Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

TFF yashauriwa kuendeleza vipaji vya Airtel Rising Stars

$
0
0

Ushauri umetolewa kwa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini (TFF) kuangalia namna ya kuwaendeleza wachezaji wanaohudhuria kliniki ya wiki moja ya Airtel Risingf Stars inayofanyika kwenye uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.

Ushauri huo umetolewa na Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars Edna Lema ambaye ni moja kati ya makocha wanaotoa mafunzo kwa wachezaji hao ambao walichanguliwa kutokana na michuano ya awamu ya sita ya Airtel Rising Stars.

Tuna wachezaji wazuri na wenye vipaji vya hali ya juu na kliniki hii inadhirihisha hivyo. Kwa wachezaji hawa kuendelea na vipaji vyao ni lazima kuwe na mipango endelevu. Kinachofanyika kwa sasa ni kwamba baada ya kliniki hii, wachezaji wataruhusiwa kurudi makwao mpaka pale tutakapokuwa na michuano ya kimataifa ndio tuanze kuwatafuta bila kujali huko walikokuwa walikuwa wanafanya nini. Bila kubadilisha hali hiyo ni vigumu kwa timu zetu kupata mafanikio, alisema Lema.
Tuliendea kufanya ziara nchini Cameroon na kushuhudia mipango yao ya kuendeleza vipaji. Kwao wanakuwa na kliniki za kudumu za wachezaji wa rika zote. Kwa kuwaweka wachezaji pamoja ujenga hali ya ukaribu kati yao pamoja na makocha pia na kwa hali hiyo sio ajabu kwa nchi hiyo kuwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia na hile ya Afrika. Natoa wito kwa TFF kubadilisha jinsi ya kutunza wachezaji wetu kuleta mafanikio kwenye timu zetu za taifa, aliongeza Lema.

Akiongelea kuhusu kliniki ya Airtel Rising Stars, kocha huyo Msaidizi wa Twiga stars alisema anaamini timu ijayo itakuwa na vipaji vya hali ya juu. Wachezaji hawa ni wazuri sana, ukipewa jukumu ya kuchangia timu inaweza kuwa mtihani umchukue yupi na kuwacha yupi. Kwakweli tunafurahi kupata vipaji hivi kutoka kwenye mashindano haya.

Lema alitoa pongezi kwa kampuni ya Airtel kuwa na program hii ya vijana ambayo kwa mwaka jana iliweza kufika mikoa tisa ya Tanzania. ‘Hii ndio njia bora na sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu, alisema Lema.

Mmoja ya wasichana wanaoshiriki kwenye kliniki hiyo Eva Willes alisema anayo furaha ya kuwa mmoja ya washiriki wa kliniki hiyo. Kwa muda mrefu nimekuwa nikicheza mpira wa miguu na nilikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji wa timu ya taifa. Kuwepo kwenye kliniki kunanifungulia milango ya kutimiza ndoto zangu. Nitaendelea kuongeza bidii pamoja na kuwasikiliza makocha kwa makini nipate mafanikio zaid, alisema Willes.
Kocha Mkuu wa Timu ya Wasichana U-17, Sebastian Nkoma akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa Kliniki ya Airtel Rising Stars yanayofanyika katika Uwanja wa Jakwaya Kikwete Dar es Salaam jana kutafuta vijana wenye vipaji kuunda Timu ya Taifa.
Kocha Msaidizi wa Timu ya Wasichana ya Twiga Stars, Edna Lema akitoa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo wakati wa kliniki ya Airtel Rising Stars yanayofanyika katika Uwanja wa Jakwaya Kikwete Dar es Salaam jana kutafuta vijana wenye vipaji kuunda Timu ya Taifa.
Wachezaji wa Timu ya wasichana U-17, wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Jakaya Kikwete wakati wa Kliniki ya Airtel Rising Stars Dar Salaam jana kutafuta vijana wenye vipaji kuunda Timu ya Taifa.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI NA MITAJI YA UMMA YAZURU MITAMBO YA MAJI YA RUVU

$
0
0
KAMATI ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC), imesema kuwa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) lina uwezo wa kumaliza tatizo la Maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kutokana na mitambo ya uzalishaji Maji ya Ruvu juu na Ruvu chini kuwa ya Kisasa na yenye uwezo mkubwa wa kuhudumia mikoa hiyo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Albert Obama, ambaye pia ni mbunge (CCM) wa jimbo la Buhingwe, mara baada ya kamati hiyo kuhitimisha ziara yake ya siku moja ya kutembelea mitambo ya uzalishaji Maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini iliyopo Mkoani Pwani.

Alisema kuwa, kamati hiyo imeshuhudia uwekezaji mkubwa kwenye miradi hiyo, hivyo kuridhishwa na kazi inayofanywa na shirika na kwamba wakazi wa Dar es Salaam na Pwani, wanaweza kuhudumiwa endapo uwekezaji huo utakamilika kwa asilimia 100.

"Tumeona kazi kubwa, nzuri inayofanywa na Dawasco na Dawasa, ikiwamo miradi mikubwa ya Ruvu Juu na Ruvu Chini ambapo mradi mkubwa wa juu utakapokamilika mwaka huu utasaidia kuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Pwani itakuwa historia." alisema.

Aidha alisema kamati hiyo imeishauri DAWASCO kubuni mbinu bora ya kuzuia upotevu wa Maji, ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wake wa usambazaji Maji ambao umekuwa na mivujo mingi hivyo kupelekea Maji mengi kupotea.

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja, alisema kuwa ziara ya kamati ya Bunge imekuja wakati mwafaka ambapo Shirika hilo linapambana kumaliza tatizo la upotevu wa Maji katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.

“Tumeanza kufanya jitihada za makusudi za kupambana na upotevu wa Maji ikiwa ni pamoja na kubadilisha dira zote za zamani za Maji pamoja na miundombinu yote ambayo ni chakavu" alisema. Nao wajumbe wengine wa kamati hiyo,Wamefurahishwa na namna ambavyo DAWASCO wanavyofanya kazi ya uzalishaji na utibuji Maji kwa ufanisi na utaalamu wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya umma (PIC) Mhe. Albert Obama (kushoto) akisalimiana na Afisa mtendaji mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) mara baada ya kamati hiyo kuwasili katika Ofisi ya Dawasco Makao Makuu jijini Dar es Salaam, ili kujionea shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo.

DR.SHEIN NA KINANA KUUNGURUMA UFUNGAJI WA KAMPENI ZA CCM DIMANI KESHO

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

KATIBU wa Idara ya Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar,  Waride Bakari Jabu amesema chama hicho kitaendelea kuishauri serikali na kutumia rasilimali zake katika kusimamia sera na mikakati yake katika  kuimarisha huduma na fursa za kimaendeleo kwa wananchi.

Alisema malengo hayo yatafikiwa endapo wafuasi wa Chama hicho na wananchi kwa ujumla watawaunga mkono, kuwaamini na kuwachagua  wagombea wanaopeperusha bendera ya CCM kwa kila uchaguzi wa kisiasa ili waweze kuwaletea wananchi maendeleo kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho.

Hayo aliyasema wakati akitoa taarifa kwa Vyombo vya Habari juu ya maandalizi ya ufungaji wa Kampeni za Chama hicho katika Uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Unguja, alisema maandalizi ya kufungwa kwa kampeni hizo yamekamilika kwa kufuata miongozo, ratiba na masharti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo alisema  Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kampeni hizo zitakazofanyika  Januari 21 mwaka huu kuanzia majira ya saa 8:00 mchana  katika Kiwanja Cha Shule (Skuli) ya Fuoni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.

Alisema Dr. Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar atawahutubia wananchi kwa kueleza sera, mikakati na muelekeo wa utekeleza wa shughuli za kimaendeleo zilizotekelezwa na Chama hicho na zinazotarajiwa kutekelezwa katika maeneo mbali mbali nchini hasa katika jimbo la Dimani.

Katibu huyo alisema viongozi wengine watakaohudhuria Kampeni hizo na kupewa fursa ya kuzungumza na wafuasi wa Chama hicho ni Katibu Mkuu wa CCM  Taifa, Abdulrahman Omar Kinana, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai pamoja na viongozi na watendaji ngazi mbali mbali za taasisi hiyo.

Aidha alisema matarajio ya CCM katika Uchaguzi wa Jimbo hilo ni kuendeleza ushindi wa kihistoria kutokana na wananchi wa rika mbali mbali kumkubali mgombea wa Chama hicho, Juma Ali Juma na kuahidi siku ya uchaguzi watamchagua rasmi bila pingamizi awe Mbunge wa jimbo hilo.

“ Tunawaomba wafuasi wetu na wananchi kwa ujumla mjitokeze kwa wingi katika Mkutano wa Ufungaji wa kampeni za CCM kesho (leo) ili muweze kusikiliza sera na mipango endelevu inayotekelezeka kwa vitendo itakayoelezwa kuwa ufasaha na Dr. Shein pamoja na viongozi wengine.

Pia wale ambao ni wakaazi na wapiga kura halali wa Jimbo la Dimani  tuendelee kuhamasishana nyumba kwa nyumba ili siku ya uchaguzi Januari 22 mwaka huu, tujitokeze kwa wingi katika vituo vya kupigia kura kwa lengo la kumpa ridhaa Juma Ali Juma aweze kuwatumikieni kupitia vipaumbele vyake.”, alieleza Waride na kuongeza kuwa CCM ndio Chama pekee kinachotambua thamani na utu wa makundi yote ya kijamii yaliyopo nchini.

Hata hivyo aliwasihi wafuasi wa CCM kufuata utaratibu na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoashiria vurugu na uvunjaji wa kanuni za wapiga kura siku ya uchaguzi badala yake wale waliotimiza umri wa kupiga kura na wamekamilisha taratibu zote kisheria wafike mapema katika vituo kwa kupiga kura na kurudi nyumba kusubiri matokeo.

Uchaguzi huo unafanyika kufuatia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Dimani Unguja, Hafidh Ali Twahir kufariki Dunia ghafla mwaka uliopita  akiwa katika utekelezaji wa Majukumu yake huko bungeni Mjini Dodoma.

SEMINA YA MAFUNZO YA KARATE KIMATAIFA YAFANYIKA JIJINI ARUSHA

$
0
0

Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Mafunzo ya karate ya kimataifa yanayoambatana na kufanya mtihani wa kupanda madaraja yamefanyika Jijini Arusha yakiongozwa na Master Shihan Shalom Avitan, kutoka nchini Israel .

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Afisa michezo mkoa wa Arusha Mwamvita Okeng’o ambapo amesema kuwa serikali imeipa michezo kipaumbele ili kupunguza tatizo la ajira nchini na amewataka wanamichezo hao kuuambikiza katika jamii kwa ujumla

Akijibu risala iliyoandaliwa na West coast Shotokan internation Karate( ASS'N) Afisa michezo huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inafanya jitihada ili kuwapatia eneo la kudumu la kufanyia mazowezi kama walivyoomba.

Naye afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuwa michezo inaimarisha afya ,ni ajira hivyo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu huku akiwasisitiza vijana kutumia fursa hiyo ili waweze kujiajiri.

Muandaaji wa mafunzo hayo hapa nchini Sensei Dady Ramadhan ambaye ni Mkufunzi kiongozi amesema kuwa wapo wanakarate wanaocheza Shotokan ambao wana daraja mbalimbali katika taaluma hiyo miongoni mwao wapo waliofanya mtihani na wamepanda daraja

Aidha amesema kila mwaka wanamuita mwalimu na kufanya mitihani ,hivyo amewataka wale wote wanaotaka kuifunza mchezo huo wahakikishe wanajicfunza kupitia wataalamu ambao wamepitia mafunzo hayo na wenye uzoefu wa kutosha.

“Unajua kwa sasa mchezo huu unawaalimu wengi ambao wamevamia hawana taaluma kabisa hivyo msikubali kuburuzwa na kufundishwa na hao watawapotosha na kuleta madhara kwani hawazifahamu kanuni na miiko ya karate.”alisema sensei Dady.

Wakufunzi wanaoingia kufanya mtihani wa kupandishwa madaraja wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza maelekeo kabla ya kuanza kufanya mtihani huo.

Wakwanza kushoto ni Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree ambaye ni raisi wa shirikisho la West Shotokan Karate Internation duniani ,akifuatiwa na Mkufunzi wa West shotokan Karate Kanda ya kaskazini Dady K.Ramadhan.
Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan akiwa anawapa maelekezo wakufunzi wanaofanya mtihani wa kupanda madaraja kabla ya darasa kuaza rasmi .
Wakufunzi wakiwa katika picha ya pamoja na Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan Degree baada ya kumaliza kufanya mitihani kwa vitendo katika hatua mbalimbali .


TPSC KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA UMMA-WAZIRI KAIRUKI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki amesema kwamba serikali kupitia Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa Umma ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa katika utumishi wa Umma.

Akiwasilisha taarifa ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa Makao Makuu ya TPSC Mtaa wa Bibi Titi Jijini Dar es Salaam , Waziri Kairuki alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa watumishi hao.

Aliongeza kuwa pia serikali inakamilisha mchakato wa mandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini.Katika kuongeza ufanisi na tija wa chuo hicho, chuo kimejenga, kuhuisha na kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu.

“Baadhi ya mifumo hiyo ni mpango mkakati mwa mwaka 2016-2021,utekelezaji kikamilifu kwa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la malalamiko na kamati za uadilifu.Waziri alisema majukumu mengine ni kuendelea kusimika mifumo ya Tehema, miundombinu ya mtandao (LASN) , Mtandao wa serikali (Govnet) , mfumo wa simu za serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM).

Waziri Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa watumishi wa Umma katika utunzaji wa kumbukumbu na Uhazili, Chuo kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza katika maeneo hayo mawili.“Rasimu ya Mitaala hiyo, imeshaandaliwa na kuwasilishwa baraza la Ithibati na Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ajili ya uhakiki na kuidhinishwa.” 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki(kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza kwa makini Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Dkt.Henry Mambo wakati alipokuwa akiwaelezea maadeleo ya ukarabati wa majengo ya chuo hicho tawi la Magogonijijini Dar es Slaam, kamati ya bunge ilifanya ziara ya kikazi katika chuo hicho jana. 
Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt.Henry Mambo, akisisitiza jambo mbelea ya wajumbe wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza,anayefuata ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki na kwa kwanza kulia ni Suzan Mlawi, Naibu Katimu Mkuu wa Wizara hiyo ya Ofisi ya Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki (kulia) akifafanua jambo kwa wajumbe wakamati ya kudumu yabunge ya Utawala na Serikaliza Mitaa wakati walipofanya ziara ya kikazi katika makao makuu ya chuo hicho,Mtaa wa Bibi Titi, jijini Dar es Salaam, jana .Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo , Jasson Rweikiza na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Utumishiwa Umma Dkt.Henry Mambo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Ino Communications Barnabas Lugwisha, akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe Angellah Kairuki wakati wa ziara hiyo jana Chuo cha Utumishi wa Umma.

UWANJA WA TOTTENHAM HOTSPURS KUGHARIMU PAUND MILIONI 750

$
0
0
Uwanja huo utagharimu £750m 

Klabu ya Tottenham Hotspur ya Uingereza imetoa picha za kwanza za uwanja wa klabu hiyo ambao unaendelea kujengwa kaskazini mwa London ambao utatoshea mashabiki 61,000 na utakuwa mkubwa zaidi katika jiji kuu la London utakapofunguliwa mwaka 2018. 

Miongoni mwa mengine, utakuwa na baa kubwa zaidi ya kuhudumia watu wote uwanjani, viti vyake vitakuwa na mitambo ya kubadili viwango vya joto na kutakuwa pia na kiwanda kidogo cha kutengeneza pombe, kiwanda kidogo cha kuoka mikate na keki. 

Mwenyekiti wa Spurs amesema uwanja huo utaleta "taswira mpya kwa michezo na burudani". Uwanja huo utakuwa na sakafu iliyopandwa nyasi ambayo inaweza kuondolewa na chini yake kutokea sakafu ya mkeka. Hilo litawezesha uwanja huo kuwa mwenyeji wa mechi za kandanda, NFL, matamasha pamoja na hafla nyingine. 

Miongoni mwa mengine, uwanja huo utakuwa na: 

.Njia iliyozingirwa kwa kioo cha kutumiwa na wachezaji kuingia uwanjani. Hii itawawezesha mashabiki kutazama yanayojiri kabla ya mechi. .Eneo la kuuzia bia la umbali wa 285ft (86.8m) ambapo kila mtu atauziwa..Mfumo mpya wa kusambaza bia ambao utawawezesha wauzaji kutoa painti 10,000 za bia kila dakika.

.Viti vitakuwa na mitambo ya kuongeza joto na sehemu za kuwezesha mtu kutumia vifaa vya USB.Kutakuwa na sehemu moja ya kuketi watu 17,000, ambayo itakuwa kubwa zaidi Uingereza. Ujenzi wa uwanja huo utagharimu £750m lakini utabuni nafasi 3,500 za ajira eneo hilo utakapokamilishwa, kwa mujibu wa klabu hiyo.Watu wataweza kuwatazama wachezaji wakiingia na kutoka uwanjani kupitia kiooWatu kwenye mgahawa wa ghorofa ya tisa wa Sky Lounge wataweza kutazama vizuri yanayojiri 

Timu hiyo ambayo kwa sasa mkufunzi wake ni Mauricio Pochettino itahitajika kutumia uwanja mwingine msimu wa 2017-18 uwanja huo unapojengwa. Chama cha Soka Uingereza(FA) kimewapa Spurs fursa ya kukodi uwanja wa Wembley ingawa pendekezo hilo limepingwa na mbunge wa chama cha Conservative Bob Blackman. 

Chelsea, ambao wanajenga uwanja mpya wa Stamford Bridge kuweza kutoshea mashabiki 60,000 pia wamependekezewa uwanja huo wa Wembley. Klabu za Uingereza zimekuwa zikijizatiti kuimarisha uwezo wa viwanja. Miaka kumi iliyopita Arsenal walijenga uwanja wao wa Emirates unaotoshea mashabiki 60,000. 

West Ham walihamia uwanja wao wa Olimpiki unaotoshea mashabiki 57,000 eneo la Stratford, London mashariki. Uwanja wa sasa wa Stamford Bridge unaotoshea mashabiki 41,663 ndio wa saba kwa ukubwa miongoni mwa viwanja vinavyotumiwa na klabu za Ligi ya Premia huku uwanja wa Old Trafford unaotumiwa na Manchester United hutoshea mashabiki 76,000.

NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto)  akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa  pili kutoka kushoto) na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la Dimani. Katikati ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa jimbo la Dimani Bi. Idaya Selemani Hamza, Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Bw. Emmanuel Kawishe (wa pili kutoka Kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya  Daftari la Kudumu la Mpiga Kura Mhandisi Isack Manyiri. 

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Serikali yafanya ukaguzi miradi ya miundombinu

$
0
0

Frank Mvungi-Maelezo

SERIKALI kupita Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imefanya ukaguzi wa miradi mikubwa 163 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2 ikijumuisha Barabara, majengo, maji na viwanja vya ndege.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu wa Idara ya Uhandisi wa Baraza hilo Mhandisi Wambura M. Wambura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ukaguzi huo.Mhandisi Wambura amesema kuwa miradi yote iliyofanyiwa ukaguzi inatekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali.

“Shughuli za kiukaguzi zilizofanyika ni pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya michakato ya manunuzi, utekelezaji wa mikataba, utekelezaji wa miradi,ongezeko la gharama za miradi, pamoja na ubora wa kazi zilizofanyika,” alisisitiza Mhandisi Wambura.

Aliongeza kuwa lengo la kaguzi hizo ni kuhakikisha kuwa thamani ya fedha inalingana na ubora wa miundombinu iliyojengwa katika eneo husika.Aidha, Mhandisi Wambura amesema kuwa katika kipindi cha 2015/2016 baraza lilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya matengenezo ya barabara kwa halmashauri zote za Wilaya pamoja na TANROADS kwa Mikoa ya Mbeya,Songwe,Rukwa,Katavi,Kigoma, na Shinyanga ambapo miradi hiyo iliyotekelezwa kwa fedha za mfuko wa Barabara.

Miradi mingine iliyofanyiwa ukaguzi wa kiufundi mwaka 2011 ni 14 iliyohusu ujenzi wa vituo vya afya na 36 ya ujenzi wa zahanati 50 iliyotekelezwa kwenye Halmashauri za Wilaya 20.Akizungumzia changamoto zilizobainika katika ukaguzi unaofanywa na Baraza hilo Wambura alibainisha kuwa ni kutozingatiwa kwa taratibu za kusimamia ubora wa kazi na maandalizi hafifu ya miradi katika hatua za mwanzo katika utengaji bajeti yakutosha,usanifu na ukadiriaji gharama za ujenzi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya majengo Bw. Kissamo Elias alitoa wito kwa wadau wa sekta hiyo kulitumia Baraza hilo kufanya kaguzi katika miradi wanayotekeleza ili kuongeza tija hali itakayochochea ukuaji wa sekta hiyo.Baraza la Taifa la Ujenzi ni kitovu cha uratibu wa sekta ya ujenzi kwa taasisi zote zinazoshughulika na shughuli za ujenzi pamoja na wadau ili kuleta umoja,uwiano, na ushirikiano katika utendaji ndani ya sekta ya ujenzi,Baraza linaendelea kusimamia na kuongoza juhudi za kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.

Baraza la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1979 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008,baraza lipo chini ya Wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano.
Kaimu Mkuu wa Idara ya Miradi ya Ujenzi kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi Injinia Wambura M. Wambura akiongea na wanahabari (hawapo pichani)kuhusu jukumu la ukaguzi wa kiufundi au kitaalam wa miradi ya ujenzi nchini jijini Dar es Salaam leo (jana).
Kaimu Mkuuwa Idara ya Miradi ya Ujenzi Injinia Wambura akiongea na wanahabari (hawapopichani) kuhusujukumu la ukaguziwakiufundi au kitaalamwamiradiyaujenzinchinijijini Dar es Salaam leo (jana).
KaimuMkuuwaIdarayaMajengokutokaBaraza la Taifa la Ujenzi Injinia Kissamo Fredrick akiongea na wanahabari kuhusu mafanikio ya Baraza hilo katika utekelezaji wa jukumu la kufanya ukaguzi wa kiufundi jijini Dar es Salaam jana (leo). (Pichana Benjamin Sawe- Maelezo).

NAIBU WAZIRI MASAUNI AIONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO SONGWE

$
0
0
Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kutembelea shamba la Mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, jijini  Mbeya.

 Afisa wa Jeshi la Magereza  akijibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea shamba la mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo la Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya.Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

 Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wakwanza kulia), kuingia ndani ya Gereza la Kilimo la Songwe,lililopo wilayani Mbalizi, jijini Mbeya,  ambapo wajumbe wa kamati walipata fursa ya kusikiliza maoni kupitia  risala iliyoandaliwa na wafungwa wa gereza hilo.Wengine ni viongozi wa gereza hilo.

 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally, akiwaongoza wajumbe wengine wa kamati hiyo kusalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, Jijini Mbeya.

 Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimpokea Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wapili kushoto), wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, mkoani  Mbeya.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

SIMBU AISHUKURU KAMPUNI YA MULTICHOICE TANZANIA KWA KUMPIGA JEKI YA NGUVU

$
0
0
Na Amina Kibwana,Globu ya Jamii .

kinara wa Standard Chartered Mumbai Marathon ambaye pia ni Balozi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Alphonce Simbu amewasili jijini dar es salaam na kueleza yaliyojiri katika mbia hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye ametoa shukurani zake kwa Multichoice Tanzania ambao ni wafadhili wa mwanaridha huyo kwa msaada waliompatia pamoja na pongezi za dhati kwa mwanaridha huyo kuchukua ushindi katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na washindani kutoka nchi tofautitofauti,

"Ninawashukuru sana dstv kwa kujitolea kwao pale wanapoona kunafaa kwani mafanikio ya Simbu yamepatikana kwa kupitia msaada huo na kuufanya mchezo huu kurudi tena kwa kasi nchini kulinganisha na awali."

Naye Katibu Mkuu wa chama cha riadha Nchini Willelm Gidabuday amesema kuwa waliamchagua Alphonce kwa kuamini kuwa nanweza na atafanya vizuri katika mchezo huo na kuweza kuiwakilisha vizuri Nchi yetu kutokana na kuweza kufanya vizuri katika mashindano yaliopita.

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Ronald Shelukindo amesema kuwa wanaendelea kumdhamini Simbu na kwamba wanatarajia kuwa atafanya vema katika michuano ijayo ya London Marathon ya mwezi April na yale ya Dunia ya mwezi Agosti na kutuwakilisha tena kama alivyofanya huko mumbai nchini India.

"Tunaendela kumdhamini Simbu na tunashirikiana kwa karibu na meneja wake na kocha ili kuhakikisha kijana anajinoa vizuri kwa ajili ya mashindabo yanayomkabili." amesema Ronald.

Kwa upande wake Mwanaridha huyo amewasifu waandishi wa habari kwa kazi walioifanya ya kutoa taarifa kwa umma kuhusu yaliyojiri huko Mumbai wakati wa mashindano hayo pamoja na Ufadhili alioupata kutoka Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kwa kumuwezesha kufanya maandalizi mazuri yenye kiwango kinachohitajika.

WAWAKILISHI WA UNEP WAKUTANA NA WAZIRI MAKAMBA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisikiliza kwa makini Wawakilishi kutoka Shirikia La Umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira (UNEP) waliokuja kumtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Wawakilishi wa Shirikia La Umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira (UNEP) pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustine Kamuzora mapema hii leo.

SIMBA MSAJILINI OKWI, ILA HAMUWEZI KUMTUMIA -TFF

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kufuatia kusitisha mkataba wake na klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark aliyokuwa anaitumikia, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeweka wazi kuwa Emanuel Okwi anaweza kusajiliwa na klabu yoyote nchini lakini hataweza kucheza mpaka msimu ujao.

Hilo limekuja baada ya taarifa kusambazwa kuwa Okwi anaweza kuitumikia tena klabu yake ya zamani ya Wekundu wa Msimbazi Simba katika mechi ya Februari 18 kama Kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Omog atapendezewa nae. 

Akizungumza na Globu hii, Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa klabu ya Simba ina uwezo wa kumsajili Mganda huyo kwa kipindi hiki lakini hawataweza kumtumia mpaka msima ujao wa ligi na hilo ni kulingana na kanuni za ligi. 

Lucas amesema kuwa kanuni za ligi haziruhusu kumtumia mchezaji ambaye amesajiliwa katikati ya ligi zaidi ya dirisha kubwa la usajili na dirisha dogo na likishafungwa basi klabu itamsajili mchezaji na hawatamtumia mpaka pale litakapofunguliwa tena. Kutokana na hilo, uwezekano wa Simba kumchezesha Okwi kwenye mechi yao dhidi ya watani wao wa jadi Yanga limeshindikana na zaidi wameambiwa wamsajili kama wanamuhitaji ila watamtumia msimu ujao na si vinginevyo. 

Taaarifa za kuachana na klabu yake, Okwi aliweka wazi kuwa atasema wapi atakapoelekea ila haijajulikana kama atarejea tena Msimbazi kwa mara ya tatu au ataamua kwenda timu nyingine. Ikumbukwe kuwa awali Okwi aliitumika Simba kabla ya kununuliwa na timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na kwenda kuishia kukaa benchi na kuamua kuachana nao na baadae kusajiliwa na Yanga na kucheza kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kurejea Simba na hatiumaye kusajiliwa na timu ya SønderjyskE ya nchini Denmark.


Emanuel Okwi

SACCOS YA POLISI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MIAKA KUMI

$
0
0
Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro.

Chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kimeendelea kujizolea mafanikio makubwa kwa muda wa miaka kumi toka kuanzishwa kwake huku kikijivunia kukopesha wanachama wake jumla ya fedha taslimu bilioni 113.7



Hayo yamethibitishwa na kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, wakatia akifungua mkutano mkuu wa nane wa Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), uliofanyika jana mkoani Morogoro huku ukiwakutanisha wajumbe na wawakilishi 172 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.



Bwana Haule, alisema kuwa,  mbali na mafanikio makubwa kupatikana pamoja na ongezeko la akiba na amana zenye thamani ya bilioni 23.095  kutokana na ubunifu wa kujenga mtaji wa ndani pia amewaasa viongozi na watendaji kuwa waadilifu na waaminifu ili kufikia malengo makuu yaliyotokana na maadhimio ya vikao vilivyopita.



Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usalama wa Raia Saccos Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias E.M. Andengenye, alisema kuwa, usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD),  itaendelea kutoa elimu kwa wanachama wake wote na kuendelea kujenga mtaji wa ndani kwa kununua hisa na kuweka akiba pamoja na kurejesha mkopo kwa wakati alisema.





Kamishna Andengenye, ameongeza kuwa, usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD),  itaendelea kuwahudumia wanachama wake wote ili kuwapunguzia makali ya maisha na kuwaepusha na mikopo yenye riba na masharti makubwa ili kukuza ustawi na uchumi wao na kwamba wamejipanga katika kuongeza idadi ya wanachama kupitia fursa walizonazo.

 Mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias E.M. Andengenye (aliyesimama) akitoa neno mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa  nane (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani morogoro jana kulia ni Kaimu Mrajis wa vyama vya Ushirika nchini Bwana Tito Haule, anayefuata ni Makamu Mwenyekiti Kamishna Albert M. Nyamhanga na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, (ACP) Leonce Rwegasila.
 Wajumbe wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wa mkutano huo Kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jana mkoani Morogoro.

Kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, pamoja na viongozi wa bodi na wajumbe wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane uliofanyika jana mkoani morogoro. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)

WAZIRI UMMY ATEMBELEA KITUO CHA AFYA BUGURUNI

$
0
0
 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amembelea kituo cha afya Buguruni akiwa na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Hermann pamoja na Mkuu wa Wilaya Bi. Sophia Mjema. Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utoaji wa huduma za Afya katika Vituo vinavyomilikiwa na Serikali. Demnark ni mmoja wa Wafadhili wakubwa wa Sekta ya Afya nchini kupitia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund). Picha Kwa Hisani ya Wizara ya Afya

DENMARK KUHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA TANZANIA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

SERIKALI ya Denmark imeahidi kuwashawishi wawekezaji wakubwa kutoka nchini humo kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Bandari, Gesi na Mafuta.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi wa Serikali ya Denmark anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Makao Makuu ya Wizara hiyo.

Bw. Hermann alielezea kufurahishwa kwake na namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuwatumikia wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo ya haraka ya kiuchumi pamoja na kuimarisha uwajibikaji, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, na kusema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi hizo.

Alisema kuwa nchi yake itasaidia juhudi hizo kwa kuzishawishi kampuni kubwa zenye mitaji na uwezo wa kiteknolojia kutoka sekta binafsi ili zije ziwekeze hapa nchini na hivyo kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.

Amesisitiza pia umuhimu wa serikali kuwekeza juhudi kubwa katika kuendeleza kilimo kwa kuwa sekta hiyo inaweza kuchochea na kutoa mchango mkubwa na wa haraka wa ustawi na maendeleo ya wananchi.

Aidha, Bw. Hermann, ambaye aliambatana na Balozi wa Denmark hapa nchini, Bw. Einar Jensen, amesifu utendaji mzuri wa Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi ikiwemo rushwa na kuishauri Serikali kuweka mfumo wa vita hiyo utakaokuwa endelevu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kutoka nchini Denmark, ukiongozwa na Waziri wa nchi anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, walipokutana Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Ujumbe kutoka Serikali ya Denmark ukiongozwa na Waziri wa Nchi-Sera, Bw. Martin Hermann, walipokutana kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera, Bw. Martin Hermann (kulia) akiwa na ujumbe wake wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam, ambapo nchi hizo zimekubaliana kuendeleza ushirikiano utakaojikita katika masuala ya uwekezaji na biashara kwa faida ya pande zote mbili. Kushoto ni Balozi wa Denmark hapa nchini Bw. Einar Jansen.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James, wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Nchi anayeshughulika na masuala ya Sera wa Denmark, Bw. Martin Hermann (hawapo pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera kutoka Denmark, Bw. Martin Hermann (kushoto) akimkabidhi Dkt. Mpango, nyaraka za kampuni zinazoonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Gesi na Mafuta wakati akiongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na Waziri wa Nchi wa Serikali ya Denmark anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann, wakati wa mazungumzo kati yao yaliyojikita katika masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na kulia kwa Waziri Dkt. Mpango, ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatib Kazungu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

mdau Luqman Ramadhani Dau alamba nondozzz ya MSc Biotechnology Chuo Kikuu cha Warwick Uingereza.

$
0
0
 Mdau Luqman Ramadhani Dau akiwa na mama yake  Mrs Zeinab Dau  na baba yake mdogo Abdul Dau akifurahia baada ya kutunukiwa nondozzz ya MSc Biotechnology kutoka Chuo Kikuu cha Warwick nchini Uingereza leo.
Mdau Luqman Ramadhani Dau akiwa na profesa wake baada ya kutunukiwa shahada ya MSc Biotechnology Chuo Kikuu cha Warwick nchini Uingereza
 Mdau Luqman Ramadhani Dau akifurahia nondozzzzz yake akiwa na mama yake  Mrs Zeinab Dau  

RAIS DKT. MAGUFULI AWAASA MABALOZI

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Dkt. Emanuel Nchimbi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. James Msekela  kuwa Balozi wa Tanzania Geneva –Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Mbelwa Kairuki kuwa Balozi wa Tanzania nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. George Madafa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Elizabeth Kiondo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Fatma Rajab  kuwa balozi wa Tanzania nchini Qatar, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza machache baada ya kuwaapisha mabalozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017. Picha na IKULU

ANGALIA LIVE! KUAPISHWA KWA RAIS WA 45 WA MAREKANI DONALD TRUMP

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA KWENYE UWANJA WA MABEWANI MJINI MAKETE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mabewani mjini Makete, januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mku)
WETO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Ujuni wilayani Makete walioziba barabara wakitaka asimame kuwasalimia Januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ndama waliokuwa wakinyweshwa maziwa wakati alipotembelea shamba la ng’ombe la Kitulu wialayani Makete Januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live


Latest Images