Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live

Nani kuibuka Miss Lindi 2013? Jibu tarehe 31 may ndani ya Lindi Beach Resorts

$
0
0
Na Abdulaziz video/Lindi yetu Blog 
Redd’s Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa tarehe 31 may,2013 ndani ya ukumbi wa Lindi Beach Resort. Jumla ya Warembo Kumi watachuana Vikali kugombania taji hilo. 
Warembo hao wako kambini Hotelini hapo kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na Redd’s Miss Lindi 2012. 
Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa vizuri na warembo wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia anataraji show itakuwa ya Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo andaliwa, hivyo amewataka wadau kujitokeza kwa wingi. 
 Viingilio vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh 10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo wahi tiketi yako mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo katika mji wa Lindi.



The Goats are Here! Dar es Salaam’s Goat Races this Saturday

$
0
0
Dar’s 13th annual charity Goat Races will take place on June 1 on The Green, Kenyatta Drive, Msasani, Dar es Salaam. The family fun day attracts thousands of people and raises millions of shillings for local charities and organisations every year. 
 With a Sea Creatures and Sailors theme, this year’s event promises great food and drinks, fancy dress competitions, a kids’ play area and fabulous prizes. Just One Goat Can Make a Difference! Tickets cost 5,000 TZS and are available at the gate on the day.For more information see www.goatraces.com .

Safari Lager yafungua Mafunzo kwa Wajasiliamali wa Wezeshwa

$
0
0
 Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo akisisitiza jambo wakati wa kuzungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasiliamali waliofaulu kuingia kwenye Mpango wake wa  "Safari Lager Wezeshwa" yaliyoanza rasmi leo kwenye hoteli ya Golden Park,Sinza jijini Dar es Salaam.
 Jaji Mkuu wa zoezi zima la kutafuta Wajasiliamali wa Safari Lager Wezeshwa,Joseph Migunda akizungumzia namna zoezi la ushiriki lililofanyika katika maeneo mbali mbali hapa nchini,mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Wajasilia mali waliopatikana kwenye Mpango wa  "Safari Lager Wezeshwa" yaliyoanza rasmi leo kwenye hoteli ya Golden Park,Sinza jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo.
 Mmoja wa Wajasiliamali walioingia kwenye mpango wa Safari Lager Wezeshwa,Jamhuri Arbogasti akionyesha moja ya bidhaa anazozitengeneza yeye mwenye.
 Baadhi ya Wajasiliamali waliofaulu kuingia kwenye mpango wa Safari Lager Wezeshwa wakiwa kwenye Mafunzo hayo yaliyoanza rasmi leo jijini Dar.

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi lawatia mbaroni watu wawili wanaodaiwa kuchochea fujo

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kusambaza taarifa za kupotosha wananchi zenye viashiria vya uchochezi na vitisho kwa serikali kwa lengo la kuvuruga amani, upendo na utulivu wa wananchi.

Akitoa taarifa kwa wandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi George Mwakajinga amesema watuhumiwa hao wamekutwa wakiwa na mabango yenye maandishi ya uchochezi kwa watu wa mikoa ya Kusini.

Amesema kati ya watuhumiwa hao wawili, mmoja anatambuliwa kwa jina la Ivon Vandu Taasa mkazi wa Sabasaba ktk Manispaa ya Lindi ambaye alikutwa eneo la kituo cha mabasi ktk Manispaa hiyo akihamasisha wananchi kuunga mkono vurugu zinazofanywa na wananchi wa Mkoa wa Mtwara akiwa akiwa na mabango ya karatasi yenye maneno "Gesi kwanza Uhai baadaye".

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi, mtuhumiwa mwingine ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, anatuhumiwa kusambaza ujumbe wa simu kwa watu mbali mbali zenye kuchochea na kutoa vitisho dhidi ya serikali na jamii na katika tukio lingine Mkazi wa kijiji cha Majengo wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi Silvanus Patrick, anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili ktk shule ya sekondari Msufini wilayani humo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi George Mwakajinga amesema kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kufanya kosa hilo usiku wakati mwanafunzi huyo akitokea dukani alikotumwa na wazazi wake kununua mafuta ya taa kwa matumizi ya nyumbani kwao.

Mwakajinga amesema baada ya mwanafunzi huyo kudai kufanyiwa kitendo hicho, aliwaarifu wazazi wake ambao walitoa taarifa kituo cha Polisi wilaya ya Nachingwea na kufanikiwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Mwakajinga amesema kutokana na kitendo hicho, mwanafunzi huyo alipelekwa hospitali ya wilaya ya Nachingwea kwa uchunguzi wa kitaalamu na kubainika kufanyiwa kitendo hicho na kwamba mtuhumiwa anatazamiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya polisi kukamilisha taratibu zote za kisheria.

Asasi, Vyama na Makundi sasa ruksa kuunda Mabaraza ya Katiba

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa mwongozo unaoruhusu kuanza rasmi kwa uundwaji wa Mabaraza ya Katiba ya asasi, taasisi na makundi mbalimbali kwa lengo la kujadili na kutoa maoni kuhusu rasimu ya katiba inayotarajiwa kutolewa na Tume hiyo hivi karibuni.
Kwa mujibu wa mwongozo ulitolewa na Tume hiyo leo (Jumatano, 29 Mei, 2013) na kusainiwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba, mwongozo utatumika kwa miezi mitatu kuanzia keshokutwa, Juni 1 hadi Agosti 31 mwaka huu.

“Mabaraza haya ya Katiba ya Asasi, Taasisi na Makundi ya Watu wenye malengo yanayofanana yatajadili na kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Katiba,” amesema Jaji Warioba na kuongeza kuwa maoni hayo yanaweza kuwasilishwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa njia ya randama, barua, andiko, muhtasari wa makubaliano.

Mwongozo huo, ambao utachapishwa katika magazeti mbalimbali ya siku ya Alhamisi (Mei 30, 2013) na kurudiwa tena Jumatatu (Juni 3, 2013), pia unapatikana katika tovuti mbalimbali ikiwemo ya Tume hiyo (www.katiba.go.tz) na ukurasa wa facebook wa Tume hiyo (Tume ya Mabadiliko ya Katiba Tanzania).

Mkwawa Alumni Day @Makumbusho (opp. IFM) 22 June 2013!

$
0
0
Maandalizi yanafanyika kwa ajili ya kuwakutanisha wale waliosoma Shule ya Mkwawa, Iringa kuanzia mwaka 1965 hadi 2005 kabla ya kuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Mkwawa University College of Education (MUCE)

Siku: Jumamosi 22 Juni, 2013
Mahali: Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa (mkabala na IFM)
Mchango: Shilingi elfu hamsini (50,000/-) @ mtu


Mchango huu ni kwa ajili ya kugharamia matangazo katika vyombo vya habari, vinywaji, chakula, ulinzi, mapambo, kukodi viti na meza, mshereheshaji (MC) na PA, live band. Tiketi zitapatikana wiki moja kabla ya siku ya shughuli

Shughuli hii itakuwa ni mwanzo wa kuchangia Chuo cha Elimu Mkwawa (MUCE) ili kuweza kujenga mabweni (hostels) kwa ajili ya wanafunzi

WanaMkwawa tuko wengi na tuna kila fursa ya kujumuika pamoja kukumbushana ya Makongoro na Magembe, Makanyagio na Lumumba, Aggrey na Shaaban Robert!

MUCE wamefungua portal kwa ajili ya Mkwawa Alumni tafadhali jisajili ili kuwa sehemu ya familia kubwa ya Mkwawa http://muce.ac.tz/index.php/alumni-registration

Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Kamati ya Maandalizi kupitia: Catherine David
Email: Cathyjeff2001@yahoo.com
Simu: +255 784/15 609 848
Mkeka wa Nguvu kuingia Iringa mjini.
Bustani ya Garden katika  Shule ya Mkwawa, Iringa.
Wadau wakipata msosi enzi hizooo

Airtel yazindua michuano ya Airtel Rising Stars 2013

$
0
0
Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo , wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo(katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu.
Baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012 wakisalimiana na Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam leo.
Wakizindua program ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2013.

CHANNEL TEN na GLOBU YA JAMII WANAKUPA MAGAZETINI LEO


JAHAZI KUNOGESHA REDDS MISS ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza,Arusha

BENDI ya Jahazi morden taarabu chini ya muimbaji mashuhuri Mzee Yusuph inatarajia kunogesha usiku wa kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Arusha (Redd's Miss Arusha 2013) itakayofanyika June 08 mwaka huu katika ukumbi wa triple A jijini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa shindano hilo,Phidesia Mwakatalima alisema kuwa shindano hilo litafanyika usiku wa jumamosi june 08 katika ukumbi wa Triple A.

Alisema kuwa jumla ya walibwende kumi na tano 15 kutoka katika vitongoji vitatu vya jiji la Arusha,watapanda jukwaani kuchuana vikali ili kuwezesha kupatikana kwa Redd's Miss Arusha 2013,vitongoji hivyo ni pamoja na kitongoji cha Njiro,Arusha mjini (Arusha city centre) pamoja na kitongoji cha Monduli.

Alibainisha kuwa mpaka sasa warembo wameshaingia kambini na tayari wameanza kujifua kwa ajili ya shindano hilo huku akibainisha kuwa kwa mwaka huu lazima mrembo wa Tanzania (Redd's Miss Tanzania) atokee mkoa wa Arusha

Alisema kuwa zawadi mbalimbali zitatolewa ikiwemo kuwasomesha warembo katika vyuo mbalimbali lugha ya kiswahili ,kingereza pamoja na kifaransa.

Shindano hilo lidhaminiwa na perfect choice super markety,libeneke la kaskazini blog,trile A fm,Radio 5 fm,sunrise Fm,Mambo Jambo Fm,Aliance francee,Geo Securty,Cassaranda wear,Meru Spring Water Pamoja na Otakef Motel.

Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa Tanzania yaahidi kuendelea kutoa ushirikiano

$
0
0
IMG_0433
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
IMG_0374
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.IMG_0406
Baadhi ya Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani wakati wa maadhimisho hayo.

Rais Kikwete awasili Japan Kuhudhuria Mkutano wa 5 TICAD

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Narita,Japan ambapo atahudhuria Mkutano wa tano wa (TICAD)unaofanyika katika mji wa Yokohama.Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan Bibi Salome Sijaona(picha na Freddy Maro).

WAZIRI MKUU PINDA AFUNGA SEMINA YA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA MJINI DODOMA LEO,PIA AONGOZA KIKAO CHA SENSA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongoza kikao cha kujadili masuala ya Sensa kwenye ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma Mayy 29, 2013.Wa pili kulia ni Makamu wa Pili wa Rais SMZ,Balozi Seif Idd.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza (wapili kulia) , Naibu Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushirika , Adam malima (kulia na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Angela Mabula wakiteta baada ya Waziri Mkuu,Kufunga semina ya waskuu wa mikoa na wilaya kuhusu usambazaji wa pembejeo , mjini Dodoma , May 29,2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Angela Mabula baada ya Waziri Mkuu,Kufunga semina ya waskuu wa mikoa na wilaya kuhusu usambazaji wa pembejeo , mjini Dodoma , May 29,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Article 4

$
0
0
BTG Group LTD (www.btgforafrica.com) is holding a one-day workshop titled: Leadership Skills for the Global Marketplace. Attendees will receive training in: 
Business Negotiations 
Cultural Intelligence 
Leadership Values 
Cyber Security Management 

The quality of your business's employees is directly related to the success of your organization. The strategies and topics covered during this workshop will give your employees the edge in advancing your business. 

Date: Thursday 6, June 2013 
Time: 9AM - 4PM 
Location: Holiday Inn, Dar es Salaam, City Centre 

For registration and details, please visit: www.btgforafrica.com/workshop 

We hope to see you there! 

KARIBUNI SANA.

Shule ya Sekondari ya Aga Khan Mzizima yafanya mahafali kwa wahitimu wa kidato cha sita leo

$
0
0
 Wahitimu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Aga Khan Mzizima jijini Dar es Salaam,wairusha juu kofia zao mara baada ya kutunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu hiyo wakati wa mahafali yao yaliyofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,Upanga jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Aga Khan Mzizima jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Furaha ya kuhitimu masomo. 
 Mmoja wa wanafunzi wa Shule hiyo akionyesha umahiri wake wa kupiga Piano wakati akitoa burudani kwenye mahafali hayo.
Sehemu ya wazazi,walezi na wageni mbali mbali waliohudhulia mahafali hayo.

TASWIRA ZA RAIS WA ZANZIBAR NCHINI CHINA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China kiwa katika ziara ya kiserikali
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na ujumbe wake wakitembelea sehemu mbali mbali za  Kihistoria zilizopo katika makumbusho ya Mji wa  Beijing nchini China kiwa katika ziara ya kiserikali. 

ETHIOPIA:Through the Diaspora eyes By Ayoub mzee

TAARIFA YA KIFO

$
0
0
Marehemu Ernest Zulu 1957 - 2013


Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Thomas Kashilillah anasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wa Ofisi ya Bunge Bwana Ernest Zulu aliyekuwa Afisa Habari Mkuu kilichotokea tarehe 23 Mei 2013 akiwa masomoni nchini Malaysia. 

Mwili wa marehemu umewasili leo tarehe 29 Mei 2013. Heshima za mwisho zitatolewa nyumbani kwa marehemu Dar es Salaam Ubungo-Kibangu tarehe 30 Mei, 2013 kuanzia saa tano asubuhi na mazishi yafanyika nyumbani kwao Peramiho, Songea tarehe 31 Mei 2013

Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina!


Dkt. Thomas Kashilillah
KATIBU WA BUNGE

mpiganaji Felix Mwagara na Lydia Mbonde wameremeta

$
0
0
 Mpiganaji  Felix Mwagara akikata ndafu na mai waifu wake Lydia Mbonde katika mnuso wao mara baada ya kumeremeta  katika Kanisa Katoliki, Hai Mjini, Kilimanjaro.

 Felix na Lydia wakifungua muziki wakati wa mnuso wao katika Ukumbi wa Hai Garden, Papa Motel, mkoani Kilimanjaro.

 Mpiganaji Felix akiwasha mshumaa unaoashiria upendo wakati wa mnuso wa Send off kwa mchumba wake Lydia. Sherehe hiyo ilifanyika Mwenge Social Hall, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mpiganaji Felix Mwagara akipongezwa na wageni mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo.

Article 23

POLISI YAWATOA HOFU WANANCHI DHIDI YA TAARIFA POTOFU

$
0
0
Na Frank Geofray,Jeshi la Polisi, Mtwara.
Jeshi la Polisi nchini limewataka wananchi kutokuwa na hofu juu ya taarifa za kutoaminika na  ambazo hazijafanyiwa uchunguzi zinazotolewa na baadhi ya watu kuhusu idadi ya watu waliofariki katika vurugu zilizotokea mkoani Mtwara.

Akizungumza na Waandishi wa habari mkoani Mtwara Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi hilo Paul Chagonja alisema idadi ya watu waliofariki ni watu watatu mpaka hivi sasa na waliojeruhiwa ni watu kumi na nane tofauti na taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa na baadhi ya watu.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Fatuma Mohamed (22), Karimu Shaibu (22) na Mussa Mohamed (28) ambapo mpaka hivi sasa mtu mmoja ndiye aliyebakia katika hospitali ya rufaa ya Ligula akipatiwa matibabu.

Chagonja alisema watu 91 walishafikishwa mahakamani kujibu makosa mbalimbali ikiwemo ikiwemo kuharibu miundominu, kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuchoma nyumba moto.

Alisema zaidi ya watu mia moja wameshajitokeza mbele ya tume iliyoundwa kwa ajili ya kukusanya malalamiko kwa yeyote ambaye anaona hakutendewa haki wakati wa kudhibiti vurugu hizo na endapo upelelezi utabaini kuwepo kwa vitendo viovu sheria itafuata mkondo wake.

Hata hivyo alibainisha kuwa Jeshi hilo litahakikisha linamkamata kila mmoja ambaye amehusika katika vurugu hizo na kumfikisha katika vyombo vya sheria.
Viewing all 110089 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>