Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1598 | 1599 | (Page 1600) | 1601 | 1602 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack ametoa msaada wa mabati 171 kwa shule za msingi tatu wilayani Kishapu mkoani hapa kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa pindi yatakapokamilika ujenzi wake.

  Telack alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi, kata ya Mwaweja wilayani hapa alipofanya ziara ya kikazi ambapo pia alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao.

  Katika msaada huo jumla ya shule tatu za Nyenze iliyopo kata ya Idukilo, Mwasubi kata ya Bunambiyu na Ilobi kwenye kata ya Mwaweja zitanufaika na msaada huo wa mabati 57 kila moja.

  Akiwa katika ziara hiyo ya kikazi wilayani hapa, Telack aliagiza wazazi wote kijijini hapo wawapeleke watoto wao na kuwaandikisha shuleni ambapo alisisitiza umuhimu wa elimu kwao.
  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja alipofanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya, Shadrack Kengese.
  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya wakifuatilia mkutano wa hadhara kijiji cha Ilobi kata ya Mwaweja wakati wa ziara ya mkuu wa mkoa wilayani Kishapu,mkoani Shinyanga.
  Mmoja wa wananchi wa kijiji cha Ilobi akitoa kero yake kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack wakati wa mkutano wa hadhara kijijini hapo.
  Wananchi wa kijiji cha Ilobi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wakati akizungumza nao kuhusu maendeleo alipofanya ziara ya kikazi.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amewataka wazazi kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli kwa kuchangia maendeleo ya elimu.

  Kumbilamoto amesema hayo katika mkutano wake na wazazi wa shule  ya Msingi Miembeni kata ya Vingunguti .

  “lazima niwambie ukweli, hili suala la elimu bure limetusaidia sana katika kata yetu ya vingunguti, hivyo ni vyema kila mtu akawa na wajibu wa kuchangia angalau kidogo katika maendeleo ya elimu kama sadaka ili watoto wetu waishi katika mazingira mazuri” amesema Kumbilmoto.

  Kumbilamoto ametolea mfano uwepo wa mabembea katika shule za msingi katika nchi za falme za kiarabu, ambako alikuwa mapumzikoni hivi karibuni ,amesema shule za vingunguti lazima ziwe na bembea kama za uarabuni.

  Aidha amepata kuchangia ndoo mbili za rangi na makopo manne kwa ajili ya kupakwa katika darasa la kwanza .

  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Idaya Ndevu mbili alimshukuru Meya huyo kwa msaada wake na kumuomba aendelee na moyo huo huo.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto akizungumza na wazazi wa mtaa miembeni katika kikao cha kamati ya shule.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akikabidhi makopo ya rangi kwa kamati ya shule ya msingi miembeni
  Baadhi ya Wananchi na Wazazi wakiwa wamekaa kwa makini wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala
  Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Miembeni,Idaya Ndevumbili akizungumza na wazazi wa shule hiyo


  0 0


  Mzee Alinanoswe Aspain Mwambapa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya anawatafuta ndugu zake wakiwemo kaka zake na dada zake baada ya kupotezana nao kwa Zaidi ya miaka Kumi iliyopita.

  Kwa mujibu wa Mzee huyo ameuomba mtandao huu kumsaidia kuwatafuta dada zake ambao ni Eni Aspain Mwambapa anayeishi Dar es salaam,pamoja na Buni Aspain Mwambapa Mkazi wa songea kwa sasa.

  Wengine ambao mzee Alinanoswe anawatafuta ni kaka zake Ismail Aspain mwambapa Pamoja na Obole Aspain Mwambapa ambao wote walipotezana Takribani miaka Kumi iliyopita.
  Mzee huyo ameueleza mtandao huo kuwa alitengana na ndugu zake hao mwaka 2001 Chunya mbeya na kutimkia Pwani ambapo mpaka sasa anaishi huko,ambapo sasa anatamani kurejea nyumbani kwake lakini hajui jinsi gani ya kuwapata ndugu zake na sasa anaishi kwa wasamaria wema walioamua kumhifadhi.

  Mzee huyo alizaliwa mwaka 1961 Tukuyu mbeya.

  Kwa mweye kumjua mzee huyu atoe Taarifa kwa namba zifuatazo ili akutanishe na ndugu yake ,

  Namba

  0713 562954 Augustino Michael
  0789682901 Lister Godfrey
  0789421644 Frank Michael
  0718 528632 Frank Michael
  0769 56 2954 Augustino Michael.

  0 0


  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Baraza la madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam kwa kauli moja limepitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kwa kuungwa mkono na madiwani wote waliozuru katika mkutano maalumu wa baraza hilo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kaimu Afisa habari na Uhusiano wa Manispaa hiyo Bi Maria Makombe imeeleza kuwa Katika mpango huo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo inakadiria kukusanya/kupokea kiasi cha Tshs 128,611,616,805.100 ambazo zimeelekezwa katika matumizi ya mishahara, utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na matumizi mengineyo.

  Fedha hizo zitatokana na makusanyo ya ndani ya Halmashauri, Ruzuku kutoka serikali kuu, Michango ya wananchi na wahisani wa Maendeleo.Aidha Halmashauri inatarajia kupokea kiasi cha Tshs 4,233,546,143.00 kutoka TAMISEMI kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara (Road Fund).

  Katika fedha hizo chanzo cha makusanyo ya ndani ni Tshs 24,006,600,000.00 ambayo ni Sawa na asilimia 26% ya bajeti, Michango ya wananchi ni Tshs 500,000,000 Sawa na asilimia 1% ya bajeti, Mfuko wa barabara ni Tshs 4,233,546,143.00 Sawa na asilimia 4% ya bajeti na ruzuku kutoka serikalini na wahisani wa maendeleo ni Tshs 59,892,884,406.00 Sawa na asilimia 69% ya bajeti.
  Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (Picha zote na Nassir Bakari)
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 kulia kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob
  Kushoto ni Muweka hazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Bi Jenny Machicho, Afisa utumishi Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ally Juma Ally, na Mchumi wa Halmashauri ya manispaa ya Ubungo Yamo Wambura wakiwa katika kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kupitisha makisio ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 (kushoto) ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo Mhe Ramadhan Kwangaya na (kulia) ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo 


  0 0

   Baadhi  ya madarasa ya shule ya msingi Tumaini iliyopo kata ya Kashai, wilaya ya Bukoba Mjini ambayo wanafunzi watahamishwa kwa kujenegwa shule nyingene katika eneo la mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai kutokana na usalama baada ya kuwa karibu na eneo la Kiwanja cha Ndege cha Bukoba.
   Baadhi ya majengo mapya ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Tumaini, yaliyopo mtaa wa Mafumbo, kata ya Kashai yakiwa kwenye hatua ya mwisho ya ujenzi wake. Shule hii inamadarasa 24 ya kuanzia darasa la kwanza hadi la Saba, na madarasa matatu kati ya hayo ni ya watoto wenye mahitaji maalumu.
   Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Rwambaizi ya Karagwe wakiwa  kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba, katika ziara ya mafunzo.
   Abiria wakiwasilisha taarifa zao ikiwemo na ukaguzi wa tiketi, kabla ya kupanda ndege ya Auric  wakitokea kwenye kiwanja cha ndege cha Bukoba wakielekea Mwanza.
  Msimamizi wa Kitengo cha Usalama, Bi. Theodora Myaka wa Kiwanja cha ndege cha Bukoba (kushoto) akimkagua abiria Bi. Jasmindee Dhaliwa, Raia wa Bulgaria huku Afisa Usalama Msaidizi, Bw. Reginald Baraka akiangalia.

  0 0

   Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar , Mhandisi Hamad Masauni,  akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi ambalo matendo ya uhalifu ikiwepo utumiaji wa dawa za kulevya na uporaji  hufanyika hapo ambapo ameuagiza uongozi wa Jeshi la Polisi kushirikiana na wananchi kuhakikisha wahalifu hao wanakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya sheria.
   Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jeraha la mmoja wa wananchi wa eneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa wa Mjini Magharibi, ambaye wiki chache zilizopita alijeruhiwa na mapanga na watu wanaofanya matendo ya uhalifu katika eneo hilo.
   Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mjini Magharibi, ASP Suleiman Khamis Juma, akizungumza na vyombo vya habari juu ya hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uhalifu katikaeneo la Mwanyanya Mikoroshini lililopo mkoa huo, wakati wa ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Idara ya Siasa na  Uhusiano wa Kimataifa  Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kutembelea maeneo sugu ya uhalifu.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kufungua rasmi Jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa  Beno Ndulu mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya watoto  mkoani Mtwara waliomfata kumsalimia mara baada ya kufungua jengo la Ofisi ya kutoa Huduma za Benki Kuu ya Tanzania Tawi la Mtwara.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara. Wengine katika Picha ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Nehemia Mchechu. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza  Mbunge wa Mtwara mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Maftah Nachuma kabla ya kufungua rasmi Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha leo mkoani Mtwara.
  Sehemu ya Nyumba hizo za Gorofa za Shirika la Nyumba la Taifa NHC katika eneo la Raha Leo mkoani Mtwara. PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi wakuu wa Vikosi vya Ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo wakati alipokuwa akiondoka Nchini kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),katika safari hiyo akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Mawaziri na Viongozi mbali mbali
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakiagana na Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati alipokuwa akiondoka Nchini leo kueleke Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe,Balozi Seif Ali Iddi leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar alipokuwa akiondoka Nchini kuelekea Indonesia kumuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika Mkutano wa kwanza wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (IORA),[Picha na Ikulu.] 04/03/2017.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla maalumu ya kuwakaribisha viongozi wa Serikali itakayofanyika Machi 5 mwaka huu mkoani Dodoma.

  Hafla hiyo imeandaliwa na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Dodoma na itafanyika mkoani humo katika viwanja vya Nyerere (Nyerere Square) kuanzia saa 8 kamili mchana.

  Afisa Habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma, Jeremia Mwakyoma ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya ujio wa viongozi hao katika Mkoa huo.

  Mwakyoma amesema viongozi wa Serikali kuhamia katika Makao Makuu ya Nchi ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano hivyo Mkoa utawakaribisha rasmi Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara waliohamia kutoka Jijini Dar es Salaam.

  “Tukio la viongozi wa Wizara kuhamia Makao Makuu Dodoma ni la kihistoria ndio maana uongozi wa Serikali ya Mkoa umeona ni vema kuweka utaratibu rasmi wa kuwakaribisha viongozi hao,”alisema Mwakyoma.

  Afisa Habari Mwakyoma amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa huo pamoja na Mikoa ya jirani kuhudhuria kwa wingi kwenye hafla hiyo.Mnamo Julai 25 mwaka 2016 katika maadhimisho ya siku ya mashujaa yalioadhimishwa mkoani Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli alitangaza rasmi Serikali kuanza mchakato wa kuhamia Dodoma ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Nchi.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Dodoma, Makao Makuu ya nchi na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wengine ambapo kesho atakuwa mgeni Rasmi kwenye Hafla Maalum ya kuwakaribisha Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara pamoja na watumishi wote wa umma waliohamia Makao Makuu Dodoma wakitokea Dar es Salaam kama sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe Rais na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi .
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mwenyeji wake,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana 

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta kitambaa pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika Ujenzi wa  Gati namba mbili litakayojengwa katika Bandari ya Mtwara.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania  Mhandisi Deusdedit Kakoko kuhusu eneo ambalo Bandari ya Mtwara walikuwa wakilihitaji kutoka sehemu nyingine.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Newala George Huruma Mkuchika mara baada ya kuwasili katika eneo la Bandari ya Mtwara.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Mtkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiaria ufunguzi rasmi wa Kituo cha Biashara cha Benki hiyo mkoani Mtwara
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kuhusu ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mnolela ambapo pia amechangia kiasi cha Shilingi milioni 15 na akamuagiza Mbunge huyo kuchangia Shilingi milioni 10 kutoka fedha za jimbo.
  Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mbunge mteule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akifUatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati aliposimamishwa njiani na Wanakijiji wa Madangwa katika jimbo la Mtama mkoani Lindi. PICHA NA IKULU


  0 0


  0 0
  0 0

  BMGHabari

  Rais wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, Ndibalema Mayanja, amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa ya ununuaji wa hisa za kampuni ya TCCI Investment.

  Mayanja ameyasema hayo Jijini Mwanza hii leo na kubainisha kwamba hisa hizo zilianza kuuzwa tangu Februari Mosi mwaka huu kwa bei ya shilingi Mia Nne na kwamba mwisho wa uuzwaji wa hisa hizo ni Machi 14 mwaka huu.

  "Njia pekee ya kijiendeleza kiuchumi hivi sasa ni kupitia hisa hivyo nunueni hisa hizi za kampuni ya uhakika ambayo kila mwaka huwapatia wanahisa wake gawiwo lao". Amesisitiza Mayanja na kuongeza kwamba hisa hizo zinauzwa katika benki ya CRDB na kwa mawakala mbalimbali walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko na Dhamana (CMSA).

  Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mwanza, Joseph Kahungwa, amebainisha kwamba walionunua hisa za TCCIA Investment mwaka 2005 kwa shilingi 250, hisa zao zimepanda bei hadi shilingi 5,000 hivyo pesa hiyo iligawanywa na kupatikana bei ya shilingi 400 ya kuuza hisa mwaka huu ambapo kwenye mauzo hayo kila mwanahisa atapata gawio la hisa 12.5 kwa kila hisa moja.

  Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, mesema jumla ya hisa Milioni 112 zinatarajiwa kuuzwa lengo ikiwa ni kampuni ya TCCIA Investment kupanua mtaji wake na kufikia Bilioni 45 kutoka Bilioni Nane za mwaka huu 2017 ambazo zimeongezeka kutoka hisa Bilioni Moja mwaka 2005 wakati kampuni hiyo inaanzishwa.

  Amedokeza kwamba hatua hiyo itasaidia TCCIA kuongeza uwekezaji wake ikiwemo ujenzi wa majengo ya kisasa na maghara ya kuhifadhia mazao katika mikoa ya Dar es salaam, Dodoma, Mtwara na Tanga pamoja na kuanzisha taasisi ya mikopo.
  Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, Ndibalema John Mayanja (katikati), akizungumza hii leo Jijini Mwanza kwenye mkutano na wadau mbalimbali wa biashara. Kulia ni Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, na kushoto ni Mshauri TCCIA mkoani Mwanza, Lazaro Kiheya.
  Makamu Mwenyekiti TCCIA mkoani Mwanza, Leopord Lema, akisisitiza juu ya umuhimu wa watanzanua kununua hisa za Kampuni ya TCCIA Investment. Pia amesema TCCIA itaendelea kushirikiana na serikali katika kuondoa changamoto za kiuwekezaji zilizopo ikiwemo upimaji wa maeneo ya ujenzi wa viwanda pamoja na uwanja wa maonesho ikiwemo Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki
  Baadhi ya wafanyabiashara na wadau wa biashara na uwekezaji wakifuatilia mkutano huo.  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto),  na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakibadilishana hati ya makubaliano yenye mkakati wa kuhakikisha nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda, zinakuwa salama hususan maeneo ya mipakani na hata kwenye barabara zote zinazotumiwa na wafanyabiashara, IGP Mangu, pamoja na ujumbe wake amefanya ziara ya kikazi nchini humo jana.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, akiwa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja nchini humo jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda 
     Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (mbele kushoto) akitoa neno mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Rwanda, (IGP) Emmanuel K. Gasana, pamoja na ujumbe alioongozana nao nchini humo jana, katika ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.
     Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Ernest Mangu (Kushoto), akiwasili nchini Rwanda, na kupokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini humo, (IGP) Emmanuel K. Gasana (Kulia) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja jana, yenye lengo la kuimarisha mahusiano, kushirikiana na kufanyakazi kwa pamoja katika kudhibiti uhalifu na wahalifu hususan maeneo ya mipakani kwa lengo la kukuza uchumi baina ya nchi zote mbili ya Tanzania na Rwanda.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  0 0


  Safari hii iliandaliwa na Asasi mbili za Uyole Cultural Tourism Enterprises na ELIMISHA kwa ushirikiano na Chama cha waendesha baiskeli Mkoa wa Mbeya na Afisa Utamaduni wa Mkoa Bw.George Mbijima.
  Awali, akiongea na wapenzi wa mchezo wa baiskeli,viongozi wa serikali na wanahabari
  Awali, wakati wa kuwaaga waendesha baiskeli Makamu mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Elias Mwasandele amewashukuru wadau mbalimbali wanaoendelea kuwaunga mkono zaidi sana Uyole Cultural Tourism na ELIMISHA kwa kufanikisha jambo hilo.
  Aidha,kwa kushirikiana na mhazini wake  wa mkoa Bw.Lucas Mhagama wameutanabaisha umma kujiunga na mchezo huo kwani ni mzuri na una maslahi mazuri kwa mchezaji na Taifa kwa ujumla.
  "....kama Mkoa wa Mbeya tumebahatika kupata mwaliko wa kupeleka wachezaji wanne kwenye mashindano ya baiskeli yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika ya Kusini...."Bw.Mwasandele alisikika akisema.
  Baada ya kupata baraka zote za mkoa kutoka kwa Afisa Utamaduni Bw.George Mbijima aliyewaasa wachezaji kuimarisha umoja,upendo na mshikamano muda wote wa safari.
  Waendesha baiskeli wafuatao walisafiri kutoka Mbeya Mjini hadi Wilayani Chunya umbali wa Kilomita 70, Tumejumuisha na muda waliotumia kufika:
  1.Ipyana Mbogela-Saa 2:15
  2.Elias Zawadi-Saa 2:17
  3.Diego Fumbo-Saa 2:28
  4.Moses Mwadonde-Saa 2:34
  5.Daudi Selemani-Saa 2:56
  6.Kianji Samson-Saa 2:59

  Hata hivyo wachezaji wawili walishindwa kumaliza safari hiyo kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwa baiskeli zao kupata pancha wakiwa wamebakiza Kilomita 10 kumaliza safari nao ni Kristola Senga na Pasia Tanganyika.
  Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima (wa katikati aliyevaa tracksuit ya Taifa) akiwa katika picha ya pamoja na waendesha baiskeli pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Uyole Cultural Tourism Enterprises na Elimisha kabla ya safari ya kuelekea Chunya
  Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Mbeya Bw.George Mbijima akizungumza na waendesha baiskeli,viongozi na wananchi katika eneo la Rift Valley wakati akiwaaga waendesha baiskeli
  Waendesha baiskeli wakiingia Wilayani Chunya baada ya kumaliza Kilomita 70 kutokea Mbeya Mjini.

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga amesema kuwa vita ya kupambana na dawa za kulevya ni kubwa kutokana na kila siku watu wanabuni njia mpya.
  Vita ya dawa za kulevya sio lelema kutokana na kuwa watu ambao wana mbinu nyingi za kufanya hivyo, lakini watakamatwa wote na hatuingii kichwa kichwa katika kufanya kazi hiyo.
  Akizungumza leo katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House) kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

  “Watu watano tumewakamta na mmojawapo aliyekuwa anasambaza dawa za kulevya Tanzania Bara na Zanzibar na jumla zaidi watu 11000 wamekamatwa ’’amesema Sianga.
  Sianga amesema mtandao wote unaofanya biashara ya dawa za kulevya wameukamata, na wanaendelea kupokea taarifa mbalimbali za kuweza kutokomeza mtandao wa kuingiza dawa hizo.
  Amesema wanatumia njia tatu katika kupata taarifa za watu wanaofanya biashara hiyo moja ni taarifa za watu za moja kwa moja ya pili utafiti pamoja wananchi.
  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakizungumza katika hafla ya timu ya Serengeti Boys chini ya miaka 17 kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani jana.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akizungumza katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani juu ya viongozi wa dini walivyo mstari wa mbele katika kupambana na dawa za kulevya.
  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Siangaakimkabidhi cheti , Rais wa TFF, Jamal Malizi katika hafla Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu walioadhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober Hoouse)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
  Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini,Rogers Sianga akimkabidhi cheti , Mwakilishi Michuzi Media Group,Emmanuel Massaka katika hafla ya Timu ya Vijana chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) kutembelea kituo cha watu waliodhirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sober House)kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
  Wadau mbalimbali.

older | 1 | .... | 1598 | 1599 | (Page 1600) | 1601 | 1602 | .... | 3286 | newer