Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live

PENDEZESHA NYUMBA YAKO NA MAGIC DECOR


VIVUTIO VYA UTALII VYA TANGU ENZI ZA MKOLONI VILIVYOPO SHULE YA SEKONDARI YA IYUNGA JIJINI MBEYA

$
0
0
 Kamati ya Utalii ya Jiji la Mbeya,  Waandishi wa Habari pamoja na Mwalimu mwenyeji Mwl Emmanuel Michael wakiwa eneo lilipo Bwawa la Kuogelea lililojengwa na Enzi za Mkoloni katika shule ya Sekondari ya Iyunga jijini humo.
 Birika la kale lililokuwa likitumika na Utawala wa Kijerumani kwa ajili ya kuhifadhia maji na vitu vingine vinavyofanana na hivyo ambalo uongozi wa Shule ya Sekondari Iyunga wamelitunza vizuri hadi hivi sasa
 Kiti hiki ni moja ya vivutio shuleni hapo kilitengenezwa zaidi ya miaka 90 iliyopita enzi za Utawala wa Kikoloni wa Kijerumani
 Ukuta huu ulijengwa na Wajerumani pembezoni mwa Mto Nzovwe kwa ajili ya Ulinzi na Usalama kwani chini ya Ukuta huu kuna Handaki kubwa linalounganisha maeneo ya ndani ya shule na nje ya eneo hilo.

Introducing Malkia Wa Nguvu - Khadija Kopa+Ray C+Nandy+Mwasiti+Maua Sama

Rais wa Gambia awarejesha kazini Askari waliojaribu kumpindua mtangulizi wake

$
0
0
Rais wa Gambia Adama Barrow ameamuru kurejeshwa katika jeshi askari sita walikua na hatia ya kuandaa mapinduzi dhidi ya mtangulizi wake Yahya Jammeh, chanzo cha kijeshi kimearifu.

"Uongozi wa kushauriana na Rais Adama Barrow, umeamua kuwarejesha katika jeshi la taifa Luteni Buba Sanneh, Modou Njie, Luteni Sarjo Jarju, Abdoulie Jobe Kapteni, Luteni Amadou Sowe na Buba Bojang " , chanzo hicho kimeliambia shirika la habari la AFP.

Aliyekua rais wa Gambia, Yahya Jammeh alisababisha majaribio kadhaa ya mapinduzi wakati wa utawala wake uliodumu miaka 22, jaribio baya la mapinduzi ni lile la mwaka 2014. Askari walijaribu kuchukua udhibiti wa ikulu ya rais wakati alipokuwa nje ya nchi.

Askari watatu walihukumia adhabu ya kifo

Askari hao sita walihukumiwa na mahakama ya kijeshi mwezi Aprili mwaka 2015, ikiwa ni pamoja na watatu ambao walihukumiwa adhabu ya kifo, lakini wafungwa hao walipewa msamaha na Rais Adama Barrow mwezi uliopita. Askari hao sita tayari wamejiunga tena na jeshi la taifa.

Desemba 30, 2014, kundi la watu waliojihami na silaha za kivita walishambulia Ikulu ya rais katika mji Banjul lakini walirejeshwa nyuma na vikosi vya Yahya Jammeh.

Wiki moja baada ya kutambua matokeo ya uchaguzi wa rais mwezi Desemba mwaka jana, Yahya Jammeh alikataa kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow. Aliondoka Gambia Januari 21 na kupelekwa uhamishoni nchini Equatorial Guinea baada ya kukabiliwa na shinikizo la kidiplomasia na kijeshi. Chanzo: RFI Kiswahili.

MAKALA YA SHERIA: NAMNA YA KUIOMBA MAHAKAMA IKUTAMBUE KAMA MZAZI WA MTOTO.

$
0
0
 Na Bashir Yakub

1.KUNYIMWA  MTOTO.


Wako  watu  ni  wazazi  na  wamezaa  lakini  wameyimwa  watoto.  Zipo  sababu  nyingi  zinazopelekea  hili. Matukio  ya  namna  hii  hayawatokei  sana  wanawake  na badala  yake  wanaume  ndio  waathirika  zaidi katika hili .  Ni  rahisi  na  kawaida  mno mwanaume  kuambiwa  na  mzazi  mwenzake   kuwa  huyu   mtoto  si  wako  hata   kama   anajua kabisa  huyo  mwanaume  ndiye  mzazi  halisi .  Leo haya  sio  maajabu  tena.
Upo  usemi  wao  kuwa mwanamke   ndiye anayejua  baba  wa  mtoto. Sitaki  kueleza  ukweli  au  upotoshi  wa  usemi huu bali  nawaza  iwapo  ni  sawa  kutumia usemi  huu   kupora  haki  ya  uzazi   wa mtu  ambaye  unajua  kabisa  ndiye  mzazi  halisi.
Na kwa  bahati  mbaya  wanaokutwa  na  kadhia  hii wamekuwa  hawajui  ni  hatua  zipi  wachukue. Wapo  wanaoamua kufanya  vurugu, wapo  wanaojiua, wapo  wanaoamua  kumuachia  mola, na  wengine  hukimbilia  serikali  za  mitaa  ikiwa  ni  pamoja  na  hatua  nyinginezo  zisizofaa.

Ukweli  ni  kuwa  hatua  hizo  haziwezi  kukusaidia  zaidi  utapoteza  muda  mwingi,  gharama  na  pengine  kuzua  matatizo  mengine  ambayo  hayakuwako.  

Basi  sasa  yafaa   ujue  kuwa  sheria  imetambua  jambo  hili  na  imeweka  taratibu  nzuri  za  kufuata  ili  kuondoa  ujeuri  wa  aina  hii.
 Sheria Namba  21, Sheria  ya  Mtoto  ya  mwaka  2009  imeeleza  nini  ufanye  kama  tutakavyoona   hapa  chini.  Lakini  kabla  ya  hilo  hebu  kwa  kutaja tu  tuone  sababu  kadhaa  zinazofanya  wazazi  hasa  wa  kike kuwanyima  wazazi  wenzao  haki  ya kutambulika  kama  wazazi  wenzao.

AZANIA KUWAKILISHA AFRIKA MASHARIKI ENGLAND

$
0
0
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes (katikati) akiwasili pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba walipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.[/caption] Naye nahodha wa Capital FM, Lassie Atrash alisema kwamba wameshindwa kufanya vyema kwa kuwa uwanja ulikuwa mdogo.
 Hata hivyo alisema ulikuwa ni mchezo safi na mshindi ilikuwa lazima apatikane na kusema kwamba ana matumaini kuwa Azania itawawakilisha vyema Afrika Mashariki huko England. Awali mchezaji John Barnes akizungumza kabla ya michezo hiyo alisema anafurahishwa na kutambua kwamba soka linatengenezwa Afrika Mashariki na hivyo kuondoa dhana potofu kwamba soka katika Afrika linapatikana Afrika magharibi pekee. 
Kikosi cha timu ya Azania Group of Companies wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akijumuika na wadau wa soka kupasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi za fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.
Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akifurahi pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania (walioko mstari wa nyuma) mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.
Wengine pichani ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko Juanita Mramba (wa pili kushoto), Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (wa tatu kushoto), Balozi wa Uganda nchini Mh. Dorothy Hyuha, (wanne kushoto) na Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda na Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kushoto).
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA







Ahadi za Rais Dkt. Magufuli zatekelezwa katika ziara yake mikoa ya Kusini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mara baada ya mahubiri katika Kanisa hilo Jumapili. Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia Waumini  wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.
 Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200 ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo.
 Kaimu Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya.
 Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha fedha ambazo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya ziara mkoani humo.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa.
 PICHA NA IKULU


MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 6,2017


Austria yautaka Umoja wa Ulaya kuwapiga marufuku wanasiasa wa Uturuki kufanya kampeni

$
0
0
Kansela wa Austria Christian Kern jana Jumapili Machi 05, 2017 alisema kuwa wanasiasa wa Uturuki wanapaswa kupigwa marufuku kufanya kampeni za kisiasa katika nchi zote za Umoja wa Ulaya.

Kern ameliambia gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag kwamba "Jibu la pamoja la Umoja wa Ulaya kuzuwiya kampeni hizo litakuwa na maana ili kwamba nchi binafsi kama vile Ujerumani ambapo wanakatazwa kujitokeza katika kampeni hizo haziishii kushinikizwa na Uturuki".
Kansela wa Austria, Christian Kern
Kiongozi wa Austria ameliambia gazeti hilo la Welt am Sonntag kwamba mazungumzo yanayofanyika kwa muda mrefu na Uturuki kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya yanapaswa kuahirishwa kutokana na hatua ya Rais Erdogan wa Uturuki kuzikanyaga haki za binaadamu na haki za msingi za kidemokrasia.

Kern amesema hawawezi kuendelea kuzungumzia kuhusu uwanachama na nchi ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijitenganisha na maadili ya demokrasia na kanuni za utawala wa sheria, Anaona kwamba kuanzishwa kwa mfumo wa urais nchini humo utakaokuwa na madaraka makubwa kutazidi kudhoofisha utawala wa sheria,kupunguza kutenganishwa kwa madaraka na kutakwenda kinyume na maadili ya Umoja wa Ulaya.

Uturiki yapigania hura ya ndio

Serikali ya Uturuki imekuwa ikijaribu kuwavutia wapiga kura miongoni mwa Wajerumani milioni tatu wenye asili ya Kituruki ambayo ni idadi kubwa ya Waturuki wanaoishi nje ya nchi hiyo kuunga mkono kuongezewa madaraka kwa Rais Tayyip Erdogan wakati kura ya maoni itakapopigwa hapo tarehe 16 Aprili.
Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan
Miji kadhaa ya Ujerumani ilizuwiya kujitokeza kwa mawaziri wa serikali ya Erdogan wiki iliopita kwa kile ilichosema sababu za usalama. Kuahirishwa kwa mikutano hiyo ya hadhara kuliikasirisha serikali ya Uturuki ambayo imeituhumu serikali ya Ujerumani kwa kutaka kuiyumbisha kampeni yake ya kura ya maoni.

Hapo Jumamosi Kansela Angela Merkel wa Ujerumani alimpigia simu Waziri Mkuu wa Uturuki Binali Yildrim kujaribu kuuzima mzozo huo na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili wanatazamiwa kukutana baadae wiki hii.

Ujerumani kutetea utawala wa sheria.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel katika makala ya mgeni kwenye gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag amesema "kwa hakika hawatoacha kukosowa kwa matukio yanayoendelea Uturuki".
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel
Gabriel amesisitiza kwaba Ujerumani itasimama kidete kutetea utawala wa sheria, uhuru wa kutowa maoni, haki za binaadamu na demokrasia.

Amepinga kukamatwa kwa mwandishi wa gazeti la Die Welt la Ujerumani Deniz Yücel kwa madai ya ugaidi kuwa sio sahihi na kumepindukia kiwango. Amesema uhusiano wa kirafiki kati ya Ujerumani na Uturuki ni mzito kuliko mvutano wa kidiplomasia wanopitia hivi sasa. Chanzo: DW.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MZUNGUMZO NA KIONGOZI WA KIKOSI CHA MIPAKA WA NCHINI UINGEREZA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza na Kiongozi wa Kikosi cha Mipaka kutoka nchini Uingereza, Richard Lloyd, wakati kiongozi huyo na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati) akimsikiliza Kiongozi wa Kikosi cha Mipaka kutoka nchini Uingereza, Richard Lloyd (wapili kulia), wakati kiongozi huyo na ujumbe wake walipomtembelea Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Uingereza na Tanzania. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

CDEA yawapiga msasa wabunifu wa mavazi na urembo wa Afrika Mashariki kwa ufadhili wa IIDEA 2017

$
0
0
Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ tawi la Afrika Mashariki. 

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka ya nchi zao wanazotoka. 

Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria na mbinu tofauti za kupata ufadhili. Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika. 
 
Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo.

Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding). Mafunzo hayo ya siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo. 

Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo. Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania na Uganda. 
 
Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo.

MTAALAM WA SAIKOLOJIA NA MAHUSIANO WA CHUO KIKUU ATOA ELIMU KWA WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Mtaalam wa Masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati alipokuwa akitoa elimu kwa wafanyakazi hao kuhusiana na jinsi ya kustahimili mazingira ya kazi, wakati wa Uzinduzi wa wiki ya wanawake duniani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakimsikiliza Mtaalam wa Masuala ya Saikolojia na Mahusiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dkt. Chris Mauki (hayupo pichani) alipokuwa akiwaelimisha kuhusiana na jinsi ya kuistahimili mazingira ya kazi, wakati wa Uzinduzi wa wiki ya wanawake duniani.

WANANCHI WANAOSAFIRI NJE YA NCHI WATAKIWA KUPATA CHANJO YA HOMA YA MANJANO

$
0
0
Wananchi wanaosafiri nje ya nchi wametakiwa kupata chanjo ya homa ya manjano pale wanapohitaji kusafiri hususan siku kumi kabla ya kusafiri na kupatiwa vitabu vipya.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu,Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati alipotembelea hospitali ya Mnazi Mmoja jijini hapa kwa ajili ya kujionea utaratibu wa kutoa chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya chanjo hiyo kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

“chanjo hii ni muhimu hasa kwa zile nchi zenye changamoto za homa hii ya manjano,kwahiyo ni vizuri kuwa na kinga kabla ya kusafiri nchi hizo ili usije pata ugonjwa huo,’nilikua nchi ya Angola hivi karibu watu karibu elfu mbili walipoteza Maisha”amesema Dkt.Mpoki Hata hivyo kutokana na wingi wa watu kwa jiji la Dar es salaam na uhitaji wa chanjo hiyo wamekubaliana kuweka taratibu ya kupunguza watu kupoteza muda wa kufika mnazi mmoja kupata chanjo hiyo,hivyo wameamua kupeleka huduma hiyo karibu na wananchi mahali walipo 

 “Muda ambao upo huku shughuli nyingi zinasimama,hivyo wataalam watakaa na kuona mahali gani panafaa ili watu msipoteze muda wakuja hadi huku mfano wa Ubungo wapate huko huko hivyo tunazitawanya huduma hizi sehemu mbalimbali kwenye vituo vyetu vya huduma za afya na taratibu zitatolewa”.

Kuhusu vitabu vipya vya chanjo Dkt. Mpoki amesema wanavyo vya kutosha hivyo hamna haja ya wananchi kuwa na wasiwasi kama watakosa vitabu kwani hakuna siku itatokea watanzania wote wakasafiri kwa siku mmoja,na hivyo utaratibu mpya utatenganisha wale watu wa kuchanja na wakubadilisha vitabu wasikae sehemu moja.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Idara Kuu ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya akikabidhiwa kitabu kipya cha kadi ya manjano na mmoja wa wauguzi wa Hospitali ya mnazi mmoja ya Jijini Dar es salaam. Katibu mkuu huyo mapema leo ametembelea kituo hicho kwa ajili ya kujionea wananchi wakipata chanjo pamoja na kubadilisha vitabu vipya vya njano hiyo ambapo mwisho wa zoezi hili ni mwezi huu.
Katibu Mkuu Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwaonesha kitabu kipya cha homa ya manjano ambacho inambidi mwananchi anayesafiri toka nchini Tanzania na kwenye nchi thelathini za Bara la Afrika anatakiwa awe amepata chanjo hiyo ili kumkinga na maambukizi ya homa ya manjano. Kitabu hicho (kadi) ni mbadala ya kile cha zamani ambapo kipo tofauti na ina lenga kudhibiti udanganyifu wa raia kupata kitabu bila kupata chanjo.
Dkt.Mpoki akiongea na wananchi waliofika kwenye kituo hipcho kwa ajili ya kupata chanjo ya homa ya manjano.
Wananchi waliofika kupata chanjo kwenye kituoni hapo wakisikiliza maelezo toka kwa watoa huduma.

WASTAAFU SASA KUHAKIKIWA MAJUMBANI NA HOSPITALINI

$
0
0
Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito kwa wastaafu wanaolipwa Pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango ambao ni wagonjwa na hawawezi kufika katika viwanja vya Karimjee na Mwalimu Nyerere(Sabasaba) kwa ajili ya uhakiki wa nyaraka zao kutoa namba za simu na majina yao ili waweze kuhakikiwa pale walipo kama ni Hospitali au nyumbani.

Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango linalofanyika katika Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo tarehe 6-10 Machi.

“Kwa sasa ninavyozungumza zoezi hili liko kwenye hatua ya mwisho katika Mkoa wa Dar es Salaam,Zoezi hili lilianza Mkoa wa Pwani na tumelifanya nchi nzima na limefanyika kwa ufanisi mkubwa sana na wastaafu wengi wamejitokeza na kama mnavyoona zoezi limekuwa likiendelea kwa utaratibu mzuri sana”,Aliongeza Bw.Mtonga.

Mtonga amesema wastaafu hao wengi ni watumishi wa Serikali ambao walifanya kazi kabla ya mwaka 1999 ambapo walikuwa hawapo katika mifuko ya pensheni ndio ambao wanalipwa pensheni na Serikali wakiwemo watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha amesema lengo kubwa la kuhakiki wastaafu hao ni kuboresha daftari la wastaafu ili kusaidia kujua ni kiasi gani cha wastaafu wapo katika kumbukumbu ya daftari la pensheni na kusisitiza wastafu ambao hawatajitokeza watafutwa katika daftari hilo.

Ukaguzi huu kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 na ukaanza tena mwezi Octoba mwaka 2016.
Uhakiki wa wastaafu wanaolipwa Pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango wakiendelea na uhakiki katika viwanja vya Karimjee leo Jijini Dar es Salaam.Zoezi hili linafanyika kwa wiki nzima kuanzia tarehe 6-10 Machi kwa wastaafu walio Dar es Salaam.
Mkaguzi wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bi.Mary Mauki akimpa maelekezo mstaafu wa Jeshi Bw.Rashid Hussein wakati wa uhakiki wa wastaafu wanaolipwa Pensheni na Wizara ya fedha na Mipango unaondelea katika Viwanja vya karimjee Jijini Dar es Salaam.
Muhasibu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Babu Kigule akizungumza na moja ya mstaafu juu ya utaratibu wa kuhakiki nyaraka za wanaolipwa pensheni na Wizara ya fedha na Mipango unaofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya fedha na Mipango wakisubiri kuitwa kwa ajili ya kuhakiki nyaraka zao.Zoezi hili linafanyika kuanzia tarehe leo tarehe 6-10 mwezi huu katika viwanja vya Karimjee na viwanja vya Mwalimu Nyerere (sabasaba).
Mkaguzi Mkuu wa ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw.Emmanuel Kizigha akihakiki nyaraka za mstaafu anaelipwa na Wizara ya Fedha na Mipango,uhakiki huo unafanyika kuanzia leo tarehe 6-10 Machi katika viwanja vya Karimjee na Sabasaba. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

TUNDU LISSU AACHIWA HURU NA KUKAMATWA TENA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu baada upande wa Jamhuri kuomba kumuondolea kesi ya uchochezi.

Hata hivyo mara tu baada ya kuachiwa huru alikamatwa tena akiwa katika viunga vya mahakama hiyo na kupelekwa moja moja katika kituo cha polisi kati.

Kabla ya kukamatwa, Mwendesha Mashtaka wakili wa Serikali Paul Kadushi amewasilisha maombi ya kumuondolea Lissu mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Kadushi amedai kuwa Mkurugenzi wa mashtaka Nchini (DPP), ameona hana nia ya kuendelea na mashtaka yaliyopo mahakamani dhidi ya Lissu chini ya kifungu cha sheria namba 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA),

Aidha kwa mujibu wa kifungu hicho kinampa mamlaka DPP ya kumuondolea mashtaka mtuhumiwa kabla ya kusikiliza ushahidi lakini anaweza kukamatwa na kushtakiwa upya.

Hakimu Shahidi amesema kwa kuwa upande wa Jamhuri umeomba kumwondolea mshtakiwa mashtaka na kwamba hawana nia ya kuendelea na keshi hiyo mahakama yake imekubaliombi Hilo.

“Mahakama hii inamuachia mshtakiwa chini ya kifungu cha (91) (1),  kama upande wa Jamuhuri ulivyowasilisha maombi yao dhidi ya mshtakiwa” alisema Shahidi.

Lissu alifikishwa mahakamani hapo mapema February akadaiwa kuwa, Januari 11 mwaka huu alitoa matamshi ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani.

BOSI WA ZAMANI WA MSD APANDISHWA KIZIMBANI LEO

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Bohari Kuu ya Madawa Tanzania (MSD), Cosmas Aron Mwaifani amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababisha kampuni ya H.H Hillal kupata manufaa ya zaidi ya shilingi milioni mia nne.

Mwaifani anashtakiwa pamoja na aliyekuwa Meneja Manunuzi wa MSD Fredrick Rubanga Nicolous.

Mbele ya Hakimu Mkazi Respicius Mwijage, wakili wa serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leornad Swai akisaidiana na Aneth Mavika alidai kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi  1 hadi 19 mwaka 2013 huko katika makao makuu ya MSD  yaliyopo Temeke jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kuwa siku ya tukio washtakiwa hao wote kwa pamoja wakiwa waajiriwa wa MSD walitumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa na kufanya mabadaliko ya mkataba namba 1 yenye kumbukumbu namba MSD/003/Q/G/2010/2011/60 wa Machi 1, 2013 na kuitisha nambambili wenye kumbu kumbu namba kama hiyo wa Machi 19,mwaka 2013.

Wakili Mavika amesema kuwa kitendo hicho kiliisababisha kampuni ya H.H Hillal kupata manufaa yasiyokuwa ya halali ya Shilingi 482,266,000/.

Washtwakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhmana baada ya kukidhi masharti ya dhamana waliyopewana mahakama iliyowataka kuwa na mdhamini mmoja kila mmmoja mwenye barua kutoa serikalini au taasisi yoyote inayotambulika na atakayeweka dhamana ya milioni 20.

Aidha mahakama imewataka washtakiwa hao kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika isiyopungua thamani ya shilingi milioni 200.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, Mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kuwasomewa washtakiwa maelezo ya awali, kwa mujibu wa wakili Swai upelelezi umekamilika.

WAZIRI NAPE NNAUYE AFUNGA FAINALI ZA KOMBE LA ULEGA CUP MKURANGA MKOANI PWANI

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia wachezaji wa timu ya mpira ya Kisiju wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwasalimia Waamuzi wa mpira wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati) akiteta jambo na Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa fainali za Kombe la Ulega zilizofanyika 05/03/2017 Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akimpongeza Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega kwa juhudi zake za muleta maendeleo kaaika jimbo lake na udahmini wake wa kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.
Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega akiongea na wageni waalikwa pamoja na wakazi wa wilayani hapo kuhusu maendeleo ya jimbo lake na lingo la kuanzisha Kombe la Ulega ambapo fainali za kombe hilo zimefanyika jana 05/03/2017 Wilayani hapo.

Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi Walalamikia Uvuvi Haramu Katika Bahari

$
0
0
Mwananchi Mvuvi wa Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kuhusiana na uvuvi haramu unaofanywa na baadhi ya makampuni katika ukanda wao wa bahari ya nungwi kwa kutumia bunduki na mishale wakati wa uvuvi wao na kuwakimbiza samaki katika maeneo hayo na wao inawalazimu kwenda kuvua sehemu ya mbali na eneo hilo kutokana na samaki kukimbilia maeneo mengine, wameitaka taasisi husika kulichunguza hilo.
Mwananchi wa Kijiji cha nungwi Unguja akizungumza na waandishi wa habari kero yao kwa waandishi kutokana na kukithiri vitendo vya uvuvi haramu, Wao wameachana na uvuvi haramu wa kutumia nyavu za matundu madogo na kuendelea kuvua kwa uvuvi unaotakiwa na Serikali kwa kutumia nyavu za macho makubwa.  
Wavuvi wa Kijiji cha Nungwi wakiwa katika eneo la ufukwe wa bahari hiyo wakati wakiongea na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali waliofika katika ukanda huo wa pwani ya nungwi wakiwa katika kazi zao za kawaida.

Africa’s Richest Man, Dangote, happy with Magufuli’s leadership style.

$
0
0
By Staff Reporter-Tanzania Information Services- MAELEZO


African’s wealthiest person, Alhaj Aliko Dangote said, on Sunday, that he was content with the leadership style of President Dr. John Pombe Magufuli and vowed to continue working with him and his government.

Welcoming the president and his delegation at Dangote cement factory in Mtwara, Alhaj Dangote said he was satisfied with every effort taken by the President and his government to strengthen investment climate in the country.

“It is a great honor and privileged to our company to have been given such an opportunity to make such a big investment in Tanzania which is worth US $650m” Alhaj Dangote told the President.

He added that his company was ready to continue supporting government measures in addressing socio economic challenges as part of the implementation of the company’s program of corporate social responsibility.

Alhaj Dangote told President Magufuli that currently the factory was producing 750,000 to 770,000 tons per year but this year production would be raised to one million tons and in 2018 the factory would reach its production capacity of three million tons per year.

On new trucks, he said that the launching of the 580 trucks has given new hope to many low income earners in the country because the trucks would distribute cement all over the country and would allow to be sold at fordable price of not more than ten thousand shillings.

WAZIRI MWIGULU, WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAJADILI UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI WA MWAKA 2016/2017 NA MALENGO YA MWAKA 2017/2018

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto meza kuu) akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/2017 na Malengo ya Mwaka 2017/2018. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara wakati wa Kikao cha Kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/2017 na Malengo ya Mwaka 2017/2018. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga wakati wa Kikao cha Kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti wa Mwaka 2016/2017 na Malengo ya Mwaka 2017/2018. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 110104 articles
Browse latest View live




Latest Images