Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEBRUARY 9, 2017


BREAKING NEWZZZ: MANJI AJISALIMISHA POLIS KUTII AGIZO LA MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu Yusuf Manji amefika katika kituo cha kati (Central Police) kwa ajili ya mahojino.Manji ambaye ni mwenyekiti wa klabu ya Yanga aliwasili majira ya saa 5 asubuhi akiongozana na mawakili wake.Baada ya kuwasili, Manji alisalimiana na wanachama wa klabu ua Yanga na kuingia moja kwa moja kituoni kuendelea na taratibu nyingine.
 Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye mwenyewe kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijuma kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Gari aliyowasili nayo Yusuf Manji.
 Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho
 Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi Kati.Picha na Hamphrey Shao- Globu ya Jamii.

UKAGUZI WA MABASI KATIKA I KITUO CHA UBUNGO WAPAMBA MOTO , ABIRIA WAPONGEZA UKAGUZI WA MABASI

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

Abiria wa walioshushwa  katika basi la Shukurani Coach linalofanya safari zake Dar kuelekea mikoa ya Kusini wamesema ukaguzi unaofanyika katika kituo cha mabasi ubungo ni mzuri kwani safari yao isingekuwa  nzuri kama wangeweza kupita bila kukaguliwa.

Akizungumza na Michuzi Blog, Shinza Lymo amesema kuwa utaratibu wa ukaguzi kabla ya basi kondoka uendelee kwa wamiliki watakuwa hawapeleki basi katika kituo hicho na kuwa wameweepusha abiria na ajali zinazotokana na uzembe.

Nae Halima Bakari amesema kuwa katika siku ambayo hatasahau ni kuzuiwa kwa basi hilo ambapo leo kitu ambacho kingetokea ni makosa ya watu kushindwa kufanya matengenezo ya mabasi wakati yanaingia katika kituo hicho .

Amesema jeshi la polisi wamekuwa makini katika kuhakikisha wanaokoa roho za watu ambao wanasafiri na vyombo vya moto hasa mabasi ya mikoani ambayo basi moja linabeba roho 100.

Kwa upande wa dereva Simwanzi Minja amesema kuwa jeshi la polisi limenyoosha wamiliki wa mabasi ambao hawataki kupeleka mabasi  yao Gereji na kituo  cha ukaguzi wa mabasi  cha ubungo kinazua safari.
Amesema kuwa kutokana na ukaguzi huo ajali zimepungua zinazotokana na mabasi mabovu kubaki matatizo ya kibinadamu ambayo nayo yamedhibitiwa ipasavyo.

Chami amesema kuna siku alimwambia mmiliki wa basi kuwa basi lake linamatatizo alikata na kuamuka kuita polisi kufanya ukaguzi ili walizuie kufanya safari kabla hajafanyiwa ukaguzi akiwa na abiria.
 Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akimueleza Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix  juu ya utaratibu wanaoufanya katika ukaguzi wa magari na kuwapongeza kwa hatua wanazozichukua kwa basi itakayoonekana na tatizo leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita ,Mponjoli Mwabulambo akiangalia ukaguzi unaofanywa katika kituo cha mabasi ubungo kabla ya mabasi hayo hayajaanza safari leo jijini Dar es Salaam na Basi hilo ni Shukrani  Coach ambalo limezuiliwa kufanya safari zake leo baada ya kubaini usukani wake hauko leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix akikagua injini ya basi kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

NIC WAPIGANA MSASA MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikala Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza katika mkutano wa Mameneja wa NIC uliofanyika Morogoro jana.Kushoto ni Romanious Hokororo, Kaimu Mkurugenzi wa Bima za Ajali na Mali .
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Sam Kamanga (hayupo Pichani) wakati wa mkutano wa Mameneja wa NIC uliofanyika Morogoro jana. 

Chief Justice and President of the Supreme Court of Kenya visits African Court

$
0
0
President of the African Court on Human and Peoples’ Rights Hon. Justice Sylvain Orě  (R) explains an issue to the visiting Chief Justice  and President of the Supreme Court of Kenya Hon David Maraga in Arusha on 8 February, 2017.   Hon. Justice Maraga was on a familiarization tour of the Court (Photo by a Correspondent). 

STEVE NYERERE EAST AFRICA STAND UP COMEDY

Viwanda Vitajengwa na Sekta Binafsi – Mwijage.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO-Dodoma.

Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema kuwa viwanda vitajengwa na Sekta Binafsi, na kazi ya Serikali ni kutengeneza mazingira mazuri ya kujenga Viwanda.

Mwijage ameyasema hayo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa majibu kuhusu ufinyu wa bajeti wa Wizara hiyo ikiwa itatosheleza kujenga Viwanda nchini, wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.

Mwijage amesema kuwa, kazi kubwa inayofanywa na Serikali kufikia uchumi wa Viwanda ni kutengeneza mazingira mazuri ya kujenga viwanda ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wawekezaji ambapo mpaka sasa Serikali imeshaongea na wawekezaji toka China, Uturuki na Misri na wote wameonyesha nia ya kujenga viwanda nchini.

Kwa upande wake Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema kuwa ni jukumu la kila kiongozi kushiriki katika ujenzi wa Viwanda kwa kutambua fursa zilizopo eneo ambalo analisimamia.

“Sera ya kuwa na Tanzania yenye Viwanda haitawezekana kwa kuiachia Wizara ya Viwanda peke yake bali kwa sisi wabunge pia kushiriki kupitia fursa ambazo zinatuzunguka,” alifafanua Ridhiwani.

Vilevile amesema kuwa ni muhimu Serikali kuendelea kuboresha hali ya umeme kwani Viwanda kwa asilimia kubwa vinaendeshwa kwa kutumia umeme wa kutosha na wa uhakika.

Nae, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa fedha zinazopelekwa Wizara ya Viwanda si kwa ajili ya kujenga viwanda bali kwa ajili ya kuzielekeza sekta binafsi zilipo fursa za kujenga viwanda.

Aidha, Mwijage amesema kwamba mpaka sasa jumla ya viwanda 2169 vimesajiliwa ambapo viwanda 170 vimesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), viwanda 180 vimesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, viwanda 1,843 vimesajiliwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) na viwanda 7 vimesajiliwa na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) vikiwemo viwanda 3 vya madawa.
Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage

SERIKALI YA UHOLANZI YAAGIZA AINA 14 ZA MBEGU ZA VIAZI NCHINI

$
0
0
SERIKALI ya Uholanzi imeingiza nchini aina 14 ya mbegu za viazi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuboresha maisha ya wakulima kupitia mradi wa kuboresha zao la viazi nchini.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mradi huo kilichofanyika mkoani Morogoro katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) jana, Mshauri wa Kilimo wa Ubalozi kwa nchi za Kenya na Tanzania, Bw. Bert Rikken alisema nchi yake imeona Tanzania ina nafasi kubwa ya kuongoza uzalishaji wa viazi kutokana na ukubwa wa ardhi na hali ya hewa.

Bw. Rikken alibainisha wameamua kuingiza mbegu hizo ili kuongeza uzalishaji kwa sababu wakulima wanazalisha chini ya tani nane hadi 10 kwa hekta, hivyo ujio wa mbegu hizi utasaidia kuongeza uzalishaji na kufikia tani 40 kwa hekta.

“Mbegu hizi ni nzuri kwa matumizi mengi, viazi vyake vina ladha nzuri na vinaweza kutumika kutengeneza chips au bidhaa nyingine zitokanazo na viazi ambazo zinaweza kusafirishwa nje ya nchi. Mradi huu ulianza kwa kutiliana saini mawaziri wa kilimo kutoka Tanzania na Uholanzi mwaka 2016 ili kuruhusu mbegu kuingia nchini ili kupata ithibati,” alisema Rikken.

Mradi huo wa miaka mitatu utakaogharimu kiasi cha Euro 388,000 sawa na Sh milioni 700, utahakikisha Tanzania inapata mbegu mpya za zao hilo na kutoa mafunzo kwa taasisi zinazojihusisha na kilimo nchini ili kuongeza uzalishaji.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw.Geoffrey Kirenga  akisisitiza  jambo wakati wa warsha ya siku moja juu ya zao la viazi nchini na namna ya kuliongezea thamani. Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bi. Jennifer Baarn, wapili kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Kimataifa  wa maswala ya Mbegu toka Uholanzi,Bw.Jos van Meggelen na kulia ni Kaimu Mthibiti Mkuu wa Mbegu toka Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu nchini(TOSCI),Dr.George Swella. Warsha hiyo iliwakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi.
 Baadhi ya washiriki waWarsha  iliyowakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi wakifurahi kwa kushikana mikono kuashiria ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kukuza na kuliongezea thamani zao la viazi nchini. Warsha hiyo ilifanyika Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Nchini(TOSCI).
 Afisa kilimo toka ubalozi wa Uholanzi Nchini,Bi.Theresia Mcha(kulia) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw.Geoffrey Kirenga mara baada ya kumaliza warsha ya siku moja juu ya zao la viazi nchini na namna ya kuliongezea thamani. Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bi.Jennifer Baarn na wapili kushoto ni Mkuu wa maendeleo ya kongani toka SAGCOT, Bi. Maria Ijumba. Warsha hiyo iliwakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi.

Baadhi ya washiriki wa Warsha iliyowakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja. Walijadili pia namna ya kukuza na kuliongezea thamani zao la viazi nchini. Warsha hiyo ilifanyika Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Nchini(TOSCI).

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

UTEKELEZAJI WA MRADI KABAMBE WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (TURNKEY III) WAANZA

YALIYOJIRI KATIKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI LEO FEBRUAY 9, 2017

$
0
0

Mkurugenzi wa hali ya hewa nchini amesema mabadiliko ya hali ya nchi yamesababisha kuongezeka kwa  hali ya joto hasa maeno ya Pwani: https://youtu.be/RtilCoojWUY

Baadhi ya wakazi mpakani  Mutukula mkoani kagera wametoa pongezi hatua zinazochukuliwa na serikali katika kudhibiti madawa ya kulevya: https://youtu.be/qy3DIx2M5mU

Wananchi wanaotumia barabara ya Mwanza wapo hatarini katika maisha yao iwapo madereva wanaotumia barabara hiyo watakiuka sheria za barabarani: https://youtu.be/pVIESU9nVZ0

Serikali mkoani Tanga imewaonya wahamiaji wasiokuwa na sifa kutojipenyeza katika zoezi la uhakiki wa wahamiaji walowezi: https://youtu.be/CriIX6GwiRs

Rais Magufuli ameagiza kuendelea na shughuli za ujenzi wa jengo jipya la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kambarage Nyerere jijini Dar Es Salaam: https://youtu.be/xpZ9UDtfJjo

Kamati za sherehe ya miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar imesema imekuwa na mafanikio makubwa na kufikia lengo lililokusudiwa: https://youtu.be/gANaFvpSeTs

Balozi wa Irani nchini ameandaa tamasha la utamaduni wa shirazi lilitakalofanyika katika ukimbi wa Jumba La taifa jijini Dar Es Salaam: https://youtu.be/nYeLpfeoV1A

Timu ya bayern Munich ya Ujerumani imesema imeshangazwa sana na kiendo cha Lahm  kutangaza kustaafu masuala ya soka; https://youtu.be/nYeLpfeoV1A

Mhe. Angela Kairuki atoa ufafanuzi dhidi matukio ya ufisadi katika vyama vya ushirika wilayani Siha; https://youtu.be/tpf-20-SaYQ

Mbunge wa Tanga ahoji mpango wa serikali wa kununua meli za kisasa ili kurahisisha usafiri wa uhakika kati ya Pemba na Tanga; https://youtu.be/KC_KfOXr23w

Je ni lini serikali italeta msajili wa hati za wiwanja mkoani Tabora? Mbunge wa Tabora kaskazini Mhe. Almas Maige ahoji; https://youtu.be/eO_ELD6qz1s

BEI YA MADAFU LEO

BREAKING NEWZZZ:ASKOFU GWAJIMA ATII AGIZO LA MAKONDA,ATINGA KITUO CHA POLISI KATI NA WAFUASI WAKE MCHANA HUU

$
0
0
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
 Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wanawasili kituo cha Polisi kati 
 Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi 
Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wamekaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi kama walivyoamriwa na Polisi.

CAG KUCHUNGUZA MAPATO YA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamis, Februari 9, 2015) alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamuagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.Waziri Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

“Vitu vingi vinavyoenda manual ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,”amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMIS, FEBRUARI 9, 2017
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL. Mhandisi Ladislaus Matindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWZ ALERT: WATUHUMIWA 17 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA SHINYANGA,MAJINA MENGINE ZAIDI YA 20 YAPO KWA DC SHINYANGA

$
0
0

Vita dhidi ya dawa za kulevya imetua mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu 17 wanaotuhumiwa kuwa ni watumiaji wa dawa hizo ikiwemo unga na mirungi wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17 kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya. 

“Mheshimiwa Rais ametangaza kuwa hii ni vita ya nchi nzima,baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya ikiendelea mkoani Dar es salaam,wametuletea majina zaidi ya 20 ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya,wanasema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa hizi”,amesema Matiro. 

“Wananchi wenyewe kwa moyo mweupe kabisa ndiyo wametuletea majina ya watu wanaotumia na kuuza dawa za kulevya ikiwemo unga na mirungi,kamati ya ulinzi na usalama tumeunda kikosi kazi cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya”,alisema Matiro. 

Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi kwa jitihada zake dhidi ya dawa za kulevya na kufanikisha kukamata watuhumiwa 17 huku akikisisitiza kuwa vita hiyo siyo ya Dar es salaam pekee bali inatakiwa kufanyika nchi nzima kwani watumiaji na wauzaji wa dawa hizo wapo kila mahali nchini. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo (hawapo pichani) Alhamis Februari 9,2017 kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya katika wilaya ya Shinyanga-Picha na Kadama  Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akielezea jinsi wananchi wa wilaya hiyo waliamua kuchukua hatua ya kupeleka majina ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wilayani humo
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akielezea kuhusu kikosi kasi walichounda kufuatilia majina ya watu wanaotajwa kuhusika na dawa za kulevya wilayani humo

******
Msikilize hapa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia watuhumiwa wa dawa za kulevya wilayani Shinyanga.

BARAZA LA VIONGOZI WA DINI LAUNGA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

BARAZA la Viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania ambalo liko chini ya Tume ya kupambana na dawa za kulevya  limeunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana na watu mbalimbali wanaotumia dawa za kulevya.

Katika hatua nyingine baraza hilo limeiomba serikali  kumuongezea ulinzi Makonda  kwa kuthubutu kutaja watu wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum ,alisema Makonda anapaswa kuongezewa ulinzi kutokana na ujasiri aliouonesha wa kuthubutu kuwataja kwa majina watu hao.

"Sisi kama baraza tunapinga vita na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika biashra au utimiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa matumizi ya dawa hizo yamekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu na yanapotokea nguvu kazi ya Taifa kwa vile wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa hizi ni vijana"alisema.

Alisema kutokana na ugumu wa kazi hiyo aliyoianzisha baraza hilo linamuombea kwa mwenyezi mungu ili ampe ulinzi wake na kinga yake na azidi kumpa moyo wa ujasiri wa kupambana na maovu yote yanayo haribu sifa ya Taifa letu na vijana kwa ujumla.

Salum alisema hivi sasa Makonda ameshanza kutengenezewa majungu, fitina na uzushi mbalimbali ili kumkatisha tamaa na aonekane mbaya kwa watanzania lakini hawatafanikiwa endapo atamtanguliza mwenyezi mungu katika mapambano hayo.

Alisema inawezekana wanaopinga au kubeza juhudi hizo ni kwa sababu tu madhara ya dawa za kulevya hayajawagusa wao na familia zao hivyo hawana uchungu na watanzania wenzao walioathirika hivyo wapuuzwe badala yake wasimame pamoja kama watanzania dhidi ya vita hiyo.

Mwenyekiti huyo wa baraza hilo alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wengine waige mfano wa Makonda wa kupambana na uovu huo mkubwa ambao ni janga kwa Taifa kwani Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.
 Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum.
 Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu baraza hilo kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za  kupambana na wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Padre John Solomon.
 Baadhi ya viongozi wa dini (waliokaa), wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.


WAZIRI PROF. MBARAWA ATEUA TIMU YA KUSIMAMIA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameteua timu mpya ya wataalamu saba kwa ajili ya kusimamia mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (Terminal III), katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais John Magufuli alilolitoa jana wakati alipofanya ziara ya kushtukiza uwanjani hapo  kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika mradi huo.

Timu hiyo inaongozwa na Eng. Julius Ndyamukama inaundwa na  Eng, Godson Ngomuo, Eng. Humphrey Kanyenye, Eng. Abednego Lyanga, Eng. Mbila Mdemu na Eng. Rehema Myeya.

“Naamini timu hii ina wataalamu mahiri, hivyo itasimamia ujenzi huu kukamilika kwa wakati na kwa kuzingatia thamani ya fedha (value for money”, amesema Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amemhakikishia mkandarasi wa kampuni ya BAM kutoka uholanzi inayojenga jengo hilo kuwa Serikali itamlipa mkandarasi huyo katika kipindi cha wiki mbili kutoka sasa.

Aidha, ameitaka timu hiyo kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika mwezi Desemba mwaka huu kama ilivyopangwa.

Kwa upande wake Meneja wa mradi huo Eng. Julius Ndyamukama, ameahidi kushirikiana na wenzake katika kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati.

Kiasi cha Shilingi Bilioni 560 zinatarajiwa kutumika katika kugharamia ujenzi huo kwa awamu zote mbili.

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemsimamisha kazi Meneja wa Fedha kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA) Bw. Simba Lugando kwa kuidhinisha malipo ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya kwa mkandarasi wa Kampuni ya DB Shapriea kiasi cha shilingi Bilioni 3.3 ambapo ujenzi wake haukufanyika ipasavyo.

 Mafundi wa Kampuni ya BAM wanaojenga jengo la tatu la Abiria (TB III) wakiendelea na kazi ya ujenzi, jijini Dar es Salaam. Kazi ya ujenzi zimeanza baada ya kutarajiwa kusimama sababu ya kukosekana fedha ambapo Serikali imesema itatoa fedha za kukamilisha mradi huo.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akitoa maelekezo kwa timu aliyoiteua kusimamia ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), mara baada ya kuteuliwa leo jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari, (hawapo pichani), mara baada ya kukagua ujenzi wa Jengo la tatu la Abiria (TB III), jijini Dar es Salaam.

WEMA SEPETU NA TUNDU LISSU WALIVYOFIKA MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR LEO

YUSUF MANJI NA ASKOFU GWAJIMA WALIVYOTINGA KITUO CHA POLISI SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA MAPEMA LEO

BAADA YA KUSOTA NDANI SIKU 7 WEMA ATOKA KWA DHAMANA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii.

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana msanii maarufu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambaye kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni tano.

Baada ya kutimiza masharti hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Thomas Simba aliwataka washitakiwa kuhakikisha hawaruki dhamana waliyotakiwa na kuhakikisha wanafika mahakamani hapo kila wanapohitajika.

Hata hivyo, aliwataka mawakili wa serikali kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo ifike mwisho. Mbali na wema washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa ambaye ni mfanyakazi wa ndani na Matrida selemani Abas ambaye ni Mkulima.

Wote watatu wanashtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, iwapo Wema na wenzake watapatikana na hatia basi watatakiwa kulipa faini isiyozidi sh.laki tano au kwenda jela.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili Pamela Shinyambala walidai kuwa Wema na wenzake watatu walitenda kosa hilo tarehe 4 February mwaka huu, huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio.

Ilidaiwa kuwa, siku hiyo walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi viwili vya banfi vyenye gramu 1.80. Hata hivyo washtakiwa wote wamekana mashtaka.

Akielezea hali ya upelelezi wakili Katuga alidai "mheshimiwa Hakimu, upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika tunasubiri taarifa kutoka kwa Mkemia Mkuu ambayo tunategemea kuipata hivi karibuni".

Hakimu Simba aliwapa washtakiwa masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao weka dhamana na milioni tano. Mshtakiwa Wema na Wenzake walitimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo February 22 mwaka huu.

Nje ya Mahakama Umati wa watu na wasanii mbali mbali walijaa nje kumlaki Wema akitoka mahakamani baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wema Sepetu akishuka katika gari ya Polisi huku pembeni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akipunga mkono akitokea katika gari hiyo kwa mbele.
Wema Sepetu akitolewa kutoka mahabusu ya Hakimu Mkazi Kisutu
Wema Sepetu akishuka katika ngazi za Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuamuriwa apte dhamana ya mahakama.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

ASKOFU GWAJIMA ALIPOZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA KUTAJWA KWAKE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima amesema kuwa ameokoka na anamtumikia mungu hivyo kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na dawa za kulevya iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni jambo ovu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Askofu  Gwajima amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam anafanya kazi vizuri lakini suala la kiutawala hawezi na kumuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli ambadilishie kazi.

Amesema yeye alikuwa Mpwapwa  katika kazi zake aliposikia kutajwa kwa jina lake na kumlazimu arudi na kuwasili pale alipoitwa bila kusubiri siku iliyopangwa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Askofu  Gwajima amesema kuwa kuhusu mali anazomiliki ni kutokana na kazi anazofanya ikiwa kuwa na kampuni mbalimbali pamoja na kufundisha masuala ya farsasafa nje nchi na kulipwa dola za kimarekani 1000 kwa saa.

Aidha amesema kuwa kulindwa kwake ni kutokana na kuwa na usalama wake hata papa ana gari ambayo haipiti risasi wakati ni mtakatifu.
Askofu Gwajima amesema Makonda anachuki na wivu dhidi yake ndio maana anamhusisha na jambo ovu ambalo linamchafu mbele ya mungu.
Amesema kuwa yuko radhi kukaa ndani miaka 40 kutokana na kupigania suala la uovu ni jambo halitawe za kuvumiliwa.
 Askofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kutajwa kwao kujihusisha na dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Katibu Mkuu wa Kanisa  la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa akizungumza na waandishi wa habari juu watavyopambana na katika kupigania Askofu wake Josephat Gwajima leo jijini Dar es Salaam.
 Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akitoka katika mkuna na kuelekea kituo  Kikuu cha polisi leo jijini Dar es Salaam.
Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akiagana na waumini wa kanisa hilo leo jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>