Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109573 articles
Browse latest View live

Lady in Red Fashion show 2017 yafana jijini Dar es salaam


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARY 12,2017

KUMBE HATA KWA WATANI NAKO MAMBO NI YALE YALE....

0
0
Huyu ana "overtake" katika sehemu ya hatari na huku mbele kukionekana gari zikija upande huo.
Huyu nae anataka kuingia barabara kubwa bila tahadhali.

SAGCOT yawataka wanahabari kuzitangaza fursa kaitika kilimo

0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT),Bw.Geoffrey Kirenga akiwasilisha mada kwenye Semina elekezi iliyoandaliwa na Kituo kwa Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu shughuli za SAGCOT katika kuendeleza kilimo na fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo mwishoni mwa wiki.
Mhariri wa Habari wa Gazeti la Mwananchi, Bw.Reginald Miruko akichangia mada katika Semina elekezi iliyoandaliwa na Kituo cha Mpango wa uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa kusini mwa Tanzania(SAGCOT) kwa wahariri na waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu shughuli za SAGCOT katika kuendeleza kilimo na fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo.Kulia kwake Mhariri wa Biashara Gazeti la Citizen,Bw.Samuel kamndaya.
Mhariri wa habari za Biashara wa Kituo cha Channel ten,Bi.Easter Zelamula akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT),Bw.Geoffrey Kirenga mara baada ya kumalizika kwa Semina iliyoandaliwa na Kituo kwa Wahariri na Waandishi waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufahamu shughuli za SAGCOT katika kuendeleza kilimo na fursa zilizopo kwenye sekta ya kilimo.Kushoto ni Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Bw.Kulwa karedia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Mpango wa Uendelezaji Kilimo katika Ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT),Bw.Geoffrey Kirenga akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari nchini mara baada ya kumaliza semina ya siku moja iliyolenga kutoa elimu kwa waandishi hao juu ya kazi na majukumu ya SAGCOT katika kuendeleza kilimo ili kiwe na tija kwa mkulima na Taifa kwa ujumla.

MAISHA YA FAMILIA YA WATU WA JAMII YA MAASAI

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAICHANGAMKIA SMART BOMBA YA VODACOM TANZANIA

0
0
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Edisa Mathias(kulia)akimpatia maelekezo Mkazi wa Machava Kigamboni jijini Dar es Salaam,James John,Juu ya huduma bora zinazotolewa na mtandao huo Wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za bure kwa kipindi cha miezi 3.
Mkazi wa mji mwema kigamboni jijini Dar es Salaam,Shabani Hussein akisajiliwa namba ya simu yake jana na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania, Armoury Shabani wakati wa promosheni ya simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za bure kwa kipindi cha miezi 3.
Mkazi wa Vijibweni kigamboni jijini Dar es Salaam,Fred Anthony akifafanuliwa jambo jana na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Edisa Mathias,Juu ya ubora wa simu mpya aina ya Smart Bomba ya kampuni hiyo yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za bure kwa kipindi cha miezi 3.

RC KILIMANJARO NA KAMISHNA MTEULE WA MAMLAKA YA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA WATEMA CHECHE

0
0
Kamishna Mteule wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya,Rogers William akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoezi kwa wananchi mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


SIKU chache  baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (Drug Control and enforcement Authority), Rogers William ameanza kutema cheche dhidi ya Wafanyabiara na watumiaji wa dawa za Kulevya.

Kamishna huyo  ametangaza kushughulika kikamilifu na baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro,wanaowatumia wanawake wajasiriamali wanaosafirisha mazao kwenda mikoani, kubeba Mirungi ama Bangi ndani ya mizigo ya mazao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck Sadiki akizungumza juu ya Dawa za kulevya mara baada ya kumalizika uzinduzi rasmi wa siku ya mazoezi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan.

William alitoa kauli hiyo wakati wa mazoezi katika uwanja wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) baada ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro , Saidi Mecky Sadiki kutoa nafasi kwa Mkuu huyo wa usalama wa taifa mkoa wa Kilimanjaro , baada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake.


“Tunayo orodha ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wengine wananchi wa kawaida wanaowatumia wanawake wasio na hatia kusafirisha dawa za kulevya kama Mirungi na Bangi kwenda mikoani….hilo nitahangaika nalo mara nitakaporejea mkoani hapa katika mapambano dhidi ya vita hii”alisema Sadiki.

Kauli ya William ilifuatia baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck Sadiki kulitaka jeshi la Polisi kufaya uchungizi wa kina ili kuwaachia baadhi ya wanawake watakaobainika kutokuwa na hatia ama kufahamu kama walitumika kusafirisha dawa za kulevya bila ridhaa yao.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna msaidizi Mwandamizi wa  Polisi,Wilbroad Mutafungwa akitoa salamu za jeshi hilo katika uzinduzi huo.


Akizungumzia kuhusu Dawa za kulevya,Sadiki alisema vita dhidi ya dawa  za kulevya za aina mbalimbali kwa mkoa wa Kilimanjaro imeanza muda mrefu na tayari zaidi ya watuhumiwa 689 wa dawa hizo wanashikiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari mwaka 2016 hadi Januari 2017.

Sadiki alisema vita hiyo ni ya kudumu yenye changamoto kubwa baada ya mkoa wa Kilimanjaro kuwa na njia nyingi za Panya katika mipaka baina ya Tanzania na Kenya, huku ikizingatiwa kwamba Kenya inalitumia zao la Mirungi kama biashara halali.

WAZIRI MKUU, MAWAZIRI KUONGOZA MAPAMBANO DAWA ZA KULEVYA

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha cheo kipya aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro Dkt. Anna Peter Makakala kabla ya kumuapisha kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro Dkt. Anna Peter Makakala kuwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw.Rogers William Sianga kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Ikulu Jijini Dar es Salaam. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw.Rogers William Sianga akisaini hati ya kiapo baada ya kuapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam.  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Omar Yusuf Mzee baada ya kumteua kuwa balozi Leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Joseph Sokoine baada ya kumteua kuwa balozi Leo Jijini Dar es Salaam. 
Viongozi walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakila kiapo cha Maadili katika utumishu wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela .


WAZIRI MKUU AKABIDHIWA KAZI YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

0
0
 Jacquiline Mrisho na Eliphace Marwa – MAELEZO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemkabidhi Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kazi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya akiwa kama Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Dawa hizo nchini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji, Anna Peter Makakala, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William Sianga pamoja na mabalozi watatu Mhe. Omary Yusuph Mzee, Mhe.Joseph Edward Sokoine pamoja na Mhe. Grace Aron Mgovano aliowateua hivi karibuni.

Dkt. Magufuli amesema kuwa Waziri Mkuu anatajwa kwenye Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa ni Mwenyekiti wa Tume hiyo ambapo Wajumbe wake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Elimu ana Mafunzo ya Ufundi, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

“Nalipongeza sana Bunge la kipindi cha mwaka 2010 – 2015 chini ya Spika mstaafu, Mhe. Anne Makinda lililopitisha Sheria hii baada ya kuona sheria za mwanzo za kupambana na dawa za kulevya hazina nguvu hivyo Wabunge wa wakati ule walisimama kwa pamoja bila kujali itikadi za vyama vyao wakapitisha sheria hii,” alisema Dkt. Magufuli.

Aidha, Dkt. Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa kusaini sheria hiyo haraka mara baada ya Bunge hilo kuipitisha kwa sababu alijua madhara ya dawa za kulevya katika nchi yetu.

Amefafanua kuwa sheria imeeleza wazi katika kifungu cha 10 cha Sheria Na.5 ya mwaka 2015 kuwa jukumu la kupambana na dawa za kulevya linasimamiwa na Serikali pekee yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya au mtu yoyote atakayekuwa amepewa mamlaka ya kusimamia Serikali.

Kwa upande wake Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa Taifa limeendelea kushuhudia kizazi chetu kikiendelea kudidimia kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya na Serikali kwa mipango yake imeendelea kukemea, kudhibiti na kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya wazalishaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa dawa hizo.

“Jambo hili limeleta athari kubwa sana kwani vijana wetu wengi wamepoteza uwezo wa kujisimamia katika shughuli zao za maendeleo kwa sababu baada ya matumizi tumeona athari kadhaa zikiwezo za kudhoofishwa kwa mwili, uwezo wa kutafakari pamoja na kutoweka kwa uwezo wa kufanya kazi,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa Taifa hili la Watanzania kwa kiasi kikubwa linawategemea vijana waweze kuleta msukumo wa maendeleo ndani ya nchi hivyo jambo hili likiachiwa linaweza kuleta athari kubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo yetu kwa ujumla wake.

Alisisitiza kuwa vita hii ilianza, inaendelea na itaendelea kupiganwa hadi imalizike hivyo Watanzania hawana budi kuunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na Serikali kuhakikisha wanatokomeza uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi yake kwa namna yoyote ile, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu ili kubaini matumizi ya dawa za kulevya ndani ya nchi hii. 

RAIS DKT. MAGUFULI AMWAPISHA KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI, KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA MABALOZI WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Rogers William Sianga Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Joseph Sokoine kuwa Balozi mpya nchini Ubelgiji, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Omar Yusuph Mzee kuwa Balozi mpya nchini Algeria, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Grace Mgovano kuwa Balozi nchini Uganda, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

KIPINDI MAALUM HOTUBA YA RAIS DKT MAGUFULI BAADA YA KUMUAPISHA KAMISHNA WA DAWA ZA KULEVYA

MNADA WA PILI WA KIMATAIFA WA MADINI YA TANZANITE WAFANYIKA JIJINI ARUSHA

0
0
Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imefanya Mnada wa pili wa kimataifa wa madini ghafi ya Tanzanite kuanzia tarehe 9 – 12 Februari 2017. Mnada huo umefanyika katika kituo cha Jemolojia (TGC) kilichopo jijini Arusha.

Kampuni tatu zinazochimba madini ya Tanzanite ambazo ni Tanzanite One Mining Company Ltd, Mathias J Lyatuu Mining na Tanzanite Africa Ltd; zilileta jumla ya gramu 990,444.04 za madini ghafi kwenye mnada huo kwa ajili ya mauzo.

Baada ya taratibu za mnada, jumla ya gramu 990,039.04 za Tanzanite ghafi ziliuzwa kwa Dola za Marekani 4,202,287.13. Hii ni sawa na 99.9% ya madini yote yalilyoletwa kwa ajili ya mauzo. Kutokana na mauzo hayo, Serikali inatarajia kukusanya mrabaha wa Dola za Marekani 210,114.36 sawa na Shilingi 466,453,871.43. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Simajiro inatarajia kulipwa Shilingi 27,987,232.29 kama Kodi ya Huduma.

Kampuni 68 kutoka nchi saba duniani ambazo ni Tanzania, Kenya, India, Sri Lanka, China, Uswisi na Ujerumani zimeshiriki katika mnada huo.

Article 0

POSHO ZA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA WILAYA YA MBINGA MILIONI 47 KATIKA VIKAO VYA BAJETI, WAMEAMUA ZIENDE KUMALIZIA MILADI

0
0
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, wameamua kutochukua posho zao za vikao viwili vya bajeti ambazo ni shilingi milioni 47, badala yake ziende zikatumike kumalizia miradi ya maendeleo ambayo imesimama katika halmashauri hiyo. Kwa undani wa habari hii hii hapa video yake.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARY 13,2017


Utamaduni wa Mtanzania ni Sehemu ya Kivutio cha Utalii: Waziri Nape.

0
0
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.

Serikali chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali mapato.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.

“Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi zetu”Alisema Waziri Nape.Aidha ameongeza kuwa Wizara yake itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni na kuziendeleza kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya ya nchi kama ilivyofanyika katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na Wasanii.

Kwa upande wa wake Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.

“Tumejifunza utamaduni wa kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.

Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana. 

WALIOTAJWA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO HAWA HAPA

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika  kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro .

Akitangaza majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa hao tayari wamekamatwa na wako katika hatua mbalimbali za kiupelelezi na taratibu zikikamilika watafikishwa mahakamani.

Miongoni mwa watuhumiwa 47 wamo watoto wawili  waumri wa miaka 17 ambao ni Wilfred Mnubi mkazi wa Bomang’ombe wilaya ya Hai na Ruben Bakari mkazi wa Njoro katika manispaa ya Moshi.

Kati ya watuhumiwa hao wanawake ni 15 na wanaume ni 32 akiwemo mzee mwenye umri wa miaka 60,Christina Ferdinand.

“Vita hii tumeianza tangu mwaka juzi,tunajua vita hii ni kubwa bahati nzuri ni kwamba njia wanazotumia wafanyabiashara wa dawa za kulevya husani mirungi na bhangi ,tayari jeshi la polisi limezibaini,maeneo ambayo dawa za kulevya zimekithiri Jeshi la polisi limekwisha baini ,operesheni hii ambayo tumeianza ni endelevu na tutaendelea kuwakamata watu hawa kwa kutumia mbinu zote tulizonazo.”alisema Mutafungwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza juu ya msako mkali ulioanza wa kuwakamata wafanyabiashara wa dawa za kulevya katika mkoa wa Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akinyunyiza marashi juu ya Mirungi iliyofungwa katika vipande vya magazeti ikiwa ni mbinu mpya inayotumiwa na wasafirishaji wa bidhaa hizo.
Baadhi  ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne.
Sehemu ya Misokoto ya Bhangi iliyokamatwa wakati wa opereshni hiyo .



Waliotajwa na kushikiliwa na jeshi la Polisi ni pamoja na:
(1)         Juma Kabwele(25).
(2)         Mohaed Kabwele (29) .
(3)         Shabani Mponda(39).
(4)         Khadija Mushiri(27).
(5)         Veronika Chuwa (39).
(6)         Mwanahamis Hussein.
(7)         Yusuph Issa(42).
(8)         Salim Massawe(48).
(9)          Hadija Mohamed(50).
(10)       Shenein Abilah(41).
(11)        Husna Mgonja(24).
(12)       Najima Desouza (46) .
(13)       Ruben Bakari (17) .
(14)       Paul Kisoka (26).
(15)       Raphael Mbuya (40).
(16)       Wilfred Mnubi(17).
(17)       Athuman Swaehe (35).
(18)       Joseph Hamis(20).
(19)       Zuber Temu(27).
(20)      Robert Kitika (18) .
(21)       Mohamed Juma (25).
(22)       Ahmad Shaban (57).
(23)      Donas Masashua(22).
(24)      Japhet Tungai (46).
(25)      Asima Mndeme (24).
(26)      Muutaz Zalia ,
(27)      Noah Singano (29).
(28)      Ramadhan Masale (40) .
(29)      Kirambati Swai(45).
(30)      Said Mrii.
(31)      Erick Henry (20).
(32)      Seif Ally(20).
(33)      Ramadhan Hassan (36).
(34)      Victor John(22).
(35)      Upendo Endkia (42).
(36)      Asia Ally(39).
(37)      Catherine Linusi (36) .
(38)      Mariam Hemed (44) .
(39)      Mwajuma Msuya (48).
(40)      Juma Yusuph (22) .
(41)      Hussein Anyokisye (17).
(42)      Musa Msangi (30).
(43)      Ramadhani Hassan (36).
(44)      Wilfred Munubi(17)
(45)       Ruben Bakar.(17)
(46)       Christina Ferdinand.(60)
(47)       Samweli Kingai(42).

BANK OF AFRICA TANZANIA YAFUNGUA MATAWI MWANZA NA MOROGORO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba yake katika halfla ya uzinduzi rasmi wa matawi mawil ya Bank of Africa Tanzania.

Akizungumza mkoani Mwanza, wakati akizindua matawi mawili kwa pamoja ya Bank of Africa Tanzania tawi la Nyanza lililopo jijini Mwanza na wakati huo huo tawi la Uluguru lililopo jijini Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella alisema ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki na kwamba Mwanza ni ya pili kuchangia katika pato la taifa.

“Nimesikia kwamba mna matawi 27, huu ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki. Naomba mfahamu kwamba Mwanza inachangia asilimia 7 ya pato la taifa. Bank of Africa Tanzania natambua kuwa mnasaidia juhudi za serikali kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi,”alisema Mh. Mongella.

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania Wasia Mushi akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Mwanza zawadi ya Visa Prepaid Card (TOUCAN CARD) ambayo itamwezesha mkuu huyo wa mkoa kufanya online purchases pamoja na kupata huduma za kifedha kwenye ATM machine Zaidi ya Milioni tatu zilizopo sehemu mbalimbali duniani.

Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa matawi hayo kwa pamoja, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi alisema : “Benki ya Afrika ipo katika nchi 18 na kwamba makao yake makuu yapo Dakar, Senegal. Hapa nchini ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam na jumla ya matawi 27.”
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella akizindua rasmi tawi la Nyanza-Mwanza na lile la Uluguru-Morogoro.

Mushi alisema katika kipindi cha miaka 10 benki hiyo imekuwa benki muhimu, imara endelevu kwa kutoa huduma zake za kibenki kwa watu mbalimbali wakiwamo wateja wakubwa, wadogo na wa kati.

VALENTINE'S DAY AT SHEKINAH GARDEN, MBEZI BEACH (MAKONDE)

WANANCHI WA MKOA WA DODOMA WAPIMA AFYA ZAO KATIKA BANDA LA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE NA KUPATA ELIMU YA AFYA

0
0
Mtaalamu wa Afya na Mazoezi ya viungo kutoka Chama Cha Wafanya Mazoezi Tanzania Waziri Ndonde akiwaelekeza wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) umuhimu wa kufanya mazoezi na aina ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Mtaalamu wa Dawa na Tiba kutoka Hospitali ya SANITAS Dk. Sajjad Fazel akiwafundisha wananchi waliokuwa wanasubiri kwenda kupima magonjwa ya moyo katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) aina ya vyakula bora wanavyotakiwa kula ili waepukane na magonjwa yasiyoambukiza. Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto hivi karibuni ilizindua kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo kwa muda wa siku mbili kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Andrew Kabeho akimpima mapigo ya moyo Afisa Muuguzi wa Hospitali ya mkoa wa Dodoma Mariam aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupima magonjwa ya moyo. JKCI ilishiriki katika kampeni ya kitaifa ya kufanya mazoezi na kupima afya bila malipo iliyoandaliwa na Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto na kufanyika katika uwanja wa Jamhuri jumla ya wagonjwa 408 walihudumiwa katika banda hilo.

Viewing all 109573 articles
Browse latest View live




Latest Images