Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

KOMREDI KINANA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA UWT TAWI LA SHIRIKISHO LA WANAFUNZI VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT, Tawi la Shirikisho la Wanafunzi vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, Anastazia Malamsha, wakati wa mazishi ya kiongozi huyo, yaliyofanyika leo katika eneo la  Shimbo, Rombo Mkuu mkoani Kilimanjaro. Anastazia alifariki dunia Jumapili, Feb 5, 2017,  katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoani huo ambapo pamoja naye viongozi wengiewatatu walifariki pia katika ajali hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa salama za rambirambi za kwake binafsi, CCM na Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli wakati wa mazishi hayo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoaheshima za mwisho kwa mwili wa Anastazia, kabla ya mazishi hayo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini wakati wa maziko.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Anastazia, mwishoni mwa maziko.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, wakiwa kwenye mazishi hayo. Anastazia alikuwa mwanafunzi wa Mwaka wa tatu katika chuo hicho Kikuu cha Ushirika Moshi.


NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT.ASHATU KIJAJI AZINDUA HUDUMA MPYA YA ‘ECOBANK MOBILE APP’

0
0
Ecobank Tanzania (ETZ) imezindua huduma mpya ya Ecobank Mobile App, hii ni njia rahisi na ya haraka ya kibenki kupitia simu za mkononi. Ecobank Mobile App itawawezesha wateja kufanya miamala mbalimbali ya kifedha ikiwemo kuhamisha fedha - kote baina ya matawi na baina ya benki, kununua muda wa maongezi, Malipo ya Ankara, kuangalia viwango vya kubadilisha fedha za kigeni, maombi na kuangalia taarifa za benki, Malipo ya kibiashara, pamoja na huduma za Kadi na hundi. 

Zaidi, Ecobank Mobile App itawawezesha wateja wa benki kuweza kuzifikia akaunti zao kupitia simu za mkononi na chaneli USSD, hivyo kuwahakikishia unafuu, upatikanaji, na kasi kwa saa 24 kwa juma huku ikiwaondolea ulazima wa kwenda au kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ambayo kwa sasa yapo nane (8).

Tukio hilo kwa sehemu kubwa lilihudhuriwa na halaiki ya watu ikiwa ni pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa Ecobank, Wateja na Wafanyakazi wa benki, Watendaji wa Kampuni ya Ecobank, Wanafunzi, Wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Wawakilishi kutoka Benki Kuu na washirika wa kibiashara wa benki hiyo.

Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alikuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo. Aliishukuru ETZ kwa ubunifu huo ambao, alisema utaenda mbali sana katika kuharakisha na kuimarisha juhudi za ushirikishwaji kifedha nchini Tanzania.

Aliipongeza benki hiyo kwa kuunga mkono juhudi na kauli mbiu ya awamu ya tano ya “Hapa kazi tu” kutokana na kuzindua bidhaa ambazo zimelenga kuwarahisishia maisha watanzania.
“Badala ya watu kubeba fedha mkononi sasa watabeba kidigitali” alisema na kuongeza kuwa utaratibu huu sio salama tu bali ni rafiki kwa kuokoa muda hasa katika kipindi hiki cha “Hapa kazi tu”.

Aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi katika kuhakikisha benki zinafanya kazi kwa usalama na kuunga mkono uchumi wa kutembea bila fedha taslim.

Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili ya kurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akipeana mkono na Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Bw. Peter Machunde mara baada ya kuzindua rasmi huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia (katikati) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ecobank-Afrika Bw. Ade Ayeyemi na Mkurugezi Mkuu wa Ecobank Tanzania Bw. Enoch Osei-Safo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa makini hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Programu hii ya kidijitali kutoka Ecobank ni mahususi kwa ajili yakurahisisha huduma za kibenki kwa njia ya haraka na usalama kupitia simu za mkononi.
Naibu Waziri wa fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akipakata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kuhusiana huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye programu ya kidijitali ya ‘Ecobank Mobile App’ iliyozinduliwa jana jijini Dar es salaam. Pamoja nae ni Kaimu Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania Bw. Peter Machunde.

DC KOROGWE AWAONYA WATUMISHI WA HALMASHAURI KUACHA KUTUMIA VIBAYA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO.

0
0
WATUMISHI katika Halmashauri ya wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wameonywa kuacha kutumia vibaya fedha za miradi zinazotokana na wafadhili kwenye maeneo yao kwani watakaobainika kufanya hivyo watashughulikiwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.


Hayo yalisemwa  na Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert  Gabriel wakati akipokea taarifa ya umalizaji wa majengo ya matatu ya maabara yalijengwa na taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayani humo.

Aidha wao kama viongozi wa serikali wilayani humo hawatakuwa na mdhara  na watumishi ambao watabainika kuihujumu miradi ya maendeleo inayopelekwa kwenye maeneo yao na wafadhili mbalimbali kwani kufanya hivyo kunachangia kurudisha nyuma kasi ya ukuaji wa maendeleo.

“Nisema wazi kuwa watumishi badilikeni kwani mimi kama kiongozi wa  wilaya hii sitamfumbia macho mtu yeyote ambaye atakuwa kikwazo cha maendeleo kwenye wilaya hii na niwaonye wenye tabia kama hiyo waiache mara moja.

Mkuu wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha Azidu Kaonekana wa pili kulia ambao wameshirikiana na A Better World kutoka Canada kufanya ujenzi wa majengo matatu ya maabara kwenye shule ya sekondari ya Patema iliyopo kata ya Mpale Wilayan
Kaimu Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Martha Kusare kulia akipokea msaada wa sola ya mobisol  kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka ikishirikiana na A Better World kutoka Canada kwa shule ya sekondari ya Patema ili kuweza kutumia nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi yao ambapo sola hiyo na ujenzi wa maabara tatu zilizojengwa na taasisi hiyo  iligharimu kiasi cha sh.milioni 75
Mkurugenzi wa Taasisi isiyoyakiserikali ya Vuga Development Initiative ya Jijini Arusha,Azidu Kaoneka akifuatilia maendeleo ya wanafunzi wa shule ya sekondari Patema wilayani korogwe Mkoani Tanga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TADB YAANZA KUTEKELEZA MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA MOROCCO

0
0
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeanza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano uliosainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa Ziara ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI alipotembelea Tanzania kwa mwaliko wa Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo mwezi Oktoba 2016.

Katika kutekeleza makubaliano hayo, ujumbe wa TADB ukiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Francis Assenga na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru upo nchini Morocco, pamoja na mambo mengine kuainisha maeneo ambayo Benki hiyo itashirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM) na kuwekeana mikakati ya utekelezaji. 

Kwa mujibu wa Bw. Assenga, pamoja na kupanga mikakati hiyo, ujumbe huo ulipata fursa ya kukagua miradi kadhaa ya kilimo na ufugaji ambayo Tanzania inaweza kuianzisha kwa mafanikio.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TAD, Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha, Bw. Albert Ngusaru (Watatu kushoto) wakiwa na wenyeji wao Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Morocco (GCAM).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga (wa pili toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Kilimo ya Morocco (Credit Agricole) Bw. Jamal Eddine Wl Jamali (Katikati). Wengine ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB  Bw. Albert Ngusaru na Wakurugenzi wawili wa Benki ya Credit Agricole Bi. Dkhil Mariem (Kushoto) na Bi Leila Akhmisse (Kulia).
Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ukipatiwa maelezo juu ya miradi ya kilimo inavyoendeshwa nchini Morocco wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga (Mwenye Kaunda Suti) na Bw. Albert Ngusaru Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha (Mwanye Daftari) walipotembelea Morocco wiki hii kuanza utekelezaji wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya TADB na GCAM.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania Bw. Francis Assenga (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Credit Agricole na Tamwil El Fellah wakati walipokagua miradi mbalimbali ya kilimo na ufugaji katika vijiji vya mji wa Khemisset nchini Morocco jana. Kulia kabisa ni Bw. Albert Ngusaru ambaye ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB.

NEWS UPDATE: MANJI, GWAJIMA WAENDELEA KUSOTA RUMANDE

0
0
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendeleea kuwashikilia Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji na Askofu Josephat Gwajima kwa zaidi ya saa 24 mpaka sasa.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema kuwa watu hao jana walifika hapo na kukutana na wapelezi .

“watu hawa wamehojiwa kuanzia jana mpaka saa za usiku kisha wakawekwa mahabusu  hivyo mpaka sasa ninavyozungumza wapo mahabusu wakisubiri utaratibu mwingine” amesema  kamanda Siro.

WIZARA YA FEDHA YAMLIPA MKANDARASI ANAYEJENGA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (TERMINAL 3) FEDHA ZOTE ANAZODAI.

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza na Wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu  kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya  Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya kuhakiki madai hayo.


 Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo.

Kamati ya Paralimpiki yaipongeza GAPCO kuhusu Kili Marathon

0
0
Kamati ya Paralimpiki Tanzania imeipongeza GAPCO Tanzania kwa mchango wake mkubwa unaohakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika michezo hususani mbio za Kilimanjaro Marathon.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Kamati hiyo, Tuma Dandi alisema wamekuwa na ushirikiano wa miaka saba sasa na GAPCO ambayo imekuwa ikiwafadhili  watu wenye ulemavu kushiriki katika mbio hizo.

“Sisi kama TPC tumeguswa mno na jitihada hizi za GAPCO kwani wamekuwa msaada mkubwa kwetu kwa muda wote huu na kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika michezo. Hii ni taasisi ya kuigwa ili kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu,” alisema na kuongeza kuwa  kuna michezo ya aina nyingi tu ambayo watu wenye ulemavu hushiriki na inahitaji udhamini.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania, Tuma Dandi akizungumza wakati wa kutoa shukrani kwa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO Tanzania kwa mchango wake mkubwa wa kuhakikisha watu wenye ulemavu hawaachwi nyuma katika michezo hususani mbio za Kilimanjaro Marathon. Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi.

Alisema kwa mwaka huu watafanya mchujo ili kupata wawakilishi watakaosafiri Moshi kushiriki katika Kilimanjaro Marathon. Mchujo huo utafanyika katika Uwaja wa Uhuru  Jumamosi Februari 11 kuanzia saa mbili asubuhi. Arusha na Moshi pia watafanya mchujo kama huu lakini siku na tarehe tofauti na hii ya Dar es Salaam.

 “Tunawaomba watu wenye ulemavu wajitokeze kwa wingi katika mchujo huu ambapo tutapata timu ya watu 37 watakaotuwakilisha kule Moshi Februari 26 katika mbio za Kilimanjaro marathon,” alisema.

Aliipongeza GAPCO kwa kuendelea kudhamini mbio za kilometa 10 kwa walemavu kwa miaka saba sasa kwani mbio hizo zimekuwa mwaka hadi mwaka.
Meneja Masoko wa GAPCO, Caroline Kakwezi alisisitiza kuwa GAPCO itaendelea kushirikiana na TPC na kuwema itagharamia usafiri, malazi na chakula kwa washiriki wote kutoka Dar es Salaam na kwa washiriki kutoka Moshi na Arusha watapewa usafiri.

Alisema GAPCO itaendelea kufanya kazi kwa karibu na kamati hiyo ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaendelea kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathon bila matatizo yoyote. “Tumeridhishwa na kazi wanayoifanya TPC na tuna kila sababu ya kuendelea kushirikiana nao,” alisema.

Mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuwa kubwa zaidi kushinda mwaka jana huku usaJili ukianzia Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mlimani City Februari 18 na 19 mwaka huu.

Mbali na GAPCO wadhamini wengine wa  Kilimanjaro Marathon 2017 ni, Kilimanjaro Premium Lager-42 km, Tigo 21km na Grand Malt kilometa tano. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel, Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Rwanda yapitisha muswada wa sheria ya kufanya Kiswahili kuwa lugha rasmi

0
0


Na. Immaculate Makilika -MAELEZO

Wabunge nchini Rwanda wamepitisha kwa kauli moja muswada wa sheria ya kuifanya lugha Kiswahili kuwa lugha rasmi nchini humo.

Kufuatia hatua hiyo, sasa Kiswahili nchini Rwanda kinakuwa moja kati ya lugha tatu za Kinyarwanda, kiingereza na kifaransa zinazozungumzwa na wananchi kama lugha rasmi miongozi mwao na kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya nne nchini humo.

Lugha ya Kiswahili nchini Rwanda inatazamiwa kuanza kutumika katika shughuli za uongozi na katika nyaraka za kiofisi.

Aidha, Waziri wa Michezo na Utamaduni nchini Rwanda, Julienne Uwaci alisema kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na lugha hiyo kuwa na wazungumzaji wengi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo kuweza kurahisisha ushirikiano katika sekta mbalimbali za maendeleo.

Aliongeza kuwa, “Kiswahili ni lugha rasmi ambayo nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatakiwa kuitumia kwa kuwa kitaongeza tija kwa nchi ya Rwanda kufaidi matunda ya utengano wa kiuchumi”

Wabunge mbalimbali wa nchi hiyo wametoa maoni, akiwemo mbunge Jean Baptiste Rucibigango ambapo alisema kuwa “Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki na hakika itakuwa na faida kuzungumzwa nchini Rwanda”.

Kiswahili kuwa lugha rasmi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, kunaleta faida nyingi ikiwemo kuongeza wigo wa shughuli za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi wananchama ambazo ni Tanzania, Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Sudani ya Kusini, pamoja na kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizi.

Hatua hiyo ya Rwanda kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya rasmi ya Taifa ni fursa ya adhimu kwa nchi jirani zinazozungumza zaidi Kiswahili ikiwemo Tanzania, kwani itasaidia raia wake kuwa na nafasi murua kushiriki katika shughuli za kibiashara na elimu.

MABALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WAKUTANA NA RAIS SHEIN

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Nchi mbali mbali (pichani) Rais akipeana mkono na Mhe,Balozi Emmanuel  John Nchimbi atakayekwenda nchini Brazil
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na   Mabalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania katika Nchi mbali mbali Duniani (Picha na Ikulu)

KINANA AMJULIA HALI DEREVA WA GARI LILILOPATA AJALI NA KUUA VIONGOZI WANNE WA CCM MKOANI KILIMANJARO

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimjulia hali jana, Jackson Kimambo ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari kutoka kwenye Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoani humo, Jumapili, Feb 5, 2017. Katika ajali hiyo watu sita walikufa wakiwemo viongozi wanne wa CCM ambapo Kinana yupo mkoani hapa, kuongoza mazishi ya vingozi hao. Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Sid Mecky Sadick
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini kitabu ha wageni Ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya KCMC ya Moshi, Kilimanjaro, Dk. Gileard Masenga (kulia), baada ya kumjulia hali dereva huyo
  Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya KCMC ya Moshi, Kilimanjaro, Dk. Gileard Masenga, akiwaaga Katibu Mkuu wa CCM Abdulraman Kinana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick, baada ya zara hiyo ya kumjulia hali, dereva huo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

KAMANDA SIRRO:UPEPELEZI BADO UNAENDELEA KWA WASHTAKIWA WA DAWA ZA KULEVYA

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AFANYA KIKAO NA WAFANYAKAZI WA WIZARA YAKE

0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi  Simba Yahya na Mwenyekiti wa chama hicho, William Mkombozi. 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi akizungumza na Wafanyakazi wenzake wa tawi hilo (hawapo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwenye idara yake wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mjumbe  wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanaidi Shabaani akiuliza swali kwa Katibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO

SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Rais Magufuli ateua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji

MBOWE AKANA TUHUMA ZA KUUZA NA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

WIZARA YA AFYA YAANZISHA KAMPENI YA HUDUMA YA UZAZI WA MPANGO

0
0
 Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu kampeni ya wiki moja ya kuhamasisha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango itakayoanza kesho tarehe 11 Kivunge Mkoa Kaskazini “A” Unguja, (kushoto) Afisa muhamasishaji kitengo shirikishi Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya Zanzibar Kasim Issa Kirobo.
 Wandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakisikiliza tarifa juu ya kampeni ya wiki moja ya kuhamasisha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango zitakayoanza kesho tarehe 11 Kivunge Mkoa Kaskazini “A” Unguja.
Mwandishi wa habari Mariyam Ame Chum kutoka ZBC TV akiuliza swali kwa Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil (hayupo pichani) kuhusu dawa za uzazi wa mpango na athari zake katika Mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

DKT. MPANGO AZIHIMIZA KAMPUNI KUCHANGAMIKIA FURSA ZA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM (DSE)

0
0
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezitaka Kampuni kubwa na za kati kuchangamkia fursa ya uwepo wa Sekta ya Soko la Mipaji, kwa kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es salaam ili kushiriki moja kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi.

Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Bungeni Mjini Dodoma, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mhe. Jamal Kassim Ali, aliyetaka kujua mchango wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa la Dar es saam (DSE), kwa wafanyabiashara wazawa.

Alifafanua kuwa kampuni kadhaa, ikiwemo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TOL Gases, Kiwanda cha Sigara (TCC), Kiwanda cha Saruji Tanga, Wakala wa Huduma za Mizigo kwenye viwanja vya ndege-Swissport na Benki ya NMB, ni baadhi ya kampuni zinazouza hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es salaam.

Dkt. Mpango alisema kuwa kampuni hizo zimechangia kukuza uchumi wa nchi ikiwemo ajira, kutoa gawiwo kwa Serikali na wanahisa, lakini pia ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa.

“Kwa mfano kwa mwaka 2015 NMB, ilitoa gawiwo Serikalini kiasi cha shilingi bilioni 16.5 na TCC shilingi billion 1.4 kwa hisa zinazomilikiwa na Serikali huku mapato yatokanayo na kodi pamoja na gawiwo, hutumiwa katika kutoa huduma mbalimbali ambazo jamii ikijumuisha wafanyabiashara wadogo hunufaika nazo”alisema Dkt. Mpango

“Vilevile, Serikali imekuwa ikitumia masoko ya mitaji kama chanzo cha upatikanaji wa fedha za bajeti (Treasury Bonds), Miradi inayotekelezwa na fedha hizi, pamoja na mambo mengine, imekuwa ikitoa ajira na fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara wazawa; wadogo na wa kati” aliongeza Dkt. Mpango

Dkt. Mpango, alibainisha kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni ndogo ndogo katika kukuza uchumi wa nchi ndio maana mwaka 2013 Soko la Hisa la Dar es Salaam lilianzisha dirisha linaloziwezesha kampuni ndogo na za kati za wazawa zisizokidhi vigezo vya kujiunga na soko hilo kupitia dirisha kuu, kutumia Soko la Hisa katika kupata mitaji kutoka kwa umma wa watanzania.

Dkt. Mpango alibainisha kuwa watanzania wengi wananufaika na uwepo wa soko la hisa, na kushiriki moja kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi huku akizitaja baadhi ya kampuni zilizonufaika na utaratibu huo wa dirisha dogo la hisa  kuwa ni Benki ya Mwalimu Commercial Bank, Swala Oil and Gas Tanzania, Maendeleo Bank PLC, Yetu Microfinance na Mkombozi Commercial Bank, ambazo zina jumla ya mitaji isiyopungua shilingi bilioni 120.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

DC ARUMERU ALEXZENDER MNYETI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE KAYOMBO

0
0
Na Mathias Canal, Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Pastory Mnyeti amezuru kijiji cha Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kutoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Kayombo aliyefariki Dunia siku ya saa mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mkoani Mwanza.

Mhe Mnyeti ametoa salamu za pole kwa wakazi wa Kijiji cha Misasi kwa kumpoteza mshauri katika kijiji hicho ambaye amekuwa nguzo kwa maendeleo ya kijiji sawia na utaratibu wake wa kuhamasisha wananchi kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mnyeti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi kabla ya uteuzi wake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameeleza jinsi alivyomfahamu Mzee Kayombo katika kuhakikisha jamii inasonga mbele katika maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Mnyeti alisema kuwa Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye pia atakumbukwa kwa kazi njema alizozifanya wakati wa uhai wake.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Mnyeti akisaini kitabu cha maombolezo kijijini Misasi
 Dc Mnyeti, MD Kayombo na familia nzima ya Mzee Kayombo walipotembelea kaburi la Mzee Kayombo
 Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Alexzender Mnyeti (Kushoto), na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakiwa katika mazungumzo
 Dc Mnyeti akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Kayombo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MAJISAFI KATIKA MAENEO YA MAKONGO JUU NA GOBA

0
0
Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), linawatangazia wakazi wa Maeneo ya Makongo na Goba jijini Dar es Salaam kuwa kuna tatizo la upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo tajwa hapo juu, kuanzia siku ya Alhamisi tarehe 09/02/2017.

Sababu ya kukosekana kwa huduma ya Maji inatokana na hitilafu ya Pampu ya kusukuma Maji .Mafundi wetu wanaendelea na jitihada ili kuhakikisha huduma ya Maji inarejea.

Maeneo yaliyoathirika na hitilafu hii ni Goba Kunguru, Goda Kinzudi, Makongo Juu yote, Mbezi Juu eneo la Baraza la Mitihani na Eneo la Mnara wa Voda.

DAWASCO INAOMBA RADHI WANANCHI WA MAENEO HUSIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (BURE), Pamoja na Dawati la huduma kwa Mteja DAWASCO  Mkoa wa Kawe 0743-451861.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

Waziri Mkuu Azitaka Taasisi za Umma Zinazodaiwa na TTCL Kulipa Madeni Yao Kabla ya Juni 30, 2017

0
0

Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka Taasisi zote za Umma ambazo zinadaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuhakikisha zinalipa madeni yao kabla ya Juni 30, 2017.

Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo, Mjini Dodoma katika viwanja vya Bunge wakati wa uzinduzi wa huduma ya 4G LTE za kampuni hiyo ya simu kwa Mkoa wa Dodoma.


“Kuhusu shilingi Bil. 11.5 ambazo TTCL inazidai Taasisi mbalimbali za Umma, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, kaa na wadaiwa sugu wote, thibitisheni madeni husika kisha mkubaliane namna ya kulipa madeni hayo. Nijuavyo kila Wizara inatenga bajeti kwa ajili ya ankara za simu, sasa hayo malimbikizo yanatoka wapi?” alisema Kassim Majaliwa.


Aidha amezitaka Taasisi hizo zinazodaiwa na TTCL kuhakikisha zinakamilisha madeni yao kabla ya kufikia Juni 30, 2017 ili kampuni hiyo iweze kufanya kazi ipasavyo na kuendana na ushindani wa kibiashara uliopo.Pia, ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka kwenye makampuni binafsi namna yanavyoendeshwa na kuiga baadhi ya mbinu zao, hususan katika kupunguza gharama za uendeshaji. 


Kassim Majaliwa amesema kwamba, Serikali ina matarajio makubwa kutoka katika kampuni hiyo kutokana na kuwa na imani kwamba kampuni hiyo ina maarifa ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa kwenye sekta hiyo.


Vile vile ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka katika mashirika ya Umma ya Simu kwenye nchi nyingine ambayo yanajiendesha kwa faida, kwa kuiga mbinu ambazo wanazitumia na kuziweka katika muktadha wa nchi ya Tanzania.


Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa pamoja na timu yake kwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia. Aidha amemtaka Waziri huyo kufuatilia kwa karibu kampuni hiyo ili iweze kutoa ushindani wa kutosha kibiashara, ijiendeshe kwa faida, itoe gawiwo stahiki kwa Serikali, ilipe kodi na zaidi ya yote fedha za Umma zilizowekezwa ziweze kutumika vizuri.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa   Mtandao wa 4G LTE  wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Edwin Ngonyani na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa   Mtandao wa 4G LTE  wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Edwin Ngonyani, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.
 Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto),Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijadiliana jambo na Mawaziri wenzake muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images