Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KC GLOBAL LINKS LTD

$
0
0

Kutokana na matatizo yaliyokua nje ya uwezo wetu, 
lile kontena la tarehe 15/01 sasa litaondoka tarehe 20/01
Mzigo wa ndege utaondoka Jumatatu jioni
Mzigo kwa meli ni £1.75 inclusive clearance
Mzigo kwa ndege ni £3.99 inclusive clearance
Hakuna handling au admin charges.
Ukiishalipia kilo zako haulipi tena
Tupigie
+44 1375 85 85 25
+44 79 038 28 119
KC TEAM..

Ufaulu Kidato Cha Pili Waongezeka Kwa Asilimia mbili

$
0
0
Baraza la Mtihani la Taifa, (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili, ambapo wanafunzi 372,228 (kati ya 435,075) wamefaulu sawa na asilimia 91.02.Kiwango hicho cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2 ikilinganishwa na asilimia 89.12 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo mwaka jana.
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde alisema jumla ya wanafunzi 435,075 walioandikishwa kufanya mtihani huo kati yao wasichana ni 189,161 na wavulana ni 183,067. 
Dk Msonde alisema ufaulu umeongezeka mwaka huu katika masomo ya msingi na wanafunzi wamefanya vizuri zaidi kwenye somo la kiswahili.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 435,075 walioandikishwa kufanya mtihani huo kati yao wasichana ni 189,161 na wavulana ni 183,067. 
c2nj-klxaaalcvy-jpg-large
KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI BONYEZA HAPA

VILIO, SIMANZI, MAJONZI VYATAWALA VIFO VYA WATOTO WA MAOFISA WA JESHI LA MAGEREZA WALIOKOSA HEWA NDANI YA GARI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Jeneza lenye mwili wa mtoto huyo likiombewa kabla ya 
kuingizwa kanisani
Wanafunzi wenzake na mtoto huyo wakiwa katika ibada ya kumuaga mwenzao.
Padre aliyekuwa akiendesha ibada hiyo akilinyunyuzia mafuta ya baraka jeneza lenye mwili wa mtoto Maria.

Baba wa marehemu, ASP Masala (wa pili kulia aliyevaa shati la kitenge), akiwa na ndugu zake na waumini waombolezaji katika ibada ya kuuaga mwili wa mtoto wake kabla ya kuondoka kwenda nyumbani kwao mkoani Rukwa kwa mazishi.
Waombolezaji wakiwa wamejipanga foleni wakati wakienda 
kutoa heshima za mwisho. Habari kamili BOFYA HAPA

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 16, 2017

MWILI WA MAREHEMU AMINA ATHUMAN KUWASILI JIJINI DAR ASUBUHI HII NA BAADAE KUSAFIRISHWA KIJIJINI KWAO LUSHOTO KWA MAZISHI

$
0
0
  Mwili wa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa asubuhi hii na boti ya kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumanne mchana. Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi akiripoti habari za michezo kombe la Mapinduzi na kumkuta mauti hayo baada ya kujifungua mtoto wa kiume, kwa bahati mbaya mtoto akafariki baada ya kuzaliwa na yeye kupata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi. Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake-Ameen

RIADHA YAIBEBA TANZANIA NCHINI INDIA

$
0
0

• Awatimulia vumbi Wakenya, Waethiopia.
• Asema ni Ushindi wa Watanzania

Mtazania Alphonce Simbu, ameibuka mshindi wa mashindano ya Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akimtimulia vumbi Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Mtanzania huyo aliongoza huku akifuatiwa na Wakenya 7 na Waethiopia 2 katika 10 bora.

Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai Marathon yanafanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji la Mumbai nchini India na ni mbio zinazoaminika kuwa kubwa kabisa barani Asia kwa idadi ya washiriki wanaomaliza.

Simbu, ambaye anadhaminiwa na kampuni ya Multichoice Tanzania, aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa 2:09:28 muda ambao ni mzuri sana kwa mbio za aina hiyo.Akizungumzia ushindi wake, Simbu amesema kuwa anaamini ushindi huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya na kwamba udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania umemsaidia sana kwani imekuwa rahisi yeye kutumia muda mwingi zaidi kwenye mazoezi na maandalizi.

Amesema anauchukulia ushindi huo kama changamoto kwa mashindano mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesisitiza kuwa ushindi huo siyo wake peke yake au Multichoice , bali ni ushindi wa Taifa zima la Tanzania.Kwa upande wake Mkuu wa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Johnson Mshana amesema Multichoice imefurahishwa sana na matokeo hayo na kwamba wataendela kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea taifa sifa kubwa.

“Tulichukua jukumu la kumdhamini simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote. Alisema Mshana na kuongeza “dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudani”

Katika mbio hizo, waigizaji maarufu wa .Bollywood John Abraham and Neha Dhupia walikuwepo kuleta amsha amsha kwa washiriki.
Mtazania Alphonce Simbu akimalizia mbio za Mumbai Marathon baada ya kuongoza na kwashinda wapinzania wake katika mbio hizo.
Mtazania Alphonce Simbu wa pili kutoka kushoto akiwa na washindi wenzake waliomfuatia mara baada ya kumalizia mbio hizoza Mumbai Marathon akiwa mshindi wa kwanza
Mtazania Alphonce Simbu akionyesha medali yake ya dhahabu aliyojishindia katika mbio za Mumbai Marathon baada ya kuongoza na kwashinda wapinzania wake katika mbio hizo.

Mkoa wa Mbeya wafikiwa na kompyuta za Bayport

$
0
0
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta nane Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock kwa ajili ya kuzigawa kwa Halmashauri nne za Mkoa huo wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kusini wa Bayport Financial Services, Emmanuel Nzuttu. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Bayport Mbeya, Mohamed Kisoki akifuatiwa na wakala wake Kurwa Lighton. Picha na Mpiga Picha wetu Mbeya.

Na Mwandishi Wetu,Mbeya

SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya, zimewataka watumishi wa umma katika mkoa wao,hususan kupitia ofisi zitakazonufaika na msaada wa kompyuta nane kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, kuongeza ufanisi wa kazi kwa kupitia vitendea kazi hivyo vilivyotolewa.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya, Nyasenga Enock, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, kwenye makabidhiano ya kompyuta zilizotolewa na Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Tunduma, Ileje, Mbeya na Rungwe, huku kila ofisi ikipokea kompyuta mbili.
Majadiliano yakiendelea katika makabidhiano hayo ya kompyuta kutoka Bayport Financial Services mwishoni mwa wiki, mkoani Mbeya.

Akizungumzia hilo, Enock alisema kwamba haitakuwa na maana kama msaada wa kompyuta za Bayport hautaongeza ufanisi kazini na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia vyema vitendea kazi hivyo vipya vinavyoweza kuleta tija kama kila mtumishi atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuwatumikia wananchi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock akigawa kompyuta hizo kwa wahusika baada ya kukabidhiwa na Bayport Financial Services.

Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

$
0
0
Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.
Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.
MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3.
Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.
KAWAIDA: Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8 Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania. 

 Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8. MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3. Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage akagua mwenendo wa Uchaguzi Mdogo kata ya Ngh'ambi

$
0
0
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe baada ya kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akikagua daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi. Kushoto kwake aliyevaa miwani ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia nyeusi) akipokea maelezo kuhusu mabango ya Uchaguzi kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa tatu kushoto) wakati alipokuwa akikagua mabango hayo nje ya kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

DC HAI AMUACHIA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO HATMA YA WATUMISHI WABADHILIFU

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinaonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati. 
 Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho. 

Nogesha Upendo ya Vodacom yaja na Tsh Bilioni 32 za M-Pesa

$
0
0
Wakati wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.

Awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio hilo kampuni hiyo  imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, Ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja wetu.

‘Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa Zaidi la faida’ Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania.

Kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea SMS inayoonyesha kiasi chako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.

Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo Zaidi ya wateja 200 washajishinidia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.

BAADHI YA WAKAZI WA MWENGE MSHINDO WA MSHITAKI MBUNGE WAO KWA NAIBU WAZIRI DKT. ANGELLINA MABULA

$
0
0

Baadhi ya wakazi wa mwenge mshindo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamemshitaki Mbunge wao Leonidas Gama kwa Naibu Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angellina Mabula kwa kuwazulumu maeneo yao.

Article 0

Wachezaji wawasili kwenye kliniki Airtel Rising Stars

$
0
0

Wachezaji bora walioibuka kutoka katika mashindano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita wamewasili rasmi leo kambini ili kuhudhuria mafunzo ya soka yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)

Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa wiki moja yanayotegemea kuanza kesho chini ya makocha wa timu za taifa za vijana yatashirikisha wachezaji nyota 65 kutoka katika mikoa mbalimbali iliyoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars mwaka jana.

Akiongea na waandishi wa habari wakati kikosi hicho kilipowasili , Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF , Salim Madadi alisema” Tumejipanga vyema kupokea wachezaji hawa na kuwanoa ili kuendelea kutafuta vipaji kwa ajili ya timu zetu za vijana za taifa, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya ya muda mfupi yatawasaidia vijana hawa kupata mbinu za mpira lakini pia kuziwezesha timu zetu kupata wachezaji bora kwaajili ya vikosi vyao.”

Mmoja kati ya wachezaji walioingia kambini hapo Amrani Rajabu Kutoka Mogogoro Alisema” ninafurahi kuona kambi hii inafanyika kama tulivyoahidiwa na kwakweli najisikia furaha kuwa mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka jana. Nimejipanga kutumia fursa vyema kwani naamini huu ndio mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mchezaji nyota duniani. nawashukuru sana Airtel kwa kuanzia mpango huu na kutupatia nafasi ya kuonyesha vipaji vyetu.”

Wachezaji waliowasili kambini ni pamoja na Anthony Alfred (Mbeya), Amrani Rajabu (Morogoro), Yassin Ally (Temeke), Adam Almasi (Temeke), Mustafa Mhando (Kinondoni), Nickson Dimoso (Morogoro), Salum Mgonza (Kinondoni), Abdul Hassan (Morogoro), Benjamin Kawambwa (Mbeya), Yusuf Abdul (Temeke), Ibrahim Ngoitame (Morogoro), Mathias Juan (Ilala), Kambi Ramadhan (Kinondoni), Daniel Ndalo (Mwanza), Salum Yohana (Kinondoni), Esmail Kovu (Temeke), Munir Mzee (Ilala), Idrissa Omar (Ilala), Patrick Reuben (Morogoro), Ramadhan Gido (Mwanza), Said Maulid (Temeke), Ally Hamisi (Kinondoni), Nyamawi Athumani (Morogoro), Jabir Masumbuko (Morogoro), Tepsi Evance (Morogoro), Ernes Kamage (Mbeya), Gustafa Simon (Ilala), Ramadhan Chundo (Temeke), Hassan Kapera (Kinondoni), Juma Abdul (Ilala), Lameck Juma (Mbeya), Shabani Mangula (Kinondoni), Michael Joseph (Mwanza), Boniface Makala (Morogoro), Abdillah Kihulo (Temeke), Albinius Haule (Mbeya) kwa wanavulana na wasichana ni pamoja na Agatha Joel (Temeke), Fadhila Esmail (Arusha), Zubeda Mohammed (Kinondoni), Faraja Hamadi (ilala), Eva Jackson (Temeke), Violet Thadeo (Temeke), Zainabu Mrisho (Kinondoni), Fumu Mohammed (Ilala), Asphat Kasindo (Temeke), Elizabeth Julius (Temeke), Stella Wilbert (Kinondoni), Hawa Ally (Zanzibar), Christina Samuel (Temeke), Anna Anrea (Kinondoni), Grace Yusuf (Ilala), Shamimu Hamisi (Temeke), Mwantumu Ramadhani (Kinondoni), Hadlfa Mussa (Lindi), Zainabu Mrisho (Ilala), Fatuma Yusuf (Ilala), Eva Michael (Arusha), Oppa Msolidi (Temeke), Yustina Mboje (Temeke) na Zainabu Mohammed (Ilala).
wachezaji nyota wavulana wa Airtel Rising Stars wakiwa na Mkurugenzi wa ufundi wa soka la vijana TFF na kocha wa zamani wa timu ya taifa , Kim Paulsen mara baada ya kuwasilia kambini kwaajili ya mafunzo ya muda wa wiki moja .
 

JUMUIYA YA MASINGASINGA WATOA MSAADA SEKONDARI YA KIWANGWA

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete wa tatu kutoka kushoto,akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh Bwana Kugis wa pili kutoka kulia,pamoja Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo wa kwanza kushoto baada ya kupokea msaada wa madawati kutoka Jumuiya hiyo.
 Mbunge wa Jimbo la Chalinze akipanda mti kuashiria sherehe  ya miaka 350 toka kuzaliwa kwa Guru Sing Sikh.
Mh.Mbunge akipokea Madawati toka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Singh.Aliyesimama katikati ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kiwangwa Ndg. Rashid

Jumuiya ya Singh maarufu kama masingasinga hapa nchini imetoa msaada wa madawati  100 na meza 100 ,vyenye gharama ya mil. 5,kwa shule ya sekondari ya kata ya Kiwangwa,chalinze wilaya ya Bagamoyo.
Jumuiya hiyo imetoa msaada huo ,ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu.
Akiongea  kwa niaba ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,Kurgis,katibu wa Jumuiya hiyo ya Singh bw .Singh alisema ubora wa upatikanaji wa elimu katika shule unategemea mchango wa kila mdau hivyo wao wameamua kuanza na madawati .
Alisema lengo ni kuhakikisha watoto wanasoma kwenye mazingira mazuri na hatimae kutimiza ndoto zao.
,"Ndugu zangu sisi Singasinga tumeamua kuanza na madawati lengo letu ni kuona watoto wakisoma katika mazingira rafiki,hatimae waweze kufika mbali kielimu”alisema Kurgis .
Akizungumza katika hafla ya upokeaji wa madawati hayo mgeni rasmi, mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete,aliishukuru jumuiya ya Singasinga kwa msaada huo na kusema utasaidia watoto kuondokana na adha ya kukaa chini .
" Leo tunawashukuru kwa madawati lakini tatizo la maji na umbali wa wanapoenda kuchukua maji vijana wetu unasababisha pia kushuka kwa viwango vya ufaulu sio tu shuleni hapa lakini katika maeneo mengi ndani ya halmashauri yetu.alieleza Ridhiwani.
Ridhiwani aliwaomba wajaribu kusaidia changamoto hiyo kwa kuiweka kwenye mipango yao kazi ya maendeleo ya jamii.
Alifafanua endapo jumuiya hiyo itasaidia kuchimba visima italeta tija katika maeneo mengi jimboni hapo maana pia watoto wanateseka kutokana shule nyingi hazina huduma ya maji.
Ridhiwani alisema kijumla Jimbo hilo limeshakamilisha kutatua tatizo la upungufu wa madawati na wanashukuru kupata ya ziada.
Mbunge huyo alisema kwasasa nguvu zao zinaelekezwa katika ujenzi wa madarasa mashuleni na kukarabati yale chakavu hivyo aliwaomba wadau wa maendeleo wajitokeze kuunga mkono suala hilo.

TANZANIA YAZINDUA FURSA ZA WANAWAKE KUWEKEZA SEKTA YA KILIMO

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akizungumza na viongozi wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo kusini mwa jangwa la sahara, wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,akiongoza na Rais wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo kusini mwa jangwa la sahara, Margaret Chacha, wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza katika ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika fursa za uwekezaji wa viwanda iliyoandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Wasaa-Tanzania Chapter inayojishulisha na bidhaa za kilimo Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika ukumbi wa 5s uliyopo eneo la Bahari beach Ununio,Dar es Salaam jana.

WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA ATCL DAR/DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

Akizindua safari hizo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) amesema safari hizo zitawezesha wafanyabiashara na wananchi wengine kutoka Dodoma na kwenda katika maeneo mengine kwa urahisi.

Amesema kuanzishwa kwa safari hizo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais, Dkt.  John Magufuli za kufufua ATCL na kuboresha usafiri wa anga nchini.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma, wafanyabiashara na wananchi wa Dodoma kutumia ndege hizo kwa safari za kwenda katika maeneo mbalimbali kwani ni za uhakika na gharama zake ni nafuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.

“Tuna ndege nzuri. Tuzitumie kwenda katika maeneo mengine kwani gharama zake ni nafuu. Kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ni sh. 165,000, kwenda na kurudi ni  sh. 299,000,” amesema.

Amesema ndege nyingine kama hiyo inatarajia kuwasili nchini Juni mwaka huu jambo ambalo litaongeza idadi ya safari za ndege hizo nchini na maeneo mengine ya nchi jirani.

Naye Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kutumia vizuri fursa hiyo ya safari za ndege za ATCL kwa kuwa utawawezesha kusafiri kwa muda mfupi tofauti na vyombo vingine vya usafiri.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana ameshukuru kwa uanzishwaji wa safari hizo kwa kuwa zitarahisisha kutoka katika Makao Makuu ya nchi na kwenda katika mikoa mingine nchini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela ameupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa namna anavyofanya kazi. Amefurahishwa na uanzishwaji wa safari hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa ATCL. Kapten Richard Shaidi ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa ujio wa ndege hizo na kwamba hiyo ni moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ya kufufua ATCL.

“Hivi karibuni tunaanza kwenda nchi jirani. Mwakani tutapata ndege nyingine kubwa itakjayokuwa inafanya safari za masafa ya kati na ya mbali.

Naipongeza Serikali kwa kutoa ahadi na kuitekeleza kwani kutoa ahadi ni jambo rahisi ila utekelezaji wake ndiyo kazi. Lakini Serikali imeweza,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ​ baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Bw. Emmanuel Korosso amesema hivi karibuni shirika hilo linatarajia kuanza safari za kwenda katika miji ya Tabora, Songea, Mtwara, Mpanda, Mafia na Jiji la Tanga.

Akizungumzia kuhusu safari za Dodoma amesema zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku ya Ijumaa na Jumatatu. Hata hivyo wanatarajia kuongeza safari hapo baadae.

DC WA KAKONKO,KANALI NDAGARA AKUTANA NA BARAZA LA MADIWANI KUJADILI MIKAKATI MIPYA YA KUONGEZA MAPATO

$
0
0
 Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara ameliomba baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Mkurugenzi kubuni vyanzo ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa kwa ukusanyaji mapato ipasavyo.

Pia aliwaomba Madiwani wa upinzani kuacha tabia ya kupinga rasimu ya pendekezo la bajeti iliyopendekezwa ya mwaka 2017-2018 pasipokuwa na hoja ya msingi ikiwa ni pamoja na kupinga kodi ya majengo ya kila mwananchi kuchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka hali inayopelekea halmashauri hiyo kushindwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.

Rai hiyo aliitoa Jana (Leo) katika kikao cha baraza la madiwani cha kuipitia na kupitisha rasimu ya bajeti inayo pendekezwa na balaza hill ambapo Ndagara aliwaomba madiwani kuwashawishi Wananchi kuchangiq shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia Ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuchangia michango mingine iliyopendekezwa kwenye rasimu ilikufikia lengo la kukusanya mapato kwa asilimia 80%.

Aidha Ndagara aliwaomba madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ilikuepuka viporo vilivyo baki kwa bajeti ya mwaka uliopitq ambapo halmashauri hiyo ilishindwa kufikia lengo na kukusanya mapato kwa asilimia 28% kutokana na kukosekana kwa vyanzo vipya vya mapato katika Wilaya.

"Ushauri wangu katika baraza hili kwenye hii bajeti mlio ipitisha nilazima kuwa na vipaumbele ilikuepuka hivi vipolo vilivyo baki niungane na Afisa mipango, tuwqshirikishe Wananchi kwa nguvu kubwa na tuache kuitegemea serikali siku zote lazima tukusanye kodi ilikuweza kuipatia halmashauri mapato kuacha kuweka vipingamizi visivyo kuwa na msingi ", alisema Kanali Ndagara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi aliwaomba madiWani kuikataa bajeti kwa hoja ya msingi, kupinga suala la kila mwananchi kuchangia shilingi 5000 kwa mwaka ni kupinga maendeleo hakuna mwananchi anaeweza kukosa kiasi hicho cha hela kwa mwaka suala la msingi tuongeze vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.

Mwakabibi alisema Madiwani wanatakiwa kuwaelimisha Wananchi juu ya ulipaji modi na kuchangia mapato ya serikali, halmashauri ya kakonko ni halmashauri ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato nchini kutokana na vyanzo vidogo vya ukusanyaji mapato halmashauri baada ya kuliona hill imeandaa vyanzo vipya vya mapato ilikuhakikisha mapato yanaongwezeka.

Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko Juma Maganga alisema halmashauri imeandaa bajeti ya shilingi bilioni 29.7 iliyopitishwa na madiwani ya mwaka wa fedha 2017 -2018 itakayo husisha makusanyo ya mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu itakayo saidia kukamilisha shuguli za maendeleo ya halmashauri hiyo.


MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara akizungumza kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,katika suala zima la kupanga mkakati mpya wa kubuni vyanzo vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.
 Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara alipokuwa akizungumza nao mapema jana katika suala zima la mkakati mpya wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.  

Muhimbili Yatoa Msaada wa Vitanda 20

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa vitanda vitano vya kujifungulia wakina mama wajawazito kwa hospitali ya Wilaya ya Mafia ili iweze kuwasaidia katika visiwa hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Muuguzi msaidizi wa hospitali hiyo, Agnes Mtawa amesema kuwa vitanda hivyo ni sehemu ya vitanda 20 vitakavyotolewana na hospitali hiyo kwa hospitali mbalimbali.

“vitanda hivi ni vile ambavyo vimekarabatiwa hapa hapa hospitali ambavyo vilikuwa vimeharibika na kwa bahati nzuri tukapata fursa ya kupewa vitanda na wahisani hivyo hivi ambavyo vilikuwa vimeharibika tunavitengeneza na kuvigawa katika hospitali zilizoomba”amesema Mtawa.

Ameongeza kuwa gharama ya kitanda kipya cha kujifungulia kinaanzia shilingi milioni moja na laki tano mpaka milioni moja na laki mbili hivyo ukarabati wa vyombo hivi unasaidia gharama za ununuzi wa vitu vipya.

Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali ambao wana uwezo kuanza kusaidia hsopitali zetukatika upande wa vifaa tiba.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akikabidhi vitanda vitano kwa Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai. Vitanda hivyo vimetatumika kwa kina mama wakati wa kujifungua.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Bi. Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vitanda hivyo.
Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

ZANZIBAR INAZIDI KUKUA KWA KASI YA KIMAENDELEO-BALOZI WA KOREA KUSINI NCHINI

$
0
0
Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong amesema Zanzibar inazidi kubadilika Kimaendeleo kutokana na kasi kubwa ya miundombinu inayoendelea kuwekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiungwa mkono na Mataifa na Taasisi washirika wa Maendeleo.

Amesema Taasisi na Makampuni ya Korea yanafurahia mabadiliko hayo na kuamua kusaidia ujenzi wa Miradi ya Kielimu akiutolea mfano ule wa Skuli ya Sekondari ya Kwarara uliomalizika hivi karibuni ili kuipa nguvu zaidi Sekta ya Elimu Zanzibar ambayo ndio kichwa cha maendeleo hayo.

Balozi Song Geum Yong alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar aliyekuwepo Visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Skuli hiyo pamoja na kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema anapata faraja kuona kuwa ujenzi wa Skuli hiyo uliopata msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Korea { KOICA }, Good Neighbors, Shirika la Utangazaji la Korea { SBS } na Taasisi ya Wasanifu Majengo ya Korea umekwenda sambamba na ujenzi wa Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Tumaini.

Balozi Song alieleza kwamba Kituo hicho cha kurekodia Matangazo ya Redio na Televisheni cha Tumaini kilichoanzishwa kwenye Skuli hiyo ya Sekondari Kwarara kwa kiasi kikubwa kitasaidia kutoa Taaluma kwa Wanafunzi pamoja na Wananchi wa sehemu mbali mbali hapa Zanzibar.

Akitoa shukrani zake kwa misaada mbali mbali inayotolewa na Korea kwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali inakusudia kujenga Bara bara ya lami inayoingia kutoka bara bara Kuu hadi kwenye Skuli hiyo ili kuwaondoshea usumbufu wa Mawasiliano Wananchi na Wanafunzi wa eneo hilo.

Balozi Seif alisema Korea ya Kusini inastahiki kupongezwa kwa jitihada zake za kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar, lakini hata hivyo alimshauri Balozi Song kutumia maarifa yake katika kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya nchi yake kuendelea kuelekeza nguvu zao katika uwekezaji wa sekta tofauti ikiwemo ile ya usafiri wa Baharini.

Alisema sekta ya Kilimo Zanzibar hasa katika upande wa umwagiliaji pia inastahiki kuungwa mkono zaidi ili kuwaongezea nguvu za uzalishaji Wakulima kwa vile zaidi ya asilima 80 ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wanaendesha maisha yao kwa kutegemea sekta hiyo.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Balozi Song Kati kati akielezea faraja yake kwa Balozi Seif kutokana na Makampuni na Taasisi za nchi yake kuonyesha azma ya kutaka kusadia maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Balozi Seif Kushoto akisisitiza malengo ya SMZ katika kuimarisha miundombinu ya sekta mbali mbali nchini ili kuwajengea maisha bora wananchi wake.
Balozi Seif Kushoto akimpatia zawadi ya vyakula vya viungo Balozi wa Korea Kusini Bwana Song mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Oisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Picha na – OPMR – ZNZ.
Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar walipokutana kwa kubadilishana mawazo.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images