Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

MBEYA CITY KUVAANA NA AZAM FC CHAMAZI KESHO


Kikundi cha Yamoto Band hakitatumbuiza tamasha la Sauti za Busara

$
0
0
JANUARY 16, 2017 — MJI MKONGWE,  ZANZIBAR:  Harakati za kukamilisha taratibu za ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band hazikufanikiwa kutokana na changamoto za ugumu wa mawasiliano baina ya uongozi wa kikundi hicho na Uongozi wa Sauti za Busara. Sauti za Busara  imesitisha taratibu za kuruhusu ushiriki wa kikundi cha Yamoto Band kwenye tamasha la mwaka huu kama ilivyotangazwa awali.
Yusuf Mahmoud, Mkurugenzi wa tamasha amesikitishwa na ugumu wa kufanya mawasilaino ndani ya muda husika kutengeneza mazingira mepesi ya uandaaji wa taratibu zote za kuhakikisha kikundi hicho kinakamilisha mahitaji yote ndani ya muda uliopangwa.

“Kuna vipaji vingi sana vya muziki Tanzania.  Vipaji hivi hufifia kwa sababu ya uhaba wa ujuzi kwa mameneja ambao hawajibu barua pepe, wanakataa kusaini mikataba, hawafiki kwenye mikutano hata baada ya kuthibitisha kuwa watashiriki, na hawapokei simu,’’ Yusuf alikaririwa akisema hayo wiki iliyopita kwenye gazeti la Sunday News.

Journey  Ramadhan, Meneja wa tamasha amesema kuwa jitihada za makusudi za kuhakikisha  Yamoto Band wanashiriki tamasha hazikuzaa matunda baada ya yeye kufika Dar es Salaam na kumsubiri meneja wa Yamoto Band afike kwa ajili ya maongezi lakini alisema yuko nje ya mji  na asingeweza kuonana naye.

“Ili kuibua, kung’arisha  na kukuza vipaji vya muziki Tanzania tunahitaji mameneja wenye kuheshimu mawasiliano yatakayowezesha wanamuziki kupata nafasi ya kuonesha vipaji vyao kupitia wadau wa muziki nchini. Pia ni vema msanii apate naasi ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataia ni lazima aanye mawasiliano kwa njia ya kieletroniki,’’ amesema Ramadhan.

Uzoefu wa kufanya kazi na mameneja wa wanamuziki  tofauti hapa nchini unaonesha ugumu wa kupokea simu, kushindwa kujibu barua pepe, kuhundhuria kwenye mikutano baina ya wadau wa muziki ili kujadili njia sahihi za kuhakikisha wasanii wanapata nafasi ya ushiriki ni changamoto kubwa zinazorudisha nyuma harakati za kukuza muziki Tanzania, amesema Ramadhan.

Yusuf ametoa wito kwa wasanii na mameneja wao kutumia tamasha la SzB  ambayo ni nafasi pekee  na sahihi ya  kutangaza na kuonesha kazi zao na kupanua wigo wa kung’arisha taaluma zao na kuongeza mawasiliano na wasanii na wadau wa muziki  kutoka sehemu mbali mbali duniani ambao hukutana kwenye tamasha hilo la siku nne mfululizo.

   

YANGA YAVUNJA REKODI YA MIAKA 30, WASHINDA 1-0 UWANJA WA MAJIMAJI

$
0
0

Ripota wa Globu, Songea.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wametoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Majimaji mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji Songea na kufikisha alama 43 wakiwa nyuma ya alama moja ya mahasimu wao Simba.

Mtanange huo ulioanza majira ya saa 10 kamili ilichukua dakika 15 kwa Deus Kaseke kuwainua mashabiki wa Yanga baada ya kumalizia krosi ya Haruna Niyonzima iliyopanguliwa na golikipa na kumkuta miguuni na kuachia shuti kali akiwa nje ya 18.

Yanga walionekana kutawala sehemu ya kiungo na kuweza kucheza mpira zaidi ya Majimaji lakini umakini wa safu ya ushambuliaji ilishindwa kuwa makini na kumalizia mipira ya mwisho iliyokuwa ikitengwa na Juma Abdul pamoja na Haruna Niyonzima.

Katika historia ya Majimaji na Yanga katikia Uwanja huo imeweza kuvunjwa leo baada ya miaka 30 kupita bila wanajangwani hao kuondoka na ushindi huku msimu uliopita wakiambulia sare.

Kali Ongala alionekana kutumia zaidi vijana katika mchezo huu dhidi ya Yanga lakini walishindwa kuonyesha umahiri wao, na ameweka wazi kuwa bado ataendelea kuwaamini vijana hao kwani ana imani watakuja kuwa wachezaji wa kutumainiwa hapo baadae.

Huu ni mchezo wa kwanza wa l.igi kuu  kwa Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kucheza ugenini na ameweza kuondoka na alama tatu muhimu ambapo zina faida kwake huku wakiangalia mechiu ya kesho baina ya Mtibwa na Simba utakaopigwa uwanja wa Jamhuri Morogoro. 

Kwenye mechi hiyo kulitokea vioja vya aina yake kwa Timu ya Yanga kushindwa kuingia vyumbani na kubadilishia nguo pembeni ya Uwanja.
 Uwanja wa Majimaji Songea taswira ya ndani kabla ya mtanange kuanza  kati ya Majimaji dhidi ya Yanga uliomalizika kwa Yanga kupata ushindi wa goli 1-0.

 Kabla ya kuanza kwa mchezo huo wakati timu ya Yanga wamewasili wakiwa wamekaa kwenye mabenchi na hawakuingia vyumba vya kubadilishia nguo.
 Wakati wa mapumziko timu ya Yanga wakiwa wanapata maelekezo kutoka kwa benchi la ufundi wakiwa hawajaingia ndani ya vyumba vya Uwanja.

AMSHA KIPAJI CHAKO NA MICHUZI TV NA IDRISSA WA MBEYA.

BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA KAKONKO LAMSIMAMISHA KWA MUDA DIWANI WA CHADEMA KWA UTOVU WA NIDHAMU

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko limemsimamisha kwa muda Diwani wa kata ya Gwalama Elia Kanjero (CHADEMA),kutohudhuria kikao kimoja cha Baraza la madiwani, kwa kosa la utovu wa nidhamu kwa baadhi ya Viongozi wa Serikali na Madiwani.


Adhabu hiyo ilitolewa jana katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri hiyo, ambapo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Maganga alisema adhabu hiyo imetolewa na kamati ya maadili ya baraza hilo ili kujenga nidhamu kwa madiwani wengine kuwa na nidhamu kama viongozi wanao waongoza Wananchi.

Maganga alisema kosa moja wapo lilopelekea adhabu hiyo ni pamoja na Diwani huyo kwenda kutolea ufafanuzi katika kipindi cha kipimajoto cha ITV wa Rasimu ya kodi ya majengo ambayo ilikuwa haijapitishwa katika halmashauri hiyo na kudai sheria hiyo inayowakandamiza Wananchi bila kibali cha mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.

Alisema Katika adhabu hiyo imeshuhudiwa na Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na Katibu wake ambae ni Mkurugenzi wa halmashauri na Mtuhumiwa atakabidhiwa barua yake ya adhabu kupitia kwa Afisa utumishi wa halmashauri.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Gwarama Elia Kanjero(CHADEMA) alisema yeye kama kiongozi wa uponzani kuadhibiwa kwasababu ya Wananchi ni faraja kwangu na nitaendelea kuwatetea Wananchi kwa uwezo wangu na nitaitumikia adhabu hiyo.

Kanjero alisema kosa lililopelekea kuadhibiwa ni pamoja na kuwashawishi madiwani kupinga rasimu ya Wananchi kulipa kodi ya majengo pamoja na kwenda kutoa maoni dhidi ya kutoshirikishwa Wananchi katika Baadhi ya mambo yanayo endelea katika halmashauri, jambo ambalo sioni kama ni kosa la kunifanya niadhibiwe.

"Suala lingine lililopelekea Kuadhibiwa ni baada ya Mtendaji wa kata ya Garama kugushi saini yake na kusaini fedha za Mfuko wa maendeleo ya kata baada ya kuleta malalamiko kwa Mkurugenzi wamuhamishi ikawa chanzo cha Mimi kuonekana sina nidhamu suala ambalo nilikuwa nikipigania haki yangu na Wananchi walio nichagua",alisema Kanjero.

RC RUKWA AZUNGUMZIA HALI YA KUTOKUWEPO KWA NJAA MKOANI KWAKE

MAJALIWA AFUNGUA DUKA LA DAWA LA MSD KATIKA HOSPITALI YA MPANDA

$
0
0
*Ni la MSD litahudumia mikoa mitatu ya kanda ya Tabora.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda lilogharimu sh. milioni 55 litakalohudumia mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Tabora.
Pia duka hilo itatoa huduma kwa vituo vya kutolea huduma za afya 580 ikiwa ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa miwili ya Kigoma na Tabora, Hospitali za wilaya sita za Nzega, Igunga, Urambo, Kobondo, Kasulu na Mpanda Mji.

Waziri Mkuu amefungua duka hilo la dawa la MSD, lililoko  katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi leo (Jumanne, Januari 17, 2017) ikiwa ni utekelezaji wa agizo alilolitoa kwa MSD Agosti 20, 2016 alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Katavi. Aliuagiuza  uongozi MSD kujenga duka hilo ili kurahisisha upatikanaji wa dawa katika mkoa huo pamoja na mikoa jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema baada ya kufunguliwa kwa duka hilo Serikali haitarajii kusikia tena katika vituo vya afya na Zahanati zilizoko mkoani Katavi na mikoa jirani  zinakosa dawa. Amewaagiza Wakurugenzi kusimamia suala hilo na kuhakikisha vituo vyote vya afya vinakuwa na dawa za kutosha.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kukutana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili kutafuta namna bora ya kutumia fedha za huduma za afya zinazipatikana katika halmashauri nchini.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imetoa sh. bilioni 1.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa wa Katavi ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.

Amesema lengo la Serikali ni kuwa na Hospitali ya Rufaa kwa kila mkoa, hivyo, Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa mipya itakayojengwa Hospitali ya Mkoa ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bw. Laurean Bwanakunu amesema ujenzi waduka hilo la Mpanda hadi kukamilika umegharimu sh. milioni 55, huku benki ya CRDB ikitoa sh. milioni 50 na MSD imeweka dawa na vifaa tiba vya sh. milioni 104.45 na vifaa vya TEHAMA vya sh. milioni tano.

Amesema kuanzishwa kwa duka hilo kutaongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa hasa dawa ambazo hazimo katika orodha zilizoidhinishwa na Serikali kutumika katika vituo vyake vya kutolea huduma za afya ila zimeidhinishwa kutumika nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Amesema dawa na vifaa tiba vilivyomo katika orodha ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) zinapatikana katika duka hilo kwa bei nafuu, hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa kwenda kuzitafuta katika maduka ya mbali na kwa bei ghali.

“Nitoe mfano mdogo wa tofauti ya dawa katika ya maduka ya MSD na maduka ya mitaani, hapa dawa ya sindano ya kutibu fungus aina ya Fluconazole inauzwa sh. 2,300 na mitaani sh. 4,500 na dawa ya sindano kwa ajili ya kushusha kisukari (Insulin) chupa moja MSD ni sh. 8,500 na mitaani sh. 20,000,” amesema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 17, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.    Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Rafael  Muhuga na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo, Wapili kulia ni Mbunge wa mapanda Mjini, Sebastian Kapufi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi  baada ya kufungua duka la dawa  la MSD katika hospitali ya Mpanda  Januari 17, 2017. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na kulia ni Mbunge wa Mapanda Mjini Sebastian Kapufi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kakitazama dawa za bibadamu baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.  Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Katavi, Muselem Said Abdallah.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kakitazama dawa za binadamu baada ya kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali ya Mpanda Januari 17, 2017.  Kushoto  ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu .
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Elizabeth Zephania , mmoja wa wazazi waliojifungua katika hospitali ya Mpanda  wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo Januari 17, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)7.

CCM YAWAASA WANANCHI KUWAPUUZA WANASIASA WANAOGEUZA MATATIZO YAO KAMA MTAJI WA KISIASA

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni vyema wananchi wakaanza kuwapuuza wanasiasa wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakigeuza matatizo ya wananchi kama mtaji wa kisiasa. 

Hayo yamesemwa na katibu wa Siasa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini. 

“CCM haitashiriki malumbano yasiyo kuwa na tija kwa lengo la kuleta uchochezi kwa wananchi kama ilivyo kwa viongozi wa vyama vya upinzani nchini, ambao wamekuwa wakitoa matamko kuwa Taifa limekumbwa na baa la njaa kama sehemu yao ya mtaji wa kisiasa, jambo ambalo Chama cha Mapinduzi kinaona hiyo ni siasa chafu” amesema Polepole.
Amesema kuwa kwanza tuwapuuze na maneno yao, kwani mwenye mamlaka ya kutangaza baa la njaa nchini ni Rais peke yake, hivyo ni vema wakajua kuwa Tanzania hatujafikia kiwango hicho, ambao wao wanakiomba, bali wanatakiwa kujua kuwa mpaka sasa tuna kiasi cha Tani Milioni 1 na nusu ambacho kitasambazwa katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu wa chakula. 

Ameongeza kuwa sera ya CCM ni kujitegemea, hivyo kama ndicho chama ambacho kinaongoza dola,hatujafikia hatua ya kukosa chakula katika nchi yetu. 

Pole Pole Ametoa wito kwa viongozi mbalimbali nchini kuacha kubweteka na kuwalaghai na kuwafarakanisha Wananchi,bali wanapaswa kuwaambia ukweli wananchi ili waweze kutunza nafaka na kuacha kutumia kwa matumizi mabaya kama kupikia pombe na masuala mengine yasiyokuwa ya lazima.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KINGDOM LEADERSHIP NETWORKS

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameuhimiza uongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania kuharakisha mchakato wa kuanzisha Chuo cha Joseph Business School hapa nchini chuo ambacho kitatoa mafunzo mbalimbali ya biashara, maadili ya uongozi na ugunduzi wa mawazo ya biashara ili kusaidia mamia ya Watanzania kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

Makamu wa Rais ametoa kauli ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania ambao walimtembelea Makamu wa Rais kumweleza hatua ambazo wamefikia katika uanzishaji wa Chuo hicho.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema wazo la uanzishaji wa Chuo hicho ulitolewa na Dkt Bill Winston ambaye ni Mwanzilishi wa Winston Ministries mwaka jana katika Maombezi ya Taifa ambaye yeye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo, anasema aliupokea kwa furaha mpango huo kwa sababu chuo hicho kitasaidia watanzania wengi kupata elimu na ujuzi wa kuimarisha biashara zao wakati taifa likielekea kwenye uchumi wa Viwanda.

Amesema hatua za uanzishwaji wa Chuo hicho hapa nchini ni fursa pekee na nzuri kwa Watanzania kujifunza ubunifu na ugunduzi katika biashara, maadili ya uongozi katika biashara ili kuongeza ufanisi katika biashara zao kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla hasa katika ulipaji wa kodi.

Kwa Upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma na Meneja Mradi Dkt Charles Sokile wamemhakikishia Makamu wa Rais kuwa hatua ambazo wamefikia kwa sasa katika uanzishaji wa Chuo hicho ni nzuri ambapo mpaka sasa wamepata majengo kwa ajili ya ofisi na maeneo ya kufundishia na hatua za usajili wa chuo hicho zipo katika hatua za mwisho.

Wamesisitiza kuwa wanataka kushirikiana ipasavyo na Serikali katika uanzishaji wa chuo hicho ambacho kitatoa elimu ya biashara hasa ugunduzi wa mawazo ya biashara nchini kama hatua ya kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda nchini.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania Ibrahimu Kaduma aliyemtembelea Makamu wa Rais na kumuelezea mikakati ya kuanzisha Chuo cha Joseph Business School kushoto ni Meneja Mradi Dkt Charles Sokile.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania uliomtembelea ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.

WAZIRI MWIJAGE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA CHA SABUNI, PWANI

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizindua Jiwe la Msingi la Kiwanda Keds.kwakushirikina na Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni (Keds) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.

Kiwanda hicho ni cha pili kujengwa katika Bara la Afrika baada ya cha kwanza kujengwa nchini Ghana.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe hilo,Waziri Mwijage amesema kuwa amefurahi kuona mapambano yakuendeleza Tanzania ya Viwanda,amesema kupitia ujenzi wa Viwanda hivyo ukuaji wa Uchumi utakuwa sambamba na ukuaji wa Maendeleo ya Watu.

Pia amesema kuwa Kiwanda hiko cha Keds kimeitoa Tanzania kimasomaso katika kutimiza asilimia 40 ya upatikanaji wa ajira pamoja na kuziomba Mamlaka za Mikoa kote nchini kuiga Mfano wa Pwani katika Uwekezaji wa Viwanda na kujifunza ukarimu kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),Clifford Tandari amesema kuwa ni fursa muhimu kwa kuwa Kampuni hiyo tayari ina Kiwanda Ghana hivyo kujengwa Tanzania kitakuwa cha pili.

Amesema kuwa baada ya Kiwanda hicho kuisha kitaokoa gharama za uingizaji wa sabuni kutoka nje.

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng,amesema tangu kuanza kwa mradi huo wametumia muda mfupi kuweka sawa ardhi ya eneo hilo pia amesema kuwa watajenga kwa uzoefu na ujuzi ili kutimiza azma ya uwekezaji bora Tanzania.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa Kiwanda cha Keds kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini, Clifford Tandari akizungumza wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Mkurugenzi wa Kiwanda hiko, Jack Feng akizungumza wakati wa uwekwaji wa jiwe la msingi katika Kiwanda cha Sabuni cha Keds.
Baadhi ya viongozi mbalimbali na wanachi wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kiwanda cha Sabuni(Keds) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani. 

PROF. MBARAWA AFANYA ZIARA OFISI ZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA, JIJINI DARA

$
0
0
Waziri Profesa Mbarwa (kushoto), akimweleza jambo Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati akitembelea Posta Kuu, maeneo ya Posta Mpya jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama cha Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,Profesa Makame Mbarawa akiwasili Ofisi za Posta Kuu ya Shirika la Posta maeneo ya Posta Mpya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Dar es Salaam leo. Kulia ni Postamasta Mkuu, Fortunatus Kapinga.(Picha zote na Kassim Mbarouk)
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Posta Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi (katikati), wakati alipofika katika ziara ya kushtukiza kwenye Ofisi za Shirika la Posta, Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo kuangalia shughili mbalimbali zinavyofanyika ofisini hapo.

YANGA YAIDUNGUA MAJIMAJI YA SONGEA 1-0 NYUMBANI KWAO

$
0
0

Timu ya Maji Maji ya Songea (WANALIZOMBE) wameshindwa kuutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kufungwa bao moja na YANGA katika mchezo uliochezwa uwanja wa MAJI MAJI mjini SONGEA mkoani RUVUMA, Hapa tumekusogezea goli la YANGA pamoja na mahojiano na makocha wa timu zote mbili.

Miss Universe Tanzania afanya onyesho la mavazi ya ufukweni huko Manila, Philippines

$
0
0
Miss Universe Tanzania ambaye anashiriki katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yanayoendelea kufanyika huko jijini Manila, Philippines, Jihan Dimack akipita jukwaani kuonyesha vazi lake la ufukweni katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yaliyofanyika katika Ukumbi wa Jpark Island Resort and Waterpark, Cebu, jijini Manila - Philippines. Warembo wote wanaoshiriki mashindayo hayo, wanaendelea na ziara katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na maandalizi mbalimbali kuelekea kilele cha shindano hilo, kinachotarajiwa kufanyika Januari 29, 2017 huko Manila, Philippines.

WAZIRI MKUU AITAKA MTWARA ICHUNGUZWE SABABU ZA KUFELI KIDATO CHA PILI

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
                                                                       
Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri. 

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda. 

Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.

“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.

Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.

Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.

Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI JANUARI 17, 2017


TIMIZA MALENGO NA NDOTO ZAKO KUPITIA ‘BONUS ACCOUNT’ YA NMB

$
0
0
Je, unafahamu kwamba ni rahisi kufikia malengo yako ya kujiwekea akiba ukiwa na “NMB Bonus Account au Business Savings Account” ambayo inakupa faida hadi 13%*? 
Mfano, ukiwa na lengo la kujiwekea akiba ya shilingi 500,000 kwa mwaka 2017 inabidi uweke kiasi cha shilingi 42,000 tu kwa mwezi na ukiwa na nidhamu ya kuhakikisha kwamba kiwango hakipungui kiasi ulichojiwekea basi utakuwa umechagua njia sahihi kuelekea kutimiza ndoto zako. Jambo la msingi ni kuhakikisha unakuwa na akaunti ambayo haiingiliani na matumizi yako ya kila siku, hii ni hatua muhimu katika kutimiza malengo binafsi uliyojiwekea ama ya kibiashara.

NMB inatambua umuhimu wa kujijengea nidhamu ya kuweka akiba na kuwaletea wateja wake bidhaa zitakazowasaidia kuweka akiba na pia kuhakikisha wanakuza na kupata maendeleo binafsi na ya kibiashara. ‘Bonus Account’ na ‘Business Savings Account’ ni akaunti maalum kwa ajili ya wateja wanaotaka kutimiza malengo yao binafsi au ya kibiashara. 

Labda ungependa kuweka akiba kwa ajili ya kulipia ada ya mwanao mwakani, kununua nyumba miaka minne ijayo au kuanzisha biashara miaka siku za usoni, ukiwa na akaunti hizi utakuwa umepata njia sahihi ya kufikia malengo yako.

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA JAJI PROF. IBRAHIM JUMA KUWA KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA

Tanzania kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System)

$
0
0
 
Kaimu Kamishna Mkuu TRA, Mary Maganga.

Katika kuhakikisha inaboresha huduma kwa wafanyabiashara ambao wanaingiza mizigo nchini kwa njia ya bandari, mipaka na viwanja vya ndege, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeeleza mpango wa Serikali wa kuanza kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao kwa hakika utamaliza tatizo la mizigo kukaa muda mrefu kwa sababu ya kukosekana vibali. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mafunzo ya siku moja kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma kwa taasisi zinazotoa vibali na wafanyabiashara, Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix alisema lengo la kuanza kutumia mfumo huo ni kuboresha huduma ambazo wanazitumia sasa ili wafanyabiashara wanaoingiza mizigo nchini waweze kuipata kwa haraka kuliko ilivyo sasa.
Meneja Mfumo wa Kieletroniki wa Dirisha Moja la Huduma, Tinka Felix akizungumza kuhusu mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System). (Picha zote na Rabi Hume - MO DEWJI BLOG)

“Ni mpango wa Serikali kuboresha huduma kwa wateja kwa kupunguza muda wa kutoa mizigo bandarini au mipakani au kwenye viwanja vya ndege, kupitia mfumo huu wateja hawatakuwa wakienda kwenye idara na taasisi za Serikali na badala yake wakiwa hukohuko kwenye ofisi zao wataweza kuomba na kupata vibali na kupata bili za malizo kwenda kulipa benki, mfumo pia utafanya kazi na benki," alisema Felix. 
 
Alisema Tanzania haitakuwa nchi ya kwanza kutumia mfumo huo na mataifa mengi yanautumia ili kurahisisha huduma kutolewa kwa haraka kwani mfumo wa sasa wa forodha (tancis system) unashindwa kufanya kazi kwa haraka jambo ambalo linasababisha mizigo kuchelewa kutolewa kutokana na muda mrefu mmiliki kutumia kutafuta vibali. Mkurugenzi wa Sera Utafiti Na Ushauri wa TPSF, Gili Teri akizungumza faida za kutumia mfumo wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System).

“Mfumo wa sasa ili mtu apate kibali anatakiwa atembelee hizo ofisi hata mara 10 na baadhi ya ofisi wanataka vibali zaidi ya kimoja lakini mfumo huu wa sasa muda ambao unatumika kuomba vibali utapungua na tunategemea kuokoa Dola milioni 65 kwa kutumia tu mfumo wa electronic single window system,” alisema Felix. 
 

Alisema kwa sasa kuna taasisi za Serikali 47 ambazo zinatoa vibali lakini mfumo wa Dirisha Moja la Huduma utatumiwa na taasisi 32 ambazo kwa pamoja zitakuwa zikitoa vibali 106. Aidha alisema Serikali imeagiza kuwa mfumo huo uanze kutumika baada ya mwaka mmoja hivyo wanategemea kuanzia mwakani mfumo ambao watakuwa wakitumia utakuwa ni wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window System) ambao utawezesha wafanyabiashara ambao wanatoa mizigo kupitia bandari, mipaka au viwanja vya ndege kupata vibali kwa haraka. 

MTWARA ICHUNGUZWE SABABU ZA KUFELI KIDATO CHA PILI-MAJALIWA

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi Wazara wa Elimu Sayansi na Telnolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenda mkoani Mtwara kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zilizosababisha shule tisa za mwisho katika matokeo ya kidato cha pili kutoka mkoani humo.
Pia ameziagiza halmashauri nchini kushirikiana na Idara ya Ukaguzi ili kuhakikisha wanawasimamia vizuri walimu jambo litakalowezesha kuboresha ufundishaji na hatimaye kupata matokeo mazuri.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Januari 17, 2017) wakati akizungumza na watumishi na wananchi wa mkoa wa Katavi alipowasili Ikulu ndogo ya Mpanda kwa ajili ya kufungua duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda.
Kwa mujibu wa matokeo hayo kati ya shule 10 za sekondari zilizofanya vibaya kwenye mtihani huo, tisa zinatoka katika Mkoa wa Mtwara na moja Tanga. Shule za Mtwara zilizofanya vibaya ni Chingungwe, Malocho, Naputa, Chanikanguo, Mtiniko, Michiga, Msimbati, Salama na Lukodoka  huku ya Tanga ikiwa ni Nywelo.
“Viongozi wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) waende Mtwara wakafuatilie kwa kina wajue kuna nini hadi shule tisa kati ya 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili mwaka jana zitoke huko,” amesisitiza.
Mbali na kuuagiza huongozi wa wizara hizo kwenda mkoani Mtwara pia Waziri Mkuu amewataka wasimamie vizuri mikoa ambayo awali ilikuwa na matokeo mabaya na sasa inafanya vizuri na wahakikishe shule za mikoa hiyo hazishuki na badala yake ziendelee kupata matokeo mazuri zaidi.
Awali, akisoma taarifa ya mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga alisema katika matokeo ya mtihani kidato cha pili ya mwaka jana mkoa wake ulishika nafasi ya pili kitaifa ukiongozwa na mkoa wa Geita.
Alisema kwa sasa wanajipanga kuhakikisha katika mitihani ya mwaka huu wanashika nafasi ya kwanza kitaifa, hivyo alitoa wito kwa watendaji wa Idara ya Elimu, wakuu wa shule, wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JANUARI 17, 2017.

RC.ZELOTHE ATANGAZA MKOA WA RUKWA HAKUNA NJAA-

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amesema kuwa Mkoa hauna njaa baada ya kufanya ziara katika maghala mbalimbali ya wajasiriamali pamoja na kiwanda cha Unga cha Energy Mills vyote vilivyopo katika mji wa Sumbawanga.

“Mmejionea wenyewe, Katika Manispaa ya Sumbawanga suala la kwamba hakuna chakula ama kuna njaa ni maneno hewa, hakuna kitu kama hicho, Chakula kipo cha kutosha nafaka karibu zote zipo,” Mkuu wa Mkoa alisisitiza.

Ameongeza kuwa wakulima wengi wameonekana kuuza mazo yao kwa wachuuzi na kusababisha wafanyabiashara wa masokoni kwenda kununua mazao hayo kwa bei na matokeo yake naoi li wapate faida nao wanaongeza bei jambo linalosababisha wananchi kushindwa kununua na wao kulalamika kuwa hakuna wateja. 

Katika suala la malalamiko ya wananchi kuosa pesa Zelote Stephen alifafanua “malalamiko yaliyokuwepo kuwa pesa hakuna, nami nakubali, kipindi hiki tulichopo ni wakati wa kilimo na wakati wa kilimo maana yake kila mtu yupo shambani, na mwezi ujao (Februari) kuanzia tarehe 20, kuna taarifa kwamba watu wataanza kuvuna maharage, kwahiyo ni dhahiri kwamba suala la njaa na bei hakuna mtu ambae atalizungumzia.”

Katika kulishuhudia hilo mmiliki wa kiwanda cha Energy Mills, Aziz Tawakali alisema kuwa mpaka sasa katika ghala lake ana tani 30 na mifuko 3400 ya unga wa sembe wenye kilo 50 kwa kila mfuko, na kuongeza kuwa kwa idadi hiyo kiwanda chake kinaweza kufanya biashara hadi mwezi wa tatu mwaka huu.

“Sio kwamba kuna njaa, na katika mwaka mzima hatujawahi kukosa stock ya chakula, na wa stock hii niliyonayo nina uwezo wa kuuza mpaka mwezi wa tatu” Azizi alithibitisha.

Nae mmoja wa wamiliki wa mashine za mpunga Mathias James amethibitisha kuwa katika Mkoa wa Rukwa hakuna shida ya chakula bali shida iliyopo ni ya wateja wa kununua chakula hicho, hivyo aliwaasa wale wote wanaosema kuwa hawana chakula cha kununua wafike katika ofisi yake.

“Kusema kuwa kuna njaa, hiyo si kweli, maana sisi tunahangaika kutafuta wateja, na wateja tunaowategemea ni kutoka Mbeya na Tunduma na wengine kutoka nchi za jirani kama Zambia na Kongo, hivyo tunawaasa wale wanaotafuta mchele, kwetu upo, tuna magunia ya mpungaya kilo 90 zaidi ya 18,000 hayana wateja, mpunga upo, mahindi yapo, waohitaji watuone,” Mathias alisisitiza.

Nao baadhi ya wajasiriamali wadogo wadogo wanouza kwa visado nao pia waliendelea kulalamikia upungufu wa fedha katika mifuko yao na kuongeza kuwa shida za wananchi si chakula kwa sasa bali pesa ndio ngumu na ndio inayotusababishia njaa.

“Njaa yetu pesa hakuna chakula kipo ila hela ya kununulia hayo mahindi ndio hakuna, kutokana na mzunguko wa biashara hela hakuna ila chakula kipo,” Deus Malonga alisema.

Nae Agness Palakata alisema “Tokea asubuhi tunauza hilo gunia halijaisha, sasa namna hii hatuwezi kurudi nyumbani uawalisha watoto, pesa hakuna, chakula kipo ila pesa ndio tatizo, shida yetu na njaa yetu ni pesa.”

Kwa kuthibitisha kutokuwepo kwa njaa Zelote Stephen aliongeza kuwa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wana jumla ya tani 15,500 ambazo zipo kwenye magala yao.

Kaimu Afisa Habari Mkoa wa Rukwa
Abdulrahman Salim.


Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images