Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Kilimanjaro Music Awards 2013 ni kesho pale pale mlimany city

$
0
0
Kilele cha tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Music Awards kinatarajia kufanyika siku ya Jumamosi, Juni 8 katika ukumbi wa Mlimani City kwa kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri katika kipindi cha mwaka 2012. Kwa mara ya kwanza mwaka huu kutakuwa na tukio la Red Carpet ambapo watu maarufu watapita kupiga picha na kufanya mahojiano ya moja kwa moja na muendeshaji ambaye ni mtangazaji wa kituo cha Channel O, Jokate Mwegelo.

Tuzo hizi zitaonyeshwa live kupitia katika mtandao wa Internet huku watumiaji wa simu za mikononi na kompyuta wasioweza kufuatilia kupitia TV zao wakiweza kutazama mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager (www.facebook.com/kilimanjaropremiumlager) na pia mtandao wa LIVESTREAM (http://new.livestream.com/KTMA2013/live) .

Wakati wa zoezi la utoaji tuzo washindi wote watapata nafasi ya kuongea na kuwashukuru mashabiki katika Social Media Lounge itakayoendeshwa na Millard Ayo kutoka Clouds FM na Sam Misago kutoka East Africa TV. Picha za matukio na kinachoendelea katika ukumbi wa Mlimani City zitakuwa zikirushwa moja kwa moja katika mtandao wa Twitter na Instagram ambayo ni ( @Kili_Lager).

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, JOHN CASMIR MINJA AWAPANDISHA VYEO ASKARI 984

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja leo amewapandisha Cheo Jumla ya Askari Magereza 984 kuwa Koplo wa Magereza, kati yao wanaume ni 845 na wanawake ni 139 baada ya kuhitimu ya kuhitimu Mafunzo ya Uongozi katika Chuo cha Magereza Kiwira, Mbeya.

Akifunga Mafunzo ya Uongozi wa Daraja la Kwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga amewapongeza wahitimu hao kwa kufanya vizuri katika masomo Yao na hivyo kustahili kuwa Viongozi katika ngazi ya kwanza(NCO's) katika Jeshi la Magereza.

Amewaasa kuzingatia kikamilifu weledi katika kutekeleza majukumu yao ya kazi na kuhakikisha Kuwa wanalinda, kutetea pamoja na kusimamia haki za wafungwa kwa mujibu wa taratibu za Magereza ili kulinda utu wa Wafungwa pamoja na hadhi ya Jeshi la Magereza.

Wahitimu hao wameshiriki kikamilifu katika Mafunzo ya Nyanja zinazohusu Utawala na Uendeshaji wa Magereza, Ustawi wa Jamii, Uraia, Afya pamoja na Mafunzo ya Kijeshi. Pia kwa kuzingatia madhara ya Adui rushwa, wahitimu hao wamefundishwa kwa kina juu ya madhara yatokanayo na rushwa, mazingira na vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Pia wahitimu hao wa Kozi Namba 20 ya Uongozi daraja la kwanza wamepongezwa na Mgeni rasmi, Kamishna Gaston Sanga kwa mchango wao wa hiari kwa kujitolea Tsh. 2,000,000/= kwa ajili ya kuboresha jiko na miundombinu mingine ya Chuoni hapo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGUA KONGAMANO LA USHINDANI WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel mjini Arusha leo Juni 7/2013. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Bw. Lawrance Masha wakati wa ufunguzi wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel mjini Arusha leo
Wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World Economic Forum) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal alipokua akifungua Kongamano hilo leo katika Hoteli ya New Arusha Hotel mjini Arusha leo Juni 7/2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World Economic Forum) na kufanyika New Arusha Hotel mjini Arusha leo Juni 7/2013. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika mashariki Richard Sezibera baada ya kufungua kongamano kuhusu ushindani kwa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lililoandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani( World Economic Forum)na kufanyika New Arusha Hotel mjini Arusha leo Juni 7/2013.

Balozi wa Ujerumani nchini amuaga Waziri Muhongo

$
0
0
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Klaus Peter Brandes amemshukuru Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ushirikiano aliompa kwa kipindi cha miaka miwili alichofanya kazi hapa nchini.

Ametoa shukrani hizo alipomtembelea Waziri Muhongo ofisini kwake mapema leo Juni 7, jijini Dar es Salaam kwa nia ya kumuaga rasmi.

Akipokea shukrani hizo, Profesa Muhongo amesifu utendaji mzuri wa Wajerumani katika nyanja mbalimbali na kumwomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Serikali yake kuwa wanakaribishwa kuja kuwekeza nchini Tanzania katika miradi ya uzalishaji na usambazaji wa umeme.

“Tunakaribisha kampuni za kijerumani zenye uwezo na zilizo makini kuja kuwekeza hapa nchini, hususan katika miradi ya umeme unaotokana na jua, upepo, majimoto na nishati mbadala,” amesema Waziri Muhongo.

Balozi Brandes anamaliza muda wake rasmi hapa nchini Juni 13 mwaka huu.
Balozi Klaus Peter Brandes (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), katika ukumbi wa mikutano wa wizara. Kulia ni baadhi ya maafisa wa wizara.

TAASISI YA HASSAN MAAJAR TRUST YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI 320 KUSAIDIA ELIMU MKOANI RUKWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la mwananfunzi aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati 320 yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini.  Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja na nusu ili aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni sehemu ya azimio alilolianzisha na kuliita "Azimio la Kasense" KADARU (Kampeni ya Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Taarifa toka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo

MAHAFALI YA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NAMBA 20 KWA ASKARI MAGEREZA YAFANA MKOANI MBEYA

$
0
0



















Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya
Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheo cha Ukoplo Askari B4448 Patric Babara kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

ROSEMARY PETER AVISHWA TAJI LA REDDS MISS NYAMAGANA 2013, BAADA YA MSHINDI WA TAJI HILO DIANA AMIMO KUDANGANYA URAIA NA UMRI WAKE

$
0
0
Rosemary Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.

Alhamisi ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.

Udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja mara baada ya shindano hilo.

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24, Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013/14
Redds Miss Nyamagana 2013/14 Rosemary Peter katika pozz, mara baada ya kutawazwa rasmi kushika taji hilo, katika hafla fupi iliyofanyika katika hotel ya New Mwanza ya kumvua aliyekuwa akishikila taji hilo Mrembo Diana Amimo baada ya kudanganya Urai wake na Umri.
Mkurugenzi wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Sash Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013.
Mkurugenzi wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada ya kuvishwa taji hilo.

Morocco inafungika kwao - Kim Pousen

$
0
0
Nahodha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Juma Kaseja akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Pullman ilikoyo Marrakech,nchini Morocco.Kushoto ni Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen.

Marrkech, Morocco

Huku Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi) dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia, Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.

Kocha huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.

“Wachezaji wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.

Alisema suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars, inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.

Alisema Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.

“Unapocheza mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana katika mechi hii,” alisema.

Poulsena alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio timu ndogo kama wanayodhani.”

Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.

“Katika hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.

Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.

Naye nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya kuelekea Marrakech.

“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.

Naye Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara nyingine kwa kushinda mechi hiyo.

“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.

Stars iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na Gambia 1.

Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania. Baada ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu.

Diwani wa kata ya Kikole Mkoani Lindi anusurika ajalini

$
0
0
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi,Mwanja Ibadi pamoja na Diwani wa kata ya Kikole,Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa,Mkoani Lindi,Haji Mulike wamenusurika kupoteza maisha katika ajali waliyoipata,wakiwa njiani kuelekea Wilayani Nachingwea,kwa shughuli za kikazi.Katika ajali hiyo mtu mmoja alipata majeraha Madogo.Picha na Abdullaziz Video
Gari walilokuwa wakisafiria Wadau hao likiwa limepinduka huku huzuni ikitawala katika eneo hilo.

The Newly appointed Tanzanian Ambassadors with their spouses, completed a one week induction Diplomatic Course at The Centre For Foreign Relations in Dar

$
0
0
Standing on the back row, from right to left: Ambassador Mbarouk Nassor Mbarouk, Mrs. Raiyan Mbarouk, Ambassador Modest Mero, Mr. John Ng'ongolo (lecturer) Front row, from left to right: Mrs. Irene Kilumanga, Ambassador Chabaka Kilumanga, Ambassador Liberata Mulamula, Mrs. Rose Mero, Ambassador Dr. Mohammed Omar Maundi (Director of The Center for Foreign Relations), Ambassador Wilson Masilingi and Mrs Marystella Masilingi.

NGOMA AZIPENDAZO ANKAL

$
0
0
Ngoma ya The Temptations ya 'Treat Her Like A Lady' ni balaa hadi hii leo

MIONDOKO YA KUMEREMETA KWENYE MNUSO

MKATAA KWAO MTUMWA

KILA LA KHERI TAIFA STARS

$
0
0
CAPTAIN JUMA KASEJA NA KIKOSI CHAKO CHA KAZI, NAPENDA KUWATAKIA KILA LA KHERI KESHO MTAKAPOTINGA HAPO VIWANJA VYA GRAND STADE MJI WA MARRAKECH KUPAMBANA NA MOROCCO.
NINA IMANI YA KUWA WATANZANIA WOTE TUKO NYUMA YENU, TUNAWAAMINI NA TUNATHAMINI UZALENDO WENU. TUNA IMANI YA KUWA MTATUMIA WEMBE ULEULE MLIOWANYOLEA HAWA WAMOROCCO UWANJA WA TAIFA NA KUWABWAGA 3-1, KWA MAKALI YALE, AMA ZAIDI KWA NIA MOJA TUU YA KUFIKA BRAZIL 2014 ……
PAMOJA NA SALAMU NAPENDA KUWATAARIFU KUWA WANA DIASPORA WA LONDON TUMEJIPANGA VIZURI ILI KUWA NYUMA YENU KATIKA SAFARI YOTE . KIKOSI KABAMBE CHA WASHANGILIAJI, KIMEONDOKA LONDON JIONI HII KUJA MARRAKECH ILI KUWAUNGA MKONO.
KIKOSI HICHO, KIKIONGOZWA NA “MEYA WA JIJI”   SIR.HARUNA MBEYU, KITAKUWA PALE “GRAND STADE” NA MAVUVUZELA YA HATAREEEE TAYARI KWA MPAMBANO HUO. 
TUKO BEGA KWA BEGA NA NYINYI MPAKA 2014 NDANI YA “ESTADIO DO MARACANA”, RIO DE JANEIRO……
NAWATAKIA USHINDI MKUBWA NA MCHEZO MWEMA “FAIR PLAY”.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TAIFA STARS.
MWENYEZI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
TAIFA STARS OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE……………!!
Mariam Mungula -MwanaDiaspora

#TeamTaifaStarsUK.

Maalim Seif mgeni rasmi kombe la mashindano ya Vyuo Vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE)

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi kikombe cha ushindi kwa timu ya Chuo cha Afya Mbweni, baada ya kupata ushindi katika mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE). Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Haji Mwita.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua timu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, wakati ikijiandaa kuvaana na timu ya Afya Mbweni, katika fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) iliyofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua kikosi cha timu ya Chuo cha Afya Mbweni, wakati ilijiandaa kuvaana na timu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, katika fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu ya juu Zanzibar (ZAHLIFE) iliyofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mashabiki mbali mbali waliojitokeza katika mchezo wa fainali za mashindano ya Vyuo vikuu na Taasisi za elimu Zanzibar uliofanyika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Maandamano ya Taasisi za elimu ya juu Zanzibar yakipita mbele ya mgeni rasmi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, katika shamra shamra za fainali ya mashindano hayo yaliyofanyika viwanja vya Amaan.

the Inter-Parliamentary Seminar at Nanyuki VII in Entebe Uganda.

$
0
0
Hon. Mukhisa Kituyi Secretary General UNCTAD presents the paper during the Inter-Parliamentary Seminar Nanyuki VII in Entebe Uganda.
Rt.Hon Magaret Nantongo Zziwa Speaker EALA adresses the Inter-Parliamentary Seminar Nanyuki VII in Entebe Uganda.
Rt. Hon Rebeca Kadaga Speaker Uganda Parliament adresses the Inter-Parliamentary Seminar Nanyuki VII in Entebe Uganda.
You Honorable thank you for coming Rt. Hon Rebeca Kadaga and Rt.Hon Magaret Nantongo Zziwa says when moving out of the conference hall during Inter-Parliamentary Seminar Nanyuki VII in Entebe Uganda.

CFA: Fung Global Fellows Program, Princeton Institute for International and Regional Studies, USA

$
0
0
Princeton University is pleased to announce the call for applications to the Fung Global Fellows Program at the Princeton Institute for International and Regional Studies (PIIRS). 

Each year the Program selects six scholars from around the world to be in residence at Princeton for an academic year and to engage in research and discussion around a common theme.

 Fellowships are awarded to scholars employed outside the United States who are expected to return to their positions, and who have demonstrated outstanding scholarly achievement and exhibit unusual intellectual promise but who are still early in their careers.

During the academic year 2014/15, the theme for the Fung Global Fellows Program will be "Global Diffusion." The Program seeks applications from scholars developing new, innovative ways to study global diffusion processes. 

The objects of diffusion could be specific modes of social categorization (such as "race" in census forms), principles of legitimation (such as democracy), government policies (such as minority quota systems, forms of conflict (such as revolutions), or cultural practices (such as Tango dancing or marrying "in white"). 

We especially encourage analytically oriented approaches that identify recurring patterns and mechanisms through rigorous comparison of multiple cases or quantitative analysis, with broad geographic (preferably trans-continental) coverage. Researchers working on all historical periods of the modern age, all regions of the world and of all disciplinary backgrounds in the social sciences and humanities are encouraged to apply.

Applications are due on November 1, 2013 (deadline 11:59 p.m. EST). To be eligible, applicants must have received their Ph.D. (or equivalent) no earlier than September 1, 2004. Fellowships will be awarded on the strength of a candidate's proposed research project, the relationship of the project to the Program's theme, the candidate's scholarly record, and the candidate's ability to contribute to the intellectual life of the Program. For more information on eligibility requirements and the application process itself, see the Program's website at http://www.princeton.edu/funggfp/
FOR  THE SOURCE, GUIDELINES OF APPLICATION  AND APPLICATION LINK https://jobs.princeton.edu/applicants/jsp/shared/position/JobDetail...

 
MAKULILO SCHOLARSHIP FOUNDATION
CALIFORNIA, USA

WABUNGE WA UINGEREZA WAFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UDOM

$
0
0
Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza umewasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake. Baada ya kupokelewa uwanja wa ndege wa Dodoma na Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu, wabunge hao wakiwa na wenyeji wao walikutana na Makamu Mkuu wa UDOM Prof. Kikula na baadaye kufanya ziara fupi kwenye hospitali ya Chuo kitengo cha matibabu ya figo na sehemu ya utakasaji wa maji yanayotumika kwa upasuaji. Ziara ya UDOM iliitimishwa dhifa fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge ikiongowa na Naibu Spika wa Bunge Mhe. Job Ngugai pamoja na Katibu wa TWPG na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Angela Kairuki katika Hoteli ya Dodoma.
Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiukaribisha Ujumbe wa wabunge watano kutoka Uingereza uliowasili nchini na kutembelea Chuo Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake. 
Naibu Spika wa Bunge,Mh. Job Ndugai akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wageni wao kutoka nchini Uingereza.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angella Kairuki akizungumza na ujumbe huo.

wana Ushikia toka wilaya za Nachingwea,Liwale na Ruangwa Wakutana leo

$
0
0
Naibu waziri Tamisemi,Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa vyama vya msingi na Ushika kikao ambacho kilitoa azimio la kujitoa Ilulu Union na kuunzisha mchakato wa kuunda chama cha RUNALI UNION.
Baadhi wa wana Ushikia toka Amcos za wilaya za Nachingwea,Liwale na Ruangwa wakiwa katika kikao cha pamoja kuazimia kujitoa katika Ushirka wa ILULU.
Wajumbe 9 waliochaguliwa katika kikao hicho kuanzisha RUNALI Union na kuwezesha chama hicho kusajiliwa ili kianze kazi Msimu ujao wa mauzo ya korosho.

Na Abdulaziz Video-Nachingwea

Vyama 46 kati ya 51 vya msingi na ushirika vya wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Liwale,mkoani Lindi vimeazimia kujiondoa kwenye chama kikuu cha ushirika cha mkoa wa Lindi cha Ilulu na kuanzisha mchakato wa kuunda chama kipya cha ushirika cha wilaya hizo kitakachojulikana kwa jina la RUNALI Union.

Uamuzi huo ambao uliozamiwa jana kwenye kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu Nachingwea chini ya uenyekiti wa Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Tamisemi anayeshughulikia Elimu ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa,Kasimu Majaliwa ambapo viongozi vya vyama vya msingi vya wilaya hizo waliridhia kwa kauli moja kuachana na chama hicho cha ushirika cha Ilulu kwa kilichodaiwa kuwa kimeshindwa kuwasaidia wakulima hata kusababisha wakulima wa korosho washindwe kulipwa malipo yao yote ya pili kiasi cha kusababisha uvunjifu wa amani na uharibifu wa mali za viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya msingi na wa Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza kwenye kikao hicho,Naibu waziri Tamisemi Kassim Majaliwa alikitupia lawama chama kikuu cha Ilulu katika uendeshaji wake kiasi cha kusababisha wananchi kuichukia serikali yao kwani viongozi wake si waadilifu kwani wamekuwa wakijikusanyia kiasi kikubwa kupitia ushuru mbalimbali zisizo za lazima ambapo alibainisha kuwa licha ya wakulima kutopata malipo stahili chama cha Ilulu kimejipatia zaidi ya shilingi Bilioni 9.9 huku wakulima wenye wakiangaika kupata malipo ya pili Aidha kufuatia azimio hilo aliwaasa wanaushirika na Maafisa Ushirika wa wilaya hizo kutorubuniwa kipindi cha mchakato wa Kuanzisha mchakato wa Ushirika wa wilaya hizo zilizokusudia kujiondoa huku akiwataka kuomba notisi ya kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Ilulu ili vyama hivyo vijiondoe kwa mujibu wa Sheria za Ushirika.

Makamu mwenyekiti chama cha msingi cha Umoja cha wilaya ya Liwale,haguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa mchakato wa Kuanzisha RUNALI alitaja baadhi ya mambo yaliyotajwa kuwa ni chanzo cha kujiondoa kwa vyama hivyo vya wilaya tatu ni ukubwa wa eneo linalohudumiwa na Ilulu jambo linalofanya chama hicho kishindwa kutoa huduma mzuri kwa wanachama wake ucheleweshaji wa vitendea kazi yakiwemo magunia na vitabu kwani Ilulu ndio waliojipa uzabuni pekee wa kusambaza huduma hizo huku akieleza kuwa malengo ya Ushirika unaokusudiwa kuanzishwa yatasaidia kupunguza baadhi ya Gharama zisizo lazima zinazokatwa Amcos mbalimbali wakati wa mauzo ya Mazao.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo alitoa wito kwa Wanasiasa kuwafikia wakulima na kuwaeleza sababu za kuwepo kwa maendeleo ya wakulima ili kuepukana na ujanja uliokuwa unafanywa na Ilulu kutokana na Makato na upandishaji wa gharama mbalimbali za uendeshaji.

kikao hicho pia kilihudhuriwa na wabunge wa majimbo ya Liwale na Ruangwa na wakuu wa wilaya hizo tatu ambao kwa nyakati tofauti waliitaka kamati ya mpito iliyoundwa wajumbe 9 Chini ya Uratibu wa Maafisa Ushirika wa wilaya hizo kuanzisha mchakato wa usajiri wa RUNALI na kuharakisha zoezi hilo linakamilika haraka iwezekanavyo ili chama hicho kipya kianze kazi ya ununuzi wa zao la korosho nje ya Chama kikuu cha Mkoa ( ILULU) Msimu Ujao.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images