Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

HAPPY BIRTHDAY

0
0
TIMU YA VIJIMAMBOBLOG NA WA DAU WAKE WANAKUTAKIA KHELI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA.


MWANDEGE FC, LUKANGA FC ZAFANIKIWA KUTINGA HATUA YA NUSU FAINALI ULEGA CUP

0
0
Timu ya Mwandege kutoka kata ya mwandege na Lukanga fc kutoka kata ya Lukanga zimefanikiwa kuingia hatua ya Nusu fainali baada ya kuzisambaratisha timu ya Mkamba ya kata ya mkamba pamoja na  timu ya Mbezi fc ya kata ya Mbezi.



Katika mechi ya kwanza, timu ya Mkamba ndio iliyotangulia kufunga timu ya Mwandege katika kipindi cha kwanza bao lililofungwa na ,Abdallah Matope na hadi wanakwenda mapimziko Mkamba walikuwa wanaongoza kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika ya 15 ya kipindi hicho timu ya Mwandege walisawazisha goli kupitia Salumu Mnyasi waliendelea kushambuliana lakini Mwandege walionekana kutakata zaidi ambapo dakika ya 25 Mussa Charles aliipatia Mwandege FC goli la pili.

Hadi dakika 90 zinamalizika Mwandege waliibuka na ushindi wa goli 2-1 na kutinga nusu fainali.

Katika mechi ya pili Lukanga FC ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Mbezi kwa goli 3-0 yote yakifungwa kipindi cha pili.
Mchezo huo ulishuhudiwa na watazamaji wengi wakiongozwa na mheshimiwa Mbunge,Abdallah Hamis Ulega.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega  akiwa anashuhudia moja ya mtanange wa kombe la Ulega Cup linaloendelea Wilaya ya Mkuranga.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Mwandege na Mkamba FC katika mashindano ya Ulega CUP mchezo uliopigwa jana.
Wachezjai wa Mwandege Fc wakipambana na wachezaji wa Mkamba Fc kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika jana, Mwandenge walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1.
Wachezaji wa Lukanga FC NA Mbezi Fc wakipambana katika mchezo wa robo fainali ambapo Lukanga ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Mbezi kwa goli 3-0 yote yakifungwa kipindi cha pili.Picha na Emmanuel Massaka.

ALICHOKISEMA SHABIKI WA NGAYA FC YA COMORO KUFUATIA DROO YA YANGA

Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya hazina ya michezo nchini

0
0
Na Eleuteri Mangi, WHUSM

Wakurugenzi wa halimashauri wameaswa kutumia fursa uwepo wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo mkoani Mwanza kwa kuwaruhusu walimu wa michezo wengi zaidi kuongeza ujuzi wao ili kuinua sekta ya michezo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipotembelea chuo hicho kujionea namna chuo hicho kinavyoendesha programu zake katika jitihada za kuendeleza sekta ya michezo nchini.

“Nawapongeza viongozi, wafanyakazi na wanachuo kwa juhudi mnazofanya katika kukiimarisha chuo hiki ambacho ni hazina ya michezo mbalimbali nchini, mmepiga hatua kubwa ya kimaendeleo” alisema Prof. Ole Gabriel.

Chuo hicho kimekuwa msingi wa kujenga wataalam wa michezo nchini kwa lengo la kuimarisha mahusiano na maendeleo ya kielimu kijamii, kielimu, kikazi na kiuchumi kwa kuzishirikisha halmashauri zote nchini.

Katika kuenedeleza michezo nchini, Prof. Ole Gabriel amewaambia viongozi wa chuo hicho kuwa wawe wabunifu kwa kuongeza programu nyingi zaidi chuoni hapo ambazo zitaongeza kipato na tija kwa chuo, wanachuo, wananchi wanazunguka chuo na taifa kwa ujumla.

Aidha, Prof. Ole Gabriel ameongeza kuwa ni vema chuo hicho wapange na kuanzisha mafunzo ya muda mfupi ili kurahisishs watu kupata elimu ya michezo na kuongeza tija katika utendaji kazi.

Kwa upande wake Mkuu wa chuo Richard Mganga akitoa taarifa yake kwa Katibu Mkuu mwenye dhamana ya michezo Prof. Ole Gabriel alisema kuwa chuo hicho kimepata Ithibati kamili mwaka 2015 na kinafundisha kozi ambazo zinafuata mitaala iliyopitishwa na Baraza la Taifa La Elimu ya Ufundi (NACTE).

Mkuu huyo aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza chuo kimekuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili kwa kozi za Stashahada ya Utawala na Uongozi katika Michezo, Stashahada ya Elimu ya Michezo, Stashahada ya Ukocha tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na wanafunzi mwaka moja tu.

Hali hiyo imefanya idadi ya wanachuo mwaka huu wa masomo 2016/2017 kuongezeka ambapo hadi sasa wapo wanachuo 99 ambapo mwaka wa kwanza idadi yao ni 46 na mwaka wa pili wakiwa 53.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa pili kushoto) akiwasili Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi mwishoni wa wiki kujionea namna chuo hicho kinavyoendesha programu zake katika jitihada za kuendeleza sekta ya michezo nchini. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa chuo Richard Mganga na wa kwanza kulia ni Rais wa Serikali ya wananchuo Cletus Mutakyawa.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa nne kushoto aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo mkoani Mwanza wakati wa ziara ya kikazi mwishoni wa wiki kujionea namna chuo hicho kinavyoendesha programu zake katika jitihada za kuendeleza sekta ya michezo nchini.

ANNE MAKINDA AONGOZA MKUTANO MKUU WADAU BIMA YA AFYA MKOANI SIMIYU.

0
0
Katika Mkoa wa Simiyu kumefanyika Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfumo wa Bima ya afya nchini (NHIF), Mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Nchini Anne Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka.

Akongea wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, alionekana kukerwa na uwepo wa baadhi ya watoa huduma kutoka katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali nchini kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi juu ya mfuko huo.

Mbali na hilo Mwenyekiti huyo alikerwa kwa baadhi ya watoa huduma wa serikali pamoja na watu binafsi, kukidhiri kwa udanganyifu wa madai kwenda NHIF, ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakipeleka madai hewa katika mfuko huo kwa ajili ya kulipwa.

" hii ni changamoto kubwa sana kwa watoa huduma wetu, wamekuwa wakituletea madai ambayo siyo halisi, na kuashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi yao, jambo hili limekuwa kero kubwa sana mfuko na, hivyo ni lazima wachukuliwe katua kuanzia ngazi za halmshauri na mikoa" Alisema

Mkutano huo umeshirikisha wadau wengi wakiwemo viongozi wa kisiasa, wabunge, Madiwani, wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wahuduma wa afya, watoa huduma binasfi, viongozi wa dini, walimu, watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali, pamoja na wananchi.

Wakichangia mada mbalimbali wadau wengi wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye sehemu za kutolea huduma, licha ya kuchangia mfuko huo kila mwaka, lucha chafu kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya.

" tumekuwa tukitumia muda wetu na wananchi wanatusikiliza na kutuunga mkono kuchangia mfuko huu, lakini malalamiko yamekuwa mengi sana, ukosefu wa dawa pamoja na lugha chafu, hapo ndipo na sisi tunavunjika moyo na hali ya kuendelea kuchangia maana kila tukienda kuhamasisha tunakumbana na maswali hayo na tunakosa majibu" Alisema Makondeko

Mbali na hilo wadau hao walilalamikia mamlaka ya dawa nchini (Msd) kwa kushindwa kutoa dawa za kutosha kwa vituo mbalimbali vya afya nchini, ambapo baadhi waliiomba serikali kuifuta Msd, na kuunda chombo kipya kutokana na kushindwa kazi, huku halmashauri zikiomba kuruhusiwa kununua dawa moja kwa moja bila ya kupitia msd.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfuko huo Mkoa wa Simiyu, mkutano huo umefanyika Mjini Bariadi katika Kanisa Katoliki Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akifungua Mkutano mkuu wa wadau wa mfuko wa Bima ya afya (NHIF) uliofanyika hivi karibuni mjini Bariadi katika kanisa katoliki, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa onyo kali kwa watoa huduma katika mkoa huo binafsi pamoja na serikali kuacha mara moja tabia ya kupeleka madai yasiyo halisi NHIF kwa ajili ya malipo.
Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.
Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.

MAMA SAMIA MGENI RASMI SIKU YA NILE.

0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Nile “Nile Day” yatakayofanyika wiki ijayo  (Februari, 22), jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na taasisi inayosimamia shughuli za wanachama wa Bonde la Mto Nile-Nile Basin Initiative (NBI).

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mha. Gerson Lwenge ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu maadhimisho hayo.

Mha. Lwenge amesema kuwa maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka miongoni mwa nchi wanachama 10 zilizo katika bonde la mto huo; ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Sudan ya Kusini na Misri, ambapo kwa mwaka huu siku hiyo inasherekewa nchini Tanzania.

“Lengo la Siku ya Nile ni kukuza uelewa kwa watu wote kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote wanachama, masuala yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali za Bonde la Mto Nile,” alisema Mha. Lwenge.

Amefafanua kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kufahamu zaidi kuhusu umuhimu wa mto huo katika kutupatia chakula cha uhakika, maji, nishati ya umeme na faida nyingi kiuchumi pamoja na kubadilishana mawazo ya jinsi ya kulinda na kutumia rasilimali za mto huo kwa pamoja na kwa usawa na uendelevu kwa ajili ya kizazi cha leo na vizazi vijavyo.

Mha. Lwenge ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na maandamano kutoka viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, upandaji wa miti, maonesho ya vitu mbalimbali vinavyohusu Sekta za Maji na Umwagiliaji, burudani za kiutamaduni, pamoja na za watoto wa shule za msingi na sekondari.

Aidha, Waziri Lwenge amewataja washiriki wa maadhimisho hayo kuwa ni mawaziri wanaohusika na maji kutoka nchi wanachama, mabalozi, wawakilishi kutoka NBI, wabunge, washirika wa maendeleo, wataalamu, wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi, taasisi binafsi, vyombo vya habari pamoja na umma kwa ujumla.

NBI ilianzishwa rasmi mwaka 1999, jijini Dar es Salaam, ambapo nchi wanachama waliungana na kukubaliana kuanzisha umoja wa ushirikiano katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto Nile.


MAAFISA MAWASILIANO (TAGCO) WAKITIMIZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS KWA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA LEO VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

WACHIMBAJI WADOGO KUMILIKISHWA ENEO LA STAMICO, BUHEMBA

0
0
Serikali imesema itatoa eneo linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Buhemba, Mkoani Mara kwa wachimbaji Wadogo wa Madini baada ya kufanyika kwa tathmini  na taratibu za kumilikishwa eneo ili wachimbaji hao wafanye shughuli hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo kulipa kodi.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo tarehe 18 Februari,2017, wakati wa ziara yake katika mgodi huo ili kuangalia shughuli za uokoaji zinazoendelea katika mgodi huo, kufuatia  ajali ya kufukiwa na kifusi kwa Wachimbaji 18  iliyotokea tarehe 13 Februari,2017, ambapo wachimbaji 13 waliokolewa siku hiyo hiyo


Prof. Muhongo  amesema kuwa, wachimbaji hao hawakuwa na leseni wala vibali halali vilivyotolewa kwao  kufanya shughuli za utafutaji dhahabu na kwamba eneo hilo linamilikiwa kisheria na STAMICO kwa leseni  PL N0. 7132/2011, na kuongeza kuwa, wachimbaji hao walivamia eneo hilo ambapo ni kosa kisheria na wanatambulika kama wavamizi.


Ameongeza kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo hilo zilifungwa tangu mwaka 1971 ambapo awali eneo hilo lilikuwa chini ya wakoloni kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT), Kampuni ya Meremeta na baadaye kuwa chini ya umiliki wa STAMICO.


Aidha, amezuia shughuli zote za uchimbaji kufanyika katika eneo hilo na kusema kinachofanyika sasa ni kuutafuta mwili wa mchimbaji mmoja ambaye bado haujatolewa. ''Hadi sasa wachimbaji 15 wamekwisha okolewa, bahati mbaya wawili walitolewa wamefariki na sasa tuendelee na zoezi la kutafuta mwili uliobaki,"ameongeza Prof. Muhongo.
 Mmoja wa wachimbaji waliokolewa katika ajali ya kifusi akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jinsi ajali hiyo ya kufikiwa na kifusi wachimbaji 18 ilivyotokea. Katikakti  anayesikiliza ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje.

 Mmoja wa wachimbaji wadogo akishuka chini ya shimo la kuingilia katika mgodi kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wachimbaji 18 katika eneo la Buhemba mkoani Mara.

 Sehemu ya Wachimbaji wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa ziara yake katika mgodi wa Buhemba  unaomilikiwa na STAMICO.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wachimbaji wadogo katika eneo la Buhemba ambapo ajali ya wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi tarehe 13 Februari,2017.




DC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA KAMATI YA MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU NA SHEREHE ZA KUMUAGA ASKOFU NKOLA

0
0
Jumamosi Februari 18,2017,kumefanyika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017. 

Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mamia ya wachungaji,viongozi na waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro. 

Mnenaji mkuu katika kikao hicho alikuwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala. 

Akizungumza wakati wa kikao hicho Askofu Dkt. Makala aliwapongeza viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa kanisa hilo,Mchungaji Jakobo Mapambano kwa kuandaa sherehe ya kumuaga Askofu Nkola ambaye amekuwa askofu wa Kanisa hilo tangu tarehe 24.10.1993. 

Askofu Makala alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa kanisa hilo kutokuwa na tamaa ya madaraka ya uongozi kwa nafasi itakayoachwa na Askofu Nkola hili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza na kusisitiza kuwa ni vyema kiongozi atakayeziba nafasi hiyo apatikane kwa utaratibu unaotakiwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakati akiwasili katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga kuhudhuria kikao chakikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017 .Kulia ni Makamu wa Askofu Dayosisi ya Shinyanga mchungaji Aaron Malyuta
Ndani ya ukumbi wa NSSF: Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala baada ya kuwasili ukumbini.
Maombi yakiendelea baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 19,2017

Bamiza Top Music Chart 18th Feb 2017

miaka 50 ya azimio la arusha

NYIMBO ZA ZAMANI ZANOGESHA USIKU WA LOVE MELODIES AND LIGHTS

0
0
Usiku wa Love Melodies and Lights ulioandaliwa maalum kwa ajili ya kuisherehekea siku ya wapendanao (Valentine’s day) ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi wa pili kila mwaka, na kwa kulitambua hilo, Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya "bongofleva" ambao ni Ben Pol, Baraka The Prince na Jux walizikonga nyoyo za mashabiki wao vilivyo katika usiku huo, uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.

MC Pilipili akiweka sawa mbavu za wageni mbalimbali waliofika katika Usiku wa Love Melodies and Lights.
 Msanii Jux akifanya yake jukwaani katika Usiku wa Love Melodies and Lights.

MBUNGE JOSEPH MBILINYI AKA SUGU NA ISHU YA MADAWA YA KULEVYA

AMSHA KIPAJI CHAKO NA SINGA WA MBEYA


Wateja zaidi kusajiliwa huduma ya Lipa kwa M-Pesa nchini

0
0
Kutokana na ongezeko la watumiaji wa huduma ya kifedha wa M-Pesa  unaotolewa na Vodacom Tanzania,Takwimu za TCRA zimeonyesha huduma hiyo inatumiwa na watu zaidi ya milioni 8,kampuni imejizatiti kusajili wateja zaidi katika huduma ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ sehemu mbalimbali nchini. 
Akiongea na wakazi wa jiji la Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka jipya na promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba Mkuu wa kanda ya Nyasa Macfadyne Minja,
,amesema kuwa huduma hii ambayo ni salama na inarahisisha maisha ya wananchi wengi hususani wafanyabiashara inazidi kukubalika ambapo kwa mwaka jana lengo la kampuni lilikuwa ni kusajili watumiaji 20,000 lakini wamevuka lengo kwa kusajili watumiaji  40,000 nchini kote.
Alisema wateja waliochangamkia zaidi ni wale wanaofanya biashara mbalimbali zinazohusisha kupokea malipo moja kwa moja baadhi zake zikiwa ni biashara za maduka ya jumla na rejareja,migahawa,vituo vya kuuza mafuta ya magari,maduka ya vifaa vya ujenzi.Alisema kutokana na ubora wa huduma hii biashara za aina mbalimbali zaidi ya 1,000 zimejisajili na zinatumia kurahisisha mihamala ya malipo ya kibiashara.
“Katika mkakati wetu wa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali huduma hii ya ‘Lipa kwa M-Pesa’ inarahisisha biashara na  kuleta usalama hususani kwa kuwezesha watumiaji kufanya biashara bila kulazimika kutumia fedha taslimu kama ilivyo katika mataifa mengi yaliyoendelea,tunatoa wito kwa wafanyabiashara kujiunga nayo na kuwa wa kisasa na kutoachwa nyuma kiteknolojia”.Alisema Minja
Sitoyo alibainisha faida nyingine za kutumia huduma hii ni kuwezesha mfanyabiashara kutuma fedha zake za mauzo kwenye akaunti yake ya M-Pesa bila kutozwa gharama zozote,kufanya malipo mbalimbali yanayohusiana na biashara bila kutozwa gharama za ziada na  kuweza kutoa fedha kwa mawakala wa huduma ya M-Pesa kwa gharama yenye unafuu mkubwa.

“Ni rahisi sana na nafuu kutumia huduma ya M-Pesa kufanya mihamala ya malipo kwa kuwa haina gharama zozote za ziada zaidi ya  kukatwa thamani ya bei ya bidhaa anayonunua mteja tofauti na kutoa fedha taslimu kwenye akaunti ya M-Pesa ambapo kuna makato ,huduma hii pia haichukui muda kufanya mhamala wa malipo”.Alisema  Minja.
Kwa upande wake,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu alisema“Vodacom inao mtandao mkubwa wa wafanyabiashara ambao tayari wamepatiwa mafunzo ya kurahisisha biashara zao kwa kutumia huduma ya M-Pesa ambao wako tayari kumwelekeza mteja anavyoweza kufaidika kwa kutumia huduma hii hususani kukoa fedha zake za makato ya kuitumia.Hivi sasa tunatoa ofa maalumu kwa watumiaji wa huduma hii ambapo kwa kila mhamala anaofanya mteja anapatiwa muda wa bure wa maongezi ambapo kwa upande wa mfanyabiashara atapatiwa zawadi kati ya shilingi 2,000/- hadi 100,000/-kwa kila mhamala kulingana na thamani ya mhamala unaofanyika kwa kuitumia”Alisema Materu.
 Baadhi ya washindi wa bahati nasibu iliyoendeshwa jana wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba na Uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania lilipo katika Jengo la Raphael Group Uyole jijini Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na wakiongozwa, Macfadyne Minja(wanne kushoto) ambaye ni msimamizi Mkuu wa kampuni hiyo kanda ya nyasa.
 Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Grace Themistocleous (kushoto) akimuhudumia mteja wa kwanza kufika kupata huduma katika Duka jipya la kampuni hiyo lilifunguliwa jana katika Majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya ,Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima..

 Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wateja wao walifika katika duka jipya kupata huduma mbalimblai katika duka jipya la kampuni hiyo lililozinduliwa jana katika majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya, Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamefurika nje ya duka jipya la Vodacom Tanzania katika majengo ya Raphael Group Uyole jijini Mbeya wakati wa Uzinduzi wa duka hilo na kujinunulia simu mpya aina ya Smart Bomba yenye laini mbili inayopatikana kwa Tsh 99,000 nchi nzima.

INTRODUCING KIDUME NANESA - NGETA ft COYO

KITU KIPYA CHA JIDE

WATANZANIA WALIOFUKUZWA NCHINI MSUMBIJI WASAFIRISHWA KWENDA MIKOA YAO

WATANZANIA WALIOFUKUZWA NCHINI MSUMBIJI WASAFIRISHWA KWENDA MIKOA YAO

Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images