Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1525 | 1526 | (Page 1527) | 1528 | 1529 | .... | 3353 | newer

  0 0
 • 01/23/17--08:53: Article 3

 • Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba.

  Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba.
  Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry.
  Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora. 


  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Dkt. Akwilina Chuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu wakala huo kufanikiwa kuvuka lengo kwa kufanya kaguzi 41,551 katika kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Usalama na Afya wa OSHA Bw. Alex Ngata.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakufuatilia mkutano wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) leo jijini Dar es salaam.(Picha na Frank Mvungi-Maelez

  0 0

  Rais wa Marekani Donald Trump amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa.
  Kwa mujibu wa taarifa ya mtandao wa Independent, mabalozi hao wametakiwa kuachia nafasi zao mara moja na kurudi nyumbani.

  Kiongozi huyo juzi alifanya ziara yake ya kwanza katika ofisi za makao makuu ya shirika la Ujasusi la Marekani CIA, na kuvituhumu baadhi ya vyombo vya habari nchini humo wakati akitoa hotuba yake, kwamba vinawagawa wananchi.

  Zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbali mbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana punde baada ya Trump kuapishwa.

  Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na wa itifaki muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza, Canada. Inatabiriwa kuwa nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Kongresi kabla ya kuanza kazi zao.

  Source: Independent

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe wakipokea mashada ya maua kutoka kwa watoto walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mapokezi rasmi na mazungumzo na mwenyeji wao Rais Dkt John Pombe Magufuli.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwalaki Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 kwa mazungumzo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan wakipiga ngoma Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwazawadia Kinyago cha Umoja na Mchoro wa Mlima Kilimanjaro Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan na mkewe Emine Erdogan walipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na mke Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mama  Emine Erdogan wakipeana mikono baada ya maongezi  Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea baada ya yeye na mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli ushuhudia uwekaji saini mikataba mbalimbali ya ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Uturuki Ikulu jijini Dar es salaam leo Januari  23, 2017 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na akiongea katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  akiongea na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe  Magufuli katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Uturuki Mhe Recep Tayyip Erdogan  na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe  Magufuli wakishuhudia ubadilishanaji hati baada ya kusaini baina ya mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa sekta binafsi Dkt Reginald Mengi na kiongozi wa msafara wa wafanyabiashara wa Uturuki katika kongamano la wawekezaji wa Tanzania na Uturuki katika ukumbi wa BoT jijini Dar es salaam  leo Januari  23, 2017.

  PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0


  Na Zainab Nyamka, 

  Globu ya Jamii

  Timu ya Azam imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Cosmopolitan inayoshiriki ligi daraja la pili.
  Azam wamewaondoa  Cosmopolitan katika michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ilichukua muda kwa Azam kuandika goli la kwanza mpaka  kipindi cha pili  baada ya John Bocco kutumia uzembe wa goli kipa ndani ya kumi na nane na mpira kumbabatiza na kurudi golini kwenye dakika ya 69.
  Haikuchukua mda sana  Shaban Idd akitumia pasi safi iliyopigwa na John Bocco ikiwa ni uzembe pia wa golikipa na kuiandikia Azam goli la pili dakika ya 76,  Cosmo wakiendelea kujitutumua angalau kurejesha matumaini kwa kikosi chao ya dakika ya 79 Fidelisi Kyangu anaipatia timu yake goli la kufutia machozi akiunganisha mpira wa kona.
  Dakika ya 80 Joseph Mahundi akiwa peke yake aliweza kuiandikia Azam goli la tatu na la ushindi na kuzima kabisa matumaini ya Cosmo.
  Kwa ushindi huo kwenye mchezo wa Raundi ya Tano, Azam FC inaungana na vigogo Simba na Yanga kwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. 
  Yanga iliitoa Ashanti United kwa mabao 4-1 Jumamosi wakati Simba jana iliitoa Polisi Dar kwa mabao 2-0, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
  Baada ya mchezo huo, Azam FC inakwenda kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba SC Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. 
  Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gardiel Michael, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Stephan Kingue/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk73, Himid Mao, Frank Domayo, John Bocco, Yahya Mohammed na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
  Cosmopolitan; George Kijombi, Ramadhan Yusuph, Maulid Jumanne, Abdul Kussy, Fidelis Kyangu, Salum Hamisi, Hassan Mussa/Hafidh Hamisi dk62, Omary Hamisi, Ally Kabunda, Nuru Thabit na Fakhi Rashid.  0 0

    FIBER BOAT 25 FEET WITH BRAND NEW YAMAHA 40HP & TRAILER FOR IMMEDIATE SALE  -- CONTACT 0772342058 


  0 0


  0 0
 • 01/24/17--00:00: Article 0


 • 0 0

                       
    RATIBA TU NI MUHALI,,HAYO MENGINE KWETU SI BAHARI?? 

  Haji S Manara.  

   Kuna kurogwa na kujiroga,Kuna kufa na kujiua pia kulia na kuliliwa, Sisi watanzania hakika tupo ktk fungu la pili, fungu la kukosa , fungu mzigo, tunajiroga,tunajiua na tunaliliwa.

  Hakika hatujui twataka nn, hatujui malengo yetu, lakini kubwa hatujui hata tutokapo wala tuendako, na leo naandika kitu kidogo tu kinachotushindwa kwenye soka letu, RATIBA

   Wakati wenzetu wanazungumzia  changamoto nzito na kubwa ktk maendeleo yao ya mchezo murua zaid duniani wa soka, Watanzania tunahangaika namna ya kupanga ratiba ya mechi zetu za ligi yetu na Kombe la Shirikisho, ratiba inayobadilishwa Kama nguo, tena mvaaji mwenyew ni mbunifu wa mavazi au mwanamitindo, ambae huvaa nguo tano Kwa siku.

  Siku za nyuma niliwahi kuwaambia Clouds fm kuwa, iwapo ratiba ya Ligi kuu nchini isipopanguliwa ntatembea bila shati toka Mtaa Msimbazi hadi zilipo ofisi za TFF pale karume stadium,

  Nilidhani Kwa kusena vile walau TFF na bodi ya Ligi wataona haya na kuhakikisha ratiba ya Ligi kuu haitabadilishwa tena, kumbe ndio kwanza wakubwa wameweka gundi masikioni, toka wakati ule ratiba ishafumuliwa Mara tatu, na leo hii imebadilishwa tena, Kwa kisinguzio kile kile, eti ratiba za Caf na za ligi zimeingiliana. 

   Ninajiuliza iwapo ratiba ya Ligi yetu ni muhali kuipanga,vipi kuhusu program nyingine za maendeleo? 

  Itakuwaje kuhusu timu yetu ya taifa juu ya ndoto zetu za mchana wa jua kali? vipi kuhusiana na zile programu hewa za soka la vijana, watoto na wanawake?

   Hakika kwetu hayo ni sawa na bahari ya Mediterranean au bahari kuu ya hadithi za Alfu Leila uleila, hatuwezi ratiba tutaweza kwenda Afcon 2019? hatuwezi kupanga ratiba tutaweza kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza mchezo huu ambao yatajwa watu bilioni tatu duniani kote wanaushabikia? 

  Kama tumerogwa aliyeturoga Kafa, hatuponi hadi Kiyama , tutakapokutana nae mchawi wetu. 

  Nimalizie Kwa kuwapa mtihani mwingine TFF na bodi ya Ligi, iwapo Kama ratiba yao ya Ligi kuu na Kombe la shirikisho haitabadilishwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu, ntamposa mlimbwende Wema Sepetu, na akikubali ntamuoa, akikataa ntatembea na boxer toka Nyumbani kwangu hadi TFF..

  0 0  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya mahasimu, Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka na Yanga kuwa na mashindano ya kimataifa ambapo itawawia vigumu kucheza siku hiyo.

  Mchezo huo uliotakiwa kufanyika Februari 18, mwaka huu umesogezwa mbele kuwapisha Mabingwa hao wa ligi kuu 2015/2016 kumaliza mechi zao dhidi ya Ngaye De Mba ambao utachezwa Februari 10 nchini Comoro na kurudiana Februari 17 katika Uwanja wa Taifa.

  Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.Februari 10, mwaka huu, 

  Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.

  0 0

                        Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  SHIRIKA la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)  kupitia shirika linalosimamia Shughuli za mazingira kambi za Nduta na Mtendeli na Vijiji vinavyo zunguka kambi (REDESO) limekabidhi Pikipiki nne, Kompyuta moja  pamoja na mafunzo kwa Madiwani vyenye thamani ya shilingi milioni 16.8 kwa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko lengo ikiwa ni Kuwawezesha maafisa Wa Maliasili kupita katika maeneo ya misitu iliyo haribiwa na Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wanawake na Vijana.

  Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Kiongozi wa UNHCR Mratibu wa Mazingira idara ya Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Thobias Sijabaje,
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala katika Kikao cha baraza la madiwani kilicho andaliwa na REDESO kwa ajili ya kutoa tathimini , kukabidhi fedha na vifaa vya ofisi kwa maafisa wa Maliasili na madiwani kuelimishwa jinsi ya kutoa elimu kwa Wanawake na vijana juu ya utunzaji wa mazingira.

  Alisema  shirika la UNHCR kwa kupitia REDESO limeamua kutoa Vifaa hivyo na mafunzo kwa madiwani kutokana na hali ya uharibifu wa mazingira  ilivyo katika maeneo yanayo zunguka kambi za wakimbizi kutokana na ujio wa wakimbizi uliopelekea athari kubwa iliyopelekea misitu mingi kuharibiwa lengo ikiwa ni kutafuta ufumbuzi juu ya Suala hilo.

  "Kwa kuzingatia hilo tumeandaa mpango wa zaidi ya bilioni moja ya uhifadhi wa mazingira ilikuweza kushirikiana na halmashauri katika kutunza misitu , kwakuanzia tumeanza na vifaa ambavyo tumtetoa kwa wataalamu kuweza kufuatilia maeneo yaliyo haribiwa kwa kiasi kikubwa ilikuweza kupanda miti na kutoa elimu ya uhifadh wa mazingira kwa Wananchi",alisema Sijabeje.

  Alisema tatizo la mazingira katika kambi za wakimbizi huwa halikwepeki katika vijiji vinavyo zunguka kambi uharibifu Mkubwa umefanyika.Baada ya kuliona tatizo hilo linalo pelekea uharibifu wa  na uongozi wa  UNHCR kuweza kuangalia jinsi gani ya kutatua tatizo hilo,  na kuamua badala ya kutumia kuni na kujenga Nyumba kwa kutumia miti waliamua kubuni njia ya ufyatuaji wa tofari zinazo tumia udongo,chokaa na Simenti pamoja na kutengeneza majiko yenye uwezo wa o tumia kuni kidogo ilikuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira. ya

  Athari zilizo sababishwa na ujio wa wakimbizi ni pamoja na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya kambi zao na maeneo yaliyo jirani na kambi hiyo, kutokana na ukataji wa miti, uharibifu wa vyanzo vya maji na  kwaajili ya matumizi ya kujengea Nyumba za wakimbizi za kudumu na matumizi ya kuni kwaajili ya kupikia.

  Aidha  Mtaalamu wa Mazingira Taifa Dkt Braiton Gwamagobe alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuingia misituni na kukata misitu bila kujali madhala yanayo weza kujitokeza hali inayopelekea ukame na uharibifu wa tabaka la ozoni unaosababishwa na hewa chafu kutokana na kutokuwa na miti ya kutosha.

  Gwamagobe alisema  wakitaka elimu ya utunzaji wa misitu na mazingira ifanikiwe ni pamoja na kutoa elimu hiyo kwa Vijana na wanawake ambao ndio watumiaji wakubwa wa maliasili za misitu kutokana na nguvu kazi waliyo nayo  inayopelekea uharibifu wa  miti kwa kuchoma mkaa, ukataji wa mbao na kulima maeneo ya vyanzo vya maji.

  Alisema katika utafiti walio ufanya katika Wilaya ya kakonko wamebaini uharibifu Mkubwa umefanyika hasa katika maeneo ya Kambi za wakimbizi na vijiji vinavyo zungika kambi hizo, na baada ya kufanya tathimini walibaini wanao jihusisha na shughuli hizo wengi wao ni vijana ambao wakipatiwa elimu watasaidia kupambana na athari hizo.

  Akitoa Shukrani zake wakati akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala aliwashukuru UNHCR kwa kuthamini umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwawezesha maafisa wa maliasili kufanya shughuli za utunzaji wa mazingira na kutoa wito  kwa maafisa hao kuvitumia vifaa hivyo kwa kazi ya utunzaji wa mazingira na si kwa kazi nyingine.

  Alisema Vifaa hivyo vitumike kuwapatia elimu Wananchi wa Vijiijini jinsi ya kutunza mazingira ,kuzungukia maeneo ya liyo halibiwa kwa ukataji miti na sio vifaa vya kufanyia Shughuli zao binafsi ilikufikia lengo la uboreshaji wa mazingira kama mkakati wa UNHCR unavyo eleza
   Kiongozi wa UNHCR Mratibu wa Mazingira idara ya Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Thobias Sijabaje,akikabidhi funguo za Piki piki  kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko katika Kikao cha baraza la madiwani kilicho andaliwa na REDESO kwa ajili ya kutoa tathimini , kukabidhi fedha na vifaa vya ofisi kwa maafisa wa Maliasili na madiwani kuelimishwa jinsi ya kutoa elimu kwa Wanawake na vijana juu ya utunzaji wa mazingira.
  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala akipokea  Kompyuta moja  pamoja na mafunzo kwa Madiwani vyenye thamani ya shilingi milioni 16.8 kwa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko lengo ikiwa ni Kuwawezesha maafisa Wa Maliasili kupita katika maeneo ya misitu iliyo haribiwa na Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wanawake na Vijana.

  0 0

  Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma kwa mwaka 2017. Mafunzo hayo yatatolewa kwa Wanawake watakaotuma maombi na watakaochaguliwa katika Mikoa hiyo husika. Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa lengo la kuhakikisha wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kutuma maombi na kujisajili kupitia Tovuti ya http://www.manjanofoundation.org/
  Mafunzo hayo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali Mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato kupitia Tasnia ya Vipodozi. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
  Awamu ya pili ya mafunzo hayo itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano na elimu ya ngozi.

  0 0


  Msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ametangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa kata mbili za Ikweha na Igombavanu zote zikiwa jimbo pacha la Mufindi kaskazini, ambapo matokea yanaonesha kuwa chama cha mapinduzi CCM kimefanikiwa kutetea viti vyote viwili katika kata hizo. 
  Taarifa ya msimamizi wa uchaguzi kupitia kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya wilaya ya Mufindi, zinaonesha kuwa, katika kata ya Ikweha jumla ya watu waliokuwa mejiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 mianane 11, (3811) waliojitokeza kupiga kura ni elfu 02 miatatu na 07, (2307) ambapo mgombea wa CCM Bw.Albeto Chaula amepata kura elfumoja mianne na 05 (1405) sawa na asilimia 61% mgombea wa CDM Bw Ayubu Masika amepta kura mianane na 77(877) sawa na asilimia 38% huku mgombea wa CUF Bw. Meshack Manga akipata kura 25 sawa na asilimia 1%.

  Taarifa hiyo imeainisha pia matokeo ya kata ya Igombavanu, ambapo waliojiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 miambili 83 (3283) wakati kura zilizopigwa zilikuwa elfu 02 na 27(2027) kati ya hizo mgombea wa CCM Bw. Rashid Mkuvasa wamejikusanyia kura elfu moja miambili 83 (1283) sawa na asilimia 63% huku mgombea wa CDM Bw.Scholar Mitimingi amepata kura miasaba na 44( 744) sawa na asilimia 37%.

   Katika uchaguzi huo jumla ya kura 64 zimekataliwa  ambapo Ikweha ni kura 36 na Igombavanu kura 28. Aidha, zoezi la uchaguzi katika kata zote mbili lilikuwa la amani na utulivu. 
  Uchaguzi wa kata hizo, uliitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi baada ya kufariki kwa waliokuwa madiewani wa kata hizo mbili kupitia chama cha mapinduzi CCM ikiwa ni miezi michache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  0 0


  SIMU.TV: Baadhi ya wafugaji wilayani Mvomero mkoani Morogoro wamelalamikia vitendo vya kukamatwa kwa mifugo yao pindi wanapo wapeleka kunywa maji mtoni kwa madai kuwa wanaharibu vyanzo vya maji. https://youtu.be/R4dlr1Rio5I

  SIMU.TV: Chama cha mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi katika kata ya Kiwanja cha ndege manispaa ya Morogoro katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana. https://youtu.be/ApFoRgpx2eU

  SIMU.TV: Wananchi wa vijiji vya Mwabagimu na Bukumbi wilayani Meatu wamelalamikia kitendo cha kampuni ya udalali kubomoa nyumba 15 za familia 4 kufuatia amria ya mahakama kutoa mari ya kubomolewa. https://youtu.be/ZE8PCf1oO8A

  SIMU.TV: Tanzania na Uturuki leo zimetiliana saini mikataba tisa ya ushirikiano wa kibiashara na uchumi huku Uturuki ikieleza nia ya kukuza biashara zaidi baina yake na Tanzania. https://youtu.be/semJhuuviEo

  SIMU.TV: Kituo cha utengamano wa watu wenye ulemavu wilayani Monduli mkoani Arusha kinachotengeneza viungo bandia kwa watu wenye ulemavu kimeeleza kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa malighafi. https://youtu.be/z_B2puPH1ik

  SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa uongozi wa mkoa wa Njombe kutembelea viwanda vya chai vilivyopo mkoani humo ili kubaini changamoto inayowakabili wawekezaji hao. https://youtu.be/BetrWfUGG94

  SIMU.TV: Tawi la tatu la Benki ya Maendeleo inayomilikiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT limezinduliwa katika mtaa wa Kariakoo jijini Dar es Salaam. https://youtu.be/5csnwgx_vHU

  SIMU.TV: Zaidi ya wadau 300 wa kilimo wanakutana ili kujadili namna ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo na kumuinua mkulima. https://youtu.be/ztk_eFZz4ds

  SIMU.TV: Klabu ya soka ya Ndanda Fc imelitaka shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kushughulikia malalamiko yao dhidi ya timu ya Simba na Mbeya city kuhusu kuwachezesha wachezaji ambao hawana leseni za kucheza nchini. https://youtu.be/YclHQZhaSnI

  SIMU.TV: Droo ya kwanza ya shinda nyumba inayoongozwa na kampuni ya Global publishers kupitia magazeti ya Champion, Ijumaa na Uwazi inatarajiwa kuchezeshwa tarehe 8 mwenzi wa pili mwaka huu. https://youtu.be/Zc8as7q58ZU

  0 0

  Habari picha na Woinde Shizza,Arusha 
  Bendi mpya ya mziki wa dance ijulikanayo kwa jina la Mount Meru Ricknest music bandi imezinduliwa rasmi mkoani Arusha ikiwaahidi wapenda mziki wa dance burudani isiokuwa na mpinzani. 
  Akiongea na waandishi wa habari jana mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo Ernest mlolere alisema kuwa kwa sasa wameitambulisha bendi hiyo kwa wakazi wa mkoa wa Arusha tu na wanatarajia kuzindua bendi hiyo rasmi katika siku ya wapendanao (valentine day ) hapa hapa jijini Arusha. 
  Alibainisha kuwa bendi hiyo ipo chini ya wakurugenzi watatu akiwemo yeye mwenyewe Ernest Mlolere, Denis Kaiza pamoja na Prisca Aloyce ambapo wamekaa chini na wakaamua kuanzisha bendi hiyo ili kuweza kuwapa burudani wakazi wa mkoa wa Arusha ambao wamekuwa wakikosa burudani ya bendi ya uhakika kwa muda mrefu. 
  Alisema kuwa kumekuwa na bendi jijini hapa lakini zimekuwa hazikoshi nyoyo za wapenzi wao wa musiki wa dance hivyo wameona wawaletee wanamusiki wenye uzoefu, wenye vipaji vya kutosha ili wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na jirani kuweza kupata burudani. 
   Rais wa bendi ya  Mounti Meru Rickernest Music Band Fabrice Kinyenya (kulialia) Akiwa anaimba katika usiku wa kuwatambulisha bendi hiyo wakazi wa jiji la Arusha
   wanamusiki wa bendi ya Mounti Meru Rickernest Music Band wakiwa wanaonyesha kiwango chao ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha
   Wanenguaji wa bendi ya Mount meru Rickernest Music Band wakifanya yao. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
  0 0

  Ukibahatika kukutana na mnyama ambaye anaweza kubadili rangi na ama kuona taswira mbili kwa wakati mmoja hata ziwe pande tofauti  jitahidi kujifunza sana maana hiyo ni kama bahati ya mtende kuota jangwani .....huenda vizazi vijavyo vitakuulizwa maswali kwa njia ya PICHA tu kwani wanyama wengi adimu wanatoweka duniani na hakuna ajuaye mustakabali

  Kinyonga anaweza kuonekana wa kawaida katika macho ya wengi, lakini kwa wale wanaojali mazingira na urithi wa taifa hii ni kesi kubwa iwapo utamchukulia POA na wanalindwa na sheria za kimataifa za uhifadhi wa viumbe walio hatarini kutokweka (Convention on International Trade in Endangered Species) kama mojawapo ya viumbe WALIO HATARINI KUTOWEKA (mara yako ya mwisho kuona kinyonga ilikua lini?).

  Kinyonga ni moja ya wanyama wanaokwenda kuwa adimu sana duniani kuwaona kwa macho (naked eyes)

  1. Karibu nusu ya Vinyonga wameshatokweka duniani kwa mujibu wa sensa mbalimbali zinazofanyika kwa njia ya uratibu na sasa yasemekana Madagascar ndiyo nchi pekee yenye karibu aina zote za vinyonga WALIOSALIA (species) ambayo inakadiriwa kuwa 160

  2. Vinyonga walio wengi na hasa wanaopatikana Tanzania huweza kubadili rangi kutoka chanikiwiti hadi hudhurungi ama yakuti yasipii na samawi, ingawa ukweli ni kwamba kuna baadhi ya vinyonga wanaweza kubadilika kwa rangi yeyote ile kwa MUDA WA TAKRIBANI SEKUNDE 20 ....hii ni kutokana na kuwa na seli zinazoangazia kwenye ngozi zao zikiwa na uwezo wa kusharabu mwanga/ joto ama kwa kukereka (mood) na si kweli kwamba wanabadili kwa kuakisi mazingira kwa mujibu wa tafiti

  3. Jicho la Kinyonga lina uwezo wa kuona TASWIRA mbili kwa wakati mmoja (360 degree) hiki ni kiwango cha juu sana miongoni mwa reptilia na wana uwezo wa kuona wadudu wadogo sana umbali wa mita 5-10
  4. Kutokana na aina ya mihanjo yake ya kusakanya mkate wake wa kila siku, Urefu wa Ulimi wa Kinyonga ni MARA MOJA NA NUSU ZAIDI YA UREFU WA MWILI WAKE , ni ngumu sana iwapo wewe ni riziki ya Kinyonga ukakatiza mbele yake hata kwa sekunde moja.

  5. Miguu ya Kinyonga imeumbwa kwa namna ambayo inaweza kuparamia mazingira yoyote yale ya miti au miamba yaani iwe ya utelezi au hata miiba.....miguu yake inaweza kukunjika ama kukunjuka KAMA KARATASI kulingana na mazingira (si rahisi sana kuelezea hili zaili ya Muumbaji mwenyewe ) yatosha tu ufahamu ya kwamba Kinyonga anaweza kupita POPOTE PALE.Imeandaliwa na Geofrey Chambua Kutoka Vyanzo mbalimbali

  zaidi nenda


  0 0

  Imeelezwa kuwa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu unaosimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) utaanza rasmi kutekelezwa mwezi Februari mwaka huu. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mjini Dodoma wakati akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Ameongeza kuwa, katika utekelezaji wa Mradi huo, Serikali imepanga kuwakabidhi Wakandarasi watakaotekeleza mradi huo kwa Wabunge ili kuhakikisha kwamba mradi husika unatekelezwa kikamilifu.

  Wakati huo huo, Kamati hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wake Dotto Biteko imeipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa ukusanyaji wa Maduhuli kwa kipindi cha nusu mwaka na kueleza kuwa, mwelekeo wa ukusanyaji huo unakwenda vizuri.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akijibu hoja za Wabunge wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Medard Kalemani na Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Justin Ntalikwa wakifuatiwa na viongozi wengine wa Wizara na Taasisi zake.

  Awali, akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Nishati na Madini kuhusu upatikanaji wa fedha na utekelezaji wa majukumu kwa kipindi cha nusu mwaka kwa Kamati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa, ameeleza kuwa, hadi kufikia Disemba 31, 2016 Wizara ilikuwa imekusanya jumla ya shilingi bilioni 201.86 sawa na asilimia 54.46 ya lengo lililokusudiwa.

  “ Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato hayo yanatokana na vyanzo mbalimbali vikiwemo ada za kijiolojia, mrahaba, ada za mwaka za leseni, mauzo ya nyaraka za zabuni, mauzo ya gesi asilia, tozo ya mauzo ya umeme na shughuli za utafiti wa mafuta na gesi asilia,”amesema Prof. Ntalikwa.
  Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwa katika kikao cha maandalizi na kwa ajili ya vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini siku moja kabla ya kuanza kwa vikao hivyo.

  Aidha, akieleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Julai hadi Disemba, 2016 Prof. Ntalikwa amesema kuwa, Wizara imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati kulingana na mpango wake na kuitaja miradi kadhaa ikiwemo mradi wa Kusafirisha Umeme Msongo wa kilovoti 400 kutoka iringa hadi Shinyanga na kueleza kuwa, ulikamilika tarehe 28 Disemba,2016.

  “ Mradi wa Kinyerezi II wenye Megawati 240 utekelezaji wake umefikia asilimia 29 na Serikali imekwishatoa mchango wake wote wa asilimia 15 sawa na shilingi bilioni 110 na mradi huu unategemewa kukamilika mwaka 2018,” amesisitiza Prof. Ntalikwa.

  Akizungumzia Mradi wa Kinyerezi I, Extension ya Megawati 185 ambao ni mwendelezo wa upanuzi wa Mradi wa Kinyerezi 1, ameeleza kuwa, mradi huo unaendelea kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

  Akizungumzia uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, ili kukuza utendaji wao, Wizara inaendelea na hatua za uanzishwaji wa vituo vya mfano vitano katika Wilaya za Kilwa, Mpanda, Chunya na Bukoba kwa ajili ya wachimbaji wadogo.

  Ameongeza kuwa, vituo hivyo vitatumiwa na wachimbaji hao kuchenjua madini yao na kujifunza namna bora ya kuendesha migodi yao kitaalam na kwa tija zaidi.
  Kaimu Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga, wa kwanza kulia akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Felix Ngamlagosi, na Mtaalamu kutoka Ewura wakibadilishana jambo kabla ya kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Watendaji Wakuu wa wizara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMIZO), Mhandisi Hamisi Komba akijibu hoja ya Wajumbe wa kamati wakati wa kikao kati ya Wizara na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini mjini Dodoma.

  0 0
  0 0

  Na  Bashir  Yakub.
  Sheria   inaruhusu  kutumia  ardhi  ya  mtu  kukopea.  Kwa  maana  mtu  ataomba  hati  yako   au  nyaraka   yako   yoyote  ile  ya  umiliki  halafu  ataitumia  kukopea. Inaitwa Rehani  ya  mtu  wa  tatu( third party mortgage).   Kifungu  cha  113 ( 2 ) cha  Sheria  ya  Ardhi  Na, 4 ya 1999  kimeeleza kitu  hiki. Hata  hivyo  yapo  mambo  tunayotakiwa  kujua  katika  mchakato  huu  wote. 
  Ili  mambo  yaende  vizuri  kutatakiwa kuwapo  mikataba  ya  aina  tatu  kama  tutakavyoona  hapa  chini.

  1.MKATABA  WA  MKOPO. 
  Mkataba  wa  mkopo  ( Loan  agreement)  ni  mkataba   kati  ya   mwomba  mkopo  na   na  taasisi  ya  fedha  inayotakiwa  kutoa  mkopo.  

  Mkataba  huu  utakuwa  na  masharti   ya   mkopo  kuhusu  urejeshaji, muda  wa  kurejesha, viwango  vya  riba,  adhabu  za  kupitisha  muda  wa  rejesho, muda  ambao  mkopo  utadumu,  nini  kitafanyika  iwapo  mkopaji  atashindwa  kurejesha, haki  na  wajibu  wa  mkopaji  pamoja  na  mkopwaji.

  Ifahamike kuwa  masharti  ya  mkopo    hayafanani.  Yanatofautiana  kutoka  taasisi  hadi  taasisi   na  pia yanatofautishwa  na  kiwango   cha  mkopo  pamoja  na  mazingira  yote  yanayouzunguka huo  mchakato. Huu  ni  mkataba  wa  kwanza.

  2.   MKATABA  WA   REHANI.

  Huu  ni  mkataba  wa  pili. Mkataba  wa  rehani ( mortgage deed ) utakuwa  ni  kati  ya  taasisi  ya  fedha  na  mtu  anayeweka  rehani. Kwahiyo  kama  wewe  unamdhamini  mtu  kwa  kumpa  nyumba  au  shamba  lako  ili  akakopee   basi  unatakiwa  kusaini  mkataba  huu.  

  Yule  ambaye  jina lake  linaonekana  kwenye  nyaraka  ya  umiliki  ndiye  anayetakiwa  kusaini   mkataba  huu.   

  3.   MKATABA  KATI  YA   ANAYEDHAMINI  NA  ANAYEDHAMINIWA.

  Aidha  usimkabidhi  mtu  hati  yako  akakopee  bila  kuwa  na  makubaliano  ya  kisheria na  huyo  mtu.  Ni  hatari  sana  kufanya  hivi   na   unaweza  kupoteza  na  wengi  wamekwishapoteza.  
  Wengi  wanachojali  ni  mtu  achukue  hela  benki  na  wewe  akupe  asilimia  zako  mlizokubaliana  basi  muishie  hapo.  Ukifanya  hivi  utakuwa  umekosea  sana.

  Wengine  huaminiana  tu  kwa  urafiki  au  undugu  na kufanya  mchakato  huu  bila  makubaliano  maalum.  Hii  si  sawa  na  ina  madhara  makubwa.

  Hakikisha unamsainisha  mkataba  huu na  hakikisha  mkataba unakuwa  na  vipengele muhimu na  vya  kisheria  vya  kukulinda  wewe na  mali  yako. 

  Moja  ya  kipengele  muhimu  ni kueleza  wazi  ikiwa  atashindwa  kulipa  deni  huko  alikokopa  ni  kitu  gani   kitakulinda  ili  mali  yako  isiuzwe   au  hata  ikiuzwa  wewe  utapata  nini  kutoka  kwake  kufidia  hiyo  hasara.


older | 1 | .... | 1525 | 1526 | (Page 1527) | 1528 | 1529 | .... | 3353 | newer