Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1549 | 1550 | (Page 1551) | 1552 | 1553 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Leo tumetembelewa na The Big Family UK ambao wamekuja kutufariji kutupa pole msiba wa baba.
  Pamoja na kutufariji , pia tulikabidhiwa keki ya pole iliyokatwa na wajukuu wa mzee Lukosi Sarah na Maria. Keki hiyo ilitengenezwa na Mnyakyusa Mrs Luhanga. The Big Family ndio waliotukatia tiketi  za ndege mimi na dada yangu kwenda msibani.

  Asanteni kwa kuja na Mungu awabariki

  CHRIS LUKOSI

   Keki ya pole
   Wajukuu wa mzee Lukosi Sarah na Maria wakikata keki ya pole
   Mfiwa Chris Lukosi amehemewa kwa upendo wa The Big Family UK
   The Big Family wakiwa nyumbani kwa Chris Lukosi
  Mrs Luhanga akimhakbidhi Chris Lukosi na dada yake keki ya pole.

  0 0


  Mrembo shabiki namba  moja  wa Lipuli Fc kikosi cha AMSHA POPO akishangilia ushindi wa Lipuli FC dhidi ya Polisi Dar kwa  kuzunguka Uwanja wa Samora mjini Iringa  na gari lililotengenezwa  kienyeji maalum kwa  ajili ya kushangilia ushindi wa Lipuli Fc


  0 0
  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula amezindua uwekezaji mkubwa wa hoteli ya kisasa ambayo ndiyo kubwa kuliko zote Mkoani humo, Mazubu Grand Hotel iliyopo Mji mdogo wa Mirerani.

  Akizungumza wakati akizindua hoteli hiyo, mhandisi Chaula amewataka wafanyabiashara na wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuwekeza kwenye mji mdogo wa Mirerani kuliko kuchuma madini hayo na kwenda kuwekeza sehemu nyingine.

  “Tunakupongeza mno ndugu yetu Elias Kipunile Maduhu kwa kufanikisha mradi huu kwani umetupa heshima kubwa watu wa wilaya hii ya Simanjiro kwani kwenye mkoa wote wa Manyara, hakuna uwekezaji mkubwa wa hoteli kama hii,” alisema mhandisi Chaula.

  Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel Elias Kipunile Maduhu, alisema uzalendo wa kuishi Mirerani ndiyo umesababisha yeye awekewe kwenye eneo hilo kwani mahali unapoishi inakubidi upathamanimi kama nyumbani kwako.

  Amesema Mazubu Grand Hotel imeshatoa ajira kwa watu 26 na lengo lao ni kuwapatia ajira watu 40 hadi 50 kwa siku za baadaye.
   Zoezi la uzinduzi wa Mazubu Grand Hotel, likiwa limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula kwa kukata utepe.
   Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula na Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel, Elias Kipunile Maduhu wakibadilishana mawazo baada ya kufanyika uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.
   Jengo la Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambao ni uwekezaji mkubwa kufanyika wa hoteli kwenye mkoa huo.
  Mkugurenzi wa Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Elias Kipunile Maduhu, akizungumza mara baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula kufanya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.

  0 0
  0 0

  Jengo la Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora kulikofanyikia zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Madiwani wa Halmashaurri hiyo pamoja na wananchi wa Halmashauri waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).

  Na Jumbe Ismailly, Igunga

  IDADI kubwa ya wananchi wa Wilaya ya Igunga, Mkoani Tabora wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao hali ambayo inachangia miili yao kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi.

  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk. Godfrey Mgongo aliyasema hayo wakati wa zoezi la kupima afya kwa watumishi,madiwani pamoja na wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) wa Halmashauri ya wilaya hiyo lililofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za Halmashauri hiyo.
   
  Baadhi ya wataalamu wa sekta ya afya waliokuwa wakitoa huduma za upimaji afya kwa watumishi wa Halmashauri ya Igunga,Madiwani pamoja na wananchi wa kawaida waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)ambapo iligundulika kuwa idadi kubwa ya wakazi wake wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya shinikizo la damu kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kupima afya zao na hivyo kuchangia miili yao kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi.

  “Kitu ambacho tumekigundua ni kwamba watumishi wengi au watu wengi wana uzito uliopitiliza,uzito mkubwa na hii inaweza ikapelekea ukapata magonjwa ambayo yatawaathiri katika maisha yao”alisema Dk.Mgongo.

  Hata hivyo mganga mkuu huyo wa wilaya alivitaja vitu vilivyopimwa na wataalamu hao kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza(TANCDA) kuwa ni uzito,shinikizo la damu,homa ya ini pamoja na kisukari na zoezi hilo limefanyika kwa siku nne ambapo lilianza kwa watumishi wa Halmashauri na baadaye huduma hiyo ilielekezwa kwa madiwani pamoja na wananchi.
   
  Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora wakiwa kwenye mkutano wa Baraza la kawaida la madiwani wa Halmashauri hiyo ambalo lilitumika pia kushiriki katika zoezi la upimaji afya kwa waliojiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).(Picha Na Jumbe Ismailly)

  Kwa mujibu wa Dk.Mgongo kati ya zaidi ya watumishi 60 wa Halmashauri hiyo waliopatiwa huduma ya upimaji wa afya, imegundulika kuwa tatizo kubwa linalowakabili watumishi hao ni uzito ingawa kuna tatizo la homa ya ini na ugonjwa wa kisukari ndiyo unaofuatia.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  JE, UNATUMIA JIKO LA GESI KUPIKIA SOMA HII MUHIMU.

  ... na uchukue tahadhari ili isitokee kwako. Hili linaweza kuwa ni kosa la kawaida katika kila nyumba.

  JINSI ILIVYOTOKEA.

  jiko la gas lilikuwa linamewaka na mapishi yakiendelea.

  Mama akaona mende jirani na sink la kuoshea vyombo. 

  Mara akachukua kopo la dawa ya mbu na kupuliza karibu na lile jiko la gas linalowaka.

  Ulitoka mlipuko mkubwa na ndani ya muda mfupi yule mama alikuwa ameungua kwa asilimia 65.

  Mumewe alikimbilia kuuzima ule moto na nguo zake nazo zilishika moto.

  Mumewe bado yuko hospitali akiuguza majeraha ya moto na bado hana habari kwamba mke wake alifariki alipofikishwa tu hospitali.

  Ni vema tukafahamu kuwa dawa zote za kuulia wadudu "Hit", "Marten", "heaven", "Raid" n.k. zina mchanganyiko wa madawa mengi yanayosababisha mlipuko mkubwa.

  Mchanganyiko huu wa madawa ni rahisi sana kusababisha mlipuko haraka sana.

  Tafadhali elimisha wanafamilia yako na rafiki zako kuhusu jambo hili, kwani yeyote yanaweza kumtokea.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  MSANII wa muziki wa kizazi kipya Benard Paul 'Ben Pol, ameachia video ya wimbo wake mpya unaitwa 'Phone' aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Mr. Eazi. 


  Akizungumza na Globu hii, Pol alisema kuwa wimbo huo ameutengeneza katika studio ya One love records, iliyopo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Tiddy Hotter. 

  Alisema tayari wimbo huo upo mtaani kwa video yake kuonekana ikiwa imetangulizwa na wimbo ambao ulitoka kwa audio. 

  Aidha Pol amewataka wapenzi wa muziki nchini waanalie ujio wa video hiyo ambao ana amini kila atakayepata nafasi ya kuiona. 

  "Nashukuru nimemaliza kurekodi na tayari video nimaenza kusambaza katika vituo mbalimbali vya Televisheni na katika mitandao mbalimbali, nina amini kila mdau anaipenda na kukubali ujio wa Phone. 

  Pol alisema ujio wa wimbo huo ni moja ya mipango yake ya mwaka 2017 na ameanza kwa kutoa wimbo huo wa 'Phone'. 

  "Wimbo wa Phone ni moja ya malengo yangu ya mwaka huu na ndiyo ujio wangu wa 2017, naomba wapenzi waupokee na kuusikiliza kila mtu ataelewa nini nimejipanga kupitia mwaka huu"alisema Pol. 

  Mwanamuziki huyo anayetamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo pamoja na, Moyo Mashine, Maneno, Sofia, Pete, Maumivu, Samboira na ameshirikishwa kwenye wimbo wa Darasa unaotamba kwa sasa nchini unaitwa muziki. 

  0 0
  0 0

  Wafanyabiashara kuunganishwa na huduma mpya ya intanenti ya  gharama nafuu ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania ili kuwarahisishia mawasiliano katika biashara zao ambapo gharama ya kuunganishwa zinawezesha unafuu wa shilingi 330,000/-

  Huduma hii iliyolenga kuwarahishia mawasiliano wafanyabiashara pia inawawezesha kufurahia huduma ya internet yenye kasi kubwa kutoka mtandao wa Vodacom.
  Huduma hii ya aina yake nchini inawezesha mteja kujipatia Kbs256  kwa gharama ya shilingi 100,000/-kwa mwezi ikiwemo na kodi ya ongezeko la thamani ambapo pia wanaweza kujipatia Mbps 2 kwa mwezi kwa gharama ya shilingi 200,000/- na huduma hizi zote mbili zinawawezesha kutumia internet bila kikomo. 
  Wateja wataunganishwa na huduma hii kutokana na mahitaji yao na watafungiwa vifaa vya kisasa vya uwezeshaji wa internet kwa kadri ya  watumiaji watakaotumia huduma hii kwenye biashara au taasisi.
  Kwa watakaohitaji huduma hii wakaingia mkataba maalumu na kampuni ya Vodacom ambao utadumu kwa kipindi cha miaka 2”.Alisema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu.
  Alisema kuwa kampuni yao imekuja na huduma hii maalumu kwa kuwa wakati wote inaleta ubunifu wa huduma zinazoendana na mahitaji ya wateja wake lengo kubwa likiwa ni kuwapatia huduma za uhakika za mawasiliano na za gharama nafuu ili kuwarahisishia maisha na kuwawezesha kufurahia intanenti yenye kasi kubwa nchini kutoka Vodacom. 
  Kupata huduma hii anachotakiwa kufanya mteja ni kutuma maombi kwenye barua pepe ya vodacombiashara@Vodacom.co.tz.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Kampuni ya Trumark inayofanya mafunzo ya kuboresha ufanisi katika jamii imefanya mafunzo ya kujitoleta kwa kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo ambaye pia ni Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Duniani kupitia Umoja wa Mataifa alisema kuwa ni muhimu vijana kutafuta na kukamata fursa mbalimbali kutoka kwenye jamii yao. Ikiwa ni pamoja na kujitolea kupitia vipaji vyao husuani elimu ili kuweza kuitumikia jamii.

  Warsha hii iliyolenga kutimiza moja ya majukumu ya kuwa Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi iliambatana na kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio, elimu na ajira huku wakiwajengea wanafunzi wa chuo hicho uwezo wa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka katika jamii yao.

  Mafunzo haya yalihimiza nguvu na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. Bi Agnes aliongeza kwa kusema kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri hasa unapoamua ikuletee mafanikio katika maisha.

  Jukwaa la Kimataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi lina washiriki kutoka nchi 198, watazamaji 900,000, washiriki 18,500 na mabalozi 410 duniani kote.

  Bi Agnes aliwashukuru Kampuni ya Kisima kwa kuweza kutambua umuhimu wakuwapatia vijana fursa nakuwezesha kufanikisha warsha hii muhimu. Na shukrani nyingine alizielekeza kwa uongozi wa chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam kwa kuruhusu kutumia chuo cha kama jukwaa la kuwapatia elimu hii muhimu wanafunzi wa chuo hicho.

  Tunategemea kufikia vijana wengi zaidi ili nao waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuwawezesha wanawake kiuchumi hususan kwa nchi yetu ya Tanzania.
   Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

  Muwezeshaji na Balozi wa Vijana kutoka East Community Youth Ambassador Platform Kamala Dickson akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
  Afisa habari wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.


  Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wakijiandikisha wakati wa semina ya kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa semina hiyo waliokaa na wanafunzi wa chuo cha ustawi wa Jamii.Picha na Zainab Nyamka.

  0 0


  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2017.

  Nape Nnauye ametoa taarifa hiyo leo katika ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na vyombo vya habari juu ya kuanza kwa sheria hiyo na kanuni zake.

  “Kwa mujibu wa kifungu cha 1 cha Sheria hiyo, ili ianze kutumika rasmi, Waziri wa Habari anatakiwa kuitangaza tarehe ya kuanza kutumika, hivyo napenda kuufahamisha Umma kuwa sheria hii imeanza kutumika tangu Desemba 31, 2016,” alifafanua Nape Nnauye.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kuanza kutumika kwa sheria hii ni jambo muhimu sana kwa tasnia hiyo kwa sababu inaihamisha taaluma ya habari kutoka fani ambayo mtu yeyote anaweza kujinasibu nayo hadi kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi, maadili yanayojulikana pamoja na vyombo vya kusaidia kusimamia utekelezaji wake.

  Vile vile amesema kuwa, sheria hiyo inaleta mfumo madhubuti wa kulinda haki za wanahabari kukusanya, kuhariri na kusambaza habari zao kwa uhuru.Pia sheria hiyo imeweka wajibu kwa wale watakaokiuka misingi na maadili ya taaluma hiyo, hivyo ukurasa mpya wa haki na wajibu umefunguliwa kupitia sheria hiyo.

  Aidha amesema kuwa, Wizara imechambua maoni mbalimbali kuhusiana na sheria hiyo ambapo moja ya maoni hayo ilikuwa ni kiwango cha elimu cha mtu atakayeruhusiwa kufanya kazi ya taaluma hiyo. Ambapo wapo waliopendekeza kiwango cha elimu kiwe cheti, wengine diploma, digrii na hata PhD na wengine walitaka awe mtu yeyote anayejua kusoma na kuandika.

  Amesema kuwa Serikali imesimama katikati ya maoni hayo, na sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni Diploma ya uandishi wa Habari. Hivyo Serikali imetoa kipindi cha miaka Mitano kuanzia Januari, 01, 2017 kwa waandishi ambao hawana sifa hizo kujiendeleza na kufikia kiwango hicho cha elimu.

  Hivyo basi, Idara ya Habari MAELEZO itaendelea kutoa “Press Card” bila kuwabana wanahabari kwa kuangalia vigezo hivi vya kitaaluma bali dhamana ya waajiri wao.

  Sheria ya Huduma za Habari, 2016 ilisainiwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Novemba 16, 2016 na kuchapishwa kwenye gazeti la Serikali Novemba 18, 2016.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akioongea na Waandishi wa Habari kuhusu siku rasmi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 pamoja na Kanuni zake za 2017 katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bungeni Mjini Dodoma 05/02/2017. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM.

  0 0

  Kushoto ni Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Pamela David Kirrita (41) akiwa na mwanamke mwingine raia wa Zambia Thelma Mkandawire (38) wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na kilo 4 za madawa ya kulevya aina ya cocaine katika hoteli moja kusini mwa jiji la New Delhi, India. 

  Naibu Mkurugenzi  Mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya cha New Delhi (NCB)  Rajinder Pal Singh amesema watuhumiwa walikamatwa katika hoteli iliyo eneo la Mahipalpur jana Februari 4, 2017. 

  “Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu, timu yetu ikatega mtego kwa Mkandawire aliyewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Indira Ghandi akitokea ughaibuni akiwa na mzigo huo. 

  “Baada ya kuchekiwa uwanjani pale aliondoka na taxi hadi hotelini. Timu yetu ilimfuatilia na kumuona mara alipofika hotelini akakutana na Pamela David Kirrita aliyekuwa aupokee huo mzigo”, alisema Mkurugenzi wa NCB tawi la New Delhi. 

   Amesema walipohojiwa Kirrita aibainisha kuwa alikuwa akiishi katika hoteli moja katika kitongoji kiitwacho Vasant Kunj tokea Januari, na kwamba alikuwa na mawasiliano na mtu mwingine raia wa kigeni ambaye ndiye angempasia mzigo baada ya kuuchukua toka kwa Mkandawire. 

  Polisi wanasema mzigo ulifichwa kwenye uwazi wa begi la safari, na kwamba Mkabdawire aliwaki kukamatwa nchini Pakistani mwaka 2015 na kukaa mahabusu kwa zaidi ya miezi sita, huku Pamela akikiri kutembelea  India zaidi ya mara sita tokea mwaka 2006.

  Kwa sheria za India, mshtakiwa atayekutwa na hatia ya madawa ya kulevya yaliyokuwa ya kibiashara ni kifungo cha kati ya miaka 10 ama 20 gerezani na faini ya Rs 1 lakh (sawa na dola za Kimarekani 15,000) ama Rs 2 lakhs (dola 3000).  0 0

  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa Tamasha la Michezo na Sanaa katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga mwezi Julai mwaka huu ambapo wanamichezo na wasanii zaidi ya 600 watashiriki. 
  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema michezo na burudani ambayo itafanyika ni pamoja na soka, mpira wa kikapu, wavu, riadha,ngumi mashindano ya magari, pikipiki, baiskeli na mpira wa pete. 
  Michezo mingine ni mchezo wa kujilinda wa Tae kwon-do, Wu- Shu, Sarakasi, ngoma, maigizo ya filamu, tamthilia, kwaya kienjili, Kaswida, muziki wa asili, muziki wa dansi,muziki wa kizazi kipya na ushairi. 
  Mwenyekiti Taalib alisema hiyo ni fursa nzuri kwa wasanii na wnamichezo hapa nchini kwani inatarajiwa kufanyika hapa nchini kila mwaka na milango iko wazi kwa wasanii na wanamichezo mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watapata nafasi ya kukutana katika kijiji chao kwa pamoja na kubasilishana mawazo na utaalamu kwa malengo ya kukuza na kuendeleza vipaji vyao pamoja na kudumisha umoja na mshikamano kati ya wanamichezo na wasanii hapa nchini. 
  Tamasha hili ambako awali lilikuwa kufanyika Juni mwaka huu limesogezwa mbele hadi Julai 13,2017 ili kupisha wasanii na wanamichezo kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na sikukuu ya Eid al fitri.
  SHIWATA katika Tamasha hilo itatoa chakula kwa wasanii na wanamichezo watakaoshiriki Tamasha hilo isipokuwa washiriki wtajitegemea wenyewe gharama as usafiri wa kwenda na kurudi. 
  Mwenyekiti Taalib alisema milango ipo wazi kwa nafasi as USHIRIKI kwa klabu za michezo mbalimbali na makundi na wasanii kushiriki katika Tamasha hilo.
  Orodha ya majina ya klabu na vikundi, bendi na washiriki na watu binafsi waijulishe ofisini SHIWATA kwa uratibu wa michezo hiyo kabla ya 28/2/2017 kuorodhesha
  majina ya timu pamoja na viongozi na namba zao za simu na michezo wanayoomba kushiriki. 
  Kutakuwa na mkutano wa viongozi wote watakaoshiriki Tamasha hilo 11/3/2017 saa 4 ukumbi wa hotel  ya Cyrstal Palace, Ilala Bungoni ili kupata taarifa za Tamasha hilo. Katika mkutano huo pia zitatolewa taarifa ya jinsi wasanii na wanamichezo wanavyoweza kujiunga na SHIWATA na kupata fursa ya kujenga nyumba zao binafsi katika kijiji cha wasanii.
  Wajumbe wa kamati ya kuratibu Tamasha la SHIWATA Julai mwaka huu katika kijiji cha wasanii cha Mwanzega, Mkuranga.

  0 0


  Australian mining company Volt Resources (ASX:VRC) recently announced that an independent German metallurgical laboratory has confirmed the high quality of the Namangale graphite concentrate. 
  The tests also show that the concentrate is highly suitable for producing commercial grade expandable graphite for flame retardant foam and graphite foil, which are two key growth markets for graphite distribution. 

  The report indicates: “expansion tests of expandable graphite made of flake graphite concentrate from Namangale were very successful compared with product from other origins.” 
  Volt notes that the German group that completed the testwork is a global specialist in graphite testing and analysis. 

  “This is highly encouraging news flow for Volt, as proposed regulatory changes in China and Europe for the mandatory use of non-toxic substances in flame retardant building materials could result in substantial future demand for expandable graphite,” the company indicates. 
  “Having independent test work confirm the suitability of Volt’s graphite product in the flame retardant building materials market is a key differentiating feature from rivals,” Volt adds. 
  Trevor Matthews, CEO of Volt, commented: “With recent initial tests in the U.S. confirming the high quality of Volt’s concentrate to be used in lithium-ion batteries, it is very encouraging to have independent confirmation that Namangale graphite concentrate is highly suitable for expandable graphite too. 
  The sales and marketing team will be targeting prospective end-user customers globally across a range graphite end-user markets. At this point in Volt’s development, it is a significant differentiating feature and competitive edge to be able to deliver concentrate that can make high quality spherical and expandable graphite for various downstream applications.” 
  RELATED:  Mahenge Graphite Total Mineral Resource Increase by 25% Namangale Graphite Project The Namangale graphite project in south-east Tanzania is wholly owned by Volt Resources. 
  In Q2 2016, the company signed three Memorandums of Understanding (MoUs) for graphite off-take with some of the largest companies in the lithium-ion battery market: Chinese Optimum Nano, Huzhou Chuangya and Shenzhen Sinuo. 
  The MoUs cover an annual production of 100,000t of graphite, of which 60,000t with Optimum Nano, 20,000t with Huzhou Chuangya and the remaining 20,000t with Shenzhen Sinuo. 
  Tanzania Graphite Tanzania’s largest graphite deposits are located in the central and east southern regions of the country. Graphite discoveries in Tanzania come mainly from Australia based graphite developers, Magnis Resources (ASX:MNS), Volt Resources (ASX:VRC) and Kibaran Resources (ASX:KNL).

  0 0  0 0

  Masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji yameendelea kuwa tatizo kwa taifa na ulimwengu mzima na ili kukabiliana na tatizo hili, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kimataifa na kitaifa katika kukabilana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
  Akiongea na vyombo vya Habari Jijini Dar es Salaam leo  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Watoto wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Margaret Mussai amesema Serikali inalaani na kukemea vikali ukatili kwani unadhalilisha na kunyanyasa hadhi na utu wa mwanamke na mtoto wa kike akisema jambo hili halikubaliki.

  Aidha aliongeza kuwa ni lazima jitihada za makusudi zichukuliwe na wadau wote kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa pamoja kuzuia na hatimaye kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii zetu, hususan kuzua ukeketaji.
  Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Bi. Margaret Mussai  pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeley ya Jinsia Bwana Julius Mbilinyi  akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani kughusu siku ya kimataifa ya kuzuia ukeketaji. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  Na Na Emmanuel J. Shilatu
  Nianze kwa kuitakia heri ya kumbukizi ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi, chama kinachoendelea kushika dola ya Tanzania toka kiasisiwe mwaka 1977 ambalo ni zao la vyama vya TANU na ASP.
  Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere (Tanganyika- Bara) na Abeid Amani Karume (Zanzibar - Visiwani) imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na utulivu huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote Yule.
  Tofauti na mataifa mengine Watanzania wako huru zaidi kwenda kokote kule ndani ya nchi na hata kuishi au kufanya kazi ama biashara bila ya bughudha yoyote endapo taratibu na sheria zitazingatiwa vyema.
  Hali hii ni tofauti na nchi nyingine zikiwemo za jirani kama vile Kenya , Kenya Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda ambapo ukabila umetalaki kuanzia ngazi ya kijiji hadi Taifa lakini kwa Tanzania hakuna ubaguzi wa rangi,dini wala kabila.
  Hiyo inatokana na uongozi imara, sera safi, upendo na kila aina ya ubora uliotukuka ndani yake kwa jamii ya kitanzania. Jambo linaloendelea kutia faraja ni kuwa tangu ianzishwe CCM imeendelea kuwa ni chama kinachotawala na kuongoza nchi. Na siri yote ya mafanikio hayo ni kutokana na kuwa nguzo imara ambazo ni Wanachama, Ilani ya chama, na Viongozi wake. Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Dar es Salaam, Tanzania.  Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, Dk. Victorina Ludovick amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao hospitali mapema kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya zao.
  Kauli hiyo imetolewa leo na Dk Ludovick kwenye maadhimisho ya Siku ya Kansa Duniani ambayo huadhimishwa Februari 04, kila mwaka. 
  Dk Ludovick ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sofia Mjema katika maadhimisho hayo, amesema kwamba wazazi wanatakiwa kuwapeleka mapema hospitali ili mtoto atakayebainika ni mgonjwa aweze kupatiwa tiba mapema kabla tatizo halijakuwa kubwa.
  Pia Dk Ludovick ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kuwahudumia watoto wenye saratani bure kwa asilimia 70 wakati asilimia 30 ya gharama za matibabu zinachangiwa na Taasisi ya Tumaini Letu.
   Mmoja wa wake wa viongozi, Germina Lukuvi akitoa zawadi kwa watoto wenye saratani katika maadhimisho ya Siku ya Saratani Duniani ambayo yamefanyika Viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam Leo. Kushoto ni  Dk Lodovick ambaye amemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sofia Mjema.
   Watoto wenye saratani hawakuwa nyuma katika maadhimisho hayo kwani wameshiriki na kucheza michezo mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku hii muhimu.
   Wazazi wa watoto wenye saratani wakifuatilia michezo mbalimbali iliyokuwa ikichezwa na watoto hao.

   Watoto hao wakicheza mchezo wa kuzunguka viti kwenye maadhimisho hayo leo.
   Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili na Chuo Kikuu cha Kairuki wakifuatilia watoto hao wakati wakicheza.
  Wanafunzi wakiwa na watoto ha oleo kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.
  Picha na John Stephen, 
  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)


  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye

  Na Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa wasanii na watu wenye majina makubwa ndio wanaoonekana zaidi katika athari za madawa ya kulevya ingawa wapo wengi katika jamii wanayotumia madawa hayo.
  Nape Nnauye ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa majibu kwa waandishi wa habari waliotaka kujua namna ambavyo wizara yake imelipokea sakata la kukamatwa kwa wasanii ambao wanatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya.
  “Kama wizara inayosughulikia suala la wasanii tunaunga mkono juhudi zozote za kupambana na jambo hili kwa sababu mwisho wa siku sehemu ya wadau wetu wanaathirika, hivyo basi juhudi za kupambana nalo zinaokoa wadau wetu,” alifafanua Nape Nnauye.
  Aliendelea kwa kusema kuwa kama wizara inayosimamia wasanii wamekuwa wakijadili na kuzungumza juu ya athari hizo za madawa ya kulevya kwa wasanii, aidha wapo wasanii ambao Serikali imewasaidiwa kupata matibabu kutokana na athari za madawa hayo, akiwemo mwanamuziki Rehema Chalamila anayefahamika kama Ray C.
  Aidha amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo hivyo hawajibiki kuuliza Wizara hiyo anapotaka kuchukua hatua zozote kwa wasanii waliopo ndani ya mkoa anaosimamia, lakini anapohitaji anaweza kuiuliza wizara hiyo.
  Nape Nnauye amesema kuwa ni kazi kubwa sana kwa mtu kutengeneza jina (brand)  lakini ni rahisi sana kubomoa, hivyo basi ni vyema busara ikatumika katika kuwashughulikia waathirika, vile vile watu wasihukumiwe kwa tuhuma.
  Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitangaza majina ya watu wanaotuhumiwa kuuza ama kutumia madawa ya kulevya wakiwemo wasanii, maaskari na wafanyabiashara na kuwataka kuripoti Polisi kwa ajili ya mahojiano. 

older | 1 | .... | 1549 | 1550 | (Page 1551) | 1552 | 1553 | .... | 3272 | newer