Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

Bamiza Top Music Chart 11th February 2017


Rais Dkt Magufuli aanda hafla ya mwaka mpya ya sherry party kwa mabalozi Ikulu, Dar es salaam

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
 Sehemu ya waalikwa wakimsikiliza  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi mbalimbali za kimataifa wanaowakilisha nchini  katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na maafisa wa wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa walioandaa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhiya mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali nchini katika hafla ya kuukaribisha mwaka mpya ya Sherry Party aliyowaandalia mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa Februari 10, 2017. Kwa picha zaidi za IKULU BOFYA HAPA

RC ARUSHA AONGOZA WANANCHI KATIKA MAZOEZI YA VIUNGO

$
0
0


Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua mazoezi ya viungo kwa kuonyesha kwa mfano kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuitikia wito wa Makamu wa Rais,Mh.Samia Suluhu Hassan wa kufanya mazoezi kila wiki ya pili ya mwezi kwa lengo kuzuia magonjwa yasiyoambukizwa na kuiweka miili katika hali ukakamavu.
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akipiga Push-Up za kutosha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo(kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro nao hawakua nyumba katika kuonyesha ukakamavu wao.Picha zote na Filbert Rweyemamu
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo(katikati) akiongoza mazoezi mepesi akiwa na viongozi wengine.


Umati uliojitokeza kushiriki mazoezi ya viungo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo(kati)akipasha pamoja na wananchi

Article 14

Muhimbili Yazindua Sehemu ya Kuchezea Watoto Wanaolazwa na Wanaopelekwa Kliniki

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto leo imezindua sehemu ya kuchezea watoto wanaolazwa na wale wanaofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu mbalimbali. 
 Sehemu ya kuchezea watoto imezinduliwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa hospitali hiyo, Dk Julieth Magandi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya. 
 Akizindua sehemu ya kuchezea watoto, Dk Magandi amesema kuwapo kwa sehemu ya kuchezea kutaongeza chachu ya watoto kuacha kuogopa hospitali kwani watavutiwa na kutambua kwamba wapo katika mazingira salama na rafiki wakati wakipatiwa huduma za matibabu. 
 “Nawapongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili licha ya kufungua sehemu hii ya michezo leo bado ndani ya jengo mmeweka vivutio vingi kwenye kuta zote za jengo la watoto ili kuhakikisha watoto wanafurahi,” amesema Dk Magandi. 
 Dk Magandi amesema kuwa sehemu hiyo ya michezo ambako pamefungwa vifaa vya kisasa vya kuchezea itawasaidia watoto wanaokaa muda mrefu hospitalini kuanzia mwezi mmoja hadi mwaka mmoja kupata faraja. 
 “Nina imani kuwa sehemu hii itawapa uhuru wa kucheza kwa nafasi na usalama zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa awali. Ni kweli ndani ya jengo kuna michoro ya wanyama mbalimbali na katuni zinazotoa taswira rafiki kwa watoto na kuondoa mawazo ya kwamba hospitali ni sehemu ya maumivu muda wote, lakini kuongezeka kwa sehemu hii ya michezo itachochea zaidi hali ya watoto kupenda kutibiwa na kujisikia huru zaidi,” amesema. 
 Pia, Dk Magandi amewashukuru Human Welfare Trust Fund kwa kujenga sehemu ya kuchezea watoto kwani wameonyesha wanawajali watoto wetu. 
 Naye Mkurugenzi wa Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hedwiga Swai akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amesema kwamba watoto wanaolazwa katika Jengo la Watoto ni wale wanaohitaji tiba za upasuaji, wenye majeraha ya moto, utapiamlo, matatizo ya moyo, wenye matatizo ya mishipa ya fahamu, figo, magonjwa ya tezi na kisukari, magonjwa ya mfumo wa damu, macho na watoto wanaohitaji ushauri wa lishe bora.
 “Sehemu hii ya michezo itatumika kwa watoto wanaokuja kliniki kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, wale wanaofatiliwa maendeleo yao baada ya kupata nafuu na wale wanaopata ruhusa ya kurudi nyumbani na watoto waliolazwa wodini,” amesema Dk Swai.
Baadhi ya wageni waliofika Muhimbili kushuhudia uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Dk Magandi.


Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi akikata utepe kuzindua sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili. Dk Magandi amezindua sehemu ya kuchezea watoto kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili, Dk Hedwiga Swai na mwakilishi wa Human Welfare Trust, Bi. Veena Jog.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi na wageni baada ya kuzindua sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili. Dk Magandi amezindua sehemu ya kuchezea watoto,
Sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi  akimshukuru mwakilishi wa Human Welfare Trust, Bi. Veena Jog.  baada ya  kuzindua sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili. 

DC SHINYANGA AKABIDHI VIFAA TIBA VILIVYOTOLEWA NA WATANZANIA WAISHIO DENMARK KWA AJILI YA WANANCHI WA SHINYANGA

$
0
0
Hapa ni katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuvisambaza katika zanahati na hospitali zilizopo katika manispaa hiyo.

Vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga
Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea 
Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
Vitanda vya wagonjwa vikiwa na magodoro yake.
Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

VIONGOZI WA TAASISI ZA UMMA SIMIYU WAHIMIZWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS

$
0
0
Na Stella Kalinga 
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,Ndg.Jumanne Sagini ametoa wito kwa viongozi na Wakuu wa Taasisi za Umma mkoani humo,  kusimamia utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ya viungo Jumamosi ya pili ya kila mwezi. 
Sagini ametoa wito huo leo katika hotuba yake kwa watumishi wa umma,wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viungo na michezo mbalimbali katika uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe.Makamu wa Rais. 
Amesema Simiyu wamejipanga kutekeleza na akawataka watumishi wa Umma kuheshimu agizo hilo na kutekeleza kama ilivyoelekezwa, badala ya kuamua kushiriki au kutoshiriki. 
"...Niombe wote wanaowasimamia Watumishi wa Umma kuhimiza utaratibu huu wa mazoezi ambao ni agizo la Makamu wa Rais ambalo limeongozana na nyaraka za Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wizara yenye dhamana na Elimu na Mafunzo ya Ufundi, lakini mara kadhaa hata Wizara ya Afya imekuwa ikisema,  Sisi kama Watumishi wa Umma hatuwezi kuchagua kutekeleza au tusitekeleze" alisema. 
Amesema kila mkuu wa Taasisi,Idara,Sehemu anapaswa kuhakikisha watumishi walio chini yake wanashiriki mazoezi ya viungo mwezi ujao(Machi) kwa kuwa  kushindwa kutekeleza Maelekezo ya viongozi pasipo sababu za msingi ni utovu wa nidhamu, ambalo ni kosa kwa mujibu wa Sheria,kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (mwenye kofia nyeupe) akiwa na baadhi ya watumishi  katika mazoezi ya kutembea kwenye Uwanja wa Halamshauri ya Mji Bariadi, wakati wa utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ya Viungo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akishiriki mazoezi ya viungo na  baadhi ya watumishi wa Umma,wanafunzi na wananchi katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi.
 Timu ya Sekretarieti ya Mkoa ikivuta kamba dhidi ya timu ya Halmashauri ya Mji Bariadi (haipo pichani) katika  Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi.
 Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na Viongozi na watumishi wa Umma, wanafunzi na wananchi walioshiriki mazoezi ya viuongo na michezo mbalimbali mjeni Bariadi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan. 
 Baadhi ya watumishi wakishiriki mbio za mita 100 wakati wa utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi ya Viungo na michezo mbalimbali mjini Bariadi.

RAMBIRAMBI VIFO VYA MASHABIKI ANGOLA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya mashabiki 17 na wengine kujeruhiwa katika tukio la watu kukimbia uwanjani kwa tishio la mabomu wakati wakati wa mchezo wa timu mbili zenye ushindani. 
Maelfu ya mashabiki, wakiwamo watoto wadogo walianza kukimbia na wengine kukanyagana hali iliyosababisha vifo uwanjani. 

Rais Jamal Malinzi wa TFF, ameelezea kushtuka kwa taarifa hizo za vifo hivyo vinavyoripotiwa kutokea Ijumaa Februari 10, 2017 kwenye Uwanja wa Angola ulioko mjini Uige, Kaskazini mwa nchi hiyo.  
Kwa masikitiko makubwa, Rais wa TFF Malinzi ametuma salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Angola (AFF); familia za ndugu waliopoteza wapendwa wao katika maisha, watu wa nchi hiyo, kutokana na vifo hivyo. 
Rais Malinzi amesema kwa nguvu za Mungu anawaombea heri ya kupona majeruhi na kwamba Tanzania inasali kuwaombea watu wa Angola wakati huu mguu. 
Mwenyezi Mungu azipokee roho za marehemu mahali pema peponi.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Watanzania mnakaribishwa katika Kanisa la Umoja Dallas

Wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro wafanya ziara katika Maduka ya Tanzanite, Arusha.

$
0
0
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, Mhe.James Millya, wametembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha ili kujionea shughuli za biashara na uongezaji thamani wa madini hayo zinavyofanyika. Ziara hiyo ni moja ya majukumu waliyopanga kuyafanya jijini Arusha, jukumu kuu likiwa ni kushuhudia jinsi Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unavyofanyika katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha. 
Moja ya duka lililotembelewa na Wabunge hao ni The Tanzanite Experience ambalo hujishughulisha na kukata Tanzanite ili kuiweka katika maumbo mbalimbali na kuing’arisha. Duka la The Tanzanite Experience pia hutoa elimu bure kwa wanafunzi na wageni mbalimbali kuhusu madini ya Tanzanite ikiwemo historia yake. 
 Ndani ya duka hilo pia kumejengwa mgodi wa mfano wa Tanzanite ambao hutumika kutoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu shughuli za uchimbaji wa Tanzanite. 
Baadhi ya Wajumbe waliofanya ziara hiyo ni pamoja na Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) na Mhe. Dunstan Kitandula Mbunge wa Mkinga (CCM).
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, wakitembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, wakitembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, wakitembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha

SIMBA YAREJEA KILELENI KWA KUITANDIKA TIMU YA PRISONS BAO 3-0

$
0
0
Timu ya Simba imejikita kileleni baada ya kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya maafande wa Tanzania Prison  kwenye mchezo uliochezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi kila timu ikitafuta goli la kuongoza, ilichukua dakika 18 kwa Simba kupata goli la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wake Juma Luizio.

Katila dakika ya 28, Ibrahim Ajib anaipatia Simba goli la pili akipokea pasi safi ya Laudit Mavugo na mpaka kufika mapumziko Simba 2-0.


Kipindi cha pili kilianza kwa Prison kutafuta goli kwa kila namna lakini Laudit Mavugo anaipatia Simba goli la tatu na la ushindi katila dakika ya 57.

Mpaka mpira unamalizika Simba wanatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 3-0 na kufikisha alama 51 akifuatiwa na Yanga wenye alama 49.
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Laudit Mavugo akijaribu kuupiga mpira kwa mtindo wa Tik Tak mbele ya Mabeki wa Timu ya Tanzania Prisons, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam jioni ya leo. Simba imeshinda bao 3-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya Tanzania Prisons, Benjamin Asukile akichuana vikali na James Kotei wa Simba, Beki Mohamed Hussein "Tshabalala" akingalia namna ya kusaidia wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeshinda bao 3-0.
 "Huondoki na mpira hapa"

Mchungaji Gwajima aachiliwa huru leo

NEWS ALERT: MABALOZI WATATU WAPANGIWA VITUO VYA KAZI

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapangia vituo vya kazi Mabalozi wapya watatu ambao aliweteua tarehe 3 Disemba 2016. 
Mabalozi hao  ni Mhe. Joseph Sokoine anayekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Omar Yussuf Mzee anayekuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Algeria na Mhe. Grace Mgavano anayekwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Ladis Komba nchini Uganda ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria. 
Balozi Sokoine ambaye anakwenda kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Deodorus Kamala ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 
Balozi Mzee kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo alishawahi kushika nafasi mbalimbali katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na nafasi ya mwisho alikuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika awamu ya kwanza ya Mhe.  Rais Dkt. Ali Mohammed Shein. 
Kwa upande wa Balozi Mgavano kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa wa Ubalozi alikuwa Afisa Mwandamizi katika Ofisi ya Rais, Ikulu. 
Mabalozi wote waliopangiwa vituo vipya vya kazi wataapishwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kesho siku ya Jumapili tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu jijini Dar Es Salaam saa tano asubuhi.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki,


Tarehe 11 Februari 2017

MKOA WA RUVUMA UMEANZA MCHAKATO WA UANZISHWAJI WA BENKI YA WANANCHI WA MKOA WA RUVUMA.

$
0
0
MKOA wa Ruvuma umeanza mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.Uanzishwaji wa benki ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu ambaye ameagiza kila mkoa hapa nchini uwe na Benki ya wananchi ili kusogeza huduma za kifedha kwa wananchi. Utafiti uliofanyika mwaka 2013 unaonesha kuwa ni asilimia 15 tu ya watanzania wanaotumia huduma za kibenki huku asilimia 85 wakikosa huduma hizo.Habari kamili tizama hii video

KONGAMANO KUBWA LA MAOMBI MAALUMU KWA WANAVYUO LAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa somo kuhusu "Funguo za Kiagano za Kupata Majibu ya Maombi yetu"
Wanafunzi wa vyuo wakiwa ukumbini.
Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiongoza maombi kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu kwani hali ya kitaaluma ipo chini ukilinganisha na mikoa mingine 
Wanafunzi wakiwa wamenyoosha mikono wakati wa maombi 
Washiriki wa kongamano wakiwa wamenyoosha mikono.




Muhimbili Yazindua Sehemu ya Kuchezea Watoto Wanaolazwa na Wanaopelekwa Kliniki

$
0
0

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto leo imezindua sehemu ya kuchezea watoto wanaolazwa na wale wanaofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu mbalimbali.

Sehemu ya kuchezea watoto imezinduliwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa hospitali hiyo, Dk Julieth Magandi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya.

Akizindua sehemu ya kuchezea watoto, Dk Magandi amesema kuwapo kwa sehemu ya kuchezea kutaongeza chachu ya watoto kuacha kuogopa hospitali kwani watavutiwa na kutambua kwamba wapo katika mazingira salama na rafiki wakati wakipatiwa huduma za matibabu.

“Nawapongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili licha ya kufungua sehemu hii ya michezo leo bado ndani ya jengo mmeweka vivutio vingi kwenye kuta zote za jengo la watoto ili kuhakikisha watoto wanafurahi,” amesema Dk Magandi.

Dk Magandi amesema kuwa sehemu hiyo ya michezo ambako pamefungwa vifaa vya kisasa vya kuchezea itawasaidia watoto wanaokaa muda mrefu hospitalini kuanzia mwezi mmoja hadi mwaka mmoja kupata faraja.

“Nina imani kuwa sehemu hii itawapa uhuru wa kucheza kwa nafasi na usalama zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa awali. Ni kweli ndani ya jengo kuna michoro ya wanyama mbalimbali na katuni zinazotoa taswira rafiki kwa watoto na kuondoa mawazo ya kwamba hospitali ni sehemu ya maumivu muda wote, lakini kuongezeka kwa sehemu hii ya michezo itachochea zaidi hali ya watoto kupenda kutibiwa na kujisikia huru zaidi,” amesema.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi akikata utepe kuzindua sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili. Dk Magandi amezindua sehemu ya kuchezea watoto kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili, Dk Hedwiga Swai na mwakilishi wa Human Welfare Trust, Bi. Veena Jog.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi akizungumza kabla ya kuzindua sehemu ya watoto kuchezea. Kushoto ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki M, Anil Verma.
Baadhi ya wageni waliofika Muhimbili kushuhudia uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Dk Magandi.

KOMREDI KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA KATIBU WA HAMASA WA SHIRIKISHO LA WANAFUNZIWA VYUO VYA ELIMU YA JUU MKOA WA KILIMANJARO, EDWIN MSELLE, LEO, WILAYANI KIBOSHO

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili.

Mazishi hayo yamefanyika leo Wilayani Kibosho, mkoani Kilimanjaro. Edwin ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa udaktari, mwaka wa nne katika Chuo Kikuu Kishiriki cha KCMC, ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM waliofariki kwa ajali ya gari, wakati waitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, Februari 5, 2017 ambapo Kinana ameongoza kwenye mazishi yao wote. 

Taratibu zikifanywa na Padre kabla ya kuingiza jeneza kaburini  


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini  

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akimwaga udongo kaburini wakati wa maziko

Kinana akikabidhi rambirambi kutoka CCM na Jumuia zake kwa Baba wa Marehemu Edwin, Christopher Mselle wakati wa mazishi hayo


Kinana akimpa pole Padre Dackshen Hangai wakati wa mazsihi hayo. 
Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba jeneza kwenda eneola maziko, wakati wa mazishi hayo .

UZINDUZI WA KAMPENI ZA UZAZI WA MPANGO ZANZIBAR

$
0
0
Na Ramadhani Ali/Maelezo 

Zaidi ya akinamama 236 kati ya laki moja wanaofika hospitali na vituo vya afya kujifungua Zanzibar wanafariki kila mwaka kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo kuacha kutumia huduma za uzazi wa mpango.

Kutokana na tatizo hilo Wizara ya Afya imeanzisha kampeni maalum ya wiki moja ya kuwahamasisha akina mama na akinababa kujiunga na uzazi wa mpango katika juhudi za kuokoa maisha ya wazazi na watoto.

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alizindua kampeni hiyo katika kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na kuwashauri akinababa kuwaruhusu wake zao kujiunga na uzazi wa mpango .

Alisema hidi sasa wanawake wanaostahiki kujiunga na uzazi wa mpango Zanzibar ni asilimia 14 tu waliojiunga na juhudi inatakiwa ifanywe ili iweze kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2020 ili kulinda afya ya mama na mtoto.

Waziri Mahmoud alisema idadi ya akinamama wanaofariki ni kubwa zaidi ya takwimu zilizopo kwani wanaojifungulia hospitali ni asilimia hamsini tu na asilimia iliyobaki wanajifungulia majumbani na hakuna takwimu zao. 

Aliongeza kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa za kusambaza huduma za uzazi wa mpango katika vituo vyote vya afya mijini na vijijini ili kuwaondoshea usumbufu wananchi hivyo amewashauri kuvitumia.

Akizungumzia vifo vya watoto chini ya miaka mitano, Waziri wa Afya alisema bado ni tatizo kubwa Zanzibar watoto 56 kati ya 1000 wanaozaliwa wakiwa hao hufariki dunia.Alisema sababu kubwa ya vifo hivyo inatokana na wazazi kucheleweshwa kupelekwa hospitali ama kutopelekwa kabisa na kupelekea kujifungua katika mazingira yasiyo salama.

Kutokana na matatizo mengi yanayowapata akinamama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, Waziri Mahmoud Thabit Kombo ameagiza kuundwa Kamati ya kitaifa itakayowashirikisha viongozi kutoka kada mbali mbali na washirika wa maendeleo kukabiliana nalo.

Mwakilishi wa Shirika la Engender Health Dkt. Martha Kisanga alisema ushiriki mdogo wa akinababa katika huduma ya uzazi wa mpango unachangia wanawake wengi kutojiunga na huduma hizo.

Katika risala ya wananchi wa Wilaya Kaskazini A iliyosomwa na Tatu Khamis Kombo walisema pamoja na vituo vingi vya afya kutoa huduma za uzazi wa mpango, mwamko bado ni mdogo na kufanyika kwa kampeni hiyo katika wilaya yao itasaidia wananchi wengi kujiunga.

Wilaya Kaskazini A na Wilaya ya Micheweni Pemba ndizo zenye asilimia ndogo zaidi ya akinamama waliojiunga na huduma ya uzazi wa mpango Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kutoka kwa mhamasishaji wa Shirika la Engender Health Joyce Ishengoma alipotembelea banda la maonyesho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha huduma hiyo iliyofanyika kijiji cha Mkwajuni Wilaya Kaskazini A.
Mwakilishi wa Shirika la Engender Health Dkt. Martha Kisanga akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya uhamasishaji wa uzazi wa mpango katika kijiji cha Mkwajuni.
Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni maalum ya uzazi wa mpango wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Baadhi ya watoto walioshiriki uzinduzi wa kampeni maalum ya kuwahamasisha wazazi wao kujiunga na uzazi wa mpango wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Mkwajuni.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji uzazi wa mpango uliofanyika Mkwajuni Wilaya ya Kasakazi A Unguja.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

UN chief: Tanzanian to lead Hammarskjold air crash review

$
0
0
Secretary-General Antonio Guterres has appointed Tanzania's former chief justice to review potential new information, including from South Africa, on the mysterious 1961 plane crash that killed U.N. Secretary-General Dag Hammarskjold.


U.N. deputy spokesman Farhan Haq said Friday that Mohamed Chande Othman (pictured), who recently retired as Tanzania's top judge, would lead the review which former U.N. secretary-general Ban Ki-moon called for in August and the General Assembly requested in a resolution adopted on Dec. 23.

Hammarskjold was on a peace mission to newly independent Congo when his plane crashed in what is now Zambia.
The resolution asked the U.N. chief to appoint "an eminent person" to review and assess the value of any potential new information "to determine the scope that any further inquiry or investigation should take and, if possible, to draw conclusions from the investigations already conducted."
An independent panel reviewing new information about the crash said in July 2015 that the United States and Britain retained some classified files, and that South Africa had not responded to several requests for information.

The panel's 99-page report put to rest claims that Hammarskjold was assassinated after surviving the crash. But it has long been rumored that his DC-6 plane was shot down, and the panel provided new information about a possible aerial attack or interference.

Ban said in a note last August that Britain again refused to release classified material in response to U.N. requests for information. He said responses from the United States and Belgium didn't alter the panel's conclusion that the possibility of an aerial attack or interference should be pursued.

Ban's note included a letter dated July 1, 2016 from South Africa's U.N. Mission saying the government fully supports the U.N. investigation and "the Department of Justice and Constitutional Development has directed that a search be undertaken for any documents, records or information."

The panel had cited documents from the South African Institute for Maritime Research that refer to "Operation Celeste," purportedly to "remove" Hammarskjold with cooperation from then U.S. CIA director Allen Dulles. It was not able to conclude whether the documents were authentic.

Ban said the United Nations also received additional information about Hammarskjold's death after the panel's report.



UZINDUZI WA MAZOEZI YA VIUNGO KITAIFA MJINI DODOMA

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>