Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live

IN LOVING MEMORY

0
0
Miss Neema Edward Mkwelele (BA Honors - Broadicasting, University of Falmouth, Cornwall, United Kingdom) 
January 05, 1989 - February 21, 2011.
 It has been six years now since you passed away, but to us  it seems like yesterday.

Your life was short with us indeed. Your bright smile, your spirit and presence are always in our hearts. 

They say that there are  reasons, they say that time will heal, but neither time nor reasons, will change the way we feel.  It  is hard forever.  Your legacy is in our heart prints you left behind.
 We profoundly miss you and Loving you more forever. 

Mom, Daddy and Mike. 
Amen.

BREAKING NYUZZZZ....: JESHI LA POLISI LAWASIMAMISHA KAZI ASKARI 12 WALIOTUHUMIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA

0
0
Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike dhidi yao. 

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni Askari.

"Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na Wasanii wote waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo" alisema IGP Mangu.
Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama. Hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.

HOSPITALI YA AGHA KHAN YAADHIMISHA SIKU YA SARATANI KWA KUCHANGIA DAMU

0
0
 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
HOSPITALI  ya  Agha Khan kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika kuadhimishia siku ya saratani duniani wameendesha uchangiaji damu kwa ajili kuokoa wgonjwa wa saratani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uchangiaji Damu katika Hospitali ya Agha Khan, Daktari wa Hospitali hiyo, Omary Sharman amesema katika kuadhimisha siku hiyo wamelenga kupata dawa chupa 100.
Amesema kuwa saratani inahitaji kuwa damu ya kutosha kutokana wagojwa kuhitaji damu kila wakati hivyo jamii ijenge mazoea ya kuchangia damu katika kuokoa wagonjwa  wa saratani pamoja wagonjwa wengine wasio na saratani.
Nae`Meneja wa Masoko na Mawasiliano waHospitali hiyo Olayce Lotha amesema kuwa damu inahitajika kwa kiwango kikubwa katika kuokoa wagonjwa wenye mahitaji ya kuongezewa damu.
Amesema Hospitali ya Agha Khan imekuwa ikifanya vipimo vya saratani ya matiti kila jumamosi ya mwisho wa mwezi bure  hivyo wanawake wanaaswa kufanya vipimo  katika hospitali ya Agha Khan.
Nae Afisa Uhamasishaji wa mpango wa Taifa wa Damu Salaama, Fatuma Mjungu amesema kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani ndio kuongezeka kwa uhitaji wa damu katika kuokoa maisha yao.
Amesema jamii inawajibu wa kujitokeza katika uchangiaji damu kutokana na uhitaji watu wenye matatizo mbalimbali na kupona kwao kunahitaji kupata damu.
 Daktari wa Hospitali ya Agha Khan, Omary Sharman akiteta jambo na mchangiaji damu ,Sreejith Menon leo katika maadhimisho ya siku saratani duniani leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salaama, Fatuma Mjungu akizungumza na Michuzi Blog juu ya wananchi kuchangia damu ili kuokoa wagonjwa wenye mahitaji  leo  jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Masoko na Mawasiliano waHospitali  ya Agha  Khan Olayce Lotha akizungumza Michuzi Blog juu wanawake kujitokeza kupima saratani kila jumamosi ya Mwisho wa mwezi bure katika hospitali  hiyo.
Sehemu ya wachangiaji damu wakiwa katika vitanda leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NDUGU WAGOMEA MAITI YA MTOTO HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mzazi Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini, akiwa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, alipozungumza na mwanahabari akidai amebadilishiwa mtoto aliyejifungua.
 Mama mzazi wa Julieth, Veronica Lucas akiwa ameshika shavu kwa masikitiko kufuatia tukio hilo.



 Shangazi yake Julieth, Judith Christopher akielezea tukio hilo 
kwa mwanahabari.
 Julieth Daud (kulia) akiwa na dada yake nje ya wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Julieth (aliyekaa kushoto), akiwa na ndugu zake nje ya
wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo.

Na Dotto Mwaibale
MZAZI Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake wamegoma kuchukua mwili wa mtoto kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake kutokana na kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kujifungua.
Akizungumza kwa masikitiko nje ya viwanja vya hospitali hiyo Dar es Salaam jana, Daudi alisema kitendo alichofanyiwa kimemuumiza sana pamoja na ndugu zake wengine.
Alisema alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith Christopher.
"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya kipimo hicho nilijisikia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.
Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.
Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.
Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.
Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.
Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mama yake kuiharibu mimba hiyo kwa nia ya kuitoa na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa mfu.
"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNN na ili mama wa mtoto aruhusiwe kutoka hospitali inatakiwa ipelekwe barua ya mwenyekiti wa mtaa wake anakoishi" alisema Christopher.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo hakuwa tayari kuzungumza kwa njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

Article 0

VOA SWAHILI: UNDANI Juu ya ukamataji watuhumiwa wa “unga” Tanzania

KAIMU MKURUGEZI MTENDAJI WA TANESCO, DKT.TITO MWINUKA AKAGUA VITUO VYA KUPOZA UMEME VYA WILAYA YA TEMEKE NA KARIAKOO

0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt. Mwinuka alisema,  ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.
“Barabra zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt. Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa Kilovolti 132.
Dkt. Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.

 Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
 Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
 Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi BOFYA HAPA

Dk.Shei awaandalia chakula Maaskari walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi

0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia mkono maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati alipowasili katika  hafla ya chakula maalum kwa Askari hao iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni (kulia) Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman ,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman  wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika   hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi  Zubeir Ali Maulid na  Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia)  wakiwa katika   hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,hafla hiyo  iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni

Open Volunteer Opoortunities in Arusha,Tanzania

0
0
The contribution of volunteers in international development is invaluable. The Foundation for African Empowerment (FAE) is seeking for volunteers to join its management team based in Arusha, Tanzania by filling the following roles:-
1.    Fundraising and Communications Manager
2.    Program Manager
3.    Finance and Administration Manager
To learn more about us, the opportunities and how to apply, please visit, http://www.thefae.org/career-2/. Also, to learn more about the advantages and what to expect while volunteering with us, visithttp://www.thefae.org/ways-to-volunteer.  

WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE WAJENGEWA UWEZO KUHUSU SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI NA HAKI YA KUPATA TAARIFA NA WAJIBU WAO JUU YA SHERIA HIZO

0
0
Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakifu  wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari  mkoani Dodoma katika  ukumbi wa Hazina  Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika kazi zao.
Mjadala huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
 Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila siku.
Wakili wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.
  Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.



CCM YASOMBA WANACHAMA WAPYA 102 WAKIWEMO WA CUF,CHADEMA NA ACT WAZALENDO WILAYANI KAKONKO MKOANI KIGOMA

0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imevuna jumla ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf.

Wanachama hao ambao wamepokelewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako ambaye aliwakabidhi wanachama hao wapya kadi 102 , akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Wilaya ya Kakonko pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilayani humo .

Zoezi hilo alilifanya jana katika Sherehe za maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko, ambapo Wanachama kutoka katika Vyama vya ACT wazalendo, NSSR Mageuzi, CHADEMA na Chama cha Wananchi CUF ambao waliamua kuvihamba Vyama hivyo kutokana na Waanzilishi wa Vyama hivyo kukosa uzalendo kwa Nchi yao kwa kuwashawishi viongozi walio chaguliwa na vyama hivyo kuipinga Serikali katika masuala ya Maendeleo.

Sambamba na zoezi hilo Ndalichako aliwaomba Wanachama Wa CCM Wilayani humo katika uchaguzi wa viongozi wa Chama 2017 kuhakikisha Wanachagua viongozi wazalendo Wanaoweza kukijenga chama katika Misingi ya Uzalendo, amani na mshikamano kama Waanzilishi wa Chama hicho walivyo kijenga Chama hicho ambacho kinazidi kuwa ni Chama kinacho wajali wanyonge.

Alisema Kauli mbiu ya maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha mapinduzi ni CCM mpya na Tanzania mpya .kauli hiyo haiwezi kukamilika endapo chama hicho kitapata viongozi wasaliti wasio na mapenzi na Chama ambao wengi wao wametumika kununuliwa na vyama vya upinzani katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo CCM imepoteza majimbo wengi kutokana na viongozi hao waliokisaliti Chama.

"Nianze kwa kuwapongeza Wanachama walio amua kurudi katika Chama cha Mapinduzi wamefanya jambo zuri sana, CCM ni chama ambacho kikitoa ahadi zake lazima zikamilike na ni chama chenye misingi ya uwajibikaji, uzalendo amani na ushirikiano ndio maana Wananchi wengi wanaendelea kukiamini chama chetu kutokana nuwaombe Wanachama Wenzangu tusikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wasio kipenda chama kikiuka Misingi ya Waanzilishi Wa chama chetu walioiweka ambayo inatusaidia Chqma hiki kuwa na Amani na mshikamano tofauti na Vyama vingine", alisema Ndalichako.

Kwa upande wake Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Wa Kigoma,Naomi Kapambala aliwashukuru Wanachama hao kwa kukiamini Chama hicho na kuamia kujiunga! Aliwaahidi Wanachama hao kuwa Chama hicho kitaendelea kutenda haki na kuwatumikia Wananchi katika misingi ya uwajibikaji na kujitegemea ilikuhakikisha Chama hicho kirudisha misingi yake ya zamani.
mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakishirika kufanya usafi katika kuadhimisha miaka 40 ya CCM .
Wajumbe na wanachama mbalimbali wa chama CCM katika kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwake,walishiriki kwenye kazi mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi na kufanya usafi
Baadhi ya ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf wakila kiapo.

WAALIMU WAISHAURI SERIKALI KUTOCHANGANYA SIASA NA ELIMU

0
0

Na Anthony John Glob Jamii.
 
 Chama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia wameitaka serikali kutokuchanganya maswala ya siasa na elimu kwakuwa yanawaathiri wanafunzi .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa miradi wa chama hicho Goodluck Moleli amesema kuwa walimu wameonekana kutokushirikishwa katika maswala ya mabadiliko ya mitaala ya elimu na badala yake kutokujua mambo yanayo endelea katika mabadiliko ya mitaala hiyo ya elimu.

‘’Leo hii tumekutana hapa katika warsha hii ya walimu iliyoandaliwa na Ceta ilikujadili ni jinsi gani ya kuboresha elimu ya Tanzania Lakini tunaiomba Serikali ipunguze maswala ya kubadilisha mitaala ya elimu mara kwa mara kwakuwa wanafunzi wengi wanashidwa kufanya vizuri katika masomo yao’’ amesema Moleli

Mbali na hayo Mwalimu wa shule ya sekondari ya Kibweheri iliyopo Kibamba Sabrina Makafu amesema mtawala bado unashida na silabasi bado haziendani na vile tunavyo fundisha darasani mfano katika somo la kingereza unakuta tunacho fundisha sio kile kinacho toka katika mitihani.

‘’Inatupa sisi ugumu wa kufundisha kwakuwa tunayofunsisha hatuna uhakika kama ni hayo yatakayo letwa hivyo tunaiomba serikali kulifanyia kazi swala hili’’ amesema Mkafu.
Mkurugenzi wa miradi wa chama cha walimu wanaofundisha masomo ya uraia Googluck moleli akizungumza na waandishi wa habari mapema leo,jijini Dar.
Mwalimu wa shule ya sekondari sabrina makafu akizungza na waandishi wa habari jijini hapa leo hii
 

DKT NCHIMBI AAGIZA MAAFISA KUSIMAMIA MIRADI INAYOTEKELEZWA WALENGWA WA TASAF

0
0
Na Gasper Andrew- Singida.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameagiza maafisa mifugo kata kusimamia kwa karibu miradi ya ufugaji kuku na mbuzi inayotekelezwa na kaya maskini zilizopo kwenye mpango wa TASAF 111.

Amesema kuku au mbuzi katika miradi hiyo wakifa kwa kukosa huduma kutoka kwa maafisa mifugo,maafisa hao watalazimika kufidia kuku au mbuzi hao watakaokufa.

Akilijengea nguvu agizo lake hilo Dkt. Nchimbi alitoa kutoka mfukoni kwake shilingi 150,000 taslimu na kumpatia afisa mifugo kata ya Kikonge Wilayani Iramba kwa ajili ya kuikarabati pikipiki yake iweze kumrahihishia kufika kwenye miradi ya kaya maskini.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo juzi muda mfupi baada ya kumaliza kukagua bwawa la kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba linalojengwa kwa nguvu za kaya maskini.Amesema serikali pamoja na wadau wanaotoa fedha kwa kaya maskini,ili ,ziweze kujikwamua kutoka lindi la umaskini.

“Njia mojawapo ya kuzisaidia kaya hizi maskini kuboresha vipato vyao,ni hii ya miradi midogo midogo ya ufugaji kuku,mbuzi na mifugo meinge.Ninyi maafisa mifugo ambao mpo karibu na kaya hizi,zisimamieni kikamilifu,msisubiri mfuatwa,ninyi ndio muifuate miradi huko iliko”,alisisitiza.Aidha, mkuu huyo wa mkoa, amewataka watendaji hao wahakikishe wana simamia watoto wa kaya maskini wana hudhuria shuleni bila kukosa.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (anayeangalia kamera) akimpatia Nya Mathias shilingi 34,500 kama malipo ya kuchimba bwawa kwa siku 15 ambapo kila siku anapaswa kulipwa shilingi 2,300. Fedha hizo zimetolewa na TASAF 111 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia miradi ya jamii iliyoibuliwa na walengwa wa TASAF.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akiangalia bwawa linaloendelea kuchimbwa na kaya maskini za kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba kupitia TASAF 111. Mkuu huyo wa mkoa ameagiza halmashauri zote zisaidie kutoa fedha ili ujenzi wa mabwawa yaliyoibuliwa na kaya masikini yaweze kukamilika kwa muda mfupi.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Stephano Mkiya akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kuanzisha ufugaji wa mbuzi na pia anamudu kuwasomesha watoto wake.
Mkazi wa kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba Mkoani Singida Elizabeth Mkumbo akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la kuhaulisha fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini, Elizabeth amesema kupitia fedha za TASAF ameweza kujenga nyumba bora ya mabati na kwa sasa ana uhakika wa chakula tofauti na kipindi hajaunganishwa na mpango wa TASAF.
Mratibu wa TASAF Mkoani Singida Patrick G. Kasango akizungumza muda mfupi kabla ya zoezi la uhaulishaji wa fedha za TASAF 111 za kunusuru kaya maskini 146 katika kijiji cha Kikonge wilaya ya Iramba mkoani hapa. Kwa mujibu wa Kasango hadi sasa kaya 39,102 maskini Mkoa wa Singida zimenufaika kwa kupatiwa zaidi ya shilingi bilioni 20.3.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

WAFANYAKAZI WA SERIKALI WILAYANI HANDENI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO WAKIHITAJIKA KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI

0
0
Wafanyakazi wa Serikalini Wilayani Handeni wametakiwa kutoa ushirikiano kwa namna yoyote ile kama kuna eneo wanatakiwa kutoa ushahidi Mahakamani. Wametakiwa kuhudhuria mahakamani ili waweze kusaidia haki iweze kupatikana kwa wakati.

 

 
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alipokuwa akihutubia wananchi na wataalamu mbalimbali kwenye ukumbi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya  siku ya sheria Nchini  iliyoandaliwa na Mahakama ya Wilaya mwaka 2017 yenye kauli  mbiu ya  “ umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi”.


Gondwe alisema “amani na utulivu ndio matunda ya Haki, sehemu yeyote iliyokosa amani na utulivu basi lazima kuna haki imepokonywa” Kuli mbiu yetu inatukumbusha wadau wote ambao tunasimamia sheria kuanzia jamii ya kawaida , wataalamu, mawakili, wanasheria ,TAKUKURU, uhamiaji na magereza tuweze kufanya kazi kwa pamoja ili haki iweze kutendeka kwa wakati na kukuza uchumi wetu.


Aidha alieleza kuwa TAKUKURU, Magereza, Uhamiaji , Wanasheria na Mawakili wa Serikali na kujitegemea hawataweza kufanikiwa katika kupambana na Rushwa na kutoa haki kama Mahakama haitakuwa mdau mkuu katika hili. Alisema kuwa kwa kuliona hilo Mahakama imetoa elimu kwa  wananchi wiki nzima juu ya umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati kuwezesha ukuaji uchumi.


Mahakama yenyewe imefahamu  nafasi ya kusimama na kuweza kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha kwamba wananchi wanoishi Handeni wanapata haki mbali na changamoto mbalimbali zinazoikumba Mahakama hasa ukosekanaji wa watoa ushahidi hali inayopelekea kuchelewa kwa kesi na maranyingine kufungwa kwa kukosa ushahidi uliojitosheleza. Mwananchi anapodai haki lazima afahamu kuwa anao wajibu wa kufanya ili haki hiyo aweze kuipata, alisema Mh. Gondwe.
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo

 Afisa upelelezi Bw. Paul Kimaro akitoa hotuba fupi wakati wa maadhimisho ya sheria
 Mkuu wa Wilaya na wataalamu mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa.
 Waendesha mashtaka wa Wilaya ya Handeni Bw.Joseph Hamisi na Nzagalila Kikwelele  wakisikiliza hotuba wakati wa maadhimisho.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wikaya ya Handeni Bw. Noel Abel akisalimia wananchi.

The Embassy of Switzerland Contributes to East Africa’s Premier Music Festival

0
0
The Embassy of Switzerland has contributed over TZS 260 million to support the Sauti za Busara music festival for the next three years. The Swiss Ambassador to Tanzania, H.E. Florence Tinguely Mattli, met with the Chairman of the Busara Promotions Board of Trustees Hon. Simai Mohammed for the handover at the Swiss Embassy offices in Dar es Salaam on February 3. 

The Sauti za Busara festival is one of Africa’s leading music events. This unique annual festival promotes respect for diversity by bringing people together to celebrate live music from across the continent. This festival’s mission is to increase visibility and accessibility for African music, develop skills and opportunities for those in the music industry and strengthen regional and international networking and partnerships. 

“Switzerland has been promoting and supporting various initiatives and events within the arts and culture sector in Tanzania for over a decade now,” said Ambassador Tinguely Mattli. “The Sauti za Busara festival is a good example of a cultural event that brings people together to enjoy the arts while contributing to economic development.”

Honourable Simai expressed appreciation on behalf of the Busara Promotions Board of Trustees for the support. “The sustainability of most cultural organizations in Africa has mostly depended on support from donors. The support from the Swiss Embassy is a huge boost for this great festival,’’ he said. 

The 14th edition of the Sauti za Busara music festival will be held between 9 and 12 February 2017 at the Old Fort in Stone Town, Zanzibar.
The Embassy of Switzerland Contributes to East Africa’s Premier Music Festival

KINANA ATEMBELEA KUWAFARIJI YATIMA KATIKA KIJIJI CHA MATUMAINI, ENEO LA KISASA DODOMA, LEO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwakabidhi msaada wa vyakula watoto wa Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kushoto ni mwanzilishi wa Kijiji hicho Padre Vincent Boseil
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Matumaini, kilichopo eneo la Kisasa Dodoma mjini alipotembelea kituo hicho kuwafariki watoto yatima, leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, ambayo kilele chake ni kesho. Kulia ni mmoja wa waanzilishi wa kituo hicho Sista Roselie.
Kinana akionyeshwa eneo ambako hutunza watoto wachanga, ambao ni yatima, kwenye Kijiji hicho cha Matumaini

Kinana akimchukua mtoto mmoja kumfurahia, katika eneo hilo la kulea watoto wachanga
 Kinana akikaribishwa ndani na Mwanzilishi wa Kituo hicho, Padre  Vincent Boseili.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MTANANGE WA KUUKARIBISHA MWEZI FEBRUARI NI KATI YA BONGO FLEVA VS VIKAWE ALL STARS, HATARIIII......USIKOSE

DIWANI DEBORA SANGA AZINDUA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ WILAYA YA ILALA ILIYO CHINI YA KITUO CHA MSAADA WA SHERIA WLAC.

0
0
Mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

Na Karama Kenyunko, Globus ya JamiiForums.

Watanzania wameaswa kuacha Tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa baadhi ya wanawake na watoto. 

Hayo yalisemwa na Diwani wa viti maalum (Chadema), Kata ya Segerea, Deborah Sanga Kwenye mkutano wa kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika kwenye shule ya msingi Tabata jijini Dar es Salaam. 

Alisema ikiwa wananchi watabaini vitendo hivyo wanapaswa kutoa taarifa mara moja katika mamlaka husika pindi wanapogundua kuwepo kwa ukatili huo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Naye Kaimu Mkurugenzi wa WLAC Wigayi Kissandu, amesema kuwa ukatili huu unamadhara makubwa sana hasa kwa wanawake na watoto. Alisema kuwa vitendo vya ukatili huu wa kijinsia vmejikita zaidi katika mila na desturi na sheria mbali mbali zinazotumika ambazo ni kandamizi. 

" Ili kupunguza au kumaliza kabisa ukatili huu inapaswa kutungwa sheria mpya zitakazomaliza sheria kandamizaji dhidi ya mwanamke kama zile za mirathi na ndoa ili kuweza kumkomboa mwanamke," alisema. 

Aidha aliongeza kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo kwa kiasi kikubwa na kwamba katika kipindi cha Januari mwaka huu WLAC kimeshapokea kesi 150 mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia. 

Kwa upande wake Inspekta Stella Mindasi wa Dawati la Jinsia la watoto kituo cha polisi Tabata, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja, januari hadi Desemba 2016 jumla ya kesi 165 zimelipotiwa zikiwemo kubaka 24 , kulawiti 15 shambulio la kimwili 37 shambulio la aibu 6 shambulio 51, kutoa luhha yabmatusi 8 kijeruhi 15, kitelekeza familia 7, kutorosha mwanafunzi. 

Katika matukio hayo jumla ya kesi 30 zimekwishashatolewa hukumu.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kulia) akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa na Mwanasheria WLAC, Wigayi Kisandu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. Picha na Muhidin Sufiani Mafoto Blog
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya vitabu Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’ kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akiwakabidhi zawadi ya vitabu Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zawadi, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

Alikiba - Mwana (Official Music Video)

OLD SCHOOL REUNION, COLUMBUS, OH KUWAKA MOTO LABOR DAY NICO NA RENATUS NJOHOLE KUINGOZA SIMBA UGHAIBUNI, WACHEZAJI WALIOTAMBA PAZI, VIJANA, DON BOSCO KUONYESHANA MAUJUZI

0
0
Kikosi cha Simba kikiongozwa na Nico na Renatus Njohole Dallas, Texas.
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba kikiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Wilson Masingingi na mkewe siku walipotwaa ubingwa Dallas, Texas wakati wa kongamano la DICOTA
Kulia ni mkuu wa Wilaya Mhe. Kasesela akiwa Hoston katika picha ya pamoja na wachezaji wa Pazi enzi hizo Vitalis Gunda na Atiki Matata aliyekuja toka Uingereza kuiwakilisha Pazi.
Timu ya Tanzania iliyoundwa na wachezaji waliotamba enzi hizo katika timu za Pazi, Vijana, Don Bosco na kwengineko wakinyanyua juu kikombe walicho kipata baada ya kuifunga timu ya Gabon
Viewing all 109606 articles
Browse latest View live




Latest Images