Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

WAONGOZA UTALII / WABEBA MIZIGO YA WATALII WATOA KILIO KWA SERIKALI

$
0
0
Waongoza utalili wanaosaidia watalii kupanda milima wameiomba serikali kutazama upya malipo wanayopewa katika utekelezaji wa kazi zao kwasababu hayalingani na ugumu wa kazi wanazofanya kuhudumia watalii.Kwa sasa waongoza watalii hao wanalipwa wastani wa kiwango cha dola 10 za kimarekani kwa siku ,kiasi ambacho hakilingani na kazi wanazozifanya.

Hayo yamesemwa na katibu wa waongoza watalii Immanuel Mollel katika sa kongamano la mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii inayofanyika kwa siku mbili katika hotel ya Palace iliyopo Jijini Arusha.

Katibu huyo amezitaja changamoto mbalimbali ambazo wanazipitia ni pamoja na kukosa mikataba ya ajira, wao kulazimika kununua leseni ili waweze kuwaongoza watalii, uharibifu wa mazingira na tabia nchi pamoja na ujangili. Kwa upande wake Katibu wa chama cha wabeba mizigo ya watalii Loshiye Mollel amesema changamoto kubwa wanazozipata ni pamoja na mazingira magumu wanayokabiliana nayo katika utendaji kazi wao.

“wakati tunapokuwa mlimani umebeba mzigo wa mgeni kuna magonjwa ya mlimani ,sasa namna ya kumuokoa huyu mbeba mizigo ya mtalii ni shida sana ,kwani itawalazimu wale ambao wapo kule juu mlimani wakushushe kwa machela hadi chini ,huko napo unakutana na changamoto nyingine hakuna gari kwani magari yapo mawili tu"

"Tupo wabeba mizigo zaidi ya 28,000,kwa siku moja tunakuwa mlimani zaidi ya wabeba mizigo (porters) 4000 au 3000,tunaiomba serikali kutuongezea magari ili kuwepo urahisi wakati wa kumsaidia mbeba mizigo ya watalii anapopata shida akiwa mlimani) mlimani.
Katibu wa chama cha waongoza Watalii (TTGA)akiwa anazungumza na waandishi wahabari na wadau wa utalii katika kongamano Utalii mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii katika ukumbi wa Palace Hotel 28 January 2017.
Katibu wa wabeba mizigo ya watalii (porters)Loshiye Mollel kongamano Utalii mambo ya utalii na uhifadhi kwa waandishi wa habari na wadau wa utalii katika ukumbi wa Palace Hotel 28 January 2017.Picha na Vero Ignatus Blog
Afisa Utalii Mkoa wa Arusha Florah Bazili akiwasilisha mada wakati huohuo akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari pamoja na wadau wa utalii.
Katibu wa jukwaa la wahariri Nevilly Meena akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa utalii katika kongamano hilo.


MADIWANI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI.

$
0
0
MADI
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ,Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,wakielekea katika wodi walimolazwa wagonjwa kwa ajili ya kutoa zawadi.
Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema na Diwani wa kata ya Kiusa,Stephen Ngasa akikabidhi zawadi ya sabuni ya unga kwa wagonjwa waliolazwa katika Hopstali ya Mawenzi.

PASS YAWATAKA WAKULIMA,WAFUGAJI NA WAVUVI KUFANYA SHUGHULI ZAO KITAALAM

$
0
0

Na.Vero Ignatus,Arusha.

Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo (Pass)imewataka wakulima na wajasiriamali wote wa kilimo ,uvuvi na wafugaji wafikirie namna ya shughuli zao kitaalam.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo Nicomed
Bohai ya kwamba wakulima wafikirie kufanya shughuli zao kibiashara,watafute elimu na maarifa ili waweze kudhaminiwa kupata mkopo wa kuendeleza shughuli zao.

Amesema kuwa wanajenga mahusiano ya kibiashara kutoka kwa wafanya biashara wakubwa kwenda kwa wadogo,ili wale ambao wameshapiga hatua wawainue wale ambao bado,kwa kutengeneza mchanganuo wa kibiashara na kutoa udhamini wa mkopo.

Aidha mkurufenzi huyo amesema kuwa Asasi hiyo ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo ipo tayari kumsaidia mtu binafsi,vikundi au makampuni kutumia huduma ya (Pass)haswa wajasiariamali binafsi amabao wana dira ambao wanafanya biashara katika hali ya ufanisi na
kibiashara.

Sambamba na hayo amesema ya kwamba asasi hiyo inashirikiana na benki washirika zaidi ya 11 kupata mkopo kwa wakulima ambao wanaoweza kufikia angalau vigezo vya msingi kwaajili ya ukopaji,huku kipaumbele kikitolewa kwa wateja wenye matokeo makubwa katika mwendelezo wa
mnyororo wa thamani kwa bidhaa za kilimo hususani katika mazao ya chakula ,biashara na mazao ya kusafirishwa nje ya nchi.

Ameainisha mikoa ambayo Pass ipo nchini Tanzania kuwa ni Mwanza ,Kigoma,Kilimanjaro,Morogoro,Mbeya, Dar-es- salaam na Mtwara,amesema wanatumia ofisi hizi za kanda ili kuwafikia wakulima kwa karibu zaidi.
Baadhi ya wakulima wakipata maelekezo katika Pass katika maonyesho ya zana za kilimo yaliyofanyika Jijini Arusha na kumalizaika jana maonesho hayo yalikuwa ya siku mbili.Picha na Vero Ignatus Blog.
Nicomed Bohai ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo Taifa (PASS)Picha na Vero Ignatus Blog.

KUKOSEKANA UZIO SHULE YA MSINGI MCHANGANYIKO PONGWE KUNA WEZA KUSABABISHA HATARI KWA WANAFUNZI.

$
0
0
WATOTO wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa ustawi wao kielimu.

Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linatishia usalama wa watoto hao.

Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa kupatiwa tiba.
Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake 
Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi hao.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani huyo.

UZINDUZI WA WIKI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA KUZALIWA KWA CCM..KONGAMANO LAFANYIKA SHINYANGA

$
0
0


Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  tarehe 05.02.1977. Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akifungua kongamano hilo ambapo aliwataka wanaCCM kujivunia mafanikio ambayo yamepatikana tangu chama hicho kianzishwe mwaka 1977. Kwa habari zaidi BOFYA HAPA


wilaya ya Mbinga yawataka wananchi kutunza chakula cha ziada

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mbinga Mhe. Consimas Mshenyi (pichani) amewataka wananchi wilayani humo kuhakikisha wanatunza ziada ya chakula walichonacho kutokana na hali ya mvua kutoridhisha  licha ya kusema hakuna njaa katika wilaya yake.


Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari kuhusu hali ya chakula katika wilaya hiyo mkuu huyo wa wilaya amesema mpaka sasa vituo vya hifadhi ya chakula wilayani hapo vina zaidi ya tani 300 huku ziada kutoka kwa wananchi ikiwa ni tani 10,000 za mahindi huku mchele ikiwa ni tani 18,000.

 “Nawataka wananchi waendelee kuhifadhi ziada ya chakula walichonacho kwani hali ya mvua si nzuri na ziada hiyo inaweza kupungua pia ziada hiyo inaweza saidia hata kwa majirani zetu” alisema DC Mishenyi.


Aidha Mhe. Mishenyi alisema kuwa hali mazao yaliyopo shambani yapo katika hali nzuri licha ya mvua kunyesha katika hali ya kutoridhisha lakini kuna uhakika wa mazao hayo kukomaa na kuvunwa kwa wakati hivyo akawataka wananchi hususani wakulima kuhakikisha wasimamia utanzaji kwa kushirikiana na wataalamu wa kilimo

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amepiga marufuku unywaji na uuzwaji wa pombe nyakati za kazi kwani kunazoletesha maendelea ya nwilaya hiyo “sitawavumilia wanaokunywa saa za kazi na wanaocheza pool table  nyakati za mchana yaani saa za kazi nitawamuagizaa kupitia kwa afisa biashara mkurugenzi kufuta leseni kwa wale vwote watakao kiuka mashart ya biashara zao ikiwemo kuuza pombe katika saa za kazi”


Kuhusu uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika Januari 22 mwaka huu  katika kata ya maguu wilayani hapa Mishenyi amewataka wanachi kupiga  kura kwa amani na kurejea makwao kusubiri matokeo, huku akiwaomba wagobea kutokuwa vyanzo kuvuruga amani na utulivu na kuwahakikishia ulinzi  wa kutosha katika uchaguzi huu 

Meya wa jiji la Dar ahimiza upendo kwenye huduma za afya

$
0
0

NA CHRISTINA MWAGALA,Dar es Salaam

MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka Madaktari ,wauguzi pamoja na watoa huduma za afya katika Hospitali Vijibweni kutumia taaluma yao vizuri ili kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kupata huduma nzuri.

Meya Isaya ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana katika hafla iliyoandaliwa na wauguzi wa Hospitali hiyo iliyopo Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakiuwaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.

Katika hafla hiyo pamoja na mambo mengine Meya Isaya alisisitiza kwamba kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa upendo kwani kazi yao ni yawito kuliko sekta nyingine.

Alisema wananchi wanapopata huduma nzuri hupata faraja lakini wanapokumbwa na misukosuko kwa watoa huduma sio jambo zuri kwani unaweza kumuongezea mgonjwa maradhi mengine na hivyo akawasihi wafanye kazi zao kwa upendo.

“ Niko pamoja na nyinyi, najua kazi yenu hii ni yawito, lakini mnaposhindwa kufanya kama ambavyo imekusudiwa hili ni tatizo, kwanini mpate sifa mbaya katika huduma yenu?” aliuliza Meya Isaya.

Awali akisoma risala Dokta wa hospitali hiyo, alisema kwamba Hospitali hiyo inatoa huduma za rufaa kwa Kata za vijibweni ,Mjimwema, Kigamboni, Tungi, Somangila, Kibada na maeneo yote ya manispaa ya Kigamboni ambapo kwa sasa hospitali hiyo ndio inayofanya kazi za hospitali ya Wilaya katika manispaa ya Kigamboni.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

FOUR YEARS DEATH ANNIVERSARY

$
0
0
MOSES TITO KACHIMA (27.01.1945 – 29.01.2013)
You are gone but not forgotten, you are a loss that we can’t replace, we loved you but God loved you more and in our hearts you will always live. 
Your love, your voice and your smile are forever imprinted in our minds. We remember and cherish the happy times together, remembering them today and forever. 
You have been a blessing in our lives and your memory lives on. We believe that you are in a better place. 

May your soul rest in eternal peace.

Eternal rest grant to him, O lord and let perpetual light shine upon him. May he rest in peace. Amen


Vacancies

Bamiza Top 20 Music Chart January 28, 2017

KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO WA JESHI LA POLISI NSATO MARIJANI AWAFARIJI ASKARI WALIOPOTEZA MALI ZAO KWA TUKIO LA MOTO MJINI MOSHI.

$
0
0
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

$
0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam. Kwa habari kamili BOFYA HAPA



MAHAFALI YA 32 YA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT) YAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika jana  27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao jana 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
 Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo jana 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM

EFM 93.7 RADIO YASEPA NA KIJIJI KATIKA TANZANIA LEADERSHIP AWARD

$
0
0
EFM redio imejinyakulia tuzo NNE usiku wa kuamkia jana katika tuzo za Tanzania Leadership Awards (T.L.A 2016) kwa vipengele vya Redio bora ya mwaka, Kampuni bora kwa ubunifu, kampuni inayokua kwa kasi pamoja na tuzo ya mwandishi bora ya mwaka ambayo imekwenda kwa mtangazaji wa kipindi cha uhondo katika redio hiyo bibie Dina Marios.

Hafla ya ugawaji tuzo hizo ilifanyika  siku ya tarehe 27/1/2017 katika ukumbi wa Hyatt regency hotel jijini Dar es salaam, ambapo redio hiyo iliwapatia heshima kubwa wasikilizaji wake kwa kuondoka na tuzo hizo.

Ni mwaka wa pili mfululizo kwa redio hio kuchukua tuzo za Tanzania Leadership Awards ambapo tuzo ya kwanza waliipata mwaka jana kwa kipengele cha redio bora ya mwaka.

Ni takribani miaka mitatu sasa tangu redio hii ianzishwe na imejipatia umaarufu mkubwa kwa kuutangaza muziki wa singeli, na kujihusisha na mambo mbalimbali ya kijamii kupitia matamasha,vipindi na kampeni mbalimbali kama vile kupanda miti (mti wangu), kuanzisha vikundi vya mazoezi (efm Jogging club), kampeni za afya, kuhamasisha jamii kujikita katika shughuli za ujasiliamali, pia kutatua matatizo katika jamii  kwa lengo la kujiweka karibu na jamii nzima .


Balozi Seif Ali Iddi akagua Bandari ya Kigomasha, Pemba

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji kuandaa mchakato wa kuwakutanisha Wataalamu wa Sekta hiyo ili wajadili na hatimae kupata kauli moja itakaobaini eneo muwafaka linalostahiki kujengwa Gati Rasmi ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba. 
Alisema hatua hiyo inastahiki kutekelezwa vyema kama ilivyoagizwa na Serikali Kuu la kutaka kujengwa kwa Gati katika Bandari ya Kigomasha ili kujaribu kudhibiti mapato ya Taifa yanayotokana na uingiaji na utokaji holela wa vyombo vya Baharini pamoja na usalama wa eneo hilo. 
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo alipokagua Bandari ya Kigomasha ambayo baadhi ya Wavuvi huitumia kusafirishia magendo akiwa katika ziara ya Siku Tatu Kisiwani Pemba kuangalia miradi ya Maendeleo na ile ya Ustawi wa Jamii. 
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshaamua na kutoa mapendekezo ya kujengwa kwa Bandari Rasmi ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema Uongozi wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Mashariki tayari umeshalipigia kelele eneo hilo la Bandari ya Kigomasha linaloonekana kutumiwa na watu wasiofahamika mazingira yao wakitokea nje ya Visiwa vya Zanzibar jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Taifa. 
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kutumia vyombo vyake vya ulinzi lazima itengeneze mazingira kuvihami Visiwa vyake kutokana na dalili zilizo wazi zinazobainisha baadhi ya wahalifu wanaingia Nchini kinyume na taratibu zilizowekwa za Uhamiaji. 
wageni.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Banadari Zanzibar Nd.Abdulla Juma kati katikakimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  wa kwanza Kulia tatizo la eneo la bandari la Kigomasha ambalo kitaalamu haliwezi kujengwa Gati kutokana na kina kidogo cha maji yake ya Bahari. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mheshimiwa Omar Khamis Othman.
 Balozi Seif akikagua Kitalu cha miche mbali mbali ya matunda, Viungo na Mbao kinachoendeshwa na Wananchi wa Kijiji cha Junguni ndani ya Mkoa Kaskazini Pemba chini ya Mradi wa Tasaf.
Balozi Seif akiridhika na hatua kubwa iliyofikiwa na Wananchi wa Kijiji cha Junguni kwa ujenzi wa Jengo jipya la Skuli ya Maandalizi ya Kijiji hicho chini ya Mradi wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF }.
Picha na – OMPR – ZNZ.

MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MOSHI WATOA ZAWADI KWA WAGONJWA HOSPTALI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI.

$
0
0
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo.
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi, Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 29, 2017

Balozi Sefue Ateuliwa Jopo la Watu Mashuhuri Afrika

$
0
0
Mwanadiplomasia mahiri wa Tanzania aliyepata pia kuwa Katibu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika Jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM tawi la Tanzania, Rehema Twalib anayehudhuria mikutano ya Umoja wa Afrika na APRM mjini Addis Ababa, Ethiopia, Balozi Sefue ameidhinishwa kwenye kikao cha juu ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika ambao ni wanachama wa APRM kilichofanyika juzi Jumamosi mchana.

“Haikuwa kazi rahisi kupata nafasi hii. Nchi nyingi za Afrika zilileta majina ya watu wao mashuhuri ili kuingia katika jopo hili muhimu. Balozi Sefue licha ya kuwa na utumishi uliotukuka kama mwanadiplomasia mkongwe pia aliungwa mkono kwa nguvu zote na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania,” alisema Katibu Mtendaji huyo.

APRM ni Mpango wa Afrika uliobuniwa na Wakuu wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuwa na chombo kitakachosaidia kuhimiza nchi wanachama kuenzi utawala bora na utoaji wa huduma bora za kiuchumi, biashara na za kujamii kwa wananchi wao kupitia mfumo wa kujitathmini zenyewe na kukosoana.

Kwa mujibu wa tovuti ya APRM, Jopo la Watu Mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri Wakuu wa Nchi Wanachama wa APRM katika uendeshaji wa Mpango huo na husimamia mchakato mzima wa kujitathmini.

Wajumbe wa jopo hilo ambao hudumu hadi miaka minne hupendekezwa na nchi zao na baada ya mchakato mrefu wenye ushindani majina ya waliokidhi vigezo huwasilishwa na kuidhinishwa na na kikao cha juu katika APRM-Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

Tanzania ni miongoni mwa wanachama 35 kati ya nchi 54 wa Nchi za AU zilizojiunga na APRM na ilijiunga rasmi na Mpango huo tangu mwaka 2004.Tayari Tanzania ilishafanyiwa tathmini ya kwanza ya utawala bora na inaendelea kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwata kushiriki vyema katika kuihuisha APRM na kuwa chombo chenye thamani kubwa kwa Afrika kama walivyotarajia waasisi wake akina Thabo Mbeki, Olusegun Obasanjo, Benjamin Mkapa na wengine.

Balozi Sefue ataungana na wajumbe wengine wapya ambao ni pamoja na Prof. Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Balozi Mona Omar Attia (Misri) Bi. Fatma Zohra Karadia (Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Prof. Augustin Loada (Burkina Faso). Wajumbe wa zamani wanaoendelea ni pamoja na  Prof. Youssouf Khayal (Chad) ambaye kwa sasa atakuwa Mwenyekiti wa Jopo hilo na Brigitte Mabandla (Afrika Kusini) ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti.

Mkutano huo pia ulijadili Ripoti za tathmini za nchi katika maeneo anuai ya utawala bora kwa nchi za Kenya (ikiwa ni ripoti ya pili kuwasilishwa), Sudan, Chad, Senegal, Djibouti pamoja na ripoti ya utekelezaji ya Zambia.

BENKI YA BIASHARA YA MWALIMU, MCB YATOA SEMINA KWA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA KISWAHILI, CHUO CHA KUMBKUMBU YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba ya ufunguzi wa chilumbo, (kongamano) la Kiswahili, lililofadhiliwa na benki ya MCB, na kufanyika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa Utamaduni palikofanyika chilumbo
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, (kushoto), akipena mikono na Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, mara baada ya kutoa hotuba yake
 Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Huduma kwa wateja wa benki hiyo, Bi.Flora Mbogo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, wakiwasikiliza washiriki mbalimbali waliohudhuria chilumbo (kongamano), hilo na wakataka kujua huduma zitolewazo na MCB.



Tanzanian seasoned Diplomat Ombeni Sefue joins AU-APRM Panel of Eminent Persons

$
0
0
By Staff Reporter

Tanzania’s seasoned diplomat, Ambassador Ombeni Sefue has been appointed to join the Panel of Eminent Persons of the African Union’s African Peer Review Mechanism (APRM) following his nomination by the Fifth Phase Government of Tanzania.
According to information confirmed by the Executive Secretary of the APRM Tanzania Secretariat, Rehema Twalib, Ambasador Sefue and other new panelists were endorsed during the Forum of Heads of State and Government held in Addis Ababa on Saturday.
Other new panelists include Prof. Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Amb. Mona Omar Attia (Egypt), Fatma Zohra Karadia (Algeria), Bishop Don Dinis Salomão Sengulane (Mozambique) and Prof. Augustin Loada (Burkina Faso).
APRM is a specialized Agency of the African Union (AU), and was initiated in 2002 and established in 2003 by the African Union in the framework of the implementation of the New Partnership for Africa's Development (NEPAD).
“APRM is a tool for sharing experiences, reinforcing best practices, identifying deficiencies, and assessing capacity-building needs to foster policies, standards and practices that lead to political stability, high economic growth, and sustainable development and accelerated sub-regional and continental economic integration,” a statement in the APRM website reads.
The statement adds: “Member countries use the APRM to self–monitor all aspects of their governance and socio-economic development. African Union (AU) stakeholders participate in the self-assessment of all branches of government – executive, legislative and judicial – as well as the private sector, civil society and the media.
“The APRM Review Process gives member states a space for national dialogue on governance and socio-economic indicators and an opportunity to build consensus on the way forward.”
On the Panel of Eminent Persons, the APRM website cites it as a crucial oversight organ with a high level mandate to ensure credibility and performance of the Mechanism.
“The Panel exercises oversight of the APRM process with a view to ensuring the independence, professionalism and credibility of the process. It is important to note that the APRM is directed and managed by a Panel of between 5 and 7 Eminent Persons. They are ‘Africans who have distinguished themselves in careers that are relevant to the work of APRM’,” reads a statement in the website.
Tanzania joined the APRM way back in July, 2004. The country’s Parliament ratified the MOU on 1st February 2005. The country’s first assessment report was presented to the Forum of Heads of State and Government in January, 2013.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images