Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

NAPE AIPONGEZA SERENGETI BOYS KWA KUFUZU FAINALI ZA AFCON GABON 2017


MISA TANZANIA YAWAKUTANISHA WABUNGE NA WANAHABARI KUJADILI NAMNA NZURI YA KUSHIRIKIANA

$
0
0
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamewakutanisha wabunge pamoja na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Mkutano huu ulikuwa na lengo la kuwajengea Wabunge na Wanahabari uhusiano mzuri katika utendaji wao wa kazi. Bunge na Vyombo vya Habari ni Mihimili miwili ya dola (Mmoja ukiwa Rasmi na mwingine usio Rasmi) inayotegemeana sana katika utendaji wake wa kazi.

Kutokana na kazi kubwa ya Bunge ambayo ni kutunga sheria na kuwakilisha Umma katika mijadala mbalimbali ya maendeleo katika ngazi za Taifa na Jimbo lazima kutumia vyombo vya Habari kwenye kazi ya kutafsiri mipango na mikakati mbalimbali inayofanywa na Bunge katika lugha ambayo mpiga kura/mwananchi wa kawaida anaweza kuelewa. Lengo kuu likiwa ni kuharakisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii nzima.

Katika siku za karibuni kumetokea changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wa muhimili huu rasmi na muhimili huu usiokuwa rasmi, na hasa kutoaminiana na kushutumiana kwa namna moja ama nyingine. Kutokana na changamoto hizo hakuna budi kwawaandishi wa habari paamoja ili kujadili changamoto na kuja na suluhisho la changamoto hizo.

Semina hiyo imeshirikisha watu 55 ikiwa ni pamoja na wabunge mbalimbali toka vyama vyote, Wahariri wa vyombo Habari vilivyoko Dodoma na Bureau Chiefs wa vyombo vya Umma na Binafsi vilivyopo Dodoma.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya bunge na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Picha na Geofrey Adroph.
Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wabunge pamoja na baadhi ya wahariri na waandishi wa habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote.
Baadhi ya wabunge wakichangia mada kuhusu kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Bunge(wabunge) na wanahabari pamoja na kutoa maoni yao ili kuboresha utoaji wa habari kwa wananchi boila kujali itikadiza kivyama.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akijibu maswali kutoka kwa wabunge katika mkutano uliowakutanisha wabunge, wahariri na waabdishi wa habari katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyoulizwa na waandishi pamoja na wabunge walioudhuria mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma. 
Mmoja wa waandishi wa habari akitoa changamoto anazozipata kwenye kazi zake za kila siku za kuripoti habari mbalimbali.

NHIF KUWAFIKIA ASILIMIA 85 YA WATANZANIA IFIKAPO 2020.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana jini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu maboresho yaliyofanywa na Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Mfuko katika kupunguza magonjwa yasiyoambukiza . Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ongezeko la usajili wa vituo vya kutolea huduma kwa wanachama wa Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernard Konga .(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 03/02/2017

HOSPITALI YA KAIRUKI YATOA HUDUMA ZA AFYA YA MACHO BURE

$
0
0
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki, ambapo upimaji wa awali wa afya ya macho umefanyika kuanzia Februari 3-4 kwa gharama za hospitali hiyo pamoja na utoaji wa miwani ya kusomea na upasuaji mdogo bure.

 Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki. 
Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki Mikochezni jijini Dar es Salaam, Athuma Makolela akichukua maelezo ya mmoja wa wagonjwa wa macho waliofika hospitalini hapo kupata huduma zilizokuwa zikitolewa kwa gharama za hospitali hiyo. 
 Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.

DKT. MARY MWANJELWA AONGOZA MAADHIMISHO YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYA YA MBEYA

$
0
0

Mbunge viti maalumu Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akiwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya chama cha mapinduzi(CCM) Mbeya mjini ambapo ndiko anakotokaea amfagilia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kazi nzuri na kuwaasa wana CCM kumtumia ipasavyo. Pichani kutoka kushoto ni Dk. Mary Mwanjelwa, Afisa muuguzi Neema Kapungu,pamoja na Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Kiwanja Mpaka ndugu Stella Moses katika mazungumzo wakati mbunge Mwanjelwa alipoenda kuwajulia hali wagonjwa.
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.
Mbunge viti maalumu Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akisalimiana na mtoto wa Bi Vumilia Daud moja kati ya akina mama walio jifungua katika Hospitali hiyo ya Kiwanja Mpaka iliyopo Jijini Mbeya.
Mbunge viti maalumu Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Ccm wilaya ya mbeya akiongoza zoezi la ugawaji wa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa walio kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Kiwanja mpaka ikiwa ni kuadhimisha miaka 40 ya chama cha mapinduzi Ccm kiwilaya maadhimisho yalitofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Sangu jijini Mbeya,
Baadhi ya wanachama wa chama cha mapinduzi Ccm wakifuatilia kwa makini mkutano wa ndani wa Mh.Dkt.Mary Mwanjelwa katika maadhimisho ya miaka 40 ya Ccm Wilaya ya Mbeya mjini. 

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al Najem walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili namna ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini itakayo fadhiliwa na serikali ya Kuwait ikiwemo uchimbaji visima vya maji, miradi ya kuendeleza elimu na kuboresha sekta ya afya. 
Waziri Mhe. Mahiga akimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Najem 
Waziri Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini wakifurahia jambo 

KONGAMANO KUJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako Ijumaa Februari 03, 2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga  lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro. Picha zaidi BOFYA HAPA

MAKAMBA AWATAHADHARISHA WATAALAM WA ATHARI ZA MAZINGIRA KUHUSU UWEPO WA VISHOKA KATIKA TASNIA HIYO:

$
0
0
Na: Frank Shija – MAELEZO
Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini wametahadharishwa kuwepo kwa matapeli wanaingilia taaluma hiyo kwa lengo la kufanya udanganyifu na kujipatia kipato.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira Tanzania (TEEA) leo Jijini Dar es Saalam.
Makamba amesema kuwa taaluma ya tathmini ya Athari za Mazingira ni ya shughuli ambayo inahitaji mkubwa sana na ni kwa mujibu wa sheria za nchi lakini kumekuwapo na makanjanja ambao wamekuwa wakifanya uraghai kwa wawekezaji na kutia doa tasnia nzima ya taaluma ya uthamini wa athari za mazingira.
“Serikali inakusudia kubadilisha kanuni na taratibu ili kuongeza udhibiti wa udanganyifu katika eneo la Tathmini ya Athari za Mazingira(IAE) kwa kuweka viwango stahiki kwa wataalamu wa tathmini ya athari za mazingira vitakavyozingatia elimu na uzoefu,” alisema Makamba.
Aliongeza kuwa ni vyema sasa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalumu hao kushirikiana kuhakikisha taaluma hiyo haingiliwi na makanjanja ili kufanikisha utoaji wa huduma zenye viwango stahiki na vya kuridhisha.
Awali akiwasilisha salamu za Bodi ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Profesa Ruben Mwamakimbullah amesema amemshukuru Waziri Makamba kwa kukubali kujumuika na wataalamu hao katika mkutano huo muhimu na kuongeza kuwa wao kama Bodi watafanyia kazi ushauri wote alioutoa na kuahidi kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta heshi kwa tasnia ya tathmini ya athari za mazingira na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Bonaventure Baya amesema kuwa mkutano huo umekuwa ukiwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ambapo utumia fursa hiyo kukumbushana mambo yanayohusu weledi na majukumu yao.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa mkutano huo ni wa tatu kufanyika ambapo umetanguliwa na mikutano iliyofanyika februari 2011 na Machi 2015 na kuongeza kuwa NEMC imekuwa ikiratibu mkutano huo kwa lengo la kuwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ili kujadili changamoto zao na kupeana uzoefu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathminiya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo) ).
Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mwandisi Bonaventure Baya akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo)
Mjumbe wa Bodi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Ruben Mwamakimbullah akitoa salamu za Bodi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mazingira Prof. Salome Misana katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam waTathmini ya Athari za Mazingira Dar es Salaam jana (leo))
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo).(Pichazotena Benjamin Sawe)

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Oman

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Oman nchini Mhe.Ali A. Al Mahruqi alipowasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Oman nchini Tanzania Mhe. Mahruqi wakionesha nakala ya hati ya utambulisho
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Balozi Mteule wa Oman nchini
Mazungumzo yakiendelea, Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Abasi Kilima akifuatila mazungumzo
Picha ya pamoja

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Iran

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mousa Ahmed Farhang aliwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza mara baada ya nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe.Farhang. Kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Iran nchini na Maafisa Kutoka Wizarani (kulia) wakifuatilia mazungumzo. Katika mazungumzo hayo Waziri alimkaribisha Balozi na kumhaidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezazi wa majukumu yake na kwa nchi ya Iran kwa ujumla, ili kuendeleza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu kati ya Tanzania na Iran.
Waziri Mhe. Balozi Dk. Mahiga akizungumza na mgeni wake Mhe.Balozi Farhang
Balozi Mteule wa Iran Mhe. Farhang akizunguza mara baada ya kuwasilisha nakala za hati za utambulisho
Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Iran nchini Tanzania Mhe. Farhang

Wema, TID na wengine katika shutuma za madawa YA KULEVYA

MTENDAJI MKUU MAHAKAMA YA TANZANIA NA WATAALAMU BENKI YA DUNIA WATEMBELEA MAHAKAMA YA MWANZO KIGAMBONI

$
0
0
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akizungumzia kuhusu ujenzi wa mfano wa majengo ya Mahakama  wa kutumia teknolojia  yenye gharama nafuu ijulikanayo kwa jina  la Moladi kwa Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia(WB),Waleed  Haider Malik (katikati) na   Mratibu wa Programu za Benki ya Dunia katika nchi za  Burundi, Malawi, Somalia na Tanzania, Preeti  Arora,(wa  pili kulia) wakati wataalamu hao walipotembelea leo  Mahakama ya Mwanzo Kigamboni iliyopo jijini Dares Salaam. Kushoto wa pili ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma na   Mhandisi Martin Frimos(kushoto).
 Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga(kulia) akizungumzia kuhusu ujenzi wa mfano wa majengo ya Mahakama  wa kutumia teknolojia  yenye gharama nafuu ijulikanayo kwa jina  la Moladi kwa Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia(WB),Waleed  Haider Malik(kushoto) na   Mratibu wa Programu za Benki ya Dunia katika nchi za  Burundi, Malawi, Somalia na Tanzania, Preeti  Arora,(katikati) wakati wataalamu hao walipotembelea leo ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Kigamboni iliyopo jijini Dares Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga (kulia) akionesha mfano wa majengo ya Mahakama  wa kutumia teknolojia  yenye gharama nafuu ijulikanayo kwa jina  la Moladi kwa Mtaalamu kutoka Benki ya Dunia(WB),Waleed  Haider Malik(kushoto wa pili ) na   Mratibu wa Programu za Benki ya Dunia katika nchi za  Burundi, Malawi, Somalia na Tanzania, Preeti  Arora(wa pili kulia, wakati wataalamu hao walipotembelea leo  Mahakama ya Mwanzo Kigamboni iliyopo jijini Dares Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania, Mhe. Zahra Maruma.Picha  na Magreth Kinabo- Mahakama ya Tanzania.


VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 108: Princess Diana, The Oscars, David Beckham, Kim Kardashian na Beyonce

HABARI NJEMA: MKATABA NA MKANDARASI WA MRADI WA UJENZI WA RELI YA UMEME KIWANGO CHA “STANDARD GAUGE” KIPANDE CHA DAR-MOROGORO (KM 205) WASAINIWA

$
0
0
Tangu kuingia madarakani kwa awamu ya tano ya uongozi wa nchi yetu, msisitizo mkubwa umewekwa katika kutekeleza ahadi ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge. 
Kwa kulitambua hilo mwaka wa fedha 2015/2016 Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) ilianza maandalizi ya Ujenzi wa reli mpya ya standard gauge kwa kuanza kuandaa makabrasha ya zabuni za kuwaajiri mkandarasi wa ujenzi wa reli ya kati pamoja na mshauri mwelekezi mnamo mwezi Mei, 2016 na hatimae, Zabuni ilitangazwa tarehe 9 Septemba, 2016 kwa kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na tarehe ya kurudisha zabuni ilikuwa 6 Disemba, 2016.

Wakandarasi 40 walinunua zabuni na baada ya tathmini ya zabuni, Ubia (JV) kati ya YAPI MERKEZİ İNŞAAT VE SANAYI A.Ş.  (Uturuki) MOTA-ENGIL, ENGENHARIA E na CONSTRUÇÃO ÁFRICA, S.A. (Ureno) ilionekana kukidhi vigezo vya kiufundi na kifedha.Timu ya watalaamu ilitumwa kutembelea miradi aliyopata kuitekeleza huko nchini Uturuki, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Msumbiji na Afrika Kusini na kujiridhisha. Baada ya majadiliano yaliyofanyika kati ya tarehe 21 january, 2017 mpaka 2 Februari 2017 hatimaye maafikiano ya mkataba yalifikiwa kufanya ujenzi kama kama ifuatavyo:-

  1. Kilometa 205 za njia kuu na Kilomita 95 za njia za kupishania treni na maeneo ya kupangia mabehewa jumla kilometa 300, kwa uzani wa tani 35 kwa ekseli,

  2. Ujenzi wa miundimbinu ya umeme, Dar-Morogororo na kwenye njia za kupishania na kupangia mabehewa ya treni,

  3. kiwango cha mwendo kasi wa treni kuwa kilomita 160 kwa saa,

  4. Stesheni 6 za abiria na 6 za kupishania treni,

  5. Kujenga wigo wa kilomita 102 kwa usalama wa watu na magari lakini vivuko vitajengwa kwa matumizi ya waenda kwa miguu na magari pamoja na mifugo.

  6. Muda wa mradi ni miezi 30 baada ya kuanza ujenzi,

Leo tarehe 3 Februari, 2017, ikiwa ni miaka 112 tangu reli ya zamani iliyopo ijengwe, serikali ya awamu ya 5 imeamua kujenga reli mpya ya standard gauge kwa mizigo tani milioni 17 kwa mwaka kwa treni ya umeme yenye mwendokasi wa kilometa 160 kwa saa na miundombinu yenye uhimili mkubwa wa tani 35 kwa ekseli. Kwa hakika nchi yetu itasonga mbele kwa kasi na kuvuna uchumi wa kijiografia ilionao.

Leo tunashuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa sehemu ya kipande cha reli ya kati kati ya Dar es Salaam na Morogoro chenye Kilometa 205 kati ya Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli na Ubia (JV) kati ya YAPI MERKEZİ İNŞAAT VE SANAYI A.Ş.  (Uturuki) MOTA-ENGIL, ENGENHARIA E na CONSTRUÇÃO ÁFRICA, S.A. (Ureno). Gharama za mradi zitakua ni dola za kimarekani 1,029,900,000 ukiongeza na kodi ya serikali dola za kimarekani 185,382,000 jumla kuu ni dola za kimarekani 1,215,282,000. Kipande hiki ni sehemu ya kwanza kati ya 5 ambazo zitatekelezwa hadi kufikia mwanza. Sehemu nyingine ambazo zimetangazwa na zabuni zake zitafunguliwa mwezi wanne mwanzoni ni:-


a)      Morogoro hadi Makutopora                336Km            (Sanifu-Jenga)

b)      Makutopora hadi Tabora                     294Km            (Sanifu-Jenga)

c)      Tabora hadi Isaka                                133Km            (Sanifu-Jenga)

d)     Isaka hadi Mwanza                             248Km            (Jenga)


IMETOLEWA NA:

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,

RAHCO

Dar es Salaam

03 Februari, 2017

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza  wakati wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Katibu mkuu wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano (sekta ya uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza  katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni
 Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu Mhe.Profesa Richard Sigalla akizungumza  katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni
 Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,Masanja Kadogosa kwa kushirikina na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki,Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio, wakisani  mkataba wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (Standard gauge) kutoka Dar es salaam hadi Morogoro unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki, Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio wakibadilishana  mikataba hiyo
 Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Meneja wa Kanda ya Africa Mashariki, Murat Hasim na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Motaengil Africa,Manuel Antonio wakiinyanyua juu mikataba hiyo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.



Sheria Ngowi kuteka soko la fashion nchini...Nini mipango yake?

MSAMA PROMOTIONS YAANZA MAANDALIZI YA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama ametangaza mbio za kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo linataraji kufanyika April 16 Mwaka huu

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Alex Msama amesema kuwa Tamasha hilo la kusifu na kuabudu,ambalo ni kubwa nchini kuliko matamasha yote litakuwa la aina yake katika mwaka huu wa 2017.
Msama amesema kuwa kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu itakuwa ni ''Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu'' ,Lengo ikiwa ni kudumisha amani ndani ya nchi yetu  katika kipindi chote
 
“Napenda kuchukua fursa hii kuwaambia wapenzi wa muziki wa injili kuwa Msama Promotion imejipanga vyema kwa mwaka huu kuhakikisha kuwa inawaleta watu pamoja katika sehemu ambayo walikuwa wanaipenda ya kumtukuza mungu kila wakati wa pasaka kwa kuimba pamoja katika Tamasha la Pasaka wakiwa na wanamuziki maharufu wa muziki wa injili nchini”amesema Msama.

Msama ameweka wazi kuwa kutokuwepo kwa Tamasha la Krissmas kumezidi kuongeza ari ya watu kutaka kushiriki tamasha la Pasaka na kujionea mambo mbalimbali yanayolijumuisha tamasha hilo ambalo huandaliwa kwa umakini mkubwa.
 
Msama ametoa wito kwa wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hili ili kuweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji. 
 
Amesema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litafanyika katika mikoa mitano ili kuwapa fursa watu wa mikoani kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili na kusema kuwa tamasha hilo litaanza katika mkoa wa Dar es Salaaam.
 
Msama alimaliza kusema kuwa kwa sasa yupo katika hatua za kukamilisha vibali mbalimba vkiwemo vya Baraza Sanaa nchini (BASATA),yote hiyo ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda katika mstari ulionyooka 

MADEREVA NA ABIRIA WA BODABODA WANAOKIUKA SHERIA MATATANI JIJINI DAR ES SALAAM

Bamiza TOP MUSIC Chart 4th Feb 2017

TEMBELEA KAOLE SNAKE PARK-BAGAMOYO KUJIONEA AINA MBALIMBALI YA NYOKA NA NDEGE PIA

$
0
0
Kaole Snake Park - Bagamoyo ndio sehemu pekee utakayoweza kuona nyoka wa kila aina na kuwafahamu kiundani, kwani ni hifadhi yenye aina mbalimbali ya nyoka na baadhi ya wanyama wengine pamoja na ndege. hutajuta kutembelea Kaole Snake Park - Bagamoyo.
Na baada ya kuufanya utalii huo wa ndani katika Kaole Snake Park, utaweza jipatia vyakula vya aina zote na vinywaji mbalimbali toka katika mghahawa wa kisasa huku ukipata upepo mwanana wa Bahari. Ni mahali pazuri kutembelea na familia. Tafadhali wajulishe ndugu, marafiki na majirani .

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images