Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

LUGHA YA KISWAHILI IWE BIDHAA YA KUUZIKA DUNIANI- WAZIRI NAPE


RAZA AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.

 Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

UUNDAJI MELI MBILI ZA MIZIGO ZIWA NYASA WAKAMILIKA ASILIMIA 98

$
0
0

Benny Mwaipaja, WFM, Kyela

UJENZI wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd ya Jijini Mwanza, inayounda meli hizo, Mhandisi Saleh Songoro, amesema hayo wakati ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo ukiwa katika zaira ya kukagua hali ya biashara mipakani mkoani Mbeya.

Amesema kuwa kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja na kugharimu shilingi bilioni 11, kutaiwezesha Kampuni hiyo kuanza kuunda meli nyingine ya tatu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.

Pamoja na meli hizo, Mhandisi Songoro amesema kuwa mradi huo pia umewezesha kujengwa kwa cherezo cha kwanza na cha pekee kitakacho iwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA katika uundaji wa meli na kuzifanyia matengenezo meli nyingine za ndani na nje ya nchi zikiwemo Malawi na Msumbiji.

Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bandari ya Itungi, Bw. Ajuaye Msese, amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuunda meli hizo ulikuwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa vyombo vya baharini vya kusafirisha abiria na mizingo ndani na nje ya nchi kupitia Ziwa Nyasa.

Meli mbili za Mv. Ruvuma na Mv Njembe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa Februari, 2017.
Bw. Juma Nassoro akipaka rangi meli ya mizigo ya Mv Ruvuma, ikiwa ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa uundaji wa meli hiyo yenye uwezo wakubeba tani 1000 za mizigo itakayokuwa ikifanya safari zake Ziwa Nyasa, wakati Ujumbe wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipofanya ziara katika Bandari ya Itungi, wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bw. Ajuaye Msese akitoa maelezo mafupi kuhusu Bandari ya Itungi, na majukumu yake kwa ujumla kwa wageni waliotembelea Bandari hiyo mkoani Mbeya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mfumo wa kuongoza meli katika chumba cha nahodha wa meli ya Mv Njombe, huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biasha na Uwekezaji Prof Adolf. Mkenda, akiangalia kwa makini mfumo huo wa kisasa namna unavyofanya kazi.
Baadhi ya wajumbe wa Serikali waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi mkoani Mbeya kujionea uundwaji wa meli mbili za mizigo wakishuka kwenye ngazi baada ya kumaliza kukagua meli ya Mv Njombe inayotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd inayoshughulika na kutengeneza vyombo vya usafiri vya majini katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM) 

PLAN INTERNATIONAL WAZINDUA MPANGO KAZI UTAKAOISAIDIA SERIKALI KUFIKIA SDGs IFIKAPO 2030

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Plan International limezindua Mpango Kazi wa miaka 5 utakaowawezesha wasichana wanaoishi katika mazingira magumu kujitambua na kujisimamia wenyewe katika nyanja mbalimbali zitakazowaletea maendeleo. 

Mpango kazi huo unaanza mwaka 2017- 2022 ukiwa na lengo la kuwasaidia wasichana 1,000,000 ulimwenguni kote.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kanda ya Nchi za Afrika Mashariki na Kusini – Plan International, Roland Angerer alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu malengo ya mpango kazi huo.

Angerer amesema kuwa Shirika hilo limepanga kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030 kwa sababu mpango huo umelenga kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto hasa wasichana na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika suala zima la maendeleo.

“Plan International wameweka mpango mkakati wa ulimwengu mzima ambao utawasaidia wasichana sio tu katika kupata elimu bali kuwafanya wawe na nguvu itakayowasaidia kujifunza, kujiongoza, kuamua pamoja na kujipigania katika mambo mbalimbali yanayowahusu,”alisema Angerer.

Ameongeza kuwa usawa wa kijinsia ni moja ya Mpango wa Maendeleo Endelevu hivyo wataweka juhudi kubwa katika kuhakikisha wasichana wanapata haki sawa na wavulana kwani usawa huo utasaidia kuharakisha maendeleo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo- Tanzania, Jorgen Haldorsen amesema kuwa nchini Tanzania mpango huo utalenga zaidi katika kuzuia ndoa za utotoni kuanzia katika ngazi ya Kitaifa hadi Vijiji ili kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki zake.

”Kwa kushirikiana na Serikali , tumeanzisha miradi ya kuzuia ndoa za utotoni katika Mikoa ya Mara, Geita,Morogoro na Rukwa na katika mikoa hiyo tunategemea kuwafikia moja kwa moja wasichana 12,000 na kuwafikia wasichana 120,000 kwa njia zingine tofauti,”alisema Haldorsen.

Amefafanua kuwa pamoja na jitihada zote na rasilimali mbalimbali kuelekezwa kwenye jamii kupitia Mikoa,Wilaya na Kata lakini bado wanatambua umuhimu wa kufanya kazi na Serikali katika ngazi ya kitaifa kwa kutoa maoni na uzoefu wao katika kutengeneza sera zinazomuhusu mtoto na usawa wa kijinsia.

Kwa upande wake Muhamasishaji kutoka Mradi wa Vijana wa ‘Youth for Change’, Upendo Abisai amelishukuru shirika hilo kwa kufanya jitihada katika kuhakikisha msichana anapata haki zake kwani ulimwengu mzima wasichana ndio wanaokumbwa na changamoto nyingi zinazowapelekea kutotimiza malengo yao. 

“Sisi kama vijana wa ‘Youth for Change’ tumepewa fursa kubwa ya kuwafikia na kuwaelimisha vijana wenzetu juu ya haki zao za msingi pia tuna nafasi ya kuwasemea wale ambao hawajapata nafasi ya kusema ili kuhakikisha wote kwa pamoja wanapata haki zao”,alisema Bi. Upendo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKERWA NA KIWANDA CHA MBOLEA CHA MINJINGU KUWEKA MBOLEA KWENYE MIFUKO INAYOONYESHA KUWA MBOLEA YA KIWANDA HICHO IMEZALISHWA KENYA

$
0
0
  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa  kiwanda hicho  kuandika barua ya kumuaomba radhi  Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho.  Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

USIKU WA DR. BANDUKA NA MAY NDANI YA UKUMBI WA KUNDUCHI BEACH HOTEL

$
0
0
Dr. Banduka na Mkewe wakiwa na nyuso za furaha baada ya kufunga Ndoa takatifu katika kanisa la Kilutheri Mwenge jana tarehe 18/02/2017 na baadae kufanya tafrija ya nguvu katika Ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel jijini Dar es salaam
Couple mpya Dr Banduka na Mkewe wakipata Selfie na Mwanasheria Nguli Dr. Saudin Jacob (Mwenye Miwani) na Ndugu Emanuel Mwaituka jana katika ukumbi wa Kunduchi Beach baada ya kufunga ndoa takatifu.
M-CPA Sais Kyejo akiwa na Mkewe Magreth Kyejo pamoja na Henry Kapinga (KAPINGAZ) wakipata Selfie baada ya kushiriki sherehe ya Harusi ya aliyewahi kuwa mwanafunzi mwenzao katika shule ya sekondari Songea Boys, Dr. Banduka Elisante jana katika ukumbi wa Kunduchi beach hotel.
Wadau mbalimbali walioshiriki katika harusi ya Dr. Banduka wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kupata ile kitu roho inapenda.

DC MUHEZA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA UBWARI KUJIONEA ZOEZI LA UPASUAJI MACHO KWA WANANCHI WALIO NA MATATIZO YA JICHO LA MTOTO.

$
0
0
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiingia kwenye kituo cha Afya Cha Ubwari leo wakati alipokwenda kuangalia zoezi la upasuaji wa macho kwa wakazi wa wilaya hiyo wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya mtoto wa Jicho iliyoendeshwa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo,Mathew Mganga na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Luiza Mlelwa. 
Baadhi ya wazee waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza wakati wa zoezi hilo la upasuaji 
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa zoezi la upasuaji huo.
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali mwakilishi wa wazee waliofanyiwa upasuaji wa macho ili viweze kuwasaidia baada ya kumalizika upasuaji huo watakapokwenda majumbani mwao wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa ,Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo,Mathew Mganga wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akagua ujenzi wa barabara ya kinduni na Kichungwani

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Ujenzi wa Bara bara ya Kinduni, Kichungwani na hatimae kuelekea Kitope unaofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utasaidia kuharakisha maendeleo ya Wananchi hasa wakulima wa Vijiji hivyo. 

Alisema Ujenzi wa Bara bara hiyo ambao umo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM unatekelezwa kufuatia ahadi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mstaafu wa Awamu ya Sita Dr. Amani Karume.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Kinduni na Kichungwani baada ya kuikagua Bara bara hiyo iliyojengwa na Wahandisi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar katika kiwango cha kifusi kuanzia Kinduni hadi Kichungwani.

Alisema Bara bara hiyo itakapokamilika rasmi itarahisisha mawasiliano ya usafiri kwa Wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanajishughulisha na kazi za Kilimo mchanganyiko katika kujipatia riziki zao za kila siku.

Balozi Seif aliwahakikishia Wananchi hao kwamba lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika hatua ya baadae ya Bara bara hiyo ni kuikamilisha katika kiwango cha lami ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akikagua jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kiombamvua lililojengwa na Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff kutekeleza ahadi za kusaidia huduma na Miradi ya Kijamii.Wa kwanza kulia ni Mshauri muelekezi wa Hoteli hiyo ya Sea Cliff ambae pia ni msimamizi wa Ujenzi wa jengo hilo la Skuli Nd. Yassir De Costa.
Balozi Seif mbae pia ni Mwakilisihi wa Jimbo la Mahonda akikagua Bara bara ya Kinduni iliyopitia Kichungwani na kuelekea Kitope iliyojengwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar katika kiwango cha kifusi.
Balozi Seif akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Kinduni na Kichungwani mara baada ya kuikagua bara bara iliyomo ndani ya Kijiji chao.Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahme Salum na Mbunge wa Viti Maalum Mh.Angelina Adam Malembeka.
Mzee Juma Abdulrahman wa Kijiji cha Kichungwani anayesumbuliwa na maradhi ya macho na Miguu akitoa shukrani kwa niaba ya wanakijiji wenzake mbele ya Balozi Seif kwa hatuanjema iliyochukuliwa na Serikali kuijenga bara bara yao.Picha na – OMPR – ZNZ.


TAARIFA YA MSIBA WA INNOCENT WAPALILA

$
0
0

Familia ya Mzee Meinuf Wapalila na Victoria Bernard Ngowi wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao Innocent Wapalila kilichotokea Leeds, Uingereza tarehe 17/02/2017.

Msiba na utaratibu wa kusafirisha mwili na mazishi unafanyika Mbezi Beach jijini Dar es salaam mtaa wa Almasi nyumba namba 7.

Kwa uingereza, msiba upo nyumbani kwa marehemu Innocent, 18 Bayswater Mount, LS8 5LP, Leeds.

Gharama za kusafirisha mwili wa mpendwa wetu ni kubwa, ukiwa kama ndugu na rafiki, tunaomba mchango wako wa hali na mali utumwe kwa dada wa marehemu Bi Mariaconsolata Wapalila kwa namba ya M-Pesa 0754 270 433 au Airtel Money 0787 376 278 au akaunti ya benki namba 10300101003 (BANK OF AFRICA).

Asante sana na mungu awabariki,
‘Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe’   

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AOMBA BUSARA ZA MASHEHE NA WAZEE KATIKA KULIONGOZA JIJI HILO

$
0
0
Meya Isaya ametoa kauli hiyo jiji hapa leo wakati wa maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume wao Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwama jiji la Dar es Salaam bila dua za waze, mashehe na viongozi wote wadini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto zilizopo. 

“ Najua changamoto zilizopo kenye jiji hili ni nyingi wazee wangu naomba mnisaidie sana, peke yangu siwezi, dua zenu na ushauri wenu ndio unaweza kunisaidia mimi kufanya mambo mazuri” na wananchi wakaishi kwenye mazingira wanayopenda” amesema Meya Isaya.

Leo hi mimi nikiwa na kiburi kweu kwa ajili ya madaraka haya ambayo nyie ndio mlionipa, sitaweza kutatua changamoto hata moja,zipo changamoto za kimiundombinu ya elimu, na nyingine, ambazo zote zinahitaji kupatiwa ufumbuzi, nawaombeni saa waze wangu mnipe baraka zenu” aliongeza.

Akizungumzia suala la maadili Meya Isaya amesema wazazi hawana budi kuwasaidia walimu, serikali na viongozi kwa ajili ya malezi bora hususani wakiwa shuleni.

Amesema ni jambo la ajabu na mtihani mkubwa kwa walimu ikiwa mzazi atakuwa mstari wa mbele kumnunulia mwanae simu hali yakuwa yupo masomoni jambo ambalo linafanya ashindwe kuzingatia masomo na badala yake kushinda kwenye mitanda ya kijami.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akisalimiana na Mwenyeji wake,Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. 

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro. 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa umakini sherehe hizo.
Kikundi cha Al Farouq kikipiga dufu wakati wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

NEWS ALERT: WAZIRI MKUU AKERWA MBOLEA YA MINJINGU KUPEWA LEBO YA KENYA, Ataka waandike barua ya kuomba radhi kwa Rais Magufuli

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini. 
Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.
Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa. 
“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.
“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?” 
Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.
Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja. Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa. 
“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.
“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”
“Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza. 
Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi. 
Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akikagua mgodi wa kiwanda cha mbolea cha  Minjingu wakati alipotembelea kiwanda hicho mkoani Manyara, Februari 19, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabala ya kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara kuanza awamu ya pili ya ziara yake mkoani humo Februari 19, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa ManyaraDkt. Joel Bendera. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WACHIMBAJI WADOGO KUMILIKISHWA ENEO LA STAMICO, BUHEMBA

$
0
0
Serikali imesema itatoa eneo linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Buhemba, Mkoani Mara kwa wachimbaji Wadogo wa Madini baada ya kufanyika kwa tathmini  na taratibu za kumilikishwa eneo ili wachimbaji hao wafanye shughuli hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo tarehe 18 Februari,2017, wakati wa ziara yake katika mgodi huo ili kuangalia shughuli za uokoaji zinazoendelea katika mgodi huo, kufuatia  ajali ya kufukiwa na kifusi kwa Wachimbaji 18  iliyotokea tarehe 13 Februari,2017, ambapo wachimbaji 13 waliokolewa siku hiyo hiyo


Prof. Muhongo  amesema kuwa, wachimbaji hao hawakuwa na leseni wala vibali halali vilivyotolewa kwao  kufanya shughuli za utafutaji dhahabu na kwamba eneo hilo linamilikiwa kisheria na STAMICO kwa leseni  PL N0. 7132/2011, na kuongeza kuwa, wachimbaji hao walivamia eneo hilo ambapo ni kosa kisheria na wanatambulika kama wavamizi.


Ameongeza kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo hilo zilifungwa tangu mwaka 1971 ambapo awali eneo hilo lilikuwa chini ya wakoloni kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT), Kampuni ya Meremeta na baadaye kuwa chini ya umiliki wa STAMICO.


Aidha, amezuia shughuli zote za uchimbaji kufanyika katika eneo hilo na kusema kinachofanyika sasa ni kuutafuta mwili wa mchimbaji mmoja ambaye bado haujatolewa. ''Hadi sasa wachimbaji 15 wamekwisha okolewa, bahati mbaya wawili walitolewa wamefariki na sasa tuendelee na zoezi la kutafuta mwili uliobaki,"ameongeza Prof. Muhongo.
 Mmoja wa wachimbaji waliokolewa katika ajali ya kifusi akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jinsi ajali hiyo ya kufikiwa na kifusi wachimbaji 18 ilivyotokea. Katikakti  anayesikiliza ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje.

 Mmoja wa wachimbaji wadogo akishuka chini ya shimo la kuingilia katika mgodi kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wachimbaji 18 katika eneo la Buhemba mkoani Mara.

 Sehemu ya Wachimbaji wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa ziara yake katika mgodi wa Buhemba  unaomilikiwa na STAMICO.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wachimbaji wadogo katika eneo la Buhemba ambapo ajali ya wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi tarehe 13 Februari,2017.



Usikose, Jukwaa La Diaspora Na Wajasiriamali Pasaka Hii...!

Article 3

MAGAZETI YA LEO FEBRUARY 20,2017


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKERWA NA KIWANDA CHA MBOLEA CHA MINJINGU KUWEKA MBOLEA KWENYE MIFUKO INAYOONYESHA KUWA MBOLEA YA KIWANDA HICHO IMEZALISHWA KENYA

$
0
0


*Ataka waandike barua ya kuomba radhi kwa Rais Magufuli
*Aagiza Waziri wa Biashara aje na timu yake

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.

Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.

“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.

“Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”

Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.

Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.

“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”

“Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.

Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.

Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.

 
  Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa  kiwanda hicho  kuandika barua ya kumuaomba radhi  Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho.  Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara ikiwa na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya. Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari 19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Washindi wawili wa kampeni ya Akaunti ya Malengo ya NBC wajishindia Toyota Hilux double cabin mpya.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi  (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya Kampeni ya akaunti ya  Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu.  Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo.
 Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi  (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya Kampeni ya akaunti ya  Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu.  Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo. 
Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo katika droo iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.   Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka 2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi,  Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na aliyesimama ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bakari Maggid. 

Mbunge wa Mkuranga aongoza tukio la kuchangia damu Dar es Salaam

$
0
0
Mgeni rasmi wa kongamano la kuchangia damu lililoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga akizungumza umuhimu wa kila Mtanzania kujitolea damu ili kuinusuru jamii yake. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

MBUNGE wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, mwishoni mwa wiki aliongozana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), lililofanyika katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo, watu mbalimbali walishiriki katika uchangiaji damu kama sehemu ya kutatua changamoto ya upungufu wa damu kwa wenye uhitaji, wakiwamo akina mama wajawazito, ajali za barabarani na majanga mengine.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, H.E Jasem Al Najem akitolewa damu katika tukio la kuchangia damu lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika uchangiaji huo, Mbunge Ulega alisema kwamba jukumu la kuchangia damu linamuhusu kila Mtanzania, huku akiwataka watu kujenga mazoea ya kujitolea damu ili kuondoa upungufu wa damu.

Alisema kwamba mahitaji ya damu kwa nchi yetu ni makubwa, hivyo amefarijika kwa kupata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi sambamba na kuongoza tukio hilo la uchangiaji wa damu, akiamini amejitolea jambo la msingi na la lazima.
Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega, akizungumza na Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem wakati wanatoa damu kwenye tukio lililoandaliwa na TYPF mwishoni mwa wiki.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem wakati anapima uzito dakika chache kabla ya kutoa damu katika tukio lililofanyika mwishoni mwiki.

“Nimefarijika kwa mwaliko wenu na jinsi nilivyoshiriki juu ya utoaji wa damu nikiamini kwamba naweza kusaidia wenye uhitaji wanapokuwa Hospitalini ambapo juu ya damu inayohitajiwa kwa kiasi kikubwa ili kuwanusuru wagonjwa wetu,” Alisema Ulega na kuwataka TYPF kuelekea jimboni kwake Mkuranga kwa ajili ya kuandaa matukio ya aina hiyo ili waendeleze juhudi zao za kuchangia damu.

Naye Balozi Najem alisema kuchangia damu ni sehemu ya malengo yake binafsi pamoja na ofisi yake, hivyo yupo tayari kusaidia kwa namna moja ama nyingine ili kuwasaidia watu wote wenye uhitaji wa damu nchini Tanzania.

“Nimejiwekea utaratibu wa kujitolea katika jamii yakiwamo haya mambo ya damu, hivyo pamoja na kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo pamoja na mliohudhuria kuja kutoa damu, naomba niwaambie bado nipo tayari kujitolea wakati wowote itakapohitajika,” Alisema Balozi Najeem.

Awali Mtendaji Mkuu msaidizi wa TYPF, Swalehe Jabri, aliwashukuru waliojumulika nao kutoa damu, akisema wamefanya jambo kubwa linalohitaji kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo, akiamini utaratibu huo umelenga kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwenye hospitali nchini.

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BARAZA LA WATOTO SHEHIA YA KIEMBESAMAKI

$
0
0

 Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizindua Baraza la Watoto wa Shehia ya Kiembesamaki katika sherehe zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki. 
Baadhi ya watoto wa Shehia ya Kiembesamaki wakimsikiliza Mwakilishi wao Mahmoud Thabit Kombo  wakati wa uzinduzi wa Baraza lao kwenye sherehe zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki Wilaya Magharibi ‘B’.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
 Katibu wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Zulfa Mohd Masanja akisoma risala wakati wa sherehe za ufunguzi wa Baraza hilo  zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi ‘B’. 
 Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Baraza hilo, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae pia ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia maonyesho ya watoto wa Baraza hilo (kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya watoto Zanzibar  Mundhir Hamdan Said. 
 Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Bimkubwa Haji Hassan akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Baraza la watoto la shehia hiyo.

BARAZA LA KUSIMAMIA MFUMO WA UTOAJI LESENI ZANZIBAR (BLRC) LATOA MAFUNZO KWA KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA FEDHA, BIASHARA NA KILIMO.

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji wa Leseni Zanzibar Vuai Mussa Vuai akimkaribisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali kufungua mafunzo ya siku moja ya Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyofanyika Ofisi ya Baraza Malindi, Mjini Zanzibar. 
 Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akifungua mafunzo ya siku moja ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyoandaliwa na Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni katika Ofisi yao iliyopo Malindi Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Waziri wa Fedha Balozi Amina Salum alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ofisi ya Baraza hilo Malindi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Yussuf Hassan Iddi ambae ni muwakilishi wa Jimbo la Fuoni akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kufungua mafunzo ya siku moja ya Kamati hiyo.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images