Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1590 | 1591 | (Page 1592) | 1593 | 1594 | .... | 3348 | newer

  0 0


  Na Lawrence Raphaely-Bunge.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai amewaahidi Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama hicho ikiwemo maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.

  Mhe Spika aliyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam ambao walimuomba awaunge mkono katika shughuli zao.

  Spika Ndugai aliwaeleza Viongozi hao kwamba kwa niaba ya Wabunge wote ameupokea ujumbe huo na atajitahidi sana katika kuhufikisha kwa Waheshimiwa Wabunge.

  “Ninawashukuru sana kwa ujumbe huu na niwaahidi kwamba tupo pamoja si katika hili tu bali katika mambo yoyote ambayo mtakuwa mkiyafanya na nawaahidi pia ushiriki wa Waheshimiwa Wabunge katika maadhimkisho hayo,” alisema Mhe Spika.

  Awali akimuelezea Mhe Spika kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Skauti hapa nchini Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Stella Manyanya ambaye aliambatana na Viongozi hao wa Skauti alisema pamoja na majukumu mengine Chama hicho cha Skauti kina kazi kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Skauti Dunia na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa pili kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) na anayefutia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) aliyeambatana na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipotembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (aliyekaa kulia) na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Picha na Ofisi ya Bunge.


  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akiwa katika kikao  na wawakilishi wa sekta binafsi wakizungumza kuhusu masuala ya ufanisi katika mchakato wa Tathmini ya athari za Mazingira. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora. Kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya Wadau wa sekta binafsi waliohudhuria kikao hiko wakiwa pamoja na Watumishi na Wataalamu toka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Usimamizi wa mazingira(NEMC) wakimsikiliza Mh. Waziri January Mkamba(hayupo pichani) wakati wa kikao hiko.
  Mmoja wa Wadau toka sekta binafsi za wenye mahoteli, viwanda na fukwe Bi. Lathifa K. Sukes akichangia jambo katika kikao hiko. (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI OMR)

  0 0

  WANACHAMA wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo baina ya taasisi hizo mbili leo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo , Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.

  Alisema kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.Mikopo hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).

  Alisema kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.

  Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya ajira.

  Kuhusu mkopo wa viwanja kwa wanachama, alisema kuwa huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya makazi ambavyo vinapataikana maeneo mbali mbali ya nchi.

  “Lengo kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi yaliyopangiliwa”,alisema.

  Alifafanua kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kupitia mkopo wa elimu , ndoto yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
  Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo.
  Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo.
  Uzinduzi rasmi ukifanyika.


  0 0

  Ndugu Wananchi,

  Tarehe 3 Machi kila mwaka watanzania wote huungana na nchi nyingine za Afrika katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika, ambayo huadhimishwa barani Afrika kila mwaka. Siku hii imetengwa kwa lengo la kukumbuka umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira barani Afrika. 

  Azimio la kuadhimisha Siku hii lilipitishwa na kuamuliwa na Baraza la Mawaziri wanaosimamia Mazingira wa nchi za Afrika kwenye mkutano uliofanyika Durban, Afrika Kusini Mwaka 2002. Siku hii iliamuliwa iwe kielelezo cha kukuza weledi kuhusu kupambana na uharibifu wa mazingira pamoja na kuenea kwa hali ya jangwa Afrika. Kuanzia wakati huo siku hii ilikuwa inaadhimishwa nchini Ethiopia kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika.

  Ndugu Wananchi,

  Kikao cha 12 cha Baraza la Mawaziri wa Mazingira (AMCEN) kiliamua kwamba maadhimisho ya siku hii yawe yanafanyika kikanda. Hivyo kuanzia mwaka 2009 maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika yalianza kufanyika kikanda katika nchi za Afrika na ndipo, mwaka 2010 nchi yetu ikapata fursa ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya yaliyofanyika jijini Arusha. 

  Aidha, Umoja wa Afrika kwa kutambua juhudi na kazi iliyofanywa na Prof. Wangari Maathai kutokana na mchango wa mwanamke huyu katika hifadhi ya mazingira na kuwezesha wanawake katika usimamizi endelevu wa maliasili na mazingira kwa ujumla waliamua tarehe 3 Machi kila mwaka iwe pia ni siku ya kumkumbuka yake iende sambamba na maadhimisho ya siku ya Mazingira Afrika. Hivyo tangu mwaka 2012 maadhimisho ya Siku ya Mazingira Afrika yamekuwa yakienda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wangari Maathai ili kutambua mchango wake katika utunzaji wa Mazingira. Mwanamke huyu alipata Tuzo ya heshima ya Nobel Laureate’s green legacy kutokana na juhudi alizofanya. 
  Kulia Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora, akitoa Tamko la Siku ya Mazingira Afrika kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mkamba, Leo katika mkutano na waandishi wa Habari Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira wa Ofisi hiyo Bw. Richard Muyungi.  0 0


  KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017. 

  Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao. Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17 Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  Katika Uhamisho huo wa Awamu ya Kwanza, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu.

  Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa nikama ifuatavyo:

  Katibu Mkuu,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

  Barabara ya Makole,
  S.L.P 2933,
  Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
  DODOMA.

  Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
  Nukushi : +255-26-2323208,
  Barua pepe : nje@nje.go.tz Tovuti : www.foreign.go.tz

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dodoma, 27 Februari, 2017.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazi Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia rasmi Dodoma. 
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga 
  Walio keti ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katika), Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara Mjini Dodoma 

  0 0

  Washiriki wa miss utalii Songea mkoani Ruvuma watembelea utalii uliopo katika wilaya ya nyasa ili kujionea vivutio vilivyopo katika ziwa nyasa na wilaya hiyo, ambapo wametembelea jiwe POMONDI lilipo LIULI na kisiwa cha LUNDO cha MBAMBABY.


  0 0

  Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.
  Meneja mradi wa Quality Group na katibu wake Leo mapema wamefikishwa katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukiuka amri ya afisa uhamiaji, na kujaribu kutoroka. Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu hiyo, Cpyrian Mkeha.
  Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Uhamiaji, Method Kagoma aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jose Kiran Meneja Mradi na Prakash Bhatt. 
  Akisoma hati ya mashtaka Kagoma amedai kuwa Februari 20, mwaka huu, washtakiwa hao wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Quality Group Ltd, walimzuia afisa wa Uhamiaji kufanya kazi zake.
  Kagoma amedai kuwa, watuhumiwa hao walikataa kuripoti katika ofisi za Uhamiaji zilizopo jijini Dar Es Salaam kwa kujaribu kutoroka nchini Tanzania kwa kupitia mpaka wa Horohoro,ambao ni mpakani mwa Tanga na Mombasa,nchini Kenya. Washtakiwa hao wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana. Mahakama iliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayeweka dhamana ya shilingi milioni tano.
  kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Machi 7 mwaka huu, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali na washtakiwa hao kuunganishwa na wenzao 14.
   
  watuhumiwa wa Manji wakipelekwa mahakamani kujibu tuhuma zao za kukiuka amri ya Afisa Uhamiaji na kujaribu kutoroka nchini.

  0 0

   Kamishna wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akimpokea Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania(CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo alipowasili katika Ofis za Sekretari hiyo kwa ajili ya kula kiapo cha Uadilifu leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akitia saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akipokea Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka kwa Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
   Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
   Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akitia saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
  Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akipokea Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka kwa Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija – MAELEZO.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetayarisha hati 214 kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliosalimisha ofa zao za umiliki wa ardhi kwenye wizara hiyo ili waweze kumiliki ardhi hizo kihalali.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini humo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mambo mbalimbali yanayohusu wizara hiyo.

  Waziri Lukuvi amesema kuwa ni rahisi kwa wananchi wenye umiliki wa ofa kutapeliwa kuliko wakiwa na umiliki wenye hati ambazo ni halali hivyo ili kuondoa changamoto hiyo wizara ilitoa muda kwa wananchi kupeleka ofa hizo ili watayarishiwe hati halali.

  “Kuwa na umiliki halali wa ardhi ni jambo kubwa kwa usalama wa wananchi wenyewe, nataka ifike siku Tanzania iwe haina mtu anayemiliki ardhi kwa kutumia ofa kwa sababu sasa hivi wizara haitoi ofa, ofa hizo zilishakoma siku nyingi,”alisema Lukuvi.

  Ameongeza kuwa ingawa muda wa kusalimisha ofa hizo za umiliki umekwisha lakini wizara hiyo inatoa muda zaidi kwa watu ambao bado hawajapeleka ofa zao katika Halmashauri zao za wilaya kupeleka ofa hizo ili waweze kumiliki ardhi hizo kwa hati. 

  Aidha, akiongelea kuhusu utayarishaji wa teknolojia itakayohusika na masuala yote ya ardhi inayojulikana kama ‘Mfumo Unganishi wa Ardhi’, Waziri Lukuvi amesema kuwa tayari Kampuni ya Kifaransa iliyoshinda tenda inaendelea na kazi na mnamo Julai mosi mwaka huu hati ya kwanza ya kielektroniki ya mfano itatolewa.

  Tayari jengo litakalotumika kwa ajili ya shughuli hizo limeshakamilika na mfumo huo bado unaendelea kutengenezwa ili kuwezesha wananchi wote wanaomiliki ardhi Tanzania wanamilikishwa hati za kielektroniki.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akionyesha baadhi ya nyaraka za ardhi wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaaml,kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Angelina Mabula na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Yamungu Kayandabila. 

  0 0

  Na Ripota wa globu ya jamii

  Wito umetolewa kwa wasanii kuacha kutumia dawa za kulevya na vileo kabla ya kuanza kufanya kazi zao,ili waweze kuongeza weledi wa sanaa kwa hadhira.

  Wito huo umetolewa na mwandishi mwandamizi wa Michuzi blog Humphrey Shao, alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la Sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).

  Akizungumza katika jukwaa hilo ,Shao amesema kuwa amefanikiwa kuandika makala nyingi,zinazousu matatizo ya dawa za kulevya kwa wasani tangu mwaka 2014 lakini mwaka huu 2017 ndipo mambo yote yamekuwa hadharani.

  “tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii halijaanza leo, na wengi wao huanzia na kilevi cha bangi na kupelekea kujiingiza kwenye dawa za kulevya hali inayo hatarisha maisha yao na kazi zao za sanaa”amesema Shao.

  Kwa upande wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi amesema kuwa, amekuwa akishuhudia wasanii wengi ambao hawawezi kupanda jukwaani mpaka walewe, hali inayopelekea wengi wao kuharibu kazi na kupoteza mashabiki.

  Ametaja kuwa mtu ukitumia madawa yakulevya au pombe katika kazi yako inakufanya upoteze umakini ambao unaweza kukupoteza katika ramani ya sanaa na heshima yako kushuka.

  Nae katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza ametoa onyo kwa wasanii wote ambao wanatumia dawa za kulevya na wale ambao hupendelea kunywa pombe kupita kiasi na kupanda katika majukwaa ya muziki.

  Mwingereza amesema kuwa kitendo cha msanii kupanda jukwaani akiwa amelewa ni kudhalilisha kazi ya sanaa ambayo ni kazi kama ilivyo kazi nyingine na kutaja kuwa ni mara chache sana kuona wakandarasi au madaktari kuona wakiwa katika kazi zao wamelewa kama wasanii wetu.
  Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka Michuzi Blog , Humphrey Shao akiongea na wasanii na Waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na BASATA juu ya tatizo la Dawa za kulevya kwa wasanii kulia kwake ni Snura Mushi na kushoto kwake ni Msanii wa Mizengwe Hemed maliyaga(Mkwere Original) na katibu mkuu wa basata , Godfrey Mwingereza .
  Katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii na waandishi habari juu ya kujikwamua katika tatizo la dawa za kulevya

  wadau wa wasanaa na waandishi wa habari wakifatilia
  Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Basata akizungumza na wasanii wa filamiu na muziki kabla ya kuingiakatika mkutano.


  0 0


  0 0


  0 0  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Wasanii na vikundi vinavyopiga muziki wa bendi wametakiwa kujitazama upya juu ya muziki huo kutumika kama chombo cha kuuzia bia kwenye Bar.
  Hayo yamesemwa na msanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini John Kitime alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habri katika jukwaa la sanaa liliandaliwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA).
  “Kuna vitu tunafanya tunaona kama vya kawaida lakini ndio vinaua muziki wetu kama leo hii bendi zinapiga kwenye bara kwa ajili ya kuuza bia na watu wanaangalia bure hivyo inamaanisha bendi zetu ndio kichocheo cha kuuza pombe katika mabaa yote mjini”amesema Kitime.
  Kitime ametoa wito kwa wasanii kuanza kubadilisha mtindo wa maisha kwani kitendo cha bendi zote kuhamia kwenye bar ni moja ya anguko kubwa la muziki wa dansi nchini

  0 0

   Download FASTA @mkitodotcom
  #jifunzekuimba
  #jifunzekuimbanajoett
  #mkitodotcom
  #learntosingwithjoett  0 0


  0 0

   Umati wa wakaazi wa Mbagala waliojitokeza kwenye mkutano wa sheikh shariff uliofanyika Jumapili tarehe 26-02-2017 katika viwanja vya ZAKHEIM Mbagala jijini Dar es salaam.Mkutano huo ndio ulikuwa wa mwisho baada ya kuwa umefanyika kwa siku tatu kuanzia Ijumaa 24-02-2017.
  Sheikh Shariff akiongea katika mkutano wa mwisho uliofanyika Mbagala Zakheim jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

  0 0

  Kampuni hii ipo Majohe, mbele ya Gongo la Mboto, Dar es salaam. Kwa mawasiliano piga simu namba 0713 448 899

  0 0


  0 0

  Akijivinjari ndani ya jiji la Dar es salaam kwenye foleni mida ya mchana ndani ya gari lake jeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo mwembamba mwenye miaka 38, akiwa ameduwaa akiiangalia picha ya samani za kulia chakula kwenye simu yake. Kwa kutumia kidole chake chembamba, kwa madaha, anaiwasha simu yake ili kunionesha picha ambazo anaziangalia.

   “Hii ni moja ya seti ya samani zetu,” anasema, huku akionesha kwa kidole picha ya seti ya samani 5. Ni moja ya bidhaa zinazotegenezwa na Molocaho by Amorette, kiwanda cha kutengeneza samani ambacho amekianzisha hivi karibuni. “Hii samani imetengenezwa kwa mabaki ya mbao ya boti ya mizigo iliyochakaa kutoka Bahari ya Hindi katika mwambao wa pwani ya Tanzania,” akisema mjasiriamali  mwenye kujituma.

  Samani za kulia chakula, ananiambia, ameombwa na familia moja kutoka Ulaya ambayo ilitembelea duka lake la samani hivi karibuni Dar es salaam wakati wa likizo majuma kadhaa yaliyopita na anakaribia kuzisafirisha kwa wateja wake wapya wa Ulaya. Lakini anakwenda kwanza mara moja kwenye kiwanda chake kuzikagua mwenyewe hizo samani kwa mara ya mwisho kabla hazijasafirishwa ili kuhakikisha zinatengenezwa vizuri.

  Jacqueline Ntuyabaliwe, mwenye kiu ya mafanikio ni mwanamke makini sana. Licha ya kuwa na shughuli nyingi pia (ni balozi wa kiafrika wa shirika la kulinda wanyama pori duniani WildAid na huudhuria baadhi ya mikutano ya bodi; mama mwenye watoto wawili mapacha wa kiume; mke wa mmoja ya wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa barani Afrika na anasimamia mfuko wa hisani kwa ajili ya elimu), Ntuyabaliwe huhakikisha anakagua mwenyewe kila samani inayotengenezwa na kampuni yake kabla haijauzwa au kusafirishwa kwenda nje.

  “Napenda vitu vyenye ubora wa hali ya juu!” anasema kwa hisia aliyekuwa malkia wa urembo Tanzania na mwanamuziki, akivuta pumzi kuonesha msisitizo. Kila kitu tunachotengeneza Molocaho lazima kiwe na ubora wa hali ya juu,” anasema. “Tunashindana na makampuni makubwa sana duniani kwa hiyo kama hatutazingatia ubora, itabidi tufunge virago vyetu turudi nyumbani.”


  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0


older | 1 | .... | 1590 | 1591 | (Page 1592) | 1593 | 1594 | .... | 3348 | newer