Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 120241 articles
Browse latest View live

Mrisho Mpoto aunga mkono harakati za RC Makonda za kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya

$
0
0
Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amefunguka kwa kusema kuwa yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaunga mkono harakati za Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda za kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya.
Akiongea Jumapili hii katika kipindi cha runinga cha Jambo Tanzania cha TBC1, Mrisho Mpoto amedai kila mtanzania anatakiwa kumuunga mkono RC Makonda kwa kuwa Madawa ya kulevya tayari yameteketeza vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
“Makonda mpaka hapo alipofikia tayari amefanya kazi kubwa sana na kila mtu katika nafasi yake anatakiwa kumuunga mkono, wengi wamekuwa wakiogopa kufanya kama alivyofanya lakini yeye amefanya hivyo,” alisema Mpoto. “Kwa hiyo huu siyo wakati wakusema kwa nini ameamua kuwaanika adharani, lakini mkumbuke mficha maradhi kifo humuumbua, kwa hiyo hata wewe kama kuna mtu unamjua unaweza kutoa taarifa katika vyombo husika ili kusaidia harakati zake ambazo ni nzuri kwa taifa letu,”
Aliongeza, “Tusiwe na tabia ya kuona madhara fulani yametokea ndipo tutangaze kusaidia, ni bora zaidi tutoe sauti zetu wakati huu ili kuwasaidia wengi zaidi, mimi nimenza kama hivi na nitaendelea kutoa sauti ya kama ninavyofanya, Madawaya kulevya hayakubaliki,”
Aidha, Mpoto aliyewahi kuwa balozi wa amani nchini, alisema kwamba amani haipatikani kwenye utegemezi na haiendani na vitendo vya uhalifu.
RC Makonda hivi majuzi aliweka hadharani majina wa watu wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya hali ambayo ilipelekea askari 12 kusimaishwa kazi kutokana na tuhuma hizo huku wasanii kama Wema Sepetu, TID, Nyandu Tozzy wakiwa ndani kwa mahojiano zaidi.

ZAIDI YA SHILINGI TRIONI 45 ZAHITAJIKA KUTOKA SEKTA BINAFSI ILI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI

$
0
0
Na Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma 
 KIASI cha Shlilingi Trilioni 48 kinahitajika kutoka Sekta Binafsi ili kufanikisha ujenzi wa miradi mikubwa ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa unaotekelezwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021 
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, amesema hayo mjini Dodoma wakati akifunga semina ya siku moja iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPS iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project) 
 "Imekadiriwa kuwa mahitaji ya fedha ya mpango huo ni takriban shilingi Trilioni 107, kati ya hizo shilingi Trilioni 59, sawa na asilimia 55, zitatokana na mapato ya Serikali na shiilingi Trilioni 48, sawa na asilimia 45 zitatokana na vyanzo vya Sekta Binafsi. 
 Amesisitiza umuhimu wa Sekta Binafsi kuwekeza zaidi kwenye kilimo na viwanda vitakavyosaidia kuongeza thamani ya mazao ya wakulima ili waweze kunufaika kiuchumi na kuendeleza nchi kwa ujumla Dkt. Mpango, ameahidi kuwa Serikali iko tayari kuhakikisha kuwa vitendea kazi muhimu vya utekelezaji wa mradi huo vinapatikana ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo ya ubia ukiwemo mradi wa ujenzi wa barabara ya njia sita kutoka Dar es salaam kwenda Chalinze.

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijabe (Mb), akizungunza wakati wa Semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu ugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akihutubia washiriki wa semina  iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma, ambapo waziri huyo ameitaka sekta binafsi kuwezesha upatikanaji wa Zaidi ya shilingi Trilioni 48 ili kusaidia ujenzi wa Miradi Mikubwa ya Maendeleo.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (wa pili kulia) akiandika mambo mawili matatu yaliyojiri wakati wa semina  iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini-TPSF iliyohusu zitaugharimiaji mkubwa wa miradi ya ubia kati ya sekta ya Umma na Sekta Binafsi kupitia mradi wa TVC (Tanzania Venture Capital and Private Equity Project), mjini Dodoma

MTI WA KIHISTORIA WAANGUKIA JUMBA LA MAKUMBUSHO DAR ESSALAAM

$
0
0
 Mti kubwa wa kihistoria aina ya Mkuyu wenye kusadikiwa kuwa na umriwa miaka zaidi ya mia moja (100) uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam umekatika tawi lake kubwa na kuangukia sehemu ya jumba hilo na kuleta madhara kidogo kwenye Jengo hilo. 
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea leo mnamo saa saba mchana wamesema hakuna mtu yeyeto alieathirika  na mti huo kwani wakati ukianza kuanguka waliokuwepo karibu walisikia mvumo mkubwa kama wa mvua kubwa unavuma na kisha wakaona tawi linaelekea chini  nao walikimbia eneo hilo haraka.
 Tawi la mti wa kihistoria ujulikanao kama Mkuyu uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni likiwa limedondokea sehemu ya jengo la Makumbusho hiyo.
 Tawi la mti wa kihistoria ujulikanao kama Mkuyu uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni likiwa limedondokea sehemu ya jengo la Makumbusho hiyo.
 Tawi la mti wa kihistoria ujulikanao kama Mkuyu uliopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni likiwa limedondokea sehemu ya jengo la Makumbusho hiyo.
Sehemu ya paa lililoangukiwa na mti huo.

MITANDAO ISITUGAWE WANASIMBA - HAJI MANARA

$
0
0
Na Haji Manara


Baada ya ushindi Musharraf wa hapo jana dhidi ya Majimaji wa goli tatu kwa bila, naamua kuperuzi mitandaoni kujua nn kimejiri huko, nn kimeandikwa na makocha wetu mahiri wa kukosoa, nakutana na vibweka vilevile vya siku zote, ahhh naamua kutoka huko na kuongea na wanangu masuala yao ya shule!!

Nimeanza na aya hiyo nikimaanisha kitu, tena kitu chenyew kwa sasa kishakuwa kama 'URADI'au ada, ni ukosoaji wa viwango vya majitaka, hususan pale Simba inapofungwa, na bad luck ukosoaji huo wa ajabu hufanywa na baadhi ya mashabiki wetu,

Mechi yetu ya mwisho tulipogongwa na Azam, ilikuwa kama jenahannam kwa sisi viongozi wa simba, hasa huku mitandaoni, ukiachana na hoja zao za tulikuwa tunaongoza ligi kwa points nane na sasa tumezidiwa na Yanga kwa points moja, ipo hoja nyingine ya wakosoaji, wanadai tumekaa miaka minne bila kuchukua ubingwa!!

Nianze na hili la points nane, ikiwa tuliwapita wenzetu kwa tofauti hyo ya points, nini ajabu Simba kupitwa point moja? factor moja ambayo haizungumzwi na wakosoaji ni je hzo points tumepoteza na nani na wapi? na kwa nn tulipoteza hizo points, hebu msomaji isafirishe akili yako na ujipe majibu mwenyew!!

Hili la kutochukua ubingwa miaka minne, je uongozi huu una muda gani ktk miaka hyo minne? na je hii ni mara ya kwanza hili kutokea kwa Simba au Yanga?hv mnazo kumbukumbu sahihi vjana wa dotcom?

Kwangu mm naamini huu ni mwaka wetu, ni mwaka ambao uongozi wenu umeamua kwa maksudi kuwapa furaha wanasimba, na ndio maana mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam, kuna hatua mahsuus ulizochukua, ambazo sisi tunaamin ztatusaidia sana kupata tunalolihitaji.Wanaasimba mpira wa miguu haupo kwa ajili ya kushinda kila siku,haupo kwa ajili ya ww kufurahi siku zote,,ukitaka kuamini hilo, nakusihi sana,achana na mchezo huu,,ruksa kupenda mchezo mwingine, Ajabu yetu timu ikifungwa wabaya ni viongozi, ikishinda wanaosifiwa ni wachezaji,

uogozi ulaumiwe kama mahitaji ya wachezaji hayatimizwi, sasa tumefungwa na Azam, viongozi hawafai, tumeshinda na Majimaji, KIAMA Kimerudi, uhhh lalaaa!!
lau mngejua juhudi zilizochukuliwa na uongozi hadi timu kurudi mchezoni kule Songea, mngekuwa mnaweka akiba ya maneno, mngekuwa hamtoki povu bila sababu yoyote,
Na kwa hili Mungu amekuwa upande wetu, lau Game na Majimaji ingekuwa dar, tungefungwa au kudroo, washabiki wengi wa dar hujitia ujuaji wasiokuwa nao, kutwa kushinda mitandaoni kuponda, lakini angalia walichofanya Songea, uwanja umetapika kama hatujatoka kufungwa, njiani ni Simba tu, kwetu hili liwe funzo, mpira hauchezwi ktk magrup ya watsapp, hauchezwi fb au insta, unachezwa uwanjani, na kuna vtu vingi vnavyofanya timu ipate matokeo.
Leo wapo baadhi yetu wanajiona wao ndio Simba zaid kuliko wengine, wanadhan wao ndio huumia timu inapofungwa kuliko wenzao, sasa hawa tuwaangalie huko mitandaoni, hawa wana nia ya kutugawa, wana nia ovu, na tusiwapuuze, tuwaondoe kuwa miongoni mwetu.
Jambo la msingi kwa sasa ni kupata points tatu kwa kila mchezo unaokuja, tunahitaji umoja kuliko kipindi chochote kile,tunahitaji kushauriana sio kukashifiana au kutukanana, Simba watsapp tunawahitaji sana ila kwa lengo la kujenga sio kubomoa,Najua wengine wataona nawakashifu, hapana, nawaambia ukweli na wakiona mchungu, hiyari yao,
Mwisho niwaambie kocha mkuu wa Simba ni mmoja tu, hatuwezi kuchukua ubingwa kwa kuwa na makocha lukuli wa mitandaoni, tuwape benchi la ufundi nafasi.
Tamati yangu ni kuwaomba tena na tena, mitandao isitumike kupotosha na kuzua uongo, mitandao itumike kiufasaha kwa maendeleo yetu, sio kutusi watu kwa kuwa upo mbali nae, maana tunajua wengine hutafuta kiki mitandaoni,
Tusonge mbele na tuanze na  Prisons kisha Gongowazi aje.

MAJALIWA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CCM YALIYOANDALIWA NA CCM MKOA WA DODOMA

$
0
0
 Washiriki wa Maadhimisho ya Ndani ya Mikaka 40 ya CCM yaliyoandaliwa na CCM mkoa wa Dodoma  wakimpungia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasalimia kwenye Kituo  cha Mikutano cha Dodoma  (DODOMA CONVENTION CENTER) leo Februari 5, 2017
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wana CCM walioshiriki katika Maadhimisho ya Ndani ya Miaka 40 ya CCM  yaliyoandaliwa na Mkoa wa Dodoma kwenye Kituo  cha Mikutano cha Dodoma  (Dodoma Convention Center) Februari 5, 2017.
Mjumbe  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  Dodoma convetion Center) , Februari 5, 2017.

 Mjumbe  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  Dodoma convetion Center) , Februari 5, 2017. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Anne Kilango, Mbunge wa Kuteuliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela (katikati)  katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya CCM yaliyofanyika  kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma (DODOMA CONVETION CENTER) Februari 5, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

IJUE Sheria ya Udhibiti na usimamizi wa Madawa ya Kulevya ya mwaka 2014 - kwa Kiingereza na kiswahili

Naibu Katibu Mkuu awatembelea Watanzania wanaoshikiliwa nchini Malawi

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi jana aliwatambelea Watanzania wanane wanaoshikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera.
Katika ziara hiyo, Naibu Katibu Mkuu  alifuatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Hassan Bendeyeko pamoja na maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi,aliwasihi watu hao kuwa wavumilivu wakati Serikali ikitafuta ufumbuzi wa suala hilo.
Balozi Mwinyi aliwaeleza Watanzania hao kuwa mazungumzo katika ngazi mbalimbali kati ya Tanzania na Malawi yanaendelea na kuna matumaini makubwa kuwa hivi karibuni ufumbuzi wa suala lao unaweza kupatikana.
Balozi Mwinyi aliendekea kuekeza kuwa yeye na wenzake wamekuja Lilongwe kushiriki kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi,   lakini wameamua kusafari  takriban kilomita 400 kutoka Lilongwe  hadi Mzuzu kuja kuwaona na kuwafikishia ujumbe kuwa Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kuwa suala hili linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.
"Nikufahamisheni kuwa jitihada katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu zinaendelea na hata Mhe.  Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokutana na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia jambo lenu lilikuwa moja ya masuala  waliyoyajadili.
Naibu Katibu Mkuu alisema kuwa alifarijika kuwakuta watu hao wote wapo salama na wenye afya nzuri na kuwajulisha kuwa ziara hiyo ya kuwatembelea na nyingine zilizofanyika siku za nyuma ni ushahidi dhahiri kwao na kwa Watanzania kwa  ujumla kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. Magufuli imedhamiria kuwahudumia Watanzania wote wa kada mbalimbali popote pale wanapoishi.
Watanzania hao wanane walikamatwa mwishoni mwa mwezi Desemba, 2016 na hadi sasa wanashikiliwa katika gereza kuu la Mzuzu. Watanzania hao ambao kati yao wawili ni wanawake  wamejitambulisha ni wakulima na wachimbaji wadogo wa madini wanatoka katika mkoa wa Ruvuma na walikwenda Malawi chini ya Taasisi ya CARiTAS kujifunza athari za migodi ya urani katika jamii. 
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


SHEREH ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CCM MKOA WA DODOMA LEO, YAFANA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Miaka 40 ya CCM mkoa wa Dodoma, zilizofanyika leo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma. Kulia ni Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Viongozi wakiwa meza kuu baada ya kuwasili ukumbini kuendelea na sherehe hizo
Wanachama wa CCM wakiwa wamefurika ukumbini wakati wa sherehe hizo
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimia wanacahama wa CCM wakati wa sherehe hizoleo katika ukumbi wa CCM wa Dodoma Convertion Centre nje kidogo ya mji wa Dodoma.


BALOZI AAHIDI INDIA KUISAIDIA SEKTA YA ELIMU TANZANIA

$
0
0
KUTOKANA na Tanzania kujikita kufufua uchumi katika sekta ya viwanda vya kati, Balozi wa India nchini, Sandeep Arya, ameihakikishia Tanzania kuisapoti kwenye suala la elimu kwa lengo la kuinua uchumi.

Akizungumza wakati akizindua maonyesho ya biashara yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara, Kilimo na Wenye Viwanda (TCCIA) mkoani Dodoma kwa kushirikiana na kampuni ya Global Education Link ya Tanzania juzi (jana), Balozi Arya alisema kukua kwa kasi uchumi wa India, kulitokana na kuwapo vyuo vingi vya elimu vyenye vifaa vizuri vya kufunduishia nchini humo.

“Kiwango cha elimu kinachotolewa India ni cha hali ya juu kutokana na upatikanaji wa vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia, jambo linalowahakikishia wahitimu kutoka vyuo mbalimbali kupata kazi kwa urahisi,” alisema Arya na kuwashauri wanaotaka kusoma nje kuwasiliana na Global Education Link kwa vile wana ushirikiano wa karibu na ubalozi huo.

Alisema suala la utandawazi na mahusiano baina ya nchi hiyo na nyingine katika kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu, linachangia kuwakutanisha watu wa aina mbalimbali kupata elimu kutokana na kuwapo na vifaa vilivyopo.Balozi Arya aliwahakikishia washiriki wa maonyesho hayo kuwa upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kufundishia nchini India, kumesaidia kutolewa kwa kiwango cha juu cha elimu.

Aidha, alisema baadhi ya mashirika makubwa duniani, viongozi wake walifanikiwa kusoma nchini India na kupata elimu iliyo bora.Ubalozi wa India umeanzisha ushirikiano na GEL katika kuwasaidia Watanzania wanaotaka kusoma nje ya nchi hasa baada ya ubalozi huo kujiridhisha na namna kampuni hiyo ya uwakala wa vyuo vya nje inavyowafuatilia wanafunzi wake hata baada ya kuwaunganisha na vyuo vya nje kujua maendeleo yao.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi katika tukio hilo aliwataka watanzania kujiimarisha katika ujuzi akisema ndio msingi wa kila kitu.Baadhi ya wanufaika wa elimu kupitia Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL), akiwamo Pelagia Mauma, alisema alifanikiwa kupata elimu bora nchini India kupitia kampuni hiyo kwa gharama iliyo nafuu zaidi.

“Gharama za elimu katika vyuo vyua India ni nafuu zaidi, hawa wenzetu hawaangalii ada bali wanachoangalia ni vipi mtu atafanikisha kupata elimu iliyo bora,” alisema Mauma.Afisa Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Dodoma, Fred Azaria pamoja na kueleza shughuli za chama chake, alisema wanalenga kupunguza umaskini kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma baada ya kuandaa maonyesho ya vifaa vya shule na zana za kufundishia kutoka India.

“Nawaomba Watanzania waweze kutumia fursa iliyopo ya kupata elimu, huku wakiwaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kujipatia elimu nchini India,” alisema. Nae Meneja wa GEL tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo alisema sababu ya kushirikik maonyesho hayo ni kutoa nafasi kwa Watanzania kuhusiana na namna gani mtu anaweza kufanya uchaguzi sahihi wa kozi ya pale anapotaka kusoma nje ya nchi.

“Tumekuwa mawakala wa vyuo vya nje kwa zaidi ya miaka kumi sasa, wengi wamekuwa wakipitia kwetu kuunganishwa na vyuo vya nje, tumeona tuje hapa ili waweze kupata ufahamu zaidi kuhusiana na uchaguzi wa vyuo vya nje na uchaguzi wa masomo ya kusomea pia,” alisema Hemed.

Hemed alifafanua kuwa kumekuwa na changamoto kubwa kwa Watanzania katika uchaguzi wa nini cha kusoma. “Utakuta wengi wanachojua ni udaktari, lakini kwenye udaktari kuna wa aina nyingi, kuna udaktari wa magonjwa ufahamu, udaktari wa meno tu, udaktari wa mifupa na kadhalika, kazi yetu ni kutoa ushauri wa aina hii. Tunafanya hivi ili kukumbushana kwa sababu kama wengi watakuwa kwenye fani au utaalamu wa aina moja, maana yake ni kwamba fani nyingine zitakosa wataalam au zitakuwa na wataalam wachache,” alisema.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep Arya.
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda akiteta jambo na Meneja wa Kampuni ya uwakala wa vyuo vya nje, Global Education Link tawi la Dodoma, Hemed Mlapakolo (mwenye shati jeupe). Kushoto ni Balozi wa India Sandeep Arya. Picha na mpiga picha wetu. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akisaidia kitabu cha wageni alipotembelea banda ya maonyesho ya Kampuni ya Uwakala wa vyuo vya nje ya Global Education Link juzi. Kulia ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.

NEWZ ALERT:WATU ZAIDI YA WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA MKOANI KILIMANJARO JIONI YA LEO

$
0
0

Habari ilizoifikia Globu ya Jamii jioni ya leo kutoka Mkoani Kilimanjaro,zinaeleza kuwa watu zaid ya watano wanadaiwa kupoteza Maisha,akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai,
Anord Swai,katika ajali ya gari dogo.Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea maeneo ya Mwika Mawanjeni maarufu kama Bar Mpya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Inaelezwa kuwa ndani ya gari hiyo walikuwemo watu sita wakiwemo viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Shauri Tanga wilayani Rombo.Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli breki na kuligonga gari dogo.

“Waliofariki ni Mwenyekiti wa Uvccm wilayani Hai na Mwandishi wa habari Leo Arnold Swai, mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro Ally Mmbaga na wanafunzi makada wa CCM kutoka vyuo vikuu vya ushirika na KCM.
 
 Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo ambaye inaelezwa kuwa amekimbizwa Hospitali kwa matibabu,Watu hao walikuwa wakitoka kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya kuzaliwa CCM wilayani Rombo”
Pichani ni aliyekuwa  Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali la Habari leo,enzi za uhai wake,Arnold Swai ambaye pia ni mmojawapo kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
 
Globu ya Jamii itazidi kuwaletea habari zaidi kutoka katika mamlaka husika,hususani Jeshi la Polisi.
 
Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi-Amin,




cameroon waibamiza Misri 2-1 na kutwaa kombe la Afcon 2017 huko Gabon

$
0
0
Timu ya  Cameroon ya safari hii ilikuwa mbovu katika historia. Angalau ndivyo walivyoonekana wiki mbili na nusu zilizopita, lakini mpira unadunda. Lolote laweza kutokea. Na baada ya wachezaji nyota wanane kujitoa kutokana na kocha wao Hugo Broos kusisitiza nidhamu, majina mengine  makubwa yakawekwa benchi. Lakini kikosi chake kilichokuwa na uzoefu mdogo kilifanya makubwa na hata kuweza kusawazisha na hatimaye kuishinda Misri kuipanchi hiyo ushindi wa mara ya tano wa kombe hilo la AFCON, na  kwanza  katika kipindi cha miaka 15.
Majina makubwa ndiyo yaliyorejea uwanjani na kuwezesha ushindi huo, magoli yote yakiwa yamefungwa na wachezaji wa akiba. Mohamed Elneny aliipatia Misri bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza lakini Nicola Nkoulou alisawazisha kabla bao la ushindi kuwekwa kimiani na Vincent Aboubakar zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo umalizike. Hakika lilikuwa goli tamu.
Msisimko ulikuwa mkubwa mno uwanjani wakati raia wa Cameroon wanaoishi Gabon walipojitokeza kwa maelfu kushangilia vijana wao, huku mabasi kibao yaliyosafiri usiku kucha  kutoka Doula na Yaounde yakileta mashabiki zaidi, na kwa mara ya kwanza uwanja wa L'Amitie ulifurika kwa mara ya kwanza.

Tanzania na Malawi zasaini kushrikiana katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba ya kufunga kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi kilichofanyika Liolongwe. kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhan Mwinyi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Francis Kasaila akiwasilisha hotuba katika kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi
Wajumbe wa kikao cha JPCC wakifuatilia kwa makina hotuba za Mawaziri wa Mambo ya Nje zilipokuwa zinawasilishwa
Sehemu nyingine ya ujumbe ikifuatilia hotuba za Mawaziri
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Malawi na Tanzania wakiweka saini mikataba ya kushirikiana katika Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga. Nyuma ya Waheshimiwa Mawaziri, kulia ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Bw. Mustafa Usi na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi.
Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini
Waziri Mahiga akisalimiana na wajumbe mbalimbali. Anayeshikana naye mkono ni Bi. Elizabeth Rweitunga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.
Picha ya pamoja kati ya Waheshimiwa Mawaziri na wajumbe walioshiriki kikao cha JPCC.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania na Malawi zasaini kushrikiana katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga
Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kimeweka mazingira mazuri ya kushughulikia mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa ambapo juhudi za kutafuta suluhu zilisimama kutokana na mabadiliko ya uongozi nchini Malawi.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga (Mb) wakati alipokuwa anasoma hotuba ya kufunga kikao hicho jijini Lilongwe siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017.
Mhe. Waziri alieleza kuwa kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Malawi ambao walifanya mazungumzo walipokuwa Ethiopia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika na kutoa wito kwa jopo la viongozi wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuongeza kasi ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Jopo la viongozi wa zamani wa SADC lililopewa dhamana ya kushughulikia suala hilo linaundwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais wa zamani wa Msumbiji; Mhe. Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini na Mhe. Festus Mogae, Rais wa zamani wa Botswana.
Waziri Mahiga alieleza kuwa japo Tanzania na Malawi zinatofautiana katika mpaka wa Ziwa Nyasa lakini tofauti hizo sio kikwazo kwa nchi hizo kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya faida ya wananchi wa pande zote mbili.
Alisema kikao hicho cha JPCC kinatoa fursa kwa pande mbili kujadili na kukubaliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano na kuweka utaratibu wa utekelezaji.
Aidha, katika kikao cha JPCC, wajumbe wanakitumia kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano yaliyoafikiwa.
“Nafurahi kusikia mmejadili na kukubaliana maeneo mengi ya ushirikiano ikiwemo biashara, kilimo, utalii, tehama, utangazaji, utunzaji wa mazingira na usafiri wa anga”. “Ni jambo la kupongezwa katika majadiliano yenu pia mmependekeza iundwe Kamati ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita ili kutathmini utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa kwa mujibu wa muda uliokadiriwa”.
Mhe. Mahiga alitoa maelezo namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyoboresha miuondombinu ya Bandari ya Dar Es Salaam, barabara na mipango ya kuboresha Reli ya TAZARA kwa kushirikiana na China ili Malawi iweze kusafirisha bidhaa zake kwa urahisi.
“Ni jukumu letu na pia ni wajibu wa kimataifa kuzihudumia nchi zisizokuwa na bandari. Hivyo, Tanzania ambayo imezungukwa na nchi nane zisizokuwa na bandari itaboresha miundombinu ili nchi hizo ziweze kusafirisha bidhaa zao bila usumbufu wowote.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Francis Kasaila alisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya bandari, barabra na reli ili Serikali ya Malawi na wafanyabiashara waweze kusafirisha bidhaa kwa urahisi. Alisema ili vituo vya mizigo vya Malawi vilivyopo Dar es Salaam na Mbeya vifanye kazi kwa ufanisi hakuna budi kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya TAZARA, barabara ya Dar es Salaam hadi Mbeya na kujenga Kituo cha Pamoja cha kutoa Huduma mpakani.
Kikao hicho kilimalizika kwa kushuhudiwa uwekaji saini wa mikataba ya makubaliano katika Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga.
Mhe. Waziri kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu amepangiwa miadi ya kuonana na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Prof. Peter Mutharika ambapo amepanga pamoja na mambo mengine kujadili suala la Watanzania wanane wanaoshikiliwa katika gereza kuu la Mzuzu kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera.
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 06 Februari 2017

KUMBUKUMBU

$
0
0
OMWANA THERESIA NYAMICHWO RUTAGERUKA

LEO 6 – FEBRUARI 2017, UMETIMIZA MIAKA 23 TANGU MWENYEZI MUNGU ALIPOKUTWAA TOKA HAPA DUNIANI.  PAMOJA NA KWAMBA KIMWILI HAUPO NASI, KIROHO TUNAKUKUMBUKA DAIMA.
TUNAADHIMISHA KUMBUKUMBU HII TUKIOMBA MWENYEZI MUNGU AWAKUTANISHE KWENYE RAHA YA MILELE NA MUME WAKO MPENDWA MWALIMU NOVATI RUTAGERUKA AMBAYE SIKU ZOTE ALIKUKUMBUKA KATIKA SALA ZAKE KABLA YA KUTWALIWA NA BWANA TAREHE 5 MEI 2010.
MNAKUMBUKWA DAIMA NA WATOTO WENU FROLIDA, ILLUMINATA, LIBERATA, DUNSTAN, JOYCE NA EDWIN PAMOJA NA WAKWE, WAJUKUU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI.
IBADA YA MISA YA KUMBUKUMBU ITAADHIMISHWA LEO JUMATATU TAREHE 6 - FEBRUARI - 2017 KATIKA KANISA LA MTAKATIFU MAURUS, KURASINI, DAR-ES-SALAAM SAA 12.30 ASUBUHI.

BWANA ALITOA, BWANA ALITWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE. AMINA

Mayrose pamoja na Baadhi ya Watanzania Waishio Marekani Katika Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa 2017, Maryland Marekani.

$
0
0
Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com
Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Vyama vya Siasa Vyatakiwa Kutoa Fursa za Uongozi kwa Wanawake

$
0
0
 Hata hivyo wamewataka wanawake kuendelea kujitokeza, kujiunga na vyama mbalimbali vya siasa pia kushiriki kugombea nafasi ili waweze kuonekana na kukwaa nafasi hizo. "Mbali na Vyama vya siasa kutakiwa kuregeza masharti na kutoa fursa kwa kundi la wanawake, wao pia wanatakiwa kujitokeza kushiriki katika siasa...na hata kugombea nafasi mbalimbali ili waonekane," alisema mmoja wa washiriki wa semina hiyo. 

Kwa pamoja viongozi hao walikubaliana kuendelea kuwaunga mkono kundi hilo katika ushiriki wa siasa ili kujenga usawa wa kijinsia katika nafasi za maamuzi kuanzia ngazi za chini na kuendelea. Kwa upande wake Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba akiwasilisha mada katika semina hiyo alisema wanawake ni wadau muhimu katika shughuli zote za kisiasa na maendeleo ya jamii hivyo kuna kila sababu ya kupewa nafasi ili waingie katika vyombo vya maamuzi. 

Alisema yapo matamko mbalimbali ya juu ya umuhimu wa kundi hilo kushiriki katika uchaguzi, japokuwa utekelezaji wake kivitendo umekuwa na changamoto kadhaa. Aidha alitolea mfano matamko hayo ni pamoja na Tamko la Kimataifa Kuhusu Haki za Binadamu (U 1948), Mkataba wa Kimataifa wa Kutokomeza aina zote za ubaguzi dhidi ya wanawake (CEDAW: 1979) na mpango kazi wa Beijing (1995). 

Pamoja na hayo alisema licha ya kundi hilo kusahaulika lakini limekuwa likitumiwa na vyama vya siasa kuhamasisha na kueneza sera zao ikiwemo kuongeza wanachama jambo ambalo linapaswa kuangaliwa kwa umuhimu hivyo kupewa fursa katika ushiriki.  
Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akiwasilisha mada katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Afisa Programu na Uchambuzi wa TGNP, Deogratius Temba (kulia) akifafanua jambo katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakichangia mada anuai katika Semina hiyoSehemu ya washiriki wa semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakifuatilia mada anuai. Semina hiyo liyofanyika Mabibo Jijini Dar es Salaam iliandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).Baadhi ya washiriki katika semina kwa baadhi ya madiwani, watendaji na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam, yaani Temeke, Ilala na Kinondoni wakiwasilisha kazi za vikundi baada ya majadiliano.


TTCL yaondoa changamoto ya Dawa kituo cha Afya cha Tandale

$
0
0
Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutatua changamoto katika sekta mbali mbali nchini ili kuboresha huduma za Kijamii zinazogusa maisha ya kila siku ya Wananchi kwa lengo la kuyaboresha na kuongeza kasi ya Nchi kupiga hatua za Maendeleo.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri Kindamba alipokuwa akikabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Kituo cha Afya cha Tandale, kilichopo Wilaya ya Kinondoni, mkoa wa Dar es salaam mwishoni mwa wiki hii. 

Msaada huo umekabidhiwa kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto, tukio lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mheshimiwa Ally Hapi ambaye ndie aliwezesha kupatikana kwa vifaa hivyo kupitia program yake maalumu ya kuwasiliana na Taasisi za Umma na Binafsi ili zisaidie kuboresha huduma za kijamii Wilayani kwake.

Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi ameishukuru Kampuni ya Simu TTCL kwa msaada iliotoa na kubainisha kuwa, msaada wa dawa na vifaa tiba utasaidia sana kuboresha huduma katika kituo hicho chenye kuhudumia idadi kubwa ya Wananchi wa kipato chini.

“Juhudi hizi za kusogeza huduma kwa wananchi ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha maisha ya watu wa hali ya chini na kuwaondoa katika unyonge unaowafanya kushindwa kutoa mchango stahiki katika jitihada za nchi kujiletea Maendeleo” Amesema Mhe Hapi

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameutaka uongozi wa Kituo cha Afya Tandale kuhakikisha kuwa unasimamia vyema matumizi ya dawa hizo ili zitumike kwenye malengo yaliyokusudiwa ambayo ni kuboresha huduma kwa Wananchi.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba amesema, TTCL imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Jamii kwenye sekta mbalimbali kama vile elimu, afya, michezo, matumizi ya teknolojia ya Habari na Mawasiliano, makundi maalum na wakati wa maafa.

“TTCL imetoa msaada huu wenye thamani ya shilingi milioni 5, dawa zilizotolewa ni pamoja na Paracetamol Syrup, Paracetamol Tabs, Diclofenac, Amoxicillin, Amoxicillin Granules, Folic Acid, Gloves Surgical, Bandage, Magnesium Trisilicate, Methylated Spirit na nyinginezo nyingi. Tunaamini kuwa msaada huu utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa dawa kwenye kituo hiki” amesema Waziri K.Kindamba. 

Aidha, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri W.Kindamba ametoa rai kwa taasisi na makampuni mengine kukusaidia juhudi za Serikali katika kusaidia huduma za Kijamii hali itayoimarisha uhusiamo mwema na Wananchi na kutoa suluhisho kwa changamoto zinazoikabili jamii katika maeneo mbali mbali nchini.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akikabdhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Tandale kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Mheshimiwa Ally Hapi akizungumza kwenye hafla ya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba kutoka Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL). Katika Haflya hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu, Bw Waziri W.Kindamba, Dr Zuhura Majapa Mratibu wa BRN Manispaa ya Kinondoni na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Tandale Dkt Emmanuel Kazimoto. 
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri W.Kindamba akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi msaada wa dawa na vifaa tiba kwa Kituo ch Afya cha Tandale, wilayani Ilala, jijini Dar es salama

Makamu wa Rais Mhe. Samia ahudhuria Mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi - Dubai.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na mmoja wa washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.
 Washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi likiendelea kufanyika jijini Dubai.
 Pichani kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya Washiriki wa mkutano wa Jopo la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi linalofanyika jijini Dubai.

DONDOO ZA MAGAZETI

MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 6, 2017

VIDEO: Je unafahamu chupa ya beer unatakiwa kunywa kwa saa moja? mtazame Dr. Ali Mzige akielezea nini maana yake!

$
0
0
Je, kwa wale wanaotumia vilevi kama bia, unajua kuwa chupa moja ya bia unatakiwa kunywa kwa saa moja?

Tumsikiliza mtaalam wa Daktari wa Afya ya Jamii na Familia Dr Ali Mzige hapa chini akizungumza na The Beauty TV juu ya suala hilo na usisahau ku-subscribe kupata updates zaidi. 
Viewing all 120241 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>