Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1527 | 1528 | (Page 1529) | 1530 | 1531 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Mkuranga.

  KIJIJI cha Wasanii cha Mwanzega kimechaguliwa kuwemo kwenye orodha ya vijiji saba ambavyo vimepangiwa kupata umeme wa Serikali wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA).

  Mtendaji wa kijiji cha Mwanzega, Kitwana Kambangwa aliwaomba wanakijiji wasipuuzie fursa hiyo kwa vile serikali imeona umuhimu wa kijiji hicho kupata umeme ili kurahisisha maendeleo.

  Akiwasomea wananchi taarifa ya Mratibu wa Vijiji na Kata wa Utawala bora na maboresho wa wilaya ya Mkuranga kuhusu mradi huo, Mtendaji wa kijiji, Kambangwa alisema wananchi wewe tayari kutoa miti yao ya mazao na mimea bila fidia ili kupisha kazi ya kupitisha nguzo za umeme wa REA.

  'Ndugu zangu Serikali ya Rais John Magufuli imetusikia kilio chetu sisi watu wa vijijini, tunaletewa umeme ili tuwe na maendeleo kama wenzetu wa mjini, tusiipuzie nafasi hii kubalini kupisha nguzo zipite bila kulalamikia fidia' alisema Mtendaji Kambangwa.

  Alisema sambamba na kijiji cha Mwanzega, vijiji vingine vitakavyonufaika na mradi wa REA ni Mbezi, Msorwa, Shungubweni, Boza, Kuruti na Mbonga ambavyo mradi huo utapelekwa moja kwa moja kwenye shule za Msingi, Zahanati, Viwanda na Shule za Sekondari.


  Mkazi wa Mwanzega Dkt. Frederick Mwakibinga akichangia mada kwa wanakijiji watakaonufaika na mradi huo baada ya kuukubali.

  Wanakijiji wa kijiji cha Wasanii Mwanzega Mkuranga wakiwa kwenye mkutano wa kuidhinisha mradi wa Ilene wa REA kupita kijijini hali jana.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua mambo mbalimbali mapema leo kwenye Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam,kuhusiana na ushindi wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali zilizofanyika hivi karibuni,za Madiwani na nafasi ya Ubunge huko Zanzibar.

  Katika mkutano huo na Waandishi wa Habari, alielezea siri tatu muhimu zilizokiwezesha Chama hicho kupata ushindi, Polepole alizitaja siri ya kwanza ni namna ya mageuzi mapya ya kimuundo na mfumo yaliyolenga kukiwezesha CCM kurudi kwenye mikono ya wananchi kwa serikali yake kujikita zaidi kushughulikia kero zinazowakabili Watanzania na kufanikiwa.

  Pole Pole alisema kuwa mabadiliko hayo yamelenga kukirejesha chama wenye misingi uliokifanya kuanzishwa kwake,akabainisha siri ya pili kuwa ushindi huo ni matokeo ya mafanikio ya serikali katika kuweka mikakati ya kubana mianya ya wakwepa kodi pamoja na vita dhidi ya ufisadi.

  “Adui yetu mkubwa ni rushwa na vitendo vya ufisadi nchini, Watanzania ni mashahidi kwani muelekeo wa serikali umekuwa thabiti na tumeona watuhumiwa wa vitendo hivyo wakichukuliwa hatua,” alisema.Alisema kuwa siri ya tatu imetokana na kazi nzuri ya utendajikazi wa serikali kwenye utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Chama.
  Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Ndugu Pole Pole alipozungumza nao mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.

  Katika hatua nyingine,Pole Pole alisema kuwa ahadi ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne, imekuwa na uhalisia mkubwa.“Na zaidi ya yote ni huduma za kiuchumi ambazo zimeendelea kutekelezwa ambapo Chama tunaipongeza serikali na kuikumbusha katika maeneo mengine tuliyowaahidi wananchi, ikiwemo kuendelea kutenga asimilia 10 ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya vijana na wanawake.

  “Hii itatoa nafasi kwa vijana na wanawake kupata fursa za mitaji na mikopo yenye masharti nafuu, hivyo suala hilo linapaswa kuwekewa msisitizo zaidi,” aliongeza.Alisema serikali inaendelea na mipango ya ujenzi wa viwanda, vinu vya usagaji mkoani Iringa na Mwanza pamoja na kiwanda cha mafuta ya Alizeti, mambo ambayo tayari Chama kimetoa maelekezo kwa serikali.


  0 0

  Na Zainab  Nyamka, Globu ya Jamii.

  Kikosi cha Azam kinatarajiwa kuingia kambini kesho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba utakaofanyika Januari 28 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru.

  Akizungumzia maandalizi kuelekea mtanange huo, Kocha wa muda  wa timu ya Azam Iddi Cheche  amesema wamejianda vizuri kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba ambao umekuwa  wa ushindani sana kutoka kila timu kutaka matokeo mazuri mbele ya mwenzake.

  Katika mchezo wa raundi ya kwanza Simba walifanikiwa kutoka na ushindi waq goli 1-0 lakini kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi mapema mwezi huu Azam waliweza kulipa kisasi kwa kuifunga goli 1-0.

  Cheche  ameweka wazi kuwa Simba ni timu kubwa na tunapokutana na timu kubwa basi lazima wachezaji wacheze kwa umakini  ili wasifanye makosa na zaidi hakuna timu inayopenda kufungwa mara mbili mfululizo kwahiyo tunajua mbinu za kutumia ili kuweza kuondoka na ushindi.

  “Kikubwa tutajituma kwa kila hali tupate matokeo mazuri mbele ya vinara hao wa ligi kuu, licha ya kuwa  na matatizo makubwa  katika safu ya ushambuliaji  ambayo imekuwa haina umakini,” alisema Cheche.

  Kwa sasa wachezaji wa Azam wamepewa mapumziko baada ya kumaliza mchezo wa Kombe la Shirikisho FA dhidi ya Cosmopolitan uliofanyika jana na Azam kutoka na ushindi wa goli 3-1.

  Kocha wa Muda wa Azam Fc Iddy Cheche


  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

  Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimeiomba Serikali kuongeza nguvu na kuhakikisha matumizi ya tiketi za elekroniki katika sekta ya usafirishaji nchini yanakuwa ya lazima.

  Hayo yamesemwa na Afisa Msimamizi wa Chama hicho ambaye anasimamia Mkoa wa Dar es Salaam Mark Serra, alipokuwa akisoma taarifa ya chama hicho kwa waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam.

  “Chakua imekuwa ikifuatilia kwa karibu mfumo huu na kubaini una manufaa makubwa sana kwa abiria ambapo watatozwa nauli halali iliyoidhinishwa na Sumatra ambazo ndizo bei elekezi kwa mujibu wa sheria,” alifafanua Serra.

  Aliendele kusema kuwa kwa kutumia tiketi za Kielekroniki itawalazimu wamiliki wa vyombo vya usafiri kutokupandisha nauli katika kipindi cha mvua au jua kali, kipindi cha wanafunzi wapotoka vyuoni au mashuleni pamoja na kipindi cha sikukuu au mwanzoni mwa mwaka, ambapo mabasi mengi huita vipindi hivyo ni vya kuvuna abiria.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Mchanjama amesema kuwa mfumo huo utamnufaisha abiria na kuokoa muda wa kwenda kwenye vituo vya mabasi kwa ajili ya kukata tiketi badala yake mfumo huu utamuwezesha abiria kukata tiketi akiwa nyumbani, ofisini au sehemu yoyote aliyopo kwa kutumia simu yake ya mkononi.

  Aliongeza kuwa mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za abiria pindi inapotokea ajali kujua abiria wangapi wamepoteza maisha, waliopata ulemavu pamoja na waliopoteza mali zao, ambapo kwa mfumo unaotumika sasa hivi ni vigumu kupata takwimu na taarifa sahihi za abiria.

  Hivyo basi kupitia mfumo huo wa kielekroniki CHAKUA itakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutekeleza jukumu lake la kumtetea abiria pindi anapopata tatizo kwa kuwa itakuwa na taarifa sahihi za abiria.

  0 0

   Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  SHIRIKISHO la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeufungia uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kuchezwa mechi za ligi kuu na daraja la kwanza hadi utakapofanyiwa marekebisho.

  Uwanja huo unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi mkoa wa Morogoro umekosa vigezo vya kutumika kwenye ligi kutokana na miundo mbinu yake hasa sehemu ya kuchezea kutofaa hivyo kuanzia leo hautatumika hadi utakapofanyiwa marekebisho.

  Uwanja huo hutumika kwa mechi mbili tu za ligi zinazohusisha timu za Simba na Yanga zinapocheza na Mtibwa Sugar kutokana na uwezo wake wakuingiza watu wengi kwakua miamba hiyo ya soka nchini ina mashabiki lukuki.

  Mechi namba 151 (Mtibwa Sugar vs Simba). Baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari. Pia kamera ya Azam Tv upande wa goli la Kusini iliangushwa na washabiki hao.

  Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas alisema katika mchezo kati ya Mtibwa na Simba uliofanyika uwanjani hapo wiki mbili zilizopita ulikosa mvuto na kuzifanya timu hizo kushindwa kuonyesha kandanda safi kutokana na ubovu wa dimba hilo.

  TFF imebaini kuwa kitendo cha washabiki kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho, licha ya kuwa ni kinyume cha kanuni lakini pia kilichangiwa na askari polisi kutokuwa makini katika majukumu yao ya kusimamia usalama uwanjani na badala yake kuelekeza umakini katika kutazama mechi.

  Vilevile sehemu ya kuchezea (pitch) ya Uwanja wa Jamhuri iko katika hali mbaya ambapo inahitaji marekebisho makubwa ili iweze kuendelea kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.

  Hivyo, Uwanja umesimamishwa kutumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom ili kutoa fursa kwa wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea (pitch), na pia askari polisi kupata maelekezo ya kutosha ya jinsi ya kusimamia usalama uwanjani badala ya kutazama mechi. Kama marekebisho hayatafanyika, uwanja huo hautatumika kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom.
  Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas

  0 0


   Na Anthony Ishengoma-MCDGC.

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha Dawati la Ulinzi la na Usalama katika shule zote  pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya Kata na Vijiji Nchini kote ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema hayo wakati akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu cha Baraza la Watoto la Taifa kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Morogoro.  Aidha amewataka wajumbe wa Kikao hicho kujadiliana kwa kina juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao Wizarani  akisema kuwa hivi karibuni vitendo hivyo vimeongezeka kwa wingi sana katika Jamii.  Aliongeza kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa Kupambana na Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa miaka mitano Serikali itahakikisha vitendo vya ukatili vinapunguzwa kwa asilimia hamsini kupitia mpango kazi huo na kuongeza kuwa vitendo vya ukatili kwasasa vinatofautiana viwango akitaja ukatili huo kuwa ni ubakaji, ulawiti, ukeketeji, mimba na ndoa za utotoni.  Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa  Caroline Augustino akiongea na vyombo vya Habari baada ya ufunguzi huo kuwa pamoja na kukutana leo jijini Morogoro pia Baraza hilo limefanya ziara mbalimbali mikoani kwa lengo la kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya radio na runinga ili jamii iweze kufahamu maana  na aina za ukatili dhidi ya watoto.
   Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis akiongea na wajumbe wa baraza hilo katika kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro,Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Caroline Augustino.
   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa na kuwapongeza kwa kazi wanazoendelea kuzifanya kwa maslahi ya watoto nchini Leo Mjini Morogoro, Kulia ni Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa ambapo aliwataka katika agenda zao wajadili ukatili dhidi ya ubakaji na ushoga na hatimaye wampelekee taarifa ili kujua nini serikali ikifanye, Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai 


  0 0


  Kama inavyojulikana kuwa Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2016 Jihan Dimack aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi wa kumi na moja mwaka 2016 aliondoka nchini tangu tarehe 11 Januari kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe kwa ngazi ya kimataifa .

  Jihan Dimack akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni yupo nchini Phillipines kwa muda wa wiki mbili sasa akiiwakilisha vyema Tanzania katika kuwania taji hilo.

  Mashindano haya ambayo yanazingatia vigezo mbalimbali pia yana utaratibu wa upigaji kura ambao umeshaziduliwa rasmi tangu tarehe 23 Januari 2017 na kura zitapigwa ndani ya siku sita hadi tarehe 30 Januari 2017 ambayo ndo finali za mashindano hayo.

  Utaratibu uliowekwa na uongozi wa Miss Universe mwaka huu ni kwamba kutakua na warembo 12 bora na kati ya hao kumi na mbili mrembo mmoja ataingia kwa kigezo cha kupata kura nyingi kupitia mtandoni.

  Hivyo basi Watanzania wote kwa pamoja tushirikiane katika hili kuhakikisha mrembo wetu kutoka Tanzania Jihan Dimack anapata kura za kutosha kumuwezesha kuingia katika fainali hizo.

  Itakua jambo la faraja sana kufanikisha ushindi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kupiga kura kwa wingi na kila mtu mmoja ana uwezo wa kupiga mpaka kura kumi kwa siku. Ushindi wa mrembo wetu upo mikononi mwetu wenyewe.

  Ili uweze kumpigia kura mrembo wetu Jihan utatakiwa kufanya mambo machache yafuatayo:

  Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:
  1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
  2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
  3) MISS U APP: Pakua Miss U app 
  4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu. 

  Tafadhali kumbuka kwa kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.
  ***Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa.  0 0


  0 0


  Na Woinde Shizza,Arusha

  Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

  Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .

  Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani.

  Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo. Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february 6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

  Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho. Alisema ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

  0 0


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird.
   Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (wa pili kushoto aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya mazungunzo na Waziri huyo alasiri.
   Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kushoto) akinywa maji ya dafu  alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0

  Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiweka kando shughuli nzito za kujenga Taifa na kubeba majukumu ya mzazi kwa kuketi chini na kumfumua nywele binti yake Aziza Tamika Kikwete kabla ya kusukwa upya nyumbani kwake Chalinze. 
  Mhe Ridhiwani ameiambia Globu ya Jamii kwamba kwake yeye hilo ni jambo la kawaida kabisa kwani anasema anatambua umuhimu kwa viongozi kupata muda na kukaa na familia nyumbani kwani kuna maisha baada ya uongozi. Aziza mwenye unri wa miaka 7 na ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mhe. Ridhwani, kachukua jina la bibi yake yaani mama wa baba yake.

  0 0

  Picha za awali za wahusika wa waraka huu ikiwa ni pamoja na watoto Amina na Seleman Kichawela na Bw. Mahmud Hassan Mihile aliyewachukua miaka 22 iliyopita ili kuwasaidia masomo huko Uingereza.

  Kutokana na kichwa cha habari hapo juu mimi AZAMA ABBASI KICHAWELE ambae kwa sasa ni mjane, mwenye namba ya simu +255 784 697319 na mkazi wa Majengo Arusha, Tanzania, na ambae ni mama wa nyumbani, nachukua nafasi hii kukutaarifu kama ifuatavyo.
  Mume wangu kwa majina ABBASI ALLY KICHAWELE ambaye kwa sasa ni marehemu alikua na rafiki wake wa karibu kwa majina MAHMUD HASSAN MIHILE aliekuwa akitumia namba ya simu +441332270462 wakati huo mwenye asili ya Kisomali na uraia wa Uingereza na Tanzania walikubaliana awachukue watoto wetu ambao ni: SELEMAN ABBASI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka kumi na AMINA JABIRI KICHAWELE aliekuwa na umri wa miaka saba aende nao Uingereza kwa ajili ya kuwasomesha.
  Siku ya kuondoka watoto hawa ilikuwa ni mwaka 1994 na waliondoka na mke wa huyo Msomali kwa majina RAHMA MIHILE.
  Mji wa kwanza walioshukia huko UINGEREZA unaitwa LEICESTER.
  Baada ya hapo mawasiliano yaliendelea kuwepo kati ya mzazi wa kiume wa watoto na Msomali.
  NB: Katika hawa watoto huyu wa kike, Amina Jabiri alikuwa ni wa mdogo wake mume wangu yaani shemeji yangu.
  Kwa bahati mbaya mume wangu, aliugua maradhi ya cancer na ilipofika mwaka 1998, nikampoteza (alitangulia mbele ya haki)
  Baada ya kifo cha mume wangu hakukua na mawasiliano yoyote kati yangu na huyu bwana aliyechukua watoto wangu. Alikata mawasiliano kabisa na wala hakutaka watoto wajue kuwa baba yao hayupo tena Duniani.
  Kwa bahati mbaya sikua na mtu mwingine mbadala wa kuweza kuniunganisha na huyu bwana ikizingatiwa pia mimi ni mama wa nyumbani sikuwa na PR kubwa.
  Leo hii ninapoandika barua hii, huu ni mwaka wa ishirini na mbili (22) toka nitengane na watoto wangu. Sisi pamoja na wanafamilia tutaendelea kutoa shukrani zetu kwa serikali ya Uingereza iwapo watoto hawa wapo salama na kwenye ajira zao. Kwetu hilo sio tatizo.
  Jambo kubwa linaloniumiza ni kutokua na MAWASILIANO na watoto wangu kwa miaka ishirini na mbili sasa. Wakati mwingine najenga wasiwasi kwamba je, wako hai? Na hali hii nitaendelea nayo mpaka lini? 
  Huyu bwana Mahamudu (msomali) nini kimemsukuma kuwa na ujasiri wa kuwaficha watoto wangu hata nisiwe na mawasiliano nao? Ana dhamira gain?
  Kutokana na maelezo mafupi hapo juu nimefikia hatua ya kuiomba ofisi yako tukufu kunisaidia kupata namna ya kuwasiliana na watoto wangu wapendwa huko waliko. Jambo hili likifanikiwa litaleta faraja sana kwangu na kwa wana familia kwa ujumla.
  Pia itakuwa ni fursa kwa watoto kutambua kuwa baba yao mpendwa alishafariki lakini mimi mama yao bado nipo hai, taarifa ambazo tuna hakika hawajazipata. Naambatanisha picha za watoto ambazo walipigwa wakati wanakaribia kuondoka mwaka 1994.
  Pia naambatinisha na picha ya Mahmud Hassan Mihile (Msomali) ya wakati huo aliyewachukua watoto kwa makubaliano na mume wangu.

  NB: Kwa mawasiliano tumia namba hizi za barua pepe
  Au Athuman Rashid Mfinanga
  Box 2614, - Arusha Tanzania
  Ph: 0754375602/0784375602

   
  Wako,
  Katika ujenzi wa Taifa
  Azama Abbasi Kichawele

  0 0


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambapo jumatano hii tarehe 25 Januari 2017 atawapatia wakazi wa kijiji cha Kinywang’anga Iringa vijijini.

  Katika ziara hii Mhe. Lukuvi atakutana na wananchi hao waliopimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba ambao kwasasa hati zao za umiliki wa ardhi hizo zimeishaandaliwa na  ziko tayari kukabidhiwa kwao.

  Ziara hii ni katika utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi wenye lengo la kufanyika kwa nchi nzima. Utekelezaji huo utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo  mengine yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.

  Sambamba na hilo, Matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na kukamilika.
  Aidha mpango huu unalenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

  Serikali ya awamu ya tano imeweka adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba. Imeandikwa na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ardhi).
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (mwenye suti nyeusi) akitatua moja ya mgogoro wa ardhi mkoani Iringa.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim katika ziara yake mkoani Arusha,Gambo ameiomba UNEP kusaidia fedha mradi wa kulinda chanzo cha maji cha Olgilai kilichopo wilayani Arumeru kinachotumika kusambaza maji jijini Arusha ambacho kimesongwa na shughuli za binadamu kikiwemo kilimo na upandaji miti ambayo sio rafiki na vyanzo vya maji. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim akiwa na ujumbe wake wakifatilia mada iliyowasilishwa na Meneja wa Baraza la Mazingira Kanda ya Kaskazini (NEMC) Novatus Mushi. 
  Mratibu wa kitaifa wa UNEP nchini, Clara Makenya akizungumza jambo kwenye ziara hiyo,kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro. 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim (kushoto kwake) naa maafisa wengine wa UN pamoja na ofisi ya Mkuu wa mkoa. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim (mwenye tai) akiangalia chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiri jijini Arusha (AUWSA) eneo la Olgilai Kata ya Kiutu alikofika kuangalia uharibifu wa chanzo hicho. 

  0 0
  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. John Ndunguru, amewaasa Wakurugenzi wa Halmashauri wa Mikoa Minne wanaoshiriki Warsha Mkoani hapa, kutumia vema fedha wanazopelekewa ambazo ziko chini ya Mfuko wa LDGD ili Serikali iweze kufikia lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Dkt. Ndunguru ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii wakati akifungua Warsha ya siku tatu ya utambulisho wa Miongozo Mikuu ya Mfumo utakaotumika katika Kuzipatia Ruzuku ya maendeleo Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini.

  Amesema, Wakurugenzi wanapashwa kusimami miongozo hiyo iliyotolewa na ambayo wataelekezwa wakati wa warsha hiyo ili kuhakikisha kuwa malengo ya uanzishwaji wa Mfumo huo yanatekelezwa ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Aidha, Dkt. Ndunguru amewataka Wakurugenzi hao kuacha mazoea ya kubaki na fedha nyingi za Mfuko wa LDGD bila kuzitumia kwa wakati, jambo alilosema linawacheleweshea wananchi maendeleo wanayoyahitaji.

  “Usifikiri kuziweka hela kwamba ni utendaji kazi mzuri…na wewe ni jipu. ukitumia fedha hizo vibaya ni jipu, lakini pia ukiziacha bila kuzitumia ni jipu jingine tena jipu baya zaidi kwani unawakosesha wananchi huduma” alisisitiza Dkt. Ndunguru.

  Nae Mshauri Mkuu kwa niaba ya Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini (JICA) Bw. Michiyuki Shimoda, amewataka washiriki wa Warsha hiyo kujifunza kwa umakini miongozo inayohusu “Local Gornvement Development Grant” ambayo itapitiwa katika kikao hicho. Amesema wanatakiwa kuwa makini katika kujifunza miongozo hiyo kwa kuwa wao ndio watumiaji wakubwa nia ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa Utawala Bora OR – TAMISEMI Dkt. Charles Mhina, amesema lengo la warsha hiyo ni kutoa Elimu ya namna ya kufanya ufuatiliaji wa shughuli zote ambazo zinafadhiliwa chini ya Mfuko wa LDGD.

  Warsha hiyo ya Siku tatu inafanyika katika Ukumbi wa Edem katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na inashirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Uchumi, baadhi ya Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekretarieti za Mikoa, Waweka Hazina na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa minne ya Dodoma, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt.John Ndunguru akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri wa mikoa minne walioshiriki Warsha Mkoani hapo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt.John Ndunguru wa nne kutoka kulia walio kaa na wa pili kutoka kushoto ni DKT.Charles Mhina akiwa na wakurugenzi wa Halmashauri katika picha ya pamoja.

  0 0

  Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

    Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa amezindua Maendeleo Bank Kariakoo jijini Dar es salaam huku akitoa pongezi kwa watumishi wa Kanisa kwa kuweza kuamua kuwasaidia Watanzania katika kuweka pesa zao katika bank hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia uzinduzi huo Askofu Dkt.Alex Malasusa,amesema kuwa ni wakati wa Watanzania kuacha kufisha pesa nyumbani na kuweka kwenye vibubu kwani bank hii itaweza kuwasaidia katika kazi zao pindi wanapokuja kuweka pesa au kuomba mkopa.

  “Hii Maendeleo bank ni ya watu wote haichague dini kwa hiyo mtu yoyote anweza kufungua Account kwa lengo la kutunza pesa zao na pia amewaasa watanzania kuwa na nidhamu ya pesa kwani wataweza kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya dini pamoja na sheria za nchi”amesema Askofu Dkt.Alex Malasusa

  Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji Mr.Ibrahim Mwangaleba amesema kuwa Maendeleo bank ni ya watu wote wa dini zote na inawakaribisha wateja waje kuweka pesa zao katika mahali salama na haitakuwa na ubanguzi wowote japokuwa ni ya Kikristo.

  “Sisi tumeamua kufungua tawi la Maendeleo bank katika eneo la Kariakoo na tunaamini kwa imani kuwa hii itakuwa bank kubwa kuliko tawi lolote hapa jijini Dar es salam na itakuwa bega kwa bega na wateja watakaokuja kuchukua mkopo kwani hapa Fedha zitakuwa na maombi kwa lengo la wateja kwenda kuwa na maendeleo ya hali ya juu”amesema Mwangaleba.
  WEK
    Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es Salam, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama (kulia). 
  WEK 1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi ya wateja wa kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo. 
  WEK 2
  Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa  akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya la Maendeleo banki, Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Amulike Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch. Frank KImambo
  WEK 3
  Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 1527 | 1528 | (Page 1529) | 1530 | 1531 | .... | 3353 | newer