Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1519 | 1520 | (Page 1521) | 1522 | 1523 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  WAZIRI Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,amesema kuwa anafanya harakati za kapambana na kazi za wasanii ziweze kupata heshima na pamoja na masilahi kwa wasanii hao hili waweze kujiongeza kipato.

  Nape ameyasema hayo leo wakati alipokutana na Wasanii juu ya masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya filamu, amesema wasanii wanafanya kazi ngumu lakini hawanufaiki na kazi wanayoifanya huku jamii ikiona mafanikio.

  Amesema katika kazi za filamu ziweze kupata heshima kunahitajika kutengeneza sera ambayo itamaliza malalamiko ya wasanii na wawekezaji wanaweza kuwekeza katika katika sekta hiyo.

  Nape amesema kuna watu wanakuja kutaka kuwekeza katika sekta ya filamu kutokana na kutokuwepo kwa sera wawekezaji hao wanakimbia na kwenda nchi nyingine zilizoweka sera.Aidha amesema kupatikana kwa sera kutapunguza maharamia wanaofanya kazi wasanii na kujipatia kipato kikubwa kuliko wale wanaofanya kazi halisi.

  "kazi za wasanii ambazo hazina stika ziko katika maghala ya TRA na kati hizo za wasanii zina kesi mahakamani.Nape amesema katika juhudi hizo kumekuwa na maneno kwa baadhi ya wasanii ya kumpiga vijembe huku akiwa anafanya kazi ya kukamata kazi hizo kwa gharama yake mwenyewe" amesema Waziri Nape.

  Hata hivyo amesema katika kupambana na maharamia baadhi ya wasanii wanashirikiana na ambao wameshiriki mkono na taarifa zote za mkutano huo wanaupata lakini hatajali na operesheni zingine zitaendelea.

  Hata hivyo ameitaka baraza la Sanaa la Taifa Basata kusajili kazi za wasanii licha ya kuwepo kwa sheria za ovyo ovyo.Katika Mkutano huo ubwabwa ulionunuliwa kwa wasanii na kuliwa uwanja wa taifa unadaiwa kutolewa na maharamia wa kazi za wasanii ambapo Waziri Nape amepinga kuwa hakuna kitu kama hicho.

  Waziri nape amewatahadharisha wasanii ambao wanajiona wana majina na kushindwa kushiriki mkutano huo na kufanya wasanii waliofika kuwa wao ndio wanashida huku akitaja kuwa jambo hilo ni la wasani wote hivyo kila mtu anapaswa kushiriki.
  Wadau wa Sekta ya Filamu wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye alipokutana nao leo Jijini Dar es salaam. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 
  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia mashine ya kudurufu santuri za muziki na video wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 
  Baadhi ya Wasanii wakiangalia kazi haramu za wasanii zilizokamatwa kwa wasambazaji zilizopo katika ghala la kampuni ya madalali ya YONO iliyopo Ilala Bungoni. 


  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jina Jipya na Nembo Mpya yenye alama ya Kipepeo, (Tpb Bank Plc) vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania Plc, kuanzia Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Prof. Lettice Rutashobya na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi, wakiangalia Jina Jipya na Nembo Mpya iliyobuniwa na Benki hiyo baada ya kuizindua rasmi  Januari 19, 2017, Tukio lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, (wa pili kulia), akimpongeza Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, kwa kazi nzuri ambayo benki hiyo imefanya kubuni Jina na Nembo Mpya itakayoanza kuitambulisha Benki hiyo katika biashara ya Sekta ya Fedha kuanzia Januari 19, 2017, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akitoa hotuba kabla ya kuzindua rasmi Jina Jipya na Nembo vitakavyo tumiwa kibiashara na Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), kuanzia  Januari 19, 2017. Tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.

   Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (Tpb Bank Plc), Bw. Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba ya mafanikio ambayo Benki yake imeyapata katika biashara ya Sekta ya Fedha ikiwemo kukuza mtaji, kupata faida na kufanikiwa kubuni Jina Jipya na Nembo Mpya ya Kipepeo, itakayoanza kutumika kuanzia leo Januari 19, 2017, baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Balozi mteule Dkt. Abdallah Possi

  0 0
  0 0


  BEI ZETU NI NAFUU KULIKO BURE
  Only £1.75 per kg
  Fridge £70
  Cooker £60
  W/machine £60
  Ukiwa na mzigo mkubwa tunaelewana tu, Hata matofali leteni tu. Hatuachagi kitu sisi!
  Bei zetu ni pamoja na. ushuru na haulipi kingine tena. 
  Tupigie:
  KC GLOBAL LINKS
  SUITE 2 CLIPPER HOUSE
  TILBURY DOCKS
  RM18 7SG
  KAZI NI KIPIMO CHA UTU  0 0

  Kiongozi wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa Bi Mayrose Kavura Majinge, siku ya Jumamosi Jan 14, ameweza kushirikiana na wadau mbali mbali jijini hapa Washington kwa lengo la kuinua Maendeleo Maalum ya Maadili Kitaifa, yaliyoanza rasmi kufanyika mwezi huu Januari hadi Disemba 2017, kwa lengo la kuinua na kudumisha maadili ya Watanzania ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazodhoofisha mfumo wa muundo wa jamii yetu ya Kitanzania.

  0 0


  0 0

  Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/17 (Azam Sports Federation Cup - ASFC), utaanza Jamamosi Januari 21, 2017 kwa timu za Majimaji na Mighty Elephant za Songea kucheza kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.

  Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza zitacheza pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Young Africans itacheza na Ashanti United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

  Jumapili Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto Africans itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

  Jumatatu Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi Mara kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

  Jumanne Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

  Januari 25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe mpya. Mechi hiyo imepangwa kufanyika Uwanja wa Uhuru

  0 0

  jamal-malinzi-1WWWWWWWWWWWWWWWWWWWWW
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye amempongeza Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) baada ya kuteuliwa na CAF kuwa mjumbe
   

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa (aliesimama) akizungumza mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua miradi ya Umeme Songwe Vijijini, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Songwe.
  Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Livingstone Lusinde akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati hiyo, pale walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje tayari ya kwenda kukagua Mradi wa Umeme uliopo kijijini hapo, Kushoto wake ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt. Medard Kalemani na Kulia kwake ni Katibu Kamati wa Bunge anaehusika na Hesabu za Serikali (PAC) Ndg. Asmin Kihemba na anaefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude. katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Ileje Mkoani Songwe.
  Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mhe. Joseph M. Mkude (aliesimama) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) pale kamati hiyo ilipomtembelea Ofisi kwake tayari kwa Ukaguzi wa mradi wa umeme katika moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje, Katika kikao kilichofanyika leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea na Kukagua Mradi wa Umeme uliopo moja ya kijiji kilichopo Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe.(PICHA NA OFISI YA BUNGE).


  0 0

  Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekutana na wadau wa sekta filamu nchini na kuoneshwa kusikitishwa juu ya shutuma dhidi yake na serikali kuwa wamekamata bidhaa haramu za wasanii na kuzirudisha kwa wamiliki kupitia mlango wa nyuma.

  Akiongea wakati alipotembelea moja ya ghala la Kampuni ya Udalali ya YONO Waziri Nape amewatoa hofu wasanii na kuwaeleza kuwa bidhaa hizo za muziki na video ziko mahali salama na zitateketezwa bila kificho muda si mrefu.

  Akiongelea kuhusu sakata hilo Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba amewaasa wasanii kuacha tabia ya kushutumu viongozi bila kuwa na ushahidi wa kutosha

  Katika Ziara hiyo Waziri Nape aliongozana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo na Wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA),COSOTA,Tume ya Ushindani wa Kibiashara(FCC) na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)

  0 0

  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi na Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa wakiangalia sanamu mtu wa kabila la Kimasai iliyochongwa kwa kutumia mti aina ya Mpingo kabla ya Wabunge wa kamati hiyo kuanza kutembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Eng. Ramo makani.
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye ( watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng.Ramo Makani (watatu kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (wa pili kulia) akizungumza na wabunge na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati walipokuwa wakiangalia zana za mawe zilizotumiwa na binadamu wa kale wakati Wabunge wa kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii walipokuwa wakitembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii, Eng. Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitia saini kwenye kitabu cha Wageni akishuhudiwa na baadhi ya Wabunge wa Kamati ya Maliasili, Ardhi na Utalii pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakiwa kwenye chumba maalumu ( strong room) cha kuhifadhia urithi wa utamaduni wa thamani kubwa kama zamadamu (hominine remains), masalia ya akiolojia, historia pamoja na sanaa ya ethnografia) leo (jana) walipotembelea Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Na Estom Sanga - Pemba.

  Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala Bora na Serikali za Mitaa imetembelea miradi inayotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- Unguja na Pemba na kuridhishwa na hatua ya Maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wake  kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.


  Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Ismail Mchemba akizungumza na wananchi wa shehia ya Ndagoni Kisiwani Pemba baada ya kukagua ujenzi wa tuta la kuzuia maji chumvi ya baharini yasiathiri mashamba ya wananchi, ametaka walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kutumia fursa ya Mpango huo kupunguza kero ya umaskini.


  Ametoa Mfano wa Miradi iliyojengwa kwa ufanisi kuwa ni pamoja na matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko, uchimbaji wa mitaro ya maji ,uundwaji wa vikundi vya kuweka akiba, na ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati miradi iliyotekelezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwa utaratibu wa ajira ya muda kisiwani Unguja na Pemba.


  Kwa kutengeneza matuta ya kuzuia maji ya chumvi, walengwa hao wa TASAF wameweza kuokoa zaidi ya hekta 200 za mashamba ya mpunga katika shehia ya Ndagoni kisiwani Pemba kwa njia ya ushiriki kwenye ajira ya muda .


  Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki amesema serikali inafuatilia kwa karibu utekelezaji wa shughuli za TASAF ili kuziboresha zaidi kwa manufaa ya wananchi.  Aidha Waziri huyo ameiagiza TASAF kuviimarisha zaidi vikundi vya kuweka akiba na  kuwekeza vipatavyo 876 kwenye shehia 78 vilivyoundwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kisiwani humo kwa kuvipatia nyenzo muhimu hususani elimu na vitendea kazi ili vikundi hivyo viwe endelevu.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF  
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF .
    Matuta ya kuzuia maji chumvi ,upandaji wa mikoko na uchimbaji wa mitaro ya maji ni Moja ya Miradi iliyojengwa kwa ufanisi Mkubwa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo mbalimbali alipokuwa akikagua bidhaa zilizotengenezwa na vikundi vya walengwa wa TASAF  .


  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na wananchi wa eneo la Vingunguti juu ya utatuzi na ushirikishwaji wa Wananchi katika kutatua kero zao.
   Vijana wa Bodaboda wakimsikiliza kwa makini Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala katika mkutano wa kutatua kero za wakazi wa Vingunguti.
  Mmoja wa wakazi wa Vingunguti akifatilia kwamakini mkutano huo ambao uliwakutanisha wananchi na Viongozi wa kata ya vingunguti katika mkutano wa kujadili namna ya kutatua changamoto za kata hiyo

  0 0

  Halmashauri ya Jiji la Tanga imeshauriwa kuandaa miradi ya kupima na kuuza viwanja vinavyoendana na mahitaji halisi ya wananchi ili kuhakikisha viwanja hivyo vinanunuliwa kwa wakati na wananchi wanavitumia shughuli za maendeleo.

  Ushauri huo umetolewa hivi karibuni na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ziara ya timu ya ukaguzi wa maradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango katika mradi wa viwanja wa mji mpya wa Pongwe unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga na Kampuni ya Amboni Sisal Properties Limited.

  Kiongozi huyo alitoa ushauri kufuatia kutoridhishwa na taarifa iliyotolewa na Afisa Mipango Miji wa jiji hilo, Bw. Joseph Mafuru kuwa mradi wa mji mpya wa Pongwe ulianza rasmi mwaka 2014 lakini hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana viwanja 510 tu kati ya viwanja 1000 ndivyo vilivyokuwa vimenunuliwa licha ya wanachi kufahamu uwepo wa mradi huo.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwnye koti jekundu) akiangalia ramani ya viwanja vya makazi na biashara ya mradi wa mji mpya wa Pongwe katika ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Tanga. Upande wa kulia (mwenye miwani) ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bw. Daudi Mayeji na aliyesimama (mwenye daftari) ni Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru, wengine ni wataalamu wa ukaguzi wa miradi walioambatana na Kaimu katibu Mtendaji.

  Kufuatia taarifa hiyo, Mwari aliamua kupitia ramani ya mradi na kubaini kuwa baadhi ya viwanja vilikuwa ni vidogo sana ikilinganishwa na mahitaji halisi ya wananchi. Vile vile baadhi ya maeneo ambayo yalionekana kuwa ni ya muhimu kwa ajili ya makazi na kwa fursa za biashara yalitengwa kwa ajili ya matumizi mengine kama maegesho ya magari.

  “Inavyoonekana wanachi wengi hawajanunua viwanja hivi kwa kuwa ni vidogo sana, watu wanahitaji maeneo yenye nafasi, sio ukijenga nyumba tu kiwanja chote kimekwisha. Nimeona kuna maeneo ambayo yanapendwa sana kwa makazi na ni fursa kwa biashara lakini hapa mmeyatenga kwa ajili ya maegesho ya magari, vitu kama hivi vinasababisha wanachi wasivutiwe na maeneo yenu,” alieleza Mwanri.
  Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru (mwnye koti jekundu) pamoja na maofisa kutoka tume ya mipango pamoja, Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na mfanyakazi wa Amboni Sisal Properties Limited (aliyesuka) wakiangali ukubwa wa eneo la Mradi wa Mji Mpya wa Pongwe (eneo halionekani pichani).

  Aliongeza kuwa mradi wa kupima na kuuza viwanja kwa wananchi ni kitu cha kutiliwa mkazo sana hususani katika maeneo ya mijini ambako kumekuwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa adhri na uwepo tatizo la makazi holela. Hivyo, ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha inatekeleza wajibu huo kikamilifu na viwanja vinauzwa kwa bei isiyowaumiza wananchi.

  Nae Mkurugenzi wa Jiji hilo Bw.  Daudi Mayeji  alieleza kuwa kutokana na mradi wa mji mpya wa Pongwe kutotekelezwa vizuri, Halmashauri ya Jiji la Tanga kwa kushirikiana na vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro imeanza kutenga na kupima kwa ajili ya kuuza viwanja kwa wananchi.  
  Alieleza kuwa viwanja hivyo vitauzwa na Halmashauri ya Jiji yenyewe  na vitakuwa na ukubwa unaozingati mahitaji halisi ya wananchi huku vikiuzwa kwa bei nafuu.

  “Mradi huo mpya umezingatia miundombinu yote muhimu na jumla ya viwanja 4,700 tayari vimepimwa,” Alieleza Bw. Mayeji.
  Sehemu ya eneo viwanja vya makazi na mbiashara katika Mradi wa Mji Mpya wa Pongwe.
  Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bw. Joseph Mafuru akiongea jambo kwa Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika mradi wa mji mpya wa Pongwe jijini Tanga. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa Idara ya Uhamiaji kuandaa semina za mafunzo ya elimu ya uraia kwa wahudumu ya hoteli na nyumba za kulala wageni nchini ili kudhibiti wimbi la wahamiaji haramu.

  Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Januari 19, 2017) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo ya Njombe na kupokea taarifa ya mkoa wa Njombe iliyotolewa na mkuu wa mkoa huo Bw. Christopher Ole Sendeka.

  Katika taarifa hiyo Bw. Ole Sendeka alisema kwenye kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba, 2016 Idara ya Uhamiaji ilibaini kuwepo kwa raia 119 wa kigeni ndani ya mkoa huo, ambapo wahamiaji haramu 42 walikamatwa.

  Waziri Mkuu alisema ni hatari kwa mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya raia wa kigeni walioingia nchini bila ya kufuata utaratibu hivyo aliitaka Idara hiyo ijipange vizuri ili kudhibiti watu wa aina hiyo.

  “Anzisheni utaratibu wa kutoa semina kwa wahudumu wa hoteli na nyumba za kulala wageni. Hawa wakipata elimu ya uraia watawasaidia katika kutoa taarifa za kuwepo kwa wageni ambao wana mashaka na uraia wao,” alisema.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa mikoa kujikita katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kuzuia mianya ya rushwa pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma katika maeneo yao.

  Alisema lazima kuwe na nidhamu ya matumizi ya fedha za Serikali zinazopelekwa katika halmashauri nchini. “fedha hizo lazima zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa yenye kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla,”.

  Aidha, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa umma kuibua maeneo mapya ya ukusanyaji wa mapato ambayo yatatumika katika utoaji wa huduma za jamii hivyo kuleta tija kwa Taifa.

  Pia aliwataka wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri miradi ya maendeleo inayojengwa katika maeneo yao kuhakikisha kama inalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na wasikubali kupokea miradi iliyojengwa chini ya kiwango.

  Awali Mkuu wa mkoa huo alisema kati ya wahamiaji haramu 42 waliokamatwa 39 ni raia wa Ethiopia, wengine wanatoka Uganda (1), Burundi (1) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (1). Wote walifikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Alisema Idara ya Uhamiaji inaendelea  na mikakati ya kuishirikisha jamii katika utoaji wa taarifa pindi wanapowatilia shaka kuhusu ukaazi wao ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia na upanuzi wa huduma za uhamiaji.

  Akizungumzia kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato mkuu wa mkoa alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 mkoa uliweza kukusanya kiasi cha sh. bilioni 7.07 sawa na asilimia 89.3 ya makisio ambayo yalikuwa sh. bilioni 7.92.

  “Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri zilikisia kukusanya kiasi cha sh. bilioni 8.22 ambapo katika kipindi cha nusu mwaka (Julai hadi Desemba, 2016) wameweza kukusanya jumla ya sh. bilioni 4.37 sawa na asilimia 53.2 ya makisio ya mwaka,” alisema.

  Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mashine maalumu za kielektroniki za kukusanyia mapato pamoja na kuondoa utaratibu wa ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mawakala katika vyanzo vingi.

  Aidha, Ole Sendeka alisema halmashauri za mkoa huo zinaendelea kupitia upya sheria ndogo za ukusanyaji wa mapato ili kuongeza vyanzo vya mapato pamoja na baadhi ya viwango vya kodi na tozo mbalimbali.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa walipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) akitoa neno la utangulizi wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb).
  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Peter Ilomo akitoa maelezo ya namna Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) unavyotekeleza majukumu yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akimsikiliza kwa makini.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF), Bi. Haighat Kitala akifafanua majukumu ya ofisi yake kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifafanua majukumu ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipoitembelea ofisi hiyo ili kupata taarifa ya kiutendaji. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jason Rweikiza (Mb) na kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu Bw. Peter Ilomo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kumaliza kikao cha kupokea taarifa ya kiutendaji ya Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF).

  0 0

  Ikiwa wateja mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiendelea kunufaika na bonasi za M-PESA zinazotolewa na kampuni hiyo,Kumetokea na matapeli wakiwalaghai wateja wa kampuni hiyo kana kwamba ni washindi wa bonasi hizo zinazoendelea kutolewa.

  Vodacom Tanzania imetoa tahadhari kwa wateja wake wote popote walipo nchini kuwa macho na matapeli ambao wanajifanya ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kuwapigia simu na kuwafahamisha kuwa wamefanikiwa kupata mgao wa fedha za gawio la huduma ya M-Pesa uliotangazwa na kampuni mapema wiki hii.

  ”KAMA WANAVYOSIKIKA KWENYE SAUTI HIYO”
  Akiongea na Mtandao huu,Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu alisema“Natoa wito kwa wateja wetu kuwa makini na matapeli wanaowapigia simu na kuwafahamisha kuwa wameshinda fedha za bonasi ya M-Pesa.

  Vodacom Tanzania haina utaratibu wa kuwapigia simu wateja kuhusiana na mgao wa fedha hizi bali inatoa mgao kwa kadri  ya mteja alivyotumia huduma hii na rekodi zote za matumizi kampuni inazo. Wanaowapigia simu wateja ni matapeli ambao wanataka kupata namba zenu za siri na kuwatajia kiasi gani cha fedha mlizonazo ili wapate frusa ya  kuwaibia fedha na msitoe namba   za siri kwa mtu yeyote”.

  Wateja watakaonufaika na mgao wa fedha za bonasi ya M-pesa awamu hii wanawekewa fedha zao kwenye akaunti zao za M-Pesa moja kwa moja na utaratibu wa kuwapigia wateja simu huwa unatumika kwenye promosheni tu kama vile promosheni inayoendelea ya”Nogesha Upendo”.

  0 0

  Dokta HARRISON MWAKYEMBE.

  Waziri wa Katiba na Sheria, Dokta HARRISON MWAKYEMBE, ametoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wa Rais JOHN MAGUFULI wa Wabunge Wawili, pamoja na Naibu Waziri kuteuliwa kuwa Balozi, huku akisisitza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haijakiukwa.
            Akizungumza na Uhuru Fm, Waziri MWAKYEMBE, ameshangazwa na baadhi ya watu kushutumu teuzi hizo za Wabunge wa kuteuliwa alizofanya Rais, huku akisema Katiba ya Nchi inampa nafasi Rais kuteua na kutengua nafasi ya mtu yoyote aliyemteua.
            Amesema ni vema watanzania wakamuacha Rais afanyekazi zake ikiwemo kufanya teuzi kwa kuwa yeye ndiye anaona mtu gani anafaa wapi na nani amteue kwa wakati gani.
            


        Jana jioni, Rais JOHN MAGUFULI, amemteua Dokta ABDALLAH POSSI kuwa Balozi, ambaye Kituo chake cha kazi na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadae.  
            Kabla ya uteuzi huo Dokta POSSI alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.
      Kwa mujibu wa Waziri MWAKYEMBE, Ubunge wa Kuteuliwa wa Dokta POSSI unakoma kufuatia uteuzi huo wa kuwa Balozi.

  0 0

  Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo. Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo.Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Valerie Msoka. Mkufunzi na mtaalamu wa masuala ya usalama barabarani kutoka Safe Speed Foundation, Henry Bantu akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Valerie Msoka.Ofisa Miradi Mkuu wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akiwasilisha mada kwa washiriki wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani. Kulia ni Ofisa Mradi wa TAMWA, Bw. Edson Sosten. Ofisa Miradi Mkuu wa TAMWA, Bi. Gradness Munuo (kushoto) akiwasilisha mada kwa washiriki wa mradi wa kampeni ya kupambana na ajali za vyombo vya moto barabarani. Kulia ni Ofisa Mradi wa TAMWA, Bw. Edson Sosten.Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo. Baadhi ya waandishi wa habari wanaoshiriki uandishi wa habari za usalama barabarani wakiwa katika mafunzo hayo.Mafunzo hayo ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa waandishi wa habari yakiendelea. Mafunzo hayo ya uandishi wa habari za usalama barabarani kwa waandishi wa habari yakiendelea.

older | 1 | .... | 1519 | 1520 | (Page 1521) | 1522 | 1523 | .... | 3272 | newer