Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1558 | 1559 | (Page 1560) | 1561 | 1562 | .... | 3285 | newer

  0 0


  0 0

  Na Mathias Canal, Mwanza

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi waliojitokeza kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu wa vitabu vitakatifu vya Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.
   Rc Mongela akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
  Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wote nchini Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiyomondi Kibamba alisema kuwa msiba huo umekuwa pigo kwa familia ya Kayombo na ukoo mzima lakini pia ni pigo kwa wananchi wote wa Kijiji cha Misasi na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla kwa kumpoteza mlezi na mshauri mzuri.


  MD Kayombo amewashukuru madaktari wa hospitali zote waliojaribu kuokoa uhai wa Mzee Raphael Kayombo hata hivyo ameeleza kuwa idadi kubwa ya watu waliohudhuria Kwenye mazishi imeonyesha kwamba Marehemu Mzee Kayombo alikuwa na mahusiano na kuishi vizuri na majiraji zake.


  Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo ameacha watoto10, Wajukuu 60 na Vitukuu 30 huku kukiwa na idadi kubwa ya vilembwe.

   Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo

  Rc Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya taswira ya fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika maelekezo mbalimbali ikiwemo ushauri katika serikali.

  Mongela aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi wote kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.

  Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.

  Ameeleza kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.  0 0  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Wizara yapokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima leo amepokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video (Video Conference Facilities) kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP). 

  Baada ya kupokea msaada huo, Balozi Mlima aliishukuru UNDP kwa msaada huo ambao alieleza kuwa utasaidia shughuli za Wizara katika ofisi mpya ya Wizara mjini Dodoma. Alisema msaada huo ni wa pili kwa Wizara katika muda mfupi ambapo awali UNDP ilitoa ngamizi, printers na cameras. 

  “Tunamshukuru Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ambaye ndio alianzisha suala hili na kuongea nanyi na kulisimamia bila kuchoka hadi leo vifaa vinapatikana” “Kwa kweli ni mtu ambaye wakati wote anapenda mambo anayoyasimamia yanatokea” Katibu Mkuu alimwambia Mkurugenzi wa UNDP nchini Tanzania, Bi. Awa Dabo. 

  Kwa upande wake Bi. Dabo baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa mazungumzo kuhusu maombi ya msaada huo yalianza tokea mwaka 2014 lakini kwa uwezo wa mungu vifaa hivyo leo vimekabidhiwa rasmi Wizarani. Alielezea matumani yake kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa Wizara na pia utaboresha na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali na UNDP.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 09 Februari 2017.
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akipokea baadhi ya vifaa vya kuwezesha kufanya Mkutano kwa njia ya video kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo Wizarani Jijini Dar es Salaam 
  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akiwa katika mzungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja Bi. Awa Dabo mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video 
  Kutoka kulia, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kisiga, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi Bw. Manyama M. Mapesi na Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakifuatilia zoezi la makabidhiano 
  Zoezi la Makabidhiano likiendelea 


  0 0  0 0  0 0


  Ni siku chache tu! zimesalia kuikamata Tarehe 11 mwizi huu 2017, kumbuka siku hiyo ni siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tz, coz wanategemea kukutatishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani hapa naizungumzia “Lady In Red”.

  Muandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, akizungmza na wabahabari Jana Tarehe 8/2/2017 huku akiwa ameambatana na wanamitindo wengine amesema kuwa,

  “Kwanza Show hii ni yakipekee pia inafaida kubwa sana kwa upcoming Designers, Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuweza kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu 11/2/2017 mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”.

  Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnaombwa kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi Asante.
  Wanamitindo wakiwa kwenye Press ya Lady In Red 2017 .


  0 0


  Na Stella Kalinga

  Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.

  Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha kuridhisha.

  Amesema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.

  Aidha , Aliandaa makadirio ya Tsh46,106,456,000 yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni ya juu kuliko uhalisia. 

  Shtaka la pili linalomkabili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali na 168/2003;

  Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya Mhe.Rais

  Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia

  (2) Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.


  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa
  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.
  Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.  0 0


  0 0

  Na Karama Kenyunko-Globu ya Jamii.

  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali hati ya kiapo ya mkuu wa upelelezi Ilala, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Denis Mujumba na kumuachia Tundu lissu kwa dhamana.

  Lissu yuko nje kwa dhamana ya shilingi milioni ishirini na mdhamini mmoja.

  Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kumsomea Lissu ambaye ni Mbunge na mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani, mashtaka yake na kuwasilisha hati ya kiapo kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.

  Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo alisema kuwa kiapo kilichowasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kina mapungufu makubwa sana.

  Amesema kuwa kukosekana kwa namba ya kesi na mahali ambapo inaonyesha muapaji wa kiapo hicho aliapa ni mapungufu makubwa.

  Ameongeza kuwa mshtakiwa Lissu anahaki ya kupata dhamana kwa kuwa shtaka analokabiliwa nalo linadhaminika licha ya kuwa na kesi tatu tofauti mahakamani hapo kama ambapo kiapo kilivyosema.

  Amesema kuwa, licha ya kuwa Lissu kweli anav mashtaka mahakamani hapo lakini hakuna shtaka hata moja ambalo amekutwa na hatia na alilokutwa nalo na hatia Kabla ya kiapo hicho jopo la mawakili wanne likiongozwa na wakili Mwandamizi wa Serikali Mutalemwa Kishenyi aliyekuwa akisaidiana na Wakili Easter Martin, Jackline Nyantori na Clementina Masawe walimsomea mshtakiwa mashtaka yake manne yanayomkabili ya kutoa lugha ya uchochezi.

  Lissu ambaye amefikishwa katika viwanja vya mahakama hiyo leo majira ya saa 11.42 asubuhi akiwa ndani ya land lover ya polisi pamoja na msanii maarufu wa uigizaji nchini Wema Sepetu na watuhumiwa wengine alikamatwa juzi mara baada ya kutoka kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Saa 12:24 mchana, Lissu alipandishwa kizimbani Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa manne ya kutoa lugha ya uchochezi.

  Tundulisu akishuka kwenye gari akiwa amebeba suti yake
  Tundu Lisu akielekea Rumande kwa ajili ya kusubiri kupandishwa kizimbani.

  Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akipelekwa mahabusu kwa jili ya kusubiri kupandishwa kizimbani

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akinyanyua kitabu cha Sheria ya Mwaka 2015 baada ya kukizindua   rasmi leo katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora (kushoto) makamo wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Majaji,Mahakimu na wafanyakazi wakati wa sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema "SIMAMIA SHERIA NA MAADILI KATIKA UTENDAJI HAKI" (Picha na Ikulu).
    Baadhi ya Mahakimu na wafanyakazi wa idara ya Maahakama Zanzibar wakiwa katika sherehe ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Na Mboza Lwandiko

  Lipa Kodi ya Ardhi kwa wakati, uepuke kutozwa Tozo, Kutangazwa kwenye Vyombo vya Habari, Kupelekwa Mahakamani na Kufutiwa umiliki wa ardhi yako, kwani Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 inaainisha gharama hizo kwa wasiozingatia ulipaji Kodi. kutozingatia kulipa Kodi ya pango la Ardhi kwa wakati, ambapo mmiliki asiyezingatia hilo kwanza; atatozwa Tozo na baadae Kupelekewa hati ya madai na kufikishwa Mahakamani kulingana na kifungu Na. 50 na hatimaye kufutiwa umiliki wa ardhi kulingana na Sheria hiyo hiyo katika kifungu Na. 49-51.

  Akizungumza na Waandishi wa habari hivi karibuni wakati wa zoezi la kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya Pango la Ardhi. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila amesisitiza kwa umma kuwa wadaiwa wote wa Pango la Ardhi wamekumbushwa na Serikali kwa muda mrefu, na hivyo ni wakati wao kuhakikisha wanalipa madeni yao yote ipaswavyo. Aliendelea kusema kuwa; kwa Mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi. 

  Dkt. Kayandabila alisema kwakuwa Kodi ya Ardhi inatambulika bayana chini ya Sheria, kila mmiliki wa Ardhi hana budi kuzingatia hilo. Malipo ya pango la ardhi yanatozwa kwa wamiliki wa viwanja na mashamba yaliyopimwa na kumilikishwa kisheria. 

  Pia mtu yeyote anayemiliki ardhi iliyopimwa kisheria iwe imeendelezwa au haijaendelezwa bado anapaswa kulipa kodi ya pango. Kila mmiliki anaongozwa na mkataba wa kulipia kodi ya pango la ardhi kila mwaka tarehe 1 (Mosi) Julai, Sheria ya Ardhi Na.4 ya mwaka 1999 kifungu cha 33 na kifungu kidogo cha 11 imetoa mwanya kwa walipa kodi kuendelea kulipa bila adhabu hadi tarehe 31 Desemba ya mwaka unaohusika. Baada ya hapo adhabu inatozwa. Mteja anapaswa kufanya malipo ya Kodi ya pango la Ardhi kwa kuwa ananufaika na matumizi ya ardhi hiyo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya Serikali.
   Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya kodi ya ardhi.
  Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI    
  TAARIFA KWA UMMA


  AWAMU YA KWANZA YA WATUMISHI KUHAMIA MAKAO MAKUU YA NCHI - DODOMA TAREHE 10 FEBRUARI, 2017


  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara kuhamia Makao- Makuu ya Nchi, Dodoma inaanza tarehe 10 Februari, 2017.


  Miongoni mwa watakao hamia katika awamu hiyo ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara ambao ni Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Naibu Makatibu Wakuu wa Nishati na Madini.


  Watumishi wengine ni pamoja na Kamishna wa Madini Tanzania, Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Maafisa. Jumla ya Watumishi wanaohamia Dodoma Awamu ya Kwanza ni 47.


  Aidha, kutokana na uhamisho huo, anuani ya Wizara  Dodoma ni;

  Katibu Mkuu,

  Wizara ya Nishati na Madini,

  Barabara ya Kikuyu,

  S.L.P 422,

  DODOMA

  Imetolewa na;


  KATIBU MKUU

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  9/2/2017
  0 0  Wahitimu wa Chuo kikuu cha Aga khan wakiingia katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
  Wahitimu wa chuo kikuuucha Aga Khan miaka wakingia katika mahafali ya chuo hiyo

  Wazazi na wageni waalikwa waliofika katika mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Aga Khan jijini Dar es Salaam


  Naibu Gavana wa Benki Kuu nchini Tanzania, Lila Mkila akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Aga Khan
  Rais wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Firoz Rasul akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa chuo hichi
  Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha Aga Khan wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa chuo hicho

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Shirika lisilo la kiserikali la Kingdom Leadership network Tanzania (KLNT) limeandaa mkutano wa pili wa Tanzania National Prayer Breakfast na mkutano wa Kiuchumi ujulikanao kama 2017 Kingdom Economic Summit.

  Mkutano huo utakaofanyika kuanzia machi 6-8 utajumuisha shirika la huduma la kimataifa ya Bill Winston kutoka nchini Marekani na unatarajiwa kuhudhuriwa na Makamu wa Raisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Samia 

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa KLNT Charles Sokile amesema kuwa mkutano huo wa uchumi unatoa nafasi ya kipekee kwa watu binafsi, wafanyabiashara, mashirika ya kibiashara na viongozi wa makanisa kuweza kujipatia ujuzi na uzoefu kutoka kwa wasemaji mkuu wa mkutano mkuu.

  "Tunajivunia kuweza kuleta tena mkutano huu kwa mwaka wa pili sasa na kuweza kuleta wageni rasmi ili kuja kuhamasisha watanzania na kuleta mabadiliko chanya kimaadili katika uongozi na biashara kwa mtu mmoja mmoja na hatimaye taifa kwa ujumla," amesema Sokile.

  Mwanzilishi wa KLNT Isaac Mpwata amesema kuwa kila mara wanajikita katika kuhakikisha wanatoa fursa za mafunzo ya kiongozi na biashara yanayojikita kwenye suala zima la maadili kama msingi wa mafanikio.

  Mpwata amesema kwa kupitia mkutano huu wanategemea kuendelea kujenga uwezo wa viongozi wetu na wafanyabiashara kwa ajili ya kubadili taifa letu kwa kutumia kanuni za uongozi wa kimaadili ili kuleta mabadiliko chanya katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
  Suluhu.
   Mwanzilishi wa Kingdom Leadership Network Tanzania (KLNT) Issac Mpwata akizungumza na waandishi wa habari kuhusinana na mkutano wa pili wa kiuchumi utakaofanyika Machi 6-8 Jijini Dar es salaam
  Katibu Mkuu wa Kingdom Leadership Network Tanzania Charles Sokile akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maandalizi ya mkutano wa pili wa kiuchumi na kuwataka viongozi mbalimbali kujitokeza, Kulia ni Mwanzilishi wa KLNT Issac Mpwata na Kushoto ni Afisa masoko  Carol Maajabu 

  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (kushoto) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa kizungumza na mawaziri mbali mbali,watendaji wa Serikali (hawapi pichani), Wajumbe wa Tume ya uchaguzi baada ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (katikati) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 09/02/2017.

  Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe,Jecha Salim Jecha (kulia) akitoa maelezo mafupi kabla ya kukabidhi Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
  Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Washauri wa Rais waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
  Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa Ripoti ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 2015 kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Mhe,Jecha Salim Jecha (hayupo pichani) katika hafla fupi iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja

  0 0   Shughuli za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) ukiendelea mbele ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani kufatia ziara ya kushtukiza  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyofanya hapo jana na kutoa Maagizo kwa Mkandarasi wa Uwanja huo kuanza kazi mara moja kuanzia leo.
   Kazi ya Umwagiliaji ikiendelea katika sehemu ya mbele ya ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani.
   Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Moja ya nguzo katika jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
   Mafundi wakiendelea na ujenzi wa sehemu ya chini ya maegesho ya ndege kama inavyoonekana.
   Mafundi wakiendelea na ujenzi sehemu ya juu ya jengo hilo la Abiria kama inavyoonekana.
  Sehemu ya mbele ya jengo hilo la Abiria kama linavyoonekana.  0 0

  Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa  kwa huduma hizo zitapokuwa tayari.

  Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
  "Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano", imesema barua hiyo.
  Wamiliki wa mitandao hiyo - Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah Mrisho -  wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.         
       
  "Gloval TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili - kama zingekuwepo - na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya," alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa Global Publishers.

  Ankal Michuzi na Millard  Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa. 

  Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.

  "Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii", alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.

  Ayo TV, Michuzi TV na Global TV,  ambazo zinaongoza kwa mbali kwa kutazamwa na watu wengi nchini na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA, kati ya vituo mtandao  takriban 51 vilivyopata barua hiyo.

  Ankal Issa Michuzi wa Michuzi TV, Millard Ayo na Askofu wa Ayo TV na Abdallah Mrisho wa Global TV wakitoka makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano walikoitwa kuchukua barua zao zinazowazuia kuendelea kutoa huduma za TV mtandao hadi hapo kanuni za usajili na leseni utapokamilika.

  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 1558 | 1559 | (Page 1560) | 1561 | 1562 | .... | 3285 | newer