Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 159 | 160 | (Page 161) | 162 | 163 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sacoma group, Bwana. Sam Ochieng, namna ambavyo bidhaa za Matunda na Mboga mboga kutoka nchini Kenya zinavyopakiwa, kusafirishwa na hatimaye kuuzwa kwenye soko la Spitfield nchini Uingereza, kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma. Umoja huo wa Sacoma wenye lengo la kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wa africa ya Mashariki. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alifanya ziara kwenye Soko la Spitafields, lililopo Stratford nchini Uingereza, kwa lengo la kujionea shughuli za Jumuiya ya Sacoma inavyoendesha shughuli zake kwenye soko hilo na jinsi ambavyo Jumuiya hiyo imeweza kuwasaidia Wakulima wa Matunda na Mboga kutoka nchini Kenya, kupata soko la kuuza Bidhaa zao hapa nchini Uingereza.
  Mheshimiwa Waziri Mkuu, akiangalia na kupata maelezo ya Ubora wa bidhaa unaotakiwa kupata soko nchini Uingereza. Pichani, mstari wa pili, (kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ungereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, kwanza (kulia) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, Uingereza Bwana Yusuf Kashangwa, maofisa wa Ubalozi na Viongozi kutoka Tanzania ambao wameambatana na Waziri Mkuu nchini Uingereza kwenye Mkutano unaofanyika leo ambao unahusu jinsi ya kutokomeza njaa na umuhimu wa Lishe bora kwa Mama na Watoto Duniani (Hunger and Nutrition). Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi za kiserikali na zisizo za Kiserikali, unakutanisha nchi kubwa Duniani, zijulikanazo kama G8, Wadhamini, Wachangiaji na Watoa misaada kwenye Asasi hizo, zenye lengo la kutokomeza njaa duniani na kusaidia kuwapatia Wamama na Watoto Lishe bora.
  Mheshimiwa Waziri Mkuu, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Soko la Spitalfields. Kushoto ni Meneja wa Masoko wa Kikundi cha Sacoma, Mama Perez Ochieng - Meneja wa Masoko wa Jumuiya ya Sacoma.


  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, akijibu maswali ya wabunge wakati wa semina juu ya wajibu wa kamati za Bunge na Wabunge kupambana na rushwa, Semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Mandeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyofanyika Dodoma juzi.
  Mkuu wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii(dean of furcuty Arts and Social Science) kutoka chuo Kikuu cha Dodoma, Davis Mwamfupe, akiwakilisha mada kwa Wabunge juu ya wajibu wa kamati za Bunge na Wabunge wa kupambana na rushwa, Semina iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na Shirika la Mandeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), iliyofanyika Dodoma juzi.


  0 0

  IMG_0131
  Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa semina hiyo.
  IMG_0121
  Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani).


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimkabidhi cheti, Mkurugenzi wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville, cha kutambua mchango wa wake katika kufanikisha matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania, Kihara Maina
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Ltd,Teddy Mapunga akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania, Kihara Maina mara baada ya kupokea Cheti cha kutambua mchango wa wake katika kufanikisha matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. 
  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (pili kushoto) akiongoza Mazoezi kabla ya kuanza kwa Matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Viatnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.
   Mjumbe wa Chama Cha Kimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.
  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine.

  0 0

  Mshindi wa shindano la BE FORWARD PHOTO CONTEST ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda,Bwa.Sunday Robert akifanya mahojiano mafupi mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,namna alivyojishindia gari aina ya Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la mtandao wa kijamii wa facebook.
  Meneja mauzo  wa kampuni ya BE FORWARD .JP ambao ni wasafirishaji wa magari kutoka Japan kwenda nchi mbalimbali,Bwa.Eiichi Mizuyama akimkabidhi Bwa.Sunday Robert mfano wa funguo mara baada ya kujishindia gari aina ya   Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la  BE FORWARD PHOTO CONTEST lililofanyika kwa njia ya Mtandao wa kijamii wa facebook.

  Bwa. Eiichi Mizuyama alisema kuwa pamoja na kumpata mshindi huyo wataendelea kufanya shindano hilo na kuwapata washindi wengine,katika suala zima la kuhakikisha kampuni hiyo ya BE FORWARD .JP inaendelea kuwajali wateja wake kwa namna mbalimbali,ikiwemo na suala la zima la umakini mkubwa katika kusafirisha bidhaa zao zikiwa salama mpaka mlangoni kwa mteja wao.

  Bwa. Eiichi ameeleza kuwa pamoja na kuwa kampuni hiyo makao yake yako Japan,lakini pia wamefungua tawi la kampuni hiyo hapa nchini katika suala zima la kuwahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma zao za uhakika.

  0 0

  Taifa Stars ambayo inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade jijini Marrakech, Morocco, imefungwa hadi  bao 2-1 na mpira umekwisha.

  Awali Taifa Stars Ilipoteza mchezo wa  kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Mechi ya leo ni ya pili kwa Stars katika uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.

  0 0


  ARUSHA, Tanzania
  JIJI la Arusha limeendelea kujijengea sifa ya kuwa moja ya maeneo yenye vituko, kufuatia kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips, kata ya Sekei jijini humo, Hamad Rashid (32) kukamatwa leo akiiba stuli inayotumika kuwekea mwenge wa Uhuru wakati mwenge ukiwa katika mbio zake mkoani Arusha.

  Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwa ajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

  Kamanda wa polisi mkoa wa  Arusha Liberatus Sabas ameithibitisha kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.

  Alisema tukio hilo lilitokea wakati mwenge huo pamoja na wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine wakiwa katika harakati za usomaji wa salamu za utii kwa Rais, kabla ya kutangazwa ratiba ya mkesha.

  Kamanda Sabas alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo alionekana kwa muda mrefu akiwa anazengea  gari lililokua limebeba kiti hicho cha akiba bila kujua kwamba kulikua na askari waliokua wakimfuatilia nyendo zake.

  Alisema muda mfupi askari mmoja  alimuona kijana huyo akisogelea zaidi gari na kuingiza mkono kisha kuchomoa kistuli hicho kwa lengo la kuondoka nacho ambapo alishuka na kuanza kunyang’anyana nae kiti hicho.

  “Unajua ni ngumu hata kueleza maana mtu na akili zake anafanya kitu cha namna hiyo. Hicho kiti kilikua ni cha akiba na kilikua ndani ya gari la wazi la mamlaka ya maji ambalo ndani yake kulikua na askari ambae alimuona na hata alivyotakiwa kukiacha aliking’ang’ania na kuanza kunyang’anyana hadi askari wengine wakisaidiana na mgambo walipotokea”alisema Kamanda Sabas.

  Alisema mara baada ya kukamatwa alihojiwa na polisi waliomkamata ambapo alijibu kuwa alikua anataka kukiangalia tu na haikua nia yake kukiiba na kuomba msamaha lakini, polisi wanaendelea kumuhoji ili kubaini nia yake hasa ya kukichukua kiti hicho, Huenda alafikmishwa mahakamani kwa kutaka kuiba kistuli cha mwenge.

  0 0

  IMG_0227
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiwa ameambatana na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya wakiwasili ukumbini.
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 
  IMG_0244
  Meza ya Majaji ikiongozwa na Chief Judge Mwandaaji wa Miss Temeke Bw. Benny Kisaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka ( wa pili kulia), Mratibu wa Miss Ilala Juma Mabakila (Kushoto) na Mkuu wa Radio France nchini Bw. Victor Willy (kulia).
  IMG_0284
  Mwandaaji wa mashindo ya Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi akiteta jambo na Chief Judge wa mashindano hayo, Ben Kisaka
  IMG_0307
  Picha juu na chini ni Washiriki 11 wa Redd's Miss Kigamboni wakifungua shindano hilo kwa show ya aina yake.
  IMG_0319
  IMG_0203
  Wanenguaji wa Bendi ya FM ACADEMIA maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani wakati wa shindano la kumsaka Redd's Miss Kigamboni 2013 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
  IMG_0369
  Pichani juu na chini washiriki wa Redd's Miss Kigamboni wakipita jukwaani mavazi ya ubunifu.
  IMG_0372
  IMG_0403
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 ndani ya Beach Wear.
  IMG_0433
  Mmoja wa majaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka akitangaza majina ya warembo waliofanikiwa kutinga tano bora.
  IMG_0450
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni waliofanikiwa kutinga tano bora.
  IMG_0485
  Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 akiwauliza maswali washiriki waliofanikiwa kutinga tano bora kwenye shindano hilo.
  IMG_0472
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 wakijibu maswali.
  IMG_0506
  Wadau wa tasnia ya urembo wakishangilia baadhi ya washiriki waliokuwa wakijibu maswali yao bila kutetereka.
  IMG_0526
  Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester anayemaliza muda wake akisubiri kukabidhi taji kwa Redd's Miss KIgamboni 2013.
  IMG_0555
  Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester aliyemaliza muda wake akimvisha taji mshindi wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (aliyeketi) wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
  IMG_0566
  Mshindi wa Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed( wa pili kushoto) na Mshindi wa tatu Irene Rajab ( wa pili kulia) pamoja na mshindi wa nne na wa tano.
  IMG_0588
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.
  IMG_0596
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.
  IMG_0601
  Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd's Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.
  IMG_0605
  Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.
  IMG_0612
  Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile
  IMG_0606
  Raia wa kigeni kutoka China aliyehudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 akichukua picha ya ukumbusho ya mshindi wa taji hilo.
  IMG_0586
  Mwandaaji wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi (kulia) na Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu pamoja na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya (kushoto) wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi.
  IMG_0220
  Raia wa Kigeni kutoka china ndani Redd's Miss Kigamboni 2013.
  VIP Table... 
  IMG_0238
  Picha juu na chini ni baadhi ya Wadau wa tasnia ya masuala ya Urembo kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar waliohudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013.
  IMG_0239
  IMG_0508
  Nyomi ya Ukweli... Clouds Tv walikuwepo kuhakikisha shindao hilo linaruka Live.
  IMG_0533
  Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisalimia Marafiki wa Asasi ya Mikumi Kids waliokutana kwa ajili ya kuchangia Mikumi Kids leo katika Mji wa Wilsele Ubelgiji. Mikumi Kids inaendesha kituo cha Watoto Yatima cha Mikumi Kids Tanzania. Balozi Kamala aliwashukuru kwa kuchangia Watoto Yatima na amewaomba waendelee kuwasaidia. Kushoto kwa Balozi Kamala ni Tausi Mpagama Mkurugenzi wa Mikumi Kids.


  0 0

  Ujenzi wa Barabara ya Mbeya kuelekea Chunya , hili ni eneo Maarufu kona ya Mkoa

   
  Barabara ya kiwango cha Rami kutoka Mbeya kuelekea Chunya eneo la Chalangwa

  Ujenzi wa Barabara ukiendelea 
   Moja ya Gari likitoka Mbeya kuelekea Chunya


   Ujenzi ukiendelea kwa kasi katika eneo hilo.
   Mmoja wa wadau akiwa katika eneo ambalo Barabara hiyo inatengenezwa.
  Picha na Mbeya Yetu

  0 0

   Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiwa katika picha ya pamoja na wabunge kutoka Tanzania pamoja na Wabunge wanaoiwakilisha Tanzania Katika Bunge la Africa ya Mashariki baada ya kufunga mkutano wa Nanyuki VII Nchini Uganda.
  Waheshimiwa Wabunge wa kutoka Zanzibar walioshiriki mkutano wa Nanyuki VII wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Uganda, Rais Yoweri Kaguta Musevini akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Africa ya Mashriki (EALA) Mhe Abdullah Mwinyi, katika Jiji la Entebbe.

  0 0
 • 06/08/13--20:00: Ngoma azipendazo Ankal
 • Kool & the Gang na ngoma yao ya 'Get Down On It' walitamba sana

  0 0

   Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
   Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
   Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
   
  Warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
    Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.
  Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd's Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala  na kufanya usafi.

  Warembo hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).

  Harambee hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
  Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

  Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mipango,Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii TANAPA,Dkt.Ezekiel Dembe akijibu changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Warsha ya TANAPA na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na mada zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama na Miradi ya ujirani mwema.Warsha hiyo ya siku nne iliyofunguliwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki inaendeleo leo ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo,Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Ubunge Ardhi,mazingira na Maliasili,Mh James Daudi Lembeli akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Warsha ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali  kwenye mada mbili zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama pamoja na Miradi ya Ujirani mwema.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaoendelea kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
   Waziri Kivuli (kambi ya Upinzani) Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh Mch.Peter Simon Msingwa akichangia kwenye moja ya mada iliohusu Masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,kulia kwake ni Mkurugenzi wa TANAPA,Bwa.Allan Kijazi na shoto ni Dkt.Ayoub Rioba.
   Mmoja wa Wahariri,Charles Misango kutoka gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali kwenye warsha hiyo mapema leo asubuhi.
   Mmoja wa Wahariri wa gazeti la The Guardian on Sunday,Rodgers Luhwago akiuliza swali kwenye moja ya mada ya leo iliyohusu Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,mapema leo asubuhi.
  Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo ya siku nne wakifuatilia kwa makini yanayojiri ukumbini humo.

  0 0


  0 0
 • 06/12/13--02:03: mambo ya kupiga nyoka
 • hili lori tumekutana nalo kijiji cha mwigu morogoro road linapigwa nyoka.gari yetu imepata pancha hapa so muda wote bila hofu jamaa wamepiga dumu 12 za liter 20!mchezo huu ndo unatutesa watz tunauziwa mafuta mabovu kwa ghali na kuharibu magari yetu!Mulika mwizi man!

  0 0

  Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akimkabidhi zawadi Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wakati wakiwa katika kikao cha pamoja na maafisa wa Polisi Makao Makuu.Bw.Sommer yupo katika ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania.

  Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Polisi Bavaria cha Nchini Ujerumani Bw. Wolfgang Sommer akiangalia jinsi ya uendeshaji wa mafunzo katika Gym ya Polisi iliyopo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) wakati wa ziara ya kutembelea na kujionea mafanikio ya Jeshi la Polisi Tanzania.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

  Jeshi la Polisi nchini limefaidika kwa kiasi kikubwa na ushirikiano uliopo kati yake na chuo cha Bavaria cha Ujerumani katika Nyanja za mafunzo, vifaa na polisi jamii jambo ambalo limewezesha maboresho ya jeshi hilo kuendelea vyema na kutoa huduma inayostahili kwa wananchi.

  Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria cha Nchini Ujerumani Wolfgang Sommer alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na baadhi ya vikosi vya Jeshi hilo kujionea mafanikio ya Polisi jamii pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika utendaji wao wa kuimarisha usalama wa raia na mali zao hapa nchini.

  Akizungumza katika ziara hiyo Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja alisema ushirikiano baina ya chuo hicho na polisi umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kupata mafunzo ya jinsi ya kuimarisha mkakati wa polisi jamii pamoja na jinsi ya kuboresha mitaala katika vyuo vyetu vya polisi.

  “Ujerumani ni moja ya nchi zilizoendelea sana duniani hivyo na sisi kupitia maboresho yetu tuna mambo mengi ya kujifunza ili kuendana na usasa unaohitajika katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania katika nyanja ya usalama”Alisema Kamishna Chagonja.

  Kwa upande wake Mkuu wa Polisi jimbo la Bavaria na Rais wa Chuo cha Bavaria cha Ujerumani Wolfgang Sommer alisema majeshi ya Polisi hivi sasa duniani yanakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuibuka kwa wahalifu wenye kutumia mbinu zilizoendelea hivyo Polisi wana wajibu wa kujifunza kwa kasi mbinu hizo.

  Bw.Sommer alisema Polisi kote duniani wapo katika maboresho hivyo kwa siku zijazo majeshi hayo yataimarika katika kupambana na uhalifu na lengo la ziara yake ni kujifunza mbinu zinazotumiwa na polisi wa Tanzania katuika kukabiliana na uhalifu.

  Katika ziara hiyo alitembelea Kikosi cha matengenezo ya magari ya Polisi ambacho kwa kiasi kikubwa kilifadhiliwa na Serikali ya Ujerumani mwaka 1994, Kikosi cha Mbwa na farasi, Chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA), Kikosi cha Polisi Anga pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

  0 0older | 1 | .... | 159 | 160 | (Page 161) | 162 | 163 | .... | 3278 | newer