Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1562 | 1563 | (Page 1564) | 1565 | 1566 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akizungumza na wafanyabishara wa soko la Ilala
   Wafanyabiahsra wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto katika mkutano wa halmashauri ya Ilala na wadau wa soko hilo.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa ameongozana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.

  0 0

  EDUCATION, SCHOLARSHIPS AND EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
  A new feature titled “Education, Scholarships an Employment” has been added on the website of the Embassy of Tanzania in Washington D.C.

  Please visit http://tanzaniaembassy-us.org/ for more information.

  For comments and/or addition: Please write to tanzaniaembassyus@gmail.com  0 0


  0 0


  Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  mwalimu  Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza  mazoezi ya viungo katika  uwanja wa  samora  Leo wa  pili kushoto ni katibu  tawala wa mkoa  wa Iringa wamoja Ayubu

  DC  Iringa  Richard  Kasesela wa kwanza  kulia  akishiriki mazoezi ya  riadha kutoka  uwanja  wa Samora mjini Iringa.
  Habari zaidi BOFYA HAPA

  0 0
  0 0

  Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) alipotembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
  Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya (kulia) akifurahia zawadi ya kitabu cha historia ya Tanzania ambacho Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Alphayo Kidata alimkabidhi kama ishara ya ukumbusho wa ziara yake nchini Tanzania. Dk. Mikuriya alitembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya alipotembelea TRA ili kujadili masuala mbalimbali na kuona maendeleo ya miradi ya Forodha inayotekelezwa na TRA kwa ushirikiano na WCO
  Meneja Mifumo ya Kielektroniki ya  Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (aliyesimama) akitoa maelezo ya jinsi Mfumo wa Forodha (TANCIS) unavyofanya kazi kwa Katibu Mkuu wa Shirika la Forodha Duniani (World Customs Organisation-WCO) Dk. Kunio Mikuriya (aliyeketi katikati). Wengine ni Meneja wa Maendeleo Ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini kutoka Shirika la Forodha Duniani Bw. Patrick Gyan (kushoto) pamoja na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa Bw. Jocktan Kyamuhanga (kulia).

  0 0

  Imeelezwa kuwa jumla ya wanawake 47 wamehitimu mafunzo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito yanayotolewa na Kituo cha Jemolojia jijini Arusha ambacho kipo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

  Hayo yalisemwa jijini Arusha na Kaimu Mratibu wa Kituo hicho, Erick Mpesa wakati wa Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unaofanyika jijini Arusha katika Kituo hicho.

  Mpesa alisema kuwa mafunzo hayo yalianza kutolewa mwaka 2014 ambapo katika Awamu ya kwanza wanafunzi 15 walihitimu, Awamu ya Pili walihitimu wanafunzi 14 na Awamu ya Tatu walihitimu wanafunzi 18.
  Mkufunzi Msaidizi katika Kituo cha Jemolojia Arusha, (TGC), Lilian Petro (wa kwanza kulia) akionyesha madini ya vito yaliyong’arishwa na wanafunzi wanaopata mafunzo katika Kituo hicho kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini. Wa Pili kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito (TANSORT), Archard Kalugendo, wa Pili kushoto ni Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) na wa kwanza kushoto ni Beatrice Lupi, Mhasibu Mkuu kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

  “Mafunzo haya hutolewa kwa muda wa miezi Saba ambapo Wanafunzi hawa ambao huwa na umri wa chini ya miaka 30 wanafadhiliwa na Mfuko wa Kuwaendeleza Wanawake chini ya Kamati ya Maonesho ya Vito ya Arusha (AGF) na Wizara ya Nishati na Madini,” alisema Mpesa.

  Mratibu wa TGC aliongeza kuwa Kituo hicho pia kinaendesha shughuli za uchongaji wa mawe ya miamba kwa kutengeneza vinyago vyenye maumbo mbalimbali kama ya wanyama, ndege, samaki na vitu mbalimbali vya urembo.

  Akizungumzia mafanikio ya kituo hicho, Mpesa alisema kuwa mbali ya kusaidia wanawake hao kupata mafunzo yatakayowasaida kujiajiri au kuajiriwa, Kituo hicho ni cha pekee Afrika Mashariki kinachoendeleza taaluma ya uongezaji thamani madini ya vito na miamba.
  Mmoja wa wanafunzi katika Kituo cha Jemolojia Arusha, Zuwena Mtoo, akionesha utaalam wa kukata na kung’arisha madini ya Vito, baada ya kupata mafunzo katika Kituo hicho kilicho chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

  Kuhusu mipango ya kuendeleza Chuo hicho alisema kuwa, Chuo kimepanga kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya diploma ambapo mitaala ya kozi mbalimbali za taaluma ya vito na usonara imeandaliwa na kuwasilishwa katika Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ambapo mchakato wa ithibati na usajili unaendelea.

  Kwa upande wake Mkufunzi Msaidizi wa TGC, Lilian Petro, alisema kuwa mafunzo hayo husaidia wanafunzi hao kutambua madini ya aina mbalimbali, kuyakata na kufahamu thamani ya madini husika.

  Aidha Lilian, Alitoa ushauri kwa wanawake mbalimbali nchini kujiunga katika fani hiyo ya ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito kwa kuwa inamsaidia mtu kujiajiri kwa kuanzisha vituo vya ung’arishaji wa madini ya vito ndani ya nchi na pia kuajiriwa.
  Samadu Mohamed, kutoka Kituo cha Jemolojia Arusha, akionesha moja ya vinyago vinavyotokana na mawe ya miamba vinavyotengenezwa katika kituo hicho.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wananchi mapema leo asubuhi katika Uwanja wa Ushirika wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoezi ya pamoja kwa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni utekelezaji wa agizo la makamu wa rais Samia Suluhu Hassan la kutenga siku moja kwa ajili ya mazoezi kila mwezi, ambapo amesema kuwa amekabidhi orodha ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, na siku ya jumatatu yatatangazwa. Amesema yapo majina 42 ya washukiwa wa biashara hiyo ya dawa za kulevya mkoani humo na Watuhumiwa watano kati yao watasifishwa mahakamani siku hiyo hiyo. Anasema waliokurupushwa Dar sasa wanataka kuhamishia mapito yao Kilimanjaro, Ametoa onyo wasijaribu kwa kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kupambana nao. Na Dixon Busagaga, Globu ya Jamii - Kilimanjaro.


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kukabidhi matembezi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, Makao Makuu ya nchi Dodoma.

  Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi mapema leo asubuhi mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.Pichani kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

  Mbali ya Makamu wa Rais kuunga mkono tukio hilo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye ,Naibu Spika wa Bunge,Tulia Ackson,Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba,Naibu waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla na wengineo sambamba na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.

  Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza mazoezi ya kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma


  Wananchi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji wa Dodoma wakishiriki mazoezi mapema leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

  0 0  0 0


  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  MWIMBAJI wa muziki wa taarab nchini Tanzania, Bi Khadija Kopa, amewataka wanawake kuendelea kujikwamua kiuchumi wao wenyewe bila kusubiri kuwezeshwa na wanaume.

  Khadija aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa duka kubwa la kisasa la urembo na nguo za wanawake linalojihusisha pia na kupamba maharusi, kukodisha na kuuza nguo za maharusi, linalojulikana kama Taiba Beauty, linalomilikiwa na mjasiriamali Twaiba Ahmed Ally.
  Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarabu nchini, Bi Khadija Kopa, akizungumza na waandishi hawapo pichani katika uzinduzi wa duka la nguo za wanawake na za harusi linalomilikiwa na mwanamama Twaiba Ahmed Ally.

  Alisema kwamba wapo wanawake wanaoamini kuwa hawawezi kuendelea hadi wawezeshwe, jambo linalohitaji kupingwa vikali ili wanawake waweze kupiga hatua kiuchumi na kujikomboa wao wenyewe.
  Mmiliki wa duka la nguo za maharusi lililopo mtaa wa Livingstone na Mkunguni, Bi Twaiba Ahmed Ally, katikati akikata keki ya uzinduzi wa duka hilo jana. Kulia ni mwimbaji wa taarabu nchini, Khadija Kopa akilishwa keki kama mgeni rasmi. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi cha Ng'ari Ng'ari kutoka Clouds Tv, Sakina Lyoka.
  Twaiba akimlisha keki Khadija Kopa katika tukio la uzinduzi huo jana.
  Bi Twaiba akimlisha keki Sakina Lyoka jana.
  Bi Sakika Lyoka akimlisha keki mmiliki wa duka hilo, bi Twaiba Ahmed. Kushoto ni Khadija Kopa.

  “Naomba wanawake tuache dhana kuwa hatuwezi kuendelea hadi tuwezeshwe na wanaume, ukizingatia kuwa Dunia imebadilika na wapo wenzetu wanaofanya kazi nzuri kiasi cha kutufanya tuige nyendo zao ili tusonge mbele, akiwamo Bi Twaiba Ahmed,” Alisema Kopa.

  Akizungumzia hilo, Bi Twaiba alisema ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawake wanasonga mbele kiuchumi, akisisitiza namna ya ujihusishaji na masuala yote ya ujasiriamali na kazi nyingine.


  “Nashukuru kwa sapoti kubwa ninayoipata, akiwamo Bi Khadija Kopa, hivyo nitaendelea kufanya juhudi ili nizidi kupiga hatua kubwa kibiashara kwa kusimamia changamoto zote zinazonikabili. “Katika duka langu nafanya shughuli zote zinazomhusu mwanamke, wakiwamo wale wanaofunga ndoa kwa kuwapamba, kuwakodisha vifaa vya harusi bila kusahau wale wanaotaka kununua kwa fedha taslimu, ofisi yangu ikipatikana katika mtaa wa Mkunguni na Livingstone, Kariakoo, jijini Dar es Salaam,” Alisema.

  Mbali na kuuza vifaa vya maharusi na nguo za kawaida za wanawake, pia Twaiba anajihusisha na ufundishaji wa upambaji kwa wanawake, shughuli inayomfanya aheshimiwe na wengi wanaojihusisha na sekta hiyo ya mitindo na urembo.

  0 0

  BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limewafukuza kazi watumishi wake wanne, kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya utoro kazini na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni 46,680,000. 

   Waliofukuzwa kazi ni Mosta Ndunguru ambaye ni Afisa tabibu na Bapara Mwang’ombe Mhudumu wa afya ambapo wote kwa pamoja wamefukuzwa kwa makosa ya utoro kazini. Walioisababishia hasara halmashauri hiyo ya shilingi milioni 46,680,000 ni maofisa misitu wasaidizi, Kelvin Haulle na Ally Almasi. Msikilize mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ambrose Nchimbi

  0 0

   The Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidata (right) welcomes the World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya when he paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration  with WCO

   The World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya appreciating a book of Tanzania History handed to him by the Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidaya as a symbol of remembrance of his visit in Tanzania. Dr. Mikuriya paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration with WCO.

   The World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya stressing  a point during a joint meeting with the Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidaya (right) when he paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA  in collaboration  with WCO.

  ·       The Tanzania Revenue Authority (TRA) Manager for Customs Automation Systems Mr. Felix Tinkasimile (standing) making a presentation on how the Tanzania Customs Integrated System (TANCIS) operates to the World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya (seated center). Looking on are the WCO Regional Development Manager for East and Southern Africa Mr. Patrick Gyan (left) and the Commissioner for Customs and Excise Mr. Jocktan Kyamuhanga. The WCO Secretary General paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration with WCO.


  0 0  0 0

  Mwakilishi Mkuu wa Michuzi Blog Kanda za nyanda za juu Kusini Fadhili Atiki aka Mr Pengo (kushoto) akiwa na makamanda wa jeshi la polisi mkoani Mbeya asubuhi ya leo wakati akishiriki na kurekodi matukio ya mazoezi ya kitaifa yaliyofanyika mkoani humo na kushirikisha maelfu ya wananchi.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza matembezi yaliyoshirikisha  Mawaziri, Wabunge pamoja na wananchi walioshiriki mazoezi hayo ambayo yamehitimishwa katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa na
  lengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika.  Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo kwa Mawaziri Wabunge pamoja na wananchi waliouhudhiria katika kushiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa na lengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Mawaziri Wabunge Watumishi na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma ambao wajitokeza katika kushiriki Mazoezi ya Viungo yenyelengo la Kupambana na Magonjwa yasiyo ambukizika Mazoezi hayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Baadhi ya wapiga picha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Rubani wa parachuti, David Eris kutoka kampuni ya HOT AIR Safaries, mara baada ya ziara ya kuitembelea Hifadhi ya Maasai Mara, nchini Kenya. Wapiga picha hao walitembelea hifadhi hiyo kufuatia mualiko kwa kampuni ya kutengeneza kamera aina ya Canon ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kamera mpya aina ya Canon D5 Mark IV, ambapo wapiga picha hao waliweza kupatiwa uzowefu wa kamera hiyo mpya iliyoongezewa ubora katika upigaji picha na video pia. Mpiga picha na Blogger, Othman Michuzi wa Mtaa kwa Mtaa Blog (wa kwanza kulia waliopiga goti) ndiye aliyekuwa mwakilishi wa wapiga picha kutoka Tanzania. na zifuatazo ni baadhi tu ya picha alizopiga katika ziara hiyo.
  Twiga 
   Duma wa Maasai Mara wakiwa mawindoni
   Mfalme wa Pori, Simba akiwa kala pozi.
   Swala na Twiga.

  Pundamilia akilia.
   Simba jike akipanga mbinu za kwenda kuwinda wakati Dume akisubiri.
   Nyati wa Maasai Mara.
   Muonekano wa vivuli vya baadi ya wapiga picha hao wakakati wa kuchomoza kwa jua.


  0 0

  KWAMBA TAREHE 08.02.2017 MAJIRA YA SAA 09:00HRS ASUBUHI, KATIKA MTAA WA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU MMOJA ALIYEJULIAKANA KWA JINA LA JUMANNE NASSIBU MIAKA 20, MGOGO NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUKUTWA AKIMWINGILIA KIMWILI MBUZI JIKE, KITENDO AMBACHO NIKOSA LA JINAI.

  INADAIWA KUWA TAREHE TAJWA HAPO JUU MAJIRA YA 6:00HRS ASUBUHI  MMILIKI WA MBUZI  AITWAYE BENEDICTOR BUNGA MIAKA 33, MKAZI WA MTAA WA MABATINI, ALIKWENDA KUWAFUNGA MALISHONI MBUZI WAKE SITA KWA KUTUMIA KAMBA. AIDHA INASEMEKANA KUWA ILIPOFIKA MAJIRA YA SAA TATU ASUBUHI (9:00HRS), MMILIKI WA MBUZI ALIKWENDA KUWACHEKI MBUZI WAKE ENEO ALIPOKUWA AMEWAFUNGA MALISHONI NA KUWAKUTA MBUZI WATANO BADALA YA SITA.

  KUTOKANA NA KUKOSEKANA KWA MBUZI HUYO MMILIKI WA MBUZI HAO ALIPATWA NA HOFU HUKU AKIJUA MBUZI WAKE MMOJA AMBAYE HAMUONI ATAKUWA AMEIBIWA NDIPO ALIANZA KUTAFUTA VICHAKANI, GHAFLA  ALINADAI ALIMUONA MTUHUMIWA JUMANNE  NASSIBU VICHAKANI AKIWA ANAMWINGILIA KIMWILI MBUZI WAKE. INASEMEKANA KUWA MMILIKI WA MBUZI HUYO BAADA YA KUONA TUKIO HILO ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA NDIPO WANANCHI WALIFIKA NA KUMSAIDI KUMKAMATA MTUHUMIWA.

  MTUHUMIWA YUPO POLISI HUKU MAHOJIANO DHIDI YA TUHUMA ZINAZOMKABILI YAKIENDELEA, PIA UTARATIBU UNAFANYIKA WA  KUPELEKWA MTUHUMIWA HOSPITALI,  ILI KUANGALIWA KAMA ANAAKILI TIMAMU,  PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA HATUA STAHIKI ZA KISHERIA DHIDI YAKE.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WAJIJI NA MKOA WA MWANZA AKIWATAKA KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA KAMA HIZO KWANI NI KOSA LA JINAI, ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAO.


  IMETOLEWA NA.

  DCP: AHMED MSANGI


  KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA


  0 0
 • 02/11/17--03:35: TANZIA UK NA MOSHI, TANZANIA

 • Kamati ya Mpito TZUK kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa Baba mzazi wa Ndugu yetu, Mtanzania na mwanajumuiya mwenzetu Ndugu Frank Mlay (Daddy Big). Marehemu Mzee  Gasper Mlay amefariki tarehe 06/02/2017, Moshi TANZANIA.
  Taratibu za msiba zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu Tanzania na mfiwa amesafiri kuelekea Tanzania, ili kuwahi mazishi. Tunaomba kumsaidia mwenzetu aweze kumpumzisha mzazi wake kwa amani , na kumuombea safari njema na Mungu ampe Faraja katika kipindi hiki kigumu. 
  Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kumfariji mwenzetu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.
  Michango yote ielekezwe moja kwa moja kwa Kutumia akaunti ifuatayo;

  Account name -  D A Wilson
  Account No. 40416290
  Sort Code.  20 - 98 - 57
  Barclays Bank.
  Kamati ya Mpito TZUK Itaendelea kuwapa taarifa zaidi za msiba na mahitaji nyumbani Tanzania, Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu kuwafariji na kuwa pamoja na familia ya Marehemu.
  Tunawaomba sana Watanzania UK na Northern Ireland tuonyeshe mshikamano kwa Upendo na Umoja kwa kumchangia Mwenzetu kwa hali na Mali tafadhali weka jina lako hapa na kiasi ulichochangia

older | 1 | .... | 1562 | 1563 | (Page 1564) | 1565 | 1566 | .... | 3286 | newer