Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

MASAUNI AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA POLISI KATIKA KIJIJI CHA UTENGULE WILAYANI MBEYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule.Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.
Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) ramani ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Utengule baada ya kuzindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.Naibu Waziri aliwashukuru wananchi hao kwa kujitolea eneo la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa jeshi ikiwa ni juhudi zao katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MCHEKESHAJI CHAKU MASTER AZISHAURI TIMU ZINAZOSHIRIKI KOMBE LA FA

$
0
0

Mchekaji wa Mjini Songea mkoani Ruvuma Chaku Master, amezitaka timu ambazo zinashiriki kombe la Azam Sport Federation (FA CUP ) hasa zile ambazo hazipo ligi kuu Tanzania bara, kukaza katika michezo hiyo ili ziweze kutwa ubinga wa FA CUP na sio kuwa wasindikizaji ama kukaa na kusema kombe hilo ni la timu kubwa tu, huku akitolea mfano wa mchezo wa mwaka jana kati ya Yanga na JKT Mlale ambayo yanga ilipata ushindi kwa tabu zaidi. Hii hapa video yake.

Wachezaji Airtel Rising Stars wachanguliwa kujiunga na timu za Taifa

$
0
0
Baada ya kumalizika kwa kliniki ya wiki moja ya Airtel Rising Stars mwishoni mwa wiki jana, wavulana 16 wamechanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya Serengeti Boys huku wasichana watatu wakichanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya wanawake - Twiga Stars na wengine 17 kuchagulia kuingia timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Kilimanjaro Queens.

Akiongea na waandishi wa habari leo kutangaza majina ya wachezaji hao, Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi alisema makocha walikuwa na kibarua kigumu kuchangua wachezaji kwani wachezaji wote walionyesha vipaji vya hali ya juu sana. Madadi alisema kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa michuano ya Airtel Rising Stars ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya, uchanguzi dhidi ya wachezaji ulikuwa wakuridhisha.

Tulikuwa na jumla ya wachezaji 65 kwenye kliniki ya Airtel Rising Stars, wavulana 40 na wasichana 25. Ni kweli kuwa wachezaji wote hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya taifa, lakini wachezaji ambao wamebaki tutaendelea kuwatumia kwenye michuano mbali mbali ya vijana. Pia wengine watachanguliwa na klabu zetu kuchezea timu zao za vijana. Natoa wito kwa uongozi kuwatumia vizuri vijana hao kwani vipaji wanavyo wanahitaji uzoefu tu, alisema Madadi.
Meneja Uhusian wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.

Mimi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, nitahakikisha Shirikisho inaengemea kwenye upande wa kukuza timu na mashindano ya vijana ili kujenga timu bora ya Taifa. Natoa shukrani kwa Airtel katika mchango wake wa kukuza soka la vijana hapa nchini. Nina uhakika Airtel itaendelea na mashindano haya ya Airtel Rising Stars ili kuendelea kuibua vipaji vya vijana wetu, alisema Madadi.
Tuko kwenye harakati za kuhakikisha tunakuwa na timu za kudumu za umri wa chini ya miaka ya 14, 17 na 19. Tukifanya hivyo tutaweza kujenga timu ambayo itafanya vizuri kwenye fainali za michuano ya AFCON ambayo itafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2019, aliongeza Madadi.
Akiongea juu ya kuchangua wachezaji, kocha mkuu wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime ambaye alisimamia kliniki hiyo alisema makocha walichangua wachezaji kulingana na mahitaji ya sasa ya timu ya Serengeti Boys. Tuliengemea kwenye wachezaji ambao wanaweza kuelewa na kuendana na mfumo wa mpira wa mashidano na wachezaji wenye uelewa wa haraka. Kama mnavyojua, timu yetu ya Serengeti imecheza mechi nyingi za kimataifa kwenye miaka miwili iliyopita na hivyo kupata uzoefu wa kimataifa.
Mkurugenzi wa ufundi wa soka la vijana Tanzania chini ya TFF, Kim Paulsen akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.

Nia yetu ilikuwa kupata wachezaji wa kuendana na mfumo huo, alisema Shime. Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza wachezaji waliochanguliwa kujiunga na timu za taifa.
Wachezaji hawa walianza kucheza michuano ya Airtel Rising Stars tangu ngazi ya wilaya. “ Airtel tunayo furaha kuweza kuwafanya wachezaji hawa kutimiza ndoto zao za kucheza mpira wa kulipwa. Kama mnavyojua mpira kwa sasa sio burudani pekee, bali pia ni ajira kwa wachezaji wengi duniani. Ni hamasa kubwa kuona vijana wakianza kujipatia riziki zao kutokana na vipaji vyao vya kucheza mpira wa miguu” alisema Mmbando.

IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA YAFANYA UKAGUZI WA HALI YA UTUNZAJI KUMBUKUMBU KATIKA OFISI ZA MAMLAKA YA MAPATO MKOANI MBEYA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Charles G. Magaya akikagua utunzaji wa kumbukumbu katika masijala ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya alipofanya ziara ya kikazi kujionea hali ya utunzaji kumbukumbu mkoani humo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Charles G. Magaya (aliyevaa koti la kijivu) akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Mbeya kuhusu namna bora ya Utunzaji wa Kumbukumbu za ofisi alipofanya ziara ya kikazi kujionea hali ya utunzaji kumbukumbu mkoani humo.

WAKINAMAMA WA KIKUNDI CHA 2SEEDS WAJIKWAMUA KIMAENDELEO CHINI YA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

$
0
0
Wakinamama wa kikundi cha 2Seeds, wa kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga,wakishirikiana na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald (wapili kulia) kumenya viazi wakati alipotembelea kikundi hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiliamali,ufugaji, Kilimo,inayofanywa na kikundi hicho na kufadhiliwa na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani.
Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds cha kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab(wapili kushoto) akimuonyesha Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe zilizotengenezwa kitalaam na kuhifadhiwa kwenye mifuko maalumu tayari kwa kuuzwa sokoni,wakati alipotembelea Kikundi hicho hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hichokilichofadhiliwa na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani.
Bibi Masoko wa kikundi cha 2 Seeds cha kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga ,Mariam Jecha (wapili kulia) akimfafanulia jambo hivi karibuni,Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (Kushoto) kuhusiana na jiko la kisasa la kukaangia chips za viazi na mihogo zinazozalishwa na kikundi hicho baada ya kupata mafunzo ya ujasiliamali kutoka kwenye taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds ya nchini Marekani yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo umefadhiliwa na na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation”
004.Moshi Abdallah na Monica Ayubu wa kikundi cha 2Seeds cha kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga,wakimshuhudia Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald,(kulia) akiangalia ubora wa vyakula vinavyosindikwa na kikundi hicho, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani.
Mratibu wa kikundi cha 2Seeds cha kijiji cha Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga, Moshi Abdallah(kushoto) akimuonyesha mradi wa kilimo cha mboga Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network la nchini Marekani.

ENEO LILILOKUWA KIOTA MAARUFU CHA CLUB BILLICANAS BAADA YA KUTEMBEZEWA NYUNDOZZ

$
0
0
Hivi ndivyo lionekanavyo eneo lililokuwa na kiota maarufu cha burudani Club Billicanas, baada ya kutembezwa nyundozz na wamiliki wa eneo hilo ambao ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), sijui ni kitu gani kingine kitajengwa katika eneo hili.

POLEPOLE AKUTANA NA MAOFISA WAANDAMIZI WA UBALOZIWA MAREKANI LEO

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Siasa katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Marilyn Gayton (kushoto), Katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Janauari 24, 2017. Wapili kulia ni Ofisa Habari wa Ubalozi huo, Lauren Ladenson. Wanaotazama Kamera ni Maofisa Waandamizi kutoka Idara za Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa na Idara ya Itikadi na Uenezi.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo wakati akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Siasa katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Marilyn Gayton, Katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. 
 Mazungumzo yakiendelea

SAFARI YA TATU YA TRENI YA KWENDA PUGU KUANZA KESHO

$
0
0

NA Anthon John, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa Shirika la Reli Tanzania( TRL) umewatangazia Wasafiri wote wa treni ya mjini iendayo pugu kuwa safari ya tatu awamu ya jioni itaanza tena siku ya Jumatano januari 25, 2017, Safari hiyo itaanza katika kituo kikuu cha Dar es salaam saa 2:15 usiku na kuwasili pugu saa 3:10 usiku.

 Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa Usafirishaji wa Reli ya Tanzania TRL Rashid Ng'hwani amesema kuanza tena kwa safari hiyo kunatokana na  kukamilika kwa kazi ya kutandika reli mpya katika eneo korofi kati ya stesheni za Llala block, Posta na Karakata.

  Aidha Ng'hwani amesema kuwa Safari za asubuhi zitaendelea kuwa mbili kwa vile kazi ya utandikaji reli bado haujakamilika.

  "Kazi ya ukarabati huanza kati ya saa 3:15 asubuhi hadi saa 8 mchana kila siku za kazi na inatarajiwa kukamilika baada ya wiki 10 tokea ianze kazi hiyo"amesema Ng'hwani.
 
Sanjari na hayo Kaimu Mkuu huyo wa usafirishaji wa reli  ameongeza kuwa ukarabadi huu utaondoa kero ya vumbi kwa abiria kwenye mabehewa kwani njia yote itawekewa kokoto za kutosha (stone ballast) ambazo hazina vumbi.

WAZIRI NCHEMBA AONGOZA ZOEZI LA UTEKETEZAJI SILAHA HARAMU 5,608 MKOANI KIGOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akikagua silaha haramu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuteketezwa wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha hizo lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Silaha haramu zikiwa zimepangwa katika uwanja wa Lake Tanganyika tayari kwa uteketezaji wakati wa zoezi hilo lililofanyika mkoani kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akiangalia silaha aina ya SMG iliyotengenezwa kienyeji ambayo ni mojawapo ya Silaha zilizoteketezwa wakati wa zoezi la uteketezaji wa Silaha haramu lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akibonyeza kifaa maalumu kwa ajili ya kuwasha moto wa uteketezaji wa Silaha haramu wakati wa zoezi la kuteketeza Silaha haramu lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Generali Emmanuel Maganga
Silaha haramu zikiwaka moto wakati wa zoezi la kuteketeza Silaha haramu lililofanyika mkoani kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali katika kupambana na uzagaaji wa Silaha haramu hapa mchini ambazo zimekuwa zikitumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba akizungumza na wakazi wa mkoa wa kigoma waliojitokeza kushuhudia zoezi la la kuteketeza Silaha haramu lililofanyika mkoani Kigoma ambapo jumla ya Silaha haramu 5,608 zimeteketezwa na Jeshi la Polisi ikiwa ni juhudi za Serikali kupambana na uhalifu hapa nchini(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi). 

NEWS ALERT: UZINDUZI RASMI WA AWAMU YA KWANZA YA MIUNDOMBINU NA UTOAJI HUDUMA YA MABASI YAENDAYO HARAKA (BRT) JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0

KUTOKA MAKTABA: Video ikimuonesha Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo eneo ya Ubungo jijini Dar es salaam miaka minne iliyopita akiwa na aliyekuwa waziri wa Ujenzi wakati huo Dkt. John Pombe Magufuli ambaye sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph  Magufuli, kesho tarehe 25 /01/2017 anatarajiwa kuzindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit - BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani jijini Dar es salam.

Uzunduzi huo utahudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia wa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird. 
Awamu ya Kwanza ya mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) yenye urefu wa kilometa 20.9 unaojumuisha barabara ya Kimara – Kivukoni, Magomeni  - Morocco na Fire – Kariakoo ulikamilika Desemba 2015. 
Aidha, utoaji wa huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka ulianza tarehe 10 Mei, 2016. Kwa sasa huduma ya mabasi katika kipindi cha mpito inatolewa katika njia nane, vituo vikuu vitano, vituo vidogo 28 na karakana moja kwa kutumia mabasi 140 yanayojumuisha mabasi makubwa 39 yenye uwezo wa kubeba abiria 160 kila moja na mabasi madogo 101 yenye uwezo wa kubeba abiria 60 kila moja. 
Mradi wa ujenzi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) umepangwa kutekelezwa kwa awamu sita kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari  katika Jiji la Dar es Salaam.


Imetolewa na:


Eng. Joseph M. Nyamhanga

 KATIBU MKUU (UJENZI)


24 Januari, 2017

WELCOME TO THE #1 SECURITY PRODUCT IN THE WORLD

RAIS DK.JOHN POMBE MAGUFULI KUZINDUA MRADI WA UDART KESHO JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Rais Dk. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (UDART) katika kituo cha mabasi Gerezani –Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa amesema katika uzinduzi barabara ya Msimbazi itafungwa na mabasi yatakwenda kugeuzia katika kituo cha Feri.

Amesema safari za mabasi zitasitishwa mpaka pale uzinduzi utakapo kuwa umekwisha na kurejea katika hali ya kawaida.

Buganywa amesema kwa abiria wanatumia kituo cha Gerezani watashuka katika kituo cha zimamoto ‘Fire’ na mabasi hayo yataendelea mpaka kituo cha Feri.

Kampuni ya mabasi hayo inawaomba radhi abaria wanaoshuka katika vituo vya msimbazi hadi Gerezani kwa usumbufu ulioitokeza.
Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa akizungumza na waandishi habari juu ya uzinduzi mradi wa mabasi yaendayo haraka kesho jijini Dar es Dar es Salaam.
Sehemu waadishi wa habari wakimsikiliza Afisa Habari wa kampuni ya mabasi yaendayo Haraka (UDART), Deus Buganywa, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jami.

Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia.

WATANZANIA waishio nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamoja na kuangalia namna ya kutekeleza kiu ya nchi ya viwanda kama ilivyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, mwenye suti nyeusi, akifurahia jambo ofisini kwa Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten, alipofika ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo hija ya mwaka huu wa 2017.

Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, hayupo pichani walipokutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuangalia fursa za kimaendeleo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mjini Jeddah, Saudi Arabia na Balozi wa Tanzania nchini hapa, H.E Hemedi Mgaza, alipofanya kikao na Watanzania waishio nchini hapa kama njia za kushirikiana na wadau hao kwa ajili ya kupeleka maendeleo ya uhakika nchini Tanzania na kuisimamia kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Akizungumzia juu ya fursa ya uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Mgaza alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa nafasi yake kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao. Alisema mbali na Watanzania hao kuwekeza kwao kama uwezo wanao, pia wanaweza kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa ajili ya kuchangia fursa hiyo ya watalii inayolipa duniani kote.
Kikao kinaendelea.


Kikao kinaendelea.

“Tukitoka hapa kila mmoja awe balozi shupavu wa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania ili pamoja na mambo mengine, tuwe tumechangia ukuzaji wa uchumi wetu kulingana na uwezo wetu kwa kupitia sekta nyeti ya utalii, ambapo pia kama sehemu ya serikali nilisikiliza maoni na ushauri wao ili tusonge mbele..

“Tuonyeshe mazuri ya nchi yetu pamoja na sisi wenyewe kushiriki katika fursa za kiuchumi kuliko kusubiri wengine wafanye wakati tunajua fika kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuiletea maendeleo nchi yetu,” alisema Balozi Mgaza.


Kabla ya kikao hicho na Watanzania, Balozi Mgaza pia alifanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten.


Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo, H.E Mgaza alijadiliana na Dr. Benten masuala mbalimbali yanayohusu maandalizi ya ibada ya Hijja ya mwaka 2017 na fursa kwa mahujaji wa Tanzania.

SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA FEBRUARI 912 MJI MKONGWE ZANZIBAR

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

VIKUNDI 40 vyenye wasanii 400 vinatarajiwa kutumbuiza Tamasha la Sauti za Busara linalotarajia kuanza kuridima Februari 9 -12 katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Mjini Zanzibar .

Akizungmza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Sauti za Busara, Simai Said amesema kuwa tamasha limekuwa likitangaza Tanzania pamoja na kuwaweka Waafrika sehemu moja.

Simai ameiomba Serikali kuunga mkono Sauti za Busara kutokana na kazi kubwa inayofanyika katika kuongezea uchumi wa nchi pamoja na kupata watalii wengi wakati tamasha hilo linapofanyika. Amesema kutokana na Tamasha hilo kuwa na vitu vingi vya kiubunifu imesaidia kuongeza ajira kwa vijana katika pande zote kutokana na kuutumia utamaduni wa Tanzania.

“Sauti za Busara limebakiza siku chache kufanyika pale Mji Mkongwe, Zanzibar 9-12/Februari kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha la Sauti za Busara lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ mwaka huu tamasha litakua na majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa/nyumbani”amesema Simai.

Amesema Watu mbalimbali wenye rangi tofauti, umri tofauti kwa mara nyingine tena wataunganishwa na tamasha kusheherekea muziki wa Ki-Afrika kwa kuwa na matarajio ya mahudhurio ni makubwa kutoka Tanzania na nje ya Nchi kufatia kujaa kwa sehemu za malazi Mji Mkongwe kwa wiki ya tamasha. Wasanii wote watatumbuiza ‘live’ muziki wa Ki-Afrika kila siku kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 7:00 usiku.Simai amesema tamasha ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanznaia ni Sh 6,000 kwa siku na Sh 20,000 kwa siku nne za tamasha.

Tamasha  hilo litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morcco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha.
Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said akitoa ufafanuzi na namna tamasha hilo litakavyokuwa siku hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani),ambapo ameeleza kuwa tamasha hilo ambalo limekuwa likiwajumuisha makundi,washabiki na wapenzi mbalimbali litabeba kauli mbiu itakayojulikana #AfricaUnited.Kulia ni ni Balozi Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad .

Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad (pichani kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na udhamini wao katika tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kuanza kurindima Februari 9-12 mjini Ngome Kongwe,Zanzibar,Balozi huyo pia amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kulidhamini tamasha hilo ambalo limekua likiibua vipaji mbalimbali na kivitangaza nchini na ulimwengu kwa ujumla,Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said,Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuph Mahmoud pamoja na Meneja wa tamasha hilo,Journey Ramadhan.
Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara,Yusuph Mahmoud akielezea mambo mbalimbali yatakayojiri ndani ya tamasha hilo,Simai alieleza kuwa tamasha hilo Wasanii watatumbuiza LIVE kwa asilimia 100.
Viongozi wa tamasha la Sauti za Busara wakizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar. PICHA NA MICHUZI JR.


MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNEP

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini ambao umepelekea mamia ya ekari za misitu kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo mpango wa upandaji wa miti kote nchini lakini bado msaada na nguvu zaidi inahitajika kutoka shirika la Mazingira la UNEP ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo nchini.

Amesema Tanzania ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Shirika la UNEP ambapo shirika hilo limeweza kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya kuhifadhi mazingira hivyo mahusiano hayo mazuri ni muhimu yakaja na mbinu bora na nzuri za kuhifadhi mazingira ili kuokoa Taifa lisigeuke jangwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini.

Makamu wa Rais pia amehimiza wataalamu wa mazingira wajikite zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi watumie nishati mbadala kama gesi na makaa ya mawe ili kudhibiti tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 2.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye ameongozana na ujumbe wake kwa ziara ya siku 2 wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Faustine Kamuzora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim na ujumbe wake . 
Picha ya pamoja.


WASHIRIKI KILIMANJARO MARATHON WATAKIWA KUJISAJILI MAPEMA

$
0
0
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa Kilimanjaro Marathon amewataka washiriki wa mbio hizokujisajili mapema ili kuepuka na msongamano dakika za mwisho.

Alitoa rai hiyo Jijini Dar es Salaam huku akisema mbio hizo zimekuwa kubwa na maarufu na hivi kuwavutia washiriki wengi  jambo ambalo linalazimu washiriki waanze kujisajili mapema.

“Mwaka jana kulikuwa na wakimbiaji zaidi ya 8000 kutoka nchi zaidi ya 45 na tunatarajia kupata washiriki wengi zaidi mwaka huu,” alisema na kuongeza kuwa Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa mdhamini mkuukwa miaka 15 mfulululizo sasa.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kilimanjaro Marathon 2017. Wengine mini mbio za kilometa 5, Meneja Masosko wa Grand Malt Tanzania kutoka kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Oscar Shelukindo anayedhamini mbio za kilometa 5, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania Caroline Kakwezi-kilometa 10 kwa watu wenye ulemavu na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata-kilometa 21.

Alisema wakati wa msimu huu wa Kilimanjaro Marathon, Kilimanjaro Premium Lager itaanza kuuzwa katika chupa mpya yenye ujazo wa mililita 375 kwa Kilimanjaro na Arusha.

YANGA WAIANGUKIA SERIKALI,WAOMBA KUUTUMIA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya Yanga  imeandika barua Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo kuomba iruhusiwe kuanzia wikiendi hii kutumia Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru mjini Dar es Salaam kwa mechi zake za mashindano ya nyumbani.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kuwa wameandika maombi hayo kwa lengo la kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa kwa michezo yao ya ligi kuu ili wachezaji waanze kuuzoea kelekea mtanange wao wa  michuano ya Afrika, ambayo watatumia Uwanja wa Taifa.

Kwa sababu hiyo, Baraka alisema wanataka waruhusiwe kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa, ili wauzoeee mapema hata mechi zao za michuano ya Afrka itakapoanza wawe tayari.

“Kama unavyojua kwa muda mrefu hatujautumia Uwanja wa wetu huu kipenzi wa Taifa baada ya kuzuiwa na Serikali kufuatia vurugu za kwenye mechi yetu na Simba baada ya mashabiki wa wenzetu kufanya fujo na kuvunja viti,”.

“Lakini tutambue kuwa tuliingia mkataba maalum na Serikali wa kuutumia Uwanja huu kwa mechi za mashindano ya Afrika na ule wa Uhuru kwa Ligi Kuu pekee na  kwa kuwa tunakaribia kuanza mechi za Klabu Bingwa  Afrika tunaiomba Serikali ituruhusu kuhamishia mechi zetu za mashindano ya nyumbani Uwanja wa Taifa, ili iwe sehemu ya maandalizi yetu ya michuano hiyo ya Afrika,”amesema Baraka.

Yanga watashuka dimbani dhidi ya Mwadui  mechi itakayochezwa Januari 29 Jumapili Jijini  Dar es Salaam na Februari 05 wataikaribisha Stand United Februari 5 na kisha kuanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Ngaya De Mbe.

Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya De Mbe kutoka visiwa vya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Picha ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akikabidhiana mkataba Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  kwa makubaliano ya kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa akitoa taarifa ya Baraza hilo katika kikao kati ya Baraza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017 
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, John Jingu  akitoa maelezo kuhusu Baraza hilo katika kikao kati ya Baraza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017.

  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na watumishi wa Baraza hilo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye makazi yake , Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake, Oysterbay  jijini Dar es salaam Januari 24, 2017. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

TAASISI YA MOYO YAFANYA UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 100 NA KUSHINDWA KUPITISHA DAMU

$
0
0


Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari  Afrika kutoka nchini Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization Procedure) kwa mgonjwa na kuzibua mshipa wa Moyo uliokuwa  imeziba kwa zaidi ya miezi mitatu (kwa lugha ya kitaalamu Chronic Total Occlusion).

Upasuaji huo ambao unatumia mishipa ya damu ulichukuwa muda wa saa moja kwa  kuzibua mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa umeziba kwa asilimia 100 na   kushindwa kupeleka  damu upande wa kushoto wa moyo.

Kambi ya Madakari wa Afrika imeanza tarehe 23/1/2017 na inatarajiwa kumalizika tarehe 29/1/2017. Hadi sasa jumla ya  wagonjwa sita wameshapatiwa huduma za matibabu ya moyo ambayo ni kuzibua mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba. Hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanatarajiwa kuruhusiwa siku yoyote kuanzia kesho.

Tangu kuanza kwa mwaka huu wagonjwa 29  wameshafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya wagonjwa hao 23 wamefanyiwa upasuaji katika kambi za ndani na wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya Madaktari Afrika.

Taasisi inaendelea kuwaomba  Madaktari wote nchini wenye wagonjwa wao wa matatizo ya  moyo wawatume wagonjwa hao katika Taasisi ya Moyo  ili waweze kupatiwa matibabu. Kwa mawasiliano zaidi wawasiliane na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na  022-2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma  wagonjwa hao.

Imetolewa na:


Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
24/01/2017

TFF YAMUONYA MWAMUZI BORA 2015/16 NGOLE MWANGOLE, YAIPIGA FAINI YANGA

$
0
0
LIGI KUU


TIMU ya Yanga imepigwa faini ya jumla ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa makosa mawili ikiwemo na timu yao kutoingia vyumba vya kubadilishia nguo pamoja na kutumia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14 (13) na (14) ya Ligi Kuu. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

Halikadhalika mwamuzi Hussein Athuman kutoka Mkoa wa Katavi aliyechezesha mchezo huyo namba 150 uliozikutanisha timu za Majimaji ya Songea na Young Africans ya Dar es Salaam, kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF limemwondoa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) baada ya kupata alama za chini ambazo hazimwezeshi kuendelea tena kuchezesha Ligi hiyo.

Mwamuzi Ngole Mwangole: Mwamuzi huyo wa kati, Ngole Mwangole wa Mbeya amepewa barua ya onyo kali na kumtaka aongeze umakini wakati akichezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kubainika kukataa bao lililoonekana kutokuwa na mushkeli la Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Licha ya kujitetea, lakini kamati haikuridhika na maelezo yake. Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa Bw. Mwangole alikuwa Mwamuzi Bora wa msimu uliopita (2015/2016) na hiyo ndiyo mara yake ya kwanza kuonekana kufanya uamuzi uliokosa umakini wakati akichezesha, TFF imeamua kumpa onyo.

Mechi namba 141 (Mwadui FC vs Kagera Sugar). Beki wa Kagera Sugar, Godfrey Taita anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu kwa kuwavamia waamuzi baada ya mechi na kuwatolea lugha chafu na vitisho kabla ya benchi la ufundi la timu yake pamoja na askari polisi kuingilia kati na kudhibiti kadhia hiyo.

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images