Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1532 | 1533 | (Page 1534) | 1535 | 1536 | .... | 3272 | newer

  0 0  0 0
  0 0


  0 0

  Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) nchini Somalia.

  Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

  "Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameliambia shirika la habari la Reuters.

  Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.

  Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."

  Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.

  Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

  Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.

  Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh. Amos Makalla akizungumza na wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwa ni utaratibu wake wa kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa mbeya kila Alhamis ya mwanzo na mwisho mwa mwezi na jana Alhamis ya Tarehe 26 ya mwezi Januari amekutana na baadhi ya wananchi wa watokao maeneo tofauti mkoani Mbeya na kueleza kero zao na kutatuliwa papo kwa papo na idara husika.PICHA NA MR PENGO-MMG MBEYA
  Bi. Fidea Lukas Mwakanyamale akitoa kero kwa mkuu wa mkoa kuhusu  jinsi alivyo mwagiwa tindikali na muajili wake Wilayani Chunya mkoa wa Mbeya..
   Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mbeya wakitua kero zao mbele ya mkuu wa mkoa alipokutana na wananchi hao
    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akitolea majibu maswali pamoja na hoja za wananchi waliofika kuwasilisha kero zao kwa mkuu wa mkoa huyo katika ukumbi mdogo wa Mkapa jijini Mbeya.
   Baadhi ya wananchi na wadau wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mkuu wa Mkoa alipokuwa akijibu hoja za wananchi kwenye ukumbi mdogo wa Mkapa jijini Mbeya .
  Mkutano ukiendelea

  0 0
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen akitoa taarifa ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), wakati wa ziara ya Naibu Waziri kutembelea idara zilizopo chini ya wizara yake.
  Naibu Waziri wa Wizar ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisindikizwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Stephen mara baada ya kumaliza kupokea taarifa ya mkoa na ya vyombo vya usalama wa mkoa huo wakati wa ziara ya kikazi mkoani hapo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza mkoa wa Rukwa kwa ziara ya kikazi.Kulia ni wakuu wa jeshi hilo mkoani hapo wakimsikiliza.
  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi Selemani Kameya akisoma taarifa ya utendaji kazi ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP George Kyando akizungumzia Mradi wa Ujenzi wa ofisi wakati Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea jengo hilo kuona maendeleo ya mradi huo na kuwataka kutumia rasilimali watu ya wafungwa waliopo mkoani hapo ili kuweza kukamilisha ujenzi huo wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani hapo.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea risala kutoka kwa askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Rukwa aliyoisoma kwa niaba ya wenzake ikiwa na maombi mbalimbali yaliyoelekezwa kwa wizara.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simiyu, Paul Mzindakaya baada ya kumaliza kupokea taarifa ya hali ya usalama mkoani Rukwa wakati Naibu Waziri alipokuwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0

  Uwanja wa Taifa.  0 0

  Ikulu ya Marekani imesema Rais wa nchi hiyo Donald Trump anaweza kutoza asilimia 20 ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Mexico ili kuweza kusaidia mpango wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili kuzuia kuingia kwa Wahamiaji haramu na madawa ya kulevya.

  Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena Nieto kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini Washington.

  Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia mtangulizi wake Vicente Fox.

  Bwana Fox amesema ana uhakika Mexico italipiza kisasi kwa kutoza kodi bidhaa zitokazo Marekani, iwapo mipango hiyo ya Rais Trump itatimizwa.

  Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump.

  Katika ziara yake nchini Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.

  Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia.

  0 0


  0 0

  Mradi umeandaliwa na AMREF shirika lisilo la kiserikali,umezinduliwa Wilayani Handeni katika ukumbi wa Kanisa la KKT na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe. Kuzinduliwa kwa mradi huo kumekuja Kufuatiwa kuwepo kwa jamii nyingi za wafugaji na jamii nyingine za kawaida zinazodumisha Mila potofu ya ukeketaji wa watoto na wanawake bila kutambua athari wanazokumbana nazo walengwa. Tathmini iliyofanyika imeonesha Asilimia 70% ya wafugaji wanafanya ukeketaji na 30% ni jamii ya kawaida ambayo inadumisha mila hizo.

  Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Mhe. Gondwe alisema kuwa jamii hazikatazwi kudumisha mila na kufanya sherehe za kimila, lakini serikali na jamii kwa ujumla haitakuwa tayari kuona tamaduni potofu kama ya Ukeketaji inaendelea kukumbatiwa na kuathiri watoto na wanawake wa Wilaya Handeni.”

  Aliongeza kuwa Vitendo vya ukeketaji vinamuathiri mtoto kisaikolojia ,kiafya, kiuchumi na Kielimu, hali inayopelekea utoro uliokithiri shuleni na watoto wengi kutomaliza shule na kuolewa katika umri mdogo , kutokana na mazingira wanayojengewa na mangariba wakiwa kwenye sherehe hizo za kiutamaduni.

  Mhe. Gondwe alieleza kuwa mradi huu ambao AMREF wameuleta kwetu tuna wajibu wa kuumiliki, kuufanya wa kwetu na endelevu hata baada ya mwaka mmoja kufika ukomo . Alieleza kuwa Kila mtoto anahaki ya kuishi na kupata haki zake za msingi ikiwemo elimu kama mtoto mwingine na kwamba jamii nzima ya Handeni iungane na kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya vitongoji hadi Halmashauri kwa shirika la AMREF kuondokana na vitendo hivyo kutoka 14% iliyopo sasa hadi 0%.

  Akielezea muundo mzima wa mradi huo, Dokta Aisha Bianaku Meneja wa Mradi alisema kuwa, Mradi huo wameamua kuuleta Handeni baada ya kufanya tahmini na kuona kwamba katika mkoa wa Tanga ikitoka wilaya ya Kilindi, Handeni ni wilaya inayofuata kwa kushiriki vitendo hivi vya ukeketaji. Alisema kuwa kata tano ndizo zitakazopewa elimu na kutoa njia mbadala kwa mangariba ambao wamechukulia kukeketa ni njia mojawapo ya wao ya kujipatia kipato.

  Elimu itatolewa kuanzia shuleni kwa waalimu na wanafunzi, mitaani , kwa viongozi wa kata na vitongoji, matabibu wa vituo vya afya, morani na wazee wenye ushawishi mkubwa katika jamii. 

  Alisema kuwa lengo ni kuwaelimisha madhara ya vitendo vya ukeketaji na kuondoa kabisa desturi hii ambayo inamadhara makubwa ya kiafya na kielimu kwa ujumla kwa watoto na wanawake hasa wakati wa kujifungua. Akaongeza kuwa AMREF imeona ni vyema kutumia jamii zetu kuleta mabadiliko katika jamii.

  Mradi huu umedhaminiwa na mdhamini anayejulikana kwa jina la Sternstunden chini ya shirika la AMREF GERMAN ili kuongezea nguvu mradi wa kupinga ukeketaji ambao kwa awamu ya kwanza utafanyika kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari 1/2017 hadi Desemba 31/2017. Kata zitakazonufaika na mradi huu kutokana na tathimini ya uwepo wa jamii ya wafugaji wengi na kukithiri kwa tamaduni hii ya ukeketaji ni pamoja na Segera, Malezi, Konje, Kwamagome na Ndolwa ambapo kiasi cha uro 176,634.22 sawa na milioni miatatu za kitanzania zitatumika kutekeleza mradi huo.

  Alda Sadango
  Afisa Habari
  Halmashauri ya Wilaya Handeni.
    Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Godwin Gondwe akizungumza na wakuu wataalamu wa Wilaya ya Handeni wakati wa uzinduzi huo.
    Baadhi ya wataalamu wa Wilaya ya Handeni walioshiriki uzinduzi huo.

   Kamati ya ulinzi na usalama  wakimsikiliza  Mhe. Mkuu wa Wilaya kwenye ufunguzi wa mradi huo.
  Daktari Aisha Bianaku ambaye pia ni mratibu wa mradi  akiwaelezea wataalamu kuhusu mradi na mikakati iliyowekwa kuwafikia walengwa.
  Bw. Henry Bendera mwezeshaji wa mradi kutoka AMREF akizungumza wakati wa uzinduzi huo. 
   Daktari Sarafina Mkua Mratibu wa afya ya uzazi kwa mama na mtoto AMREF kitaifa akielezea baadhi ya athari za ukeketaji. 


  0 0
 • 01/27/17--03:06: BEI YA MDAFU YA LEO


 • 0 0


  Na.Vero Ignatus,Arusha.

  Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)imewataka wakulima kubadilisha kilimo kuwa biashara ,waondokane na kilimo cha kawaida na kuwa na kilimo cha kisasa na kufahamu kilimo mkataba.

  Hayo yamesemwa na meneja mradi Martin Mgallah alipokuwa katika maonyesho ya zana za kilimo Jijini Arusha na kusema kuwa wametenga zaidi ya dola za kimarekani milioni kumi na tano kwaajili ya kuwawezesha wakulima katika zao la Alizeti pekee ndani ya miaka mitano (2016-2021)

  “Taasisi itamuwezesha mkulima kuongeza kipato chake cha mwaka kwa kubadilisha kilimo kuwa biashara,tunaangalia pia mfumo wa masoko,tunamuwezesha mkulima kufahamu kilimo mkataba yaani akishalima na kuvuna mazao yake asihangaike tena kutafuta soko bali atauza mazao yake kwa bei nzuri,tunamuunganisha na soko moja kwa moja”alisema meneja mradi Martin.

  Amesema kuwa wakulima zaidi ya 60,000 watanufaika na mradi huo,huku akianisha mikoa ambayo wataanza nayo ambayo ni pamoja na Manyara,Shinyanga,Singida,Dodoma,Iringa,Njombe,Mbeya Songwe ,Katavi,Lindi,Rukwa na Mtwara.

  Martin amesema kuwa lengo kubwa la( AMDT) kuhakikisha kuwa mkulima anazalisha kilicho bora ,amesema mazao ambayo wataanza nayo ni Alizeti,mahindi,na jamii ya mikundekunde katika mikoa tajwa.

  Aidha amesema kwaba wanampatia mkulima elimu sahihi,namna ya kulima kilimo cha kisasa,kumuelimisha mkulima kuwa na bima itakayomuwezesha kupata nyezo za kisasa za kilimo hivyo amewataka wakulima kuwatembelea ili waone ni kwa namna gani wanaweza kunufaika na program hii.

  Pichan ni Martin Mgallah ambaye ni Meneja mradi wa Taasisi ya kuendeleza mifumo ya kimasoko katika kilimo Tanzania (AMDT)Picha na Vero Ign atus Blog 27januari2017.
  Wakwanza kushoto ni akiyevaa tshirt nyekundu ni Hellen Wakuganda kutoka Asasi ya kusaidia sekta binafsi ya kilimo(PASS)akifuatiwa na aliyepo katikati Al-Amani Mutarubukwa kutoka (AMDT)akifuatiwa na Juliana Nganyangwa kutoka (AMDT)wakitoa elimu kwa wakulima Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.27 january 2017.

  0 0

  Shirika la Umoja wa Mataifa nchini limeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi kwa kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na kuwapa elimu kuhusu maangamizi hayo.

   Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alisema ni jambo jema kwa wanafunzi hao kupata elimu kuhusu maangamizi ambayo yalifanywa na kiongozi wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler kwani hata wao wanaweza kuja kuwa viongozi kwa miaka ijayo hivyo kama watapatiwa elimu mapema watajifunza ni mambo gani kiongozi anapaswa kufanya na yapi hapaswi kwa faida ya kila mmoja. 

  “Kwa nyie kama wanafunzi ambao kwa miaka ya baadae wengine mtakuwa viongozi mnapaswa kujifunza kwa jambo kama hili ambalo alifanya Hitler kuwa sio jambo jema, kila binadamu ana haki sawa hakuna ambaye anamshinda mwenzake na huo ndiyo msimamo wa Umoja wa Mataifa,” alisema Vuzo. 
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi kutoka shule ya Chang'ombe, Kibasila, Jitegemee, Kigamboni, Dar es Salaam, Gerezani, Airwing na vijana kutoka Temeke Youth Development Network (TEYODEN) kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto ambapo watu mil. 55 wanakadiriwa kuwa walipoteza maisha. (Picha na Rabi Hume - MO Dewji Blog)

  Aidha Afisa Habari huyo alizungumza kuhusu siku mauaji ambayo yalifanywa na Hitler wakati akiwa kiongozi wa Ujerumani katika kipindi cha mwaka 1933 hadi 1939, “Alikuwa akichagua watu ambao wanaonekana kuwa tofauti na kuwaondoa katika jamii ya Wajerumani, anawapeleka katika kambi maalumu na anawaua wengine wanawekwa katika kambi maalumu wanafanyishwa kazi ngumu bila malipo na waliokuwa wanashindwa na wao wanauawa kwa kuchomwa moto hadi kufa, 

  Vuzo aliongeza kwa kusema kuwa, “Mauaji ya moto ni mauaji hatari kuwahi kutokea duniani, ilikuwa ni dhana ya Adolf Hitler kutaka Wanazi kuwa ni watu ambao wamenyoka lakini kumbe ilitakiwa aishi na watu wote katika jamii lakini alipinga hilo,” “Lakini pia alikuwa hawapendi Wayahudi, walikuwa wafanyabiashara wazuri lakini yeye aliwapinga na hata akawa anawambia wananchi wake kuwa Wayahudi kuwa hawafai katika jamii na wasinunue kitu chochote kutoka kwao.” 
  Afisa Habari wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Susann Keller akizungumza kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kuadhimisha na Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto.

  Kwa upande wa Afisa Habari wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Susann Keller alisema kitendo ambacho kilifanywa na Hitler hakikubaliki na ni jambo ambalo Wajerumani wamekuwa wakijutia kila muda kutokana na vitendo vya kikatili ambavyo vilifanyika vilivyosababisha watu wanaokadiriwa kufikia milioni 55 na kati yao milioni sita wakiwa ni Wayahudi kupoteza maisha. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Elimu kwa ajili ya maisha Bora ya Baadae.” .

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi Miembeni
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akimkabidhi mifuko mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya miembeni, Kuruthumu Hamisi


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
  Katika kutekeleza sera ya elimu bure Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti , Omary Kumbilamoto amekabidhi mifuko 12 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Miembeni.

  Kumbilamoto amesema kuwa mifuko hiyo ya saruji ni kwa ajili ya ujenzi wa  sakafu ya madarasa mawili ambayo yamekamilika lakini yalikuwa ayana sakafu.
  “mimi nilipita hapa nikafanya ziara na kujionea mapungufu yaliyopo katika ujenzi wa madarasa haya ambayo yalianza kujengwa na kamati ya maendeleo ya shule kwa kushirikiana na wananchi hivyo nimeona nichangie hii mifuko 12 ya Saruji”

  Kumbilamoto amewashukuru wananchi waliofika katika hafla hiyo kwani wameweza kujichangisha  na kupata shilingi laki mojana ishirini ambazo zitaweza kununulia mchanga wa kujengea.Ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuweza kusaidia maendeleo ya elimu katika kata ya vingunguti.
  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Hidaya Hamisi amemshukuru Naibu meya kwa msaada huo ambao utaweza kusaidia kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo na kuondoa msongamano kwa wanafunzi.
   Naibu meya wa Manispaa wa Ilala, Omary Kumbilamoto akikabidhi mifuko ya saruji kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni, Hidaya Hamisi
   Picha ya pamoja na ya Naibu Meya na wazazi wa wanafunzi wanaosoma Miembeni shule ya msingi


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa ruksa kwa Klabu ya Yanga na Simba kutumia Uwanja mkuu wa Taifa katika michezo ya ligi kuu ya Vodacom kuanzia  kesho ambapo kutakuwa na mtanange wa baina ya timu ya Simba na Azam FC utakaopigwa kwenye dimba hilo kuanzia saa 10 jioni.

  Uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 ulifungiwa na Serikali kumika baada ya mchezo wa Oktoba mosi baina ya Simba na Yanga kutokana na vurugu zilizosababisha uharibifu uliofanywa na mashabiki wa Wekundu hao kuvunja viti 1871.

  Ofisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Alfred Lucas imemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kwa kukubali ombi la kuwaruhusu kuendelea kutumia uwanja huo huku pia akimpongeza Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye kwa kusimamia hadi kufikia hatua hiyo.

  "Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na TFF inampongeza Rais Magufuli kwa kuruhusu mechi za ligi kuu ya kuchezwa katika uwanja wa Taifa pia Waziri Nape kwa kusimamia hadi kufikia hatua hii" alisema Lucas.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ameishukuru Serikali ya India kwa ufadhili wake wa miradi ya maji katika miji 17 nchi ambayo inalenga kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wengi nchini.

  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 68 ya Siku ya Kitaifa ya Jamhuri ya India sherehe ambazo zimeambatana na Uzinduzi rasmi wa majengo ya ofisi mpya ya Ubalozi wa India hapa nchini.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema ufadhili wa miradi ya Maji pamoja na miradi mingine unaofanywa na Serikali ya India kwa Tanzania Bara na Zanzibar unadhihirisha wazi mahusiano mazuri yaliyopo yaliyoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mahatma Gandhi wa India.

  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa India ni moja ya washirika muhimu katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo na Serikali itaendelea kufanya kazi kwa karibu katika maeneo mengi ikiwemo ya kikanda na kimataifa kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na India.

  Amesema kwa miaka mingi sasa mahusiano ya kindugu yamekuwa yaakiimarika katika sekta mbalimbali ikiwemo kisiasa,kidiplomasia,kibiashara, masuala ulinzi, utamaduni na mwingiliano wa watu na watu. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam mbele ya Balozi wa India Bw. Sandeep Arya .
  Balozi wa India hapa nchini Bw. Sandeep Arya akimuonesha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan picha mbali mbali zenye kuonyesha historia ya urafiki baina ya Tanzania na India wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi wa India jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India hapa nchini.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Jengo jipya la Ubalozi wa India lililopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.  0 0

  Watumiaji wa simu za mkononi wameaswa kutokutoa namba za siri za simu zao wanapopigiwa simu au kutumiwa ujumbe mfupi yaani SMS. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Jacquiline Materu, alisema“Natoa wito kwa wateja wetu kuwa makini na matapeli wanaowapigia simu na kuwafahamisha kuwa wameshinda fedha za Promosheni ya Nogesha Upendo au bonasi ya M-Pesa. 

  Vodacom Tanzania haina utaratibu wa kuwapigia simu wateja kuhusiana na mgao wa fedha za bonasi ya M-Pesa bali inatoa mgao huo kwa kadri ya mteja alivyotumia huduma hii na rekodi zote za matumizi kampuni inazo sambamba na utaratibu uliowekwa na Benki Kuu. 

  Materu alisema kampuni inawapigia simu wateja wa Promosheni ya Nogesha Upendo tu na kuwajulisha kuwa wameshinda na fedha zao hutumwa moja kwa moja kwa njia ya M-pesa ndani ya masaa 48 bila kuwataka wateja hao kutoa taarifa zozote za siri juu ya namba zao. Wengine wanaowapigia simu wateja kuhusiana na bonasi ni matapeli ambao wanataka kupata namba za siri na kuwatajia kiasi gani cha fedha mlizonazo ili wapate fursa ya kuwaibia fedha,” alisema Materu.

  Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Bi. Jacquiline Materu

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu

  0 0

  Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limekamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro amesema kuwa mnamo Januari 22 mwaka huu jeshi la polisi lilikamata gari aina ya Toyota karina lenye namba za usajili T 950 DFN baada ya msako  wa jeshi hilo katika maeneo ya Bandari jijini Dar es salaam.

  ‘’Gari jingine ambalo tumelikamata Toyota landcruseir Prado lenye namba zasajili T 959 DFT gari hili katika uchunguzi wetu liliibiwa September 16 mwaka jana na badaye kuonekana maeneo ya Mwanza januari 21 Mwaka huu’’ Alisema Kamishina Simon Sirro.

  Kamishina Sirro amesema kuwa jeshi hilo pia limewakamata watuhumiwa kwa wizi  wa pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jijini  Dar es salaam na Pwani pamoja na mkoa wa Morogoro baada ya operesheni iliyofanywa na jeshi hilo .

  Amesema kuwa jeshi hilo limewakata vinara saba wa utengenezaji wa kadi bandia za chanjo ya homa za manjano ambapo huziuza kwa watu wanaofika katika hospitali ya Mnazi moja kwaajili ya kupata huduma za matibabu kabla yakusafiri nje ya nchi.

  ‘’Baadhi yawatuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na Aisha Hassani(29) mkazi wa Vingunguti, Yakobo Msenga (42) mkazi wa Chanika, Oliver Bwegege mhamasishaji (58) mkazi wa Kigogo’’ Ameongeza Sirro.
   Kamishina wa Polisi wa kanda maalm ya Dar es Salaam CP Saimon Sirro akizugumza na waandishi wa habari juu ya Jeshi la polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kuhusu kukamata magari matano ambayo yanasadikiwa kuwa yaliibiwa katika vipindi tofauti katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel massaka, Globu ya jamii.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha silaha aina ya SHORTGUN PUMP ACTON iliyo kutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huko Boko njiapanda leo jijini Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionesha kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano zilizokamatwa maeneo ya Hospital ya Mnazi mmoja jiji Dar es Salaam.
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionesha magari yaliyokuwa yameibiwa katika sehemu mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
   Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha mitambo ya kutengenezea Gongo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro  akionesha mkasi wa kuvunja.

older | 1 | .... | 1532 | 1533 | (Page 1534) | 1535 | 1536 | .... | 3272 | newer