Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1591 | 1592 | (Page 1593) | 1594 | 1595 | .... | 3278 | newer

  0 0


  0 0

  Mdee Music presents their latest music act Mimi Mars, sister to celebrated Tanzanian pop music queen Vanessa Mdee in her debut single "SHUGA", produced at Hightable Sounds. Shot in Dar es Salaam by the Tanzania director Hanscana, the colorful music video has cameos by Tanzanian superstars like Navy Kenzo, Rosa Ree, Wildad, Quick Rocka just to name a few. 
  "SHUGA" is nothing but sweetness. 
  "SHUGA" will leave you on a sugar high, thanks to its dose of funky freshness. Mimi Mars is a media personality who has over the years established herself as a respected YouTube, TV personality and mcee.
  In her new music venture, the husky-voiced songstress lures you into her world with a sultry tone and her amazing vocals. Thanks to Mdee Music, the creators of mega hits including Niroge, Hawajui, Never Ever, Nobody but me ft South Africa's K.O. – Mimi Mars is already in great company as she takes on a new career path. 
  MIMI MARS ON SOCIAL MEDIA
  Twitter: @mimi_mvrs11
  Instagram: @mimi_mvrs11
  Snapchat:@ms.mars1

  0 0

   Wadau waliojitokeza kutembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakipitia majarida na vipeperushi vilivyokuwa vikitolewa na wafanyakazi wa Benki hiyo. 
   Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Kulia) akikaribishwa kutembelea Banda la TADB na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Saidi Mkabakuli (Kushoto). 
   Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Kulia) akisalimiana na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania waliokuwa wakitoa huduma wakati wa Kongamano la Wadau la SUA linaloendelea Mkoani Morogoro. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi, Bw. George Nyamrunda na Afisa Mipango na Sera Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Mzee Kilele (wa pili kushoto).
   Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Kilimo, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (Wapili Kushoto) wakimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Mwenye tai nyekundu) kufungua Kongamano la Wadau la SUA. Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Wadau la SUA mara baada ya kufungua Kongamano hilo. Wengine waliokaa ni  Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe  (Kulia).

  0 0


  Kundi maarufu la wapenzi,washabiki na wanachama wa Simba SC (NGURUMO ZA SIMBA) limefanya uchaguzi wa viongozi wake watakaoongoza kwa kipindi cha miaka minne. Uchaguzi umefanyika jana huko Kitumbini  jijini Dar es Salaam.
  Waliochaguliwa ni:
  MWENYEKITI : ABUUBAKAR SHAABAN, MAKAMU MWENYEKITI: AMINA SAID "EMMY CAZORLA".
  WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI:1.SALUM HAMAD, 2.MWANAIDI MBWERA, 3.ABUBAKAR, MWINCHANDE NA 4.CRIS MLAGANI.
  Pichani viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama.

  0 0


  0 0
 • 02/27/17--12:30: STEVE NYERERE ALONGA

 • 0 0


  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  TIMU ya soka ya Kisiju Fc inayotokea Kata ya Kisiju imekuwa ya kwanza kutangulia hatua ya fainali ya michuano ya kombe la Mbunge Ulega (Ulega Jimbo Cup) baada ya kuifunga timu ngumu  ya Lukanga Fc kwa bao 1-0.
  Kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Mkuranga ambao pia ulihudhuliwa na wanhanchi wengi pamoja na mbunge  Abdallah Ulega, timu zote zilionesha uwezo mkubwa wa kucheza soka la uhakika huku maelfu ya watazamaji waliohudhulia. 
   Waamuzi mchezo huo iliyochezeshwa jana ni, Niacheni Mohamed aliyesaidiwa Mtuwi Stanley  pamoja na Mharami Mahenga.Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji ambayo yaliinufaisha timu ya Kisiju ambayo ilijipatia bao la pekee katika  dakika ya 62 lililofungwa na Mud Mbwete aliyeunganisha mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na mchezaji Mohamed Taita iliyounganishwa na Mbwete na kujaa wavuni.
  Baada ya bao hilo Lukanga waliongeza kasi ya mashambulizi wakitaka kupata bao la kusawazisha lakiki walinzi wa Kisiju na kipa wao Hassani walikuwa imara. 
  Timu  ya kisiju inaingia fainali ya Ulega Cup itakayofanyika mwanzoni mwa machi mwaka huu
  Akizungumzia mchezo hio  Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega aliwashukuru waamuzi kwa kuchezesha kwa umakini sanjali na wachezaji wa timu zote mbili kwa kuonesha mchezo wenye nidhamu na kuongeza  kuwa vijana wameonesha uwezo  katika kucheza soka.
   Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akisalimiana na wachezaji katika mchezo wa Nusu Fainali  kati ya timu ya  ya kisiju na Lukanga katika kiwanja mpira Mkuranga.
   Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na timu ya Kisiju FC
   Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akiwa na timu ya Lukanga FC
   Mchezo ukiendelea kati ya uwanja
  Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa Nusu fainali katika ya timu ya  ya Kisiju na Lukanga katika kiwanja mpira Mkuranga.

  0 0
  0 0

  Leo mida ya saa mbili  asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi ya Iringa aliibiwa mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo inasadikwia aliibwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi. 
  Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema " nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza. Baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toka  asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona" . 
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako wa muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini. 
  Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtot huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mtuhumiwa huyo wa wizi  wa mtoto. 
  Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala. Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.
   Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla "pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusiowajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu" alisisitiza Mkuu wa wilaya.
  Mkuu wa Wilaya ya iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3 usiku huu.​
  Mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.
  Mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.


  0 0


  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
  Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi.
  Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.
  Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.
  Pia mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.
  “Katika kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam. 
   Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.


  0 0


  0 0


  kusoma magazeti mengine bofya hapa

  0 0

  Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. 

  Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. 

  Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.

  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

  Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
  ‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
  Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Wagonjwa wa Satarani wanaotibiwa katika taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam wataanza kunufaika na huduma bora kwa njia ya kisasa kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano kutokana na mchakato wa serikali kuimarisha huduma za taasisi hiyo.


  Wakati jitihada hizo za serikali zinaendelea sekta baadhi ya sekta binafsi zimeanza kuunga mkono jitihada hizo za serikali ambapo kampuni ya mawasiliano ya Vodacom kupitia taasisi yake ya kuhudumia masuala ya kijamii imetoa msaada wa kompyuta 10 za kisasa kwa taasisi hiyo.


  Akiongea wakati wa kupokea msaada huo katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo leo,Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo,Dk.Julius Mwaiselage,amesema kuwa msaada huu umepatikana katika kipindi mwafaka ambapo hospitali hiyo iko katika mchakato wa kuendesha huduma zake kidigitali.

  Dk.Mwaiselage alisema kuwa hivi sasa kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kutibiwa hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kuwa ili kuwahudumia ni kuwa na huduma za kisasa katika kila idara kwa njia ya TEKNOHAMA na tayari serikali na wadau mbalimbali wameanza kufanikisha mchakato huo.


  Aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada hizo “Tunawashukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa kuunga mkono jitihada za kuboresha huduma zetu ili ziweze kuwa bora zaidi na tunatoa wito kwa taasisi nyingine kuendelea kutuunga mkono katika mapambano haya ya kutokomeza ugonjwa wa Saratani nchini na kuwapatia huduma bora wahanga wa ugonjwa huu”.Alisema.

   Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania  wakiwa na misaada mbalimbali  kwa ajili ya wagonjwa wanaopata  matibabu   katika Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam  wakati walipowasilia kwenye taasisi hiyo  hivi karubni  kutoa msaada   wa kompyuta 10 za kisasa kwa taasisi hiyo kupitia kitengo chake cha Vodacom Tanzania Foundation. Msaada huo utarahisiha utoaji wa huduma bora kwa angonjwa.

   Mkuu wa Kitengo cha  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Tanzania  Jacqueline Materu (kulia) na Mkurugenzi wa mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi  Clarence Ichwekeleza (Kushoto) wakimsikiliza kwa makini  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam  ,Dk.Julius Mwaiselage, wakati alipokuwa akishukuru kwa Taasisi ya  Vodacom Tanzania Foundation  kwa  kuwapatia msaada wa Kompyuta 10 za kisasa  kwa ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

   Mkuu wa Kitengo cha  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Tanzania  Jacqueline Materu (kulia) , Mkurugenzi wa mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi  Clarence Ichwekeleza (wapila kulia )  na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Sandra Osward,  (wapili kushoto) wakimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam  ,Dk.Julius Mwaiselage,(kushoto) wakati alipokuwa akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya  Komputa  kati ya 10 za kisas alizopewa msaada na Taaisi ya Vodacom Tanzania Foundation , kwa ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa wanaotibia katika Taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha  Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom,Tanzania  Jacqueline Materu (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uchunguzi wa Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam  ,Dk.Julius Mwaiselage,(kushoto)  moja ya kompyuta kati ya 10 za kisasa zilizotolewa msaada na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation  kwa ajili ya kusaidia kutao huduma bora kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  '
  Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa mawasilianao wa Wizara ya ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi  Clarence Ichwekeleza (wapili kulia) na Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Foundation Sandra Osward.


  0 0

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikagua gwaride maalum lililoandaliwa, ukaguzi wa gwaride hili huashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka husika.

  Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania

  Nchi yoyote yenye kuzingatia misingi ya Utawala wa Sheria, huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta amani na Maendeleo ya kiuchumi katika taifa husika.

  Hii inajidhihirisha kupitia Kaulimbiu ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini, 2017 ambayo ni ‘Umuhimu wa Utoaji Haki kwa wakati kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.’

  Kauli mbiu hii ina maana ya kuwa kukamilishwa mapema kwa mashauri ya jinai, Rushwa na Uhujumu Uchumi ambayo yanaendeleza amani na usalama katika jamii ni chachu ya maendeleo ya uchumi.
  Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania iliadhimisha Siku ya Sheria nchini, ambayo huashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama ambapo shughuli za usikilizaji wa Mashauri huanza rasmi.

  Kwa mwaka huu, sherehe za Siku ya Sheria nchini ziliadhimishwa rasmi tarehe 02.02.2017, ambapo kila Mkoa uliadhimisha, kwa upande wa Dar es Salaam, Sherehe hizi zilifanyika katika Kiwanja cha Mahakama kilichopo Chimala karibu na Hospitali ya ‘Ocean road’ ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia watumishi na wageni waalikwa katika Siku ya Sheria nchini iliyofanyika Februari 02, 2017.

  Aidha; Sherehe za Kilele cha Siku ya Sheria nchini zilitanguliwa na Maonyesho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza rasmi Januari, 28 hadi Februari 01, 2017, Maonyesho ya Wiki ya Sheria yalifanyika nchi nzima lengo kuu likiwa ni kutoa elimu ya Sheria kwa Wananchi juu ya huduma na taratibu mbalimbali za Kisheria.

  Kwa upande wa Dar es Salaam, Maonyesho ya Wiki ya Sheria yalifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini humo, Wadau walioshiriki ni pamoja Mahakama yenyewe kama mwenyeji, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mahakama Kuu Zanzibar, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Mahakama (AGC), Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Mkemia Mkuu wa Serikali, Chuo cha Uongozi wa Mahakama IJA, Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Huria, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

  Wengine ni Tume ya Kurekebisha Sheria, Taasisi zinazotoa msaada wa Kisheria (Legal Aid), TAKUKURU (PCCB), Polisi, Magereza, Msajili, Mabaraza ya Ardhi,  Chama  cha Wanasheria
  Tanganyika (TLS), Tume ya Kurekebisha Sheria, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA, Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA),  Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Sekretarieti ya Msaada wa Sheria, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ‘Tanzania Network of Legal Aid Provider (TANLAPS),’ Legal Aid and Human Centre na NHIF.
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Jaji Prof. Ibrahim Juma akisoma risala yake ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika Februari 02, 2017, waliopo nyuma ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu ni baadhi ya Wahe. Majaji wa Mahakama ya Tanzania.

  Katika maonesho hayo kulikuwa na uwakilishi wa ngazi zote za Mahakama kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama ya Rufaa ambapo taratibu/huduma mbalimbali za Kimahakama zilitolewa kwa wananchi waliopata fursa ya kutembelea mabanda ya Maonesaho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


  0 0

   


  0 0
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akimkabidhi vifaa vya shule Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani, Tuwaje Mohamed kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ambao wanatoka katika familia duni. Wa pili kulia ni Caroline Magoti.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akimkabidhi sare za shule, Esther Amon.

  Wanafunzi wakiwa darasani.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akiwakabidhi sare za shule baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam, wanafunzi hao wanatoka katika familia duni.
  Wanafunzi waliopata vifaa vya Shule wakiwa katika picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 1591 | 1592 | (Page 1593) | 1594 | 1595 | .... | 3278 | newer