Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR DKT.SHEIN AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Vuai Naimu wakati wa utoaji wa Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,ambapo majimbo mbali mbali walikabidhiwa vifaa hivyo hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimkabidhi vifaa mbali mbali vya michezo mwakilishi wa Jimbo la Kwahani CCM Sufiani khamis wakati wa utoaji wa Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,ambapo majimbo mbali mbali walikabidhiwa vifaa hivyo,hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akimkabidhi vifaa mbali mbali vya kuendeshea mashindano ya mpira wa Miguu kwa timu za Vijana majimbo ya CCM wilaya za Unguja,Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Abdalla Mwinyi Hassan,vifaa hivyo vilivyotolewa na  Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Aman
 Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa majimbo ya Unguja CCM na Vijana wakiwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali na Vijana wa Majimbo na ya CCM Unguja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mhe,Mohamed Raza Daramsi,ikiwa ni katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo, hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
Picha na Ikulu. 

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Rais Museveni atembelea viwanda vya Bakhresa jijini Dar leo,awakaribisha Watanzania Kuwekeza Nchini Uganda

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.

RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NCHINI NA KUREJEA NYUMBANI

$
0
0
 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka  ma kurejea nchini kwake. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakifurahia jambo wakati walipokwenda kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.

SENSEI Rumadha Fundi na wanafunzi wa Tanzania wa Goju Ryu karate kupandishwa ngazi mwaka huu

$
0
0
Sensei Rumadha Fundi, mwakilishi wa Jundokan So Honbu Tanzania, na wanafunzi waandamizi toka " Jamhuri Kaizen Dojo  na Zanaki Dojo " za Dat es salaam wanakitarajiwa kupandishwa ngazi ya chama hicho baada ya semina ya 
(European Jundokan Gasshuku) Mnamo mwezi July 14 hadi  16, 2017. katika mji wa Marki,  nje kidogo ya mji wa Warsaw, Poland.
Hali kadhalika Sensei Rumadha amepewa mwaliko huo ikiwa ni sehemu ya kwenda kukutana  na walimu wakuu ( Masters) toka Okinawa,  Japan,  na kufanya mtihani wa shahada ya nne "Yondan" ya Goju Ryu chini ya mwenyekiti wake, Master Kancho Yoshihiro Miyazato. 
Maandalizi makubwa yanatarajiwa kwa wanafunzi wa Tanzania ambapo hatimaye watapandishwa ngazi za ualimu za " Sensei " mara baada ya  Sensei Rumadha kuwasili  nchini baada ya semina hiyo ya Poland.
 Sensei  Rumadha na wanafunzi wake wa wakilishi wa Tanzania Senpai Waheed na Senpai Jesse wakiwa mazoezi jijini Dar es salaam ni hivi karibuni. 
Sensei  Rumadha na wanafunzi wa Zanaki Dojo wakiwa mazoezi jijini Dar es salaam ni hivi karibuni. 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 27,2017

WAFANYAKAZI WA ZANTEL WACHANGIA DAMU KUSAIDIA WENYE MAHITAJI

$
0
0

Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel Kitengo cha Ugavi Bi. Mainda Madiwa Chanika akichangia damu kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana na wingi wa watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi hilo lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Fatuma Mjungu akizungumza na vyombo vya habari wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watanzania wengine lilowahusisha baadhi ya wafanyakazi wa Zantel lililofanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo ya jumla wa Kampuni ya Zantel, Deo Ngonyani akishiriki katika zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo lililifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kulia) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel Kitengo cha Uhasibu Bw. Ally Abdallah akichangia damu kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana na wingi wa watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi hilo lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.

masoud Kipanya


BAADA YA MIAKA 53 HATIMAYE WANANCHI WA MTAA WA IGUNGANDEMBWE MANISPAA YA IRINGA WAPATA MAJI SAFI NA SALAMA

$
0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.

Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.

“Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.

Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho. 
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima 


UTOAJI TAARIFA ZA MIRADI YA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA UMMA UNAVYOSAIDIA KUPAMBANA NA RUSHWA

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika  ujenzi wa miundombinu ya Umma  kwani ni muhimu kuwa na miundombinu mizuri na bora ili kutoa huduma bora na kurahisisha ufanyaji kazi hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi katika nyanja zote muhimu zikiwemo za biashara, utalii na mawasiliano.

Matumizi makubwa ya fedha za Serikali yanatumika katika ujenzi wa miundombinu ya Umma ambapo matumizi hayo yanahusisha karibu asilimia 53 ya Bajeti nzima ya nchi.

Miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Umma inayoelezewa hapa ni ile ambayo inajengwa kwa fedha za Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi wote ikiwemo ya barabara, hospitali na vituo vya afya,shule na vyuo,nyumba za kuishi pamoja na ofisi mbalimbali. 

Ingawa Serikali inajitahidi kuhakikisha nchi inakuwa na miundombinu bora itakayochochea maendeleo, lakini jitihada hizo zimekuwa zikikwamishwa na changamoto mbalimbali zinazojitokeza pindi mradi husika unavyoanza kwani wahusika hawatumii fedha kama zilivyopangwa na badala yake wanafanya kwa makadirio ya chini na kufanya ujenzi kutokuwa imara.

Hali hiyo inasababisha Serikali kupata hasara kwa kupoteza fedha nyingi na kuambulia kubaki na majengo yasiyo na viwango ambayo mwisho wake hushindwa kutumika na kuilazimu Serikali kuanza upya ujenzi husika. 

Kwa kuwa Serikali hii ni sikivu na imejipanga kuhakikisha nchi inafika katika uchumi wa kati basi mambo hayo hayana nafasi na hayawezi kutokea tena katika nchi hii watu kuachiwa huru kutumia vibaya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

Kwa kuhakikisha hilo,Serikali kupitia Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) chini ya Mkakati wa Kukuza Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Ujenzi Tanzania (CoST-Tanzania) imejipanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo ili kuondokana na rushwa pamoja na ubadhilifu wowote wa fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mkakati huo unalengo la kupambana na rushwa, usimamizi mbaya katika ujenzi pamoja na changamoto zingine zinazopelekea ubadhilifu wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya miundombinu ya Umma kwa kukusanya taarifa za miradi hiyo ya ujenzi ili  kuhakikisha kama thamani ya miundombinu iliyojengwa inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,(Ujenzi), Mha. Joseph Nyamuhanga alikaririwa akisema kuwa “Sekta ya Ujenzi ni sekta moja wapo inayoonekana kukithiri kwa rushwa duniani kwa sababu takribani asilimia 10 hadi 30 ya Bajeti yake inapotea kwa njia ya rushwa na usimamizi mbaya hivyo ili kuondoa dhima hii ni lazima kukusanya na kutoa taarifa kwa wananchi juu ya ujenzi wa miundombinu hiyo”.

Mwanariadha afia getini Kili Marathon

$
0
0
Mwanariadha, Charles Maroa kutoka nchini Kenya amefikwa na mauti katika hospitali ya KCMC mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuanguka katika geti la viwanja vya Ushirika wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro zilizofanyika jana Februari 26.

Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa alisema kuwa Mwanariadha huyo alikutwa na umauti huo jana majira ya saa tano asubuhi katika hospitali la KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.

"Tumepokea taarifa za kifo cha Mwanariadha huyo alietambulika kwa jina la Charles Maroa,ambaye ni raia wa Kenya (Mkurya), baada ya kukumbwa na hali hiyo alikimbizwa hospitali ya KCMC kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka ghafla katika geti kuu la kuingia katika viwanja vya Ushirika hapa mjini Moshi wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro na tunaendelea na uchunguzi kujua nini kilitokea mpaka kuelekea kifo chake" alisema.
Mwili wa Mwanariadha huyo umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.

Serikali kutoa matrekta ili kuinua kilimo biashara kwa wanawake.

$
0
0
SERIKALI imeahidi kutoa pembejeo za kilimo cha kisasa yakiwemo matrekta kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupitia taasisi inayojihusisha na kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT) ili waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo cha kisasa hususani cha kibiashara.

Ahadi hiyo ya Serikali ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha kwa Niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye harambee kukusanya fedha kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Land O’ Lakes kwa kushirikiana na CAWAT na kufanyika jijini Dar es salaam mwshoni mwa wiki.

“Serikali ipo tayari kutoa pembejeo hizo za kilimo cha kisasa yakiwemo matrekta bora kabisa ambayo yataolewa kwa vikundi vya kina mama wanachama wa CAWAT ambao wataonyesha nia na uwezo wa kutekeleza kilimo cha kisasa hususani cha kibiashara. Zaidi wanufaika hao watahakikishiwa soko la uhakika kwa kile watakachozalisha,’’ alisema Ole Nasha ambae pia yeye binafsi alitoa mchango wa mil. 2 kwenye harambee hiyo.

Alisema serikali ipo tayari kushirikiana na taasisi yeyote nchini yenye nia ya dhati katika kuleta mabadiliko yenye tija yatakayoliwezesha taifa kuongeza kasi yake katika kuelekea uchumi wa viwanda na mapinduzi ya kilimo.  
 Mkurugenzi Mradi kutoka taasisi ya Land O’ Lake Dr Rose Kingamkono akizungumza kwenye harambee ya kukusanya fedha  kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya washiriki wa harambee hiyo.
 Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha  akizungumza kwenye harambee hiyo.  Ole Nasha alimuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye harambee hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa!
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini  (TADB) Bw Francis Assenga akizungumza kwenye harambee hiyo.Benki hiyo ilitangaza nia yake ya kutenga sh milioni 600 kuwezesha miradi ya taasisi  ya CAWAT. 
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha akipeana mkono wa pongezi na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa pesheni wa PPF, Lulu Mengele ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa mfuko huo kwenye harambee hiyo.


NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT.ASHATU KIJAJI AFUNGUA TAWI JIPYA LA FIRST NATIONAL BANK JIJINI ARUSHA

$
0
0
First National Bank (FNB) Tanzania imeendelea kupanua wigo wake kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la PPF Plaza jijini Arusha kwa lengo la kuhudumia ongezeko la idadi ya wateja katika mkoa huo.

 Akizungumza wakati wa ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dave Aitken alisema uzinduzi wa tawi la FNB Arusha umelenga kukidhi ongezeko kubwa la wateja na mahitaji ya huduma za kibenki na kifedha katika kanda ya kaskazini. 

“ Uzinduzi wa tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wa uwekezaji endelevu uliolenga kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia ni kwa maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania” Aitken alisema tawi la Arusha ni la kumi miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mitandao ya matawi kwa kusudi la kuyafikia maeneo mengi ya nchini.

 “First National Bank (FNB), daima tunafikiria njia ambazo zinaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Arusha litasaidia kuwapatia huduma zote za kibenki wananchi wa mkoa wa Arusha na wanaoishi maeneo jirani kwani maeneo haya yote yamedhiirika kuwa na biashara mbalimbali zinazokua kwa kasi,” alisema Aitken. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Arusha huku akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa FNB, Dave Aitken(wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la Arusha, Mh. Calist Bukhai (kulia). 
Meneja wa Tawi la FNB Arusha, Genevieve Massawe akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji jinsi mashine ya kisasa ya kuweka fedha (cash deposit) na kutoa fedha. Mashine hiyo ya kisasa inamuwezesha mtumiaji kuweka fedha zake benki muda wa masaa 24 imewekwa kwenye tawi hilo jipya ili kuwawezesha wananchi kuweka akiba fedha zao muda wowote ule. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akimrekebishia kipaza sati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la FNB Tanzania la Arusha mwishoni mwa wiki. 


RC MRISHO GAMBO ATEMBELEA NYUMBANI KWA HAYATI EDWARD SOKOINE

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli. 

Mh.Gambo alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko Mkoani Morogoro, Mkuu wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi majirani wanaozunguka familia hiyo na kusema maneno machache ambapo Alisema 

"Kutembelea maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania Taifa letu kwa uzalendo mkuu, inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa Uadilifu na uwajibikaji,ili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa." 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.
Mh.Gambo akiwa ameambatana na Mjane wa Sokoine Pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali,Wakitoa Heshima kwenye kaburi la Hayati Sokoine.  
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Gambo akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Sokoine.Picha na Msumbanews.com


JARIDA LA OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU LA MWEZI JANUARY, 2017


RC DKT KEBWE AAGIZA ZOEZI LA USAJIRI WA WAFUGAJI KWENDA SAMBAMBA NA USAJIRI WA WAKULIMA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewaagiza Viongozi wa Serikali Mkoani humo ngazi ya Wilaya hadi kata kuwa na madaftari ya kuwasajiri wakulima ifikapo Machi 31, mwaka huu.


Dkt. Kebwe ametoa agizo hilo Februari 22 mwaka huu wakati anatembelea kiwanda cha kuzalisha Mpunga cha KPL kilichopo katika Wilayani ya Kilombero ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano aliyoifanya Wilayani humo.

Katika maelezo yake Dkt. Kebwe amesema zoezi la usajiri wa wafugaji pamoja na mifugo yao lazima liende sambamba na zoezi la usajiri wa wakulima kwa lengo lilelile la kupata takwimu halisi kwa Mkoa mzima na si kuwa na takwimu za mezani.

“Sambamba na kazi ambayo tuliianza mwaka jana mwezi wa sita ya utambuzi wa mifugo kazi ambayo inaendelea awamu ya pili, madftari ya wafugaji sehemu kubwa yameanza kuwepo wafugaji wanatambuliwa. Kwa hiyo vitu hivi viwili lazima viende sambamba hii inasaidia kutengeneza maoteo katika Halmashauri zetu. Huwezi kufanya maoteo bila kuwa na tax base” alisema Dkt. Kebwe

Mkuu huyo wa Mkoa ameonekana kuridhishwa na juhudi zinazooneshwa na baadhi ya wakulima hususani wa Wilaya ya Kilombero kujihusisha katika kilimo na kusema amejionea mwenyewe watu wamelima mashamba makubwa ingawa mvua zimechelewa kunyesha tofauti na maeneo mengine ambapo wamelima maeneo madogo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Steven Kebwe akishiriki katika kazi ya kiwekea mifugo alama ikiwa ni utambuzi wa mifugo hiyo.
Ng’ombe ambao tayari wamesha wekewa alama.

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kufungua mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma kesho

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kesho (28 Februari 2017) atafungua mkutano wa siku moja wa Watendaji Wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma utakaojadili nafasi za Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa II wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.


Mkutano huu ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina utafanyika Ikulu – Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 asubuhi.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema kwamba malengo ya mkutano ni kukusanya maoni ya viongozi kuhusu nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano; kuzungumzia changamoto tarajiwa katika utekelezaji wa majukumu haya na; kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.


“Mashirika ya Umma yana nafasi na uwezo mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17–2020/21 wenye kaulimbiu ‘Maendeleo ya Viwanda kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu’,” alisema Profesa Semboja.


Profesa Semboja aliendelea, “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mkutano huu unawakutanisha viongozi kutoka Serikalini na Mashirika ya Umma kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu wa jinsi mashirika haya yatakavyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa maendeleo endelevu.”


Pamoja na mambo mengine, mkutano utajadili namna ya kuboresha mifumo ya  kiundetaji ndani ya mashirika na mahusiano miongoni mwa mashirika na taasisi za Serikali;kufungamanisha mipango ya mashirika ya Umma na Mpango wa Pili wa Maendeleo; kutathmini kiwango na aina ya rasilimali zinazohitajika kuwezesha utekelezaji wa mipango na; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango.


Mkutano utawakutanisha zaidi ya washiriki 100 kutoka Wizara, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Udhibiti takribani 52 hapa nchini.


 Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano –Taasisi ya Uongozi.


WENYEVITI WA MITAA WATAKIWA KUWATUMIKIA WANANCHI BILA YA KUWABAGUA-DC HAPI

$
0
0
Na Anthony  John Glob Ya Jamii. 

Watendaji katika Manispaa ya Kinondoni wakiwemo venyeviti wa mitaa wametakiwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za vyama vyao.

Akitoa wito huo, mkuu wa wilaya hiyo ALI HAPI wakati akizungumza na watendaji wa kata ya Ndugumbi, amesema baadhi ya watendaji hasa wenyeviti wa mitaa katika baadhi ya sehemu wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwanabagua wananchi kwa itikadi za vyama vyao ,hali inayochangia pia kukosa huduma muhimu za kijamii.

Ametolea mfano upo mtaa mmoja ukionekana chama fulani hupati maji ,kwasababu kiongozi wa mtaa huo anatoka chama fulani na chama kingine huruhusiwi kuchota maji.

Ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha, hivyo siasa na vyama vya siasa visiwagawe kwani hivyo husaidia ktk kuzipata nafasi hizo za uongozi tu.

Mkuu wa wilaya pia amekagua mradi wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Mwalimu Nyerere huku akimuagiza injinia wa manispaa hiyo SIMON LIACHEMA kuangalia mfumo wa kisasa katika utengenezaji wa matundu hayo ya vyoo ili kuwapa urahisi wanafunzi pindi wanapotumia vyoo hivyo.

Katika hatua nyingine amekagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu mkuu katika shule ya sekondari Turiani na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa walimu wa shule hiyo pindi watakapoanzisha chama chao cha kuweka na kukopa SACCOS pamoja na kutembelea soko la Babati.    


 .mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi  Akizungumza na wananchi katika soko Babati lililopo kinondoni Jijini dar es salaam.
 .Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akikagua mradi wa majengo  mbali mbali katika  shule ya msingi Mwalimu Nyerere akiwa na walimu  wa Shule Hiyo leo hii iliyopo kinondoni Jijini Dar es salaam. 

HAKUNA MABADILIKO YA UTAWALA WA ZANZIBAR YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA HIVI KARIBUNI-BALOZI SEIF ALI IDI .

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Idi amewaasa wana CCM na wananchi nwote Nchini kuacha tabia ya kuhamanika kutokana na uvumi unaoenezwa mitandaoni kwamba yapo mabadiliko ya utawala wa Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mirai yao ya maendeleo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye Hfla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.

Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ataendelea kuviongoza Visiwa vya Unguja na Pemba hadi utakapofanyika uchaguzi mwengine mwaka 2020 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Michezo kwa Timu zinazoshiriki Mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja hapo ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wanamichezo wa Timu za Majimbo wakifuatilia hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zao hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
Kikundi cha Utamaduni cha CCM Mkoa Mjini Big Star kikitoa burdani wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamuj Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa Kusini Unguja Mh. Mohamed Raza ambae ia ni mdhamini wa mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja nje ya ukumbi wa CCM Aman Mjini Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

VODACOM YAWAFANYIA HAFLA FUPI WANARIADHA WATANZANIA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary(kulia)akimkabidhi simu aina ya Samsung Galaxy S6 edge plus,Ahasina Omary alieibuka mshindi katika mbio za walemavu za Kilimanjaro zilizofanyika mwishoni mwa wiki,Vodacom Tanzania iliwafanyia hafla fupi baadhi ya washindi watanzania ili kuwapa moyo Watanzania hao wajitume zaidi siku zijazo.
 Baadhi ya wanariadha watanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa chama cha riadha Tanzania(kulia)baada ya kukabidhiwa zawadi zao za simu aina ya Samsung Galaxy S6 edge plus na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary(wapili kulia)wakati  wa  hafla fupi iliyoandaliwa na  Vodacom Tanzania kwa ajili ya wanariadha  watanzania ili kuwapa moyo kujituma zaidi siku zijazo.
 Mwanariadha Mtanzania alieshiriki mbio z nusu marathoni na kushika nafasi ya 11,Joseph Teophil kipoke zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy S6 edge plus toka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania,Ashutosh Tiwary(kulia)wakati  wa  hafla fupi iliyoandaliwa na  Vodacom Tanzania kwa ajili ya wanariadha  watanzania ili kuwapa moyo wajitume zaidi siku zijazo,Kushoto ni Banuelia Brigton

Mkuu wa kanda ya Kasikazini wa  Vodacom Tanzania,Henry Tzamburakis(kulia)akimkabidhi simu aina ya Samsung Galaxy S6 edge plus,Peter Sulle alieshika nafasi ya 17 katika  mbio za Kilimanjaro Marathoni KM 42 zilizofanyika mwishoni mwa wiki,Vodacom Tanzania iliwafanyia hafla fupi baadhi ya washindi watanzania ili kuwapa moyo  kujituma zaidi siku zijazo.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images