Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109977 articles
Browse latest View live

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE IKSHIRIKIANA NA TAASISI YA SAVE CHILD HEART YA NCHINI ISRAEL YAWAPELEKA WATOTO NANE KUTIBIWA MAGONJWA YA MOYO NCHINI HUMO

$
0
0
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiongea na waandishi wa habari kuhusu watoto nane wanaokwenda  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Hili ni kundi la nne la watoto kwenda kutibiwa nchini humo tangu mwaka 2015 ambapo JKCI ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Save Child Heart  ya kuwapeleka wagonjwa nchini Israel hadi sasa watoto 40 wameshatibiwa na wanaendelea vizuri. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi   Robert Mallya.
 Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamekwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo wakifuatilia kwa karibu mkutano wa waandishi wa Habarai uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaongoza watoto wanaokweda kutibiwa magonjwa ya moyo  nchini Israel kuingia kwenye gari kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege kuanza safari ya kuelekea nchini humo. Serikali kupitia JKCI  kwa kushirikiana na Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini humo kwa ajili ya matibabu ya moyo.
 Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) , ndugu na watoto wanaokwenda kutibiwa nchini Israel wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa safari ya watoto hao ya kuelekea nchini humo kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Picha na Anna Nkinda - JKCI

PROF. MBARAWA AZINDUA SCANNER MPYA

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akitilia saini na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (kulia) ya kukabidhiana scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko.
 Muonekano wa Scanner Mpya ambazo zimenunuliwa kwa msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Scanner hizo mpya moja imefungwa katika bandari ya Dar es Salaam na nyingine itafungwa katika bandari ya Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa  Scanner, mara baada ya kuzindua scanner mpya zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.  



Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

IFC yazindua kampeni ya kukuza uelewa kwa watumiaji wa simu, kutuma na kupokea pesa moja kwa moja kutoka mitandao yote

$
0
0
Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia, IFC imezindua kampeni ya Huduma ya kutumia fedha kwenda mtandao wowote bila garama.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa kutoka  Benki Kuu Tanzania,  Bernard Dadi amesema   huduma hiyo mpya itawanufaisha  wananchi kupunguza garama za kutumia fedha kwenda mitandao mingine.

Amesema kuwa kampeni hiyo itaongeza uelewa wa watumiaji simu za mkononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila garama.

"Uwezekano huu wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mtumiaji, unatarajiwa kuongeza idadi ya watu wanaofaidika na huduma za kifedha nchini", amesema Dafi

Amesema kuwa kufanikiwa kwa Huduma hii ambayo kampeni yake ina lengo la kufikia watu milioni moja katika kipindi cha miezi sita kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya Kwanza duniani ambako makampuni ya simu yamekubaliana  na wateja wao kutumiana fedha moja kwa moja.
Kampeni hiyo inayoongozwa na FEM Tanzania Ltd,  inafanikishwa kwa msaada wa BOT, Taasisi ya Bill & Gates na Shirika la the Financial Sector Deepening.

Amesema, uchunguzi iliofanywa na IFC imebaini ukosefu wa uelewa wa Huduma hiyo miongoni mwa watumiaji kwa kukosa kuaminiana miongoni mwa makampuni ya simu na ushindani kwenye masoko.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, BOT, Bernard Dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari,hawapo pichani juu ya Huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote bila garama.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo y Taifa, BOT Bernard Dadi wa nne kutoka kushoto na wadau mbali mbali wa kampuni za simu nchini, wakiangalia onyesho la uzinduzi kutoka kwa Vijana wanaofanya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Huduma ya kutuma fedha kwenda mitandao yote.
 Mkurugenzi Bernard Dadi wa pili kulia, Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedun na wadau wengine mbali mbali kutoka katika makampuni ya simu wakifuatilia kampeni za uzinduzi wa Huduma za fedha kwa njia ya simu bila garama yoyote. 

RIWAYA KUPATIKANA KUPITIA PROGRAMU MAALUM NCHINI

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) umezindua mfumo maalum wa kuuza,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” leo Jijini Dar es Salaam.



Akizindua Programu hiyo Katibu Mkuu wa Umoja huo Bw. Bw.Ibrahim Gama amesema kuwa wameamua kuanzisha programu hii ili kuwawezesha wanachama wa UWARIDI kuweka riwaya zao kwa ajili ya kuuzwa na wao kujipatia malipo kutoka kwa mtengenezaji wa app hiyo.



“Kwa miaka mingi waandishi wa riwaya wamekuwa wakijaribu kutafuta njia mbalimbali za kunadi kazi zao ili kuwafikia wasomaji wao kwa urahisi,na tukaona changamoto wanazopata katika kuzipata kazi zetu na hivyo tukaamua kuandaa program hii itakayowawezesha kupata riwaya zetu kwa urahisi zaidi kwani utahitaji kuwa na programu hii tu kwenye simu yako ili kusoma muda wowote”,Aliongeza Bw.Gama.



Katika mfumo huo kutapatikana riwaya za waandishi mchanganyiko ikijumuisha waandishi nguli na wachanga  ambapo mpaka sasa zaidi ya waandishi 20 wameweka riwaya zao katika mfumo huo na zinaendelea kuongezeka kila siku.
 Katibu wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Ibrahim Gama akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa programu(App)  ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Rais wa UWARIDI Bw.Hussein Tuwa.
 Rais wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Hussein Tuwa akizungumzia uanzishwaji wa programu(App)  ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu wa Umoja wa umoja huo Bw.Ibrahim Gama na Abdillahi Muna kutoka Dau Technology ltd.
 Mwakilishi kutoka Dau Technology Limited Bw.Abdillahi Muna(wa kwanza kulia) akieleza jinsi program ya “UWARIDI APP” iliyozinduliwa leo na Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) kwa ajili ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu.Dau Technology ndio watengenezaji wa App hiyo.Wengine ni Rais wa Umoja huo Bw.Hussein Tuwa na katibu wake Bw.Ibrahim Gama.

ALI KIBA KUTIMKA USIKU HUU KWENDA MAREKANI,KUPIGA SHOO TANO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Siku moja mara baada ya kuwasili nchini akiwa na tuzo ya MTV base msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba, ameondoka nchini kwenda Marekani kwa ajili ya maonyesho yake ya kimuziki katika nchi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa globu ya jamii ,mdogo wa msanii huyo Abdul Kiba amesema kuwa kiba amerudi nchini kwa ajili ya kuleta tunzo kwa Watanzania na hivyo kesho jioni tunaondoka kwenda marekani.

“tunaondoka kwenda marekani na tutafanya maonyesho matano katika miji tofauti ya nchi hiyo hivyo mashabiki wetu waendele kutegemea kupata makubwa kutoka kwetu” amesema Abdul Kiba.

Amesema kuwa  kwa sasa ratiba yao ipo taiti katika kufanya maonyesho ya kimataifa na wakirejea watafanya kitu kikubwa kwa watanzania na Afrika kwa ujumla.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba.

WAZIRI MAGHEMBE AONGOZA TAMASHA LA KUMBUKIZI LA VITA VYA MAJIMAJI NA KUZINDUA MAKUMBUSHO YA HAYATI DR. RASHID MFAUME KAWAWA MJINI SONGEA

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe akiweka silaha ya jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Majiyaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya SongeaBalozi wa Ujerumani nchini Tanzania.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof.Jumanne Maghembe (katikati) akizungumza na wananchi kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Maji na uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Wengine ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge ( wa pili kulia) Mbunge wa viti maalum wa Ruvuma, Jacquiline ngonyani ( wa kwanza kulia) Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Egon Kochanke ( wa kwanza kushoto) pamoja na Chifu wa wangoni, Emanuel Zulu (wa pili kushoto) . Picha na Lusungu Helela- WMU)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof.Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilis Mahenge wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa akitunukiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa katika kulitumikia taifa kwa uzalendo mara baada ya kuzinduzia jana Makumbusho ya Hayati Rashidi Kawawa yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea. Picha na Lusungu Helela- WMU).

DINNER PARTY YA ALLY KIBA ILIVYOFANA DOUBLE TREE HOTEL DAR ESS SALAAM

$
0
0
 Ali Kiba akiwa anazungumza  na wadau walifika katika hafla ya chakula cha jioni na wasani wenzie na Waandishi wa habari
 Msanii Omy Dimpoz, Billnas na Peti Man wakuache wakijadili jambo kwenye hafla ya chakula cha jioni cha Ali Kiba
 Rafiki wa Karibu wa Ali Kiba , Jokate Mwengelo  akijadili jambo na jirani yake katika hafla hiyo.

JUMUIA YA WAZAZI WATAKIWA KUUUNGA MKONO SERIKALI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuia hiyo kutoka katika Kata mbalimbali za wilaya ya Ilala, alipokutana nao katika kikao maalum cha kujitambulisha kwao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala. Kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo. 

Akizungumza kwenye kikao hicho, pamoja na mambo mbalimbali Mkandawile ameitaka Jumuia ya Wazazi katika mkoa wake na maeneo mengine nchini, kuunga mkono hatua ya serikali kuingia katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Mkandawile amesema, Kama sehemu ya Wanana CCM, Jumuia hiyo haiba budi kuunga mkono mabambano hayo kwa kuwa Serikali inatekeleza ilani ya CCM, ibaraya 118 hadi 119.
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akiwasili ukumbini. Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo na kulia ni Katibu wa Jimbo la Ilala Christopher Lugemalila.
Wajumbe wakimsikiliza Mkandawile wakati akizungumza na watendaji na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ilala. Picha zote na Bashir Nkoromo.


TRA NA WASHAURI WA KODI 100 WAJADILIANA SHERIA ZA KODI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Obadia Kameya akifungua semina ya  elimu ya sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ambapo washauri wa masuala ya kodi walijadili namna ya utekelezaji wa mabadiliko mbalimbali katika sheria za kodi nchini.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza wakati wa semina ya  kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko katika sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
 Washauri wa masuala ya Kodi (Tax Consultants) walioshiriki katika semina ya kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko ya sheria za kodi nchini iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na kampuni ya ushauri wa masuala ya kodi ya Hanif Habib & Co.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu jijini dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Obadia Kameya akiwa katika picha ya pamoja na Washauri wa masuala ya kodi (Tax Consultants) baada ya semina ya majadiliano ya namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko na maboresho katika sheria za kodi nchini kuisha.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu ya Tanzania.

JE UNAJUA MASHAHIDI WANAOTAKIWA UNAPOANDIKA WOSIA ?.

$
0
0
Na  Bashir   Yakub.


1.MGAWANYO  WA   WOSIA.


Wosia  umegawanyika  mara  mbili .  Upo  wosia  wa  maandishi  na  upo  wosia  wa  mdomo.  Wosia  hizi  zote  zinakubalika  alimradi  zimekidhi  vigezo  vya  kisheria  vinavyohitajika.


( a ) Wosia  wa  maandishi .  Ni wosia  ambao  unakuwa  umeandikwa. Unaandikwa  na  mtoa  wosia  na  unashudiwa  na  mashahidi. Ni  wosia  ambao  unahimizwa  sana   kwakuwa ni  wa  kuaminika zaidi.


( b ) Wosia  wa mdomo. Huu  ni  wosia  ambao  haukuandikwa  isipokuwa  aliyeutoa  alitamka  tu  kwa  maneno. Ni  wosia   unaokubalika  ikiwa utakidhi vigezo  vya  kisheria.


2.   MASHAHIDI   WANAOTAKIWA   KUSHUHUDIA   WOSIA.


( a ) WOSIA  WA   KIKIRISTO.

Sheria  inayotumika   kwa  wosia  unaoandikwa  na  mtu  aliyeishi  maisha  haya  inajulikana  kama  “The  Indian  Succession  Act  1865”. Kwa  wakristo wanaoandika  wosia  ni  sharti  kufuata  misingi  ya  sheria hii  ili  wosia  zao  kuwa  halali.


Sheria  hii  imezigawa  wosia  mara  mbili.  Kwanza  wosia  wa  upendeleo( privileged  will)  ulio  katika kifungu  cha  52   cha sheria  hiyo  na  wosia  usio  wa  upendeleo( unprivileged  will) ulio kifungu  cha  50. 


Wosia  wa upendeleo  ni  wosia  unaoruhusiwa  kutolewa  na  watu  maalum  kwa mfano  wanajeshi  wanapokuwa  vitani  na  mabaharia  wanapokuwa  baharini  huko  bahari  ya  mbali .


Wosia  usio wa  upendeleo   unawahusu  watu  wa  kawaida wasio  hao  waliotajwa. Unaitwa  wa  upendeleo  kwasababu wamepunguziwa  masharti  kutokana  na  mazingira  wanayokuwemo.


Kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  52  wosia wa upendeleo ukiwa  wa  maandishi  sio  lazima  kuwa   na  mashahidi  au  kuwa  na  sahihi  ya  mtoa  wosia. Maandishi  tu  yasiyo  na  mashahidi  yanakubalika  na  ndio  maana  unaitwa  wa  upendeleo.


Na kama  ukiwa  wa  mdomo  basi  mashahidi  wawili  wanahitajika  ili  ukubalike.


Kwa  wosia  Usio  wa  upendeleo  unaotumiwa na  watu  wa  kawaida  mashahidi  wanaohitajika  ni watu  wawili  au  zaidi  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  50. Mtu  mmoja  hakubaliki  kuwa  shahidi.   Mashahidi  hawa  hutakiwa  kumshuhudia  mtoa  wosia  akisaini  wosia.


KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.


RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMATANO YA MAJIVU KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO (ST PETER) OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa wakiwatakia heri ya Masista katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF

$
0
0


Mfuko wa Pensheni wa LAPF unatarajia kufanya mkutano wa tisa wa wadau tarehe 9 na 10 Machi, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha. Mgeni rasmi katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).
 
LAPF imekuwa ikifanya mikutano hii ili kutoa taarifa za undeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni mbali mbali ili kuboresha utendaji wa Mfuko. Aidha mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya jamii nchini (SSRA).

Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Hifadhi ya Jamii Tanzania”. Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huu mada mbali mbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu jatwa hapo juu. Mada nyingine zitahusu Utendaji wa Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, Taarifa ya uwekezaji pamoja na Taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.

Kadhalika katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano LAPF itazindua huduma ya Mkopo wa Kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha Popote na LAPF) kwa kushirikiana na benki ya CRDB. Huduma hii imewanufaisha sana wanachama wa Mfuko wanaoanza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao ili kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango, nk kwa riba nafuu.

Vilevile siku ya ufunguzi wa mkutano tarehe 09 Machi, 2017 itakuwa ni siku ya maadhimisho ya figo duniani hivyo basi LAPF itatumia siku hii kuwapa fursa wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali ya KCMC.

LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa. Waalikwa wanaweza kuthibitisha ushiriki wao na kujisajili kwa kutembelea tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz . LAPF inawahamasisha wadau wote kujisajili kupitia tovuti ili kupunguza msongamano siku ya mkutano.

Aidha, siku ya pili ya mkutano tarehe 10 Machi, 2017, LAPF pamoja na washiriki wote wa mkutano wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wanatarajia kushiriki katika mazoezi ya kutembea ikiwa ni kuunga mkono utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.

Karibuni waalikwa wote kwa ustawi wa Mfuko.

  Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini kuhusu mkutano na wa tisa wa wadau wa LAPF utakaofanyika jijini Arusha Machi 9-10.kushoto ni  Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba na kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.
Pichani kulini ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata akielezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia mfuko huo wa Pensheni wa LAPF,Kushoto ni   Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo mapema leo,jijini dar
Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.

MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM KUFANYIKA DODOMA MACHI 3, 2017

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WAZIRI WA AFYA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ofisini kwake, Ikulu jijini  Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini  Dar es Salaam. 

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION WAHITIMISHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam. 

Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 32 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Yamemalizika. Wanawake 32 wa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. 

Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yatafanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya,Mtwara,Tabora na Kigoma.Image may contain: 12 people, people sitting and outdoor
Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na Taasisi za Fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa 
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.Wanawake wa mji wa Dar es Salaam walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Dar es Salaam .
Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and sunglasses
Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAONGOZA UENDESHAJI WA ZOEZI LA KUKAGUA VIWANDA VIANAVYOZALISHA POMBE AINA VIROBA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe kali(viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
Mashine zinazotumiwa na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo.

How Ngoma Africa Band has survived the storm to become one of the most sought-after African bands in Germany

$
0
0
It is not easy for an African band to survive for long in a European country. One of the few bands to survive the storm is Ngoma Africa Band, a Tanzanian band based in Germany.
Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja, leader of Ngoma Africa Band
Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja, leader of Ngoma Africa Band
Founded by Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja, Ngoma Africa Band is now 23 years old, and continues to thrill fans throughout the country with “Bongo Dansi” – Rumba influenced danceable music from Tanzania. The band sings mainly in Kiswahili.
Ngoma-Africa-Band1Kamanda Ras Makunja admits that it has been a tough journey. “Many promoters in Germany and in other European countries don’t like promoting African music. They instead prefer to promote Rock, Blues, Punk, etc. That makes it very difficult for us African musicians to find a chance of performing before large crowds,” he says.
Kamanda Ras Makunja however reveals that they’ve learnt to rely on their own efforts to promote and market their music. Due to the fact that they’ve survived against all odds, some people have nicknamed Ngoma Africa Band members “Strong Aliens” or Anti-Riot Squad.
Ngoma-Africa-bandThe band’s main secret of success is to play authentic Rumba music and ensure that in each concert, all the fans dance right from the beginning to the end. Ngoma Africa Band has a unique and intelligent way of involving and interacting with fans during concerts. Both female and male dancers, dressed in Tanzanian traditional multi-coloured costumes do join the fans in the dance hall to give them a closer taste and look of the majestic Rumba moves as well as the vigorous sexy Soukous moves.
“Our fans are our bosses. We play the music they love and make them happy. And they in turn help promote the band,” says Kamanda Ras Makunja.
Ngoma Africa Band has composed songs on various themes such as love, corruption, press freedom and solidarity. It has also played a major role in fighting racism and promoting integration of Africans in Germany.
Ngoma-Africa-singer-Jessicha-OuyahKamanda Ras Makunja says racism is widespread in Germany, but the situation is not as bad as it was a few years ago.
“I’ll never accept to be a victim of racism. I will instead always fight for my right whenever I face racial discrimination,” Kamanda Ras Makunja says.
A few years ago Ngoma Africa Band held a nationwide tour to back the anti-racism campaign “We are One”.
“Music has the power to break down barriers and bring people together,” Kamanda Ras Makunja says.
He feels very happy when Germans and Africans take to the floor during their concerts. “Our concerts bring together people from all backgrounds just to have fan. That is our way of fighting racism and facilitating integration,” Kamanda Ras Makunja says with pride.
Ngoma-Africa-band-thrilling-fansHe strongly appeals to Africans in Germany to make efforts to integrate in their local communities. “The only way to live a meaningful life here is to integrate in the local society.”
Last January Ngoma Africa Band released a single titled “Mapenzi ya Pesa” (Love of Money).
“We are working on our next CD to feed the souls and hearts of our fans with extraordinary and authentic African music,” Kamanda Ras Makunja says.

MAHAKAMA YAIONYA NHC

$
0
0

Na Humphrey Shao,Globu ya jamii

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imelitaka shirika la Nyumba nchini (NHC) kuheshimu amri ya mahakama na kuondoa notisi walizowapa wakazi wa Keko mpaka kesi ya msingi itakapoisha.

Jaji Beatrice Mutungi wa mahakama hiyo amewaonya NHC leo baada ya wakili wa wapangaji wa magorofa ya Keko yaliyopo barabara ya uwanja wa taifa jijini, Daniel Lisanga kuwasilisha maombi ya kupinga wateja wake kuhamishwa.

Katika maombi hayo, Wakili Lisanga anapinga kitendo cha NHC kupeleka notisi ya siku 14 kwa wateja wake akitaka wahame katika nyumba hizo kabla kesi ya msingi waliyofungua haijaisha. 

Akiongea mahakamani hapo, wakili Lisanga amesema kuwa Februari 27, mwaka huu wakati shauri hilo la ardhi lenye namba 23 likiendelea kusikilizwa, kwa makusudi na huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria NHC Ilipeleka notisi ya siku 14 kwa wapangaji hao ikiwataka wahame.

Hata hivyo, NHC wameidharau amri ya mahakama iliyotolewa na Jaji Augustine Shangwa, Oktoba 6, mwaka juzi iliyowataka kutowabugudhi wapangaji hao mpaka kesi ya msingi itakapoisha.

NHC wanadaiwa kuwatumia Ubapa Auction Mart kwenda kuwaondoa wapangaji hao ambao ni jumla ya familia 60 zinazoishi katika block C,F,G na H. 

Akizungumza nje ya mahakama wakili Lisanga amesema kuwa madai ya msingi ya shauri hilo bado yako mahakamani hivyo wamesikitishwa sana na kitendo cha kudhalilishwa kwa wateja wake kinachoendeshwa na NHC.

“Idara ya mahakama ni muhimili na inastahili kuheshimiwa na mtu yoyote ambaye yupo chini ya sheria”, amesema.Hata hivyo mahakama haikuweza kuendelea na shauri hilo leo baada ya wakili wa NHC, Aloyce Sekule kushindwa kufika mahakamani.
Wakili Daniel Lisanga, akizungumza na wapangaji wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC), mara baad aya kutoka mahakama ku jijini Dar es Salaam.
Wapangaji wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC),wakitoka nje ya mahakama kuu Tanzania.

MTOTO WA MAREHEMU JOHN KOMBA ATOA WIMBO KUUNGA MKONO MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0

NA BASHIR NKOROMO.

Ikiwa sasa ni takriban miaka miwili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT), Kampteni John Komba, kufariki Dunia, Mtoto wake Gerald John Komba, ameibuka na kutoa wimbo wa kuiunga mkono Serikali katika mapambano yake mapya dhidi ya dawa za kulenya nchini Tanzania.

Gerald aliyezaliwa mwaka 1986 jijini Dar es salaam, amesema, ameamua kutoa wimbo huo wenye maudhi ya kwaya, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba yake, Marehemu John Komba aliyefariki  Dunia, Februari 28, 2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar e Salaam, alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake, Tangibovu kwa Komba.

Mtoto huyo wa Jihn Komba aliyekuwa mwanamuziki nguri wa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kwaya, amesema, wimbo aliotoa nimarejeo ya wimbo ambao ulitungwa na nguri huyo, kukemea usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya miaka zaidi ya kumi iliyopita, lakini baada ya kuurekodi haukuwahi kuimbwa na TOT wala kuchezwa kwenye vituo vya Radio au Televisheni.

Gerald ambaye amesomea Sheria katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine kilichopo Mwanza,  Tanzania,  baada ya masomo ya shule ya Msingi katika shule ya Kawe "A" na shule yasekondari Mbezi Beach High school, anasema katika kuutoa wimbo huo, hakubabaisha kwa kuwa na yeye anacho kipaji cha kuimba japo amekuwa hakitumii sana. 

Zamani Shule ya Kawe A' ilifahamika kwa jina la Tanganyika Packers, lakini baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kubaini kuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers kimeshakufa, akaamua shule hiyo kubadilishwa jina.

NAPE NA MAVUNDE WAVIPA SHAVU VIKUNDI VYA JOGGING DODOMA

$
0
0
Na Raymond Mushumbusi .

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde wameamua kuchukua jukumu la kuwa walezi wa vikundi vya Jogging vilivyopo Dodoma.

Azma hiyo imetolewa jana Mjini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na vijana kutoka vikundi vya Jogging mbalimbali Dodoma alipokutana nao na kushiriki mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri.

Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa watahakikisha kuwa kila mtaa unakuwa na kikundi cha Jogging ili kuleta hamasa ya michezo na Utamaduni wa kufanya mazoezi.

“Mimi na Mhe. Naibu Waziri Mavunde tutakuwa walezi wenu kwani ukikaa karibu na ua waridi lazima utanukia” alisistiza Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde ametoa wito kwa vijana wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kujiungana vikundi vya Jogging ili kuendeleza na kukuza Utamaduni wa michezo nchini.

“Niwaombe vijana wa Dodoma wajiunge na vikundi vya Jogging na kujihusisha na masuala ya michezo ili wakuze vipaji vyao na kujenge Utamaduni wa michezo” Alisisitiza Mhe. Mavunde.

Aidha mmoja ya mwanachama wa kikundi cha Jogging ya Muungano Bw. Zebedayo Marko amesema kuwa wamefarijika sana na viongozi wao kujitoa kuwa walezi wa Klabu za Jogging Dodoma kwani itasaidia kuleta hamasa kwa vijana wengi kujihusisha na michezo.

Baada ya tamko kutoka kwa viongozi hao sasa vikundi vya Jogging Dodoma zitafadhiliwa vifaa vya michezo na mahitaji yote yahusuyo mazoezi kwa klabu hizo.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na vijana wa Jogging club Mjini Dodoma mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017. 

 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushirki michezo mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Viewing all 109977 articles
Browse latest View live




Latest Images