Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1537 | 1538 | (Page 1539) | 1540 | 1541 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Songwe.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amewaonya mawakala wa forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma/Nakonde kuacha Mara moja tabia ya kuwachelewesha madereva wa malori yaendayo masafa marefu kwa makusudi ili wapewe rushwa.

  Prof. Mkenda ametoa onyo hilo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva wa malori waliodai wamekuwa wakicheleweshwa kuvuka mpaka huo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano.

  Wadereva hao wameeleza kuwa mawakala wa forodha wamekuwa wakiwaambia kuwa nyaraka zao zinazohusika na mizigo wanayosafirisha zimekuwa zilicheleshwa na kituo cha Forodha upande wa Zambia.

  Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Kituo cha Nakonde, Bw. Nase Lungu, amekana kuhusika na ucheleweshaji huo na baada ya ukaguzi wa moja ya nyaraka hizo ilibainika kuwa upande wa Zambia unatoa nyaraka hizo kwa wakati lakini zimekuwa zikifichwa na Mawakala wa Forodha upande wa Tanzania.

  Wakitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo, madereva hao wamesema kuwa mawakala wa forodha kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza kuwa mtandao wa intaneti wa Upande wa Zambia unaotumika kuchakata nyaraka zao uko chini, hivyo walitakiwa kutoa shilingi 10,000 kwa kila nyaraka ili “kurahisisha” kazi hiyo kwa kuwapa kitu kidogo maafisa wa forodha wa Zambia.

  “Mawakala wengine wa forodha wana nyumba zao za kulala wageni hapa Tunduma kumbe wanatulazimisha kukaa hapa ili tulale kwenye nyumba hizo hali inayotutia hasara na wanatumia kutokujua kwetu kutudanganya kwamba mtandao uko chini wakijua hatuna uwezo wa kufuatilia huko Zambia” alieleza kwa masikitiko dereva mmoja 

  0 0

  Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau kesho Jumatatu Januari 30, kwa pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.

  Uzinduzi wa kampeni hizo unaopewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’ utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam saa 5.00 asubuhi ambako wadau na wafamilia wa mpira wa miguu wanakaribishwa.

  Tayari timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali hizo za za Olimipiki.

  Kambi hiyo imepigwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.

  Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0


  0 0

  Na Benny Mwaipaja, WFM, Songwe 

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amewaonya mawakala wa forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma/Nakonde kuacha Mara moja tabia ya kuwachelewesha madereva wa malori yaendayo masafa marefu kwa makusudi ili wapewe rushwa.

  Prof. Mkenda ametoa onyo hilo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva wa malori waliodai wamekuwa wakicheleweshwa kuvuka mpaka huo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano.

  Wadereva hao wameeleza kuwa mawakala wa forodha wamekuwa wakiwaambia kuwa nyaraka zao zinazohusika na mizigo wanayosafirisha zimekuwa zilicheleshwa na kituo cha Forodha upande wa Zambia.

  Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Kituo cha Nakonde, Bw. Nase Lungu, amekana kuhusika na ucheleweshaji huo na baada ya ukaguzi wa moja ya nyaraka hizo ilibainika kuwa upande wa Zambia unatoa nyaraka hizo kwa wakati lakini zimekuwa zikifichwa na Mawakala wa Forodha upande wa Tanzania.

  Wakitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo, madereva hao wamesema kuwa mawakala wa forodha kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza kuwa mtandao wa intaneti wa Upande wa Zambia unaotumika kuchakata nyaraka zao uko chini, hivyo walitakiwa kutoa shilingi 10,000 kwa kila nyaraka ili “kurahisisha” kazi hiyo kwa kuwapa kitu kidogo maafisa wa forodha wa Zambia.

  “Mawakala wengine wa forodha wana nyumba zao za kulala wageni hapa Tunduma kumbe wanatulazimisha kukaa hapa ili tulale kwenye nyumba hizo hali inayotutia hasara na wanatumia kutokujua kwetu kutudanganya kwamba mtandao uko chini wakijua hatuna uwezo wa kufuatilia huko Zambia” alieleza kwa masikitiko dereva mmoja 

  Baada ya kubaini uwepo wa vitendo hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA upande wa Tunduma kuandika kibao chenye namba za simu za Mkuu wa TRA mpakani hapo zitakazotumiwa na madereva wanaocheleweshwa kwa makusudi kutoa malalamiko yao.

  “Tunataka madereva mtumie siku moja tu kukamilisha nyaraka zenu ili muendelee na safari yenu vinginevyo tutadumaza biashara kati ya Zambia na Tanzania na pia tutaifanya Bandari yetu ya Dar es salaam kushindwa kuleta tija” aliongeza Prof. Mkenda 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe, Bw. Juma Irando (katikati), na maafisa kadhaa wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji, wakitoka katika Ofisi za Mkurugenzi wa Mji wa Tunduma kuelekea mpakani mwa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma na Nakonde
  Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee (kulia), akiueleza ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji namna idara yake ilivyojiandaa kuanza kutoa huduma ya pamoja mpakani kati ya maofisa kutoka Zambia na Tanzania ambao watakuwa wakitumia ofisi moja kuwahudumia watu wanaotumia mpaka huo kuvuka kwenda kila upande wa nchi (Tanzania na Zambia)
  Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa pamoja na maofisa wa mamlaka ya Mapato kutoka Zambia wakiangalia hali ya biashara na uwekezaji katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde ikiwa ni maandalizi ya kuanza rasmi kwa utoaji wa huduma wa pamoja kati ya nchi hizo mbili ili kuboresha mazingira ya biashara baada ya kusainiwa kwa mikataba ya kuanzishwa kwa huduma hiyo katika mpaka huo
  Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato kutoka Zambia (ZRA) walipotembelea upande wa pili wa mpaka huo-Nakonde ili kujionea maandalizi ya kuanza rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya Tanzania na Zambia baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzishwa kwa huduma hiyo Februari mosi, 2017

  Ujenzi wa Kituo cha Pamoja Mpakani upande wa Tanzania-Tunduma, ukiendelea kwa kasi na una tarajiwa kukamilika baada ya miezi 16 ijayo

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


  0 0
 • 01/29/17--09:53: TAARIFA YA MSIBA
 • Eng Joseph Shega wa Nyumbu Kibaha anasikitika kutangaza kifo cha mama yake mzazi MARIETHA  LUSAMBO kilicho tokea jana asubuhi katika Hospitali ya Mpanda Katavi Mazishi yatafanyika kesho Jumatatu kuanzia mchana tarehe 31 Janary 2017 wilayani Mpanda.

  HABARI ZIWAFIKIE 

  Kaka wa marehemu Emily Lusambo akiwa Kisa Rukwa

  Mh Sebastian Kapufi Mbunge wa Mpanda mjini

  Wifi wa marehemu Angelina Kisunga wa Kibaha Pwani

  Watoto wote wa marehemu wajuu wote waliopo Dar es salaam Arusha Kilimanjaro 
  Kibaha  Sumbawanga 

  Wafanyakazi wa shirika la nymbu kibaha, majirani wote wa kwa matiasi kibaha, pamoja na marafiki wote

  Bwana ametoa Bwana ametwa jinalake lihimidiwe Amen

  0 0

   Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa leo  Januari 29, 2017 mnamo  saa 9:40 alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali . Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia.

  Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.


  Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika!


  Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame  Mbarawa  .Mkuu wa TRL Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi , Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S. Chillery wako  katika eneo la ajali! .


  Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es Salaam na  inatarajiwa kuwasili saa 2 usku.


  Aidha  uongozi wa TRL umehakikisha umma na wateja wake kuwa njia ya reli  kati ya Ruvu na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji  zirejee kama kama kawaida.


  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:

   Kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL

  Ndugu Masanja Kungu Kadogosa

  Januari 29, 2017

  DAR ES SALAAM 

  Baadhi ya Mabehewa ya  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.
   Baadhi ya Mabewa mengine yakionekana kuacha njia

  Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017. 

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

    
  ZOEZI LA UOKOAJI WACHIMBAJI 15 WALIOFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MGODI WA DHAHABU GEITA   LAKAMILIKA KWA MAFANIKIO


  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha  umma kuwa, Zoezi la kuwaokoa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi  tarehe 26/01/2017 kwenye mgodi wa dhahabu eneo la kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Wilayani Geita limekamilika kwa mafanikio.


  Ajali ya kufukiwa wachimbaji hao iliyohusisha Watanzania 14 na raia 1 wa China ilitokea kwenye leseni ya uchimbaji wa Kati wa madini ya dhahabu yenye Namba ML 492/2013 inayomilikiwa na Bw. Ahmed Mubarak Adam.


  Chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni kuanguka kwa shaft ya mgodi huo na kufukiwa na kifusi wakati wachimbaji hao wakifanya kazi mgodini chini ya ardhi.


  Tukio la uokoaji limefanikiwa leo tarehe 29/01/2017 ambapo wahanga hao walianza kutolewa shimoni kuanzia saa 5 hadi saa 5:30 asubuhi wote 15 wakiwa hai ingawa walikuwa wamedhoofika kiafya.  Aidha, wachimbaji hao wamepewa huduma ya kwanza katika eneo la ajali na kisha kukimbizwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Geita. Hadi sasa wachimbaji hao wapo Hospitali wakiendelea na matibabu kwa uchunguzi zaidi wa afya zao.


  Juhudi za kuokoa wachimbaji hao  ambazo zilifanyika kwa kufukua kifusi katika eneo la ajali zilianza mara baada ya tukio hilo kutokea. Uongozi wa Mkoa wa Geita ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Meja. Jen.(Mst) Ezekiel E. Kyunga ulishirikiana na Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni za Madini mbalimbali mkoani Geita katika zoezi la ufukuaji kifusi ili kuokoa maisha ya wchimbaji hao


   Kampuni zilizoshiriki kwa kutoa mitambo na vifaa mbalimbali ni Kampuni ya Busolwa Mining Ltd; Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM); Kampuni ya Nyarugusu Mining Ltd; Nsangano Mining Project; Metchell Tanzania Drilling; WAJA Hospital pamoja na wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Geita wakiongozwa na Viongozi wa wachimbaji madini Wilaya, Mkoa na Taifa.


  Akizungumza mara baada ya kuokolewa wachimbaji hao, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa hali na mali kufukua kifusi na hatimaye kufanikiwa kuwatoa wachimbaji chini ya ardhi wakiwa hai.


  Dkt. Kalemani amewaomba Watanzania kuendelea na moyo huo pale majanga kama haya yanapotokea. Aidha, Dkt. Kalemani ameagiza shughuli zifungwe kwa muda wa siku tano kwenye mgodi uliopata ajali kuanzia tarehe 29/01/2017 ili kutoa nafasi kwa Kamishna wa Madini kufanya tathmini ya hali ya usalama wa mgodi na kutoa maelekezo kabla ya shughuli kuanza.


  Vilevile, amewataka wachimbaji wawe watulivu katika kipindi ambacho tathmini ya hali ya usalama wa mgodi inafanyika na kuagiza Uongozi wa Mkoa kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarishwa eneo la mgodi ili watu wasiweze kuingia na kuhatarisha maisha yao. 


  Pia, ameagiza ukaguzi wa kina ufanyike kwenye migodi mingine ya wachimbaji wadogo na ya kati eneo la Nyarugusu na kwingineko nchini ili kuhakikisha kuwa migodi inakuwa salama kwa wachimbaji wa migodi husika.


  Imetolewa na;

  KATIBU MKUU

  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  29/1/2017
  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na viongozi wa mataifa mabalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika jengo jipya la kituo cha  Amani na Usalama (JULIUS NYERERE) lililopo katika Makao makuu ya Umoja wa Afrika Addis Ababa nchini Ethiopia. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Viongozi Wakuu wa Mataifa mbalimbali hawapo (pichani) katika Jengo jipya la Kituo cha Amani na Usalama kilichopewa jina Rasmi la Mwalimu Julius Nyerere, Addis Ababa nchini Ethiopia.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kutangazwa rasmi kwa Jina la Mwalimu Julius Nyerere katika kituo hicho cha Amani na Usalama.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wakielekea katika Kituo cha Amani na Usalama cha Makao Makuu ya Umoja wa Afrika kilichopewa jina la Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Addis Abba nchini Ethiopia. PICHA NA IKULU  0 0

  Uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo umesababisha hasira kuu duniani kote na wahamiaji wakikataliwa kupanda ndege kuingia Marekani. 
  Raia waliokuwa na hati halali za kusafiria kutoka Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen walizuiliwa kwenye viwanja vya ndege, wakati wale waliokuwa wameshapanda ndege wakishikiliwa baada ya kutua Marekani. 
   Katika tukio moja, abiria watano wa Iraq na mmoja wa Yemeni, waliokuwa na visa halali, walizuiliwa kupanda ndege ya EgyptAir iliyokuwa ikitoka Cairo kwenda New York na hatimaye kuelekezwa kwenye ndege zinazorudi kwenye nchi zao. 
   Mwanamke mmoja aliyekiambia mauaji ya Isis nchini Iraq mwaka 2014, alizuiliwa kupanda ndege mjini Baghdad, baada ya kusubiria visa kwa miezi mingi ili akaungane na mumewe ambaye tayari yupo Marekani. 
  Rais Trump amepiga marufuku kwa miezi mitatu wakimbizi toka nchi saba duniani, ili kuchuja magaidi wa kiislamu wasiingie nchini humo. 
   Wakimbizi kutoka Syria wamepigwa marufuku kimoja. 
   Hata hivyo, jaji mmoja alitoa ruhusa Jumamosi kwa raia kutoka nchi hizo saba waliokuwa wameshaingia nchini humo, wale waliokuwa njiani, wenye visa halali kukaa Marekani. Waandamaji kadhaa walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Trump. Maandamano zaidi yatafanyika Jumapili hii.
  Rais Donald Trump wa Marekani akionesha kwa wanahabari hati ya kupiga marufuku wahamiaji wa kiislamu kutoka kwenye nchi zenye raia wengi wa dini hiyo akiwa Ikulu ya Marekani ya White House.
   Waandamaji walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Rais Trump. Maandamano zaidi yametarajiwa kufanyika Jumapili hii.
   Waandamaji walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Rais Trump. Maandamano zaidi yametarajiwa kufanyika Jumapili hii.
  Waandamaji walikusanyika kwenye viwanja vya ndege nchini Marekani Jumamosi hii kupinga uamuzi huo wa Rais Trump. Maandamano zaidi yametarajiwa kufanyika Jumapili hii.

  0 0


  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Katiba na sheria  Mtandao na Mbunge wa Muheza Mhe. Balozi Adadi Rajabu akiongea na  wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania 
  Wajumbe wa Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania
  wakipewa somo
  Wajumbe wa Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania wakifuatilia mada
  Mjumbe wa kamati ya bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Katiba na sheria Mhe. Profesa Anna Tibaijuka akitoa neno
  Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Katiba na sheria  Mtandao na Mbunge wa Muheza Mhe. Balozi Adadi Rajabu katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge na wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania 

  0 0

  Na Binagi Media Group
  Umoja wa waendesha bodaboda mkoani Mwanza umepongeza zoezi la ukaguzi wa vyombo hivyo linaloendeshwa na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani.
   Mwenyekiti cha umoja huo, Bw. Makoye Kayanda, amesema zoezi hilo linaangazia maeneo makuu manne ambayo yamekuwa yakihatarisha usalama wa watumiaji wa bodaboda wakiwemo abiria.
  "Cha kwanza ni uvaaji wa kofia ngumu, cha pili leseni ya udereva, cha tatu kuwa na BIMA na nne ni ubebaji wa mishikaki. 
  "Kuna baadhi ya abiria zaidi ya 14 wametozwa faini kwa kukataa kuvaa kofia ngumu, sasa lazima tufuate sheria bila shuruti", alisema Kayanda huku akipongeza zoezi hilo.
  Bw. Kayanda aliwasihi waendesha bodaboda wote kuzingatia utii wa sheria bila shuruti ili kuondokana na mazoea yanayoweza kuhatarisha maisha yao na abiria wao pia huku akiwaonya baadhi ya abiria kuepuka tabia ya kukataa kutumia kofia ngumu kwa kisingizio cha uchafu.
  "Kupanga ni kuchagua, kama hutaki kuvaa kofia nguvu ya unayopewa na bodaboda, nunua ya kwako ama mfuko wa plastiki ili ukipewa kofia uvalie maana kuna watu wanapata ajali wanapasuka vichwa na inakuwa ni tatizo kwa familia zao na taifa kwa ujumla", alihimiza Kayanda.
  Mwenyekiti wa bodaboda mkoani Mwanza, Bw. Makoye Kayanda

  0 0


  0 0

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema miradi ya Kijamii inayoendeshwa kupitia Mfuko wa wa Maendeleo ya Jamii Tanaznia {TASAF } inalazimika kuibiliwa na wananchi wenyewe katika maeneo yao kwa vile wao ndio wanaoelewa mazingira yanayowazunguuka. 
  Amesema Serikali Kuu kazi yake kubwa ni kuongeza nguvu za uwezeshaji katika kuona miradi hiyo inaimarika na kukua kwa lengo la kuwaondoshea ukali wa maisha Wananchi wake katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba. 
  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo akiwa katika ziara ya siku Tatu Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo wakati alipokagua miradi ya Tasaf katika Bonde la Kidau Ndagoni kuona maendeleo ya ujenzi wa Tuta la kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri wakulima wa bonde hilo. 
  Alisema yapo maendeleo makubwa yaliyopatikana tokea kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF)  hasa katika kuzisaidia Kaya Maskini zilizozongwa na ukali wa maisha ziwe na miundombinu ya kujiendesha Kimaisha kupitia miradi wanayoianzisha. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi na wakulima hao wa Bonde la Kidau pamoja na wale wote wanaopata huduma kupitia mfuko wa Tasaf kutokana na juhudi kubwa wanazozichukuwa katika kuimarisha miradi yao ikiwemo ile ya sekta ya kilimo iliyokuwa tegemeo kubwa la wananchi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia 8%. 
   Mhandisi wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Pemba Nd.Talib Bakari kushoto akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuangalia Tuta la kuzuia Maji ya Bahari linaloendelea kujengwa kwenye Bonde la Kidau Ndagoni kupitia Mradi wa TASAF.
   Muonekano wa Tuta la Kuzuia maji ya Bahari kwenye Bonde la Kidau Ndagoni likiwa katika hatua za mwisho kukamilika ujenzi wake kwa zaidi ya asilimia 90%. 

  Balozi Seif akiangalia eneo la Bonde la Kidau ambalo limeathirika kwa maji ya Mvua akiambatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi Kulia yake.
  Picha na  OMPR – ZNZ.


  0 0

  Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inalaani vikali uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
  Akizungumza na Waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema maelfu ya mifugo kutoka nchi jirani ya Kenya imekuwa ikiingizwa ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti muda wa saa 11 jioni, Amesema katika kukabiliana na changamoto ya uharibu wa chanzo kikuu cha maji ya Serengeti kwa asilimia 47.2 ya maji yote, tayari mifugo 1700 imeshakamatwa Mbali na mifugo hiyo.
  Waziri Maghembe alisema kuwa maelfu ya Matrekta ya kutoka nchini Kenya yameletwa kulima katika maeneo yanayopakana na Serengeti Aliongeza kuwa hivi karibuni kilimo kimeshamiri ambapo kipindi cha nyuma wakazi walikuwa wanalima na ng’ombe (maksai) ila sasa matrekta ya Kenya yanalima na kufungua mashamba makubwa.
  Kufuatia hali hiyo, Waziri Maghembe ameagiza kuwa raia wa Kenya wenye mifugo Loliondo warudi makwao mara moja, Mkoa na Wilaya uchukue hatua kuwaondoa mara moja Pia, Matrekta yote ya nchi ya Kenya yawe na usajili wa kodi (Tax Clearance) toka TRA au yarudi kwao mara moja Aidha, ameagiza kuwa eneo la 1,5002km liwekewe alama mara moja na uwekaji alama ukamilike ifikapo tarehe 30 Machi, 2017. 
   Kwa upande wa Utalii, ameziagiza kampuni zote za utalii ambazo hazina usajili wa kitaifa zinazofanya biashara kwa mikataba ya vijiji ziripoti Wizarani ndani ya siku saba, Ikiwa pamoja na kuonyesha usajili wao, kuonyesha vitalu walivyopewa na Serikali pamoja kuiridhisha Serikali kama wanalipa kodi. 
   Awali, akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa Pori Tengefu la Loliondo, Waziri Maghembe alisema anatambua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anasimamia mazungumzo ya wadau wote ili kuleta utatuzi wa mgogoro huo. ‘’Nimeambiwa kuwa mwelekeo wa mazungumzo ni mzuri nahimiza mazungumzo yaendelee, lakini nimeona nikingoja hadi mazungumzo hayo yaishe Hifadhi ya Taifa ya Serengeti itakuwa haipo.’’ alisisitiza
   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Waandishi wa habari jana  mjini Dodoma,  kuhusiana na  uchochezi unaofanywa na Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Loliondo na Ngorongoro ya kuwahimiza wananchi kuchunga, kulima na kukata miti katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo hali inayochangia kukausha  vyanzo maji yanayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
  Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 

  Picha na Lusungu Helela- Maliasili

  0 0
  0 0


  Na Ripota wa Globu, Iringa


  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve ameanza rasmi kutimiza ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuangalia namna ya kuwasaidia wakina mama wa mkoa huo kujiinua kiuchumi.

  Katika ziara hiyo mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Rose ameanza kutimiza ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ndani ya jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa.

  Ziara yake ya kwanza imeanza Januari 28 2017 katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kutembelea kata za Mtitu na Ukumbi na aliweza kuongozana na mbunge viti maalumu kutoka mkoa wa Songwe Juliana Shonzana pamoja na viongozi wa UWT wilaya ya Kilolo.

  Pamoja na mambo mengine Rose ametoa jumla ya shilingi za kitanzania milioni moja na laki tisa ( 1,900,000) kwa jumuiya ya akina mama (UWT) wilaya ya Kilolo kwa ajili ya kujiimarisha na kuinua vikundi vya vya akina mama wa jumuiya hiyo. 

  Rose anaamini kuwa UWT ni kiungo kikubwa na muhimu ndani ya Chama cha Mapinduzi hivyo kama jumuiya ikiwa imara kwa kupitia miradi mbali mbali basi italeta hamasa ndani ya chama na ameahidi kuwa ziara hii ni endelevu na itakuwa ya mkoa mzima.
  Mtendaji Agentina Myovela (kulia) na diwani wa viti maalum wa kata ya ukumbi wilaya ya kilolo Rehema Nyasi wakitoa maelezo kwa Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (katikati) juu ya ujenzi wa kituo cha afya kinachoendelea kujengwa katika kata hiyo.

  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve akipata maelezo kutoka Kwa katibu wa UWT Wilaya Yusuph Mgovole juu ya ujenzi wa ukumbi wa jumuiya hiyo ambapo aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) Kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.
  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (wa pili kulia) akikabidhi kiasi cha pesa shilingi laki Saba (700000) kwa akina mama wa UWT kata ya Mtitu katika ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki ikiwa ni moja ya ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuwainua akina mama wa mkoa huo kiuchumi, kulia ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana.
  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve (wa pili kulia) akikabidhi kiasi cha kiasi cha pesa shilingi laki Sita (600000) kwa akina mama wa UWT kata ya Ukumbi katika ziara aliyoifanya mwishoni mwa wiki ikiwa ni moja ya ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuwainua akina mama wa mkoa huo kiuchumi, kulia ni Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana.
  Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana akipokea zawadi kutoka kwa akinamama wa UWT kata ya Ukumbi katika ziara iliyofanywa na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve mwishoni mwa wiki hii.

  0 0


  Na Mahmoud Zubeiry

  Kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, David Abdallah Burhan amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Bugando, Mwanza.
  Kipa huyo wa Kagera Sugar ya Bukoba alifikishwa hospitalini hapo jana kutoka Bukoba na kwa bahati mbaya asubuhi ya leo ameaga dunia. Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime Kianga ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Burhan (ambaye ni  mtoto mshambuliaji wa zamani wa Pan Africans, Abdallah Burhan)  alikuwa anasumbuliwa na Malaria.
  Mexime alisema matatizo hayo yalianza wakati wamekwenda Singida kucheza na wenyeji, Singida United mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) katikati ya wiki. 
   Alisema alipanga kumuanzisha David Burhan katika mchezo huo, lakini hali yake ikabadilika ghafla hivyo akampanga kipa mwingine, Juma Kaseja badala yake.
   “Tumecheza mechi, baada ya mechi wakati tunarudi, tunafika Biharamulo, macho yake yakaanza kubadilika yakawa ya njano, ikabidi alazwe pale, kesho yake akahamishiwa hospitali ya mkoa wa Kagera, ambako baada ya kupimwa wakasema apelekwe Bugando,”alisema Mexime. 

  0 0

  Abiria wakishuka kutoka katika kivuko cha Mv. Kigamboni kinachotoa huduma ya usafiri kati ya eneo la Magogoni na Feri, leo Jijijini Dar es salaam.


  Abiria wakipanda katika kivuko cha Mv. Magogoni kinachotoa huduma ya usafiri kati ya Ferry na Magogoni, leo Jijijini Dar es salaam.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaonyesha wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini sehemu ya malipo ambapo wagonjwa wanalipia huduma. Wageni hao walitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni ili kuona huduma za matibabu ya moyo wanazozifanya pia waliahidi kuimarisha mahusiano kati yao hii ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili wa masomo kwa madaktari wataokwenda kusoma katika chuo hicho.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini wakiangalia jinsi upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization) unavyofanyika katika chumba Cath Lab kilichopo katika Taasisi hiyo.
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akielezea jinsi upasuaji wa Magonjwa ya Moyo unavyofanyika katika taasisi hiyo wakati wageni kutoka Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini walipotembelea wodi aliyokuwa amelazwa mmoja wa wagonjwa aliyefanyiwa upasuaji. Kutoka kulia ni Prof. Martin Valler, akifuatiwa na Afisa Muuguzi Roger Kibula, watatu kulia ni Prof. Simon Nemutandani na wa pili kushoto ni Dkt. Marion Bergman.
  Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mhadhili kutoka chuo Kikuu kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) Prof. Johnson Rwakatare akimuonyesha vipimo vya moyo (ECHO) Prof. Martin Valler Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Afya wa Chuo kikuu cha Witwatersrand cha Nchini Afrika ya Kusini alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete hivi karibuni.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza wataalamu wa afya kutoka Chuo Kikuu cha Minnesota cha nchini Marekani huduma za matibabu ya moyo wanazozitoa wakati walipoitembelea Taasisi hiyo hivi karibuni. Picha na Anna Nkinda - JKCI

  0 0

   Sehemu ya uwanja wa klabu ya Manchester United Old Trafford ulishika moto asubuhi ya leo kabla vikosi vya zimamoto kufika na kuuzima.
  Shuhuda wanasema walianza kuona moshi mkubwa ukifuka  katika jukwaa la kusini la uwanja huo maarufu liitwalo Sir Bobby Sharlton Stand.Klabu ya Manchester united ilisema katika twitter yake kuwa moto mdogo uliosababishwa na hitilafu ya umeme ulizuka kwenye moja ya lifti na wazima moto waliitwa na kufanikiwa kuuzima. Hakuna madhara makubwa yaliyotokea.
   Vikosi vya zimamoto vikiwa vimeudhibiti moto huo
  Jukwaa ulikozukia moto huo

older | 1 | .... | 1537 | 1538 | (Page 1539) | 1540 | 1541 | .... | 3285 | newer