Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live

UNDP YAJENGA VYOO VYA SHILINGI MILIONI 510 KUSAIDIA USAFI KILIMANJARO

$
0
0
Mwakiishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania ,Alvaro Rodriguez,akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi.

Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.

Wakati wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.

Katika kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na UNDP Tanzania ilisaidia mkoa wa Kilimanjaro  Sh Mil 510 kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi 10 ili kusaidia kuezesha usafi kwa wanafunzi na walimu wao.

Hadi kufikia sasa jumla ya matundu 178 yamejengwa katika shule 10 ambapo matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya wavulana.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mwakilishi makzi wa UNDP.Alvaro Rodriguez alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwepo kati ya serikali ,wao na shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha mazingira ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.

Alisema kutokuwepo kwa mazingirabora ya usafi ni chanagamoto kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.

Rodriguez alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo wanafunzi ,walimu na walezi sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba wanatoa elimu bora .

“Watoto wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za mahudhurio shuleni na wakati huo huo masUala ya usafi yatakuwa yameboreka na hivyo kuwa na wanafunzi na familia zenye siha njema.”alisema Rodriguez.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umja wa MAtaifa kuendelea kutoa msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya dunia yanayohusiaa na usafi ,mazingira na maji safi yanafanikiwa ifikapo mwak 2030.

Naye mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba pamoja n kuishukuru UNDP kwa kazi nzuri waliyofanya pia alizitaka jumuiya za maeneo yaliyojengewa vyoo kuiliki msaada huo kwa kuhakikisha wanaitumia na hivyo kuisadia kufikia malengo ya dunia 2010.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakizindua rasmi vyoo vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi za kufadhiliwa na UNDP.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alavaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakitizama vyoo vilivyojengwa na UNDP katika shule ya Msingi Mandela.


“Operesheni Lipa Kodi ya Pango la Ardhi” yaendelea

$
0
0
Ikiwa Operesheni Lipa Kodi ya Pango la Ardhi inaendelea, ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya pango la Ardhi huku ikiendelea na kuhabarisha Umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, katika vifungu Na. 49 na 51 ambavyo vinadhihirisha ruhusa ya mmiliki kufutiwa umiliki wa ardhi kama mmiliki hatazingatia kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.
Kwa upande wake; Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb), amekuwa akifanya ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi sehemu mbalimbali nchini.

Katika picha ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb) akikagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi sambamba na kuhakiki kumbukumbu za umiliki wa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza. Alioambatana nao ni Maafisa Ardhi na Afisa TEHAMA.

MBUNGE VITI MAALUMU IRINGA AENDELEA NA ZIARA KATIKA WILAYA YA MUFINDI

$
0
0
MBUNGE wa Viti Maalum Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Rose Tweve ameendelea na ziara zake katika Wilaya za mkoa huo ambapo mwishoni mwa wiki hii alitembelea kata ya Wambi iliyipo kwneye wilaya ya Mufindi.

Rose katika moja ya ahadi zake wakati wa kampeni aliweza kuwaahidi wanawake wa mkoa huo kuwainua kiuchumi hususani katika kuwawezesha kwa kuwapatia fedha na pia kuwashauri kujiunga na vikoba na pia kuhakikisha jumuiya za wanawake zinakuwa imara.

Akiwa katika kata ya Wambi, Rose amezungumza na wakina mama wa Jumuiya ya wanawake wa Mkoa wa Iringa (UWT) na kuwataka kujiingiza katika masuala ya ujasiriamali ili kuweza kujiinua kiuchumi hasa katika kujiunga na vikundi vya Vikoba.

Rose amewaambia kuwa, wanawake wanatakiwa kubadilika na kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume kwani watakapojiwezesha kiuchumi wataweza kuondokana na utegemezi ambapo pamoja na hayo aliweza kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwenye jumuiya hiyo.

Wanawake wa kata ya Wambi wametakiwa kuwapa fursa sawa watoto wa kike na kiume katika suala la elimu kwani itakuwa ni moja ya fursa ya kuwawezesha kielimu.

Katika ziara hiyo, Rose aliongozana na Diwani wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando ambapo katika mkutano huo na wakina mama wa kata yake aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) na kuwataka wajishughulishe na kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume.
 Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akizungumza na wanawake wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake endelevu ya kati ya Wambi Wilaya ya Mufindi.
  Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akisalimiana na Mtendaji wa kata ya Wambi Veronica Masenga akiwa pamoja na Diwani wa Viti Maalum Asha Nyenza (katikati) na Diwani wa wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando wakati wa ziara kwenye kata hiyo.
  Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akikabidhi fedha kiasi cha Shilingi cha laki sita (600,000) kwa moja ya akina mama wa  wanawake wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Iringa, kulia ni Diwani wa wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando ambae alishiriki kwenye ziara hiyo na wa kwanza kushoto ni Diwani wa 

NEWS ALERT: MBOWE AITIKIA WITO POLISI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameitikia wito wa Jeshi la Polisi mchana huu, katika kituo cha Polisi kati, Jijini Dar es salaam. tayari kwa mahojiano juu ya tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA UJERUMANI WATEMBELEA TIC

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akizungumza wakati wa mkutano wake na ujumbe wa baadhi ya wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani, waliotembelea Kituo hicho ili kuona fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini. 

 Sehemu ya ujumbe wa wafanyabiasha kutoka nchini Ujerumani, ukiwa katika Mkutano na uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kuzungumzia fursa mbalimbali za uwekezaji nchini.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji wa TIC, Zacharia Kingu akizielezea fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini wakati wa Mkutano na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani, waliotembelea Kituo hicho ili kuona fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini. 

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE BABATI NA MBULU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017. Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafa, Mama Sanka baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya wilaya ya Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MDAU JOSINA NCHIMBI ALAMBA NONDOZZZ YAKE OUT

$
0
0
Mdau Josina Nchimbi kwa furaha akiwa ameshika kitabu chenye majina ya wahitimu wa Degree mbali mbali 2017 katika chuo Kikuu Huria Tanzania ambapo Bi Josina amehitimu Shahada ya Uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera. HONGERA SANA JOSINA.
Mdau Josina Nchimbi pichani (wapili kutoka kushoto) akiwa na wahitimu mbali mbali kwenye mahafali ya 32 ya Chuo kikuu Huria yaliyofanyika Mkoani Njombe.
Mdau Josina Nchimbi na ma uncle zake wakiwa wenye furahaa baada ya Josina kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Elimu ya Utawala, Mipango na Sera, Chuo Kikuu Huria kwenye mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika Mkoani Njombe.

TEA YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU NA KAMPUNI YA SUNSHINE

$
0
0
MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.


Kwa mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku akibainisha kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya Sunshine.


“Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.


Akiishukuru TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.

SERIKALI YATOA TAMKO KWA BODI YA LIGI, YATAKA AMANI KATIKA MECHI YA JUMAMOSI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Serikali imewataka bodi ya ligi kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua  waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri sheria 17 za soka kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa ili kuzuia athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo uharibifu wa mali za uwanja.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa michezo kutoka Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Yusuph Singo leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni katika maandalizi ya kuelekea mechi ya watani wa jadi na kuwaasa viongozi wa bodi ya ligi kufanya maamuzi sahihi ili kuepusha vurugu zitakazoweza kujitokeza.

Singo alisema kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba mosi mwaka jana na kushuhudiwa vurugu kubwa zilizopelekea viti 1781 kuvunjwa, zilitokana na maamuzi mabovu ya waamuzi wa mchezo huo.

“Tunaitaka bodi ya ligi kupanga waamuzi wazuri kwenye mchezo huu kwakuwa unavuta hisia za watu wengi na pia tunawaomba mashabiki kuwahi mapema na kutojihusisha na vurugu zozote kwani ulinzi utakuwa wa kutosha” alisema Singo.

Kwa upande mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Inspekta Hashim Abdallah alisema ulinzi utaimarishwa vya kutosha na wale wote watakaovunja sheria watachukuliwa hatua stahiki ukizingatia uwanja wa huo umefungwa kamera maalum kwa ajili ya ulinzi.

“Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia timu zao kwa amani lakini watakao jihusisha na vurugu tutawashughulikia ipasavyo” alisema Inspekta Hashim.

Wakati huo huo mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amevitaja viingilio hivyo kuwa viti vya bluu na kijani itakuwa shilingi 7,000 viti vya ‘orenji’ itakuwa shilingi 10,000, VIP B na C itakuwa shilingi 20,000 huku VIP A ikiwa ni shilingi 30,000.

Mbali na hilo, uongozi wa uwanja huo uliweza kuwapeleka waandishi katika chumba chenye mitambo ya kamera za ulinzi (CCTV) ambapo takribani uwanja mzima kuna kamera 119 zilizozunguka kila sehemu.
Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Yusuph Singo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura.
Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Inspekta Hashim Abdallah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa na kutoa rai kwa mashabiki wa timu hizo kuja kwa ustaarabu.
Waandishi wa habari wakiwa wanapata maelekezo ya namna kamera zilizopo uwanjani zinavyotumika.

INTRODUCING: KAMOBA - LADY JAYDEE Ft. HAMOBA

Makamba apigilia msumari pombe za viroba

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira , January Makamba amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo pombe inapatikana kirahisi.

Kauli hiyo inatokana na agizo la waziri mkuu juu ya kuzuia matumizi ya  pombe  za mifuko ya Plastiki kutokana na adhari za pombe katika jamii.
Makamba ameyasema hayo leo wakati akitangaza juu ya uzuiaji wa viroba katika mifuko ya plastiki, amesema kuwa kuanzia Machi moja ni marufuku kwa  pombe za mifuko ya plastiki ni mwisho na wataofanya biashara hiyo watachukuliwa hatua.

Amesema kuwa wanaanda kanuni ambazo zitabana biashara hiyo kutokana na kufanywa kwa muda mrefu bila serikali kupata kodi biashara ya pombe katika mifuko ya plastiki.

Makamba amesema kuwa biashara hiyo itakuwa ngumukwa watengenezaji kutokana na masharti  yaliyokuwepo kwa wale ambao wataomba biashara hiyo.Aidha amesema  kuwa kamati za ulinzi wilaya kufanya operesheni katika maeneo yao ikiwa katika mipaka ambayo pombe za  viroba zinaweza  kuingia.

Makamba amesema kuwa pombe za viroba inatakiwa kuwa historia na kuanza kuwepo kwa pombe katika chupa za plastiki au kioo kwa milimita 250 .
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo Richard Muyungi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo Richard Muyungi.

WAZIRI MKUU: HOSPITALI YA HAYDOM KUPANDISHWA HADHI

$
0
0



Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina kipingamizi na wazo la kuifanya hospitali ya rufaa ya Haydom kuwa ya kanda kwani hatua hiyo itaupunguzia mzigo Serikali.

“Serikali hii ni sikivu, na kuifanya hospitali hii kuwa ya kanda ni kazi ndogo. Kwa hiyo nitamleta Waziri wa Afya aje awaongoze kusimamia vigezo vya kuifanya hospitali hii iwe ya kanda,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Februari 20, 2017) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Haydom kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kata.

"Serikali haina kipingamizi na wazo lenu, cha msingi ni vigezo muhimu vifuatwe. Kwa hiyo, nitamleta Waziri wa Afya awasaidie kuangalia vigezo," amesisitiza.

“Kama vigezo havipo, tushirikiane kuvikamilisha kwa sababu uwepo wa hospitali hii kwa hadhi ya kanda kunaisadia Serikali kutokana na nafasi yake kijiografia,” amesema Waziri Mkuu

“Nia yetu ni kupunguza gharama kwa mgonjwa anayelazimika kutoka Simiyu hadi Bugando (Mwanza) au kutoka Arusha hadi Muhimbili (Dar es Salaam).  Hapa ni katikati na nimearifiwa kuwa wagonjwa kutoka mikoa mitano ya Tabora, Simiyu, Arusha, Singida na Manyara wanafika hapa kupatiwa matibabu,” amesema.

Amesema Serikali imepokea maombi kwa ajili ya watumishi wanaotakiwa kwenye hospitali hiyo na kwamba hivi karibuni itaajiri watumishi kati ya 5,000 hadi 6,000 wa sekta ya afya peke yake. “Tumekwishaanza kuajiri, tumeanza na sekta ya elimu kwa kuajiri walimu 4,693 ambao wote ni wa fani ya sayansi. Na sekta inayofuata ni ya afya, kwa hiyo hao watumishi 90 wanaohitajika watapatikana kwenye kundi hilo hilo,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

DC SAME AAGIZA WANAFUNZI KUWA NA MITI YA KUITUNZA

$
0
0
Na Mathias Canal

Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule amewaagiza walimu wakuu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kusimamia zoezi la upandaji miti kwa kumkabidhi kila mwanafunzi mti mmoja ambao atautunza katika kipindi chake cha masomo.

Dc Senyamule ametasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilayani humo kilichohudhuriwa na walimu wote wa shule za msingi na sekondari, Waratibu elimu, Maafisa Tarafa, Wazazi, Wanafunzi wawakilishi pamoja na baadhi ya Viongozi wa dini. 

Kikao hicho kilichokuwa na lengo la kukubaliana na kupata namna bora ya kuboresha elimu na kiwango cha ufaulu Wilayani Same, Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo kwa namna maalumu kwa ajili ya wanafunzi kufundishwa kwani mafanikio ya jitihada zao pekee katika kujisomea na kufundishwa darasani haitoshi bali wanahitaji kuongezewa msukumo na utaalamu zaidi kwa masomo ya ziada.

“Sote hapa kwa umoja wetu ni lazima tutambue kuwa matokeo bora ya wanafunzi waliopo darasa la saba, wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita yapo mikononi mwa walimu hivyo njia bora ni kutatua matatizo yanayowakabili walimu ili tuweze kufikia lengo” Alisisitiza Mhe Senyamule

Ameeleza kuwa endapo Changamoto za makundi yote zitatekelezwa kwa kufuata utaratibu ikiwemo kila mmoja kutumia nafasi yake ipasavyo katika kufuatilia mwenendo wa wanafunzi kwa kuanzia Walimu, Serikali, Wazazi, na Wanafunzi Wilaya hiyo itakuwa na matokeo makubwa katika matokeo yajayo.

Staki alisema kuwa Wilaya ya Same imeanza imeanza kukua kielimu kupitia matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwani Wilaya hiyo imeshika nafasi ya 62 kati ya Halmashauri 184 ambapo kwa Mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 103.Aidha katika matokeo ya kidato cha pili Wilaya ya Same imeshika nafasi ya 37 kati ya 184 kwani mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 47.

Pia amewataka viongozi wote katika kada mbalimbali kutumia vyema uongozi wao kwa kuwatumikia wananchi huku akiwasihi kutumia lugha nzuri pindi wanapozungumza nao kwani kiongozi yeyote atakayetumia lugha mbaya anapaswa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo. 

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Same amepinga vikali matumizi ya Dawa za kulevya ambapo amesema kuwa kwa Wilaya hiyo baadhi ya wananchi wake ni wazalishaji wakubwa wa zao aina ya Mirungi ambalo pia limepelekea vijana wengi kutumia huku wakijiweka kando na elimu kwa kuamini kulima zao hilo sehemu ya mafanikio yao ya haraka.

Dc Staki amesema uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea na oparesheni ya kuteketeza matumizi ya mirungi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matumizi ama uuzaji wa zao hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule

AWAMU YA PILI YA MAFUNZO YA WAJASILIAMALI WANAWAKE WA MKOA WA DAR ES SALAAM YALIO CHINI YA TAASISI YA MANJANO YAENDELEA

$
0
0
Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila Akitoa Mada kwenye Mradi wa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali kupitia Taasisi ya Manjano Foundation. Mafunzo hayo yalianza wiki iliyopita kwa lengo la kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania kupitia bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano. Washiriki wataweza kujisimamia na kujikita vizuri kwenye biashara ya vipodozi na kujua mbinu mbalimbali za biashara kwa lengo la kumjengea uwezo mwanamke wa Kitanzania.
Image may contain: 3 people, people sitting and text
Washiriki wa Mafunzo ya Usajiriliamali na Urembo yalio chini ya Manjano Foundation wakisiliza kwa makini mada mbalimbali kuhusu mafunzo hayo ya kuwapa uwezo wa kuthubutu kufanya biashara, kujisimamia na kujua mbinu mbalimbali za biashara.Image may contain: 5 people, people standing
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Washiriki walionufaika na Mradi huo.
Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili uwezo wake ikiwa pamoja na kuisaidia jamii yake iliyomzunguka. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano.

Awamu ya Pili ya Mradi huu Ulizinduliwa na waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage mnamo tarehe 14 Februari 2017, ambapo alisema amefurahishwa sana wwa mwanamke wa Kitanzania kuzindua mradi unaowawezesha wanawake kujiongezea kipato na kujiajiri hasa kwenye sekta ndogo ya Urembo yenye fursa kubwa ya kukua.

VITUO VINAVYONYAYASA WAGONJWA VILIVYOPO NDANI YA MPANGO WA HUDUMA YA AFYA (NHIF), KUFUTIWA USAJILI VIKIBAINIKA

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

MWENYEKITI wa Bodi ya mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF) Anne Makinda amesema kuwa kituo chochote kilichosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wateja wa mfuko wa bima ya afya, ambacho kimeajiri wahudumu wenye mfumo wa unyanyasaji kwa wagonjwa ikiwemo Lugha za kejeli kwa wateja vitaondolewa kwenye mpango wa huduma ya afya.

Makinda alisema hayo leo wakati wa mkutano wa wadau wa NHIF na CHF Mkoani Kagera katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera Mjini Bukoba.

"Hivi wewe mtoa huduma wa afya unapotoa lugha ya kejeli na vitisho,matusi kwa wagonjwa unapata faida gani?,unapata fedha kiasi gani?sasa naagiza vile vituo ambavyo tumevisajiri kutoa huduma zetu ambavyo bado vinaendekeza mfumo wa kunyanyasa wagonjwa, sasa tunasema basi hatuwezi kuvumilia kinachofuata kuwafuatia sajili alisema Makinda.

Aidha aliwaagiza wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kuweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanaondoa kero hiyo haraka iwezekanavyo kwani watu wakijiunga na bima lengo ni wapate huduma stahiki ikiwemo mapokeo mazuri jambo ambalo linampa mgonjwa faraja hata kabla ya kupata dawa.

Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Anna Makinda akifungua mkutano wa wadau wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Benard Konga akiongeo na wadau wa mfuko huo(hawapo pichani)wakati wa kikao cha wadau wa mfuko wa NHIF kilichofanyika leo Mkoani Kagera

Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akieleza changamoto na mafanikio ya mfuko katika Mkoa wa kagera kwa wadau wa mfuko wa Bima. 


Baadhi ya wadau wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa bima ya afya na viongozi kutoka makao makuu ya mfuko huo.


KINANA AKUTANA NA BALOZI WA UINGEREZA HAPA NCHINI LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo, leo Feb 20, 2017. 
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, wakifurahia jambo, baada ya kuketi kwa ajili ya kuanza mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Feb 20, 2017.
 Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga ambaye alihudhuria mazungngumzo hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya mazungumzo yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 20, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpugia mkono wa kwa heri, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, wakati akiondoka katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 20, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga. 

JWTZ YAPANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO IKIWEMO GOFU NCHINI .

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya kanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati akifunga Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.

Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa kujenga Viwanja vya kanda na Lugalo kuwa na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la Michezo kwa Wananchi.

Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya Gofu lakini bado wataendeleza Uwanja wa Lugalo pale ambapo watangulizi wake wameishia na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.

Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya  Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mrisho Sarakikya wakati akishiriki Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mshindi wa kundi la Wanawake wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).


MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MBULU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimiana wanakwaya wa Shule ya Sekondari ya Singiland wilayani Mbulu wakati alipowasili kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu kuhutubia Mkutano wa hadhara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu mkoani Manyara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

Mahakama ya Tanzania yatarajia kukamilisha miradi ya ukarabati na ujenzi wa majengo yake 70

$
0
0
Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha miradi ya ukarabati na ujenzi wa majengo 70 ya Mahakama katika kipindi cha miaka miwili ili kusogeza karibu huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

Ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi, majengo ya Mahakama kuu katika mikoa tisa yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili, Mahakama za Mikoa sita zitajengwa ndani ya miezi 6-12 wakati Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 zinatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2017.


Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma alisema Mahakama kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo (TBA), Chuo Kikuu cha Ardhi, Baraza la Ujenzi la Taifa, Benki ya Dunia na wadau wengine wanaendeleza na kukamilisha miradi ya ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa tisa nchini.

Aliitaja mikoa ambayo majengo ya Mahakama Kuu yatafanyiwa ukarabati na mengine kujengwa ndani ya kipindi cha miezi 24 kuwa ni Mbeya, Kigoma, Mara, Tanga na Dar es salaam. Mikoa mingine ni Arusha, Morogoro, Mwanza na Dodoma. Alisema nia ya Mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila Mkoa ili kusogeza huduma za Mahakama kwa wananchi.

“Tunapaswa kuwa na Mahakama Kuu 26 kwenye kila ngazi ya Mkoa, kwa sasa tunazo Mahakama Kuu kwenye kanda 14 tu”, alisema Kaimu Jaji Mkuu. Aidha, mikoa 12 isiyokuwa na Mahakama Kuu ni pamoja na Songwe, Katavi, Njombe, Lindi, Kigoma na Mara. Mikoa mingine ni Singida, Morogoro, Pwani, Simiyu, Geita na Manyara.

Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa wakati huo huo, Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi katika mikoa sita ya Manyara, Geita, Simiyu, Njombe, Katavi na Lindi katika kipindi cha kati ya miezi 6 na mwaka mmoja.

Kwa upande wa Mahakama za Wilaya na zile za Mwanzo, Kaimu Jaji Mkuu alisema wanakusudia kujenga Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 ambazo zitakamilika ifikapo Desemba 2017.

Alisema hatua hii ya ujenzi wa Mahakama hizi si tu kwamba itasogeza karibu huduma za Mahakama kwa wananchi bali pia italeta mabadiliko makubwa ya miundombinu ya mahakama na kuweka historia ya upatikana wa miundombinu kwa wingi na kwa kifundi kifupi.
Viewing all 109973 articles
Browse latest View live




Latest Images