Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 1516 | 1517 | (Page 1518) | 1519 | 1520 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), kuhakikisha vijiji vyote nchini ambavyo havijaunganishwa na huduma ya  mawasiliano vinaunganishwa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

  Aidha, Profesa Mbarawa amesisitiza mfuko huo kutoa kipaumbele kwa vijiji vyote vilivyomo sehemu za mipakani ili kuimarisha ulinzi na uharaka wa mawasiliano katika maeneo hayo.Amewaagiza UCSAF kukutana na mitandao ya simu ili kukamilisha kazi  kwa mujibu wa mkataba kwa kata 121  ambazo hazijapata huduma ya mawasiliano hapa nchini.

   “Nia ya Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote nchini vinapata huduma ya mawasiliano ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba ili kuwezesha mikakati mingine ya kuboresha Mifumo ya Tehama katika shule na Hospitali kuendelea na hivyo kuhuisha huduma za Tehama katika Sekta za afya na elimu”, amesema Profesa Mbarawa.  Profesa Mbarawa ameonya kampuni za simu zitakazoshindwa kupeleka mawasiliano katika maeneo waliyopangiwa kwa wakati zitapokonywa masafa katika maeneo husika ili kuzipa kampuni zilizo tayari.  Naye Mjumbe wa Bodi ya UCSAF Bw. Godfrey Simbeye, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa Bodi yake imejipanga kuhakikisha inaratibu huduma zote za Tehama zinazotolewa na taasisi mbalimbali nchini ili kuweka uwiano wa huduma hizo nchini kote.  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Eng Peter Ulanga, amesema kuwa mfuko huo umejipanga kupeleka mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara ili kutoa haki kwa wakazi wa maeneo hayo kunufaika na fursa za mawasiliano na kuchochea maendeleo.  Takribani asilimia 94 ya Wakazi wa Tanzania wanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni kufikia asilimia 100 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.


  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kumbukumbu za wateja wanaohudumiwa  na kampuni ya simu TTCL kanda ya Kaskazini eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akisisitiza jambo kwa maofisa wa kampuni ya Simu TTCL kanda ya Kaskazini alipokagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), akisalimiana na viongozi wa Idara za wizara yake hiyo jijini Mbeya baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.Wengine ni viongozi wa idara za wizara yake jijini hapo( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akizungumza na aliyewahi kuwa kiongozi katika Serikali zilizopita,Profesa David Mwakyusa (kushoto), baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisindikizwa na kiongozi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe baada ya kuwasili jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bi. Nasama Massinda akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti walipotembelea Soko la Hisa leo Jijini Dar es Salaam.
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti walipotembelea Soko hilo leo Jijini Dar es Salaam
  Meneja Miradi na Biashara wa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Patrick akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi Soko hilo linavyofanya kazi.


  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Mhakama ya mwanzo ya RUANGWA mkoani LINDI, Imewahukumu watu 21 kifungo cha kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya shilingi elfu 40 kwa kila mmoja.

  0 0

   Kamanda Muroto na wezake wakikagua bustani ya mboga.
   Kamanda Muroto akiwaangalia wanaJKT katika shamba.
   Kamanda Muroto (kushoto) na wezake wakijadiliana jambo.
   Wana JKT wakilima shamba lao.
   Bwawa la maji yanayotumika kumwagilia kwenye bustani ya mboga.


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.


  Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam DIT, imesema kuwa katika kufikia uchumi wa viwanda lazima vijana waandaliwe kwa ujuzi wa kuweza kutumika katika sekta hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa akisaini makubaliano na Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba amesema sekta ya viwanda inahitaji watu wenye ujuzi hivyo Taasisi ya DIT itakwenda na kasi ya kufua vijana wenye kwenye mafunzo mbalimbali.

  Profesa Ndomba amesema kuwa makubaliano ni kwa ajili ya kuwapa mafunzo vijana 1000 katika chuo cha DIT Mwanza katika utengenezaji wa bidhaa za ngozi kutokana na Tanzania kuwa na mifugo mingi Afrika hivyo vijana watazalishwa na kuweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta ya ngozi.

  Amesema DIT itakuwa bega kwa bega na serikali katika kuwaandaa katika sekta ya viwanda wakiwa na ujuzi ambao utawezesha viwanda hivyo viweze kukua katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

  Nae Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki amesema makubaliano hayo yatakuwa endelevu kutokana na nia ya serikali katika kufikia vijana kuwa na ujuzi ambao unaweza kutumika na taifa likapata maendeleo.

  Amesema katika utafiti uliofanywa na hiyo pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, inaonyesha kuwa watu walioko katika soko la ajira wanaujuzi mdogo.

  Msaki amesema katika uandaji huo ni pamoja na VETA kuwa na mafunzo mbalimbali ya kutambua watu wenye ujuzi na kuwapa vyeti ili waweze kutambulika katika kufanya shughuli zao.

  Aliongeza kuwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 serikali imetenga bilioni 15 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa vijana ili waweze kuwa sehemu soko la ajira.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafunzo wanayotoa katika taasisi hiyo na umuhimu wa ushiriki katika uchumi wa viwanda leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki wakisaini makubaliono ya Mafunzo kwa vijana 1000 katika Chuo cha DIT Mwanza.
  Mkuu wa Taasisi ya DIT, Profesa Preksedis Ndomba akibadilishana hati za makubaliano na Mkurugenzi wa Ajira wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Ally Msaki leo jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya waandishi habari wakiwa katika mkutano huo.

  0 0

   Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Evarist Nyawawa (kushoto) na  Dk Hussein Hassanali wakimfanyia upasuaji mmoja wa wagonjwa ambapo wengine huwapandikiza mishipa ya damu kwenye moyo juzi katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
   Madaktari mbalimbali wakiendelea na kazi katika chumba cha upasuaji moyo
   Mmiliki wa Blog hii ya Kamanda wa Matukio, Richard Mwaikenda (katikati) akiwa na wanahabari wenzie wakijiandaa kufanya coverage kwenye chumba cha upasuaji
   wakiendelea na upasuaji
   Mtaalamu wa Usingizi wa Kituo cha Moyo cha Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Edwin Lugazia akitumia kompyuta kuhakikisha hakuna hitilafu yoyote inatokea kwa mgonjwa aliyekuwa anapandikizwa mishipa ya damu kwenye moyo  katika kituo hicho kilichopo Muhimbili, Dar es Salaam.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini-TIC,Clifford Tandari akizungmza na Globu ya Jamii kuhusu Kongamano la Uwekezaji baina ya Makampuni ya Tanzania na Uturuki litakalofanyika Januari 23 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT).

  Kongamano hilo litahususha Makampuni 157 kutoka Uturuki ambayo yatakuwa katika Sekta mbalimbali kama vile Nishati, Madini, Afya, Uchukuzi, Utalii, Maliasili, Kilimo, Mifugo, Chakula na Vinywaji.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  0 0

   Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akizungumza wakati Kamati yake ilipokwenda kukagua mradi wa Ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe na Morroco Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya PIC kuhusu mradi wa ujenzi wa Nyumba katika eneo la Kawe.
   Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)  Mhe. Albert Obama (Mb) akielezea jambo wakati Kamati yake ikikagua ujenzi wa nyumba unaofaywa na NHC katika eneo la Kawe
  Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC Bw. Nehemia Mchechu akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya PIC wakati wakikagua ujenzi wa Nyumba katika eneo hilo la Kawe.
  (Picha na Ofisi ya Bunge)


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii Morogoro.

  Timu ya Simba imeshindwa kuondoka na ushindi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro  baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana na wakata miwa wa Morogoro  mtibwa Sugar mechi iliyochezwa leo.

  Baada ya matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 45 akiwa  mebel kwa alama mbili dhidi ya mahasimu wao Yanga wenye alama 43 baada ya mechi yao ya jana kushinda dhidi ya Majimaji Songea.

  Baada ya mchezo huu Simba wanakutana na Azam Januari 28 kwenye Uwanja wa Taifa.
  Henry Joseph akipambana na mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
   Kipa wa Mtibwa akiondosha mpira langoni mwake  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
  Wachezaji wakiwa wanasubiri kupigwa kwa mpira langoni mwa Simba.
   Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya akiwa amemfanyia madhambi Rashidi Mandawa  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela(kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr. William Mafwele, mwenye miwani ni mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba .

  Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela leo alitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Tagamenda linalofadhiriwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la DFID. Wakati wa ziara hiyo aliyoongazana na Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Dr William Mafwele pamoja na mhandisi wa Manispaa, Eng. Lihamba.

   Akipokea taarifa ya kazi, aliambiwa kuwa Mhandisi msimamizi wa Mradi amekuwa kikwazo cha utendaji na utekelezaji wa majikumu ikiwemo hata kunyanyasa wafanyakazi. Ndio maana mradi umekuwa unasua sua.

   Mkuu wa wilaya aliamuru Mhandisi Raymond Swai aondolewe haraka na asikanyage kabisa eneo la mradi akionekana mita 100 achukuliwe hatua. " 
  OCD mtafute haraka Raymond Swai mpe amri amri hii kama anabisha atatakiwa aondoke Iringa" Alisema Mkuu wa wilaya. Muda huo saa 5 asubuhi bado Mhandisi huyo alikuwa hajafika kazini kufanya kazi na kupelekea kazi kutoanza kwa wakati.

  Mkurugenzi wa Manispaa Dr Mafwele alionyesha wasiwasi wa mradi kumalizika kwa wakati kwani mkandarsai amekuwa anaishiwa vifaa mara kwa mara . Mkuu wa wilaya alimuagiza Mkandarasi kuleta vifaa haraka wiki ijayo atapita kukagua tena. 
  Mradi huo wenye thamani wa 5.3 bilioni unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 3 kama mkandarasi atafuata ratiba.​

  0 0

  *Awaonya viongozi wa siasa wasiwavuruge wananchi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa mpaka wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa muda mrefu.

  Mgogoro huo ambao ulianza kusuluhishwa tangu mwaka 1997, umepata suluhu kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu na kuwajumuisha Wakuu wa Mikoa hiyo miwili, Wabunge wa Kiteto na Kilindi, wenyeviti wa Halmashauri na madiwani wa kata mbili za mpakani pamoja na wananchi wa kata hizo.

  Waziri Mkuu pia amewataka wanasiasa na viongozi wengine kutowavuruga wananchi na badala yake wawaongoze vizuri na kutoa maelekezo kwa mujibu wa sheria za nchi.Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Januari 18, 2017)  wakati akizungumza na wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi katika kijiji cha Lembapili wilayani Kiteto, mkoani Manyara ambako ni kuna mpaka wa  wilaya hizo mbili alipokwenda kutatua mgogoro huo.

  Amesema viongozi wa wilaya hizo lazima wafuate sheria na wawaelekeze wananchi umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mipaka iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro.

  Akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa mpaka, Waziri Mkuu amesema nchi ilishaweka mipaka ya mikoa na wilaya zake yote tangu zamani na kumbukumbu zipo zikiwemo za mpaka wa  wilaya hizo tangu mwaka 1961 kwa  tangazo la Serikali namba 65 na hakuna mabadiliko. Hivyo, aliwasisitiza wauheshimu na kuufuata.

  Amesema Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itakwenda kuweka alama vizuri na viongozi wa wilaya hizo watashirikishwa. Alama hizo zitawekwa na kifaa maalumu, hivyo amewataka wahusika watoe ushirikiano.

  Waziri Mkuu amesema katika kipindi ambacho Serikali itakuwa ikiweka alama hizo, wananchi waendelee na shughuli zao hadi hapo zoezi litakapokamilika na wala wasibughudhiwe.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizugumza na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   (kushoto),  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera wakiwa katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka  wa wilaya ya Kiteto na Kilindi  Januari 18, 2017.  Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya  Mafisa na Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri   Mkuu, Kassim Majaliwa  akielekea kwenye moja ya  jiwe la mpaka wa  wilaya ya Kilindi na Kiteto wakati alipokwenda  kwenye kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa Kiteto na Kilindi kutatua  mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. 
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa watalaam wa upimaji ardhi kuhusu jiwe la alama ya mpaka wa wilaya ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha  mpakani cha Lembapuli  Januari 18, 2017. . Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata  maelezo kuhusu ramani inayoonyesha mpaka  wa wilaya  ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha mpakani cha Lembapuli wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wialya hizo Januari 18, 2017.  Mheshimiwa  Majaliwa apia alifuatana na Mawaziri , William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na George Simbachawene  wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Januari 18, 2018. 

  PICHA NA IKULU

  0 0


  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


  Ligi kuu ya Vodacom  imeendelea leo katika viwanja mbali mbali huku katika mchezo wa uliozikutanisha  timu ya Azam Fc na Mbeya City ukimalizika kwa suluhu ya timu hizo kushindwa kufungana.

  Katika mchezo huo ambao ulianza saa moja usiku katika uwanja wa Chamazi Complex uliopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

  Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake kwa timu zote zikishambuliana kwa vipindi na kucheza kwa kujiamini na kujituma kuhakikisha wanajaribu kupata ushindi lakini bahati aikuwa upande wowote.  Katika mchezo huo ambao mbeya City imeweza kucheza na wachezaji wawili  ambao washawahi kuchezea timu ya Azam  ambao ni Mrisho Ngassa na Zahoro Pazi  na kuonyesha kuwa mwiba kwa timu hiyo kwa kujaribu kulishambulia lango la timu yao ya zamani mara kadhaa.

  Mrisho Ngassa ambaye ameingia katika kipindi cha pili mara baada ya kutoka kwa Tito Okelo ameweza kufanya mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji kwa kuwa tishio katika lango la Azam Fc.

  Ngasa ambaye ameweza kucheza kwa kuonyesha uzoefu wa hali ya juu kwa kuweza kusaidia upande wa kati  na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki kutokana na staili yake ya mchezo .
  Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo
  Kikosi cha Azam Fc.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
  0 0


  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

  Serikali imevitaka vyombo vya habari nchini kuwa chachu ya mabadiliko katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchumi wa kati.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye katika ziara yake kwa vyombo vya habari vya Clouds, Mlimani na Azam, ziara inayolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo baina ya Serikali na vyombo vya habari nchini.

  “Serikali ya Awamu ya Tano imejikita katika ajenda mbalimbali ikiwemo kutoka katika hali ya uchumi tuliona nao sasa kuelekea uchumi wa kati hivyo vyombo vya habari vinatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha suala hili linawafikia na kuleta uelewa kwa wananchi”alisema Mhe. Nnauye.

  Waziri Nape alisisitiza kuwa, kumekuwa na mitazamo tofauti katika vichwa vya wananchi au jamii kwa ujumla kuhusu suala zima la kuelekea uchumi wa kati, hivyo ni jukumu la vyombo vya habari nchini kuweza kuwaelewesha nini maana halisi ya uchumi unaolengwa kuufikiwa.

  “tumesikia ya kwamba uchumi wa nchi umekuwa kwa asilimia saba, mwananchi wa kawaida hawezi kuwa na uelewa wa kujua ni vipi uchumi wa nchi unakuwa, hivyo vyombo vya habari vina mchngo mkubwa katika kuifanya jamii kuwa uelewa juu ya ukuaji wa uchumi” alisisitiza waziri Nape.


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media group wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Mlimani Tv na Redio iliyo chini ya Mlimani Media wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Uhuru Production inayomiliki vituo vya azam Tv na Redio wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia sehemu mbalimbali za studio za Azam Tv na Redio iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza katika Kipindi cha Alasiri Lounge kinachorushwa na Azam Tv iliyo chini ya Uhuru Production wakati alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wake na changamoto wanazozipata katika kutekeleza majukumu yao.

  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM.


  0 0

  Na Zuena Msuya, Iringa

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini, Unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Awamu ya kwanza na ya Pili ili kuona thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika mradi huo.

  Mwenyekiti wa PAC, Livingstone Lusinde alisema hayo mkoani Iringa wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA, katika vijiji na Taasisi mbalimbali zilizopitiwa na Mradi huo.

  Lusinde alifafanua kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo baada ya kuona miundombinu iliyotumika na maendeleo ya wananchi katika maeneo ambayo yamepitiwa na miradi hiyo.

  ” Tumepita katika vijiji mbalimbali hapa Iringa ambayo nimepitiwa na REA,tumeona namna ambavyo mradi huo umetekelezwa na tumeona miundombinu iliyotumika na maendeleo yake hivyo hatuna budi kusema wazi kuwa tumeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu”, Alisema Lusinde.

  Lusinde aliwasisitiza wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Umeme vijijini, kutumia miundombinu imara inayokwenda sambamba na thamani halisi ya matumizi ya fedha za Serikali katika kutekeleza wa miradi hiyo ili kutimiza malengo yaliokusudiwa na kuondoa hasara za makusudi zinazoweza kujitokeza.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Merard Kalemani,(kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Livingstone Lusinde( kulia) wasikiliza hoja za Wajumbe wa Kamati ya PAC, (hawapo pichani) kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani Iringa.
  Wajumbe wa Kamati ya PAC, wakisikiliza taarifa ya Mkoa wa Iringa, kabla ya kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa MIRADI ya Umeme vijijini mkoani Iringa.
  Wajumbe wa Kamati ya PAC,wakikagua Miradi ya Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyamahana mkoani Iringa.
  Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Livingstone Lusinde ( kushoto) akiruka pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi, wakati wa ziara ya kukagua Miradi ya Umeme Vijijini.


  0 0
 • 01/18/17--20:36: Our condolences
 • Salaam Alaikum Razabhai and family:

  We are reaching out to you at one of the most difficult times of your life.
  On behalf of ZIDO donors, ladies of the nudba group, Mumtaz Suleman, myself and our families, we wish to express our deepest condolences to you and your family on the sudden and tragic accident that claimed Brother Altaf’s life. 
  Brother Altaf’s hard and persevering work to help the severely disabled and the very sick people including the Hydrocephalus project in Tanzania will not be forgotten and may Allah (s.w.t.) reward him abundantly Ameen. 
  I remember 4 years ago, when we found 4 year little albino child Hatibu in Zanzibar, with a huge infected boil on his head. Brother Altaf took prompt action and had Hatibu admitted immediately at Muhimbili hospital where he was diagnosed with stage 4 skin cancer. Hatibu had surgery, radiation and other treatment. Today Hatibu is cured enjoying normal life because of the speed and prompt action taken by Brother Altaf.
  Brother Altaf helped to facilitate surgery when the Nudba Group requested assistance for young Jumua Mubarak, who had a condition called  Hydrocephalus and Spinal Bifida Aculta.  This one surgery opened up the doors for other children with this condition and the Nudba Group was able to sponsor close to 100 such surgeries. 
  We pray that Allah rest his soul in peace and in the vicinity of the Ahlul bayt (a.s.) and may Brother Altaf continue to receive reward for his hard work.
  We have worked with Brother Altaf and yourself for several years and we hope to continue to work with you to help the less privileged in the coming years. 
  May Allah give you the Sabr to get 
  through this very difficult time - Ameen

  With duas from
  Reyhana Merali (ZIDO)
  Mumtaz Suleman - Nudba Group

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Januari 18, 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam. Pichani, Makamu wa Rais, akipiga picha na Bw. Mshomba mara baada ya mazungumzo yao. (PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS).
  Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, (kulia), akimsikiliza Mkurugenzio Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 18, 2017.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mmkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba Januari 18, 2017.

older | 1 | .... | 1516 | 1517 | (Page 1518) | 1519 | 1520 | .... | 3285 | newer