliyopelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kutoa tamko tarehe 16 Februari, 2017 akiwa Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha uzalishaji, usambazaji,  uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) kuanzia tarehe 1 Machi 2017; Baadaye tarehe 20/2/2017 na tarehe 28/2/2017 nilitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu ufuatiliaji wa agizo hilo.
  Ili kutekeleza kwa ufanisi agizo hili serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuratibu Operesheni Maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya serikali na kuchukua hatua stahiki.
  Kikosi Kazi hicho kiko chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, na kinajumuisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango,  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.
  Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote  kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na  Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya.  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. 

  Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).
  Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu operesheni maalum  katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii ilitokana na kuwepo  kwa viwanda vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets)  ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.

  0 0  Globu ya Jamii inatoa taarifa kwa Wenye ndugu waliosafiri kwenye Basi la Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam,yamepata ajali mlima Kitonga hivi punde,ambapo taarifa kutoka kwa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wameeleza kuwa katika ajali hiyo wamejeruhiwa abiria 12.

  Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigongana na basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni .
   
  Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akielezea kuwa  taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.
   
  Moja ya Lori lililogongwa na kumbukia korongoni

  0 0

  Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

  MBUNGE wa jimbo la Mji wa Kibaha,mkoani Pwani,Silvestry Koka,awataka vijana kuacha kujibweteka na kuwa tegemezi,badala yake wajikite katika shughuli ndogondogo ili kujiinua kiuchumi.

  Amesema anatambua tatizo kubwa ni kukosa mitaji kwa vijana lakini,nguzo pekee ya kupata msaada kirahisi ni kuunda vikundi ili kuweza kuwawezesha mikopo na masuala mengine ya maendeleo.

  Koka aliyasema hayo,mjini Kibaha baada ya kuzindua mradi wa chama cha madereva wa pikipiki ,Mailmoja wa mashine ya kuoshea magari(Car Wash).

  Aliwaomba wale walioanza ujasiliamali kuacha ubinafsi bali wawasaidie wengine wasiojua ili hali waweze kutoka kimaisha pasipo kukaa vijiweni bila kuwa na mwelekeo wowote.Aidha Koka aliwasihi madereva hao kujenga umoja na mshikamano utakaowasaidia kulinda maslahi na faida wanazozipata.

  Hata hivyo, aliahidi kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili vijana na makundi mengine ikiwemo wanawake ili kuweza kupiga hatua kiuchumi jimboni humo.

  Mbunge huyo,alifafanua kwamba tangu aanze uongozi wake ameshasaidia makundi mbalimbali ya ujasiliamali ya wanawake na vijana zaidi ya sh.mil.180 kutoka mfukoni mwake.“Nimejipanga kuendelea kuviwezesha vikundi hivyo kwani ni moja ya kutimiza vipaombele vyangu nilivyojiwekea japo kuwa vijana bado hawajajipanga kikamilifu”alieleza Koka.

  Awali,Koka alizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa kata ya Mailmoja na anaendelea na ziara yake aliyoianza jimboni hapo.
  Mbunge wa jimbo la Mji wa Kibaha ,Silvestry Koka,akizindua mradi wa kuosha magari wa chama cha madereva pikipiki Mailmoja Kibaha.(Picha zote na Mwamvua Mwinyi)

  0 0

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO

  Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

  Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.

  Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.

  Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

  Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.

  Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.

  0 0

  Na chalila Kibuda,Globu ya jamii

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira, January Makamba amesema shehena za viroba vilivyopatikana katika viwanda,Maghala, Maduka ya Usambazaji pamoja na sehemu za starehe zikae kizuizini mpaka serikali itakapotoa tamko kwa watu hao.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitoa taarifa ya operesheni, Makamba amesema viroba vilivyokamatwa vina thamani ya sh. bilioni 10.83 na operesheni inaendelea kwa kuwahusisha wenyeviti wa serikali za mitaa.

  Amesema kuwa operesheni hiyo imebaini kuwepo viroba vyenye Stika za Mamlaka Mapato Nchini (TRA) zikiwa zimegushiwa na wanaofanya biashara hiyo.Makamba amesema watu waliofanya ukiukaji wa Sheria wa biashara hiyo wanajiandaa kuwafungulia mashitaka.

  Waziri Makamba amesema na viroba vilivyopatikana baadhi watavipeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali juu ya madhara kwa matumizi ya binadamu.
  Aidha amesema kuna baadhi wafanyabiashara walikwenda kufungua kesi ya kuzuia operesheni waligonga mwamba kutokana sheria ya kufanya kazi hiyo.

  Aliongeza kuwa kuna baadhi raia wa kigeni wanafanya kazi bila kibari na kutaka Idara ya Uhamiaji kufatilia raia hao.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, January Makamba akizungumza na waandishi habari juu matokeo ya operesheni viroba leo.


  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara baada ya kukagua kiwanda chake cha Saruji mkoani Mtwara.
  Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani Mtwara.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua kituo cha kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mtwara katika siku ya mwisho wa ziara yake katika Viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara.

   Wananchi wa Mtwara wakifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya mashujaa mkoani Mtwara
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mtwara mara baada ya kumaliza kuwahutubia katika viwanja vya Mashujaa mkoani Mtwara-PICHA NA IKULU.
  0 0

   Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 
  Viongozi wa dini pamoja na waumini wa Dini ya Kiristo jijini Dar es Salaam wametakiwa kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuwaukoa vijana katika vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya hapa nchini. 
  Hayo ameyasema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo katika Kanisa la KKKT usharika wa Kimara aalipoungana na waumini wengine kwenye ibada ya maombi ya kumuombea Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu yakiwamo madawa ya kulevya,
  Katika salamu zake RC Makonda amesema viongozi wa dini wanaweza kuibadilisha jamii ambayo inataka kupotea kupitia maneno ya Mungu, na kwamba watu wanaoingiza dawa za kulevya hawana nia njema na vijana ambao ndio nguvu kazi ya nchi hivyo wanahitaji kuokolewa katika lindi la matumizi ya dawa hizo ambayo ni  janga kubwa katika taifa. 
  Aidha RC Makonda amesema kuwa ataendelea kusimama imara katika utekelezaji wa majukumu aliyopewa bila kuhofu wala kumuonea mtu yeyote. Naye Mchungaji wa Kanisa hilo,
  Mchungaji Wilbroad Mastai (pichani) amesema waumini wana mchango mkubwa katika kuwasaidia viongozi kutokana na athari za dawa hizo na kutawaka kuondoa hofu kwa binadamu na kumtanguliza Mungu mbele.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiombewa na Askofu Mstaafu  Mwamasika leo ibada ya maombi ya kumuombea  Rais Dk. John Magufuli, Watendaji wa serikali pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kuevya jijini Dar es Salaam katika kanisa la KKKT Kimara jijini Dar es salaam leo.
  Sehemu ya waumini katika katika Kanisa la KKKT Kimara  jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waumini wa  Kanisa la KKKT  Kimara ambalo leo limeendesha ya  ibada ya maombi ya kumuombea  Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza na waumini wa  Kanisa la KKKT  Kimara ambalo leo limeendesha ya  ibada ya maombi ya kumuombea  Rais Dk. John Magufuli, Watendaji pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam dhidi ya mapambano dhidi ya maovu ikiwemo dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein  akiwa na Mhe, Airlangga Hartarto miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia pamoja na Viongozi wa wengine wa Nchi hiyo pia akiwepo na Waziri wa Kilimo, Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed walipowasili katika uwanja wa Ndege wa Nchi Indonesia leo. Rais Shein anamuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA) nchini humo. Picha na IKULU

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba (katikati) akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya operesheni maalum ya kutokomeza pombe kali aina ya viroba mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakulana Dawa (TFDA),Hiiti Sillona kushoto ni Kaimu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya.
  Na Lilian Lundo – MAELEZO
  Pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki maarufu kama ‘viroba’ zenye thamani ya shilingi Bilioni 10.8 zimekamatwa Jijini Dar es Salaam katika msako wa pombe hizo uliofanyika kuanzia Machi 01 mpaka 03, mwaka huu.
  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba  leo Jijini, Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu operesheni ya utekelezaji wa maelezo ya Serikali ya kusitisha pombe hizo za viroba hapa nchini kuanzia Machi 01, mwaka huu.
  “Jumla ya katoni 99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (Viroba) zimekamatwa ambapo katoni 69,045 ni zenye ujazo wa  na mililita 50, katoni 29,344 zenye ujazo wa mililita 100, katoni 782 zenye ujazo wa mililita 90 pamoja na katoni 10,625 za chupa zenye ujazo wa mililita 100. Thamani yake ni Shilingi Bilioni 10.83,” alifafanua Makamba.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, jumla ya viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali, maduka ya jumla 18, maghala 4, baa 3 na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia viroba vilikaguliwa katika opesheni hiyo. 

  0 0


  SIMU.TV; Bodi ya shirika la reli nchini TRL yawataka wafanyakazi wa shirika hilo kubadilika katika utendaji wao ili shirika hilo liweze kuwa na tija.https://youtu.be/_x0yl252YD4 

  SIMU.TV; Shirikisho la mifuko ya hifadhi ya jamii nchini TSSA yakubaliana na serikali kujenga viwanda vikubwa 27 nchini ili kuunga mkono sera ya sasa ya uchumi wa viwanda. https://youtu.be/GpYK4NOOdFM 

  SIMU.TV; Operesheni ya kukagua uzuiaji wa utengenezaji na pombe za Viroba yafanikiwa kukamatwa kwa shehena yenye thamani ya shilingi bilioni 10 tangu ianze.https://youtu.be/TYQa6l548Pg 

  SIMU.TV; Mshambuliaji hatari wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Samatta aendelea kutema cheche huko Ubelgiji baada ya kuifungia timu yake goli 2.https://youtu.be/RpMoIZlC0vs 

  SIMU.TV;  Mabingwa watetezi wa ligi kuu klabu ya Yanga imebanwa koo na Klabu ya Mtibwa sugar baada ya kulazimishwa sare ya 0 kwa 0. https://youtu.be/_qCejQWunHo

  0 0


  0 0  0 0

   Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi akifungua kongamano la Wanawake Jijini Tanga ambalo lilikuwa na lengo kuu la kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi kwa wanawake ikiwemo fursa za kiuchumi sambamba na kupambana na dawa za kulevya kwa jamii lililofanyika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tanga leo
   Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Tanga,Mwatumu Dossi  wa pili kutoka kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga, Fortunata Manyeresa wakati wa kongamano la wanawake Jijini Tanga kuelekea siku ya wanawake dunia kushoto ni Rehema na Yahaya Seumbe ambaye ni Afisa kutoka Ofisi ya Maendeleo ya Jamii kwenye Jiji la Tanga wakifuatilia kongamano hilo.
   Baadhi ya Wakina wanawake jijini Tanga  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo
   Sehemu ya Umati wa wanawake wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo la wanawake wa Jiji la Tanga kuelekea siku ya wanawake Dunia ambapo kilele chake itakuwa ni Machi 8 mwaka huu
   Baadhi ya waandishi wa habari jijini Tanga wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo wa kwanza kulia ni Burhan Yakub wa gazeti la Mwananchi, Bertha Mwambela wa TBC TV na Sussan Uhinga wa Clouds TV.
  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Madawa ya kulevya nchini Bw. Rogers Sianga, mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.
   Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi  mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017
  Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Lindi na Mtwara jioni ya leo March 5, 2017.  
  PICHA NA IKULU

  0 0

   MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wameshindwa kuipiku Simba kileleni baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani kwenye mchezo wa ligi kuu iliyofanyika Machi 5, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro. 
  Yanga watajilaumu wenyewe kutoka na kushindwa kuzitumia nafasi tatu za wazi za kufunga mabao ikiwemo ya penati iliyotolewa katika dakika ya 33 baada ya beki wa timu ya Mtibwa Sugar Ally Lundega kuunawa mpira eneo la hatari. 
   Mwamuzi wa mchezo huo Hamedi Kikumbo kutoka Dodoma ,aliamuru ipingwe penati kuelekea langoni mwa timu hiyo na mchezaji Saimon Msuva wa Yanga alipewa jukumu la kupinga penati hiyo. Lakini badala ya kupinga mpira huo kulenga lango la Mtibwa Sugar alijikuta akipaisha juu ya lango la wapinzani wao na kuikosesha timu yake bao hali iliyoamsha shangwe za mashambiki wa Mtibwa Sugar waliopewa ushirikiano na wenzao wa Simba kushangilia kwa nguvu kutokana na kukosa bao hilo. 
   Katika mchez huo Yanga ilikuwa na nafasi nzuri ya kuweza kuipuku Simba kwa idadi ya mabao endapo mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar ingepata ushindi ili kufikisha pointi 55 sawa na mtani wake wa jadi Simba isipokuwa wangepishana kwa mabao ya kufunga . 
  Mchezo huo ulikuwa ni wa vuta nikuvute ambapo Yanga iliweza kutawala mchezo katika kipindi cha kwanza na dakika 15 za kipindi mwisho kwa kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar, lakini ukuta wa Mtibwa Sugar ulikaa imara na kuondoa hatari zote langoni mwao hadi mwisho wa mchezo.
   Kikosi cha wachezaji wa timu ya Yanga kabla ya mchezo wao na Mtibwa Suga katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo Machi 5, 2017
   Kikosi cha wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar , kabla ya mchezo wao na Yanga  katika uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo.
  Jukwaa la  mashabiki wa timu ya Yanga wakifuatilia mpira uwanja wa Jamhuri wa Morogoro leo
  Mshambuliaji  Saimon Msuva wa Yanga akipiga na kukosa penati katika mchezo huo
   Mchezaji wa Yanga Justine Zulu akisongwa na beki wa timu ya Mtibwa Sugar Ally Shomari katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika Machi 5, mwaka huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Morogoro, timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.
  Mchezaji wa Yanga , Saimon Msuva akijaribu kuwatoka mabeki wawili wa timu ya Mtibwa Sugar , Ally Makarani ( kushoto) pamoja na Ally Shomari ( kulia) wakati wa mchezo wa ligi kuu uliofanyika Machi 5, mwaka  huu kwenye uwanja wa Jamhuri wa Morogoro, timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.  
  Habari na Picha na John Nditi, 
  Globu ya Jamii, Morogoro

  0 0

   Msanii na mtayarishaji wa Filamu ya Gate Keeper, Vicent Kigosi 'Ray' akizungumza na Waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa uzinduzi wa filamu yake ya GateKeeper katika ukumbi wa Cinema wa Quality Plaza jijini Dar es salaam.  Picha zote na Humprey Shao wa Globu ya Jamii.
   Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Rj Company Blandina Chagula 'Johari ' akiwa na baadhi ya Mashabiki wa Bongo Movie
   Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akiwa na Mwandishi na mtunzi wa filamu ya Gate Keeper Ally Yakuti kabla ya kuanza kuonyeshw akwa fimau hiyo katika ukumbi wa Quality Centre
   Wasanii walioshiriki katika filamu ya Gatekeeper wakiwa katika picha ya pamoja ya zuria jekundu kabla ya kuingia katika ukumbi wa cinema.

  0 0

  Wataalam wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 05 Machi, 2017  wako katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme pamoja na kukutana na wadau wa nishati jadidifu.
   Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company, Alex Andoya (katikati) akielezea maendeleo ya  kampuni hiyo katika uzalishaji wa umeme mara baada ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kufanya ziara katika kampuni hiyo, Mbinga mkoani Ruvuma ili kujionea maendeleo ya shughuli zake. Wataalam hao wako katika  ziara ya  kukagua miradi ya umeme pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam.

   Mtaalam kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company,  Mhandisi Jasper Bubelwa (kulia) akielezea mfumo wa uendeshaji mitambo wa  kampuni hiyo

  Wataalam wa Nishati Jadidifu,  Emillian Nyanda, (wa pili kutoka kulia) na Mhandisi Stephan Kashushura ( wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company mara baada ya kumaliza ziara katika kampuni hiyo. Kushoto kabisa ni Fred Tawete kutoka  Wizara ya Nishati na Madini 


older | 1 | .... | 1599 | 1600 | (Page 1601) | 1602 | 1603 | .... | 3286 | newer