Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1536 | 1537 | (Page 1538) | 1539 | 1540 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Kituo cha kuzuia na kupunguza majanga ya kimaumbile nchini Thailand kimetangaza kuwa, watu 90 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali zinazoendelea kunyesha katika mikoa 12 ya kusini mwa nchi hiyo.

  Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imeinukuu serikali ya Thailand ikisema kuwa, watu hao wamepoteza maisha kutokana na mvua hizo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa kutokana na ongezeko la mafuriko, mawimbi makali ya bahari na kuendelea kunyesha mvua. Kituo hicho kimetangaza kuwa, hadi sasa mikoa saba ya kusini mwa nchi hiyo bado ina hali mbaya.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo jumla ya watu laki nane wameathiriwa na mvua hizo ambazo bado zinaendelea kunyesha. Hii ni katika hali ambayo kituo cha utabiri wa hali ya hewa kimetabiri kunyesha mvua kubwa ambazo zitakuwa kubwa zaidi katika maeneo ya kusini kuanzia leo Jumapili na kuendea kuyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. 
  Utabiri huo pia umetahadharisha juu ya ongezeko la mawimbi makubwa yenye mwinuko wa zaidi ya mita mbili hadi tatu ambayo yatayakumba maeneo ya pwani ambayo hutembelewa sana na watalii.

  Kufuatia hali hiyo, serikali imetuma maelfu ya askari kwa ajili ya kuwaokoa maelfu ya wakazi wa vijijini waliozingirwa na mafuriko sanjari na kukarabati barabara na madaraja katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU


  0 0

  Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa asubuhi ya leo. Wachimbaji hao walikumbwa na kadhia hiyo, siku mbili zilizopita baada ya udongo kufunika sehemu ya kutokea. ila kwa juhudi mbalimbali walizokuwa wakizifanya, waliweza kuwasiliana na waliokuwa nje ya mgodi na hatimae kufanikiwa kuokolewa leo asubuhi.

  Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo.
  Hivi ndivyo zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji.
  Baadhi ya Raia wa kigeni wenye asili ya China wakimjulia hali mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa walikumbwa na dhoruba hilo la kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita.

  0 0

  Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania siku ya tarehe 26 na 27 Januari, 2017 wamefanikiwa kukaa na baadhi ya wabunge kutoka kamati ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Katiba na sheria pamoja na miundo mbinu katika kikao kilichoongozwa chini ya mwenyekiti wake Mbunge wa Muheza Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabu, pamoja walionyesha ushirikiano wao katika kuboresha usalama barabarani kwa maendeleo ya Taifa letu.

  Wajumbe wa kikao husika walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na hali ilivyo sasa, ambapo ilielezwa kuwa hali ilivyo kulingana na takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.25 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 hadi 50 hujeruhiwa na wengine hupata ulemavu wa kudumu wengi wao wakiwa ni vijana wenye nguvu kazi ya Taifa. Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) 2015.
  Kwa upande wa Tanzania Bara, taarifa kutoka jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016 jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani. Katika vifo hivyo wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676. Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo idadi yake 3,649 ikifuatiwa na pikipiki kwa idadi ya 2,544.

  Kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini, Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera zinazohusu usalama barabarani Tanzania umeona umuhimu na kuchukulia jambo hili kulifanyia kazi kwa kina. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 76 ya ajali zote zinatokana na vyanzo vya kibinadamu kama vile Ulevi, Mwendokasi, Uzembe, Uchovu, kupuuzia au kutokuwa makini uwapo barabarani na kutokutii sheria za Usalama Barabarani. Tuna amini matendo haya ya kibinaadamu yana dhibitika kisheria, hivyo basi tunaisihi serikali kuboresha sheria.
  Kama wadau wa Usalama Barabarani, tunadhani kuna umuhimu wa sheria sasa kuboreshwa, na hivyo utashi wa kisiasa unatakiwa. Ndiyo maana tukaitisha majadiliano ya pamoja na Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko ya sheria kwa ufanisi na kwa haraka.

  Wabunge waliohudhuri kikao hiki kwa ujumla wao, waliona umuhimu wa kuwa na mikakati ya kitaifa ya kupunguza ajali na walikiri kwa nia moja na kukubali kuunda Mtandao wa Wabunge wanaotetea usalama barabarani.

  Maeneo ambayo tunayapa kipaumbele katika maboresho ya sheria ni kama haya yafuatayo: a) Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.
  Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

  IDADI  ya Wanawake wanaojiandaa  na mashindano ya miaka 10 ya klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania  imeongezeka na kuongeza joto la maadhimisho ya klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Februari Jijini Dar es salaam.

  Mmoja wa wachezaji hao ni aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake Hawa Wanyenche ambaye kwa muda mrefu hakuwa akionekana viwanjani kucheza lakini sasa ameibukia katika klabu ya Lugalo.
  Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake Hawa Wanyenche akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.


  Akizungumza wakati wa mazoezi yake katika klabu ya lugalo Hawa alisema anaona kiwango chake kinaanza kurejea kutokana na kutokuwa uwanjani muda mrefu na anaamini kuibuka na ushindi katika mashindano hayo na yeyote yajayo ili kurejesha heshima yake.

  “ Unajua ni muda mrefu sijaingia uwanjani na falsafa yangu ni kuishinda sio kushindwa na siri ya kushinda ni mazoezi ndio maana nimeanza mapema hivyo wanawake wengine wanajua wako vizuri katika golf waje tupambane”. Alisema Hawa.
  Aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa Wachezaji wengine wa Vilabu vingine nao kujipanga na kuhakikisha wanashiriki ili kufanikisha mashindano lakini pia kuzihirisha uwezo wao.
  Mchezaji Nicholous Chitanda (katikati) wa klabu ya Lugalo akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.

  Naye Mchezaji Vicky Elias alisema  muda umekwisha na ukizingatia kuna uwezekano wa wachezaji  kutoka katika nchi mbalimbali kuja kushiriki michuano hiyo hivyo mazoezi pekee ndio yatakayowafanya kuibuka na Ushindi.
  “ Wachezaji wengi wamekamia mashindano haya lakin I nitashinda ingawa nikishindwa nitakubaliana kwa kuwa ni moja ya matokeo katika Golf kwani mchezo huo hautabiriki” Alisema Vicky.

  Kwa Upande wake mchezaji Chipukizi Habiba Likuli alisema  kikubwa ni kukabiliana na ushindani na kuibuka na ushindi na kulibakiza kombe la historia kwa klabu.
  Mchezaji Habiba Likuli wa klabu ya Lugalo akiwa katika mazoezi kujiandaa na mashindano ya maadhimisho ya miaka 10 ya klabu ya gofu ya JWTZ yanayotarajiwa kufanyika februari jijini Dar es salaam.


  “ Mashindano yaliyopita nilicheza katika kundi la Watoto Junior lakini kutokana naKiwango changu ninaimani nitakuwa na uwezo wa kuchezea kundi la Wanawake Ladies katika mashindano hayo kama kanuni zitaruhusu” Alisema Habiba.
   Kwa upande wake  Kapteni wa Klabu ya golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema  katika kuyapa uzito mashindano hayo  wamepeleka mialiko katika nchi za Zambia,Kenya,Malawi ,Zimbambwe , Rwanda na Uganda.

  Aliongeza kuwa tarehe na mgeni Rasmi katika Mashindano hayo anatarajiwa kutangazwa na mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Jumanne saa nne katika Klabu hiyo.
  Mchezaji wa klabu ya lugalo Vicky Elias ( wakwanza kushoto) akipiga mpira wakati wa mazoezi kujiandaa na maadhimisho ya miaka 10 ya klabu hiyo jijini Dar es salaam. wanaomtazama ni Hawa Wanyenche (katikati) na Salim Mwenyenza (kulia). (picha na Luteni Selemani Semunyu).

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye leo Januari 29, 2017  alikwenda kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembela.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakizungumza na Mfanyabaishara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye  leo Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salam kumtembelea 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea. 

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea. 

  0 0


  0 0

  Jumuia ya Watanzania Leicester, UK inapenda kuwaarifu Watanzania, wenye nasaba na Tanzania pamoja na marafiki wa Tanzania kuwa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Dokta Asha Rose-Migiro (katika picha ya maktaba akiwa na mdau Freddy Macha, London) atafanya ziara katika mji wa Leicester kwa utaratibu ufuatao: 
  SIKU:         JUMAMOSI
  Tarehe       04.02.2017. 
  Ratiba itaanza kwa Mheshimiwa Balozi kutembelea shughuli mbali mbali za kimaendeleo za wajasiriamali wa kitanzania hapa Leicester. 

  Saa Nane Kamili mchana (2.00pm) Mheshimiwa Balozi atafanya mazungumzo na Watanzania, marafiki na wenye nasaba na Tanzania katika ukumbi huu: 
  ST MATTHEWS NEIGHBOURHOOD CENTRE,
  10 MALABAR ROAD,
  LEICESTER UK LE1 2PD 
  Tunatumia fursa hii kukualikeni nyote katika kikao hicho kitachokuwa na umuhimu wa pekee. Masuala mengi muhimu yatafafanuliwa na Mheshimiwa Balozi, yakiwemo: 
  - Ufafanuzi na maelezo kuhusu Uraia pacha (dual citizenship)
  - Umiliki ardhi kwa diaspora
  Pamoja na mengi mengine. 
  Tafadhali tufike bila kukosa.
  Tafadhali tuwaarifu na wenzetu.
   Shukran.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU

  0 0

   Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi Mhe. Aisha Nyerere akionesha bango kabla ya kanza kwa matembezi ya Uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali kabla ya kuanza kwa matembezi ya zinduzi wa wiki ya Sheria leo jijini dar es salaam.

   Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongoza Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo.Kushoto ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome.

  Sehemu ya Watumishi wa Mahakama wakiwa kwenye Matembezi hayo.

  Watumishi wa Mahakamaya watoto wakiwa kwenye Matembezi hayo.

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akizungmza wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Picha zote na Lydia Churi wa Mahakama.  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akionesha moja ya fomu zinazotumika katika Uchaguzi wakati akifanya mahojiano na Mtangazaji Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Shaban Kissu.
  Mtangazaji Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Shaban Kissu (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji Mwandamizi wa TBC, sHaban Kissu.Picha na Hussein Makame, NEC

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili wilayani Nkasi kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara zilizopo ndani ya wizara yake na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nkasi, Juma Khamis Ali (kushoto), akikabidhi taarifa ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara yake(hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya wilayani Nkasi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi. Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda(kulia) akizungumza na wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani),wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo ,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia) wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Naibu Waziri huyo wilayani humo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha ndani na watumishi wa idara zilizopo chini ya wizara yake wilayani Nkasi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

  Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, jana, Januari 28, 2017, imeadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM, kwa kufanya usafi na kutoa vifaa mbalimbali kweye zahanati ya Kibamba, Ubugo jijini Dar es Saaam. Pichani, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya hiyo, Lucas Mgonja (wapili kulia), akikabidhi ufagio kwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Mwahawa Kiroboto. Kushoto ni Muuguzi Mfawishi wa Zahanati hiyo, Jesca Mpolanigwa.
  Mgonja (Wapili kushoto) akiongoza badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni kukata miti na kufyeka nyasi kwenye Zahanati hiyo
  Badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni wakishiriki kufanya usafi kwenye Zahanati hiyo
  Baadhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi Kinondoni wakifanya usafi kwenye Zahanati hiyo.


  0 0

  Mtanange kati ya Yanga na Mwadui Fc ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, unaendelea hivi sasa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku timu zote zikionyesha kusambuliana kwa zamu. kipindi cha pili cha mchezo huo kimeanza hivi punde na Yanga inaongoza kwa bao 2-0 yaliyowekwa kimiani na Mshambuliaji Obrey Chirwa.Globu ya jamii iko uwanjani hapa kukuhabarisha kinachoelezea.
   Kikosi cha Mwadui FC.
   Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akipimana ubavu na Malika Ndeule wa Mwadui Fc, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, unaendelea kuchezwa hivi sasa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Yanga inaongoza kwa bao 1-0.
   Kipa wa Mwadui, Shaaban Kado akijiandaa kuupiga mpira.
  0 0

  Mtumishi wa Umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itakapofika tarehe 1 Machi, 2017 atakua kajiondoa kazini mwenyewe.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali jijini Dar es salaam.
  “Watendaji Wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki” Waziri Kairuki alisisitiza.Aliongeza Serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha zoezi la kuondoa Watumishi hewa, zoezi ambalo limefika ukingoni na siku za karibuni ajira zitarudishwa.
  Waziri Kairuki aliwataka Watendaji Wakuu kuweka mikakati ya kuepuka watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwasababu jambo hilo limeumiza na kupoteza rasilimalifedha nyingi za Serikali.
  Alisema anatambua kuna Wakala zenye upungufu wa Watumishi hivyo zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo alielekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya mahitaji halisi ya Watumishi.
  Waziri Kairuki, pamoja na hilo alielekeza Wakala zenye Watumishi wa mikataba zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya Taasisi.
  Waziri Kairuki aliongeza kuwa yapo malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali. Aliainisha masuala hayo ni pamoja na Watumishi hewa, taarifa chafu za Watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za Umma, kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.
  Alifafanua kuwa amegundua kupitia taarifa mbalimbali kuwepo kwa  changamoto ya mawasiliano hafifu kati ya Wizara mama na Wakala zilizo chini yao ambapo taarifa kutoka katika Wakala hazichambuliwi inavyostahili na hata zinapochambuliwa na wizara mama, hazitoa mrejesho kwenda katika Wakala.
  Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro alizitaka Wakala za Serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania.
   Alisema matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha Wakala za Serikali zinapunguza utegemezi kwa Serikali kwa kujitegemea kimapato kutokana na vyanzo vyake vya ndani hasa kwa Wakala zinazoingiza mapato makubwa kutokana na huduma zinazotoa.
  Serikali ilianzisha Wakala kwa lengo la kuzifanya vyombo vya kutekeleza majukumu kwa niaba ya Serikali kwa tija na ufanisi zaidi, pia kupunguza urasimu na hivyo kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

  0 0

  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongoza Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo.Kushoto ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome.
  Jaji Mfawidhi wa MahakamaKuu Divisheni ya Kazi Mhe. Aisha Nyerere akionesha bango kabla ya kanza kwamatembezi ya Uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali kabla ya kuanza kwa matembezi ya zinduzi wa wiki ya Sheria leo jijini dar es salaam.
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakamawakiwakwenye Matembezi hayo.
  Baadhi ya Watumishi wa Mahakamawakiwakwenye Matembezi hayo.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akizungmza wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .


  PICHA ZOTE NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za pole na pongezi Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa kazi nzuri na kubwa waliyoifanya ya kuwaokoa wachimbaji wadogo 15 waliofukiwa na maporomoko ya udongo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa RZU uliopo katika Kijiji cha Nyarugusu, wilaya ya Geita katika mkoa wa Geita.


  Tukio hilo la kufukiwa wachimbaji hao wadogo 15 wakiwemo Watanzania 14 na Raia Mmoja wa China lilitokea usiku wa Tarehe 26 Januari mwaka 2017.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa furaha taarifa za kuokolewa kwa wachimbaji hao wadogo na amesifu na kupongeza jitihada za kuwaokoa wachimbaji hao  zilizofanywa na Serikali ya Mkoa wa Geita, Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa mkoa wa Geita, Wamiliki wa Migodi ya Dhahabu na wananchi kwa ujumla kwa kutoa vifaa mbalimbali vya uokoaji jitihada ambazo zimepelekea kuokolewa kwa wachimbaji hao wakiwa hai.


  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa“jitihada ,Umoja na Mshikamano ulioonyeshwa na makundi mbalimbali katika kuwaokoa ndugu zetu waliofukiwa na maporomoko ya Udongo wakiwa kazini huko Geita ni mfano mzuri na wakuigwa na wananchi na taasisi nyingine nchini katika kujitolea kwa hali na mali hasa vifaa vya uokoaji kwa ajili ya kusaidia watu wanaopatwa na majanga ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama walivyofanya ndugu zetu wa mkoa wa Geita nawapongeza Sana”.


   Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wamiliki wa migodi kote nchini wahakikishe wanafanya kazi zao za
  uchimbaji wa madini kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria kama hatua ya kuepuka madhara yanayoweza kutokea wakiwa wanafanya shughuli zao za uchimbaji wa madini.  Kupitia kwako Mkuu wa mkoa wa Geita napenda kutuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kutokea kwa tukio hilo na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wachimbaji hao ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu Katika Hospitali ya Serikali ya mkoa wa GEITA matibabu mema ili waweze kupona haraka na kurejea kwenye kazi zao za kujitafutia riziki.


  Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Kudhibiti Maafa nchini, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita na kupekelea kuchukuliwa hatua za haraka katika kushughulikia ajali hiyo.


  Imetolewa na

  Ofisi ya Makamu wa Rais wa

  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Dar es Salaam            

  29-Jan-2017.  0 0

  SERIKALI ya Mkoa Mara kwa kupitia Katibu Tawala wake, Mheshimiwa Ado Mapunda, imewaagiza watendaji wa serikali mkoani humo kuhakikisha kompyuta walizopewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, zinaelekezwa kwenye shule za kata ili kuchangia ukuzaji wa kiwango cha elimu.

  Mheshimiwa Mapunda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati anapokea kompyuta sita kutoka Bayport zilizoelekezwa katika Halmashauri ya Tarime, Rorya na Manispaa ya Musoma, huku kila ofisi ikipata kompyuta mbili ikiwa ni mwendelezo wa ugawaji wa vitendea kazi kutoka kwenye taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa.


  Akizungumza katika makabidhiano hayo, Katibu Tawala huyo alisema lengo la Mkoa wao ni kuona kiwango cha elimu kinapiga hatua kubwa, hivyo wameona msaada huo uelekezwe zaidi katika shule za kata kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu muhimu za wanafunzi wao.Alisema kufanya hivyo kutaongeza ukuzaji wa elimu ya wanafunzi wa mkoani Mara, ili iwe njia ya kuandaa wataalamu wazuri kwa kutumia vema teknolojia ya kompyuta inayoboresha utendaji wa kazi.

  “Tunashukuru wenzetu wa Bayport wa Kanda ya Ziwa pamoja na Makao Makuu kwa kutuletea msaada huu mkubwa kwetu ambao kwa hakika tutautumia vizuri katika Mkoa huu wa Mara ili ulete tija kama mlivyokusudia wakati mnafikiria kusambaza.


  “Ofisi yetu imeagiza kompyuta hizi zisambazwe katika baadhi ya shule za kata kwa kuzitumia kwa namna moja ama nyingine ili wanafunzi wetu wasonge mbele zaidi kwa kuanzia kurekodi vizuri takwimu zao kama njia ya kugundua tunafanya juhudi za kutuvusha hatua ya juu zaidi,” Alisema Mapunda.


  Naye Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema ndoto zao zinaelekea kukamilika kuhakikisha kwamba msaada wa kompyuta zao unafika kwa haraka kama walivyokusudia na kuuzindua mwaka jana jijini Dar es Salaam.


  “Kompyuta tulizotoa Mara na Kanda ya Ziwa ni mwendelezo wetu wa kutoka kwenye kompyuta 125 tulizomkabidhi Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, huku 80 zikielekezwa mikoani na kuufanya mzigo wote ufikie 205 wenye thamani ya Sh Milioni 500,” Alisema Mercy.


  Mbali na Mara, Bayport pia walikabidhi kompyuta mbili kwa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, mkoani Mwanza na kuifanya Kanda ya Ziwa kuvuna kompyuta nane za taasisi hiyo ambapo pia ilitangaza kuwa utaratibu huo wa kufikisha kompyuta utaendelea katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wakiamini utasaidia kuongeza ufanisi katika ofisi za umma.
  Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, akimkabidhi kompyuta sita Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ado Mapunda kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ofisi za umma mkoani Mara. Wengine kwenye tukio hilo ni watumishi wa Bayport, akiwamo Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Bayport, Lugano Kasambala wa kwanza kushoto. Picha na Mpiga Picha Wetu Mara.

  0 0


  Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa  ligi baada ya kutoka na ushindi wa goli 2-0 kwenye mchezo uliofanyika leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

  Obrey Chirwa aliyeingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuifungia timu yake goli 2 katika dakika ya 69 na 82.

  Yanga waliingia uwanjani wakitafuta ushindi wa aina yoyote ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu  hizo zilienda mapumziko wakiwa hawajafungana.

  Mwadui waliokuwa makini katika safu yao ya ulinzi waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga na kuwafanya kushindwa kupata goli la mapema.

  Kila upande walifanya mabadiliko kwa ajili ya kusaka ushindi huo, na baada ya matokeo haya Yanga anaongoza ligi akiwa na alama 46, akifuatiwa na Simba mwenye alama 45 huku Azam akiwa na alama 34.

   Wachezaji wa Timu ya Mwadui, wakiusindikiza mpira kwa macho wakati ukiingia wavuni, baada ya kupigwa kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa na kuipatia timu yake goli la kuongoza.
   Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa na Simon Msuva wakishangilia ushindi wao dhidi ya Mwadui Fc, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni hii katika Dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.
   Furaha ya ushindi kwa wachezaji wa Yanga.
   Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwania mpira na Beki wa Mwadui, Nassor Chollo, wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika Dimba la Taifa, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 2-0.


  0 0

  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa katika hali ya kuamsha hari na morali ya kufanya kazi kwa watendaji wa Jeshi la Magereza amefanya ziara ya kikazi katika baadhi ya Magereza ya Mkoa wa Morogoro na Pwani mwishoni juma hili.

  Ziara hiyo imejumuisha Magereza ya Mbigiri, Wami Kuu, Wami Vijna, Mahabusu, Kihonda, Kingolwira Complex yote ya mkoa wa Morogoro na Shule ya Sekondari Bwawani na gereza Ubena vya mkoani Pwani.

  Kutoka kwa Kaimu Jenerali maafisa na askari aliwapata taarifa fupi ya Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha gereza Mbigiri Mkoani Morogoro kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Alisema uwekezaji huu ni kwa faida ya Jeshi kama Taasisi hivyo ni vizuri kila askari akalifahamu hilo.

  Katika ziara hiyo pia alipata wasaa wa kufanya vikao na watendaji ambapo maafsa, askari na watumishi raia walipata fursa ya kuuliza maswali moja kwa moja kutoka kwa Mtendaji mkuu wa Jeshi la Magereza ambapo baadhi ya mambo yalipatiwa majibu ya papo hapo na mengine kupewa ahadi ya kutatuliwa katika siku za usoni hasa yenye uhusiano na masuala ya kibajeti.

  Miongoni mwa masuala yaliyoonekana kuwa ni tatizo sugu ni pamoja na huduma za maji, usafiri, matibabu kwa wafungwa na mahabusu, sare za askari, posho mbalimbali kulingana na stahiki ya kila askari na mambo mengine madogo madogo ambayo yote kimsingi yanagusia suala la fedha.

  Katika vikao hivyo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alitolea maelekezo baadhi ya mambo yaliyohitaji kauli ya Makao Makuu ya Jeshi lakini pia aliwahakikishia kuwa ofisi yake itaendelea kushughulikia kero zote na kusaidia kwa haraka pale inapohitaji kwa kutegemeana na hali ya fedha kwa wakati huo.

  Kaimu Kamishna Jenerali aliwaasa maafisa askari kuwa waangalifu wanapotumia mitandao ya kijamii hasa kwa kuzingatia viapo vya utumishi wao.“Ninyi ni askari wenye viapo vya utii wa mamlaka zilizopo, jiepusheni na mijadala ya mitandaoni kwani mingine iko kinyume na maadili ya kazi zetu. Ukipokea ujumbe usiofaa futa kabisa badala ya kuusambaza” alisisitiza Dr. Malewa
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kulia) akitembelea jengo la Karakana ya Ufundi ya Gereza Wami Vijana. Jengo hilo pamoja na kuendelea kutumika lakini bado linahitaji kukamilishwa kujengwa na kuwekewa miundombinu ili liweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akipata maelezo mafupi ya kiutendaji kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu wa Magereza (SP) Zephania Neligwa (aliyesimama) ofisini kwake wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali Mkoani Morogoro aliyoifanya mwishoni mwa juma.
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Gereza Kihonda. Jengo hilo linashengwa kwa jitihada za Mkuu wa Gereza hilo kwa kushirikiana na maafisa na askari wa kituo hicho. Viongozi wengine hapo ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka, Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na Mkuu wa Gereza Kihonda Kamishna Msaidizi wa Magereza Ben Mwansasu.
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akiendelea kusikiliza hoja mbalimbali za maafisa na askari wa Gereza Kihonda wakati wa ziara ya kikazi kituoni hapo. Aliyesimama ni Mkaguzi Msaidizi wa Magereza (A/Insp) Amani Moses akichangia jambo wakati wa kikao hicho
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akikagua maendeleo ya moja ya nyumba za zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea katika gereza la Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba kituoni hapo. Aliyefuatana naye ni Mkuu wa Gereza la Wanawake Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Luhembe.


older | 1 | .... | 1536 | 1537 | (Page 1538) | 1539 | 1540 | .... | 3270 | newer