Taharuki imetamalaki jijini Seattle, Marekani, kufuatia kuchomwa moto kwa msikiti wa Bellevue, WA, (angalia picha) ambao huwa unatumiwa na jumuiya ya Waislamu jijini humo, wengi wao wakiwa Watanzania.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, moto huo ulizuka alfajiri ya Jumamosi na mtu mmoja mwanaume mwenye umri wa miaka 37 ametiwa mbaroni kwa kutuhumiwa kuhusika na hujuma hiyo baada ya kukutwa eneo la tukio.
Kikosi cha zimamoto cha Bellevue kinasema kilifika msikitini hapo alfajiri hiyo na kukuta miali ya moto ya futi 40 ikiunguza sehemu za nyuma za msikiti huo, ambapo vikosi 13 vilivyofika vilifanikiwa kuuzia, Hakukuwa na majeruhi walioripotiwa.
Bellevue ni mji ulio upande wa Mashariki (Eastside) wa King County, Washington, Marekani, ukiwa upande wa pili wa Ziwa Washington kutoka Seattle. Ukiwa ni mji wa tatu kwa ukubwa katika eneo la jiji la Seattle metropolitan, Bellevue ambao unajulikana kama mji unaokua pembezoni (satellite city), ulikuwa na wakaazi wapatao 122, 363 katika sensa ya mwaka 2010. Watanzania wengi wanaishi hapo.
Uongozi wa msikiti huo umetoa taarifa katika tovuti yake mapema leo Jumamosi kuhusu moto huo, na kueleza kwamba nyumba hiyo ya ibada imefungwa. "As Salaaam Aleikum. Kulikuwa na mototo sehemu ya nyuma ya msikiti wa Bellevue (Kituo cha Kiislamu cha). Moto ulianza mnamo saa tisa alfajiri Jumamosi (14/1/2017 ) na msikiti huo hauwezimkutumika mpaka itapotangazwa”, ilisema taarifa hiyo.
“NDUGU WANA WATANZANIA KWA UJUMLA NAOMBA TUUNGANE PAMOJA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU TENA AMBACHO JAMII YETU YA KIISLAM INAPITIA KWA KULAANI KWA PAMOJA KITENDO CHA WATU KUINGIA MSIKITINI NA KUUCHOMA MOTO.
" TUWATAKE POLISI, FBI NA VYOMBO VYOTE VYA ULINZI NA USALAMA MAJIBU YA KWANINI MSIKITINI UCHOMWE MOTO? TUWATAKE ULINZI WA KUTOSHA KWA FAMILIA ZETU.
"TUUNGANE PAMOJA KWA SALA NA DUA KUOMBA MWENYEZI MUNGU MOYO WA SUBRA NA KUSAMEHE”, AMSEMA MMOJA WA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA WA SEATTLE BW. DOLA KWENYE UJUMBE WAKE ULIOSAMBAZWA MTANDAONI.