Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1515 | 1516 | (Page 1517) | 1518 | 1519 | .... | 3282 | newer

  0 0
  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizaya hiyo, Meja Generali Gaudence Milanzi (kushoto) wakiwakaribisha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipowasili katika ofisi za Wakala ya Miti za Mbegu Tanzania (TTSA) mjini Morogoro jana kwa ajili ya kuona kazi na miradi ya wakala huyo. Kushoto ni wajumbe wa kamati hiyo, Silafi Maufi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa na Godwin Molel (wa pili kushoto), Mbunge wa jimbo la Siha.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhandisi Atashasta Nditiye (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mohammed Kilongo alipowasili na kamati yake katika ofisi za Wakala wa Miti za Mbegu Tanzania mkoani Morogoro jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Wizara ya Maliasili na Utalii, Marry Faini na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (wa pili kulia).
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akisistiza jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) mkoani Morogoro jana.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wanne kushoto) akitoa maelezo ya mtandao (kulia) wa kugundua matukio ya moto kwenye maeneo ya misitu nchini unavyofanya kazi kwa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Mtambo huo upo chini ya usimamizi na utafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume  ya Mipango ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Bibi Florence Mwanri imefanya ziara katika Kiwanda cha Tanga Cement kilichopo Mkoani hapa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.

  Katika ziara hiyo, Bibi Mwanri alipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na eneo linalotumika kuchimba malighafi za kutengenezea saruji, teknolojia ya kisasa inayotumika kuendesha mashine kiwandani hapo pamoja na kuangalia hatua mbalimbali zinazotumika katika uzalishaji wa saruji.

  Akiwa katika eneo linalochimbwa mawe ya kutengenezea saruji, Mwanri alieleza kuwa kiwanda hicho kina wajibu wa kuhakikisha sheria  na taratibu za utunzaji wa mazingira zinazingatiwa muda wote ili kuhakikisha mazingira yanabaki salama licha ya shughuli za uchimbaji kuendelea kufanyika. 
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akiuliza namna mifumo ya komputa ya kiwanda hicho inavyoendesha shughuli za uzalishaji wa saruji katika kiwanda cha Tanga Cement.

  Mwanri alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuwa nchi ya Viwanda na kuharakisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayosisitiza kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  Naye Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Ben Lema alisema kuwa kiwanda hicho kimeendelea  kutoa ajira kwa watanzania katika kada mbalimbali ambapo kwa sasa kua ajira zaidi ya 600 ambapo ajira 300 ni za moja kwa moja huku ajiara 300 zingine ambazo sio za moja kwa moja zinajumuisha wauzaji, wasambazaji, wasafirishaji na wengine walioko katika mnyororo huo.
  Meneja wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema akionesha aina za malighafi na aina mbalimbali za saruji zinazozalishwa na kiwanda hicho.

  Aliongeza kuwa bidhaa za kiwanda hicho bado zinafanya vizuri sokoni licha ya ushindani uliopo kufuatia kuanzishwa kwa  viwanda vingi vinavyozalisha saruji kwa kuwa mahitaji ya saruji bado ni mwakubwa sokoni.

  Lema alieleza kuwa viwanda vya saruji vinapata faraja kubwa kwa kuwa miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali na hata inayotekelezwa na sekta binafsi inatumia saruji inayotengenezwa na viwanda vya ndani.
  Meneja wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema (mwenye Miwani) akimwonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jenkundu) eneo (halipo pichani) linalochimbwa na kiwanda hicho kwa zaidi ya miaka 30 kwa ajili ya kupata malighafi zinazotumika katika kutengeneza saruji kiwandani hapo. Wengine ni Maofisa wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo walioambatana na Kaimu Katibu Mtendaji katika ziara hiyo.


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akiwa na wawakilishi wa kampuni zinazodhamini mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Marathoni 2017 pamoja na jeshi la Polisi ,akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mbio hizo.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 15 wa mbio za kimataifa za Kilimanjaro Marathon 2017 ,uzinduzi uliofanyika Kibo Palace Home mjini Moshi.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.


  0 0

  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko, on Tuesday morning engaged Senior Editors and Journalists at the Imperial Royale Hotel in Kampala, Uganda.

  As part of the Secretary General’s publicity and outreach programme to the Republic of Uganda, on the sidelines of the ongoing 5th Session of the East African Legislative Assembly sitting in Kampala, Amb. Liberat Mfumukeko hosted a Media breakfast meeting, during which he expounded on his priorities during his five-year tenure which began in April 2016.

  The Secretary General said he would focus on few priorities that will deliver quick results and on those that will touch on the lives of East Africans and address their basic needs such as food, health, education and improved incomes.
  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko( M) with Uganda’s Second Deputy Prime Minister and Minister of EAC Affairs, Rt. Hon. Kirunda Kivejinja (L) and Dr James Njagu, Chief de Cabinet to the Secretary General.

  He said a big percentage of EAC resources will be directed to sectors such as Agriculture, Health, Education, and Employment creation.

  “To achieve this I will strive to establish strategic partnerships with the Development Partners, the Private Sector and also the Civil Society Organizations and of course with you, Members of the fourth Estate”, said Amb. Mfumukeko.

  The Secretary General highlighted some of the key achievements in the regional integration process that include the robust implementation of the Single Customs Territory, which has resulted in drastic reduction of the period taken to clear goods from over 20 days to three (3) to four (4) days on the Central Corridor; and from 21 days to four (4) days from Mombasa to Kampala and 18 days to six (6) days to Kigali, on the Northern Corridor.

  Amb. Mfumekeko disclosed that out of the 15 border towns earmarked to operate as One Stop Border Posts, 11 had already been completed, adding that 10 of these were already operational.
  On the Common Market, the Secretary General said EAC Partner States had enacted new laws to conform to the Protocol, adding that currently Kenya, Rwanda and Uganda were allowing their respective citizens to enter and exit their territories using National Identity cards.

  READ MORE HERE

  0 0

  Benjamin Sawe.

  Mkuu wa wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amepiga marufuku matumizi ya nafaka kutengenezea pombe za kienyeji ili kujikinga na baa la njaa.

  Ndejembi amesema kumekuwa na tabia ya wananchi kufanya sherehe zisizokuwa na tija ikiwemo zile za jando na ngoma za asili kwa kutumia nafaka

  Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Ndejembi  amesema hivi sasa wilayani Kongwa kipo chakula cha kutosha majumbani, sokoni na kwenye Maghala yanayotumika kuhifadhi chakula.

  Amesema chakula kilichopo kikitumika vizuri kitawatosheleza wananchi mpaka pale watakapovuna mazao mengine katika msimu wa mavuno ujao.

  “Kongwa chakula kipo cha kutosha, wanaosema hakuna chakula ni wafanyabiashara wanaotaka kuzua hofu ili wapandishe bei ya mazao na wanasiasa waliokosa ajenda” Alisema Ndejembi.

  Mkuu huyo wa wilaya amesema hakuna sababu ya kuficha kama itatokea kuna upungufu wa chakula lakini kwa sasa hakuna upungufu wowote wa chakula wilayani Kongwa.

  Ndejembi amefanya ziara ya kutembelea maghala ya chakula yaliyopo Kibaigwa wilayani Kongwa ambako pia kuna soko la mahindi la kimataifa na kujiridhisha na chakula kilichopo.

  “Mahindi yapo ya kutosha na kama unavyojua hili ni soko la Kimataifa inamaana kungekuwa na upungufu ungeanzia hapa” Alisema Ndejembi.

  0 0


  Wasichana wanne wa Tanzania wakiaga kwa kupungia mikono huku wakiwa na Bendera ya Taifa waliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni Farida Mjoge,Elizabeth Betha, Edna Chembele na Ummy Mwabondo. (PICHA, HABARI NA RICHARD MWAIKENDA).
  Kamishna Mkuu wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), Symphorosa Hangi (kushoto) akiwakabidhi wasichana wanne, Bendera ya Taifa katika hafla ya kuwaaga kwenda Uganda ambako watakutana na wenzao 31 kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati katika mafunzo ya uongozi na utamaduni katika nchi hizo. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia niElizabeth Betha, Edna Chembele, Farida Mjoge na Ummy Mwabondo. 

  Na Richard Mwaikenda

  WASICHANA wanne wameondoka kwenda Uganda kwenye programu maalumu ya kubadilishana uzoefu wa mafunzo ya uongozi na utamaduni.

  Wakifika Uganda wataungana na wenzao 31 kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na Kati, ambapo watapigwa msasa wa mafunzo hadi Januari 25, mwaka huu watakapotawanywa kwenda nchi mbalimbali.

  Wasichana hao wanachama wa Chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA),waliondoka Uwanja wa Ndege wa Kimaitafa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, juzi kwa Ndege ya Kenya Airways, baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Kamishna Mkuu wa Tgga, Symphorosa Hangi.

  Wasichana hao 35 watagawanywa katika nchi hizo nane ambapo nchini wataletwa watatu kutoka katika baadhi ya nchi hizo, kuja kujifunza masuala ya uongozi na utamaduni.

  Akizungumza wakati wa kuwaaga wasichana hao, Kamishna Mkuu wa Tgga, Hangi alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wasichana ili wawe viongozi bora wa baadaye katika nchi zao ikiwemo pia kujiamini na kujithamini.

  Alitaja nchi zitakashiriki kwenye programu hiyo ambayo kwa hapa nchini ilianza mwaka jana, kuwa ni; Tanzania, Kenya, Uganda, Zambia, Rwanda, Burundi, Zimbabwe na Afrika Kusini.

  Alisema kuwa watakapokuwa kwenye nchi hizo husika, kila mmoja ataishi maisha ya kujitegemea kwa kwenda vijijini kuishi na wananchi na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali ya maisha ikiwemo uongozi, utamaduni, kujiamini na kujithamini. Gharama za kwenda katika nchi hizo hufahiliwa na Taasisi ya FK Norway ambayo huwapatia nauli, fedha za malazi, posho na masuala ya afya.

  Alisema kuwa watakaporejea nchini Julai mwaka huu, watapaswa kutoa mrejesho wa waliojifunza huko, ili usaidie kuwaelimisha wasichana wengine nchini.
  Kamishna akiwakabidhi nyaraka mbalimbali.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na: Lilian lundo - MAELEZO

  Serikali ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza ikiwa nchi inakabiliwa na janga la njaa na wala si taasisi, asasi za kiraia au wanasiasa.

  Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha UDP John Cheyo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu mijadala mbalimbali inayoendelea katika vyombo mbalimbali vya habari kwamba Tanzania imekabiliwa na tatizo la njaa.

  Cheyo alisema kuwa, huwezi kusema nchi ina njaa wakati vyakula vipo katika masoko mbalimbali hapa nchini. Amewataka watanzania kutofautisha kupanda kwa bei za vyakula na janga la njaa.

  Aidha, Cheyo alisema kuwa tatizo hilo tayari limetatuliwa na Serikali kwa kutoa tani milioni 1.5 za mahindi  ambazo zitasambazwa nchi nzima kwa ajili ya wananchi kununua.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa mahindi hayo kuuzwa kwa uangalifu kwani gharama yake itakuwa ni ya chini, hivyo kuna watu ambao watajitokeza kununua kiasi kikubwa na kwenda kukihifadhi kwa ajili ya kukiuza kwa gharama ya juu baadae.

  Vile vile aliwataka watanzania kuwa na tabia ya kutunza vyakula badala ya kuuza vyakula vyote mara wanapovuna, ili vyakula hivyo viweze kuwasaidia pale ambapo mvua zinakuwa zimechelewa kama ambavyo imekuwa kwa mwaka huu.

  0 0

  Mwanasiasa wa Italia, Antonio Tajani amechaguliwa kuwa Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya, akichukua nafasi inayoachwa na Rais anayemaliza muda wake, Martin Schulz kutoka Ujerumani. Tajani amethibitishwa baada ya uchaguzi wa duru ya nne uliokuwa na ushindani mkali uliofanyika jana mjini Strasbourg, Ufaransa.

  Antonio Tajani, mshirika wa Waziri Mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi, anachukua nafasi ya Martin Schulz kutoka Ujerumani, aliyemaliza muda wake. Tajani anayetoka katika muungano wa vyama vya kihafidhina vinavyofuata siasa za wastani za mrengo wa kulia wa European People's Party, EPP alimshinda kwa kura 351 Muitaliano mwenzake, Gianni Pitella kutoka muungano wa vyama vya siasa za wastani za mrengo wa kushoto vya kisoshalisti na kiliberali, S&D aliyepata kura 282.

  Kura 633 zilikuwa halali kati ya jumla ya kura 713 zilizopigwa katika duru ya mwisho ya uchaguzi, huku wabunge 80 wakiwa hawajapiga kura. Akizungumza baada ya ushindi huo, Tajani ambaye amekuwa mjumbe wa bunge la Umoja wa Ulaya tangu mwaka 1994 ameahidi kutetea demokrasia na uhuru wa wananchi wa Umoja wa Ulaya.
  Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Antonio Tajani. 
  ''Huu ulikuwa mchakato wa kidemokrasia na kama nilivyosema leo, nitakuwa rais wa wote, nitamuheshimu kila mwakilishi na nitayaheshimu makundi yote,'' amesema Tajani.
  Ahadi alizotoa.

  Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 63, anajulikana kutokana na aina yake ya uwazi na washirika wengi, pamoja na ukaribu wake na Berlusconi. Aidha, ameahidi kupambana na ugaidi na kushughulikia masuala ya uhamiaji ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wanasiasa wa mrengo wa kulia.

  Kwa upande wa wanasiasa wa kijani, ameahidi kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kwa wale wa mrengo wa kushoto amewaahidi kushughulikia suala la ukosefu wa ajira. Amebainisha kuwa uhuru ni jambo muhimu kwa Umoja wa Ulaya, muhimu kwa historia na mustakabali wa umoja huo.
  Rais wa Umoja wa Ulaya anayemaliza muda wake, Martin Schulz (kulia) akiwa na Rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya, Antonio Tajani.
  Rais anayemaliza muda wake, Martin Schulz, amempongeza Tajani baada ya kuchaguliwa na amemtakia kila la heri katika majukumu yake mapya. Amesema yuko tayari kushirikiana naye kwa sababu Umoja wa Ulaya unahitaji bunge lenge nguvu na madhubuti.

  Tangu mwaka 2014, Tajani ambaye pia ni mwanasheria, amekuwa makamu wa rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya. Pia amewahi kufanya kazi katika Halmashauri ya Umoja wa Ulaya. Kuanzia mwaka 2008 hadi 2010 alikuwa kamishna wa usafiri na kisha kuwa kamishna wa viwanda kuanzia mwaka 2010 hadi 2014.

  Majukumu ya rais wa Bunge la Umoja wa Ulaya ni pamoja na kuangalia bajeti na shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria na kuhakikisha taratibu za bunge zinafanyika vizuri. Rais pia analiwakilisha bunge hilo katika masuala ya kimataifa na katika migogoro ya aina yoyote ile ya kisheria.Imeandikwa na Mtandao wa DW.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana akimkaribisha Balozi wa China hapa nchini, Dk. Lu Young, alipofika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha katika ukumbi wa mazungumzo Balozi wa China hapa nchini Dk. Lu Young, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dk. Lu Young, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo .

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtambulisha Katibu mpya wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinza, wakati wa mazungumzo yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Saalaam, leo. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Kampuni ya ndege ya Air India hii leo inazindua ndege itakayokuwa na viti vya wanawake pekee kwa lengo la kukabiliana na unyanyasaji wa kingono .

  Viti sita vitahifadhiwa kwa ajili ya wanawake, kwa ndege kadhaa. Wanawake kadhaa akiwemo muhudumu mmoja wa ndege wamelalamikia ndege hiyo wakidai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono na abiria wa kiume.

  Mkuu wa muungano wa Abiria nchini humo amepinga mpango huo wa viti, akiutaja kuwa wa kiubaguzi.

  Hatua ya kutenga viti kulingana na jinsia fulani sio jambo la kawaida kimataifa.BBCSWAHILI.

  0 0  0 0

  Chanzo cha Maji cha Shiri kilichopo wilaya ya Hai.
  Madiwani wakiwa katika chanzo cha maji cha Shiri walipofanya ziara kutembelea vyanzo hicho na kupata maelezo.
  Madiwani wakipata maelezo kutoka kwa Meneja Ufundi wa Mamlaka hiyo ,Patrick Kibasa namna maji yanavyotibiwa.
  Madiwani wakiwa katika chanzo kipya  cha maji cha Mkashiringi .
  Meneja Ufundi wa MUWSA,Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa madiwani mara baada ya kutembelea chanzo cha maji cha Njoro ya Goha.


  0 0

   Mkurugenzi wa Uraghabishi na Habari – TACAIDS Jumanne Issango akizungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mratibu wa Shughuli za Vijana TACAIDS Bibi. Grace Kessy, Mratibu Mwandamizi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro na Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam, Dkt. Fredy Frank.
   Mratibu Mwandamizi wa Shirika la Restless Development Bw. Oscar Kimaro akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uraghabishi na Habari – TACAIDS Jumanne Issango na Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam kutoka Shirika la PACT, Dkt. Fredy Frank (katikatika).
    Mratibu wa Shughuli za Rufaa kwa Watoto na Walezi waishio katika mazingira magumu Dar es Salaam, Dkt. Fredy Frank akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na wawakirishi kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Restless Development na Shirika la PACT uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.


  0 0

  CHAMA Cha Wanyakazi wastaafu wilaya ya Singida kimesema kuwa idadi kubwa ya wafanyakazi waliostaafu utumishi wa serikali hawajui kuwa  wanapaswa kulipwa mafao kwa kipindi cha miaka mitatu mara baada ya mume au mke wa mnufaika wa mafao hayo atakapofariki.
  Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyakazi Wastaafu Mkoa wa Singida,Shabani Mwanja aliyasema hayo kwenye mkutano wa wanachama wa chama hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kituo cha walimu Nyerere,Manispaa ya Singida.
  Alifafanua Mwanja kwamba  iwapo mtumishi wa serikali aliyestaafu anapokea mafao ya uzeeni,endapo atafariki mwenza wake atapaswa kulipwa mafao hayo( Survival Penshen) kwa kipindi cha miezi 36 (miaka mitatu) yeye pamoja na mtoto ambaye alikuwa bado tegemezi wa marehemu.
  “Watumishi wale wanaopokea pensheni serikalini akifariki mwenza wake analipwa survaival Penshen miezi 36 au miaka mitatu yeye na mtoto wake ambaye alikuwa bado tegemezi wa marehemu,mnanielewa hapo ?”alihoji Makamu Mwenyekiti huyo.
  Aidha Mwanja alibainisha pia kuwa kama mama amefariki wakati alikuwa akipokea malipo ya pensheni,baba atalipwa miezi 36 na mtoto tegemezi ambaye alikuwa bado ana umri mdogo,au mama vile vile atalipwa kwa ajili ya mume wake aliyefariki akiwa analipwa pensheni na mtoto ambaye alikuwa tegemezi.
  “Hiyo mlikuwa mnaielewa sasa ikitokea nenda kwenye mfuko unaohusika utalipwa Survaival Penshen,sawa eeeh ?”aliwahoji wanachama hao wa wafanyakazi wastaafu.
  Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Singida,Hassani  Dumwala aliweka bayana kwamba lengo la kuanzishwa kwa chama hicho ni kupigania maslahi ya wafanyakazi wastaafu ili waweze kunufaika na huduma wanazotakiwa kupatiwa na serikali baada ya utumishi wao kufikia ukomo.

   Baadhi ya wanachama wa chama cha wafanyakazi wastaafu wa wilaya ya Singida wakipiga kura za kukubaliana kuahirishwa kwa mkutano huo baada ya wajumbe wa kata nne kutohudhuria kwenye mkutano huo na nhivyo kupangwa kufanyika tena jan,31,mwaka huu.(Picha zote na Jumbe Ismailly)

  0 0
 • 01/18/17--04:12: TAARIFA • 0 0

  Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.

  Ntetema amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.

  Mwasisi wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.

  Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.

  Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

  Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau  kuhusu ualibino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.

  Binagi Media Group
  Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
  Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
  Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa 
   Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro.

  Jeshi la Polisi nchini, limeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wao kote nchini huku ikiweka dhamira ya kutoza riba ya mkopo kwa  asilimia 10.5 kwa mwaka.  Akifungua mafunzo ya siku mbili yanayofanyika mkoani Morogoro, Kaimu kamanda wa Polisi hapa (ACP) Leonce Rwegasila, alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu na uzito wa mkutano huu ni vyema kila mshiriki akazingatia mahudhui ya kile kitakachotolewa ili kuwa mjumbe mzuri kwa kupeleka elimu mahala alikotoka, alisema.  Hata hivyo, alisema, katika mafunzo haya zipo mada pamoja na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa ili kuja na majibu mujarabu yatakayowezesha kuwa na Saccos imara na yenye kukidhi mahitaji kwa  wanachama wao ambao ni askari Polisi pamoja na familia zao.

  Kwa upande wake Meneja Mkuu wa URA SACCOS LTD (SSP) Kim O. Mwemfula, alisema zipo huduma zilizoanzishwa za uhakika za ushirika wa kuweka akiba na kukopa kupitia Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), ambapo askari aliye mwanachama wa ushirika huo uweza kuweka na kukopa kwa riba nafuu ili kuweza kuboresha maisha yake na familia yake katika Nyanja za Kielimu, Biashara na hata Ujenzi wa nyumba.  Ameongeza kuwa, masuala ya ustawi kwa askari yamesaidia kujenga utulivu wa akili kwa askari Polisi pamoja na kuboresha suala la ustawi wa usalama wa raia na mali zao na kulifanya taifa kuwa la amani na utulivu na kukabiliana na aina zote za matishio ya kiuhalifu na wahalifu.
  Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akipokea taarifa ya washiriki wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kutoka kwa (ASP) Emmanuel Katabi, kulia ni Meneja Mkuu wa URA SACCOS (SSP) Kim O. Mwemfula, na wamwisho ni (ASP) Bakari H. Mzungu.
  Mwezeshaji Mkaguzi wa Polisi (INSP) Edwin B. Mkole , akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za utoaji wa mikopo kwa wanachama wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakati wa mkutano mkuu wa nane wa chama hicho unaofanyika mkoani Morogoro.

  Baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakiwasili mkoani Morogoro, kuhudhuria mkutano mkuu wa nane wa chama hicho utakaofanyia kwa muda wa siku mbili na kuwashirikisha watendaji na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

      Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane unaofanyika mkoani Morogoro. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi).

  0 0

  Jana kampuni ya bidhaa za kucha, Lavy iliandaa semina kwa ajili ya baadhi ya watengeza kucha wanaotumia bidhaa zao ili kufundishana mawili matatu kuhusu bidhaa hizo na sekta nzima inayohusu masuala ya kucha. Semina hii ilifunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Afya, Doctor Kigwangala.
  Changamoto kwenye sekta hii ni nyingi kuanzia kwenye bidhaa, utengenezaji wa kucha, sehemu husika za kutengeneza kucha pamoja na watengeneza kucha wenyewe.Mbali na Lavy kuelimisha matumizi sahihi ya bidhaa zao pia imegusia changamoto nyingine nyingi zikiwepo usafi na usanifu na sekta hii.
  Mh. Doctor Kigwangala akizawadiwa notebook kwa ajili yake na bidhaa za Lavy kwa ajili ya Mke wake.
  Flaviana Matata akitoa somo kuhusu usafi wa vifaa na saluni kwa ujumla, huku akigusia kuhusu huduma bora kwa wateja itakayokua chachu ya kuongeza mapato ya saluni na idadi ya wateja.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Na Greyson Mwase, Mwanza

  Wananchi wa wilaya ya Ukerewe wameipongeza serikali kwa kasi ya miradi ya umeme katika wilaya hiyo, na kuongeza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi hususan za uvuvi.

  Waliyasema hayo katika nyakati tofauti jana katika ziara ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini yenye lengo la kujionea hatua iliyofikiwa ya maendeleo ya miradi hiyo inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy

  Akizungumza kwa niaba ya wenzake Katibu wa Kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank Matondane alisema kuwa kitongoji hicho hakikuwa na ndoto ya kupata umeme wangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika lakini matumaini yamepatikana baada ya kuanza kwa utekelezaji wa miradi ya umeme katika kitongoji hicho kupitia kampuni ya Rex Energy.

  Alisema mara baada ya wananchi kuhamasishwa na wataalam kutoka kampuni ya Rex Energy na kuona zoezi la ujenzi wa miundombinu ya umeme, walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kutodai fidia hali iliyorahisisha utekelezaji wa mradi huo.

  Matondane alisema kuwa mahitaji ya umeme katika kitongoji cha Ghana/Siza chenye wakazi wanaokadiriwa kuwa kati ya 2,500 hadi 5,000 ni makubwa husuan wavuvi wanaohitaji umeme kwa ajili ya kwenye majokofu ya kuhifadhia samaki.

  Aliongeza kuwa shule pamoja na maduka ya madawa baridi yanahitaji umeme na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, uchumi katika kisiwa hicho utakua kwa kasi kutokana na fursa zilizopo na kuvutia wawekezaji kwenye ujenzi wa kiwanda cha kusindika nyama ya samaki.
  Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto mbele) akibadilishana mawazo na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kwenye ziara ya kuelekea katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.
  Sehemu ya kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply kilichopo Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya Jumeme Rural Power Supply, Sitta Ngissa (katikati) akielezea hali ya uzalishaji umeme kwa kutumia nishati ya jua katika kituo hicho, Kushoto ni David Mwakigonja kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
  Mfumo wa kuongozea mitambo na vifaa vya kuzalisha umeme katika kituo cha kuzalisha umeme cha kampuni ya Jumeme Rural Power Supply.


older | 1 | .... | 1515 | 1516 | (Page 1517) | 1518 | 1519 | .... | 3282 | newer