Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1561 | 1562 | (Page 1563) | 1564 | 1565 | .... | 3284 | newer

  0 0  0 0

  Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

  JESHI la polisi Mkoani Kigoma  linamshikilia mtu Mmoja kwa kosa la kukutwa na vipande vitatu vya Pembe za ndovu  vyenye uzito wa kilo 15  vyenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 500 akivisafirisha kutoka Katavi kuvileta kigoma kwa ajili ya kuviuza.

  Sambamba na tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia Wahamiaji halamu 231, Bangi keye 220, mtambo Mmoja wa kutengenezea pombe ya moshi na watuhumiwa 10 wakiwa na  lita 217 , watuhjmiwa hao ni wauzaji na wapikaji kitendo ambacho ni kinyume na sheria za Nchi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Kigoma Naibu kamishina Wa Jeshi la polisi , Fredinandi Mtu alisema mnamo tarehe februali6 mwaka majira ya saa sita huko katika Kijiji Cha Kazuramimba Wilayani Uvinza Askari walipokea taarifa kuwa kuna wizi umetokea  Katika Gari ya Saratoga Iliyokuwa ikitokea Tabora kuja  Kigoma , askari Walifanya upekuzi na kukamata begi la abiria mmoja jina lake limehifadhiwa kwaajili ya upelelezi  likiwa na  vipande vitatu vya meno ya tembo.

  Kamanda Mtui alisema Upelelezi wa tukio hilo unaendelea ilikufahamu mahali mtuhumiwa alipotoa vipande hivyo vya meno ya tembo , Mtuhumiwa atafikishwa  mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika kwa hatua zaidi za kisheria.

  "Jeshi la polisi Mkoani Kigoma tunawaomba Wananchi Kuendelea kuunga Mkono jitihada za vita dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za watu wanao jihusisha na   vitendo hivyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na kukomesha vitendo hivyo.

  Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Wilaya ya Kigoma, Iddi Salumu alisema katika Mapori ya Kigoma hakuna pembe za ndivu za aina hiyo zilizo kamatwa vipande hivyo vinaweza kuwa vimetokea katika Mkoa Wa Katavi au katika hofadhi ya TANAPA ya Seruu .

  Alisema Kigoma Ndio njia kuu ya Kupitishoa mozigo hiyo na biashara kubwa inafanyikia Bchini Burundi , kwa Nchi ya Burundi biashara hiyo imeruhusiwa na majangiri wengi wanatumia Njia ya Mkoa Wa Kigoma kupitishia mizigo hiyo.

  Salumu alisema katika kuhakikisha biashara hiyo inadhibitiwa wameamua kuboresha Doria kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na polisi waliopo Mipakani ilikuweza kudhibiti na kufanya ukaguzi wa mizigo yote inayopita kuelekea Nchini Burundi.

  0 0


  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

   Tanzania Girl Guides Association (TGGA) wanategemea kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa njia ya kufanya shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii.

  Maadhimisho hayo yanayojulikana kama ‘thinking day’ yatafanyika Februari 22 mwaka huu ambapo shughuli za kuisaidia jamii zitaanza Februari 10 mwaka huu.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Makao Makuu wa Chama hicho, Rosaldina Majuva alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

  Bi. Rosaldina amesema kuwa siku ya maadhimisho ya chama hicho inaambatana na siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi wao akiwemo Lord Baden Powell ambaye alikuwa kiongozi wa Boy Scout pamoja na Kamishna Mkuu wa Girl Guides na Girl Scouts, Lady Olave Baden Powell (mkewe).

  “Tumepanga kuadhimisha siku hii muhimu kwa kufanya shughuli za kijamii zikiwemo za kutoa misaada kwa wahitaji, kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach na Magomeni na kupanda miti, kutoa elimu ya kujithamini, kujitambua na kukataza unyanyasaji pamoja na kutembelea kituo cha wazee wa Kigamboni,”alisema Bi. Rosaldina.

  Kwa upande wake Katibu wa chama hicho, Grace Shaba amefafanua kuwa chama hicho kimelenga kupanua uelewa wa wanawake kwa ujumla kuhusu uzalendo, majukumu ya nchi yao, kujenga ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia kambi za mafunzo, kutembelea na kuwasiliana kwa njia za teknohama pamoja na kuwa tayari kufanya kazi kwa manufaa yao na ya Taifa.

  “Dira yetu ni kuwa na jamii yenye wasichana na wanawake waliowezeshwa kufikia uwezo wa juu kabisa katika kutimiza malengo yao na kuwa rasilimali bora ya Taifa,”alisema Bi. Grace.

  Nae Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides Association, Symphorosa Hangi amesisitiza wanawake na watoto wa kike kujiunga na chama hicho kwani kinatoa elimu ya masuala ya kijamii na kiuchumi yatakayosaidia kuwainua wanawake na watoto pamoja na taifa kwa ujumla.

  Mpaka sasa kwa Tanzania,chama hicho kipo katika mikoa 22 kikiwa na jumla ya wanachama 101,824.
   Kamishna wa Makao Makuu wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Rosaldina Majuva alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya chama hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kutoka kulia Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa Hangi na Katibu wa chama hicho, Grace Shaba.

  Katibu wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Grace Shaba akifafanua kuhusu malengo ya chama hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni  Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa Hangi, kushoto ni  Kamishna wa Makao Makuu wa chama hicho, Rosaldina Majuva.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kikosi cha Yanga SC kinatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho asubui kuelekea nchini Comoro kwenye mji wa Moroni  tayari kwa mchezo wake wa kwanza ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Ngaya.

  Msafara utakuwa na wachezaji ishirini(20) benchi la ufundi nane( 8 )pamoja na viongozi wawili(2). Baada ya kikosi kuwasili kinatarajiwa kufanya mazoezi yake kesho jioni kwenye uwanja utakaochezewa mchezo siku ya jumapili.

  Wachezaji wanaoondoka kesho ni.

  Deogratius Munish,
  Ally Mustafa
  Deud Kaseke
  Haruna Niyonzima
  Thaban Kamusoko
  Amissi Tambwe
  Mwinyi Haji
  Saimon Msuva
  Geoffrey Mwashuiya
  Saidi Makapu
  Hassan Ramadhani
  Juma Mahadhi
  Yusuph Mhilu
  Obrey chirwa
  Nadir Haroub
  Justine Zulu
  Kelvin Yondani
  Juma Abdul
  Oscar Joshua
   Emmanuel Martin.

  Benchi la ufundi wanaoondoka ni:

  Kocha Mkuu George Lwandamina
  Kocha msaidizi Noel Mwandila
  Kocha msaidizi Juma Mwambusi
  Daktari wa timu Edward Samwel Bavu
  Kocha wa Makipa Juma Pondamali
  Meneja wa timu Hafidhi Saleh  
  Mtaalamu wa viungo Jacob Sospeter Onyango.
  Mohamed Omary Mwaliga

  Viongozi wanaosafiri.

  Mussa Mohamed  Kisoki (Tff)
  Paul Malume (Yanga Sc)a

  0 0


   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasisitiza watumishi wa umma nchini kutumia Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal)  alipokuwa akizindua Tovuti hiyo mkoani Dodoma leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) wakifurahia uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifuatilia maelezo kuhusu Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) baada ya kuizindua rasmi mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi  Stella Manyanya (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Karama Kenyunko.

  Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe amehukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni tano au akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

  Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Cyprian Mkeha.

  Hata hivyo, mshtakiwa Mgawe alifanikiwa kulipa faini hiyo na kuwa huru.
  Mahakama pia imemuachia huru naibu wake aliyekuwa anashughulikia huduma, Hamad Koshuma baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashataka dhidi yake.
  Akisoma huku hiyo, hakimu Mkeha alisema, upande wa mashtaka kupitia ushahidi wa mashahidi watano uliowasilishwa mahakamani hapo umeweza kuthibitisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa Mgawe alitenda kosa hilo la matumizi mabaya ya madaraka.

  Alisema katika ushahidi inaonesha wazi kuwa mshtakiwa  Mgawe alisaini  mkataba huo wa kibiashara na Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC), kwa ajili ya kuifaidisha kampuni hiyo.

  Katika utetezi wake, Mgawe alisema kuwa, yeye hakuwahi kusaini mkataba wa kibiashara kwa ajili ya ujenzi wa gati bali alisaini mkataba kwa ajili ya kupata mkopo ambao alipata baraka kutoka katika bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo na kuwa kitendo hicho hakikuipaatia serikali hasara yoyote.
  Hakimu Mkeha alisema kuwa haiwezi kubishaniwa kuwa, Mgawe alisaini mkataba kati ya TPA na CCCC   Desemba 5, 2011.

  Aliongeza kuwa mkataba huo ulikuwa kwa ajili  ya matumizi ya huduma za uhandisi, manunuzi pamoja na  ujenzi wa gati 13 na 14 .Kwa upande wa mashtakiwa wa pili, Koshuma Hakimu Mkeha alimuachia huru akidai kuwa mtuhumiwa alikuwa akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka ambayo hakuwa nayo.

  Katika ushahidi na vielelezo vilivyoletwa na mshtakiwa huyo inaonyesha kuwa aliteuliwa kuwa naibu Mkurugenze  Juni 1, 2012 huku upande wa mashtaka ukileta tuhuma kuwa mshtakiwa nae alisaini mkataba huo tarehe  Desemba 5, 2011.

  Aliwataka upande wa Jamuhuri kuhakikisha wanapeleleza  vya kutosha tuhuma zinazomkabili mtu  ili hata kama  ataachiwa na mahakama basi aachiwe kwa kuwa hana kosa siyo kwa mapungufu ya upelelezi.

  Awali ilidaiwa kuwa Desemba 5, mwaka 2011 Mgawe na mwenzake walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni ya upanuzi wa gati namba 13 na 14, katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC), bila kufuata taratibu za sheria ya manunuzi.

  Inadaiwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ya utumishi wa mamlaka hiyo kwa nafasi ya mkurugenzi mkuu na naibu wake.

  Aidha, katika hati ya mashtaka, watuhumiwa hao wanadaiwa kuweka saini mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo ya kichina bila zabuni shindanishi, ambapo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma namba 21 ya 2004, ambapo walitumia dola za kimarekani milioni 600. 
   Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe baada ya kukutwa na hatia ya kifungo ambacho kina faini sh.milioni tano ambapo ameweza kulipa faini hiyo na kuachiwa kuwa huru leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe akipongezana na aliyekuwa Naibu wa Mamlaka  ya Bandari  anashughulikia huduma, Hamad Koshuma ambaye   Mahakama pia imemuachia huru  leo   katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

  0 0

   

  Delighted to introduce Mr Mussa Loth Kaaya a k a Big Jahman. Born and raised in Arusha and is the 11th child born to a family of 12 children He is known for his artistry of Reggae, Ragga & Dancehall. He officially began engaging in the music industry back in 2000. He unloaded his first hit to which he named it "ANANIKUNYWA" feat MEDY PACK .. Although the hit single put Jahman in the music spotlight, but he continued to Hustle as an entrepreneur. 

  With that at hand he found himself in a position where one had to be set aside" unfortunately it had to be his music. 
  After remaining silent for three years he could not ignore his ongoing thirst and the passion of music, hence we saw him back in 2004 with another hit "SINA SENTI" to which he collaborated with his companion Rapper Fid Q (the most prolific Hip-hop artist to Emerge from Tz in East Africa) that were recorded at AKIL RECORDS studio, (Ilala DSM ) 
  "I can not deny the fact that it was somehow strenuous to keep my music alive and yet you are required to feed the belly, considering my entrepreneurship was growing at ridiculous speed, One had to make a choice! One had to multitask! One had to prioritise! I don't regret my decision to keep my music as Part time job" but I must admit I missed bringing pleasures to an audience...(consenting Jahman). 
  He continued to do collaborations with various artists including recording many hits in various studios back in 2013. Jahman met a producer from Sweden called FUNDI SAMUEL and recorded yet another "bullet" to which is known as "Sweet sweet" comprising Additional vocals from Saraha (musician from Sweden whose career in music originated in Tanzania and now has grown a good ambassador of Kiswahili in Europe) 
  Again .. entrepreneurial- continued to demand most of Jahman's valuable time, which he had to give it to... thus he took himself out of equation for another three years. But again; there is a beast which needs feeding! 
  And now in 2017 he has officially returned to the industry equipped with his own Studio ;titled MUSIC FARM. Jahman is adamant to step up and transform his music to a more professional level this time .. I will quote "some people entertain ideas others put them to work" - Jahman is on the second wording! He is the worker! He has decided to voluntarily sign under the label of CHEUSIDAWA .. to of which the C.E.O of the company is his buddy of all ages called Fid Q. Since he decided to return to the GAME he has decided to awaken our spirits by blessing us with another "HIT SINGLE" called #MABUNDI/OWLS.. missed bringing pleasure to an audience and as soon as our guests heard about my hit single they wanted to hear me play, but there it was., which was recorded and mixed at his own studio- MUSIC FARM and produced by an highly skilled new generation producer goes by the name ;STAR JAY .. MABUNDI/Owls went through verifications and mastering by all time FATHER oF BONGO FLAVA producer P-FUNK MAJANI .. MABUNDI/owls is one of the FEEL GOOD MUSIC but we can also insist this particular song has the etiquette of the feel of a "NIGHT LIFE VIBE" 

  We hope you enjoy it as much as we did and continue to do so.
  For bookings / comments or further questions feel free to contact with cheusidawatv @ gmail.com or call Phone

  +255653043117

  0 0


  0 0

  Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imekutana nakufanya kikao na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TPDC mjini Dodoma.
  Wataalam wa TPDC katika kikao hicho walipata fursa ya kuwasilisha mada za taarifa ya maendeleo ya miradi ya Shirika hilo.

  Aidha, katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Prof. Sufian Bukurura na Mkuu wa Taasisi ya Utafiti (REPOA) Dk. Donald Mmari waliwasilisha mada kuhusu utafiti walioufanya kuhusu Shirika la Mafuta la Taifa linavyoweza kujiendesha kwenye mazingira ya sheria mpya nchini.

  Akihitimisha kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa Kamati yake imepokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TPDC na kwamba Kamati itakaa nakuifanyia kazi.

    Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa akifungua kikao kulichoikutanisha Kamati ya PAC na TPDC mjini Dodoma

   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC, Prof. Sufian Bukurura akiwasilisha mada mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika kikao kilicho ikutanisha Kamati hiyo na TPDC mjini Dodoma.

    Mkuu wa Taasisi ya Utafiti (REPOA) Dk. Donald Mmari akiwasilisha Mada mbele ya Kamati ya PAC mjini Dodoma

  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakimsikiliza mtoa mada kutoka TPDC katika kikao hicho.

  0 0

  Mgeni rasmi katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu Kwa Watoa Msaada wa Kisheria katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo aliwataka wananchi kuwa wanajitokeza kutoa ushahidi katika kesi kutokana na kuwepo taarifa kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kuendelea kutokana na ushahidi kukosekana.
  Mkurugenzi wa shirika la PACESH Perpetua Magoke akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema shirika lake limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga dhidi ya ukatili wa kijinsia.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ni wakati mzuri sasa wananchi wakabadilika na kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika familia zao na jamii kwa ujumla
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akisisitiza jambo ukumbini Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akimkabidhi Kompyuta mpakato bwana Buyamba Ngogeja kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria katika kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya ya Kishapu.Laptop hizo zimetolewa na shirika mama la Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.
  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0
 • 02/10/17--10:59: HABARI KUTOKA TELEVISHENI
 • 0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. JohnMagufuli, wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Waziri Magemebe wakati wa misa hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, na kutokakulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Deogratius Rutta, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Iddi Juma na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo. Arnold alifariki dunia katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, Februari 5, 2017.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiifariji familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.

  0 0


  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James (pichani) akizungumza na wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu  kumlipa Mkandarasi anayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 3. 
  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya  Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo. 

   Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo. Picha na Mpiga picha Wetu


  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii  Timu ya Azam FC, imetia nanga mkoani Pwani, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho wapinzani wao Ruvu Shooting utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Mabatini mkoani humo.


  Mchezo huo nunaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 Alasiri utakuwa wanushindani mkubwa sana hasa baada ya Azam kukumbuka sare ya mechi ya awali iliyomalizika kwa goli 2-2.

  Kikosi cha Azam FC kimeondoka jana kikiwa na morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na mazoezi makali wanayopewa chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mromania, Aristica Cioaba, Msaidizi wake, Idd Cheche na Kocha Makipa, Idd Abubakar.


  Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa wanakwenda huko kuendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuichapa Ruvu Shooting.

  “Tunawaheshimu wapinzani wetu, tunajua upinzani wanaotuonyeshaga kila tunapokutana, lakini tumejipanga kufanya vizuri, rungu lililotumika kuua tembo ndilo litakalotumika kuua sisimizi, tunawaomba mashabiki wetu wasubirie kufurahi,” alisema.

  Hadi hivi sasa Azam FC imefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi 37 katika nafsi ya tatu kwenye msimamo ikilingana kwa pointi na Kagera Sugar iliyochini yake, inazidiwa pointi 12 na kinara Yanga aliyejikusanyia 49 na Simba iliyonafasi ya pili nazo 48.

  Msafara wa Azam FC umeondoka na jumla ya wachezaji 21, ambao ni makipa Aishi Manula, Mwadini Ally, Metacha Mnata, mabeki ni Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Yakubu Mohammed, Bruce Kangwa, Gadiel Michael, Ismail Gambo, Abdallah Kheri. 


  Viungo ni Nahodha Msaidizi Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Masoud Abdallah, mawinga Joseph Mahundi, Khamis Mcha, Ramadhan Singano na washambuliaji Yahaya Mohammed, Samuel Afful na Shaaban Idd.

  Wachezaji wengine waliobakia wameachwa kwa sababu mbalimbali, nahodha John Bocco, Salum Abubakar, Stephan Kingue, Daniel Amoah, wakiwa ni wagonjwa, huku winga Enock Atta Agyei kibali chake cha uhamisho kikiwa bado hakijawasili nchini.

  0 0
  0 0


  0 0

  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora,amewaagiza waganga wakuu wa wilaya za Mkoa huo kuhakikisha kwamba wanaume wote watakaougua na kulazwa Hospitalini kwa ugonjwa wowote ule,wawaambie kuwa ugonjwa huo unatokana na uchafu unaotoka kwenye sehemu za siri za mwanaume huyo kutokana na kutofanyiwa tohara.

  Katibu Tawala huyo,Dk.Thea Ntala alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

  “Nimewaagiza waganga wakuu wote wa wilaya kuwa mgonjwa yeyote mwanaume akiwepo Mheshimiwa diwani,akiwepo mheshimiwa mbunge wakilazwa pale Hospitali awe anaumwa jino,awe anaumwa sikio,awe anaumwa mkono mwambie hivi hili tatizo lako linatokana na uchafu unaotoka kwenye sehemu za siri kwa kutofanyiwa tohara”alisisitiza katibu tawala huyo.

  Kwa mujibu wa Dk.Ntala haiwezekani katika Mkoa wa Tabora wakaendelea kukaa na wanaume ambao mpaka sasa bado hawajafanyiwa tohara kwani kuendelea kukaa na watu wa aina hiyo kunachangia kwa namna moja au nyingine ongezeko la maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.

  “Hatuwezi kukaa Tabora,hatuwezi kukaa na hicho kitu na ndiyo maana ugonjwa huu wa Ukimwi unaendelea kutokana na sababu za kuendelea kuwepo kwa watu wasiofanyiwa tohara,nimewaagiza MADMO,RMO hili nimewaagiza wote Tabora kuhakikisha wanawafanyia uchunguzi wanaume wote wanaolazwa iwapo wamefanyiwa tohara”alifafanua huku akiwaacha waliohudhuria mkutano huo wakiangua kicheko.

  Hata hivyo Dk.Ntala alibainisha kwamba hivi sasa baadhi ya wanaume wamekuwa wakihudhuria kwenye semina kupatiwa elimu ya juu ya umuhimu wa kufanyiwa tohara huku wengine wakiamua kwenda kwa hiyari yao kufanyiwa tohara hiyo kwenye maeneo yanayotoa huduma hizo.

  Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa mabusha,Dk.Ntala alitumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kumeza dawa kwani dawa za ugonjwa huo zinatakiwa kumezwa na wanaume pamoja na wanawake na kuonya dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii ya kuamini kwamba ugonjwa wa mabusha hauwahusu wanawake bali unawahusu wanaume peke yao.

  “Madiwani mnisaidie kwenye mikutano wanawake wanafikiri ukiongelea ugonjwa wa mabusha ni wanaume,aah mwanamke anapata mabusha kwenye matiti yaani badala ya kuwa na saizi ya kawaida kama ya RAS anakuwa na saizi kubwa kama tikitimaji fulani hivi…sijui kama kuna watu wanapenda magodoro makubwa”alibainisha katibu huyo tawala.  Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya igunga,mkoani tabora wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo

  Mbunge wa jimbo la Manonga,wilayani Igunga,mkoani Tabora,Mhe.Hamisi Gullamali(wa kwanza kulia) wakiteta jambo na katibu wake wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Jengo la ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora, mahali kulikofanyikia mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani.
  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora,Dk.Thea Ntala akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na madiwani,watendaji wa Halmashauri ya wilaya pamoja na viongozi wa chama na serikali waliohudhuria mkutano huo wa kawaida wa Baraza la madiwani uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

  0 0

  * Waziri Mkuu asema Serikali haitamuonea mtu yeyote
  *Aomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za Serikali

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itapambana na janga la dawa za kulevya na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.

  Ametoa kauli hiyo leo jioni (Ijumaa, Februari 10, 2017) bungeni mjini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuahirisha mkutano wa sita wa Bunge la 11.

  Lengo la Serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri kwa maana ya wauzaji na wasambazaji. Dhamira ya Serikali ni kupambana na janga hili kwa dhahiri na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki,” amesema.

  Akizungumzia idadi ya watu ambao hadi sasa wamekwishakamatwa katika nchi mbalimbali, Waziri Mkuu amesema takwimu za jumla zinaonyesha kuwa Watanzania 515 wamekamatwa na kufungwa gerezani kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

  “Nchini China Watanzania walioko magerezani ni zaidi ya 200; Brazili kuna Watanzania 12; Iran wako Watanzania 63; Ethiopia Watanzania saba na Afrika Kusini wako Watanzania 296,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema moja ya hoja za Kamati za Kudumu za Bunge iliyojadiliwa na kuibua hisia kali katika mkutano huu wa Bunge ni kuhusu vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya na akawaomba Watanzania wote waiunge mkono Serikali juu ya vita hiyo.

  “Watanzania wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofika kiafya kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Vita hii inayopiganwa sasa dhidi ya uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizo,” amesisitiza.

  Amesema dawa hizo za kulevya, huingia zaidi kutumia njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipakani kwa njia ya magari binafsi au mabasi kupitia nchi za Kenya, Uganda na Mpaka wa Tunduma.

  Ameyataja madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa fahamu kwa mtumiaji ikiwamo kuchanganyikiwa, kuwa na ulevi usioponyeka kirahisi na kusababisha kifo kama mtumiaji atazidisha matumizi ya dawa za kulevya. “Madhara ya kiuchumi ni pamoja na gharama kubwa za kuwatibu waathirika wa dawa za kulevya, gharama kubwa za uchunguzi wa kimaabara kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na watumiaji wa dawa za kulevya kushindwa kujisimamia na kuendesha maisha yao,” ameongeza.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini zifanye maoteo na kuyawasilisha Bohari Kuu ya Dawa kabla au ifikapo tarehe 05 Machi 2017 ili kutekeleza azma ya Serikali ya kusambaza dawa kwa wakati.

  “Dhamira ya Serikali ya kusambaza dawa kwa wakati kwenye Halmashauri zetu haitafanikiwa endapo Halmashauri zitachelewa kuwasilisha maoteo ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi. naomba kutoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge, mpate wasaa wa kufuatilia mchanganuo wa usambazaji dawa katika Halmashauri zenu ambao hutolewa na Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,” amesema.

  Amesema hali ya upatikanaji wa dawa nchini inaendelea kuimarika huku akitolea mfano kiasi cha sh. bilioni 91 ambacho kimeshatolewa, kati ya sh. bilioni 251 zilizotengwa sawa na wastani wa sh. bilioni 20 kwa mwezi.

  Ili kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaatiba nchini, Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kununua madawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya mawakala.

  “Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba, utaratibu huo umeanza na tayari Serikali imekamilisha taratibu za kimkataba na wazalishaji watano wakubwa wa ndani ambao watanunua baadhi ya dawa kutoka ndani ya nchi, wakati mikataba mingine 76 ya wazalishaji wa nje iko katika hatua za mwisho. Matarajio yetu ni kwamba, utekelezaji wa mikataba ya nje utaanza katika mwaka wa fedha 2017/18,” amesema.

  Amesema kutokana na uamuzi huo wa Serikali pamoja na jitihada za Serikali za kuongeza bajeti ya ununuzi wa dawa, Bohari ya Dawa imeweza kununua aina 105 za dawa muhimu sawa na asilimia 78 ya aina 135 ya dawa muhimu zinazohitajika nchini.

  “Shabaha yetu ni kwamba, ifikapo Juni, 2017 usambazaji wa dawa muhimu nchini kote uwe umefikia asilimia 85. Taarifa hiyo imetolewa kwa kila Mheshimiwa Mbunge ili aweze kufuatilia kwa karibu dawa na vifaatiba vinavyoletwa na Serikali kwenye Halmashauri zenu,” amesema.

  Bunge limeahirishwa hadi Jumanne, Aprili 4, 2017.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  IJUMAA, FEBRUARI 10, 2017

older | 1 | .... | 1561 | 1562 | (Page 1563) | 1564 | 1565 | .... | 3284 | newer