Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1531 | 1532 | (Page 1533) | 1534 | 1535 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Singida.

  Viongozi, Watendaji na Watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Singida wametakiwa kuhakikisha taarifa zote za mapato na matumizi zinawafikia wananchi wote katika ngazi ya Kata na Kijiji ili waweze kuelewa hasa kiasi cha fedha zilizoingizwa na Serikali katika Halmashauri na namna zinavyo tumika.

  Agizo hili limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi katika ziara yake ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kujenga Uelewa wa pamoja, utumishi wa pamoja, na kasi ya pamoja ili kufikia lengo pamoja kwa maslai  mapana ya Taifa.

  Kwa upande wa Wakuu wa Idara na Vitengo Dkt Nchimbi amewaagiza wawe na taarifa za kila siku za watendaji na watumishi katika mnyororo wote wa kiutendaji na kiuongozi na kuepuka kutegemea taarifa za makaratasi na ili kuimrisha utendaji wa kuzingatia matokeo yanayo onekana.

  Niaibu sana kwa Mganga Mkuu wa Wiwala (DM) kushindwa kutoa takwimu pale unapo ulizwa swali nje ya ofisi yako juu ya idadi ya watoto waliozaliwa ndani ya siku tatu katika wilaya yako au Afisa Elimu wa Halamashari unashindwa kutoa jibu la ni Walimu wangapi katika Halmashauri yako hawakuingia kazini kwa sabau za kiafya. Sinto penda hali hii iendelee kujitokeza katika Mkoa wa Singida. Aliongeza Dkt Nchimbi.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wa pili kutoka kushoto) akishiriki kupalilia zao la mtama Mtama katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.
   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki kupanda Mihogo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

   Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi (wapili kutoka kulia) akishiriki kikamilifu katika shughuli za kilimo katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

  Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi akishiriki chakula cha mchana baada ya kukaribishwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwenge Singida katika ziara aliyoifanya Mkoani humo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA  0 0

  Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk Selemani Sewange wakiweka saini makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto waliosimama) ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah, Kaimu Mhariri wa Habari Leo, Nicodemus Ikonko na Mwanasheria wa TSN, Mwadawa Sakware (kulia)
   Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Dk Selemani Sewange wakikabidhiana makubaliano ya kukuza lugha ya kiswahili kupitia gazeti la Habari Leo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka kumi ya gazeti hilo, jijini Dar es Salaam. 
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,akizungumza kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la HabariLeo,iliyofanyika leo katika uwanja wa Taifa,jijini Dar.Waziri Nape alisema kuwa Gazeti hilo lililoanza kuchapishwa rasmi Desemba 21, 2006,limekuwa na  mchango mkubwa sana katika juhudi za kuepuka migawanyiko ya kisiasa nchini, na kuimarisha juhudi za kuendeleza umoja wa kitaifa. 

  "Na hili likiwa ni mojawapo ya malengo ya msingi na kusudio la kuanzishwa kwa Gazeti la HabariLeo na kwa kweli niwapongeze kwa namna mlivyolifanya kwa kiwango cha juu kabisa,Muda wa miaka 10 sio mdogo kwa uhai wa gazeti hasa kutokana na ushindani mkubwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia ya habari hapa nchini na duniani kote.",alisema Waziri Nape.


   Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi akizungumza  kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 10 ya gazeti la HabariLeo,iliyofanyika leo katika uwanja wa Taifa,jijini Dar.
   Mgeni rasmi,Waziri Nape akizindua bahati nasibu ya watoto waliozaliwa desemba 21,2006,anaeshuhudia pichani kulia Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi 
   Uongozi wa TSN ukimkabidhi zawadi ya Picha Waziri Nape .
   Waziri Nape pamoja na uongozi wa TSN ,Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi (kushoto) na Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah (kulia) kwa pamoja wakikata  keki maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo.
   Waziri Nape akimlisha keki Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN), Dk Jim Yonazi 
  Wafanyakazi wa kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) na wageni mbalimbali wakifuatilia matukio ya maadhimisho ya sherehe za miaka kumi ya gazeti la Habari Leo, yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.PICHA NA MICHUZI JR.
  0 0

  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohamed Waziri (kulia) akimkaribisha Balozi wa Msumbiji kwenye maonesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi nchini Kenya.
  Ofisa wa Ubalozi wa Venezuela Nairobi, Jose Gregorio Ayila Torres (katikati) akibadilishana mawazo na Kaimu Balozi wa Tanzania (kulia). Kushoto ni mmoja wa wasanii wa Tanzania, Raza Mohamed.
  Raia wa Uswisi waliofika kwenye maonesho wakijadiliana jambo wakati wa maonesho hayo yaliyoshirikisha wasanii 14 kutoka Tanzania wa uchoraji yaliyoanza toka jana katika ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.
  Wapenda sanaa wa Kenya wakikagua kazi za wasanii wa Tanzania kwenye ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.
  Wadau wa sanaa wakifurahia maonesho yaliyowakutanisha Wasanii wa sanaa ya uchoraji 14 kutoka Tanzania huku yakihudhuliwa na wadau mbalimbali kutoka nchini Kenya 

  0 0

  Thanks

  0 0

  Dodoma.

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe atawasilisha Bungeni wiki ijayo muswada wa kihistoria wa msaada wa kisheria kwa wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama za mawakili katika kutetea na kupigania haki zao nje na ndani ya mahakama.

  Jumatano wiki hii Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilimaliza zoezi lililochukua wiki nzima la kukutana na wadau mbalimbali wa sheria kubadilishana nao mawazo kuhusu muswada huo na baadaye kumwita Dk. Mwakyembe kujibu baadhi ya changamoto zilizojitokeza.

  Katika kuhitimisha zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa, alimpongeza waziri huyo kwa kuzingatia kwa karibu maoni ya wadau na Kamati, hatua ambayo itawezesha muswada huo kupita bila upinzani mkubwa.

  Sheria ya Msaada wa Kisheria itawezesha kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania wananchi wasio na uwezo wa kuhudumiwa na mawakili kwenye masuala ya kisheria kupata msaada huo kutoka kwenye vikundi mbalimbali vya msaada wa kisheria vitakavyokuwa na wasaidizi wa kisheria nchi nzima.

  Maelfu ya vijana waliomaliza sekondari na vyuo mbalimbali watapatiwa mafunzo maalum ya kisheria na kutambuliwa rasmi kuwa wasaidizi wa kisheria watakaosambazwa mijini na vijijini kutoa huduma hiyo.

  Mitaala ya mafunzo hayo iliishaandaliwa na Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) na hadi sasa zaidi ya vijana 4,700 wameshapitia mafunzo hayo.

  Akihojiwa mjini Dodoma jana, Dk. Mwakyembe alisema sheria hiyo itakuwa mkombozi kwa wanawake wengi nchini wanaonyanyaswa na taratibu za kimila zilizopitwa na wakati kwenye masuala ya ndoa, talaka, mirathi, umiliki wa ardhi, uasilia wa watoto na kadhalika.

  “Itakuwa mkombozi kwa wanyonge wote wakiwemo watoto yatima, wazee, wajane, walemavu na kadhalika, wanaodhulumiwa kwa kutokujua sheria na haki zao”.

  0 0

  Wajasiriamali toka vikundi mbalimbali mkoani Ruvuma wamehamasishwa kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ili kurahisisha matibabu wawapo katika shughuli zao za kawaida, Wajasiriamali watakaojiunga na mfuko huo na kuwa wanachama watalipia shilingi 76,800 kwa mwaka ili kupata matibabu kupitia mfuko huo.Attachments area Preview YouTube video Watanzania wametakiwa kujiunga na vikundi ili waweze kujiunga na bima ya afya NHIF


  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Ujumbe wake wamewasili nchini Zambia kwa ajili ya kufanya ziara ya kutembelea njia nzima ya Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi  la TAZAMA ili kukagua miundombinu yake pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa vituo vinavyotumika kusukuma mafuta hayo.

  Ziara hiyo ya kutembelea Mkuza wa Bomba inaanza rasmi leo Tarehe 27 Januari huko Ndola nchini Zambia na kumalizika Tarehe 31 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam..

  Ziara hiyo inafuatia makubaliano ya Marais wa nchi husika, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Edgar Lungu ya Tarehe 28 Novemba, 2016 kuhusu kuboresha Bomba hilo la TAZAMA kwa manufaa ya nchi zote mbili.

  Imeelezwa kuwa Ziara hiyo itafanyika kwa kufuata njia ya Mkuza kwa kupitia vituo vyote vinavyosukuma mafuta na baadaye kikao cha pamoja cha viongozi hao kitakachofanyika jijini Dar es Salaam. 

  Ziara hii imechagizwa pia na  ziara ya Rais Lungu  kwenye kituo cha TAZAMA Jijini Dar es Salaam ambapo ilielezwa kuwa ufanisi wa Bomba hilo umeshuka ikilinganishwa na hapo hapo awali kwani lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 1.1 za mafuta kwa mwaka lakini kwa sasa linasafirisha tani 600,000 tu.  

  Hivyo ili kuboresha miundombinu ya TAZAMA, nchi hizo zimekubaliana kushughulikia kwa pamoja chanzo cha kuzorota kwa utendaji kazi wa TAZAMA ili Bomba hilo liweze kuendeshwa kwa faida kwa kunufaisha pande zote mbili.

  Ziara  hiyo pia imelenga kufanya tathmini kwa kukagua Mkuza wa Bomba na maeneo yanayopendekezwa kujengwa bomba la kusafirisha Mafuta Safi (Finished Product) na Gesi Asilia kutoka Tanzania hadi Zambia kupitia njia ya Mkuza huo (wayleave) wa Bomba la TAZAMA.

  Imeelezwa kuwa ziara hiyo itafanywa kwa ushirikiano wa Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakiambatana na Makatibu wakuu, pamoja na viongozi waandamizi kutoka nchi zote mbili sambamba na uongozi wa TAZAMA.

  Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la TAZAMA linaloanzia nchini Tanzania hadi mji wa Ndola nchini Zambia lina urefu wa kilomita 1,710 na kipenyo cha inchi 8 hadi 12 na lilianza kazi Mwaka 1968.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza jambo alipowasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda Jijini Lusaka, Zambia. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia) na ujumbe wake kutoka Tanzania walipowasili Lusaka Nchini Zambia. Kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Zambia, Brigedia Jenerali Emelda Chola na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kutoka Tanzania, Profesa Justin Ntalikwa.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza jambo alipowasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda Jijini Lusaka, Zambia.  Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongozana na  Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma (kulia) alipowasili Jijini Lusaka, Zambia kwa ajili ya ziara ya kutembelea Bomba la TAZAMA.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amewaagiza wakurugenzi, waratibu wa Tasaf, watendaji wa kata, watendaji wa vijiji na wenyeviti wa vijiji Mkoani humo kuhakikisha kwamba haki inapatikana katika kufanya mchujo kwa zile kaya ambazo hazistahili kuingizwa katika mpango wa kuzinusuru kaya masikini (TASAF)

  Ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara yake ya siku ya nne katika wilaya za kalambo na Nkasi Mkoani humo kwa kuzitembelea kaya za walionufaika na mpango wa TASAF ambao bado wanaendelea kunufaika na wale ambao waliondolewa katika mpango huo baada ya kukosa vigezo na hatimae kutakiwa kurudisha pesa hizo.

  “nimezunguka nimebaini kuwa zoezi hili limekuwa likifanyika hovyo hovyo, hakuna umakini, hakuna usimamizi, hakuna ufuatiliaji, matokeo yake kwenye mradi wameingizwa watu wenye sifa na wasio na sifa, Wakurugenzi na waratibu wasimamie zoezi hili, wasiwaachie wenyeviti na watendaji wa vijiji peke yao katika hili,”

  Zelote Stephen alifanya ziara hiyo ili kujiridhisha kuwa kaya ambazo hazistahili kuingizwa katika mpango wa TASAF wanatendewa haki katika kuondolewa kwenye mpango huo lakini pia kujua sababu zilizopelekea kaya hizo kuingizwa kwenye mpango bila ya kuwa na vigezo na kuachwa kaya zenye vigezo.

  “Wale wote ambao hawana vigezo na kweli ionekane kwamba hawana vigezo vya kuwepo basi watolewe kwasababau sehemu zingine utakuta kwenye mpango huo wameingizwa wastaafu, mke wa mwalimu, mjumbe wa smc yumo humo humo, hii haifai,” Zelote alifafanua.

  Katika ziara yake hiyo iliyolenga kufuatilia mchujo wa kaya hizo, Zelote Stephen alibaini kuwa wakurugenzi pamoja na waratibu wa TASAF wilaya wanakosa umakini katika kuzifanya shughuli zao na hatimae kubaki maofisini kusubiri ripoti zitokazo vijijini bila ya kufuatilia kwa kina kwa kufika katika maeneo husika ili kujua hali halisi.

  “Mimi nina taarifa kwamba fedha za ufuatiliaji wa TASAF zikifika tu katika Ofisi ya Mkurugenzi, kama zimefika asubuhi basi mchana tu hakuna senti tano, zote zimeshanyanganyiwa na hatimae makusudio ya fedha zile hayatimii na ufuatiliaji haufanywi,” Alisisitiza.

  Nae mratibu wa TASAF Mkoa wa Rukwa, James Kapenulo aliongeza kuwa kaya zote ambazo zilinufaika na TASAF kwa kuwa na mashamba na nyumba nzuri ambazo kabla ya TASAF hawakuwa nazo, familia hizo ndio ziwe za mfano na ziendelee kuwezeshwa ili tathmini itakapokuja kufanywa ioneshe hali halisi ya mafanikio ya mpango huo.

  “Hatuwezi tukaendelea kuwaweka wale ambao wakipewa pesa za TASAF wanaishia kwenye vilabu vya pombe na kumuacha yule ambae akipewa pesa hizi ananunua kuku au mbuzi au bati na kuwapeleka watoto shuleni, hayo sio madhumuni ya mpango huu, huyu aliyefanikiwa baada ya TASAF ndiye ametoka weye umaskini.

  Naye mnufaika wa TASAF aliyetolewa kwenye mpango huo Mathias Mwanakatwe alimshukuru Mkuu wa wa Mkoa kwa kuweza kuliona hilo na kulishughulikia kabla hali haijawa mbaya zaidi kwa wale wananchi wenye wivu na chuki kwa wale waliofanikiwa kutokana na kuwepo kwa mpango huo wa TASAF.

  Kaya 550 mbazo hazistahili kuwepo katika mpango huo kwa Mkoa wa Rukwa.


  0 0

  Kampuni ya Bia ya Serengeti imewapatia Watanzania zaidi ya milioni mbili kote nchini maji safi na salama bure katika kipindi cha miaka sita iliyopita kupitia programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha.

  Kupitia programu yake inayofahamika kama Maji kwa Uhai, SBL imechimba visima vya kisasa 16 katika mikoa minane na kuwezesha jamii katika maeneo hayo kupata maji ya uhakika na salama.

  Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha alisema kwamba kampuni hiyo ya bia imejikita katika kupunguza uhaba wa maji katika maeneo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitaabika kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

  “SBL ina sera iliyojikita katika ustawi wa jamii yetu ambapo Maji ya Maisha ikiwa ni moja ya maeneo manne ya kipaumbele ambayo kampuni yetu imeyafafanua katika malengo yake ya kutoa msaada kijamii kwa jamii inamofanya shughuli zake, alisema Wanyancha akifafanua maeneo mengine ya kipaumbele kama Kutoa Stadi za Maisha, Mazingira Endelevu na Kuhamasisha Unywaji wa Kistaarabu.

  Wanyancha aliongeza kwamba kwa kutoa huduma ya maji ya uhakika katika jamii, SBL imewawezesha watu kutumia muda mwingi zaidi katika uzalishaji kuliko kusafiri umbali mrefu kutafuta maji.Aliongeza, “licha ya kuboresha afya za wakazi wa maeneo hayo, upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya jamii unahakikisha kuwa watoto hususani watoto wa kike wanaosoma shule wanapata muda mzuri wa kuhudhuria shuleni kwa uhuru zaidi bila usumbufu”.

  Mkurugenzi huyo wa Mahusiano alieleza kwamba mpango wa Maji ya Maisha kwa mwaka 2017 ni kuanzisha miradi zaidi katika maeneo ya Ngare Nairobi, wilayani Siha, Chang’ombe B wilayani Temeke (Dar es Salaam) na Karatu na Likamba katika mkoa wa Arusha ambapo miradi yote itawanufaisha wakazi zaidi ya 300,000.
   
  Moja ya mradi wa maji uliodhamiwa na kampuni ya Serengeti Breweries Limited uliozinduliwa mapema Novemba mwaka jana katika Kijiji cha Makanya wilayani Same katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha. 

  Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mradi wa maji ulioweza kuwafikia watanzania milioni 2 katika programu ya hisani ya kusaidia jamii inayoendeshwa na kampuni hiyo inayolenga kuboresha maisha katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema jana katika hoteli ya Morena Mkoani Dodoma. 

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala ameitaka mamlaka ya uhamiaji kuharakisha kufanyia Uchunguzi kwa kaya 180 ambazo zilibainika kuwa na baadhi ya wakuuu wa kaya wanadhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.

  Pia kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

  Kauli hiyo alitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga, ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Watanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

  Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo, iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

  Ndagala alisema kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitishwa na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa kuchukuliwa hatua .

  "Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache, moja wapo ni wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanatumia kunywea pombe, na mambo mengine. nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.
  MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,wakati Ndagala alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga
   MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,aliyenufaika na mradi wa Kaya Masikini wa TASAF,wakati  alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.
   Baadhi ya Wanakijiji cha Nyaronga wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.
  0 0


  *Ni wale waliohusika na upotevu wa sh. milioni 700

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi  Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo.

  Amesema zaidi ya sh. milioni 700 zilizopelekwa katika halmashauri kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

  “Mkuu wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua. Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200  na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ alisema.

  Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa  kufuatilia kiasi kingine cha sh milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili ya maendeleo ambazo nazo hazijulikani zilipo. “Tafuta waliohusika popote walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,”

  Mbali na kutoa agizo hilo kwa Mkuu wa Mkoa, pia Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inashirikiana nayo inafanya uchunguzi ili kubaini watu waliohusika na upotevu huo.Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali haitowavumilia watumishi wote wanaojihusisha na vitendo vya ubadhilifu wa fedha za umma, hivyo amewataka watumishi wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na maadili.

  Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma nchini kuacha tabia ya kudokoa fedha za maendeleo zinazopelekwa katika Halmashauri zao kwa sababu Serikali iko macho na itawashughulikia wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.Aidha, Waziri Mkuu alitoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazopelekwa kwenye maeneo yao na kuhakikisha zinatumika kama ilivyokusudiwa.

  Awali akiwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Michael Lameck alisema alimueleza Waziri Mkuu kwamba awali walikuwa wanapata maji ila kwa sasa hayatoki kutokana na uchakavu wa miundombinu hali iliyowafanya kuchangishana na kupata sh. milioni 95 kati ya 200 zinazohitajika.

  Kufuatia hali hiyo Waziri  Mkuu alimuagiza Mhandisi wa Maji wa Wilaya hiyo, Bw. Nasib Mlenge kwenda kijijini hapo leo  Januari 27 kukutana na Bw. Lameck ili kushirikiana naye na kuangalia alipofikia na kuendeleza uboreshaji wa miundombinu hiyo ili wananchi hao wapate maji.

  “Mwenyekiti amechangisha sh. milioni 95 na kununua baadhi ya vifaa nyinyi mnashindwa nini. Lazima muwe makini na matatizo ya wananchi na Serikali haitaki masuala ya urasimu. Watu wana shida ya maji na mnajua tatizo mmekaa tu,” alisema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  IJUMAA, JANUARI 27, 2017.
  Wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa wakilizuia gari la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakimtaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akienda mjini Ludewa kutoka mgodi wa chuma wa Liganga Januari 26, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alisimama na kuwahutubia.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Lusitu wilayani Ludewa walioziba barabara wakitaka asimame na kuwasalimia alipokuwa akitoka kwenye mgodi wa chuma wa Liganga kwenda mjini Ludewa Januari 26, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri, mjini Ludewa Januari 26, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amewakabidhi hati miliki 810 za ardhi kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga kilichipo Mkoani Iringa.

  Wananchi hawa wamekabidhiwa hati hizo za umiliki wa ardhi baada ya kupimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba wanayoyamiliki na kuandaliwa hati miliki ambazo walikabidhiwa na Waziri wa Ardhi Mheshimiwa William Lukuvi kijijini hapo.

  Katika tukio lingine Mheshimiwa William Lukuvi amezindua masijala ya ardhi ya kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa ili kuboresha huduma ya utoaji na uhifadhi wa hati miliki za ardhi.

  Akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho mara baada ya kuwakabidhi hati miliki zao za ardhi na kuzindua baraza hilo Waziri Lukuvi aliwasihi wananchi hao kuzihifadhi na kuzitunza hati zao hizo ili kuepukana na migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wengi wasio na hati miliki nchini.

  Nae Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) walioshirikiana na Serikali kuwezesha uandaaji wa hati miliki hizo Ndugu David Thompson amemshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi kwa kuja na kuwakabidhi Wananchi hati hizo na kuwaombaa Wananchi kuzitumia kwa maendeleo yao.
  Wakazi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoa wa Iringa wakiwa na hati zao za umiliki wa ardhi mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi (aliyevaa miwani) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) Ndugu David Thompson na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Richard Kasesela.
  Baadhi ya hati miliki za ardhi zikiwa zinaandaliwa ili kugawiwa kwa wananchi wa Kijiji cha Kinywang’anga Mkoani Iringa.
  Ndugu Yohanes Keng’ena na Mkewe Elizabeth Makang’olo wakipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.
  Bibi Catherine Abdallah akipokea hati miliki ya ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi.


  0 0

  Gari nne za kubebea wagonjwa na mbili za huduma zilizotolewa msaada na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Ulimwenguni (UNFPA) kwa ajili ya kutoa huduma katika Hospitali na vituo vya Afya Zanzibar zikiwa mbele ya Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Hashina Begum na Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo wakisaini makabidhiano ya magari manne ya kubebea wagonjwa na mawwili ya huduma yaliyotolewa na Shirika hilo katika sherehe zilizofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Dkt. Hashina akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya funguo za magari hayo kwenye sherehe zilizofanyika Wizarani kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA Dkt. Hashina Begum akilijaribu moja ya gari lilililotolewa msaada na UNFPA akwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Kaimu Muwakilishi wa UNFPA Tanzania Dkt. Hashina wakinyanyua moja ya vifaa tiba vilivyotolewa na UNFPA kwa ajili ya wodi ya mama wajawazito na watoto.

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo.

  0 0

   Diwani wa Kata ya Sandali, Abel Tarimo (wa pili kulia) akimkaribisha mgeni Rasmi ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilungule na Mkurugezi wa  Yamoto Bend, Said Fella (kulia) wakati akiwasili katika hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana kabla ya ufunguzi huo.
   Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo akizungumza jambo katika hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam jana.
   Diwani wa Kata ya Sandali,  Abel Tarimo (wa pili kushoto) akizungumza jambo wakati wa  hafla ya  ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto uliofanyika Kata ya Sandali Dar es Salaam  kabla ya ufunguzi huo  na kupata nafasi ya kumkaribisha mgeni rasmi, kuanzia kulia ni  Afisa Maendeleo Kata ya Sandali, Anuciatha Kayombo,  Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na kushoto ni Diwani ya Kata ya Kilungule, Said Fella
  Mgeni rasmi, Diwani ya Kata ya Kilungule Saidi Fella (kushoto) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa hafla ya ufunguzi wa Kampeni ya Tunaweza inayopinga ukatili wa wanawake na watoto, wakwanza kulia ni  Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo na  Diwani wa Kata ya Sandali,  Abel Tarimo
  Diwani Fella katika picha ya pamoja na kikundi cha ngoma cha Hisia Theater Group.


  0 0
 • 01/26/17--23:55: KUMBUKIZI ZA KUSHANGAZA
 • Enzo Ferrari ambaye ndiye mwanzilishi wa magari aina ya Ferrari. Anafanana SANA na Mchezaji wa mpira wa Arsenal  Mesut Ozil. Maajabu ni kwamba Enzo  alifariki Mwaka ambao ndio Ozil alizaliwa.

  0 0

  Katika kuitikia wito wa serikali ya Awamu ya Tano wa Kujenga Tanzania ya Viwanda, Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza (Corporation Sole) limeingia ubia na Mifuko ya Jamii ya PPF na NSSF wa kufufua kilichokuwa kiwanda cha Sukari kilichopo Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro.

  Kiwanda cha sukari cha Mbigiri kilisimamisha uzalishaji tangu mwaka 1996 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchakavu wa mitambo. Lakini kutokana na kuwa eneo zuri kimkakati yaani uwepo wa raslimali ardhi ya kutosha, nguvu kazi ya baadhi ya wataalam wa zamani wa kiwanda hicho, chanzo cha maji kuwezesha kuendesha kilimo cha umwagiliaji kumezishawishi taasisi zingine kushirikiana na Jeshi la Magereza kuwekeza katika eneo hili.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kukagua eneo la Uwekezaji, Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dkt. Juma Malewa amesema uwekezaji huu utakuwa na faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira, upatikanaji wa sukari ya kutosha nchini lakini pia wakulima wa eneo hilo watapata soko la uhakika la kuuza miwa katika kiwanda hicho.

  Aidha Kaimu Kamishna huyo ametoa wito kwa wananchi kutovamiwa maeneo ya majeshi kwani mengi yamehifadhiwa kwa shughuli za baadae zenye maslahi mapana kwa taifa.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio amesema matarajio yao ni kuona kiwanda kinaanza mapema iwezekanavyo hivyo, ametoa wito kwa wananchi wa maeneo jirani kuchangamkia fursa ya kulima zao la miwa kwa maana sasa watakuwa na uhakika wa soko lililo karibu nao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kyaharara amesema kuwa kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 30,000 kwa mwaka na kitahitaji tani 500,000 za miwa hivyo ni fursa nzuri kwa wananchi wa maeneo jirani.

  “Ni matarajio yetu kuwa kiwanda hiki kitaongeza ajira, kitainua uchumi kwa wafanyakazi na wanakijiji, tutapata wanachama wengi zaidi lakini pia tutakuwa tumeongeza uwezo wetu vizuri zaidi wa kuwahudumia wanachama wetu kupitia uwekezaji huu” Alihitimisha Prof. Kahyarara.
  Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye miwani) na ujumbe wake wakiwasili Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro jana tarehe 26.01.2017 tayari kwa kukagua eneo la uwekezaji wa Kilimo cha Miwa na Uzalishaji wa Sukari. Wa kwanza nyuma yake ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara, mshauri mwelekezi katika mradi huo ndugu Seleman Karanga akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa PPF ndugu William Erio.
  Ujumbe wa Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha Mbigiri kati ya Mifuko ya Jamii ya NSSF, PPF na Jeshi la Magereza kupitia Shirika la Magereza (Corporation Sole) wakikagua baadhi ya maeneo ya ndani ya kiwanda cha zamani cha sukari cha Gereza hilo kilichosimamisha uzalisha zaidi ya miaka 10 iliyopita.
  Ujumbe wa Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha Mbigiri kati ya Mifuko ya Jamii ya NSSF, PPF na Jeshi la Magereza wakipata maelezo kutoka kwa Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) Angolwise Pilla (wa pili kushoto) ambaye ni mfanyakazi wa zamani kilichokuwa kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri kilicho simamisha uzalisha zaidi ya miaka 10 iliyopita.
  Viongozi waandamizi kutoka Jeshi la Magereza, PPF na NSSF wakipata maelezo ya namna kiwanda cha sukari cha Gereza Mbigiri mkoani Morogoro kilivyokuwa kikifanya kazi kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa kiwanda hicho Mrakibu Msaidizi wa Magereza (ASP) Angolwise Pilla (wa nne kushoto). Viongonzi hao walitembelea kiwanda hicho jana ikiwa ni hatua za awali za uwekezaji wa ubia katika uzalishaji wa sukari nchini kati ya Taasisi hizo tatu.


  0 0

   Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wake na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo (katikati). Mkutano huo ulijadili masuala mbalimbali mojawapo ikiwa ni uboreshaji wa Bomba la Mafuta Ghafi la TAZAMA. Kushoto ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma.

   Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kushoto) akizungumza jambo Ikulu ya Zambia Jijini Lusaka mara baada ya kumaliza mkutano wake na Ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto kwake). Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Zambia, Balozi Grace Mujuma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Tanzania, Profesa Justin Ntalikwa.

   Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano uliofanyikia Ikulu ya Zambia.

  Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (wa tatu kushoto mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na Ujumbe kutoka Tanzania na Baadhi ya Mawaziri wa nchini Zambia.


  0 0

  Maonesho ya sanaa za uchoraji ya Wasanii 14 kutoka Tanzania yameanza rasmi tarehe 25 Januari 2017 kwenye ukumbi wa maonesho wa Village Market Nairobi.
  Watu waliotembelea maonesho hayo siku ya kwanza ni pamoja na Mabalozi na wadau mbalimbali wa sanaa kutoka Kenya na nchi za nje. Maonesho hayo yatachukua wiki mbili.
  Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Bi. Talha Mohamed Waziri (kulia) akimkaribisha Balozi wa Msumbiji kwenye maonesho hayo.
  Ofisa wa Ubalozi wa Venezuela Nairobi, Jose Gregorio Ayila Torres (katikati) akibadilishana mawazo na Kaimu Balozi wa Tanzania (kulia). Kushoto ni mmoja wa wasanii wa Tanzania, Raza Mohamed.
  Raia wa Uswisi waliofika kwenye maonesho.
  Wapenda sanaa wa Kenya wakikagua kazi za wasanii wa Tanzania
  Wadau wa sanaa wakifurahia maonesho hayo jijini Nairobi.

  0 0


  0 0

  Na Bashir Yakub. 

  Yafuatayo ni maneno/taarifa/maudhui ya msingi yanayotakiwa kuwa kwenye wosia . Taarifa yoyote kati ya hizi ni ya muhinu na inacho kitu cha msingi na cha kisheria inachosimamia na kulinda. Maana yake ni kuwa kukosekana kwake kutaathiri wosia wako kwa namna moja au nyingine.

  ( a ) Anza kwa kuandika kichwa( heading). Kichwa utaandika kawaida kama unavyoandika kichwa cha barua au taarifa nyinginezo. Mfano “WOSIA” au “ WOSIA WANGU MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI”, vyovyote kitakavyoandikwa muhimu kiwepo kichwa.

  ( b ) Kinachofuata baada ya kichwa ni sentensi muhimu sana. Ni sentensi inayolenga kuondoa utata mbeleni.

  Mfano ; “ HUU NI WOSIA WANGU NA WA MWISHO MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI”.

  Ni sentensi inayoazimia kuwa hakuna wosia mwingine baada ya huo. Ni sentensi inayolenga kufuta/kuondoa aina yoyote ghushi.

  ( c ) Kinachofuata ni kipengele ambapo mtoa wosia/mwandika wosia anajitambulisha kwa majina kamili, anuani na tarehe ya kutoa/kuandika wosia. Anuani ijieleze vizuri. Isiwe tu P.O. BOX… ikaishia hapo. Ieleze namba ya nyumba kama ipo, mtaa, kata, wilaya na mkoa. Na anuani nzuri ya kuweka ni ile ya pahala yalipo makazi yako ya kudumu wewe mtoa wosia. Ikiwa unayo makazi mawili ya kudumu kwa wale wa mitala basi chagua mojawapo.

  Mfano: “WOSIA HUU UMEANDIKWA LEO TAREHE 13 / 2 / 2017 NA MIMI PASCHAL STEVEN MUTIGANZI WA NYUMBA NAMBA 13 , MTAA WA MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA YA KINONDONI, MKOANI DAR ES SALAAM, wa S.L.P 100 .

  ( d ) Andika sentensi ya kuvunja wosia nyingine zilizopita. Hii ni pale ambapo umeandika wosia mpya na kufuta ule wa nyuma. Lakini hata kama haujawahi kuandika wosia ila sasa ndio unaanza basi hakuna ubaya pia ukiweka sentensi hiyo.

  Mfano ; “WOSIA HUU UNAFUTA WOSIA NYINGINE ZOTE NILIZOWAHI KUTOA/KUANDIKA HUKO NYUMA”.

  ( e ) Kinachofuata ni kipengele kinachotaja orodha ya mali ulizonazo. Habari si tu kutaja mali, bali pia ni kuzichambua mali hizo na kutaja pahala zilipo kila moja. Mali utazitaja kwa namba. Namba 1….2……3…..n.k. Mfano ; “JUMLA YA MALI NILIZONAZO NI, 1. NYUMBA NAMBA 13 , ILIYOPO MTAA WA MWINJUMA, KATA MWANAYAMALA , WILAYA YA KINONDONI, MKOANI DAR ES SALAAM. 2. GARI…..”( taarifa za gari au mashine yoyote zitajwe kama ilivyo kwenye kadi yake ya usajili)……( endelea kutaja mali )

  ( f ) Kinachofuata ni kipengele kinachotaja orodha ya warithi/wanufaika wa mirathi. Wataje kwa majina yao yote.
  Mfano; “WARITHI WANGU KATIKA WOSIA HUU NI 1………………………..2……………………………3…………………..”n.k.


older | 1 | .... | 1531 | 1532 | (Page 1533) | 1534 | 1535 | .... | 3272 | newer