Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

ZOEZI LA KUHAKIKI WATUMISHI WASTAAFU LAANZA MKONI KIGOMA.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha na mipango wameitaka serikali kurekebisha viwango vya malipo ya pensheni wanayolipwa sasa kufuatia kupanda kwa gharama za maisha ambako hakuendani na hali halisi ya malipo wanayolipwa.

Wakizungumza katika zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na wizara ya fedha na Mipango linaloendelea mkoani Kigoma, Wastaafu hao wamesema kuwa kwa sasa kiwango wanacholipwa wastaafu waliostaafu utumishi wao muda mrefu hakiendani na malipo yanayotolewa kwa wastaafu waliostaafu hivi karibuni.

Shaban Funenge mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania alisema kuwa wastaafu wengi ambao wamestaafu kwa zaidi ya miaka 10 wamekuwa na manung’uniko sana na kwamba serikali haina budi kufanya maboresho kwa wastaafu hao na kuondoa tofauti zao.Akizungumzia zoezi la Uhakiki linaloendelea Patrick Maganga alisema kuwa zoezi limekuja wakati muafaka ambao malalamiko ya wastaafu yamekuwa mengi na kwamba ametaka zoezi hilo liende sambamba na maboresho ya malipo kwa wastaafu hao.

Kwa Upande wake Emilia Maibori ambaye ni Mwalimu Mstaafu alisema kuwa mafao ya wastaafu yanapaswa kutolewa kwa wakati muafaka badala ya wastaafu kulalamika kufuatia kucheleweshwa kwa malipo hayo akieleza kuanza kupata malipo hayo mwaka 2015 kuafuatia kushindwa kupata malipo hayo tangu mwaka 2005 alipostaafu ambapo ameeleza kuridhishwa na zoezi la uhakiki linaloendelea.

Akieleza kufanyika kwa uhakiki huo Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa ndani wa serikali,Stanslaus Mpembe alisema kuwa kwa zaidi ya mikoa 21 ambayo uhakiki huo umefanyika mafanikio yamekuwa makubwa na idadi kubwa ya wstaafu wamekuwa wakijitokeza.Mpembe alisema kuwa licha ya wastaafu wanaojitokeza pia serikali imetoa fursa kwa wastaafu ambao wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali kufikiwa na watumishi wanaoendesha zoezi hilo na kwamba ndugu wa wastaafu hao wametakiwa kujitokeza kutoa taarifa za wastaafu hao ili waweze kufuatwa maeneo walikolazwa.

Wakati zoezi likiendelea mikoa mbalimbali nchini Mkaguzi huyo alisema kuwa baada ya zoezi kupita kwenye mkoa husika wastaafu ambao hawajahakikiwa wanatakiwa kujiorodhesha kwenye ofisi za hazina ndogo za mikoa waliyopo kabla ya muda wa zoezi hilo haujamalizika.

Naye ofisa habari wa Wizara ya Fedha na Mipango Ben Mwaipaja amewataka watumishi waastafu kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la uhakiki kwenye mikoa yote watakayo pita.

"Mpaka sasa tumeshapita jumla ya Mikoa 21 bado mikoa ya lindi,Mtwara na Zanzibar ambapo napo zoezi litaendelea ninawaomba wastaafu wajitokeze ili wasije poteza haki zao"alisema Mwaipaja.

WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha wakifanyiwa uhakiki mkoani Kigoma. WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha wakifanyiwa uhakiki mkoani Kigoma

NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la  kupandisha bei za vyakula.

Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.

“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.

Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.

Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.


 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.     
JUMATATU, JANUARI 16, 2017.


NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WABUNGE WAWILI NA BALOZI MMOJA.

NAIBU ANASTAZIA WAMBURA APOKEA BENDERA YA TAIFA TOKA KWA MISS TEEN HERITAGE 2016 NA KUZINDUA KITABU CHA "UTAMU WA CHUNGWA SI RANGIYE"

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (katikati) akiongea na Waandishi wa habari huku akiwasisitiza Vijana kuiga mfano bora aliofanya Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya changamoto alizopitia wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya zawadi mbalimbali alizopata wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akipokea Bendera ya Taifa toka kwa Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.

WAFAMASIA WAASWA KUFANYA KAZI KWA MAADILI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema maduka yote ya famasi yanatakiwa kuwa na mtaalam wa famasia.

Akizungumza katika semina ya utoaji leseni kwa wafamasia pamoja na miongozo, amesema wafamasia wanafanya kazi za maisha ya binadamu hivyo kuwa na duka la famasi bila kuwa fani ya famasia ni kosa kisheria.

Elizabeth amesema wafamasia lazima wafanye kazi kwa maadili yaliyowekwa na watakaokwenda kinyume baraza hilo litachukua hatua.

Elizabeth amesema kwa sasa nchi hii inapoelekea kwenye sera ya  Viwanda ni fursa kwa wafamasia kuungana kwa kuwa kiwanda cha kuzalisha dawa.

Aidha amesema sheria inataka kila duka la famasi kuwa na mfamasia mmoja. Amesema soko la wafamasia ni kubwa hivyo wanahumuimu sana serikalini pamoja sekta binafsi. Elizabeth amesema mwaka 2013 walikuwa na wafamasia 350 na kufikia mwaka jana wamefikia wafamasia 1400.
Msajili wa baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafamsia iliyofanyika ukumbi wa. TFDA ,jijini Dar es Salaam.
Wafamasia wakila kiapo 
Sehemu ya wafamasia wakiwa katika semina.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii .

WAZIRI NAPE AFANYA ZIARA TBC

$
0
0

Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.

Waziri Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.

“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.

Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.

“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.

Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.
 Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe Akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipofanya ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati alipokutana na uongozi wa Shirika hilo wakati wa ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na uongozi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara ya  kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

SERIKALI YAWAONDOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA NCHINI.

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
SERIKALI imesema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazodai kuwa hali ya chakula ni mbaya.



Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji na chakula nchini.



“Ndugu waandishi ukweli ni kwamba hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha sana katika maeneo mengi, hivyo siyo kweli kwamba kuna tatizo la njaa kama baadhi ya watu wanavyojaribu kupotosha,” alisisitiza Dkt. Tizeba.



Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa hali nzuri ya chakula, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kuweka akiba ya chakula kwa kununua jumla ya tani 62,087.997za mahindi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na chakula cha kutosha,

Dkt. Tizeba amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali  imejipanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula ambapo hadi  kufikia Januari 8 mwaka 2017 imenunua jumla ya tani 62,087.997za mahindi sawa na asilimia 62 ya lengo ililojiwekea.



“Kati ya kiasi kilichonunuliwa, tani 38,162.280 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,925.717 kupitia vikundi vya wakulima hivyo hadi kufikia tarehe 12 Januari, 2017 Wakala wana akiba ya tani 88,152.443 za mahindi,” alisema Dkt. Tizeba.



Waziri Tizeba ameongeza kuwa hadi kufikia katikati ya mwezi Januari, 2017 hali ya chakula na upatikanaji wake hapa nchini bado ni ya kuridhisha na hasa upatikanaji wa vyakula kama mchele na maharage ikilinganishwa na zao la mahindi.



Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, FAO, TFNC pamoja na wadau wengine wanaendelea kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe nchini ambayo inatarajiwa kukamilika Januari 28 mwaka 2017 na itazihusisha Halmashauri 55, tathmini hiyo itaiwezesha Serikali kupata taarifa za uhakika zaidi kuhusu hali ya chakula na lishe nchini.



Amefafanua kuwa kutokana na hali ya mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli na msimu kutokuridhisha katika maeneo mengi ya nchi, Serikali imewashauri wakulima kutumia mbegu zitakazokomaa mapema na kupanda mazao yanayostahimili ukame pamoja na kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya.

Aidha, Sekta binafsi zimehamasishwa kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba.

Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshwaji juu ya hali ya upatikanaji wa chakula hapa nchini ambapo Dkt. Tizeba amesema huo ni upotoshaji wenye lengo la kuwatia hofu wananchi.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Charles Tizeba9hayupo pichani) na waandishi hao kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (hayupo pichani) kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini, mkutano umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

MBUNGE WA TANGA AWAOKOA ASKARI WA JIJI LA TANGA NA KIPIGO KUTOKA KWA WASAFIRISHAJI

$
0
0


MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimikakuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwana wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madaiya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.

Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimuMbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasina Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiasharahao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.

Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu naAssad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasanchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya garilinaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.

Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupomkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoaniDodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio nakuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisizao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.

Akizungumza  na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwawatulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzikutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketihivi karibuni mjini hapa.

  Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukuaushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyumena utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambayealisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo nawanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zoteambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.

Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo naatakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambolililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine zakielektroniki.

Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za TangaMombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi nikutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jamboambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj MustaphaSelebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs nahawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashinehizo.

Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari nakulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu zakutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.


 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani (Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza shughuli zake hii leo ambapo katika wiki hii takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kabla ya kurejea Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo.

(Picha na Ofisi ya Bunge) 

MAAFISA TEHAMA WA MAHAKAMA YA TANZANIA WAPEWA DARASA

$
0
0
NA MAGRETH KINABO – MAHAKAMA

Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga amewataka Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wa Mahakama ya Tanzania kutumia elimu na ujuzi ili kuweza kutatua changamoto zilizopo kwenye masuala ya TEHAMA.

Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji huyo wakati akifungua mafunzo hayo ya muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, ambayo yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).

“Mnatakiwa kutumia elimu mliyonayo , ujuzi mtakaoupata ikiwemo kuwa wabunifu katika vitu vipya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifumo ya TEHAMA, alisema Mtendaji Mkuu, Bw. Kattanga.

Aliongeza kuwa maafisa hao wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa pamoja kwenye shughuli za mifumo ya TEHAMA. Pia aliwataka kutumia ujuzi watakaoupata kuwafundisha wengine.

Bw. Kattanga aliwataka maafisa hao kuwa na uweledi katika ya masuala ya Serikali Mtandao, kujituma kufanya kazi na kuacha tabia ya kulalamika ,ikiwemo kuwa na mtandao wa kubadilishana mawazo katika masuala ya kitaaluma.

Akitoa mada kuhusu Shughuli za Wakala ya Serikali Mtandao, Bw. Bakari alisema dhima yake ni kusogeza huduma za Serikali kwa wananchi kupitia dirisha moja, ili kuwezesha utendaji wa shughuli hizo kwa gharama nafuu , ubora , wakati na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Alisema mfumo huo pia unasaidia kuboresha huduma za Serikali katika jamii.Mafunzo hayo yamehusisha maafisa TEHAMA 25 kutoka katika kanda zote za Mahakama ya Tanzania.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwa Maafisa TEHAMA kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania . Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yenye lengo la kuongeza ujuzi yameanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa na Mahakama ya Tanzania kwa ushirikiano wa Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga akifundisha wakati akifungua mafunzo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) ya muda wa wiki moja yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yenye lengo la kuongeza ujuzi yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Baadhi ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) wakiwa katika mafunzo ya muda wa wiki moja kuhusu kuwajengea uwezo na ujuzi kwenye masuala ya TEHAMA yaliyoanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam. Mafunzo hayo yanafanywa kwa ushirikiano wa wa Mahakama ya Tanzania na Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).
Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Wakala wa Serikali Mtandao, Dkt. Jabir Bakari akitoa mada juu ya Serikali Mtandao wakati wa mafunzo ya Maafisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania.Mafunzo hayo ni ya muda wa wiki moja yameanza leo katika jengo la Shule ya Sheria lililopo Sinza, Kijitonyama jijini Dares Salaam na yanafanywa kwa ushirikiano wa Mahakama na Tanzania Wakala ya Serikali Mtandao(EgA).(PICHA NA MARY GWERA).

HOSPITALI YA MAFYA YAFAIDIKA NA VITANDA KUTOKA MOI

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA APOLO, BANGALOLE YA NCHINI INDIA WAWAFANYIA WAGONJWA UPASUAJI WA MOYO

$
0
0
 Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari  wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kumuwekea  milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Valuves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Kutoka kulia ni Dkt. Sathyaki Nambala, akifuatiwa na Dkt. Bashir Nyangasa  na kushoto ni Dkt. Lebighe Khan.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari  wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakiendelea na kazi ya kumfanyia  mgonjwa upasuaji wa kumuwekea  milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Val uves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Mgonjwa huyo milango yake miwili ya moyo haikuwa inafanya   kazi vizuri ya kupitisha damu.

Picha na Anna Nkinda - JKCI

MAC AUTO ACCESSORIES YAJA NA KIFAA KIPYA CHA ULINZI WA MAGARI

WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAHAKIKIWA KIGOMA

$
0
0
 Mkaguzi Mkuu wa Ndani Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe akimhudumia mstaafu wakati wa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango, linalofanyika katika Halmashauri ya Mji wa Kigoma, Mkoani Kigoma.
 Baadhi ya Wastaafu Mkoani kigoma wakisubiri kuhakiki taarifa zao katika zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
 Bibi Lucy Suzereje aliyekuwa mtumishi wa chuo cha maendeleo – Kihinga Mkoani Kigoma, akiwa ameshika kitambulisho chake cha kustaafu akisubiri kuhakiki taarifa zake za kustaafu kwenye ukumbi wa Halmashauri ya  Manispaa ya Kigoma.
 Bw. Jumanne Mtumwa Kiragu (aliyevaa kofia) ambaye alikuwa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Idara ya Magereza akitoa taarifa zake za kusataafu kwa Mkaguzi wa ndani wakati wa zoezi la kuhakiki taarifa za wastaafu Mkoani Kigoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Taasisi za umma marufuku kujenga vituo binafsi vya kuhifadhi Data

$
0
0
 SERIKALI imezitaka taasisi zake kote kuachana na mpango wa kujenga Vituo binafsi vya vya kuhifadhia kumbukumbu (Data Center) na badala yake kutumia Kituo cha Serikali cha kuhifadhia Data na kumbukumbu (NIDC) chenye uwezo na hadhi ya Kimataifa. Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao na Makao Makuu ya Kampuni ya Simu Tanzania TTCL. 

Mheshimwa Mbarawa amesema, Serikali imetumia fedha nyingi sana kujenga miundo mbinu ya kituo hicho mahiri katika eneo lote la Afika Mashariki na kusisitiza kuwa, Taasisi za Serikali ni lazima zitumie kituo hicho na kwa zile zenye mpango wa kujenga vituo binagsi, ziachane na mpango huo ambao ni matumizi mabaya ya fedha za Umma.

 'Natoa agizo kwa taasisi zote za Umma, ziachane kabisa na mpango wa kujenga Data Centres. Serikali imebeba jukumu hilo, imejenga kituo cha hadhi ya juu kabisa, sote tukitumie kituo hiki. Kila taasisi zijikite katika majukumu yao ya msingi, hili la Data Centre watuachie Serikali kwa kuwa tumeshalitekeleza, hatuwezi kuendelea kutumia fedha nyingine kwa eneo hili, tuelekeze fedha hizo katika maeneo mengine muhimu.' 

Akiwa katika Makao Makuu ya Kampuni ya Simu nchini TTCL, Mhe Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Kampuni hiyo kuongeza kasi ya utendaji kazi na ubunifu ili kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta hiyo sambamba na kukidhi kiu ya Wananchi ya kupata huduma Shirika lao.
Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Afisa Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw Senzige Kisenge (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya Utendaji wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Katikati) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (Wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL waliotembelea Kituo cha Huduma kwa Wateja kilichopo Makapo Makuu ya Kampuni hiyo mara baada ya kukitembelea Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kilichopo kijitonyama Jijini Dar es Salaam leo.Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi. Pichani ni Muonekano wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unavyofanya kazi.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mbarawa akizungumza na menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) leo alipotembelea Makao Makuu ya TTCL na Kituo cha Serikali cha Kuhifadhia Data na Kumbukumbu (NIDC) kinachoendeshwa na kampuni ya TTCL.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa TTCL, Prygod Kimweri.Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri. Baadhi ya maofisa waandamizi wa TTCL wakiwa katika mkutano huo na waziri.


Waziri Makamba atoa maelekezo katika kikao kazi

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba akiwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.  Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava mara baada ya kuwasili katika Chuo Kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya Kikao kazi cha Menejimenti ya Ofisi yake.
 Sehemu ya Menejimenti timu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe  January Makamba kabla ya kuanza kikao kazi katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) na Eng. Bonaventure Baya Mkurugenzi Mkuu (NEMC) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bw. Ntime Mwalyambi akiwasilisha mada katika kikao kazi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Mzumbe.

HOSPITALI YA MAFIA YAPATA VITANDA KUTOKA MOI

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

$
0
0

Simu.tv: Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba amesema Tanzania haina shida ya chakula wala njaa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu; https://youtu.be/GJ5cbTSEBu4

Simu.tv: Baada ya kuenea kwa taarifa za kuibuka kwa baa la njaa nchini, hii hapa ndio hali ya upatikanaji wa chakula mkoani Mbeya; https://youtu.be/ldf32b3YIxo

Simu.tv: Mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi amesema mkoa huo hauna tatizo la chakula na kuwataka wananchi kutunza chakula kilichopo; https://youtu.be/c4aGbU82Ghw

Simu.tv: Rais Dkt John Magufuli amefanya uteuzi wa wabunge wawili wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na balozi mmoja; https://youtu.be/dM8ynF2ixpc

Simu.tv: Waziri wa habari Nape Nnauye ametembelea shirika la utangazaji TBC na kuwataka watangazaji kulitumikia taifa kwa uzalendo; https://youtu.be/74B-bJ2ebxE

Simu.tv: Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa amezuiliwa na jeshi la polisi mkoani Geita kutokana na sababu za kiusalama; https://youtu.be/bAX7U5NAG1w

Simu.tv: Mpango wa kuendeleza kilimo kwa ukanda wa kusini umewawezesha wakulima wa viazi mkoani Njombe baada ya kupatiwa mbegu bora; https://youtu.be/Gq87HzGIF3g

Simu.tv: Wafanyabiashara nchini wameliomba shirika la viwango TBS kuongeza kasi ya ukaguzi bidhaa ili kuendana na kasi ya kibiashara na ushindani; https://youtu.be/VXk8CqqiuZM

Simu.tv: Fahamu maendeleo na tathimini ya ukuaji wa soko la hisa jijini Dar Es salaam DSE kwa wiki iliyopita; https://youtu.be/96hzPscpYlk  

Simu.tv: Shirikisho la soka nchini TFF limesema linaziangalia kwa umakini mkubwa mechi za timu kubwa ili kuhakikisha kila timu inapata matokeo halali; https://youtu.be/Ec_-VPRM1n4

Simu.tv: Kunako michuano ya soka barani Afrika AFCON tumekukusanyia hapa matokeo ya michezo iliyopigwa hapo jana na siku ya leo; https://youtu.be/Z8uQNei_-9U

Simu.tv: Fani ya urembo na mapambo imetajwa kuwa ni fani mojawapo inayoweza kuwapatia ajira vijana wengi nchini Tanzania; https://youtu.be/pMd-5IUo4ns

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MAREHEMU AMINA ATHUMAN JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman  walipokuwa wakioutoa nyumbani kwake Banana, Dar es Salaam leo, kuliingiza kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Lushoto kwa mazishi. 
 Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, marehemu  Amina Athumani ukiombewa dua nyumbani kwake, Banana, Ukonga.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto (kushoto) akimzungumzia marehemu Amina kuhusu uchapakazi wake enzi za uhai wake.
 Sehemu ya waombolezaji
 Mgane wa marehemu Amina, Towfiq Majaliwa akifarijiwa na Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru Ndg. Ramadhani Mkomwa.


Introducing K Star Ft Dayna Nyange - "Nitulize"

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images