Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa shughuli za maendeleo. 

Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali. 

Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa macho,Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu wachache 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo 

Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori tengefu katika wilaya hiyo.


Mgodi wa Buzwagi mbioni kufungwa

0
0
Kaimu Kamishna wa Nishati na Madini, Ally Samaje (anayetoa maelezo) akielezea Mpango wa Serekali wakati wa kufunga Mgodi wa Buzwagi. Wengine katika picha ni Wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Viongozi Waandamizi kutoka Mgodi wa Buzwagi.

Na Rhoda James – Kahama.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa ameuongoza ujumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini ili kukagua na kuhoji utendaji na ushiriki wa mgodi wa Buzwagi katika masuala ya kijamii mkoani  Shinyanga hivi karibuni.  

Katika ziara hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeutaka Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kuwashirikisha wananchi pamoja na wafanyakazi wa Mgodi huo Mpango wa kuufunga Mgodi huo (Mining Closure plan) unaotarajia kufunga shughuli zake za uzalishaji wa Dhahabu ifikapo Desemba 2017, huku shughuli za uchejuaji zitaendelea kwa miaka miwili. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko (wa pili kushoto) akimsikiliza Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Assa Mwaipopo (hayupo pichani) akielezea shughuli za uzalishaji wa Dhahabu katika Mgodi huo. Kushoto kwake ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na wengine ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi.

Haja hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko mara baada ya kuwasili na kukutana na uongozi wa mgodi huo wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa mgodi huo. 

Biteko alisema kuwa Wananchi na wafanyakazi lazima wawe sehemu ya ufungaji wa Mgodi huo kwa kuwa jambo hilo ni kubwa kwani litatikisa Uchumi wa wananchi wa Kahama na pia Halmashauri ya Kahama itakosa Ushuru wa Huduma ambazo Mgodi huo umekuwa ukilipa kila mwaka.

“Mgodi huo unalipa Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na wafanyakazi katika mgodi huo wana ajira kwa hiyo mipango ya kufunga mgodi huo iwe sehemu ya wananchi kwa asilimia mia” alisisitiza Biteko.
Muonekano wa Mgodi wa Buzwagi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Aidha Biteko alitaka ufafanuzi zaidi kutoka kwa Uongozi wa Mgodi huo ni sababu zipi zinazopelekea mgodi huo kufungwa. Vilevile, alitaka Uongozi kuijulisha kamati hiyo jambo ambalo mgodi huo unawaachia wanannchi wa Kahama mara baada ya shughuli za uzalishaji kufungwa. 

AZAM WAWATUPIA LAWAMA WAAMUZI WA MECHI YAO DHIDI YA MBEYA CITY

0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baada ya kulazimishwa sare na Mbeya City katika mchezo wa jana uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi, benchi la ufundi la Azam limelalamikia maamuzi mabovu ya waamuzi waliochezesha mechi hiyo.



Wakitoa malalamiko hayo kupitia mtandao wao, wamelalamikia maamuzi yaliyokuwa yakifanywa na waamuzi hao katika dakika 45 za kipindi cha pili na kushangaza watu wengi hadi wachezaji uwanjani na kusema kuwa wanaamini kuwa hayo yalikuwa  yakifanywa na waamuzi kana kwamba wakitaka mtanange huo uishe kwa sare.


Kwenye mechi hiyo  mwamuzi wa kati alikuwa ni  Florentina Zabron akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Josephat Bulali na namba mbili, Gasper Ketto.

Malalamiko hayo yanakuja zaidi hasa baada ya mwamuzi Florentina, kushindwa kufanya maamuzi tukio la kufanyiwa madhambi ya makusudi mshambuliaji wa Azam FC, Shaaban Idd na beki Haruna Shamte wakati akimiliki mpira ndani ya eneo la hatari kuelekea langoni mwa Mbeya City.

Licha ya dakika nyingi kupotezwa kwa mbinu za upotezaji muda za wachezaji wa Mbeya City katika vipindi vyote, mwamuzi wa akiba Omary Kambangwa alionyesha dakika nne tu za nyongeza.

Sare hiyo inaifanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 31 na kubakia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 14 na kinara Simba mwenye pointi 45, ambayo nayo imelazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar jana.

Katika mchezo huo Azam FC imewekuwa timu ya kwanza kuanza  kutumia ubao wa kielektroniki wa kubadilishia wachezaji.

Kikosi cha Azam FC leo:

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Himid Mao/Domayo dk 59, Salum Abubakar, John Bocco (C), Yahaya Mohammed/Afful dk 74, Joseph Mahundi/Shaaban

Mufuruki na ujumbe wake wamtembelea Waziri Makamba ofisini kwake jijini Dar leo

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba (wa kwanza kushoto) akiwaongoza kupitia Makabrasha ya masuala ya Mazingira, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akijadili jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki alimpotembelea Waziri Makamba Ofisini kwake mapema hivi leo.
Wakifurahia jambo kwa pamoja Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Bw. Ali A. Mufuruki, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.

YULE JAMAA WA BODA BODA KULE SIJUI KAPATWA NA NINI??

MHE. MHAGAMA ASHAURI CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO OFISI YA WAZIRI MKUU (MAKAMU SACCOS) KUWA WABUNIFU

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameshauri uongozi wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Ofisi ya Waziri Mkuu (Makamu Saccos) kuwa na ubunifu katika utendaji ili kuleta manufaa zaidi kwa wanachama wake.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanachama wa Chama hicho uliofanyika Januari 19, 2017 mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwepo na mikakati madhubuti ya kubuni miradi itakayowezesha chama kuwa na vyanzo vyake vya mapato na kuwa na mikakati ya kuongeza wanachama wapya kwa kuzingatia umuhimu wa chama hicho.“Ni muhimu kuwa na mikakati madhubuti ya kubuni miradi, kuongeza wanachama pamoja na kuwa na vitu vya kiupekee na vya kiufanisi vitakavyokisaidia chama kuwa imara katika utendaji wake”, alisema Waziri Mhagama.

Aliongeza kuwa chama hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wanachama wake amabapo wengi wao wamekuwa na maendeleo mbalimbali kutokana na uwepo wa fursa za mikopo isiyokuwa na masharti magumu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akisalimia wanachama waChama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wao wa mwaka Uliofanyika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 19 Januari, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama wa Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu Januari 19,2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe Chama cha Akiba na Mikopo Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kwanza wa mwaka Januari 19, 2017 Mkoani Dodoma.
 Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchasi akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wanachama wa Akiba na Mikopo wa Ofisi hiyo Mkoani Dodoma Januari 19, 2017.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

TAARIFA KWA UMMA: KAMBI ZA UPASUAJI WA BILA KUFUNGUA KIFUA KWA WAGONJWA WA MOYO

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo atembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo  alipotembelea  Taasisi hiyo jana. Kushoto ni Afisa Muuguzi Edna Kajuna.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo  mara baada ya kutembelea   Taasisi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo  mara baada ya kutembelea   Taasisi hiyo

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA KATIKA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA CHA JNIA

0
0
 Waziri Mbarawa (katikati), akisikiliza kwa makini maelezo ya Mhandisi Mohamed Millanga kuhusu ujenzi huo.
 Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga akitoa maelezo kwa Waziri Mbarawa.
 Waziri Mbarawa akikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TB III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.  
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliamo, Prof. Makame Mbarawa (kushoto), akipata maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi Mhandisi Mohamed Millanga wakati waziri alipofanya ziara jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Salim Msangi.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Thank you - OBAMA

0
0
The White House, Washington

My fellow Americans,
It's a long-standing tradition for the sitting president of the United States to leave a parting letter in the Oval Office for the American elected to take his or her place. It's a letter meant to share what we know, what we've learned, and what small wisdom may help our successor bear the great responsibility that comes with the highest office in our land, and the leadership of the free world.
But before I leave my note for our 45th president, I wanted to say one final thank you for the honor of serving as your 44th. Because all that I've learned in my time in office, I've learned from you. You made me a better President, and you made me a better man.
Throughout these eight years, you have been the source of goodness, resilience, and hope from which I've pulled strength. I've seen neighbors and communities take care of each other during the worst economic crisis of our lifetimes. I have mourned with grieving families searching for answers -- and found grace in a Charleston church.
I've taken heart from the hope of young graduates and our newest military officers. I've seen our scientists help a paralyzed man regain his sense of touch, and wounded warriors once given up for dead walk again. I've seen Americans whose lives have been saved because they finally have access to medical care, and families whose lives have been changed because their marriages are recognized as equal to our own. I've seen the youngest of children remind us through their actions and through their generosity of our obligations to care for refugees, or work for peace, and, above all, to look out for each other.
I've seen you, the American people, in all your decency, determination, good humor, and kindness. And in your daily acts of citizenship, I've seen our future unfolding.
All of us, regardless of party, should throw ourselves into that work -- the joyous work of citizenship. Not just when there's an election, not just when our own narrow interest is at stake, but over the full span of a lifetime.
I'll be right there with you every step of the way.
And when the arc of progress seems slow, remember: America is not the project of any one person. The single most powerful word in our democracy is the word 'We.''We the People.''We shall overcome.'

Yes, we can.
President Barack Obama

WAZIRI NAPE ATEMBELEA IDARA YA HABARI (MAELEZO NA KUZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia mfumo wa zamani wa kuhifadhia magazeti alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bibi. Zawadi Msalla  na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi, Katibu wa Waziri Bw. Octavian na Afisa Habari Mkuu John Lukuwi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akimuonyesha habari iliyoandikwa katika gazeti la Mzalendo la miaka ya nyuma Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipotemmbelea Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. John Lukuwi akimuelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye ( aliyekaa) namna Kamera ya kupigia picha za majengo marefu inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Waliosimama wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia saver kwa ajili ya kuhifadhi Picha za matukio mbalimbali alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Idara hiyo Bw. John Lukuwi.

OMBI LA UANACHAMA WA ZANZIBAR KUJADILIWA CAF

0
0
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha ombi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) la Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF. Katika kikao chake cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Januari 12, mwaka huu kiliamua kupitisha ombi hilo kuwa moja ya ajenda za Mkutano Mkuu wa CAF utakaofanyika Machi 16, 2017 huko Addis Ababa, Ethiopia.

Hivyo sasa Mkutano Mkuu huo utapiga kura na kama Zanzibar itapata idadi ya kura theluthi mbili yaani 2/3 ya wanachama wote, itatangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF ambako atakuwa na haki mbalimbali za kama mwanachama.

Haki hizo ni pamoja na kushiriki michuano yote inayoandaliwa na kusimamiwa na CAF na hii ni pamoja na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), fainali za Afrika Wanawake (AWCON), fainali za vijana (AFCON U17 na AFCON 20)na pia kuhudhuria mikutano mbalimbali ya CAF kama mwanachama kamili, kupokea na kusimamia kozi mbalimbali za CAF nakadhalika.

Pia itakuwa na fursa ya kupiga kura katika masuala muhimu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) tofauti na sasa ambako inapata fursa ya klabu zake zinazoshika nafasi ya juu katika Ligi Kuu ya Zanzibar kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa shukrani kwa Mheshimiwa Nape Nnauye – Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano Tanzania pamoja na Mheshimiwa Rashid Ali Juma - Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanizbar (SMZ) kwa kufanikisha hatua hiyo.

Pia, TFF inatoa shukrani kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarus Faina pamoja na Rais wa Heshima wa TFF Leodegar Chilla Tenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa CAF na Marais wa Heshima wa TFF Said Hamad El Maamry ambaye ni Mjumbe wa kudumu wa CAF na Mzee Muhiddin Ndolanga na wadau wote wa familia ya mpira wa miguu kwa mafanikio ya hatua hii.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa sasa linajikita kwenye kampeni nzito ya kuomba kura za kutosha kuhakikisha kwamba Zanzibar inapata nafasi hiyo ya uanachama kamili.

Kadhalika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia viongozi wake wako kwenye mchakato wa kumfanyia kampeni Rais wa Heshima wa TFF, Bw. Leodegar Chilla Tenga kuhakikisha anashinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji (Council) ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Leodegar Tenga anawania nafasi hiyo kutoka nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza akishindana na Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zambia, Kalusha Bwalya na Kwesi Nyantakyi wa Ghana.

TFF inaomba Watanzania wote na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kutuunga mkono katika juhudi na jitihada zetu za kuona Zanzibar inapata nafasi hiyo kadhalika Tenga anakuwa mjumbe kwenye baraza la ushauri huko FIFA.

NAIBU WAZIRI MASAUNI AKUTANA NA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA JIJINI MBEYA

0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoulizwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa ziara ya kikazi iliyofanyika leo jijini Mbeya.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Kanali Mstaafu Masoud Ally.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kapteni Mstaafu Goerge Mkuchika, akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali yaliyoelekezwa kwa Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kamati hiyo imekutana  jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
 Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Juliana Shonza (katikati) akizungumza wakati wa kipindi cha kuuliza maswali yaliyoelekezwa kwa Idara zilizopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi .Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo.Kamati hiyo ya Bunge  iko jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
 Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa akizungumza wakati wa mkutano na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,iliyokutana jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
 Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi , Asumsio Achachaa, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwenye Idara yake na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wa mkutano na kamati hiyo iliyokutana Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi(ACP)  Paul Kajida, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwenye Idara yake na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama(hawapo pichani),  wakati wa mkutano na kamati hiyo iliyokutana  Jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

UJENZI WA DARAJA LA KIJICHI NA TUANGOMA KUANZA

0
0
Serikali ya Manispaa ya wilaya ya Temekee na kampuni ya Ujenzi ya China CRJE  wametiliana saini mkataba wa Ujenzi wa Daraja litakalo unganisha  eneo la kijichi na Tuangoma  wilayani humo.

Akizungumza katika hafla hiyo mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Temeke   ambaye pia ni katibu tawala  Wilaya hiyo Hashim Komba  , amesema daraja hilo linajengwa ili kuondo usumbufu wanaoupata  wananchi wanaoishi  maeneo hayo kwa kuzunguka Kigamboni na kongowe wakati wa masika.

Aidha afafanua kuwa Daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 800 na barabara za mitaa zaidi ya kumi zenye urefu wa Kilomita 1.8   na  barabara  nyingine zenye urefu wa kilomita 84 zote zitajengwa kwa kiwango cha lami na kitapimwa viwanja zaidi ya mianane kuzunguka eneo  la mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya Ujenzi CRJE Zhao Yefang ameshukuru kupewa kazi hiyo ana ameahidi kufanya kwa viwango kama walivyo jenga Daraja la Kigamboni watahakikisha ubora na thamani ya hela vinazingatiwa na ndani ya mwaka mmoja watakabidhi Daraja hilo.
Wakisaini Mkataba katikati ni Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Ilala Bw Abadallah Chaulembo,Kulia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke Bw Nassib Mbaga na Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi CRJE Bw Zhao Yefang
  Katibu mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw Hashim Komba akiongea na Wananchi wa Kijichi kuhusu swala zima la Utengenezwaji wa Daraja hilo ili kuondoa Usumbufu wanaoupata wananchi kuzunguka Kigamboni na Kongowe wakati wa Msimu wa Masika.
Mstahiki Meya wa Temeke Bw Abdallah Chaulembo akizungumza na wananchi wa Kijichi kuhusu ujenzi wa Daraja unaotarajia kuanza mapema Mwaka huu katika Eneo hilo
Baadhi ya Wananchi wa Kijichi wakiwa Katika Mkutano huo.
 

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI ZA EASTERN AFRICA WAKUTANA ARUSHA KUJADILI NAMNA YA KUUNDA MIFUMO YA USAFIRISHAJI UMEME KWA NCHI HIZO

0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha umeme (Eastern Africa Power pool (EAPP) zimekutana jijini arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa urahisi tofauti
na sasa .

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt.Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za Eastern Africa power pool (EAPP) mapema leo.

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani kuna uwezekano mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo. 

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.  "Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme kwa bei ndogo"aliongeza Palangyo. 

Hata hivyo kwa upande Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Tanesco,Bi Leila  Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo Tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya Tanzania kwenda nchini Kenya,Zambia,pamoja na nchi nyingine .

Muhaji alisema kuwa Tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii
itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo
zimeeendelea Duniani. 

"Hata hivyo mara baada ya mkutano huo,Wakuu wa nchi zinazozalisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni Mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

KAMATI YA BARAZA LA WAWAKILISHI INAYOSHUHULIKIA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA YAKUTANA

0
0
 Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayoshughulikia masuala ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa Simai Mohamed Said (wa pili kulia) alipokuwa akitoa mchango wake wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati Ujumbe wa Kamati hiyo  walipotembelea Ofisi hapo Ikulu Mjini Unguja leo kuzungumzia utekelezaji wa masuala mbali mbali yanayohusu Ofisi hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Wawakilishi inayoshulikia masuala ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa Omar Seif Abeid akitoa maelekezo wa Watendaji wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo wakati ujumbe wa Kamati hiyo ulipokutana na watendaji hao ikulu Mjini Unguja kuzungumzia masuala mbali mbali ya kiutekelezaji (kushoto) Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Nd. Salum Mauli Salum.

KAMANDA RAS MAKUNJA AHOJIWA NA RADIO BBC KISWAHILI JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 Kiongozi wa bendi maarufu Ngoma Africa aka FFU-Ughaibuni yenye makao nchini ujerumani mwanamuziki Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mapema tu alihojiwa na radio BBC Kiswahili katika kituo chao Mikocheni jijini Dar.
Akiongoza mahojiano hayo mtangazaji Omari Mkambala
alimlima maswali Ras Makunja ambapo katika moja ya majibu yake mwanamuziki huyo alisisitiza na kutoa wito kwa Watanzania walio nje ya nchi kuwa mstari wa mbele kwa kuwapa ushirikiano bendi na wanamuziki wa Tanzania pale wanapoziona fursa za kimataifa ili muziki wa Tanzania ufike nje ya mipaka na kupata soko zaidi la kimataifa
Kamanda Ras Makunja alisema muziki wa dansi na mengineyo ya Kitanzania ina nafasi nzuri nje ya nchi kama Watanzania wenyewe walio nje wakatakuwa na uzalendo wa kuzipigania  bendi za nyumbani kutumbuiza katika majukwaa kimataifa. msikose kusikiliza mahojiano hayo katika radio BBC idhaa ya Kiswahili.
 mahojiano hayo yaliongozwa na mtangazaji Omari Mkambala

HAKI ELIMU YAZINDUA MPANGO KAZI WA MWAKA 2017-2021

0
0
 Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akifungua pazia kuashira uzinduzi wa dira ya mwaka 2017 mpaka 2021 nchini.

 Mwenyekiti ya bodi ya taasisi ya Haki elimu nchini, Profesa Martha Qorro akihutubia wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Dira ya tasisi hiyo kuanzia 2017-2021.
 Mkurugenzi wa taasisi ya haki elimu nchini,John Kalaghe akizungumza wakati wa mkutano wa uzinduzi wa Dira ya haki elimu 2017-2021.
 Baadhi ya wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari walioshirikikatika uzinduzi huo wakifatilia kwa makini.
 Picha ya Pamoja ya wajumbe wa bodi wa taasisi ya Haki elimu na wadau muhimu kwa tasisi hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKURUGENZI MUHIMBILI: TUTAENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAHUDUMU MUHIMBILI

0
0
Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili ( MNH),  Profesa  Lawrence Museru  leo amekutana na wahudumu  wa  Afya  katika  hospitali hiyo pamoja na mambo mengine  amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.

Pia, mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi  ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  na baadhi ya wahudumu wa afya  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Profesa Museru  amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali , lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.

" Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora  na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana  ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.

Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda  14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo  ili kuongeza  ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao. 
Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo leo.
 Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo.  Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAANDAA SEMINA YA MAPITIO YA MRADI WA MARADHI YASIOPEWA KIPAUMBELE

0
0
Na Ali Issa, Maelezo Zanzibar.

Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo cha maradhi ya yasio pewa kipaumbele (kichocho, matende, na Vikope)kimo katika harakati za kuyatokomeza kabisa maradhi hayo katika maeneo ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa leo huko Mkoa wa Kusini Unguja katika Hoteli ya visital inn Jambian na Dr.wa maradhi hayo Khalifan Abdalla Mohamed wakati wa semina ya mapitio wa mradi uliomaliza wa kuyatokomeza maradhi hayo .

Amesema maradhi ya kichocho na matende yaliathiri sana wananchi wa visiwa vya zanzbar katika miaka ya thamanini na kupelekea wengine kupata maradhi ya matende hadi hii leo jambo ambalo kwasasa maradhi hayo yanaonekana kutoweka kutokana na jitihada za Serikali na washirika wake wa maendeleo kulivalia njuga tatizo hilo.

Amsema kwa sasa hali hiyo inaridhisha kwakiasikikubwa na sehemuzilizo bakia nichache kuliitokomeza tatizohilo “Tuna tarajia kuyamaliza maradhi ya kichocgo na matende kwani imekuwa nadra kupokea wagonjwa wamaradhi haya ispokuwa niwale wale wagonjwa wazamani tu walioathirika na matende,kichocho,na  zipo baadhi ya maeneo ambayo hayajamalizika maradhi hayo kama vile kamgamba,kinyasini,moga,kizimkazi na kwapemba micheweni kwa”alisema DR Khalifan.

Nae mwenyekiti wa mradi wa kutokomeza maradhi hayo kutoka Nchini giniva katika shirika Global Schistosomiasis Alliance Dr Lorenzo Savioli amesema mapitio ya semina hiyo ni kuangalia vipi kuisaidia Zanzibar  kwa kuwapatia madawa na kufikia lengo la kuyatokomeza maradhi hayo.
Amsema  wananchi wazitumie dawa hizo kwa rika zote na hazina matatizo yoyote bali zinapoza zaidi maradhi mengine kama vile mapele mabaka na mipasuko mwilini.

Alisema wazitumie dawa hizo bure na nifrusa kwao ,kwani nchini kwao dawa hizo ni ghali mno kwa mwananchi wa Tanzania.

Nae mkurugenzi wa Maendeleo ya maji Zanzibar Muhamed Iliasa Mohamed alisema katika kuondoa tatizo la kichocho Zanzibar ni kuhakikisha kupeleka maji safi na salama katika maeneo yote ya zanzbar ili wananchi waweze kutumia maji safi na kuacha kutumia maji ya mito na mashimo.
Aidha alisema wanalazimika maji kuyatia dawa yakuulia vimelea vya maradhi hayo ili visiwe na nafasi ya kuathiri wananchi wanapo yatumia.
 Washiriki mbali mbali wa Semina wakifanya mapitio ya Mradi wa kutokomeza Maradhi yasiopewa kipaumbele (Kichocho,Matende na Vikope) katika ukumbi wa Hoteli ya VISITAL INN iliopo Jambiani Mkoa wa kusini Unguija.
 Mwenyekiti wa kutokomeza Maradhi hayo kutoka  Shirika la Global Schistosomiasis Alliance (GSA) Dr Lorenzo Savioli,akizungumza na waandishi wa Habari namna walivyodhamiria kuyatokomeza maradhi haya katika Nchi ya Zanzibar.
Mkurugenzi Maendeleo ya Maji Moh’d Iliasa Moh’d akizungumza na Waandishi wa Habari,  namna walivyokusudia kuwapelekea Wananchi huduma ya Maji maeneo yote ambayo yamegundulika na maradhi ya kichocho hayana maji salama watafikisha huduma ya Maji safi na salama haraka iwezekanavyo .
Viewing all 109588 articles
Browse latest View live




Latest Images