Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1546 | 1547 | (Page 1548) | 1549 | 1550 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
  SERIKALI imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania haina mamlaka kisheria ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na taasisi za fedha nchini zikiwemo benki katika kutoa mikopo.
  Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma, Februari 3, 2017 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya msingi yaliyoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Mhe. Issa Ali Mangungu, aliyetaka kujua kama serikali inaweza kuandaa utaratibu maalumu wa riba elekezi itakayowawezesha wanawake na vijana kupata mikopo kwenye benki kwa riba nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi
  Aidha Mbunge huyo alitaka kufahamu kama Serikali inaweza kuziagiza benki za biashara kulegeza masharti ya dhamana kwa vijana na wanawake ambayo amedai yanarefusha mchakato wa upatikanaji wa mikopo kwa makundi hayo.
  Dkt. Kijaji amesema kuwa viwango vya riba katika benki na taasisi nyingine za fedha hupangwa na taasisi husika kwa kutegemea mambo mengi ikiwemo nguvu ya soko, sifa za mkopaji, ushindani katika soko, gharama za upatikanaji wa fedha, mwenendo wa riba za dhamana za serikali, gharama za uendeshaji na matarajio ya mfumuko wa bei.
  Amesema kuwa Benki Kuu imepewa mamlaka kisheria kusimamia Benki na Taasissi nyingine za fedha hivyo haiwezi kuingilia upangaji wa riba za mikopo kwenye taasisi hizo kwakuwa jambo hilo linapingana na mfumo wa uchumi wa soko huria.
  “Kutoa maelekezo kwa benki na taasisi za fedha kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuzichukulia hatua endapo zitapata hasara kwa kutumia riba iliyopangwa ama kuelekezwa na Benki Kuu” alisisitiza Dkt. Kijaji
  Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa Benki Kuu imeendelea na jukumu lake la msingi la kuhakikisha kuwa mfumo huo unaendeshwa kwa kuzingatia sheria zilizowekwa ili kulinda maslahi ya Taifa na uchumi kwa kusimamia ongezeko la ujazi wa fedha ili kuhakikisha linakwenda sambamba na mahitaji halisi ya uchumi ili kudhibiti mfumuko wa bei.

  Ameyataja majukumu mengine ya BOT kuwa ni kuhakikisha kuwa ongezeko la mikopo ya benki haliathiri uzalishaji mali kulingana na malengo ya ujazi wa fedha, kuhakikisha kuwa soko la dhamana la serikali linaendeshwa kwa ufanisi ili liweze kutoa riba elekezi kulingana na hali ya soko na uchumi kwa ujumla.

  0 0

  NA HAMZA TEMBA - WMU

  "Haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwasababu ya watu wachache wenye tamaa ya kupata utajiri wa harakaharaka, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa, awe nani, shikeni, wala msijali mtu cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake, sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe".

  Hiyo ilikua ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House)  Jijini  Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2016 kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili inayofanywa na kikosi kazi kilichoundwa na Wizara hiyo.

  Katika ziara hiyo, Rais Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alishuhudia meno ya tembo 50 yaliyokuwa yamekamatwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita Jijini Dar es Salaam, alioneshwa pia gari lililokuwa limebeba meno hayo na watuhumiwa wanane wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya meno ya tembo.

  Rais Magufuli aliwapongeza askari wote waliopo katika kikosi cha kupambana na ujangili pamoja na raia wema wanaotoa ushirikiano katika mapambano hayo na kwamba anatambua kazi nzuri wanayofanya na anawaunga mkono.

  Katika hotuba yake ya kwanza ya kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Rais Magufuli alitoa vipaombele kadhaa vya kutekelezwa na wizara zake huku Wizara ya Maliasili na Utalii akiipa majukumu makuu matatu; kupambana na ujangili, kutatua migogoro ya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi na kuongeza mapato ya Serikali.

  Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Prof. Jumanne Maghembe; Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani; Katibu Mkuu, Meja Generali Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki imejipanga kutekeleza majukumu yake makuu ya uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kuendeleza Utalii pamoja na vipaombele ilivyoelekezwa.

  Mara tu alipoteuliwa kuingoza wizara hiyo, Prof. Maghembe alitangaza vita na majangili na kubainisha kuwa kipaumbele chake kikubwa kitakuwa ni kupambana nao. “Niwaambie majangili sasa wakafanye kazi nyingine ama wakae nyumbani, kiama kinakuja huko”, alisema.

  Alisema kuwa atasimamia kwa uhakika maliasili za Watanzania kwa sababu mambo ya maliasili ndiyo eneo alilobobea kwenye usomi wake.
  “Tutajitahidi pia kutangaza utalii na kuongeza mapato ya sekta hii kama tulivyofanya kwenye miaka ya 2006 hadi 2008, tuliongeza bei za vitalu na ada kwa mnyama mmoja mmoja anayewindwa,”  alisema Profesa Maghembe siku aliyoapishwa.

  Mikakati ya Wizara kukabiliana na ujangili

  Ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili tangu uongozi wa Serikali ya awamu ya tano uingie madarakani, taarifa iliyotolewa na Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii, inaonyesha kuwa katika kipindi cha mwezi Novemba, 2015 hadi mwezi Oktoba 2016 Wizara hiyo imefanikiwa kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ujangili ikiwemo kuanzisha kikosi kazi maalum cha kupambana na ujangili.

  Kikosi kazi hicho cha kudhibiti uhalifu wa Misitu na Wanyamapori nchini(Wildlife and Forest Crime Unit),kinasimamiwa na Watendaji wa Sekta ya Wanyamapori kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika ngazi za juu za uwezeshaji (Facilitators) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini.
   Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya hiyo (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam Oktoba 29, 2016. (Picha na Ikulu)

  Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam Oktoba 29, 2016. (Picha na Ikulu).

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Habari na Mwene Said wa Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.

  Koplo Lugano (39),katika kesi ya kuhujumu uchumi dhidi ya raia wa China, Yang Glan maarufu kama Malkia wa pembe za ndovu (66) amedai mahakamani kuwa alishiriki kumkamata mshtakiwa wa tatu Manase Philemon (39).

  Koplo Lugano ambaye ni shahidi wa Upande wa Jamhuri, pia ni mpelelezi kutoka Kituo cha Polisi Stakishari, alidai kuwa alifanikisha kumkamata mshtakiwa huyo akiwa katika sehemu ya starehe njiapanda ya majumba sita kwa kushirikiana na makachero wenzake.

  Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alidai kuwa yeye ni mwajiriwa wa jeshi la polisi katika idara ya upelelezi.

  Alidai kuwa Aprili 18, 2014, aliitwa na bosi pamoja na wenzake na kupewa jukumu la kumtafuta na kumkamata Manase kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili wa meno ya tembo.“Tulianza msako baada ya kupata taarifa kwamba Manase anapendelea kukaa sehemu mbalimbali za starehe… Aprili 20,2014 tulifanikiwa kumkamata eneo la Njiapanda ya Segerea” alidai.

  Akifafanua zaidi shahidi alidai kuwa baada ya kufanikiwa kumkamta walimuweka chini ya ulinzi na kumfikisha kituoni, walipomhoji kuhusu tuhumu hizo alifikishwa mahakamani.

  Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Februari 16 na 17, mwaka huu.

  Katika kesi ya msingi,Glan na wenzake wanakabiliwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. Bilioni 5.4.

  Mbali na Glan na Manase, mshtakiwa mwingine ni, Salvius Matembo (39) wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22,mwaka 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali ikiwamo meno ya tembo.
  Pia, washtakiwa wanadaiwa wakati wa tukio la kwanza walikutwa na wakifanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1889 zenye thamani ya Sh bilioni 5.4 bila ya kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

  Katika shtaka jingine, ilidaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, mwaka 2014 kwa makusudi Glan akiwa raia wa China, aliongoza na kufadhili kufanyika makosa ya jinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 vya meno ya tembo bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

  Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya kuhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, Kusafirisha na Kuuza Meno ya Tembo kwa nia ya kujipatia faida.

  Ilidai kuwa Mei 21, mwaka 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.

  0 0


  Dotto Mwaibale, Kisarawe

  HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association.

  Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.

  Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.

  "Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.

  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.

  Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.
  Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga. 
  Semina ikiendelea.
  Meza kuu.
  Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.


  0 0

  Vodacom yazindua simu mpya ya Smart Bomba
  ·        Matumizi  yake yapo kwenye lugha ya Kiswahili
  ·        Inauzwa ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha intanenti  chenye GB 30 za buree kwa miezi 3!

  Dar es Salaam,Jumatano Februari 03,2017:Sasa ni wakati wa watanzania kufurahia ubunifu wa kiteknolojia wa mawasiliano unaoendana sambamba na mazingira yao halisi na kufurahia kupata taarifa na burudani kwa njia ya interneti ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,mtandao unaoongoza nchini wataweza kujipatia simu za kisasa zinazotumia interneti aina ya Smart Bomba.

  Simu za Smart Bomba ambazo zimezinduliwa rasmi nchini  leo zinapatikana kwa gharama nafuu ya shilingi 99,000/-muundo wa matumizi yake uko katika lugha ya taifa ya Kiswahili pia zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na kifurushi cha interneti  chenye GB 10 za buree kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom  mahali popote na wakati wowote.

  Mbali na muundo wa matumizi ya simu hii kuwa katika lugha ya Kiswahili na kwendana  na mazingira halisi ya maisha ya watanzania walio wengi,simu za Smart Bomba zina umbo la kuvutia,nyepesi na zina kioo cha mbele,cha ukubwa wa kutosha,zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya android inaongeza kasi ya kuperuzi internet,inayo kamera ya kurekodi na kupiga picha kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu vilevile inao mfumo wa utambuzi wa ramani ya maeneo mbalimbali ujulikanao kama GPS ambao unatoa maelekezo kuonyesha mahali mtu alipo na mahali aendapo kwa urahisi hususani madereva wa teksi ambao huwapeleka wateja wao sehemu mbalimbali wasiozijua,na zimeunganishwa na program za simu za kurahisisha Maisha za Vodacom kama vile M-Paper.

  Akiongea wakati wa  uzinduzi wa simu hii,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama,alisema wakati ni huu wa kila mtanzania kuweza kufurahia matumizi ya simu za kisasa zinazotumia internet (Smart Phones) kwa ajili ya kupata taarifa na burudani kutoka mitandaoni kutokana na kupatikana kwa mara ya kwanza kwa gharama nafuu nchini.

  “Kuingia sokoni kwa simu za Smart Bomba za gharama nafuu na zilizotengenezwa kwendana sambamba na mazingira na Maisha ya watanzania walio wengi zikiwa zimeunganishwa na GB 30 kwa matumizi ya miezi 3 ya mwanzoni ni ofa ya kipekee ambayo imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu  walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua”.
   Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama(kushoto) akimshuhudia Balozi wa kampuni hiyo,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3. 

   Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama.


  Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiwaburudisha wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  0 0

  Daktari Bingwa Upasuaji wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Nicephorus Rutabasibwa (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Job Ndugai  (wa tatu kushoto) Dar es Salaam jana wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT)  wa Bunge, Lily Mraba aliyelazwa katika Taasisi hiyo
   Muuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Zaituni Bembe (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai  Dar es Salaam jana mara baada ya kutoka katika Taasisi hiyo, wakati alipokwenda kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba.
  Daktari wa Mishipa ya Fahamu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)  Hamisi Kinyerero akiagana na maofisa wa Bunge walioongozana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba. aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa MOI. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA )

  0 0


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imezindua na  kuitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote.

  Akiongea kuhusu Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando aliseme “Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo

  Kutuma pesa kwenda mitandoa yote kwa bei nafuu wateja wetu wanaweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa tozo ileile wakati wowote mahali popote pale nchini. Haya ni mapinduzi ya kipekee katika huduma za kifedha ambapo tumewezesha wateja wetu kufanya miamala hiyo kwa urahisi zaidi bila kujali gharama.

  Kupata vifurushi  bora kupitia Airtel Money OFA KABAMBE vyenye ujazo zaidi kuliko vifurushi vya mitandao mingingine yote: Kupata hii piga *150*60# kisha nunua kifurushi kupia Airtel Money kwa kuchagua No.6 OFA KABAMBE  , Pia vipo vifurushi vya UNI packs sasa vinapatikana kupitia huduma ya Airtel Money hivyo kuwawezesha wanafunzi kujiunga na vifurushi hivyo kwa urahisi zaidi

  Kutuma pesa kwenda benki na kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money kwenda Benki-  sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kufanya miamala hiyo kwenye benki 38 ambazo tayari tunaushirikiano nazo. Kadhalika wateja waweza kutumia ATM za umoja switch na CRBD zaidi ya 1105 nchini kwa kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money masaa 24 kila siku. ushirikiano huu umeongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi

  Na pia tunawewezesha wateja wetu kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana  kwa wateja wetu na mawakala nchini, Mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi laki 5 na kujipangia yeye mweye alipe lini SIKU, WIKI au baada ya  MWEZI. Airtel Timiza ni suluhisho kwa mahitaji ya mikopo ya haraka ya kutatua changamoto za kijamii lakini pia inawawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji kwaajili ya biashara  zao papo hapo.

  “Ndio maana tunaseme? Relax Airtel Money mambo yote” alisisitiza Mmbando

  Huduma ya Airtel Money, kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi ya kifedha nchini hasa  katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Mwezi uliopita Airtel Money pia ilifanikiwa kugawa gawio la shilingi bilioni 3.5 kwa watejawake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.


  Meneja Uhusiano wa Airtel akitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote. Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na huduma nyingi zenye faida zaidi kwa kupiga tu *150*60#

    

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.

   Sehemu ya wasimamizi wa miradi na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani)

   Kutoka kushoto, Milka Digha,  Alika Ilomo na Costa Mosha kutoka Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Nishati na Madini  wakinukuu maelekezo  mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa katika kikao hicho.  0 0


  Jacquiline Mrisho – MAELEZO


  The Permanent Secretary in President’s Office, Honorable Peter Ilomo has commended the Construction Sector Transparency Initiatives (CoST - Tanzania) for enlightening the Government on the use of public money due to their focus on enhancing transparency.

  Hon. Ilomo said this in a meeting involving various stakeholders in the construction industry held at the Holiday Inn auditorium in Dar es Salaam on behalf of Minister of State, Public Service Management and Good Governance, Honorable Angellah Kairuki.
    
  Hon. Ilomo said that, CoST’s activities focuses on enhancing transparency in construction industry through disclosing information on delivery of public infrastructure something which will help to identify potential efficiency savings which complements Public financial management together with procurement reforms.
                        
  “The work being done by CoST – Tanzania is an opportunity for the Government and the Public in general to track on how Public money is being spent on infrastructure delivery, such tracking will definitely save the country’s money through reduced corruption, improved management and delivery of better performing infrastructure,” Hon. Ilomo said.

  Hon. Ilomo added that, the information included in its Infrastructure Data Standard is required to be disclosed by law to Regulatory Authorities so, CoST is actually helping Procuring Entities to comply with already existing legal and regulatory requirements so as to help them on fulfilling their obligations.
    
  Hon. Ilomo has encouraged CoST and the National Construction Council (NCC) to broaden their efforts and to undertake more disclosure activities especially in Procuring Entities because the output from those activities  will be used by oversight organs to expand their data sources.

  Meanwhile, CoST’s Chairman, Eng. Kazungu Magili explained that, disclosure  of information benefits related to Public financed construction projects will allow the public to know the perfomance of  certain projects so as to raise Government reputation to its citizen.

  “Through this transparency we expect to support the better management of Public finances, prevent corruption and to be used as a catalyst by bringing the disclosed information to the Public which shall help other Government’s Anti-corruption Instruments to make follow up,” Eng. Magili said.

   In this year, CoST intends to evaluate at least ten construction projects including the construction of flyovers, buildings built by Tanzania Buildings Agency (TBA) especially the construction of the new University of Dar es Salaam hostels also buildings built by National Social Security Funds (NSSF) together with National Housing Construction (NHC).

  0 0

  Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, (aliyekaa katikati) na afisa biashara wa benki ya KCB tawi la morogoro, Lela Kisinda (aliyekaa kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Morogoro.
  Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Benki ya KCB mkoani Morogoro.
  Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hyo jijini Morogoro 
  Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Allen Mhidze akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro. 
  Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Grace Makoye akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  Kampuni ya Bima ya UAP na Old Mutual   imetoa mafunzo kwa wadau wa kilimo Tanzania,katika kuwezesha wakulima  kupata bima ya kilimo kwa ajili ya majanga yatakayojitokeza katika kilimo hicho.
  Akizungumza katika mafunzo hayo kwa Taasisi za Fedha  yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,  Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima hiyo , Raymond Komanga amesema kampuni ya  bima imekuwa ikitoa bima katika kilimo kwa miaka mitatu na kutaka taasisi za fedha kutoa mikopo katika kilimo.
  Amesema aina za bima zilotewazo na kampuni hiyo ni  bima za  ukame, mafuriko, Wadudu waharibifu kama nzige, moto, Magonjwa ya Mazao, Upepo mkali pamoja na uharibifu utokanao na mvua za mawe au barafu katika mashamba.
  Komanga amesema katika kuendesha bima katika kilimo kampuni imeenda mbali katika kutoa bima ya Mifugo kwa ajili Ukame, Magonjwa ya Mlipuko pamoja na ajali ambayo imaweza kutokana mifugo kufa wakati ikisafirishwa.
  Taasisi za fedha  zilizoshiriki mafunzo hayo ni Benki  ya Akiba, NBC and Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania  (TADB) na wadau wengine ambao wanamchango katika sekta ya kilimo ili kuwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima.
  “UAP Tanzania imekuwa ikitoa bima za kilimo na mifugo kwa miaka mitatu sasa, uwelewa na mwitikio wa bima hizi umekuwa ukiongezeka siku baada ya siku nchini ili kuwafikia wakulima na wafugaji wengi nchini tumeamua kuwahusisha wadau wengine wa kilimo yakiwemo mabenki yanayowakopesha wakulima”amesema Komanga.
   
  Aidha amesema mafunzo ya  wadau  wa kilimo itasaidia kupanua wigo wa uelewa na kuwafikia wakulima wengi nchini kwa kuwafanya wakulima na wafugaji kwenda kisasa ya kuwa na  kinga katika  shughuli zao.
   
   Ameongeza kuwa bima ni miongoni mwa vitu vinavyofanya mkulima na mfugaji  kuwa wa kisasa na kuleta ufanisi na mapinduzi ya kilimo nchini.
   Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya Bima  ya UAP na Old Mutual  , Raymond Komanga akitoa maelezo kwa mdau wa kilimo aliyehudhuria mafunzo ya  wadau wa kilimo juu ya kutumia bima katika kilimo na ufugaji leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya washiriki wa Mafunzo wa Wadau wa Wakilimo watakaowezesha kilimo kuwa na Bima iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Picha ya pamoja wadau wa kilimo walioshiriki mafunzo juu ya kutumia  bima  ya kilimo na Ufugaji leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Mkufunzi kutoka tasisi wa masuala ya sheria juu manunuzi ya Umma , Hamis Tika akizungumza na watumishi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
  Baadhi ya wafanyakazi wa tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakisikiliza kwa makini juu ya mafunzo ya masuala ya manunuzi.

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma PSPTB, Ally Songoro akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete .

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, akizungumza kabla ya kumkaribisha kaimu mkurugenzi mkuu wa PSPTB .


  .Kaimu Mtendaji mkuu wa PSPTB,Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa manunuzi na watendaji wa tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mwanadamizi wa Mahusiano ya Umma na Masoko Shamimu Mdee na mratibu mkuu wa utafiti na ushauri PSPTB Amos Kazinza wakifuatilia mafunzo

  0 0  Na Dotto Mwaibale

  DEREVA wa gari dogo teksi yenye namba za usajili T 625 AWS amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akiliendesha kutoka mjini akielekea Uwanja wa Ndege kugongana na gari dogo lenye namba T 214 CFX aina ya Corolla lililokuwa likiingia Barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Biashara la Quality Centre eneo la Mtava jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  Mashuhuda wa ajali hiyo wakizungumza na waandishi wa habari eneo la ajali walisema ajali hiyo ilisababishwa na gari hilo dogo aina ya Corolla lililokuwa likiingia barabara ya Nyerere bila kuchukua tahadhari.

  "Chanzo cha ajali hii ni gari hilo dogo aina ya corolla ambalo liliingia barabara ya Nyerere bila ya dereva wake kuchukua tahadhari na kama dereva wa gari namba T 625 AWS angekuwa katika mwendo wa kawaida madhara yake yasingekuwa makubwa kiasi hicho" alisema shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Mlugulu.

  Mlugulu alisema baada ya magari hayo kugongana gari hilo aina ya Corolla liligeuka na kwenda kuyagonga magari mengine namba T 596 BCG na T 741 DEK yaliyokuwa yamesimama yakisubiri kuingia upande ambao lipo Jengo la Kibiashara la Quality Centre.

  Katika ajali hiyo gari namba T 625 AWS liliacha njia na kuhamia upande wa pili wa barabara ya kutoka Tazara kwenda mjini.

  Baada ya ajali askari wa usalama barabarani walifika na kupima ajali hiyo na kuchukua maelezo ya madereva wote wanne ambapo magari mawili T 214 CFX na T 625 AWS yakiondolewa na  magari ya kukokota magari mabovu (Breck Down) na kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zingine za kisheria.
   Wananchi wakimuangalia dereva wa teksi aliyejeruhiwa baada ya gari lake lenye namba za usajili T 625 AWS kugongana na gari dogo lenye namba usajili T 214 CFX wakati likiingia barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Kibiashara la Quality Centre Dar es Salaam leo asubuhi.
   Mwonekano wa Teksi hiyo namba T 625 baada ya kugongana.
   Wananchi wakiangalia ajali hiyo.
   Wananchi wakiangalia gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX baada ya kuyagonga magari namba T 741 DEK na T 596 BCG katika eneo hilo la Mtava.
   Askari wa Usalama Barabarani akipima ajali hiyo.
   Gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX likiwa eneo la ajali kabla ya kuondolewa.


  0 0


  NA Anthony John Glob jamii

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwakamata wale wote ambao hawajafika kuripoti kituoni hapo kwa kufuatia tuhuma za uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya.

  Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walitakiwa kuripoti katika kituo cha polisi centro na hawajafika ambao ni Rashidi makwilo (chidi benzi,Samir Kheri (mr blue) pamoja na wamiliki wa klabu za kuuza pombe.

  "kuna watu walio waita lakini hawajafika mpaka sasa hawajafika naliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wote ambao hawajafika mpaka juma tatu", amesema 

  Sambamba na hayo Mkuu huyo wa mkoa ameongeza majina matatu ya maaskari polisi na wasanii ambao wanatakiwa wakamatwe kwa tuhuma za kushirikiana na wauza madawa ya kulevya pamoja na Vanesa mdee na mwana dada Tunda kufika katika kituo cha kati.

  Makonda ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kutokomeza hali ya uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.
   Mwanadada maarufu hapa jijini Dar,Wema Sepetu  akiwa na mmoja wa wasaidizi wake wakiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
   Mmoja wa wasanii anaetambulika kwa jina la kisanii Babuu wa Kitaa akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
   Baadhi ya watu waliofika kituo cha polisi kati kujionea watuhumiwa mbalimbali wa Madawa ya kulevya walioitikia wito wa kuitwa kutoka kwa RC Paul Makonda
    Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,maarufu kwa jina la kisani T.I.D akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
  0 0

  JUMUIYA YA WATANZANIA LEICESTER INASIKITIKA KUWATANGAZIA KUWA ZIARA YA MH. BALOZI DKT ASHA-ROSE MIGIRO MJINI LEICESTER ILIYOPANGWA KUFANYIKA TAREHE 4/2/17 HAITAWEZA KUFANYIKA TENA KUTOKANA NA SABABU ZISIZOWEZA KUZUILIKA. 

  TAARIFA NA TAREHE MPYA YA ZIARA HIYO ITATOLEWA MARA ITAKAPOJULIKANA. 
  SHUKRAN

  0 0
  0 0  JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano

  Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao ya siku tatu kubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili.

  Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.

  "Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".

  Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha. 

  Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017. 
  Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege. 
  Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Ubwa na mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana. 


  0 0

  Na Yassir Adam, Globu ya Jamii

   Tanzania ni moja kati ya nchi za Jumuiya yaAfrika mashariki ambayo haijaondoa vikwazo vya Kiforodha jambo linalowakwamisha Wananchi kufanya biashara katika Soko la Afrika Mashariki.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurungezi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF Godfrey Simbeye amesema utekelezaji wa vikwazo hivyo utawasaidia wananchi kufanya biashara kutoka sehemu moja hadi nyingine.

  "bado hatujapiga hatua ya kutosha ya kuondoa vikwazo visivyo vya Kiforodha ambapo Tanzania haijatekeleza kwa asilimia 27 tofauti na Kenya kwa asilimia 24 pamoja na Uganda kwa asilimia 15."

  Simbeye amesema sheria mbalimbali zilizopo zinatakiwa zibadilishwa ili kufungua na  kupunguza vikwazo vya ufanyaji wa biashara ili kupunguza vikwazo na  kufikia Soko Afrika Mashariki.

  "vikwazo vingi vilivyopo ni ucheleweshaji usiokuwa wa lazima katika Mizani,taratibu za forodha zenye usumbufu pamoja na kuwepo kwa Mifumo tofauti ya kutoa vibali,Ukaguzi na Upimaji."

  Kwa upande wake Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Fredy Kavula akaeleza kuwa lengo kubwa la kuondoa Vikwazo katika biashara ni kurahisisha biashara za Ndani na Nje kuvuka Mipaka na kufikia Soko la SADC na pia kufikia Mikataba ya Shirika la biashara la Dunia WTO.

  "Wizara kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya kusimamia na kuondoa vikwazo vya biashara imeweza kuondoa Vikwazo 114 na vilivyobakia ni 19 ambavyo bado kamati inavifanyia kazi kupitia Taasisi yenye Wajumbe wa kamati husika iliyojumuisha Taasisi binafsi pamoja na Serikali            vitakavyorahisisha Biashara za ndani na nje kuvuka Mipaka"            
  Mkurugenzi Mtendaji  Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa Habari katika Mkutano huo uliohusu Uondoaji wa Vikwazo vya Kiforodha vya kibiashara Nchini                         
                         Baadhi ya Wadau mbalimbali kutoka serikalini na  Sekta Binafsi waliohudhulia katika mkutano huo

  0 0  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.

  Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imethibitisha hilo pasi na shaka kwamba Tanzania ndiyo yenye nafasi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Aprili 2, mwaka huu huko Gabon baada ya Madagascar kuenguliwa kutokana na kutoandaa vema fainali hizo.

  Taarifa hizo za CAF kutoka Libreville, nchini Gabon zinathibitisha kwamba Kamati ya Utendaji ya CAF imeipa ushindi Tanzania dhidi ya timu ya Jamhuri ya Congo ambayo katika michuano ya kufuzu, ilimchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyezidi umri kinyume cha kanuni za kanuni za michuano hiyo.

  Katika michezo hiyo ya kirafiki na ushindani, Serengeti Boys ilipoteza mchezo wa 16 tu dhidi ya Congo ilihali kulikuwa na rufaa kuhusu mmoja wa wachezaji wa Congo ambaye alionekana kuwa na umri mkubwa. Mchezaji huyo ni Langa Lesse Bercy.

  CAF, kwa nyakati tofauti ikiwamo Novemba 10, 2016 na Desemba 15, mwaka jana walitoa agizo kwa Congo Brazzaville kumpeleka kijana huyo Cairo, Misri kwa ajili ya vipimo vya MRI ili kuthibitisha au kupangua madai ya Tanzania. Congo Brazzaville hawakupeleka.

  Januari 12, mwaka huu 2017 iliamriwa kwa mara nyingine kijana huyo kupelekwa jijini Libreville, Gabon ili kufanyiwa vipimo vya MRI, lakini hakupelekwa na katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF, kimeamua kumaliza suala hilo na kuipa ushindi Tanzania.

  Siku 10 ziliisha Januari 23, mwaka huu lakini tangu hapo kumekuwa na maswali ya kutosha kuhoji nafasi ya Tanzania yakitoka kwa Watanzania kupitia wanahabari, lakini TFF ilisimama kidete kutangaza kuwa tunasubiri uthibitisho wa CAF ambayo leo Februari 3, mwaka huu imetangaza rasmi kuwa Tanzania itacheza fainali hizo.


  0 0


older | 1 | .... | 1546 | 1547 | (Page 1548) | 1549 | 1550 | .... | 3278 | newer