Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1556 | 1557 | (Page 1558) | 1559 | 1560 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Anthony John, Globu ya Jamii

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , limesema Jalada la kesi ya kukutwa na bangi Msanii maarufu na Mlimbwende , Wema Sepetu bado linapitiwa na Mwanasheria wa Serikali na baada ya kukamilika kwa upelelezi atapelekwa mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema jeshi la polisi limeshafanya kazi yake hivyo taratibu za kisheria za kesi ya Msanii huyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.

  Amesema katika mapambano ya dawa kulevya, wananchi na raia wema wameaswa kuacha kutoa habari za uvunjifu wa amani katika mkoa wa Dar es salaam,badala yake wajikite kutoa taarifa zilizokuwa za kweli.

  "Unapotoa taarifa ambazo si za kweli haumdanganyi kamishina Sirro ,unakuwa unalidanganya Jeshi la polisi ,kwa ujumla naomba raia wema waendelee kutoa taarifa lakini watoe taarifa za uhakika"amesema Sirro.

  Pia Siro ameongeza kuwa Jeshi la polisi limejipanga vizuri kwa kuwapokea watakao fika siku ya ijumaa lakini kikubwa wafike waje waripoti.

  0 0

  SERIKALI imesema kwamba tatizo la maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu ya maisha.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani hapo.

  Akiongea na mbele ya Watendaji wa Bodi hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo, Waziri Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo alitaja taarifa ya Shirikala Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n inayoonyesha takribani watu milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.

  “Matatizo haya yamekuwa yakisababisha vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote, hata hivyo taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu wanaougua magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 136,710 mwaka 2011/2012 hado wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.

  Ameongeza kuwa, takwimu za hospitali ya Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miaka mine kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za afya na utengamao.

  Aidha, kwa kutambua majukumu makubwa ya hospitali hiyo na kutatua changamoto zinazohusiana na magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi ya hospitalini hapo lengo likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji wa Huduma Bora za Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.

  “Ninayo furaja leo kushiriki nanyi katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na Wajumbe waliouteuliwa kutoka maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”, alisema Waziri Ummy.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mwenyekiti wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mganga Mkuu na Katibu wa Bodi ya Hospitali ya Miremb, Erasmus Mndeme akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mkurugenzi Msaidizi Hospitali ya Mirembe, Bibi. Doroth Gwajima akiongea na Wajumbe wa Bodi leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Mwalimu Ali Mbaga wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo. Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.(Picha na Bashir Nkoromo).

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BENKI ya DCB imeendelea kufanya droo ya pili ya bahati nasibu ya pili ya kampeni ya kuweka Amani inayoitwa Boresha maisha na DCB huku Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha (Bahati nasibu) Taifa Bakari Maggid na kufurahishwa kwa juhudi zinazofanywa na benki hiyo katika kuwapata washindi.

  Droo hiyo iliyoanza mwezi Januari iliweza kuwapata washindi wa wa kwanza 20 waliopata tisheti, watatu waliopata fedha taslimu na wawili wakiopata simu za mkononi

  Akizungumza kabla ya kuanza kwa droo hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Steven Dede amesema kampeni hiyo ilianza Novemba 28,2016 na droo hii ya pili ni kwa wateja walioekwa pesa kwenye akaunti zao kuanzia Desemba 28 hadi Januari 31.

  Dede amesema akaunti zitakazohusika ni akaunti ya akiba binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI na kuwataka wateja wa benki hiyo na wasio wateja , watu binafsi, wajasirimalina taasisi mbalimbali kunendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hilo kwa kufungua akaunti na kuweka amana.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Steven Dede akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na droo ya pili inatochezwa na benki hiyo ya weka amana na DCB na Boresha maisha na DCB
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kwa droo hiyo akishuhudiwa na mkaguzi wa michezo ya kubahatisha( bahati nasibu) Taifa Bakari Maggid (wa pili kulia).

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Ugunduzi wa gesi asilia nchini umepelekea kushuka kwa gharama za umeme kwa asilimia 33.26 kwa mwaka 2014 hadi 2016.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ameyasema hayo leo Bungeni, Mjiji Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge viti Maalum Maida Hamad Abdallah kuhusu faida zilizopatikana tangu kugundulika kwa gesi asilia.

  “Faida kubwa iliyopatikana kutokana na ugunduzi na matumizi ya gesi asilia nchini ni uzalishaji wa umeme wa bei nafuu kwa kutumia Gesi Asilia ikilinganishwa na mafuta. Uzalishaji umeme kwa kutumia Gesi Asilia umeongezeka kutoka uniti 2,714.25 milioni kwa mwaka 2014 hadi uniti 4,196.4 milioni mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 54.61,” alifafanua Dkt. Kalemani.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa Gesi Asilia umepelekea kushuka kwa bei ya umeme kutoka wastani wa shilingi 188.56 kwa uniti mwaka 2014 hadi wastani wa shilingi 125.85 kwa uniti mwaka 2016.

  Akitolea ufafanuzi zaidi juu ya faida zinazopatikana kutokana na matumizi ya Gesi Asilia, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa maeneo ya Mikocheni, Jijini Dar es Salaam zikiwemo nyumba za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanatumia Gesi Asilia ambapo gharama wanayoitumia kwa mwezi haizidi shilingi elfu 25,000, na wanatumia kwa kupikia aina zote za vyakula hata vile vinavyotumia muda mrefu kuiva kama vile maharage na makongoro.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, mpaka sasa jumla ya viwanda 37 vinatumia nishati inayotokana na Gesi Asilia, ambayo gharama yake ni nafuu ukilinganisha na gharama ya nishati nyingine.Aidha, amesema kuwa Wizara yake imepata ufadhili wa Dola Mil. 150 kutoka Afrikan Development Bank kwa ajili ya kusambaza gesi katika mikoa Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.

  Prof. Muhongo amesema kuwa usambazaji huo utakapoanza na kufika maeneo ya Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam yatafungwa mabomba mengine kwa ajili ya kupeleka gesi katika mikoa mingine kama vile Morogoro, Mbeya na Iringa.Aidha amesema gesi ambazo zinatumika kwa sasa ni gesi salama ambazo hazilipuki ukilinganisha na gesi za miaka ya nyuma.

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lilianza utafiti wa masuala ya mafuta na Gesi Asilia nchini mwaka 1950, ikihusisha utafiti katika maeneo ya bahari ya kina kirefu, maziwa na nchi kavu. Gesi Asilia iliyogundulika katika maeneo ya bahari ya kina kirefu ni futi za ujazo trilioni 47.08 na katika nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 10.17 hivyo kuwa na jumla ya futi za ujazo trilioni 57.25 za Gesi Asilia inayojulika kama “sweet gas” yaani gesi yenye kiwango kidogo sana cha salfa (sulphur).

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha (kamari) anahesabiwa kufanya kosa.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Asha Abdullah Juma juu ya kuongezeka kwa maduka ya kucheza Kamari yanayojulikana kama Jack Pot katika miji mingi hapa nchini hivyo kusababisha uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya vijana.

  “Michezo yote ya kubahatisha ikiwemo kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha namba 4 ya mwaka 2003, sura 41 pamoja na Kanuni zake,” alifafanua Dkt. Kijaji.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendesha biashara ya michezo ya kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka nyingine za biashara.

  Vile vile sheria hiyo inakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.Aidha mtu yoyote ambaye atamruhusu mtoto chini ya miaka 18, kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha anahesabika kufanya kosa na anastahili kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja.

  Dkt. Kijaji amesema kuwa ikiwa kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa kubahatisha, Bodi inamamlaka ya kumfutia leseni.Hivyo basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha.Pia, Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia vijana wao kucheza michezo ya kubahatisha pale wanapoona kuwa uchezaji wao unakuwa na matokeo hasi.

  Hata hivyo amesema kuwa, michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu na sheria kama shughuli nyingine. Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa, wanaoendesha michezo hiyo wanazingatia sheria na kanuni zilizowekwa pamoja na wazazi, walezi na jamii kuhakikisha vijana wanazingatiia mila na desturi zinazolinda maadili ya Kitanzania wanapokuwa wanajishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.

  0 0
 • 02/08/17--08:20: GADO
 • Drug barons Vs drug Addicts

  0 0


  0 0


  0 0

   
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na makadrasai alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 02/08/17--20:53: Article 24


 • 0 0
 • 02/08/17--20:54: Article 23


 • 0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro, Mwalimu Ali Mbaga, wakati wa mazishi yaliyofanyika jana Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiongoza kwenda  nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongozamazishi hayo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiongoza kwenda  nyumbani kwa marehemu Mbaga, kuongoza mazishi hayo.
  Waombolezaji wakipeleka jeneza lenye mwili wa marehemu Mbaga kwenye eneo la kuswaliwa wakati wa mazishi hayo.
  Maziko ya Mwili wa marehemu Mbaga yakifanyika.


  0 0


  0 0
 • 02/08/17--21:29: Article 19


 • 0 0


  NA ESTOM SANGA- SHINYANGA

  Walengwa wa Mpango wa kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF mkoani Shinyanga wameeleza kunufaika na fedha zinazotolewa na mfuko huo kama ruzuku kwa kuanzisha miradi midogo midogo na hivyo kujiongezea kipato na kupunguza tatizo la umaskini lililokuwa linawakabili kabla ya kuanza kwa Mpango huo.

  Wakizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea baadhi ya kaya za walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Manispaa ya Shinyanga baadhi ya walengwa hao wameeleza kuwa wameweza kuanzisha miradi ya ufugaji wa nguruwe, mbuzi, ng’ombe na kuku kwa kutumia ruzuku ya fedha walizozipata kupitia utaratibu wa uhawilishaji fedha unaofanywa na TASAF.

  Walengwa hao wamesema kabla ya kuingizwa kwenye utaratibu wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini,walikuwa wakihangaika na kushindwa kupata fedha za kuanzisha miradi midogo midogo kutokana na kutokuwa na fursa ya kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha na hivyo kutopea katika dimbwi la umaskini.

  “Ninaishukuru sana serikali kwa kutuletea TASAF kwani imetufungua macho na kuwa chachu ya maendeleo kwani sasa naishi kwenye nyumba yangu niliyoijengwa baada ya kudunduliza fedha kutoka TASAF” amesisitiza Bi.Christina Ndimila (70) mkazi wa Ndala A katika manispaa ya Shjinyanga.

  Walipoulizwa wanawezaji kuanzisha miradi hiyo ilhali baadhi ya watu wanadai kuwa ruzuku ya fedha inayotolewa na TASAF ni ndogo, walengwa hao wamesema kuwa matumizi sahihi na kuzingatia masharti ya Mpango ndiyo kumewawezesha kujiwekea akiba kidogo kidogo ya fedha hizo kila wanapozipata.

  “ Ukizipata fedha za TASAF na kuzila zote utaziona kuwa ni ndogo ,lakini ukipata na kuziwekeza kwenye mradi wowote mdogo fedha hizo huongezeka baada ya muda mfupi na hivyo kukupa uwezo wa kujiendeleza” alisisitiza Bi. Joyce Jindai Lubunga(59) mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini anayeishi katika mtaa wa Banduka nje kidogo ya manispaa ya Shinyanga.
  Mmoja wa walengwa wa TASAF katika manispaa ya Shinyanga akiwa nje ya nyumba yake aliyoijenga kwa fedha za ruzuku kutoka TASAF ikiwa ni jitihada za kuboresha makazi yake na picha ya chini mlengwa huyo akiwaonyesha Waandishi wa habari baadhi ya mbuzi aliowanunua kutokana na ruzuku hiyo.
  Mmoja wa walengwa wa TASAF bi. Maria Gabriel Picha ya juu akiwa karibu na nyumba yake ya zamani na chini ni nyumba yake mpya aliyoijenga baada ya kupata fedha za ruzuku kutoka TASAF.Picha inayofuatia ni bomba la maji alilovuta kutokana na fedha za ruzuku hiyo. 
  Mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini Bi.Perpetua Tungu picha ya chini akiwa katika bustani yake ya mboga aliyoianzisha kutokana na fedha za ruzuku kutoka TASAF kama sehemu ya kujiongezea kipato. Picha ya chini inaonyesha nyumba anayoendelea kuijenga kwa kutumia fedha hizo ikiwa ni jitihada za kuboresha makazi yake. 
  Mmoja wa walengwa wa TASAF BI. Rehema Naligigwa katika manispaa ya Shinyanga akionyesha banda analolitumia kufuga nguruwe baada ya kupata fedha za ruzuku kutoka TASAF.


  0 0

  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia Mhe. Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) akipokea kompyuta kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Song Geum Young, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi na wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia Dkt. Bernard Archiula. 
  Mhe. Balozi Sefue akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Bodi na Uongozi wa Chuo cha Diplomasia mara baada ya kupokea ufadhili huo kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Korea. 
  Balozi Mwinyi akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo aliipongeza Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kuendelea kuwa mdau wa maendeleo katika sekta mbalimbali nchini hususan sekta ya Elimu. 
  Sehemu ya Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia wakimsikiliza Balozi Sefue (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa neno la shukrani.


  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amosi Makalla akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa Taasisi ya Mfuko wa Uwekezaji Mradi (BRAC) na baadhi ya Wajasiliamali kutoka katika vikundi vipatavyo 20 vya jijini Mbeya.

  Mkuu wa mkoa Wa Mbeya Mh.Amos Makalla akizungumza na baadhi ya akina mama wa jijini Mbeya wanao kopeshwa na Taasisi ya Mfuko wa Uwekezaji Mradi (BRAC) jijini Mbeya.RC Makalla ameipongeza taasisi hiyo kwa kuvikopesha vikundi hivyo vya ujasiliamali,dhamira kuu ikiwa ni vikundi hivyo kuongeza uzalishaji wa Mahindi na ufugaji wa kuku kwa wingi.Taasisi ya BRAC imevikopesha vikundi vipatavyo 20 kiasi cha shilingi milioni 770 kwa ajili kuendeleza miradi yao mbalimbali ikiwemo ya ufugaji kuku na kilimo

  RC Makalla pia amewaagiza maafisa Ugani kuwatembelea Wafugaji na wakulima mara kwa mara ili kuwapa maelekezo namna ya kuiendeleza na kuisimamia vyema miradi yao mbalimbali,ambayo imekuwa ikiwapatia kipatao na kuendelea kuwakwamua katika suala zima la kupambana na umaskini

  "Nimefurahishwa sana na juhudi zenu za ujasiliamali,hakika ndio njia nyingine mbadala ya kujiingizia kipato na kuhakikisha suala la umaskini linakuwa historia miongoni mwenu,hivyo nawapongeza sana na msikate tamaa"alisisitiza RC Makalla huku akiongeza kwa kuwataka Wananchi kufanya kazi,kwani maendeleo hayaji kwa watu kukaa na kuyasubiri bila kufanya jitihada zozote.
  Baadhi ya kuku wa kienyeji wanaofungwa na vikundi hivyo vya ujasiliamali mkoani Mbeya.
  Baadhi ya akina Mama Wajasiliamali wanaounda vikundi 20 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao mara baada ya kuwatembelea kwenye maeneo ya miradi yao wanayoiendeleza baada kukopeshwa fedha na taasisi ya BRAC

  0 0


  0 0


  Hussein Makame, NEC-Bukoba

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevihimiza vyama vya siasa kutoa elimu ya mpiga kura kwa wapiga kura na wanachama wao bila ya kuegemea itikadi ya vyama vyao kwani sio wote wanaowaelimisha ni wanachama wao.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akitoa elimu ya mpiga kura kupitia kituo cha Redio Kasibante Fm kilichopo mjini Bukoba.

  Alisema mdau namba moja wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni chama cha saisa na kwamba NEC inakutana na vyama hivyo mara kwa mara kushauriana namna ya kutoa elimu ya mpiga kura na namna ya kuwafikia wananchi wengi.

  “Kwa hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavihimiza vyama vya siasa kutoa elimu ya mpiga kura kwa wapiga kura na kwa wanachama wao pia” alisema Bw. Kawishe na kuongeza:

  “Tena tunawasihi vyama vya siasa wasitoe elimu kwa njia ya itikadi za kichama watoe elimu isiyoegemea itikadi yoyote kwa sababu kuna wengine sio wanachama wa chama chake lakini watawapigia kura” 
   Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba (hawapo pichani) wakati akitoa elimu ya Mpiga Kura shuleni hapo.Kulia kwake ni Afisa Uchaguzi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Bw. Erick Bazampola, Mkuu wa shule hiyo Bw. Raymond Mutakyawa na wasaidizi wake. 
   Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bukoba wakimsiliza Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe, wakati akitoa elimu ya mpiga kura.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1556 | 1557 | (Page 1558) | 1559 | 1560 | .... | 3283 | newer