Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1530 | 1531 | (Page 1532) | 1533 | 1534 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
  Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo mkoani Songwe.
  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
  Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi baada ya kutembelea mpaka wa Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (mwenye kitambaa cha pink) akisaidiwa kuvuna muhongo aliozawadiwa na mkulima wa kijiji cha Mwankonko Manispaa ya Singida Gideoin Itambu juzi alipofanya ziara katika Manispaa ya Singida kukagua shughuli za kilimo.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akikagua shamba la muhongo kwenye shamba la mkulima wa kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida Gideion Itambu juzi na kuagiza shule zote za Msingi na Sekondari Mkoani Singida kuhakikisha zinakuwa na shamba la muhongo lisilopungua ekari moja kwa ajili ya chakula cha wanafunzi na nusu ekari kwa ajili ya chakula cha walimu.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akipanda muhongo kwenye shamba la mkulima wa kijiji cha Mwankoko Manispaa ya Singida Gideon Itambu.

  0 0

  KAVAZI LA MWALIMU NYERERE linayo furaha kuwakumbusha Watanzania, Waafrika na wapenda haki na usawa duniani kwamba ifikapo tarehe 5 Februari 2017, Azimio la Arusha litakuwa limefikisha miaka hamsini, au nusu karne, tangu kuzaliwa kwake. Kama njia ya kuadhimisha miaka hamsini ya Azimio, KAVAZI limepanga kuandaa mazungumzo ya siku mbili, kuanzi tarehe 22 hadi 23 Februari mwaka huu. Mazungumzo hayo yatafanyika katika ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 9 alasiri. Mada kuu itakuwa: Simulizi za Azimio la Arusha.

  Azimio la Arusha lilikuwa waraka mojawapo wa kimapinduzi ulioandaliwa na kutekelezwa barani Afrika. Aidha, katika mazingira ya mapambano ya ukombozi ya wakati huo, Azimio liliwafarijisha na kuwatumainisha Waafrika kote duniani. Kama uhuru wa Ghana ulirejesha heshima ya Mwafrika, kama alivyosema C.L.R. James, mwanamajumui maarufu, basi Azimio lilikuwa ni matumaini ya mnyonge kujikomboa kutokana na makucha ya unyonyaji wa ndani na wa kibeberu. Kauli mbiu ifuatayo ya Azimio ilipokelewa kwa shangwe, ikawa wimbo wa kitabaka wa wavujasho:

  Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na wala tusipuuzwe tena.

  Kwa kulitumia Azimio kama dira na itikadi ya ukombozi na maendeleo, viongozi wa kisiasa wa kizazi cha kwanza, waliahidi na kudhamiria kwa dhati kujenga jamii na nchi ya kijamaa inayoheshimu na kulinda misingi ya usawa wa binadamu wote; isiyo na ubaguzi wa aina yoyote na isiyo na unyonyaji. Yaani nchi ya kijamaa, inayojitegemea, isiyo na matabaka ya wanyonyaji na wanyonywaji, au kwa maneno mengine, wavunajasho na wavujajasho

  Ni matarajio yetu kwamba mazungumzo hayo ya siku mbili ni fursa adhimu kwa washiriki kukumbushana kuhusu historia ya mapambano ya ukombozi na ujenzi wa taifa na bara lao. Aidha, washiriki watasimuliana, watajadiliana, watatafakari, watadadisi na kulichambua Azimio pamoja na kuainisha mafunzo yanayotokana na falsafa, itikadi pamoja na utekelezaji wake. Wote mnakaribishwa.

  Issa Shivji (Profesa)
  Mkurungezi, Kavazi la Mwalimu Nyerere, COSTECH

  0 0

  Three Reggae bands will perform at this year’s Sauti za Busara music festival under the banner of #AfricaUnited, suggesting that it’s high time music stakeholders take a second look at the power of Reggae as a genre on the continent.

  Among the 40 bands, Reggae vibes will reverberate with musician and activist Rocky Dawuni of Ghana, Sami Dan & Zewd Band of Ethiopia, and Bob Maghrib of Morocco.

  Sauti za Busara stands behind Reggae music’s well-known messages of unity, peace, love as well as challenging the status quo. After pouring over 600+ artist applications, Sauti za Busara’s decision to select three Reggae artists signals a challenge for young musicians and music managers to invest in Tanzania Reggae and expand their musical scope. 

  Festival director Yusuf Mahmoud explains, “These three Reggae artists are undoubtedly the some of the best African Reggae representatives on the continent. We’re confident many Tanzanians love Reggae not only for its rhythms but also for its messages of hope to all those who struggle for justice and freedom.”

  The music collective of Bob Maghrib was founded in 2011 as a tribute to the visionary Reggae artist Bob Marley. As a fusion band, the group melds Moroccan melodies with Reggae beats to create unique rhythms that honor linked African roots. 

  Legendary Rocky Dawuni has shared the stage with epic musicians Stevie Wonder, Peter Gabriel, Bono, Jason Mraz, Janelle Monae, John Legend, and others. Dawuni was named one of Africa’s Top 10 Global stars by CNN and his sounds unite a pan-African range of generations and cultures, weaving in Swahili lyrics in songs such as “Nairobi Nakupenda.”

  Sami Dan arrived on the music scene with a background in engineering and a youthful passion for music. Early experiences writing and performing songs in Form 5 and 6 convinced him to follow a musical path. He formed Zewd Acoustic Band in 2014 and he hasn’t looked back since. Songs like “Fikir Selam” or “Love, Peace” moves fans with its smooth grooves and message of peace and love above all. 

  Sauti za Busara, mentioned by CNN as one of 7 top African music festivals that are too good miss, will take place in Stone Town, Zanzibar between the 9th and 12th of February, 2017.
  More information: busaramusic.org

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yaleyale yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo, Maxence Melo.

  Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.

  Wakili wa serikali, Mohamed Salum alisema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao na waliamua kushindwakutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo.

  Hata hivyo upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
  Mpaka sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bondi ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.

   Maxence Melo akijaribu kumueleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
   Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao


  0 0  0 0

  Rais John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.  Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Mh. Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja.  Katika matembezi hayo Mhe. Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.

  Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria.  Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria


  Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.


   Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.


  Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)

  0 0

  Askari wa Usalama barabarani jijini Dar es salaam leo wamekamata gari aina ya NOAH ikiwa imebeba watoto 34 pamoja na mwalimu wao na kufanya jumla ya watu 35 katika gari Wanafunzi hao ni wa darasa la kwanza na pili kutoka shule za Diamond, Olympio, Kisutu, Maktaba na Bunge. Gari hiyo imekamatiwa eneo la mzunguko wa  Gerezani  likielekea Vijibweni-Kigamboni.Dereva na wahusika wa gari hiyo wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Msaidizi wa Waziri wa Nchi TAMISEMI Bi.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa Watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula (wapili kulia).
  Baadhi ya washiriki wa mkutano baina ya USAID na TAMISEMI uliofanyika katika ofisi za TAMISEMI jijini Dar es Salaam wakifuatilia hoja kutoka kwa wasilishaji wa mada leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Sekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Andrew Komba akichangia mada wakati wa mkutano baina ya TAMISEMI na USAID kuhusu Afya ya mama na motto leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay mara baada ya kumaliza mkutano kuhusu Afya ya Mama na Mtoto leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja washiriki wa mkutano baina ya TAMISEMI na USAID kuhusu Afya ya mama na mtoto leo jijini Dar es Salaam.Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID) nchini Tanzania Tim Donnay, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi la Shirika la Maendeleo la Taif (NDC), Samuel  Nyantahe baada ya kuwasili kwenye ueneo la mgodi wa Liganga wilayani Ludewa kukagua maendeleo ya  hatua muhimu zitakazowezesha kazi uchimbaji chumakuanza haraka.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Eric Mwingira kuhusu  sampuli ya chuma  kilichogunduliwa katika mgodi wa Liganga  wakati alipotembelea mgodi huo Januari 26, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mlima utaoelezewa na watalaamu kuwa uana hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea mgodi wa chuma wa Liganga wilayani Ludewa Januari 26, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea eneo lenye mlima anaoelezewa na watalaamu kuwa una hazina kubwa ya madini ya chuma wakati alipotembelea   mgodi  wa chuma wa Liganga wilaya Ludea Januari 26, 2017. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Samuel Nyantahe.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amewapongeza uongozi wa benki ya DCB kwa kuweza kuwasogezea huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" kwani kwa hatua hiyo ni wanakuwa miongoni mwa benki zinazoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia za kisasa.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya Sitta amesema kuwa kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki na zaidi anautaka uongozi wa bodi ya DCB kuongeza juhudi na ubunifu katika kuileteta mafanikio zaidi siku zijazo na kuendelza sifa nzuri iliyopatikana.

  Ameongeza na kusema kuwa, kuna changamoto ,mbalimbali katika sekta za kibenki zinakabiliana nazo ila ametoa ushauri kwa manispaa za Dar es salaam kutumia benki hiyo katika shughuli zao za kibenki ili kuiwezesha kupata amana za kudumu na zaidi amesisitiza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wataendelea kuwa mstari wa mbele kutumia DCB kwani wameweza kufaidika na gawio la kila mwaka.

  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka amemshukuru mstahiki  meya kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa huduma ya kipesa ya 'DCB Jirani' na "DCB Pesa" na kumshukuru kwa hatua nzuri ya Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kwa kukubali kupitisha mfuko wa mkopo ya  wanawake na vijana katika benki ya DCB.

  Msimbachaka ameziomba manispaa hizo kuleta fedha za asilimia 10 ya mapato yao zinazotengwa na kila manispaa kwa ajili ya mfuko huu ili benki iendelee na mpango wake wa kuwakopesha wajasiriamali kwa niaba yao.

  Akieleza kuhusiana na DCB Jirani, Msambichaka amesema kuwa kwa kutumia huduma hii ya kisasa wateja wa DCB wanaweza kufaidika kwa kupata huduma za kibenki katibu na mahala anapoishi bila kufuata tawi la benki hiyo, kwa upande wa DCB Pesa mteja ataweza kutumia simu kulipia huduma mbalimbali kama Dawasa, Luku, DSTV, kununua muda wa maongezi, kukopa mikopo midogo midogo kwa ajili ya kuendeleza biashara na pia wafanyakazi wataweza kutumia kwa kuomba nusu ya mshahara.

  Mbali na hilo, pia DCB waliweza kuwakabidhi zawadi zao wateja waliofanikiwa kushinda kwenye droo ya awali ya Kampeni ya kufungua na kuweka amana na DCB benki ambapo washindi 20 waliweza kukabidhiwa zawadi zao za Tshirt, wawili walikabidhiwa simu za mkononi aina ya Smartphone na wengine watatu walipatiwa ada ya shule kwa ajili ya watoto.

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (katikati) akikata utepe wa kuzindua  huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" sambamba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa (kushoto).
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta (kushoto) pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB Prof Lucian Msambichaka (katikati) wakizindua magari ya DCB Jirani na DCB Pesa  jana Jijini Dar es salaam, pembeni ni  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa.

  Wafanyakazi wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kindondoni Benjamin Sitta jana Jijini Dar es salaam.


  0 0


  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea rufaa kutoka Klabu ya Polisi Dar es Salaam dhidi ya Klabu ya Simba kuhusu kumchezesha Mchezaji Novalty Lufunga katika mchezo wao wa Raundi ya Tano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup 2017.

  Madai ya Polisi ni kwamba Mchezaji Novalty Lufunga alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Simba na Coastal Union katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup 2015/2016 uliofanyika Uwanja wa Taifa, Aprili 11, mwaka jana.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufaa hiyo kwa kukosa vigezo vya kikanuni katika uwasilishaji wake na hivyo kukosa sifa ya kusikilizwa. Hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 18 (1) na (2) ya Kanuni za Kombe la Shirikisho la Azam Sports HD.

  Kanuni ya 18 (1) inasema: “Malalamiko yoyote kuhusiana na mchezo yawasilishwe kwa maandishi kwa kamishna wa mchezo au TFF sio zaidi ya masaa sabini na mbili (72hrs) baada ya kumalizika mchezo.”

  Kanuni ya 18 (2) inasema: Ada ya malalamiko ni shilingi laki tatu (Tshs 300,000.00). Malalamiko yo yote yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada na kuwasilishwa nje ya muda uliowekwa hayatasikilizwa.”

  Hata hivyo, Shirikisho linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kadi nyekundu aliyopewa Mchezaji Novalty Lufunga katika mashindano ya Azam Sports Federation Cup 2016/2017.

  Kwa utaratibu wa mashindano haya ambayo ni ya mtoano, adhabu za kadi (njano na nyekundu) zitolewazo uwanjani, zinakoma mwisho wa msimu wa shindano husika isipokuwa kadi hizo zikiongezwa adhabu ya kinidhamu (suspension) ambayo itafahamisha kwa klabu na mchezaji kwa maandishi.

  Kadhalika, Kanuni ya 16 ya Kanuni za Kombe la Shirikisho Sehemu ya Tatu inaeleza wazi kuwa matumizi ya kanuni za ligi zitahusika maeneo yanayoruhusu uendeshaji wa shindano la mtoano.

  “Adhabu zote zinazohusisha katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam HD zitahusisha na shindano hili tu,” inasema kanuni ya 16 (3) na (4).


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

  Shindano la  wajasiliamali kwa vyuo vikuu mbalimbali nchini linategemea kuanza hivi karibuni likidhaminiwa na Benki ya Barclays nchini Tanzania.Kupitia benki hiyo kumezundiliwa mpango wake mpya wa udhamini kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mratibu wa mradi huo Victor Mnyawami amesema kuwa wataweza kuzunguka vyuo vikuu vyote kwa ajili ya kupata washindani.

  “ujasiliamali ni muhimu sana katika uchumi wa taifa hili hivyo ni vyema tukawa na wahitimu wa vyuo vikuu ambao wataweza kujitengenezea ajira zao wenye kuliko kusubiri kuajiriwa” amesema Mnyawami.

  Kwa upande wake afisa uhusiano wa Barclays, Hellen Siria amesema kuwa mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kuungana na vijana wengine kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini ujerumani.

  Hellen amesema kuwa vijana watakaopata fursa ya kupita kwenye mchujo watapata nafasi ya kupata mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia kujiajiri.
   Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la  wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na shindano hilo.
   Meneja uhusiano wa Benki ya Barclays nchini, Hellen Siria  wakijadiliana jambo na  Kiongozi wa Taasisi inayoandaa shindano la  wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini, Victor Mnyawami kuhusu mchango wa Bank hiyo katika kusaidia jamii hasa wanavyuo. 
   Meneja uhusiano wa Benki ya Barclays nchini, Hellen Siria  akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya udhamini wa benki ya Barclays kuhusu shindano la wajasiliamali kutoka vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

  0 0


  Taarifa kuhusu Mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi, Tuzo za AU kwa SSRA na TRA na Mkutano wa AU-Addis Ababa

  Mkutano wa Nne wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi umepangwa kufanyika mjini Lilongwe, Malawi tarehe 03 hadi 05 Febuari 2017. Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalamu wa sekta mbalimbali kutoka Tanzania na Malawi.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb), anategemewa kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo. Aidha, Uongozi wa Mkoa wa Mbeya ambao umekuwa ukishiriki katika vikao vya maandalizi, unategemewa kushiriki katika mkutano huo.

  Lengo la mkutano huu ni kujadili na kutathmini hatua zilizofikiwa katika utekelezwaji wa makubaliano yaliyofikiwa katika Mkutano wa Tatu wa JPCC uliofanyika Tanzania, tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003.

  Miongoni mwa mafanikio yaliyofikiwa kwenye utekelezaji wa makubaliano ya mikutano iliyopita kwa upande wa Tanzania ni pamoja na; Kuanzishwa kwa mradi wa Kituo cha Huduma za Pamoja Mipakani (One Stop Border Post – OSBP) katika mpaka wa Kasumulu/Songwe ambao umefikia katika hatua nzuri; Idara za Uhamiaji, Polisi na Forodha za nchi zetu mbili zinaendelea kushirikiana katika kutoa huduma na kudhibiti abiria na mizigo katika maeneo ya mpakani.

  Pia, Mamlaka ya Bandari Tanzania imeruhusu Mamlaka za Malawi kuwa na maeneo yao katika bandari zetu, kwa ajili ya kuhifadhia mizigo na bidhaa nyingine zinazopitia nchini kabla ya kwenda Malawi. 

  Aidha, mkutano huo utatoa fursa kwa nchi zetu mbili kujadiliana na kukubaliana kuhusu maeneo mapya ya ushirikiano. Miongoni mwa maeneo hayo (kwa upande wa Tanzania) ni pamoja na: Kuanzisha ushirikiano katika sekta ya usafiri wa majini, ambapo mbali na faida za kiuchumi, safari hizo zitaimarisha mwingiliano wa watu na kupunguza tofauti zilizopo. Kwa hivi sasa Serikali inajenga meli tatu, mbili kwa ajili ya kusafirisha mizigo na moja kwa ajili ya abiria. 

  Maeneo mengine ni kuanzisha Mkataba wa ushirikiano katika Sekta ya Usafiri wa Anga (BASA); Kuanzisha mfumo wa kurahisisha ufanyaji biashara kwa ajili ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo hasa katika maeneo ya mpakani; Kuanzisha ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira na masuala ya afya ikiwemo magonjwa ya mlipuko hususan maeneo ya mipakani; na Kuanzisha ushirikiano katika sekta ya elimu ya vyuo vikuu na vyuo vingine vya amali.

  Tangu kuanzishwa kwa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi nchi hizi mbili zimeshafanya vikao vinne vya Tume hiyo. Kikao cha mwisho kilifanyika hapa Dar es Salaam, Tanzania tarehe 24 hadi 30 Juni, 2003 na kuhudhuriwa na viongozi na wataalam wa sekta mbalimbali kutoka nchi zetu mbili.
  Bi Mindi akimkabidhi Bi. Sarah kombe la ushindi kwa niaba ya Wizara. Bi. Kibonde aliipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. 
  Meneja wa Mradi wa Mfumo wa Forodha wa TANCIS kutoka TRA akipokea zawadi ya cheti cha ushindi kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga. 
  Picha ya pamoja ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, TRA na SSRA.


  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akifungua maonesho ya siku mbili ya kimataifa unaofanyika kwenye viwanja vya taasisi ya Utafiti wa Kilimo Selian(Sari)jijini Arusha.

  Mtaalamu wa Mawasiliano wa taasisi ya Agriculture Markets Development Trust(AMDT),Al-amani Mutarubukwa(kulia)akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kulia)kuhusu taasisi hiyo inayowajengea uwezo wakulima katika mazao ya Ufuta na Mahindi katika mikoa mbalimbali nchini. 
  Meneja wa Kampuni ya Monsanto nchini,Frank Wenga(kulia)akizungumza na wakulima waliofika kwenye maonesho hayo kujifunza mbinu za kilimo chenye tija. 
  Wakulima wakipata maelezo kutoka kwa wataalamu namna ya kupata mazao bora .


  0 0


  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali lazima ijiridhishe ni kwa namna gani itafaidika na uwekezaji katika miradi ya makaa ya mawe na chuma kabla haijaanza.

  Amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za mazungumzo na muwekezaji kabla ya kuanza uzalishaji kwenye miradi ya makaa ya mawe ya Mchuchuma na chuma cha Liganga.

  Miradi hiyo inatekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Ltd (SHG) ya China. Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Januari 26, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundindi baada ya kukagua eneo la mradi wa chuma cha Liganga.

  “Madini haya yana viwango vya juu vya ubora, hivyo ni lazima tuwe makini kabla ya kuanza kwa uzalishaji wake. Kwani chuma chetu ni bora na tutachimba kwa zaidi ya miaka 50,”. “Hivyo maeneo haya ni nyeti na lazima Serikali ijipange vizuri na kujiridhisha kama vipengele vyote vya mkataba vimetengamaa ndipo mradi huo uanze,” amesema.

  Hata hivyo amesema mradi huo hautachukua muda mrefu utaanza hivyo wananchi wawe na subira. “Hatutaki kusikia tena suala la mikataba mibovu tunataka mikataba itakayoleta tija. Akizungumzia suala la fidia kwa wananchi wanaopisha mradi, amesema kabla haujaanza lazima walipwe fidia zao na tayari fedha zipo muwekezaji anasubiri ruhusa ya Serikali.

  Amesema kuna baadhi ya watu wamejipenyeza na kutaka kuiibia Serikali kupitia suala la ulipaji wa fidia. Serikali haiko tayari kuona wananchi hao wakitumika kama madaraja ya wizi. Waziri Mkuu amesema watu hao ambao hawahusiki na eneo hilo wamesababisha gharama za fidia kuwa kubwa, hivyo wataalam wanatathmini ili kubaini wahusika kabla ya kulipa.

  “Tunataka wananchi wenyewe waliokuwa hapa ndiyo tuwalipe fidia yao kwa mujibu wa tathmini husika. Fidia yenu mtalipwa baada ya kuwaondoa wezi wote waliojipenyeza. “Kuna watu wanataka kuiibia Serikali kwa mgongo wenu, hili hatutakubaliana nalo. Tupo makini vumilieni inalifanyia kazi suala letu. Hakuna haki ya mtu itakayopotea,” amesema.

  Naye Naibu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd (TCIMRL) Bw. Eric Mwingira amesema miradi ya Liganga na Mchuchuma inatekelezwa kwa mfumo unganishi ambayo ina vipengele vitano kikiwemo cha mgodi wa chuma cha Liganga.

  Amesema mgodi huo wa chuma una uwezo wa kuzalisha tani milioni 2.9 kwa mwaka huku kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma Liganga kitazalisha tani milioni 1.1 kwa mwaka. Bw. Mwingira amesema kipengele kingine ni mgodi wa makaa ya mawe Mchuchuma wenye uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka.

  “Kipengele cha nne ni kituo cha kufua umeme cha megawati 600 huko Mchuchuma. Kati ya hizo megawati 250 zitatumika Liganga katika kuchenjua na kuzalisha chuma cha pua na megawati nyingine 350 zitaingizwa kwenye msongo wa Taifa ili kuiuzia TANESCO,” amesema.
   

  Pia kutakuwa na njia ya msongo wa umeme wa kilowati 220 kati ya Mchuchuma na Liganga na barabara ya mkato kutoka Mchuchuma hadi Liganga.

  Amesema gharama za uwekezaji katika mradi huo unganishi ni Dola bilioni tatu, ambapo dola milioni 600 ni mtaji wa muwekezaji na mkopo utakuwa dola bilioni 2.4. Awali Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Deo Ngalawa alimuomba Waziri Mkuu kuwaeleza wananchi hao ni lini watalipwa fidia za kupisha mradi wa chuma Liganga na mradi huo utaanza lini.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU, ALHAMISI, JANUARI 26, 2017.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul  Makonda amekutana  na Umoja wa Madereva Tax Wilaya ya Ilala ilikusikiliza  kero zao zinazowakabili katika kazi yao.

  Makonda ameyasema hayo leo alipokutana na madereva hao, amesema kunahitaji madereva wa tax kuwa mfumo bora wa kusaidia jiji la Dar es Salaam kuwa na huduma bora ya usafiri wa tax na wenye usalama

  Amesema ni vyema kukawepo kifaa maalum kitakachoonesha umbali wa mteja anapokwenda ili alipe kulingana na umbali huo na ajue bei hiyo kuliko kukadiriana, pia amesema katika kufanikisha hayo serikali yake itaziondoa Tax bubu zote, na utaratibu wa kuweka rangi na namba kwenye magari utarudi ili Tax zote zitambulike.

  Aidha amesema madereva wa tax kutoa taarifa za matukio ya kiharifu pale wanapohisi abiria waliyempakia ni mtu wa kufanya matukio ya kialifu.
   Makonda amesema wakitoa taarifa za uhalifu watalisaidia Taifa kuwa katika hali ya usalama, huku akiwataka ndani ya wiki moja wakae wajadiliane waje na mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote.

  Makamu Mwenyekiti wa Madereva  mkoa wa Dar es Salaam, Jacob Anyandwile amesema madereva hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutozwa kodi kubwa na Mamlaka ya mapato nchini (TRA) pamoja na uwepo wa huduma ya Tax kwa njia ya mtandao unafanywa na kampuni ya UBA ambayo  imechangia kuharibu  soko ya usafiri huo.
  Amesema kampuni ya UBA inatoza bei ndogo zaidi, pia gharama za uendeshaji hazilingani wanajikuta wao wanalipa kodi kubwa zaidi kuliko kampuni hiyo.

  Katibu Mkuu wa Umoja huo Ramadhani Ashiru ameeleza kuwa kampuni hiyo ya UBA inatumia Tax bubu ambazo hazitambuliki kisheria.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza  na Umoja wa Madereva Tax na kusikiliza kero zao, ,leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Wamiliki wa Tax Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Ashiru akifafanua jambo katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZTO) ACP Awadhi Haji akitoa elimu kwa madereva wa Madereva Tax leo jijini Dar es Salaam.

  Mkutano ukiendelea

  0 0  Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli.
  Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka Waandishi waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  Baada ya kutoka na ushindi dhidi ya Cosmo Politan wa magoli  3-1 na kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la FA, Klabu ya Azam , Jumamosi itakuwa kibaruani kuvaana na Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 

  Tayari kikosi cha Azam  kimeanza rasmi mazoezi juzi jioni kwa ajili ya kujiandaa na mtanange huo unaotarajiwa kuwa ni wa kisasi kwa pande zote mbili kutokana na aina ya matokeo yaliyotokea katika mechi zao za mwisho walizokutana msimu huu.

  Wakati matajiri hao wa Azam Complex wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, Simba nayo itataka kupooza machungu ya kufungwa na Azam FC kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi (1-0) Januari 13 mwaka huu.

  Kocha Mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba aliingia na mbinu mpya za kuweka fedha mezani ili kuwapa motisha wachezaji wake kufanya mazoezi kwa nguvu ambapo aliwagawa katika makundi manne ya wachezaji sita na kuanza kuwashindanisha.


   Cioaba anatarajiwa kuwa katika benchi la ufundi la Azam katika mchezo huo wa Jumamosi dhidi ya Simba huku akitaka kuweka rekodi ya kutokupoteza mechi hiyo muhimu.


  Kuelekea mchezo huo, manahodha wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ na Shomari Kapombe, wametoa neno kwa upande wa wachezaji wenzao namna walivyojithatiti kuibuka na pointi zote tatu dhidi ya wapinzani wao hao.

  “Tukikutana na Simba tunakuwa tunacheza mpira wa kujuana na pia wa kuogopana, lakini naamini ni mechi ngumu, watakuwa na mipango yao na sisi tutajipanga kwa upande wetu, naamini tutajituma na tutaweza kupata ushindi,” alisema nyota huyo.

  Bocco ataingia kwenye mchezo huo akiwa na rekodi ya aina yake ya kuifunga mabao mengi Simba kuliko mchezaji mwingine yoyote kihistoria, akiwa tayari ameshaziona nyavu zao mara 18 katika mechi za mashindano mbalimbali.


  0 0

  Ujumbe wa watu watano kutoka Chuo Kikuu cha Tiba cha Minnesota kutoka nchini Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendajji wa hospitali hiyo, Profesa  Lawrence Museru.

  Ujumbe huo umeongozwa  na Mkuu wa masuala ya utafiti  katika Idara ya Magonjwa ya dharura kutoka Chuo hicho,  Profesa Michelle Biros .

  Katika mazungumzo hayo Profesa Museru ameuleza ujumbe huo mikakati na malengo mbalimbali ambayo MNH inafanya katika kuhakikisha huduma za kibingwa zinafanyika nchini ikiwa ni pamoja na upandikizaji wa figo, kuweka kifaa maalum cha usikivu  na kuongeza wodi kwa ajili ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum.

  Kwa mujibu wa Profesa Museru, MNH inakabiliwa na changamoto ya wataalam  katika baadhi ya maeneo ikiwamo ICU.

  Maeneo waliotembelea ni  Idara ya Magonjwa ya  dharura na Ajali, Idara ya Mionzi, Mwaisela -wodi moja, Jengo la watoto na Jengo la wazazi namba mbili -Wodi 35.
   Mmoja wa msimamizi wa wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu wa hospitali hiyo, Trustworthy Majuta akifafanua jambo wa ujumbe huo leo.
   Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa Nje, Dk Raymond Mwenesano akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo leo. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).


older | 1 | .... | 1530 | 1531 | (Page 1532) | 1533 | 1534 | .... | 3272 | newer