Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 149 | 150 | (Page 151) | 152 | 153 | .... | 3270 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA UJENZI        
    
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  30/05/2013

  Baadhi ya vyombo vya Habari vimekuwa vikitoa taarifa potofu kwamba kumekuwepo na upotevu wa shilingi 252,975,000,000.00 ambazo zimelipwa kwa miradi hewa.  Wizara inapenda kutoa taarifa rasmi kwamba taarifa za vyombo hivyo vya habari si za kweli na zinalenga kupotosha umma. 
  Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) inatekeleza miradi mingi ya barabara nchini.  Hivi sasa miradi ya barabara yenye urefu wa Km. 11,154 ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji kote nchini. 
  Ujenzi wa Barabara hizi hutumia fedha nyingi na Serikali inalipia kazi hizo za ujenzi kulingana na hati za madai (Interim Payment Certificates – IPCs) zinazotoka kwa Wakandarasi na Wahandisi Washauri wanaojenga na kusimamia miradi hii.  Aidha, malipo hufanyika baada ya IPCs kuhakikiwa na Wahandisi Washauri, TANROADS na Wizara yenyewe. 
  Ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuimarisha mtandao wa barabara nchini, katika mwaka wa fedha 2011/12 Serikali iliweka Kasma maalum ya ujenzi wa miradi ya barabara na kuitengea jumla ya shilingi 252,975,000,000.00 katika bajeti kwa ajili ya kulipia kazi za barabara zinazoendelea. 
  Fedha zote zilitolewa na HAZINA kwa madhumuni hayo na kwa kufuata taratibu za Serikali.  Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS ililipia kazi za barabara kwa maana ya madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri wa miradi mbalimbali inayoendelea.  Aidha, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alipatiwa na anayo taarifa ya jinsi fedha hizo zilivyotumika. 
  Fedha hizi zilitumika vizuri na zimesaidia kufanikisha utekelezaji wa programmu ya barabara nchini kwa kulipia madai ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri kwa wakati.  Aidha, katika Mwaka 2011/12, Wizara ilitumia zaidi ya shilingi 252,975,000,000.00 zilizotengwa kupitia mradi maalum.  Kazi za barabara kwa jumla zilitumia  shilingi 662,308,000,000.00 fedha za ndani. 
  Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia umma kuwa hakuna upotevu wowote wa fedha. Taarifa zinazotolewa katika  baadhi ya vyombo vya habari kuwa kuna upotevu wa fedha ni za upotoshaji.

  Balozi Herbert E. Mrango
  KATIBU MKUU

  0 0

  ONYESHO kubwa ambalo ni uzinduzi wa Shindano la QS Queens 'Utamu Extra' linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya kesho ya Juni Mosi katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala, pia limepangwa kuwa sehemu maalum ya kuenzi mchango wa msanii Albert Mangwea, aliyefariki nchini Afrika Kusini.

  Ngwea amepangwa kuletwa kesho Jumamosi kwa ajili ya maziko yake yaliyopangwa kufanyika mkoani Morogoro, huku onyesho hilo la maombolezo likihudhuliwa na wakali kibao wa muziki hapa nchini lilioandaliwa kwa muda mrefu na kilele chake kuwa Jumamosi hii.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, leo mchana, Meneja Masoko wa Kampuni ya QS Mhonda J Entertainment, Freddy Felix, alisema kuwa shindano hilo litafanyika pia katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kupata warembo 20 watakaoishi katika Jumba moja kwa ajili ya kupata kimwana huyo wa QS Queens.

  Alisema kuwa wasanii wengi wamepangwa kupanda jukwaani kwa ajili ya kuomboleza msiba huo, akiwamo Ney wa Mitego, Wanaume Halisi, ikiongozwa na Juma Nature, MB Dog, Diamond, Inspector Haroun, Madee, H-Baba, Snura, Khadija Kopa, Solid Ground Family na wengineo, wakiwamo wasanii chipukizi, Amor na Shalviny.

  “Wasichana wote wanaotaka kushiriki shindano hili ambao ni kama uzinduzi wake, watajiandikisha katika fomu maalum ukumbini hapo, ambapo baadaye watatafutwa wengine ambao wote wataishi kwa miezi miwili katika nyumba moja itakayotembelewa na watu mbalimbali.


  “Huku mshindi akijishindia gari la kifahari, pia wanapokuwa katika jumba hilo kila siku mtu atalipwa kadri tutakavyokubaliana, huku tukiamini kuwa huu utakuwa ni mwanzo mzuri katika shindano hili,” alisema Felix.


  Kwa mujibu wa Felix, shindano hili kabla ya kupatikana warembo hao litatembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara, kama vile Mwanza, Tanga, Morogoro, Mbeya, Iringa na kwingineko kwa ajili ya kutafuta msichana mmoja wa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

  Aidha QS ilitangaza kuwa mabinti wanaotakiwa kushiriki katika shindano hilo ni wale wenye vipaji maalum na uwezo wowote wa kupambanua mambo, huku kigezo cha elimu kikiwekwa pembeni.

  Shindano hilo pia litaonyeshwa katika vituo vya Channel Ten, DTV, Clouds, ambapo huko kote wadau na wapenzi wa mambo ya urembo na burudani watapata fursa ya kuwapigia kura washiriki kabla ya siku ya kilele chake kitakachofanyika baadaye mwaka huu.

  0 0


  0 0

   Rai hiyo imetolewa na Mzazi wa kijana aliyeshinda shilingi milioni 100, katika Promosheni ya “VODACOM MAHELA” Bw. Nicodemus Nalisis ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Kigoma kujenga tabia ya kushiriki mashindano mbalimbali yanayotolewa na kampuni za simu za mkononi hapa nchini Mzee Nicodemus alisema hayo leo katika uwanja wa ndege mkoani Kigoma wakati alipowasili kumpokea kijana wake Valerian Nicodemus Kamugisha aliyewasili mkoani hapa mara baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi milioni 100 Jumatatu ya wiki hii baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo. 
   Alisema kuwa hatua ya kushiriki mashindano hayo yatatoa fursa ya ushindi kwa wananchi wengi mkoani Kigoma hivyo kuongeza uwezekano wa mkoa wa Kigoma kutoa washindi wengi katika mashindano yanayoendeshwa na Vodacom na kupadilisha maisha yao ya kiuchumi na kimaendeleo kiujumla. 
  Bw Nicodemasi alieleza kufurahishwa na hatua ya mwanae kushinda katika shindano hilo nakwamba mbali na hiyo kuwa fedha hizo ni msingi mzuri wa maisha ya kijana huyo lakini pia ushindi huo ni fahari kwa wananchi wa Kigoma na historia kubwa ya kijana huyo na familia,
  Alisema ingawaje yeye alishiriki katika promosheni hiyo bila mafanyikio na mwanae kushinda basi anampongeza kwani sawa sawa kama yeye kashinda tu.Alisema.
   Licha ya kuipongeza Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa mashindano mbalimbali likiwemo la VODACOM MAHELA na kwamba hatua hiyo inachangia katika kukuza na kupanda uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja na familia kwa ujumla. 
   Aidha mmoja wa majirani wa familia ya mshindi huyo Bw Jackson Kakwaya mfanyabiashara wa bidhaa madukani alisema hatua ya ushindi wa kijana huyo inapaswa kuwa hamasa tosha kwa watu wengi wa mkoa huu kushiriki katika shindano hilo kikamilifu. Alisema ushindi huo umemfanya aamini kuwa hakuna upendeleo katika shindano hilo na hakutarajia kama ingewezakana mkazi wa kigoma kushinda shindano tena la fedha nyingi kiasi hicho. 
   Alisisitiza Vodacom kuendeleza program kama hizo hatua ambayo alisema inawapa fursa washindi kuboresha maisha yao ghafla kutoka katika hali ya chini au ya kawaida nakuwa tajiri kwa muda mfupi. 
   Hata hivyo Bw Kakwaya alisisitiza umuhimu wa kijana aliyeshinda shindano hilo na kunyakua milioni 100, kukaa chini na kupanga mikakati madhubuti itakayo boresha maisha yake na familia badala ya kuzitumia katika anasa. 
   Kwa upande wake mshindi wa Vodacom Mahela Bw Valerian Kamugisha mbali na kupongeza Vodacom kwa kumkabidhi zawadi hiyo alikiri shindano hilo kutokauwa na mianya yoyote ya rushwa nakusema kuwa hana ndugu katika kampuni hiyo lakini ameshinda. 
  Aliwataka wananchi kuamini mashindano yanayoendeshwa na Vodacom nakushiriki mara kwa mara jambo ambalo litaongeza idadi ya washindi mkoani Kigoma nakuondoa dhana kuwa Kigoma haiwezi kutoa mshindi ni mwisho wa reli. 
  “Hakuna aliyeamini kuwa Kigoma ingeweza kutoa mshindi tena mtu kama mimi, lakini ndio hivvo nimeshiriki kikamilifu bila kuchoka hatimaye nimeibuka na milioni 100” alisema Kamugisha. 
   Bw Kamugisha pamoja na kushinda alisema ataendelea na kushiriki mashindano mengine ya Vodacom ili kupata fursa zaidi kushinda fedha zingine huku akiwashauri wananchi hasa vijana mkoani Kigoma kuchangamkia fursa hizo kujaribu bahati ili kuboresha maisha.
   Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela,Bw.Valerian Kamugisha, akishuka kwenye ndege mkoani Kigoma nyumbani kwao na kulakiwa na baba yake mzazi mara baada ya kukabidhiwa pesa zake hapo juzi
    Meneja wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Bw. Kasinde Umella (kulia)akisalimiana na Baba mzazi wa Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela,Mzee Nicodemus Nalisis,alipofika uwanja wa ndege kumlaki kijana wake Bw.Valerian Kamugisha(katikati)alipowasili Kigoma mara baada ya kukabidhiwa kitita chake hapo juzi.

   .Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela,Bw.Valerian Kamugisha,akilakiwa  na Meneja wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Bw.Kasinde Umella alipowasili uwanja wa ndege Kigoma nyumbani kwao baada ya kukabidhiwa rasmi pesa zake juzi.
   Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela, Bw.Valerian Kamugisha, akiwaonyesha majirani pamoja na babake mzazi moja ya picha aliyotolewa kwenye gazeti la Habarileo jinsi alivyokabidhiwa pesa zake  hivi karibuni,mara baada ya kuwasili mkoani Kigoma nyumbani kwao.
  Baba mzazi wa Mshindi wa shilingi Milioni 100 wa Promosheni ya Vodacom Mahela,Mzee Nicodemus Nalisis,akiongea machache mara baada ya kijana wake Kamugisha kuwasili Kigoma salama salimini akiwa milionea


  0 0

  Na Abdulaziz Lindi 
  Kijana Ismai Mayoba (31) anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri Manispaa ya Lindi ambaye amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo 
  Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.
    Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndg Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie moto huku akijua ni kosa kisheria 
  Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo
  Kijana Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove, mkaazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, akiwa katika ward namba 6 hospital ya Sokoine -Lindi baada ya kuchomwa moto na vibaka


  0 0

   Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza siku ya Fainali ya Mashindano ya Mchezo wa Pool kwa Vyuo vya Elimu ya Juu yanayodhaminiwa na Bia ya Safari,yatakayofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga.
   Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna fainli hizo zitakavyokuwa.
   Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (katikati) akikabidhi Kombe litakalokabidhiwa kwa Mshindi wa Jumla katika Fainali za Mashindano ya Safari Pool kwa Vyuo vya Elimu ya Juu kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga (kushoto).Fainali hizo zitafanyika siku ya Jumamosi na Jumapili kwenye Viwanja vya Leaders Club,Jijini Dar es Salaam.Kulia  ni Mtatibu wa Mashindano hayo,Peter Zackaria .
  Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta,Luiza Mbuttu akiimba akapela ya moja ya nyimbo za Bendi yake ambayo itatoa burudani siku hiyo.

  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein katikati wakiwa katika picha ya pamoja na Viongizo wa Kampuni ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE) nchini China,pamoja na ujumbe aliofuatana nao,mara baada ya kuwasili katika Ofisi za kampuni hiyo huko katika Mji wa Nanjing jimbo la Jiangsu nchini China akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa jamhuri ya Watu wa China.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akifuatana na Makamo wa Rais wa Kampuni ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE) Bibi Chen Jie,wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo katika Mji wa Nanjing jimbo la Jiangsu nchini China akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu wa China.
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,pamoja na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu vifaa mbali mbali vya mawasiliano zikiwemo simu katika Ofisi ya Kampuni ya Teknolojia ya mawasiliano ya habari (ZTE) wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo akiwa katika ziara ya Kiserikali kwa mualiko wa Serikali ya jamhuri ya Watu wa China,katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu.


  0 0

  Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa itafanya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana  katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
  Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo vya redio vya TBC Taifa, ZBC Redio na vituo vya televisheni vya TBC 1 na ZBC TV na vituo vinginevyo vya redio na televisheni.
  Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.
  Tume inawaomba wananchi na wadau kufuatilia uzinduzi huo kwa makini kupitia vyombo hivyo vya habari.
  Imetolewa na:
  Assaa Rashid,
  Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba

  Alhamisi, Mei 30, 2013 

  0 0

  HUDUMA MPYA YA KIFURUSHI 
  NEW DOOR TO DOOR SERVICE
  TUNACHUKUA MZIGO MLANGONI KWAKO UK NA TUTAUFIKISHA MLANGONI KWAKO DAR
  UKILIPA HAPA UK HAULIPI TENA DAR, SISI TUTAKULETEA MZIGO NYUMBANI KWAKO!
  Baada ya kushughilikia kwa kina mapungufu yaliyojitokeza mwanzo, 
  sasa tumerudi na huduma ya kifurushi tena ikiwa imeboreshwa zaidi.
  BEI ZETU KAMA KAWAIDA HAZINA KIGUGUMIZI NA SI ZA KUUMIZA

  AIR CARGO TO DAR NOW £3.50 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO ZANZIBAR NOW £3.00 INCLUSIVE CLEARANCE!
  AIR CARGO TO NAIROBI/MOMBASA NOW £2.80 INCLUSIVE CLEARANCE!
  KIFURUSHI KWA KONTENA DAR/ZANZIBAR NOW £2.20 INCLUSIVE CLEARANCE!

  NDEGE ZINAONDOKA KILA WIKI MARA MBILI
  MZIGO WOWOTE LETE TU
  MINIMUM WEIGHT IS 40KILOS
  KAMA UNATAKA KUAGIZA KITU AU KUFANYA BOOKINGS TUWASILIANE KWA NAMBA HAPA CHINI
  40'HC CONTAINER TO DAR/MOMBASA £1,800
  CHEZEA SERENGETI WEWE!
  CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
  SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243

  HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
  Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodomamay 30, 2013.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Mary Nagu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema wakiteta Bungeni Mjini Dodoma May 30,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, January Makamba, Bungeni mjini Dodoma, May 30,2013.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiataifa, Bernad Membe akisoma bajeti ya Wizara yake, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa,Bungeni Mjini Dodoma May 30,2013.
  Mbunge wa Mwanza Mjini Ezekiel Wenje akiongozwa na Mbunge wa Mtera,Livingstote Lusinde (kushoto ) na Ofisi wa Bunge ( jina halikupatikana) kutoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya hotuba yaupinzani kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa aliyokuwa akiisoma kupingwa na wabunge wa CUF, Bungeni mjini Dodoma May 30, 2013/ (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0
 • 05/30/13--10:42: MSIBA MZITO GLOBU YA JAMII
 • Marehemu Felician M. Makwaia

  MICHUZI MEDIA GROUP Inasikitia kutangaza kifo cha Mzee Felician M. Makwaia ambaye bi baba mzazi wa mmoja wa wakurugenzi wake Bw. Christopher Makwaia, kilichotokea leo May 30, 2013 huko Bombay nchini India alikokuwa amekwenda kwa matibabu baada ya 
  kupambana kwa muda mrefu na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.

  Mipango ya kusafirisha mwili kuurejeshwa nyumbani kwa mazishi inafanyika. 
  Msiba upo nyumbani kwa marehemu Sinza Mori,Jijini Dar es Salaam.

  Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.
  Tutaendelea kuwafahamisha hatua kwa hatua ya kiatakachoendelea katika msiba huu mzito.

  Kwa mawasilian0 ya aina yoyote piga simu namba
  0659 528446

  BWANA ALITOA , NA BWANA AMETWAA
  JINA LAKE NA LIHIMIDIWE

  AMIN

  0 0

  Na Mzalendo Albert, Arusha

  Alichokisema Rais Jakaya Kikwete kwenye mkutano wa kutafuta amani nchini DRC hakina ubaya wowote, kupelekea Wanyanrwanda wamjie juu na kuanza kumshambulia kwa lugha ambazo hazina ustaarabu kutokana na matamshi yake ya kutaka amani ipatikane kwa mazungumzo.  Pengine kwa kuanza nielezee kwa ufupi alichosema Rais Kikwete ambacho kimesababisha Wanyarwanda wanatahamaki kiasi hiki.

  Ajenda ya mkutano ilikuwa ni juhudi za kutafuta amani nchini DRC.  Inaeleweka kwamba vikundi vingi vya waasi kutoka nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu vinafanya shughuli zake kutokea DRC.  Vikundi hivyo kwa miaka mingi vimekuwa viki destabilize DRC kwakuwa muda mwingi vimekuwa vikiendesha mapigano ndani ya Congo.  Juhudi za kuvisambaratisha vikundi hivyo kwa njia za mapigano hazijazaa matunda kwa zaidi ya miaka 19 sasa.

  Miaka yote, Tanzania imekuwa ni kimbilio la wanyonge Barani Afrika. harakati za ukombozi wa nchi zote kusini mwa Afrika zimefanyikia Tanzania.  Aidha, Tanzania kwa miaka mingi imefanya juhudi za kutafuta amani sio nchini Congo peke yake, bali katika eneo lote la ukanda wa maziwa makuu. Mengi yamefanywa ikiwa ni pamoja na:
  1) kuwa msuluhishi katika mazungumzo ya kutafuta amani Rwanda, Burundi
  2) Kuwa mwenyeji wa wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi, DRC
  3) Kupeleka majeshi ya kulinda amani

  Kitu kumoja ambacho Tanzania imejifunza katika miaka yote hii, ni kwamba mapigano/vita mara nyingi sio suluhu ya kudumu ya kumaliza uhasama.  Mazungumzo ndio njia bora yenye kuweza kuleta maridhiano.  

  Ipo mifano mingi ya matunda ya mazungumzo.  Leo hii kikundi kilichokuwa kinajulikana kuwa ni cha kigaidi nchini Burundi FNL, ni sehemu ya Serikali ya Burundi kwa sababu, wote walitoa nafasi ya mazungumzo.

  Vikundi vingi vya kigaidi vya DRC, viligeuka kuwa vyama vya siasa na kushiriki kwenye uchaguzi, kwa sababu vilikubali mazungumzo.

  Leo hii DRC inafanya mazungumzo na vikundi vya waasi na vya kigaidi nchini Uganda ili kutafuta suluhu.  Mazungumzo haya yametokana na juhudi za wakuu wa nchi za maziwa makuu ambayo Rwanda ni mjumbe.  Hivi nani asiyejua jinsi gani vikundi hivyo vilivyofanya vitendo vya unyama na mauaji kwa wananchi wasio na hatia? Wameua, wamebaka, wameiba.....wamefanya kila jambo hovu, lakini bado imeonekana busara ya kukaa mezani kuzungumza. 

  Ukiachilia mifano ya kwenye ukanda huu, ipo mifano mingine mingi tu nje ya ukanda.

  Nothern Ireland
  Yaliyotokea Ireland ya kaskazini kila mtu anafahamu. Maelfu ya watu waliuawa kutokana na vitendo vya kigaidi vya IRA.  Lakini mwisho wa yote, Serikali ilikaa nao meza moja, matokeo yake ni amani kupatikana Nothern Irrland.

  Msumbiji na Angola
  Huko Msumbiji nani asiyekumbuka magaidi wa Renamo walivyoua maelfu ya watu nchini humo. Lakini mwishowe walikaa mezani na Frelimo, amani ikapatokana.   Hata Angola, nani asiyekumbuka Jonas Savimbi alivyoua mamia ya wananchi wasio na hatia. 

  ANC na apartheid
  Huko Afrika ya kusini nani  asiyejua kwamba maelfu ya watu walipoteza maisha yao kutokana na sera za ubaguzi na manyanyaso ya serikali ya makaburu. Lakini baada ya kuitikia wito wa kuzungumza, leo hii wanaendelea kuishi kama taifa moja.

  Wayahudi na wajerumani
  Pengine mifano niliyoitoa waweza kusema haifanani na Rwanda,kwa kuwa nchi zile haziku experience mauaji ya kimbari.  Lakini huko Ujerumani, mauaji makubwa yalifanyika dhidi ya Wayahudi.  Kila mtu anafahamu hilo.  Lakini leo hii ndugu wale hawaendelezi uhasama....

  Baada ya mifano hiyo, ni dhahiri kabisa kwamba alichoshauri Rais Kikwete ni sahihi kabisa.  Nchi zote za maziwa makuu ambazo zina vikundi vinavyohasimiana navyo, watumie njia ya mazungumzo kama njia bora ya kumaliza uhasama na kutoa fursa kwa wahusika waondoke Congo na kurejea nchini mwao.  

  Kwa kesi ya Rwanda...sio kweli kwamba kila mwanachama wa FDLR alihusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Wapo wana FDRL ambao walizaliwa baada ya 1994 na wanaishi uhamishoni  ikiwa ni pamoja na DRC. 

  Hivi ni haki kuwajumisha hao kwenye kundi la magaidi waliofanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994?  

  Je hatuoni kutoa fursa ya mazungumzo itawawezesha wana FDLR ambao hawakuwa na hatia na wala hawakuwepo mwaka 1994 kupata fursa ya kurejea nchini mwao?  

  Na je Rwanda haioni busara ya kutumia njia ya mazungumzo itawezesha kufikia makubaliano na waasi hao wawatoe waliohusika na mauaji ya kimbari wakashitakiwe?

   Kufanya mazungumzo hakumaanishi ni kutoa msamaha, la hasha.  Kufanya mazungumzo ni kuweka mazingira ya kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kuweka misingi ya kuchukua hatua mbalimbali kwa wahusika.

  Wanyarwanda wame overreact na kuwa emotional pasipo kuwa na sababu ya msingi.  Rais Kikwete na watanzania kwa ujumla, ni watu wa mwisho kuwa sympathiser wa wanachama wa FDLR waliohusika na mauaji ya kimbari mwaka 1994 na wale wanaoendeleza mapigano hivi sasa huko DRC kwani athari za vitendo vyao vilitugharimu sana.... kwani sio tu vilikiuka misingi ya utu ambayo Tanzania inaiheshimu na kuipigania siku zote, bali pia ilitugharimu kwa kupokea wakimbizi katika vipindi tofauti. Vitendo vyao bado vinaendelea kutugharimu hadi leo. Uwepo wa majeshi ya Tanzania kulinda amani nchini DRC  ni matokeo ya vikundi vya aina ya FDLR kuvuruga amani nchini DRC.

  Ikumbukwe pia Kitendo cha Tanzamia kuwa Mwenyeji wa Mahakama ya Kimataifa ya Kimbari ICTR, ni ushahidi tosha wa namna ambavyo Tanzania haiungi mkono mauaji ya kimbari  yaliyotokea Rwanda, haina huruma kwa wale wote walooshiriki katika mauaji ya kimbari.  


  Hivyo, hapa kama kuna mtu wa kuomba radhi, ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na wanyarwanda wengine wote walio over-react na kumshambulia Rais Kikwete.

  Kusoma walivyomsema Rais Kikwete BOFYA HAPA

  0 0

  Mdau Shaffih Dauda wa Clouds FM akiongozana na Ismail Sota walitembelea ofisi za SERENGETI FREIGH UK huko Uingereza kujionea jinsi boxi linavyopigwa Pamoja na kujionea wazee wa kazi wakipiga boxi.
  Mdau Shafii ambaye pia ni mmiliki wa blog ya sports iitwayo Shaffihdauda.com aliingia mkataba wa kuwarusha hewani wazee wa kazi bila malipo kwa mwaka mzima baada ya kufurahishwa na jinsi wazee wa kazi walivyoweza kulirusha jina la Tanzania/Serengeti UK na kuwa mfano bora kwa vijana wengine wenye nia ya kujiajiri.
  Mzee wa kazi Chris Lukosi akimshukuru Shafii Dauda kwa ofa yake
  Mzee wa kazi akipiga boxi
  Mkataba ukisainiwa

  0 0


  Finance Vice President of the African Development Bank (AfDB) Charles Boamah will host an online press conference on the last day of the Annual Meetings of the African Development Bank

  MARRAKECH, Morocco, May 30, 2013/ -- Finance Vice President of the African Development Bank (AfDB) Charles Boamah will host an online press conference on the last day of the Annual Meetings of the African Development Bank.

  Journalists interested in attending this event will be able to ASK QUESTIONS LIVE VIA THE INTERNET.

  Speaker: Mr Charles Boamah, Finance Vice President of the African Development Bank (AfDB)

  Date:        Friday May 31, 2013

  Time:        From 14:00 GMT (Time Converter: http://goo.gl/Ib1wS)  

  Languages:    English

  How it works: This service is FREE and only requires a computer connected to the internet.  0 0

  Courtesy of GongaMx

  0 0
 • 05/30/13--13:04: Article 6


 • 0 0

  Je,Ushapiga kura yako kwa Mshiriki umpendae kwenye kinyang'anyiro cha tuzo za Kili??Kama bado Piga sasa,ambapo utamuwezesha Mshiriki upendaye kupata Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.Unachotakiwa kukifanya ni Kutuma Code ya mshiriki huyo kwenda Namba 15345 au unaweza kupiga kura yako kwa kuingia kwenye Tovuti hii www.kilitimetz.co.tz pia unaweza tuma email kwenda ktma2013@innovexdc.com

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Makete,Mh Josephine Matiro akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake,mapema jana alipokuwa akikagua uhai wa mashina ya chama hicho katika kijiji cha Tandala,Wilaya ya Makete mkoani Njombe.Kinana na ujumbe wake wako ziarani mkoani Njombe katika kuimarisha shughuli za chama,kuangalia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa CCM na pia kuzungumza na Wananchi kuhusiana na matatizo yao mbalimbali yanayowakabili .
  Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi Ndugu Abdulrahman  Kinana akizungumza na Wananchi wa kata ya Iniho jana ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe,Kinana alizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara mambo mbalimbali ikiwemo na kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kutekekeleza miradi yake yote iliyoahidi ikiwemo ya barabara,maji na umeme,aidha aliwataka wananchi kubeza baadhi ya vyama vya siasa vinanvyoeneza chuki kwa watanzania na kuindosha amani iliyopo.Kinana akiwa sambamba na ujumbe wake ameyazungumza hayo wilayani Makete katika kijiji cha Ukwama ikiwa siku ya nne ya ziara yake mkoani Njombe kutembelea mashina ya chama hicho pamoja na kufanya mikutano ya hadhara kueleza serikali ilichotekeleza.
  Katibu  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Nape Nnauye  akimtambulisha aliyekuwa mwanachama wa CHADEMA,Keffa Lupiana pichani kushoto kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata ya Iniho,Wilaya  ya Makete mkoani Njombe.
  Mbunge wa Jimbo la Makete na Naibu Waziri wa Maji Dkt.Binilith Mahenge akieleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yaliyofanywa jimboni  mwake katika kutekeleza Ilani ya CCM kwenye mkutano wa .
   Sehemu ya Wananchi wakishangilia jambo wakati ndugu Kinana alipokuwa akizunngumza nao kwenye mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa shule ya msingi ya ukwama mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe .
    Sehemu ya Wananchi wakiwa kwenye uwanja wa kata ya Ukwama wakimsubiri Ndugu Kinana  azungumze nao mapema leo jioni ndani ya wilaya ya Makete mkoani Njombe.

  0 0

   Wa pili kutoka kushoto ni Kamishna wa Bunge Mhe. Abdul Karim Shah (Mb), Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilillah, ndugu wa mke wa marehemu Zulu na mke wa marehemu Ernest Zulu nyumbani kwa maerhemu Zulu, Ubungo Kibangu wakati wa kuuga mwili wa marehemu Ernest Zulu
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Bwana Jossey Mwakasyuka akisoma wasifu wa Marehemu Ernest Zulu.
  Jeneza lenye mwili wa marehumu Zulu likiwa katika chumba maalum nyumbani kwao Songea baada ya kusafirishwa kwa ndege kutoka Dar es Salaam. Picha na Prosper Minja - Bunge


  0 0

  WATANZANIA MLIOPO UINGEREZA HUSUSAN LONDON NA VITONGOJI VYAKE  MNAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUZISHANGILIA TIMU ZETU TANZANIA BARA   NA  ZANZIBAR ISLANDS.

  KUANZIA  JUMAMOSI YA  TAREHE 01/ 06/ 2013

  TANZANIA INA MECHI MBILI JUMAMOSI KICK OFF SAA SITA KAMILI MCHANA NA SAA TISA JIONI.


  HAKUNA KIINGILIO (NI BURE ) NI FAMILY DAY NA KUTAKUWA NA NYAMA CHOMA 


older | 1 | .... | 149 | 150 | (Page 151) | 152 | 153 | .... | 3270 | newer