Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

THIS IS WHY YOU SHOULD DEFINITELY SHOP FOR YOUR VALENTINE ON JUMIA THIS YEAR!

$
0
0
LOVE IS IN THE AIR! Yes, it’s that time of the year again where you will start seeing red and pink in display windows all around shopping malls and retail shops. Your partner is then throwing hints about wanting something for this special occasion, that’s when you know Valentine’s Day is right around the corner.
 Preparation for this day involves checking the date beforehand and cashing in your wallet or bank account in order to plan for ways to win over your loved one once more on this special day.
The shopping experience can be exhausting, time consuming and totally clueless for most people wanting to show their affection to their loved ones on Valentine’s day. That’s where JUMIA comes in and saves the day.
We have many special surprises for all our buyers during this Love themed month. Place your order now by visitng www.jumia.co.tz  and find out what suprise we have for you as you receive your package!
If you want to make your shopping experience easy, convenient and fun here are few reasons why you should shop for your Valentine on JUMIA this year:

●    OFFERS/ DISCOUNTS: Escape the hustle of Negotiations this month! Our sellers have offered the best deals for you to shop on JUMIA with price discounts enabling you to shop for your loved ones at a reasonable price.
●    CONVENIENT: By shopping online you can reach multiple shops which are just clicks away and available easily on your phone, laptop or tablet. Shop anywhere and anytime that is convenient for you.
●    VARIETY: No need to locomote around the city searching for different products that are rarely available at the same place. You can shop for shoes, clothings, tech devices, home furniture and personal pleasure products all in one place. JUMIA offers a great variety of products for your liking.
●    EASY RETURN / EXCHANGE: Not everyone will nail the perfect Valentine gift for their loved ones. It could be the wrong size for him/her or simply not what she had wished for. Nevertheless JUMIA’s return/ exchange policy has you covered. Each seller has their own return policy and time frame so be sure to check that out when you are placing your order.
●    SAVE TIME: JUMIA understands that Time is as precious as Money. Think of the gas money, traffic jam, overcrowding you will be avoiding if you simply order online that special something for your loved one.
●    SOUND SHOPPING SUGGESTIONS: For the clueless shopper who have no idea what to get their valentine this year, we are here for you! JUMIA will have selected products to give you gift ideas this year. Feel free to also ask us online for Gift Ideas and our team will respond to you to ensure you have a great shopping experience.
Be sure to check out our social media channels FaceBook, Twitter and Instagram as we continue to spread the LOVE this month with offers and giveaways.
For any inquiries regarding your order or any other assistance you may need don’t hesitate to call us for free on 0800 710 024

MASHINDANO YA GOLF QUARTER 6,2016 LUGALO YAFIKIA TAMATI CHINI YA VODACOM TANZANIA

$
0
0
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, kanda ya Kawe jijini Dar es Salaam,Straton Mchau(kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mshindi wa jumla wa mashindano ya Golf Quarter 6 ,2016, Hatibu Kisenkoro wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam,Iliyoandaliwa na Lugalo Breakfast Community Group na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Katikati ni kaimu Kapteni,Mada Margwe.
Mshindi wa Tatu wa mashindano ya Golf Quarter 6 2016, Godfrey Kilenga akikabidhiwa simu na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania,Kanda ya Kawe jijini Dar es Salaam, Straton Mchau (kushoto)wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Lugalo Breakfast Community Group na kufanyika katika viwanja vya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam chini ya Udhamini wa Vodacom Tanzania.Katikati anayeshuhudia ni Kaimu Kapteni, Mada Margwe.
Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Golf Quarter 6 2016, yaliyoandaliwa na Lugalo Breakfast Community ,Profesa Mahebu Nyirabu(kulia) akikabidhiwa simu na Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania,Kanda ya Kawe jijini Dar es salaam Straton Mchau (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.Katikati ni Kaimu Kapteni, Mada Margwe.
Mshindi wa jumla wa mashindano ya Golf Quarter 6 ,2016,Hatibu Kisenkoro (kulia) akikabidhiwa kikombe cha Ushindi na Ofisa Uendeshaji wa Klabu hiyo,Captain Amanzi Mandengule (kushoto) wakati hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya Golf Lugalo jijini Dar es Salaam,Iliyoandaliwa na Lugalo Breakfast Community Group na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Katikati ni Kaimu Kapteni,Mada Margwe.
Zawadi mbalimbali.

UZINDUZI WA BODI YA TANO (5) YA WADHAMINI WA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF TAREHE 04 FEBRUARY, 2017

$
0
0


Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) alipokea maelezo ya utangulizi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Karani Bee na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo. Kulia ni Mkurugenzi mkuu wa LAPF Bw. Eliud Sanga na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyozinduliwa pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa LAPF wakisilikiza kwa makini hotuba ya uzinduzi wa Bodi toka kwa Mgeni Rasmi Mh. George Simbachawene, Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
Mwenyekiti wa Bodi ya tano (5) ya Wadhamini Prof. Faustine Karani Bee akitoa maelezo ya msingi kuhusu Mfuko wa LAPF mbele ya Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko tarehe 04 Februari, 2017.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb). akitoa hotuba ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Mfuko wa LAPF mbele ya Mwenyekiti wa Bodi, Wajumbe wa Bodi, Menejimenti ya Mfuko na wanahabari, tarehe 04 Februari, 2017.
Mmoja wa Wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Ndg. Tumaini P. Nyamuhokya akijitambulisha mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya Mfuko wa LAPF.
Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi wa Bodi ya tano (5) ya mfuko wa LAPF Waziri wan chi – Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqarro, Mwenyekiti wa Bodi Prof. Faustine Bee, Wajumbe wa Bodi pamoja na Menejimenti ya Mfuko mara tu baada ya uzinduzi wa Bodi.

RWANDAIR KUANZISHA SAFARI ZINGINE MBILI KIMATAIFA, YAFANYA PUNGUZO LA ASILIMIA 45

$
0
0
Shirika la Ndege la RwandAir linatarijia kuanzisha safari zake za kuelekea nchini India na Zimbabwe mwanzo mwa mwezi wa nne mwaka huu, zikianzia Mjini Kigani nchini Rwanda.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo, Meneja mkazi wa Shirika hilo, Ibrahim Bukenya amesema  kuwa safari za Mumbai nchini India zitakuwa mara nne kwa wiki kupitia Kigali na kila siku kuelekea Harare nchini Zimbabwe.
Bukenya ameendelea kusema kuwa Shirika hilo la RwandAir limepunguza bei zake kuelekea miji 21 kwa asilimia 45%.Kwa mawasiliano zaidi kwa hapa Dar es salaam, email sales.dar@rwandair.com simu 022 2103435 au 0782 039152 na Arusha email sales.jro@rwandair.com simu 0785 869109 au 0732 978558. Unaweza pia kupata huduma za RwandAir kupitia kwa wakala wao aliyeko karibu nawewe.

DC TANGANYIKA,SALEH MHANDO AKABIDHI HUNDI YA SHILINGI MILIONI 56.7 KWA AJILI YA VIKUNDI 24 VYA WANAWAKE NA VIJANA

$
0
0
Kazi ya kuwawezesha vijana na akinamama katika wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,imeanza rasmi. 
 
Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika  Mh.Saleh Mhando akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli,leo wameshirki kupalilia shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu pamoja na kukabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana. 
 
DC Mhando amesema kuwa lengo ni kuhakikisha hadi Juni 2017 kiasi cha milioni 150 zinatotewa na Halmashauri ya Wilaya kuwawezesha vijana na akinamama watakaojiunga katika vikundi dani ya Wilaya ya Tanganyika.
 Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (tatu kulia) akikabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana katika kijiji cha Kabungu wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi.
Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (shati jeupe) akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli wakishiriki kupalilia shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu pamoja na kukabidhi hundi ya Milioni 56. 75 kwa ajili ya vikundi 24 vya wanawake na vikundi 8 vya vijana.  
 Mkuu wa Wilaya hiyo ya Tanganyika Mh.Saleh Mhando (shati jeupe) akiwa sambamba na viongozi wengine mbalimabli wakikagua shamba la Karanga la kikundi cha vijana ktk kijiji cha Kabungu Wilayani Tanganyika.

MAKAMU WA RAIS WA JICA ATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI NCHINI LEO

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford  Tandari (wa nne kushoto) pamoja na Makamu Kiongozi wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Tomiyoshi Kenichi wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa JICA na TIC mara baada ya mkutano wao uliofanyika leo kwenye Kituo hicho. 
Makamu Kiongozi wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Tomiyoshi Kenichi akiongozana na ujumbe wake, wakati walipotembelea Kituo cha Uwekezaji nchini kitenge cha huduma za mahala pamoja, wakiongozwa na Mwenyeji wao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford  Tandari (suti ya Bluu).
Kaimu Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa TIC, Mathew Mnali akieleza jambo kwa Makamu Kiongozi wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA), Tomiyoshi Kenichi, alietembelea kituo hicho leo.

CCM KIGOMA YAVUNA WANACHAMA WAPYA 868 AKIWEMO MWENYEKITI WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO NA CUF WILAYANI KAKONKO

$
0
0

CHAMA Cha CCM Mkoa wa Kigoma kimevuna jumla ya Wanachama wapya 868 kutoka vyama mbalimbali vya siasa akiwemo mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo Venasi Busunzu wa wilaya ya Kakonko na Mwenyekiti wa CUF Kilembwe Omari mgombea udiwani kata ya Sinuka wamekabidhiwa kadi ya chama hicho jana, katika hitimisho ya sherehe za madhimisho ya kutimiza miaka 40 ya CCM.

Akihitimisha sherehe hizo jana zilizo fanyika Kimkoa Katika kijiji cha Mwakizega Wilayani Uvinza Mwenyekiti wa CCM kigoma Amani Kabourou , alisema katika maadhimisho waliyoyafanya Mkoa mzima katika Wilaya zote walipatikana wanachama wapya 726 na kutoka vyama vya upinzani ni wanachama 146 ambao walikabidhiwa kadi katika sherehe za maazimisho zilizo fanyika jana katika Kijiji cha Mwakizega kata ya Mwakizega Wilaya ya Uvinza.

Alisema wanachama hao Waliamua kurudi katika Chama hicho kutokana na Shughuli kubwa zinazo fanywa na chama hicho , ambapo mpaka sasa kuna Maendeleo Makubwa yaliyo fanyika katika Kipindi cha Mwaka mmoja cha uongozi wa serikali unaongozwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Kabourou alisema Kwa sasa Viongozi wa chama hicho wameweka mikakati wa kukisafisha chama hicho kwa kuondoa viongozi wote wasio na sifa wanaokichafua sana na kuifanya CCM kuwa mpya na Serikali mpya kutokana na Misingi iliyo wekwa na waanzirishi wa Chama hicho.

Akizungumzia hatua hiyo, aliyekuwa mwenyekiti wa ACT wazalendo Bususnzu alisema amegundua mapungufu makubwa katika chama cha awali hali ,iliyomshawishi kujiunga na ccm ni pamoja na viongozi kuhamasisha misuguano kwa jamii ,ili nchi isitawalike lakini kwa awamu ya serikali ya wamu ya tano ya John Magufuli ni kigezo cha upinzani kukubali uwajibikaji wake wenye tija kwa wananchi.

Akizungumzia hilo Kilembwe Omari alisema amerudi kundini akiwa na wananchama 34 kutoka chama cha ACT wazalendo ,akidai amerudi kwa baba na mama yake akiwa na wenzake hao,sababu aminiye na kubatizwa ameokoka na anatumaini atakuwa mumini mzuri wa chama hicho.

Akiongezea hilo Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF,wilaya ya Kakonko Amana Ramadhani alisema anapokea kadi kwa hiari japokuwa amekulia katika upinzani akiwa mwenyekiti wa kina mama kwa miaka 15 wa chama cha CUF,kwa sababu ya sera zake akijua kitawakomboa wananchi,kumbe kipo kwa ajili ya kupata ruzuku ya serikali.


h

Taarifa ya Serikali Toka Bungeni


VIPINDI MAALUM VYA RADIO KUPINGA UKATILI VYA ZINDULIWA

$
0
0
Wizara ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii leo imezindua wa vipindi maalumu vya Radio ambavyo vinalenga kuelimisha jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto hapa nchini.  

Vipindi hivi vitakuwa vikirushwa na Radio maalufu nchini ‘RADIO TIMES 100.5 FM ambayo itashirikiana na wataalamu wa Wizara kusimamia na kuratibu maandalizi ya uendeshaji wa vipindi vya elimu na stadi za kuzuia ukatili wa kijinsia katika jamii. 

Akaiongea katika sherehe fupi ya uzinduzi wa vipindi hivyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema ubunifu wa vipindi hivi na Radio Times 100.5  ni sehemu ya mwitikio wa tasnia ya habari katika kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto ambao ulizinduliwa Desemba, 2016. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria mwanzo wa urushaji vipindi maalumu vya kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Ameongeza kuwa uzinduzi wa vipindi maalum vya elimu kwa umma ni kielelezo thabiti kwamba RADIO TIMES FM inadhamira ya dhati ya kusaidia juhudi za Serikali kuimarisha ulinzi na usalama wa mama na mtoto.  

Bi Sihaba aliendelea kusema kuwa  anatambua kuwa REDIO TIMES FM ni chombo binafsi ambacho kimetambua kuwa kinaowajibu wa kuhakikisha kuwa wanawake na watoto katika nchi yetu wanafurahia upatikanaji wa haki zao na wanaishi katika mazingira salama. 

Pia amewapongeza wanahabari wa vyombo vyote vinavyoelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu athari za ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kujadili afua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto na madhara ya ukatili huo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga akijiweka tayari kurusha kipindi maalumu cha kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha ametoa rai kwa vyombo vingine vya habari kufuata nyayo za Radio Times FM katika kukuza uelewa wa jamii kuhusu athari za ukatili dhidi ya wanawake na watoto.  

Katibu Mkuu huyo ametaja ukatili kuwa na athari  ambazo huwapunguzia uwezo wanawake na watoto katika kupata haki ya kushiriki shughuli za uzalishaji kwa uhuru na amani huku akaizitaja takwimu za Jeshi la Polisi kuwa zinaonesha vitendo vya ubakaji kwa mwaka 2015 vilifikia 3,444 na matukio ya shambulio, kujeruhi na matusi vilikuwa14,561. 

Aidha utafiti wa Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2010 inaonesha kuwa asilimia 39 ya wanawake wa umri wa miaka 15 – 49 walifanyiwa ukatili wa shambulio na vilevile Taarifa ya Utafiti wa Ukatili dhidi ya Watoto ya mwaka 2011 ilibainisha kuwa asilimia 72 ya wasichana na asilimia 71 ya wavulana nchini walifanyiwa ukatili wa vipigo. 

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa mtoto 1 kati ya watoto 3 wa kike na mtoto 1 kati ya watoto 7 wa kiume walifanyiwa ukatili wa kingono.  Aidha, takwimu zinaonesha kuwa watoto 15 kati ya watoto 100 wa kike hapa nchini wamefanyiwa ukeketaji.

Kwa ujumla takwimu hizi zinaonesha jinsi gani tatizo hili lilivyokubwa katika jamii zetu, hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua hatua thabiti kuzuia ukatili huo aliendelea kusema.

SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI KUTOKA CCM.

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya watu saba wakiwemo viongozi na wanachama wanne wa CCM ambao ni Ndg Ally Mmbaga, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa, Ndg Arnold Swai, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Hai, Ndg Anastazia Innocent Malamsha, Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) na Ndg Edwin Msele, Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro siku ya Jumapili ya tarehe 05th Februari 2017.

Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni ikihusisha gari ya mizigo aina ya Fuso na Toyota Hilux Surf iliyokuwa imewabeba Viongozi wa CCM waliokuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo na kusababisha vifo vyao.

Kutokana msiba huo, Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Ndugu Iddy Juma, familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanachama wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kufuatia vifo vya Viongozi wetu. 

Wana CCM nchi nzima, tunawaombea majeruhi kupona haraka, na tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu.  Amina.
Imetolewa na,

HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA, ITIKADI NA UENEZI

06/02/2017.

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

“Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” Alisema Waziri

Alisisitiza kuwa programu hizo ni pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa rasmi, mfumo wa mafunzo kwa vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza mafunzo kwa watanzania kulingana na soko lililopo kwa sasa.

Pamoja na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.

“Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi wala dini ya mtu bali kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri.

Aliongezea kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

“Serikali itatumia sekta zenye uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za Kilimo, majenzi, Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira mazuri kwa vijana kupata fursa za ajira”.

Mhe. Mhagama alisisitizia bungeni kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zitatumika kama chachu ya kuangalia maeneo yanayohitaji kusaidia kwa haraka na kupunguza changamoto hiyo kwa vijana.

“Kwa kuangalia tafiti ya Hali ya Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014 na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.

Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali bado ina wajibu wa kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya vijana.

Jalada la kesi ya mauaji Aneth Msuya laitwa mahakama kuu

$
0
0
Jalada la kesi ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mwenzake, Revocatus Muyela dhidi ya mauaji ya Aneth Msuya  limeitwa mahakama kuu.

Kesi hiyo, ilipaswa kutolewa uamuzi leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu anayeisikiiza lakini imeshindikana  kwa sababu jalada la kesi hiyo limeitwa Mahakama Kuu.

Hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo Wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwa sababu   hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.

Lakini kabla ya hakimu Mwambapa kutoa uamuzi,  ndugu wa marehemu waliwasilisha barua iliyopelekea zoezi la kusomwa uamuzi kusogezwa mbele.

Kwa mujibu wa barua hiyo wanataka hakimu ajitoe kusikiliza kesi hiyo kwa sababu hawana imani nae.

Kufuatia hivyo, mahakama kuu imeitisha jalada hilo. kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 20 mwaka huu kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

 Erasto Msuya, ambaye alikuwa mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzanite, pia aliuawa kwa kupigwa risasi, Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni,  kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Mapema hakimu Mwambapa alikuwa atoe uamuzi juu ya hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi pamoja na upande wa mashtaka ambapo Wakili John Malya aliomba washtakiwa hao waachiwe huru kwa sababu   hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia washtakiwa hao mahakamani hapo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa yeye aliiomba mahakama iwape muda ili waweze kutekeleza amri ya mahakama iliyotolewa.

Baada ya Wakili Kishenyi kuomba muda wa kutekeleza amri hizo za mahakama, Wakili Malya aliiambia mahakama kuwa amri ya mahakama ni sheria na upande wa mashtaka umekataa kutekeleza sheria hiyo, washtakiwa wanashikiliwa bila ya kuwa na hati yoyote inayowashikilia mahakamani hapo hivyo aliomba waachiwe huru.

Kishenyi alieleza kuwa siyo kwamba wameshindwa kuitekeleza amri ya mahakama ama vinginevyo, wanaomba muda na kwamba wanaweza kuiarifu mahakama kama wanakata rufaa ama la.

Washtakiwa hao kwa pamoja  wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth Msuya, kwa kumchinja, nyumbani kwake, Kibada Kigamboni Mei 25,2016.

Miriam  ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alikuwa mke wa aliyekuwa kaka wa Aneth, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama bilionea Msuya.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DKT. JUMA MALEWA APOKELEWA KWA KISHINDO MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokelewa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo baada ya kuapishwa rasmi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akipokea salaam ya heshima toka katika Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari(hawapo pichani) kwa ajili yake kwa heshima.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Maofisa na askari wa Jeshi la Magereza kwa ajili yake kwa heshima kama inavyoonekana katika picha.
Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga(kulia) akiteta jambo na Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi hilo Makao Makuu ya Magereza mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa mara baada ya kutoka kuapishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Ikulu Jijini Dar es Salaam Februari 6, 2017. 

WALEZI,WENYEVITI WA MITAA WAPEWA SIKU KUMI KUBAINI WATUMIAJI DAWA ZA KULEVYA

SERIKALI HAINA MAMLAKA KUWEKA UKOMO WA RIBA INAYOTUMIWA NA MABENKI

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali haina mamlaka ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na mabenki katika kutoa mikopo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameeleza hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi Machano Othman Said juu ya lini Serikali itaweka utaratibu wa kupunguza riba ya mikopo walau kufikia asilimia 10 – 12 badala ya sasa ambayo ni asilimia 17 – 20.
“Mabadiliko ya Sekta ya Fedha ya mwaka 1991 yalipelekea Serikali kujitoa katika uendeshaji wa moja kwa moja wa shughuli za kibenki nchini ili kuruhusu mfumo wa soko huria, hususan nguvu ya soko kuamua viwango vya riba za mikopo, riba za amana na gharama nyingine za huduma za kibenki,” alifafanua Dkt. Ashatu Kijaji.
Aliendelea kwa kusema kuwa viwango vya riba za mikopo na riba za amana pamoja na riba za mikopo kati ya benki na benki hupangwa kwa kuzingatia gharama za upatikanaji wa fedha, gharama za uendeshaji, riba za dhamana za Serikali, sifa za mkopaji na hatari ya mkopaji kutolipa mkopo pamoja na kasi ya mfumuko wa bei.
Aidha Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kutoa maelekezo kwa mabenki kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuyachukulia mabenki hatua endapo yatapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza.
Vile vile amesema kuwa kiwango cha hatari ya kutolipa mkopo ni miongoni mwa vigezo vinavyotumiwa na mabenki katika kupanga viwango vya riba za mikopo, ambapo kwa sehemu kubwa gharama za riba za mikopo hutegemea zaidi gharama za upatikanaji wa fedha pamoja na gharama za uendeshaji.
Pia amesema kuwa, ni muhimu kutambua kwamba kadri riba za mikopo zinapokuwa juu, ndivyo riba za amana zinapokuwa juu pia, ambapo wastani wa riba za kukopa kwa mwaka mmoja mwezi Juni, 2016 ulikuwa asilimia 13.67 wakati wastani wa riba za amana za mwaka mmoja ulikuwa asilimia 11.52 ikiwa ni tofauti ya asilimia 2.25.

MARTIN KADINDA NA MARAFIKI WA WEMA WASHINDA MAHAKAMANI HUKU AKISEMA YEYE SIO MENEJA WAKE MSANII HUYO KWA SASA

$
0
0
 Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam  pamoja na wanasheria

Na Humphrey Shao, 
Globu ya Jamii

Mbunifu wa mitindo maarufiu nchini, Martin Kadinda amesema kuwa yeye sio meneja wa msanii Wema Sepetu kwa sasa bali amefika mahakamani hapo kama rafiki wa karibu wa msanii huyo.
Kadinda amesema hayo katika maongezi maalum na mwandishi huyu  juu ya uhusiano wake na Wema Sepetu kwa sasa hasa mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya.
“Kwa sasa mie sio meneja wa Wema.K wa sasa mimi ni rafiki yangu tu wa karibu hivyo nimeamua kuja hapa kwa ajili ya kujua rafiki yangu amefikia wapi katika kipindi hiki ambacho anapitia magumu” amesema Kadinda

Amesema  kuwa yeye kwa sasa anaendelea na biashara yake ya kushona suti tu hili aweze kujipatia ugali wake wa kila siku na sio kujihusisha na makundi ambayo sio sahihi.
Kadinda na marafiki kadhaa wa Wema wameonekana mahakamani hapo wakisubiri kwa hamu kumuona rafiki yao anafikishwa hapo lakini hakufikishwa kama ilivyoelezwa awali.
 Baadhi ya marafiki  wa Wema Spetu wakiwa wamesimama kusubiri msanii huyo kuletwa mahakamani
 Jike Shupa na wenzie wakiwa wamekata tamaa mara baada ya kuambiwa Wema haletwi mahakamani


MBUNGE VITI MAALUM AIPONGEZA SERIKALI KWA KUFUNGUA VITUO VYA BENKI YA WANAWAKE MKOANI IRINGA

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Rose Tweve akiuliza swali bungeni.

Na Ripota wa Globu, Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Iringa Rose Tweve ameipongeza serikali kwa kuweza kufungua vituo vya benki wa wanawake mkoani humo na kutaka kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo mengine kwani wanawake wameamua kujiwezesha kimaisha kwa kujihusisha na ujasiriamali.


Rose alisema hayo baada ya kujibiwa swali bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla kuhusiana na kufungua kituo kwenye wilaya ya Mufindi ambapo kuna benki ya Mufindi Community Bank (MUCOBA)  kwani ni moja ya maeneo yanayokuwa kwa kasi sana ndani ya mkoa wa Iringa..



Akijibu swali hilo, Kigwangalla alisema kuwa mpaka sasa wananchi zaidi ya 6850 wameweza kupata mikopo kutoka katika benki ya wanawake ambapo zaidi ya wanawake 5350 wamechukua kutoka wilaya Makambako na Iringa Mjini lakini pia wanawake kutoka wilaya ya Mufindi wamefaidika pia.


Akifafanua zaidi kuhusiana na mpango mkakati wa serikali wa kuongeza vitu hivyo , Kigwangalla amesema kuwa kukosekana kwa mtaji wa kutosha kwenye serikali ndiyo sababu kubwa ya kushindwa kutanua vituo vya benki ya wanawake mikoa mbalimbali kwani mpaka sasa wameshafungua takribani mikoa saba nchini.

Mpaka kufika Desemba 2016 mikoa iliyoweza kupata huduma ya kituo cha benki ya wanawake ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Dodoma na Iringa  ambapo wamefungua vituo 252 nchini na tayari mkopo wa takribani milioni 120 zimeshapokeshwa kwa wananchi 146 wa Iringa wakiwemo wanawake 117 na wanaume 32.

Kigwangwalla alisema kuwa madirisha hayo ya mkoani Iringa yalifunguliwa mwaka 2014 ila mchakato bado unaendelea na iwapo serikali itafanikiwa kupata mtaji wataongeza vituo mkoani humo.

NEWZ ALERT: MOHAMED MATUMLA KUFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA MOI

$
0
0
Bondia Mohamed Matumla anafanyiwa upasuaji wa kichwa muda huu baada ya ngumi aliyopigwa kuleta madhara kwenye kichwa chake na damu kubainika kuwa imevujia huku  hali yake ikiwa nzuri

Taarifa zilizotufikia ni kuwa Vipimo vya CT scan vimeonyesha kuvuja kwa damu na imejikusanya sehemu moja na madaktari wanahangaikia kunusuru maisha ya mwanamasumbwi huyo ambaye hali yake si nzuri.

Operation ilichelewa kufanyika mapema kwa kuwa alihitajika kuongezewa damu, "tumefanikiwa kupata damu ameshaongezewa na akitoka chumba cha upasuaji ataongezewa damu nyingine"

Wapenzi na wadau wa ngumi kwa muda huu tumuombee DUWA mwenzetu operation yake ifanikiwe

SADICK & CO LTD ipo na mgonjwa toka aliposhuka kwenye ulingo  na kusimamia matibabu yake yote

Tutaendelea kuwapa taarifa baada ya kutoka chumba cha upasuaji na hali yake itakavyokuwa inaendelea. 
Promota STONE                      

RAUNDI YA SITA AZAM SPORTS FEDERATION CUP 2016/201

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii



Raundi ya Sita ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) yaani Azam Sports Federation Cup – 2016/17, itaanza Februari 24, 2017 kwa michezo minne kuchezwa kwa siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaopigwa saa 1.00 jioni.

Michezo hiyo kwa mujibu wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.

Mechi nyingine itakuwa ni kati ya The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.

Jumapili Februari 26, mwaka huu timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Jumatano Machi 1, 2017 Simba SC itacheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam wakati Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA SHIRIKA LA WAKIMBIZI

$
0
0
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto) ,baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala  ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi kutoka wizarani hapo, Harrison Mseke.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya(kushoto), alipofika ofisini kwake  kujadili masuala ya wakimbizi wanaohifadhiwa  katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi(UNHCR), Chansa Kapaya (kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri huyo,kujadili masuala  ya wakimbizi wanaohifadhiwa katika kambi mbalimbali nchini Tanzania.Mazungumzo hayo yamefanyika leo  jijini Dar es Salaam.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images