Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1593 | 1594 | (Page 1595) | 1596 | 1597 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Muonekano wa baadhi ya Nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam zikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA), Arch. Elius Mwakalinga, akifafanua hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa nyumba kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo jijini Dar es Salaam.
   Muonekano wa moja ya mtungi wa kutengenezea gesi ukaa (Biogas), inayoendelea kujengwa katika Nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), eneo  la bunju jijini Dar es Salaam. Gesi hiyo itatumika kutoa huduma kwa wakazi wa eneo hilo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  Na Erasto T. Chingoro- Msemaji Kitengo cha Mawasilino Serikalini, WAMJJW

  Katika kuitikia agizo la Serikali kuhamia Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy A. Mwalimu amefika kwenye Ofisi za Wizara yake iliyopo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma, sehemu ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii na kukutana na watumishi wa Wizara yake.

  Mhe. Ummy alipokelewa kwa shangwe na bashasha na watumishi wa Wizara yake - Idara Kuu ya Afya na Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bibi Sihaba Nkinga. Waziri alipata muda wa kusalimiana na watumishi 106 waliotangulia kuhamia Dodoma katika Awamu ya kwanza ya Uhamisho na kujiridhisha na ari waliyonayo watuimishi.

  Akiwa hapa UDOM, Waziri Ummy alitembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma za matibabu ya kibigwa kwa wagonjwa zinapatikana kupitia Hospitali hiyo iliyoko eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma, ambayo imefungwa vifaa vya kisasa ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali yaliyoshidikana.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mhe. Waziri alifafanua kuwa katika kuhakikisha Serikali inasogeza huduma za afya kwa wananchi wake, wanafunzi na viongozi wanaohamia Dodoma, Hospitali ya Benjamini Mkapa imekamilisha kufunga vifaa vya kisasa vya matibabu ikiwa ni ‘MIR’ mashine ya ‘mamography’ inayotumika kuchunguza magonjwa ya saratani ya akinamama, na kwamba mashine hiyo inapatikana hapo hospitalini pekee hapa nchini.

  Kufuatia kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa madaktari, wahuguzi na watumishi wa kada mbalimbali, Wizara itaangalia uwezekano wa kufanya uhamisho wa ndani ili kupunguza uhaba wa watumishi uliopo katika hospitali hiyo. Aidha, Wizara imeahidi kuwasiliana na Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kupata watumishi wakutosha kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watumishi.
   Waziri Ummu Mwalimu akijadiliana jambo na Katibu  Mkuu wa Wizara hiyo Bi Sihaba Nkinga
  Picha ya Pamoja

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  KIWANDA cha Vigae cha Twayfod kinatarajia kuajiri watu 4000 wa moja kwa moja na pamoja na ajira za muda mfupi 2000.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji  nchini, Clifford Tandari amesema kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya Tanzania ya viwanda imeanza kutimia.
  Tandari amesema kuwa wanaendelea kuchakata makampuni mbalimbali ambayo yameonyesha dhamira ya kutaka kuwekeza katika sekta ya viwanda hivyo ni fursa ya watanzania kuchangamkia ajira zinazojitokeza.

  Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitakachojengwa katika mji wa Chalinze kitatumia malighafi zinazozalishwa hapa nchini ambapo kuna maeneo yatapata mapato yatayotokana na malighafi hizo.
  Ameongeza kuwa kiwanda cha vigae kitaanza hivi karibuni hivyo watu wakae tayari kuchangamkia fursa za awali ajira zitakazotolewa.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (TIC), Clifford Tandari akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya uwekezaji wa viwanda uliofikiwa katika nchi naja  jijini Dar es Salaam. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0


  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam mapema leo. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza katika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ambao ulikuwa na lengo ya kujadili nafasi za Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa II wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akitoa ukaribisho kwa Watendaji Wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma kwa niaba ya waandaji wa mkutano huo uliofanikiwa kuleta pamoja wakuu wa mashirika zaidi ya 70 nchini.
  Sehemu ya Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Mashirika ya Umma wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Tume ya Mipango na kufanyika Ikulu, Dar es Salaam mapema leo.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (aliyeketi katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wapili kutoka kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (wapili kushoto), Kaimu Msajili wa Hazina Bw. Mihalale Mwakibinga (kushoto) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango Maduka Kessy (kulia) katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Bodi wa Mashirika ya Umma.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (aliyeketi katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wapili kutoka kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (wapili kushoto), Kaimu Msajili wa Hazina Bw. Mihalale Mwakibinga (kushoto) na Naibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango Maduka Kessy (kulia) katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Mashirika ya Umma.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amewataka wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Mashirika ya Umma na Mamlaka za udhibiti kuwa wabunifu na kutumia fursa na rasilimali zilizopo nchini ili kuleta maendeleo chanya.

  Amebainisha hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano.

  “Rai yangu leo ni kwamba kwenye majadiliano yenu pendekezeni na kufanya mashirika ya umma yawe endelevu,yapanuke zaidi na kuliongezea Taifa mapato na ndio maana nafarijika sana kuona mkutano huu unajumuisha wadau wote muhimu ili pamoja na kuweka mikakati ya namna mashirika ya umma ya Tanzania yanavyoweza kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango wa Maendeleo,”Alisema Majaliwa.

  Akielezea hali ya mashirika ya umma nchini,Waziri Mkuu amesema kuwa utegemezi wa mashirika unaendelea kupungua na mchango na gawio kutoka kwenye mashirika hayo unaendelea kuongezeka na kuhimiza kuongezeka kwa ubunifu na matumizi mazuri ya rasilimali chache zilizopo na kuongeza kati ya mashirika 65 ya kibiashara,mashirika 8 yanaendeshwa kwa Ruzuku ya Serikali,wakati mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.

  Ameagiza kuboreshwa kwa mwongozo wa kupata wajumbe wa Bodi na kuwaagiza kuweka mwongozo rasmi wa namna ya kupata wajumbe hawa kwani ni sehemu inayolalalmikiwa sana na wananchi.

  Amesema kuwa wameyashirikisha mashirika ya umma kwenye utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa sababu vipaumbele vya mpango wa pili wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano ambayo ni ujenzi wa viwanda vya kuimarisha kasi ya ukuaji wa uchumi,miradi mikubwa ya kielelezo na miradi wezeshi kwa maendeleo ya viwanda ikiwemo barabara,reli,nishati,bandari maji na mawasiliano.

  Aidha ameagiza kuondolewa kwa urasimu katika shughuli za mashirika ya umma kwani unakwamisha uboreshaji na maendeleo ya mashirika ya umma. 

  Waziri Mkuu pia ametoa rai kwa viongozi wote wa mashirika ya umma kutosaini mikataba isiyo na tija kwa Taifa ambayo inapelekea kupata hasara kubwa na kuhimiza mashirika haya kushirikiana na mashirika ya nje pamoja na sekta binafsi ili kupata nguvu ya pamoja katika kukuza uchumi.

  “Ni lazima mashirika ya umma yakafanya kazi kwa pamoja na kwa kushirikiana ikiwemo kubadilishana mbinu na utaalamu ili kulifikisha Taifa hili katika azma yake ya kukuza Uchumi wa viwanda kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu”,Alisisitiza Mh.Majaliwa. 
  Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa akisoma Hotuba leo 28 February 2017 ya ufunguzi wa Mkutano kuhusu nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano Mkutano huo Umefanya katika Ukumbi wa Kikwete Ikulu Dar es salaam. Picha na Pmo
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akionyeshwa Picha na Rais wa Kampuni ya China National Materials Company Ltd (SINOMA), Peng Jianxin ambaye Kampuni yake inatarajia kujenga kiwanda cha Cement Mkoani Tanga mwisho kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bwana Maritin Shigela , Shughuli hiyo imefanyika leo 28 February 2017 katika Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Ostabay Dar es salaam. Picha na Pmo


  0 0

  Balozi wa Kuwait nchini Mhe.  Jasem Al Najem (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Africa Relief Organisation Bw. Sami Al  Azib wakiwa na hati ya mkataba uliowekwa kati ya Kuwait  Red Crescent Society  na Africa Relief Organisation wa kuchimba visima 16 katika shule tofauti jijini Dar es salaam katika hafla ndogo iliyofanyika katika Ubalozi wa Kuwait hivi karibuni.

  0 0
 • 03/01/17--01:15: Article 23
 • Make your Car  look new and stylish all the time.Meet the PIMP Cars Specialists in MacAutoAccessories @ Sinza Mori for genuine car parts and accessories ie Car Audio Systems| Car Security Alarms Installations | Wheels & Tyres |Leather Seat Covers | Batteries |Car Perfumes | American tinteds installations | HID Lights & Bulbs| Riverts | Pimpin Cars | Call our Hotlines 24/7 ::::::::::::☎️ 0715000890 or 0767 120 111 or 0767 120 222/0767120444

  0 0

  Mmoja kati ya warembo waliovalia vivazi vya mwanamitindo nguli na wa kimataifa Asya Idarous Khamsini akipata picha kwenye siku ya Swahil iliyofanyika Hampton Inn College Park, Maryland siku ya Jumapili Feb 26, 2017 na kuhudhuriwa na watu kibao. Katika tamasha hilo ambalo ndio ilikua kwa mara ya kwanza kuanzishwa likiwa limeratibiwa na Bwn. Mgaza ambaye amesema litakua likifanyika kila mwaka.
   Watatu toka kushoto ni mwanamitindo nguli na wa kimataifa Asya Idarous Khamsini akipata picha ya pamoja na wadau wa DMV kutoka kushoto ni Mayor Mlima, Joha Nyang'anyi, Dedi Luba, Terry Shomari na Asha Hariz.
   Watatu toka kushoto ni mwanamitindo nguli na wa kimataifa Asya Idarous Khamsini akiwa katika picha ya pamoja na tano ladies. Kutoka kushoto ni Tuma Kaisi, Asha Nyang'anyi, Jska Jojo na Asha Hariz

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Nchini Khamis Mwijuma ‘Mwana FA’ amesema kuwa hakuna mpango wowote wa kurejesha kundi la East Coast, bali wana mpango wa kufanya kazi ya pamoja.

  Mwana Fa amesema hayo katika mahojiano maalum na globu ya jamii kuhusu mpango wa kundi hilo ambalo lilipata kutamba katika miaka ya tisini.

  “Hatuwezi kurudisha kundi la East Coast, ila tuna mpango wa kurekodi nyimbo kati yangu mimi Ay na Gk, watu wanapaswa kujua hivyo kuliko kusikiliza maneno ya watu” amesema Fa .

  FA ameseja kuwa ni vigumu kwa sasa kurudisha kundi hilo kwani mfumo wa maisha na muziki umebadilika na ukitaka kurudisha kundi kutahitjai mazungumzo mengi sana.

  Aliendelea kusisitiza kuwa bado watendelea kufanya kazi pamoja lakini sio kurudisha kundi kama ilivyokuwa zamani.

  0 0


  Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China lina mpango wa kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa vya mawasiliano nchini kwa ushirikiano na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

  Rais wa Shirika hilo Yuan Yong ametoa kauli hiyo 1-Mar-2017 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

  Yuan Yong amemweleza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Serikali ya China pia ina mpango wa kuikopesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kiasi cha shilingi bilioni 600 ili kuipa uwezo wa kiteknolojia na kupanua mtandao wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini hasa vijijini.

  Rais huyo amesema lengo la mkakati huo ni kuifanya TTCL kuwa Kampuni bora inayotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya kisasa kuliko kampuni yeyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan  akizungumza na Rais wa Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China Bw.Yuan Yong (kulia) pamoja na ujumbe wake, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  10:Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan  akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Shirika la Datang Telecom International Technology Company Limited la Serikali ya China Bw.Yuan Yong na ujumbe wake mara baada ya kupokea taarifa ya mpango wa serikali ya China wa kuikopesha TTCL ili kuipa uwezo wa kiteknolojia  na kupanua mtandao wa mawasiliano vijijini na mijini pamoja na kujenga kiwanda cha kutengeneza vifaa vya mawasiliano hapa Tanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).  0 0  Kituo cha televisheni cha EATV kwa kushirikiana na taasisi ya haki za wanawake (HAWA), wamezindua kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kununulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.

  Akizungumza katika mkutano na wanahabari,jijini Dar leo, Afisa Masoko wa EATV,Brendansoa Kileo amesema kuwa Kampeni hiyo inazinduliwa wakati tukielekea siku ya Wanawake Duniani Machi 8.


  "Nasi kama kituo cha habari kinachofanya biashara zake nchini,tumeona kuwa tuna wajibu wa kutumia vituo vyetu vya EATV na East Africa Radio kuhamasisha jamii kuwachangia watoto wetu wa kike kutatua tatizo",alisema  Brendansoa.

  Amesema kuwa kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wa kike kukosa kuhudhuria shule kati ya siku tano hadi saba kwa kukosa pedi za kujisitiri wakati wa hedhi .“kwa mwaka inakadiriwa mwanafunzi wa kike hukosa kuhudhuria shule kwa siku 60 hadi 70 kutokana na kukosa pedi tu , hali ambayo imekuwa ikichangia kutofanya vizuri katika masomo yao”amesema Brendansoa.

  Amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakihatarisha afya zao kwa kutumia matambara kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi na kusababisha aibu pale ambapo vitambaa vinapovujisha damu.

  Wakati huo huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria ameongeza kusema kuwa ili kuchangia kampeni hiyo,wanatarajia kila Mwananchi atakayeguswa na tatizo hilo basi anaombwa kuchangia kuanzia kiasi cha shilingi Elfu Tano (5,000/=),ili
   kuwasaidia watoto wa kike kupata pedi na kuhudhuria shule. 

  "Katika kampeni hiyo EATV na East Afrika Radio itahamasisha uchangiaji wa fedha na taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA FOUNDATION),iliyosajiliwa kwa mujibu wa taratibu za nchi mwaka 2011,itahusika na kupokea na kusimamia fedha zote zitakazochangishwa na kusimamia ununuzi na usambazaji wa pedi hizo mashuleni",alisema Joyce Kiria.


  Kiria aliongeza kwa kueleza taratibu za uchangiaji kuwa,unaweza kutuma fedha hizo kwa M-Pesa kupitia namba 5530307 ama kupitia akaunti ya CRDB namba 0150258750600.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo kuhusiana na uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.

  Pichani kulia ni  Afisa Masoko wa EATV,Brendansoa Kileo akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria  pamoja na Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko.

  Wa pilia kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.


  Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza kwenye mkutano huo.


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Bi Lekhethe Mmakgoshi kutoka Afrika Kusini akiongoza Ujumbe wa Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wanaofanyakazi zao ndani na nje ya Bara la Afrika mara walipofika Ikulu Mjini Unguja leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Wakurugenzi Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wanaofanyakazi zao ndani na nje ya Bara la Afrika unaoongozwa na Bi Lekhethe Mmakgoshi kutoka Afrika Kusini (wa pili kulia) walipofika Ikulu Mjini Unguja leo (Picha na Ikulu)

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii

  VIONGOZI wa kamati ya Utendaji wa Yanga wakutana leo kujadili masuala mbalimbali ya klabu hiyo kutokana na kuwa katika hali ngumu ya ukata inayoikabili.

  Kutoka ndani, kikao huo ulioanza toka asubuhi kimekuwa cha siri sana wakiwa katika majadiliano makali na pia ikionekana kutaka kuinusuru klabu hiyo kutoka kwenye hali hiyo ambapo imepoteza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba.

  Kamati ya Utendaji wa Yanga wameamua kukutana leo ikiwa ni siku mbili baada ya Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa kuweka wazi hali ya ukata wa klabu hiyo, pia wachezaji kulalamika kuhusiana na kutokulipwa mishahara yao.

  Pia, kumekuwa na taarifa kuwa mchezaji wa kimataifa kutokea nchini Zimbambwe kuweka wazi kuwa baadhi ya viongozi walidanganywa kuwa anaweza kucheza katika mechi dhidi ya Simba wakati si kweli.

  Mbivu na mbichi za kikao hicho cha kamati ya utendaji kitajulikana baada ya kumalizika na maamuzi hayo ni kwa ajili ya kuiokoa Yanga kuweza kuhakikisha inafa nya vizuri kwenye michezo iliyobaki na kutetea ubingwa wake.

  Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga

  0 0

                    
  Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Zanzibar (ZFU) unafikiria kuandaa mpango maalum wa kuwawekea Bima ya Afya wanachama wake kwa lengo la kuwakomboa wakati wanapokumbwa na matatizo ya Kiafya.

  Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Chama hicho Mohamed Abdulla Laki  akiuongoza Ujumbe wa Viongozi Wanne wa ZFU wakati wa mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.

  Mohamed Abdulla Laki alisema inakuwa aibu na masikitiko makubwa  pale  Msanii ambaye ni kioo cha jamii anapoonekana akidhalilika wakati akitafuta huduma za matibabu kipindi anaposumbuiliwa na matatizo ya kiafya bila ya kupata msaada wa uhakika.

  Alisema wapo baadhi ya wasanii katika zama tofauti zilizopita waliowahi kukumbwa na kadhia hiyo na kuishia katika mazingira ya kusikitisha huku jamii ikijisahau kwamba  wasanii hao walitumia nguvu, ujuzi na uzalendo wao katika kuielimisha jamii hiyo kupitia fani ya sanaa.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Uongozi huo ulifika kumtaarifu rasmi azma yao ya kuandaa Tamasha la kuibua vipaji vya wasanii wanchanga Zanzibar linalotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu.


  Balozi Seif  akiwa katika picya ya pamoja na Uongozi wa Chama cha Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya  aliofanya nao mazungumzo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kulia ya Balozi Seif ni Msanii Jamila Abdulrahman { Babyjay } na Mohamed Abdulla Laki. Kushoto  ya Balozi Seif  ni Msanii Abdulkheir Chum na Msanii Rashid Mustapha ambae ni msemaji wa Chama hicho. Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Katika kuisaidia benki ya damu hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam. 

  Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendo kupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.

  Shughuli hiyo ya uchangiaji iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.

  Akizungumza wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo wanapotakiwa kufanya hivyo.

  “Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.

  Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni ya Zantel-Zanzibar Mohamed Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lilloandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel  Laurent.

  Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Mohammed Ali akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.   
  Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.


  0 0

  Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.

  Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za aina nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya wiki mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro. 

  Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha hizo zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na Sale vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.

  Alisema mafanikio hayo yalitokana na taarifa ambazo zilibainisha kwamba kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano makali baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na kuwataka wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba silaha hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.

  Akibainisha vijiji ambavyo silaha hizo zilipatikana kuwa ni Olorieni Magaiduru zilipatikana silaha aina ya Chinese 56 SMG moja yenye namba MT. 70B 1 2730021 na risasi 21 pamoja na silaha aina ya Semi Automatic Rifle (S.A.R) yenye namba KN 250374 ikiwa na risasi nne.

  Katika kijiji cha Oldonyasambu ilipatikana silaha aina ya Mark IV yenye namba ZKK 5602 pamoja na silaha nne aina ya Chinese 56 Sub-Machine Gun (SMG) zikiwa na risasi 19. Silaha hizo nne ni Chinese 56 SMG yenye namba RT 7663, bunduki ya pili namba yake ni 563631144 na bunduki mbili nyingine hazikuwa na namba.

  Kamanda Mkumbo alisema katika kijiji cha Sale silaha aina ya Chinese 56 SMG yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15 kwenye magazine ilipatikana pamoja na silaha nyingine mbili tofauti ambazo ni S.A.R yenye namba 25032534 na Mark III yenye namba 263126.

  Aidha kamanda Mkumbo aliwataka wananchi wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria wazisalimishe mara moja kwenye ofisi za mitaa, vijiji na hata vituo vya Polisi vyovyote vilichopo karibu huku akitoa onyo kwa wale ambao watakaidi na wakikutwa nazo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Alisema Operesheni hiyo ni endelevu na itakuwa katika maeneo tofauti ya mkoa huu na si wilaya ya Ngorongoro pekee.
   Silaha mbalimbali zikiwemo SMG 6 pamoja na risasi 59 zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika katika wilaya ya Ngorongoro.
   Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo akionyesha silaha mbalimbali zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro iliyofanyika wiki mbili zilizopita.
   Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionesha waandishi wa habari baadhi ya silaha  zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha akiwaonesha waandishi wa habari moja ya silaha ya kivita aina ya Chinese 56 Sub Machine Gun (SMG) iliyopatikana kwenye operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.

  0 0

   Eng. Athu Chulla akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam. Pembeni kwa Naibu Waziri ni Mratibu wa Ujenzi wa nyumba hizo, Arch. Christina Shayo.
   Mratibu wa Ujenzi wa nyumba  zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Christina Shayo (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani,  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.
   Muonekano wa moja ya nyumba za wananchi zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Magomeni ikiwa katika hatua ya msingi, Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.
  Mafundi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiendelea na ujenzi wa nyumba za wananchi katika eneo la Magomeni. Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akizungumza na Balozi wa Singapore nchini, Mhe. Tan Puay Hiang, alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo yao Mhe. Dkt. Kolimba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili sambamba na kutambua mchango wa Serikali ya Singapore kwa Tanzania katika sekta ya Elimu sambamba na kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma. 
  Mhe. Tan Puay Hiang nae akizungumza ambapo alieleza Serikali ya Singapore itaendelea kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Singapore pamoja na kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan uwekezaji katika masuala ya nishati na miundombinu.
  Mazungumzo yakiendelea.Kushoto ni ujumbe alioambatana nao Mhe. Tan Puay Hiang. 
  Picha ya pamoja. 

  0 0

  MSHAMBULIAJI wa Yanga wa kimataifa kutoka nchini Mzimbabwe Donald Ngoma amesema ataondoka katika klabu hiyo kukwepa mambo ya ovyo ya uongozi.

  Ngoma amesema hayo wakati akizungumzia tuhuma dhidi yake juu ya kutocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumamosi, Yanga ikichapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Amesema kwamba ataondoka Yanga baada ya kuchoshwa na 'madudu' ya uongozi wa timu, mchezaji huyo amesema kwamba mashabiki na wapenzi wa Yanga wamekuwa wakimshutumu na kumtukana kutokana na taarifa zisizo za kweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye. 
    
  “Nimekuwa kimya wakati wote nikitukanwa juu ya sababu za kutocheza, wakati ukweli ni kwamba mimi nina maumivu ya goti. Taarifa nyingi zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba sitaki kucheza kwa sababu ninataka kuondoka katika timu, nashangaa wapi wanapata hizo taarifa,”amesema Ngoma.

  Amesema Daktari ambaye Yanga walimtumia kumtibu yeye alikuwa ‘tapeli’ na ameilia fedha klabu bila kufanya kazi yoyote. “Daktari alikula fedha za viongozi wa klabu na kuwadanganya kwamba alikuwa ananitibu amenipeleka hospitali, wakati ukweli ni kwamba nilikuwa ninatibiwa katika hospitali nyingine kwa gharama zangu mwenyewe,”amesema Ngoma.

older | 1 | .... | 1593 | 1594 | (Page 1595) | 1596 | 1597 | .... | 3272 | newer